Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109978 articles
Browse latest View live

MPOGORO AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 281 SENETI YA VYUO NA VYUO VIKUU NA KUVUNA WANACHAMA WA CHADEMA MKOANI IRINGA LEO. Inbox x

$
0
0
Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg.Rodrick Mpogolo akimkabidhi cheti cha pongezi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndg.Kenani kiongosi katika sherehe ya Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Naibu katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg.Rodrick Mpogolo akitoa vyeti kwa wahitimu wa Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogolo akipokea baadhi ya bendera na jezi za chadema wakati akimkaribisha ndg Godfrey Maiko aliojiunga rasmi na CCM Leo  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg Rodrick  Mpogolo akimvisha kofia ya CCM ndg Godfrey Maiko aliojiunga rasmi na CCM Leo  katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akipeana Mkono na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini Ndg Damalo aliporejesha kadi ya Chadema na Kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi Leo katika Mahafali ya Seneti ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Iringa yaliyo fanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.


SIKU YA WAJANE DUNIANI 2018

Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi

$
0
0
Na mwandishi wetu
VETERANI wa timu ya soka ya Uingereza ya Liverpool, Sami Hyypia amewataka vijana Watanzania kuongeza bidii katika kuhakikisha kwamba wanafikia hatua za juu za uchezaji soka hivyo kupata nafasi ya kucheza Ulaya.
Pia amesema ni matumaini yake kuwa mamlaka za utoaji leseni hazitawazuia vijana kwenda Ulaya kujaribu bahati zao.
Alisema hayo wakati wa kiliniki ya soka aliyoifanya kwa vijana wa Serengeti boys jana alipokuwa akishiriki nao katika mafunzo na mazoezi.
Alisema kwamba yeye hakuwa na kipaji kikubwa kuliko alivyoviona kwa vijana hao lakini ameweza kufikia hatua za juu kabisa za uchezaji wa soka kutokana na kujituma kwake.
Alisema amewaambia vijana kuangalia zaidi juhudi kwani kipaji pekee hakitoshi kumfanya mtu kuwa gwiji katika soko.
Alisema pamoja na mafundisho ya walimu ni kazi ya mchezaji mwenyewe kuona udhaifu wake uliopo na kuufanyia kazi ili aweze kuwa mwanasoka bora wa kutegemewa.
Akihojiwa mwanasoka huyo ambaye aliwika sana katika enzi zake alisema kwamba amefurahishwa na uchezaji wa timu hiyo hasa kwa pasi ndefu na kusema kwamba vijana wote wameonesha kuwa na vipaji vikubwa.
Alisema hata hivyo kwamba amewaambia wachezaji awali kuwa na kipaji pekee hakutoshi lakini ni lazima mtu binafsi kufanyakazi ya ziada kuondoa udhaifu wake ambao binadamu wengi wanakuwa nao ili kuwa mahiri katika uchezaji.
Sami ambaye yupo nchini kuangalia michuano ya kombe la benki ya Standard Charted  inayofanyika leo na kushirikisha timu 32 zinazowania kwenda Anfield kuona mechi za msimu mpya timu ya Liverpool  ndani ya EPL na kuzungumza na magwiji na kupata nafasi ya kunolewa, amesema siri kubwa ya mafanikio ni kujituma kwa mchezaji pamoja na kwamba anakipaji na walimu wazuri.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akimtambulisha Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) kwa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kulia) pamoja na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza kwa makini Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) na Mshauri Mkuu wa Ufundi katika Programu za Soka la Vijana nchini, Kim Paulsen wakiangalia uzoefu wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya gwiji huyo hapa nchini.


 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya gwiji huyo hapa nchini.
 Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakijinoa baada ya kupata mafunzo na mbinu mbalimbali wakati wa kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia hapa nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MITANDAO ISITUMIKE KUKWAMISHA SHUGHULI ZA SERIKALI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza mifumo ya utoaji huduma Serikali kwa njia ya mitandao isitumike kukwamisha shughuli za Serikali au mipango ya utoaji huduma kwa wananchi.

Amesema watakaobainika kuhujumu mifumo hiyo wachukuliwe hatua za kinidhamu na amesisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitawavumilia watumishi wasio waadilifu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 23, 2018) mara baada ya kuzindua mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma.Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2018 iliyotolewa na Umoja wa Afrika (AU) ni “Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika na Malengo ya Maendeleo Endelevu”.

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watumishi wa Umma wote nchini, wananchi, Sekta Binafsi, Sekta ya Umma, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Kisiasa na Wadau mbalimbali, kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa.“Hii ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo Malengo ya Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika (AU) na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ambayo yamehimizwa na Kaulimbiu ya mwaka huu,”.

Pia Waziri Mkuu amewaagiza Watendaji Wakuu wa Taasisi zinazosimamia mifumo hiyo pamoja na maafisa waliopewa dhamana ya kuwahudumia wananchi kupitia mifumo hiyo, wahakikisha wanailinda na kuitumia vema ili iweze kuwa na tija na manufaa yaliyokusudiwa.

Mifumo hiyo aliyoizundua inahusu utoaji Huduma Serikalini ambayo ni Mfumo wa Usajili wa Vizazi na Vifo, Mfumo wa Taarifa za Kitabibu, Mfumo wa Taarifa za Ununuzi, Mfumo wa Kumbukumbu za Kielektroniki na Mfumo wa Ofisi Mtandao. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kwenye uzinduzi wa mifumo tisa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Katibu Muhtasi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Kholuu Ramadhan, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Johari Swalehe kwa niaba ya mwanae Seif Ramadhan, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mkurugenzi wa TEHAMA, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Cuthbert Simalenga, wakati akikagua mabanda kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi cheti cha kuzaliwa Shukran George kwa niaba ya mwanae Magreth Msomba, kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini Dodoma Juni 23, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

ZFDA WATEKETEZA TANI 20 ZA MAZIWA YALIYOHARIBIKA

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 23.6.2018

Wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) imewakumbusha Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za Chakula kutoka nje kuhakikisha wanafuata miongozo, sheria na kanuni za usafirishaji ili kuhakikisha bidhaa zao zinafika nchini zikiwa salama kwa matumizi ya wananchi.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti wa Chakula na Dawa Dkt. Khamis Ali Omar alisema hayo katika Jaa la Kibele kwenye zoezi la kuteketeza maziwa yaliyoharibika kwa kusafirishwa kwenye kontena moja na mizigo mengine ikiwemo gari kutoka Dubai.

Alisema baadhi ya maboksi ya maziwa yalipasuka kutokana na msukosuka wa meli baharini na kuharibu maboksi mengine yaliyopelekea maziwa yote yakose sifa ya matumizi ya binadamu.Aliwashauri wafanyabiashara kuheshimu chakula na kukiepusha na viashiria vyote hatari wakati wa kuvisafirisha na kwenye maghala ili kuwaepusha wananchi na athari zinazotokana na chakula kibovu .

Maziwa hayo yenye uzito wa tani 20 yaliingizwa na mfanyabiashara Essak Suleiman wa Darajani tarehe 6 mwezi huu yakiwa yameshaharibika na kuamua kuyazuia yasiingie sokoni.Mkuu wa Kitengo cha Uchambuzi wa athari zitokanazo na chakula wa ZFDA Asha Suleiman amewashauri wananchi wanapopewa sadaka ya chakula kuwa waangalifu kwani wamegundua baadhi ya wafanyabiashara hutoa sadaka zilizokwisha haribika baada ya kukosa soko.

Aidha amewashauri wananchi wanapokuwa na shaka ya chakula na kuhisi kinadalili ya kuharibika kutoa taarifa Wakala wa Chakula Dawa na Vipodi ili kwenda kukiangalia na kupata uhakika wake kabala ya kuanza kukitumia.Wakati huo Mfanyabiashara Essak Suleiman alieingiza maziwa hayo alisema sababu iliyopelekea mzigo huo kuharibika ni upakiaji mbaya uliofanywa na wenye meli, joto kali na kuchelewa kuondoka meli Dubai kuja Zanzibar.
WAFANYAKAZI wa ZFDA wakiteremsha Maziwa yalioharibika kwenye gari kwa ajili ya kuyaangamiza katika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
KAIMU Mkurugenzi ZFDA Dkt. Khamis Ali Omar akizungumzia zoezi la Uteketazaji wa Maziwa tani 20 yalioharibika katika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.
GARI aina ya Katapila likisaga maziwa yalioharibika na yasiyofaa kwa matumizi ya Binaadamu katika zoezi lililofanyika Jaa la Kibele Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Abdalla Omar Maelezo Zanzibar

SPIKA NDUGAI AONGOZA HAFLA YA UZINDUZI MAALUM YA UJENZI WA VYOO BORA KWA MAENDELEO YA MTOTO WA KIKE NCHINI YA KUCHANGISHA FEDHA

$
0
0
pika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa hafla Maalum ya Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana

Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan(kushoto) na Spka wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) wakifurahia maonyesho ya Waheshimiwa Wabunge (hawapo kwenye picha) ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
Waheshimiwa Wabunge wakiingia kwa kuimba wakati wa Maonyesho yao ikiwa ni njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia), Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) wakishikilia hundi ya sh. Millioni 100 waliopewa na kampuni ya Uchimbaji Madini ya GEITA GOLD MINING mchango wao kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Lucy Mayenga akiwapungia mkono wageni waalikwa wakati wa Maonyesho ya mavazi yaliyotolewa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kama njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana 
Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Vicky Kamata na Waheshimiwa wenzake wakiwaburudisha wageni waalikwa na Wabunge katika onyesho la kuimba lililoandaliwa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kama njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangish a fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

ASILIMIA 7 HADI 16 YA WANAWAKE WOTE DUNIANI NI WAJANE

$
0
0
Na Anthony Ishengoma WAMJW.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa unaonesha kuwa kati ya asilimia 7 na 16 ya wanawake wote duniani ni Wajane.  

Jamii imetakiwa kuendeleza mipango na kuongeza juhudi zaidi katika kukabiliana na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na kuwainua wajane ili wapate uwezo wa kiuchumi wa kuzihudumia familia na wategemezi wao kwa kuwa ndiyo muhimili pekee wa familia iliyoachwa.

Akiongea kwa niaba ya Mgeni rasmi wa kongamano la Wajane liliofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa Bi. Honoratha Rwegasira amepongeza juhudi za wadau wa maendeleo na serikali katika kuwasaidia wajane kuleta usawa wa kinjisia na kuinua ushiriki wao katika ngazi za kutoa maamuzi.  

Aidha Bi.Rwegasira ameitaka jamii kuacha mila potofu kama vile kunyanganya mali mjane, kuozesha watoto wa kike katika umri mdogo, kurithi wajane na nyingine zote zinazoweza kumdhoofisha mwanamke katika jitihada zake za kujikwamua kifikra, kiutamaduni, kiuchumi,kijamii na kisiasa.
 Mkurugezi  Msaidizi  Idara ya Jinsia, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza akitoa hutuba yake kwenye  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
 Afisa Mwandamizi  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi .Sirivia Siliwa  akitoa mada kuhusu Chimbuko la  Siku ya  Wajane Duniani wakati wa Kongomano la Wajane lilifanyika leo Mjini Dodoma.
 Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma  Bi. Honoratha Rwegasira  akitoa hutuba ufunguzi  kwa niahaba ya Mgeni rasmi wakati wa  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma.
Wajane wa Mkoa  wa Dodoma wakiwa kwenye  Kongomano la Wajane lililofanyika leo Mjini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MATUKIO KATIKA PICHA MATEMBEZI YA SIKOSELI VIWANJA VYA MWEMBAYANGA

$
0
0
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na watoto wenye sikoseli baada ya matembezi yaliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Sikoseli Tanzania Dkt. Deo Soka akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu baada ya matembezi ya siku ya sikoseli katika viwanja vya Mwembeyanga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakatikati) akiwa katika matembezi ya siku ya Sikoseli, kushoto kwake ni mwakilishi wa WHO na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Felix Lyaviva Siku ya sikoseli Duniani huazimishwa Juni 19

Wadau wa sikoseli wakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kunyoosha viungo baada yakumaliza matembezi ya Km 3 ambayo yalikomea katika viwanja vya Mwembeyanga.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mwembeyanga na Wadau wa Sikoseli wakati wa matembezi ya siku ya Sikoseli ambayo kauli mbiu yake ni *Kuwa mjanja, Ijue Sikoseli*

WANAWAKE KWA KUSHIRIKIANA NA WAUME ZENU ANDIKENI WOSIA KABLA MAUTI HAIJAWAKUTA

$
0
0

Na.Vero Ignatus Arusha.

Imeelezwa kuwa kuandaa wosia mapema kabla ya kifo inasaidia kuepuka mogogoro ya mirathi ambayo imekuwa ikiwakumba wajane.

Hayo yamesemwa na Naibu meya wa jiji la Arusha Viola Lazaro katika maadhimisho ya siku ya wajane duniani mkoani iliyofanyika Palace Hotel Mkoani Arusha.Akitoa changamoto wanazo pitia wajane Bi Janet Mgane amesema matatizo ya Mirathi, Wajane kushindwa kufahamu sheria na kesi kuchukua muda Mrefu.

Akijibu risala iliyosomwa na mratibu wa tawia Kanda ya KaskaziniJuliet Mgani, Naibu meya amesema changamoto kubwa waliyonayo ni wanawake wengi kutokuzifahamu haki zao kisheria na kikariba."Wanawake wengi amabao ni wajane wanashindwa kupambana kushinda kesi kwa kutokufahamu sheria na kikatiba" Alisema naibu meya.Mmoja wa wajane bi Agness Omari (78)ametoa ushauri kwa wajane wajiheshimu na kuwalea watoto walioachiwa na waume zao waliotangulia mbele za haki.

Kauli mbiu ya siku ya wajane duniani "wajane tusibaki nyuma katika kuelekea uchumi wa viwanda na malengo ya maendeleo endelevu 2030.

Naibu Meya wa Jijila Arusha Viola Lazaro akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wajane duniani yaliyoyanyika katika Hotel ya Palace mkoani Arusha ambapo alikuwa mgeni rasmi.Picha na Vero Ignatus 
Mratibu wa chama cha wanawake wajane Jijini Arusha(TAWIA) bi Janet Mgane akisoma risala mbele ya mgeni rasmipamoja na wanawake wajane waliohuduria katika kuadhimisha siku yao mkoani Arusha ambapo zaidi ya wanwake 50 waliwezakuhudhuria huku ikiwa ni mara yao ya kwanza kuadhimishwa mkoani hapo.Picha na Vero Ignatus .
Wakwanza kulia ni Mratibu wa chama cha wanawake wajane mkoani Arusha bi Janet Mgane,akimkabidhi mgeni rasmi risala Naibu meya wa jiji la Arusha Viola Lazaro,katikati ni diwani wa viti maalum chadema Happy Charles akufuatiwa na Mkurugenzi wa jinsia na mahusiano ya jamii kutoka shirika la Civil and Legal Aid Organization Ranto Muhochi.Picha na Vero Ignatus
Diwani wa viti maalum chadema Happy Charles akizungumza na wanawake wajane katika ukumbi wa Hotel ya Palace Jijini Arusha. 
Meneja wa Biashara kutoka Benki ya CRDB Rose Wilium akizungumza na wanawake wajane akiwaelekeza namna ya kufungua akaunti na namana ya kujikwamua kiuchumi. Picha na Vero Ignatus 
Pichani ni baadhi ya wanawake wajane (TAWIA)pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha wanawake wajane nchini,wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Meya wa Jiji la Arusha Viola Lazaro.Picha na Vero Ignatus 
Baadhi ya waandishi wa habari Mkoani Arusha walioalikwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa katika Hotel ya Palace.Picha na Vero Ignatus 

WASHINDI WA KAMPENI YA MATUMIZI YA "TEMBOCARDVISA" WA BENKI YA CRDB WAUNGANA NA MASHABIKI LUKUKI WA SOKA NCHINI RUSSIA

$
0
0
 Washindi wa Promosheni ya Shuhudia Kombe la Dunia na TemboCardVisa ya Benki ya CRDB, Nuru Nassor Kisome (katikati) na Danford Martin Muyango (wa pili kulia) wakiwa na washabiki wa timu ya Mexico walipokutana kwenye Treni wakati wakielea kwenye Uwanja wa Spartak, jijini Moscow, Urusi kushuhudia mtanange kati ya Ubelgiji na Tunisia. Hawa ni washindi wa waliopatikana kupitia Promisheni hiyo, ambayo inamuwezesha mteja wa Benki ya CRDB anayefanya miamala mingi zaidi kupitia kadi ya TemboCardVisa kila wiki, kujishindia safari ya kushuhudia mechi mbalimbali za fainali hizo. Mpaka sasa washindi wanne tayari wameshahudhuria mechi hizo. Picha zote na Othman Michuzi.
 Meneja Masoko wa Benki ya CRDB, Jadi Ngwale (kulia) akiwa na Washindi wa Promosheni ya Shuhudia Kombe la Dunia na TemboCardVisa ya Benki ya CRDB, Nuru Nassor Kisome (kushoto) na Danford Martin Muyango muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Ubelgiji na Tunisia, uliochezwa kwenye Uwanja wa Spartak, jijini Moscow, Urusi.
 Washindi wa Promosheni ya Shuhudia Kombe la Dunia na TemboCardVisa ya Benki ya CRDB, Nuru Nassor Kisome (kushoto) na Danford Martin Muyango wakifurahi kwa pamoja huku wakionyesha kadi ya "TemboCardVisa" ya Benki ya CRDB iliyofanikisha kuwafikisha nchini Urusi kushuhudia Kombe la Dunia.
 Nuru Nassor Kisome ambaye ni mmoja wa washindi wa Promosheni ya Shuhudia Kombe la Dunia na TemboCardVisa ya Benki ya CRDB akionyesha furaha yake akiwa uwanjani hapo. 
 Muendeshaji Msaidizi wa Libeneke la Michuzi, Othman Michuzi akiwa na Washindi wa Promosheni ya Shuhudia Kombe la Dunia na TemboCardVisa ya Benki ya CRDB, Nuru Nassor Kisome na Danford Martin Muyango pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya CRDB, Jadi Ngwale.
 Wakiwa nje ya Uwanja wa Spartak, Mjini Moscow.
Baadhi ya wadau kutoka nchini Tanzania wakiwa nje ya Uwanja wa Spartak baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Ubelgiji na Tunisia.

MICHUZI TV KATIKA KOMBE LA DUNIA JIJINI MOSCOW: SHANGWE ZA MASHABIKI KUELEKEA MECHI YA UBELGIJI NA TUNISIA

MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA DUNIANI KUFANYIKA MKOANI IRINGA JUMANNE JUNI 26, 2018

MAKONDA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA AFRICANA KINZUDI

$
0
0

Na Emmanuel Masala, Globu ya jamii 

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Barabara ya Africana Kinzudi yenye urefu wa kilometer 3.3 ambayo ujenzi wake utagharimu zaidi ya Sh.Million 900.

Ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami inaenda sambamba na uwekaji wa matuta, mitaro ya maji, taa za barabarani, Calvert na alama za watembea kwa miguu ambapo itajengwa na TARURA. 

Baada ya kuzindua Barabara hiyo jana RC Makonda amefanya mkutano wa hadhara na wakazi wa Kata za Wazo na Mbezi Juu uliolenga kupatia majibu ya changamoto zinazowakabili kwenye sekta ya miundombinu, elimu, afya, maji,ardhi na usafiri.

Ambapo wakazi wa Kata hizo wamefurahia kuona kero zao za muda mrefu zimepatiwa ufumbuzi wa haraka.Pia wakati wa mkutano huo RC Makonda ameelezea miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa kwaajili ya usafiri wa treni kutoka Wazo kuelekea Mwenge, Airport na Posta ambayo itasaidia usafiri na kupunguza msongamano wa magari.

Aidha RC Makonda amewataka wananchi waliojenga kwenye hifadhi ya barabara ya Afrikasana Kinzudi kushirikiana na seri kali kuhakikisha ujenzi unafanikiwa.Makonda amewata wakazi waliojenga ndani ya hifadhi ya bomba la maji kutokea Ruvu kushirikiana kwa kina na DAWASA.

Pamoja na hayo ameagiza kila mtaa kuwa na ramani ya mipango miji ili kukabiliana na migogoro ya ardhi na utapeli ambapo pia amewataka wananchi waliocheleweshewa kupatiwa vibali vya ujenzi kufika ofisini kwake Julai 1 mwaka huu.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda sambamba na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi wakiweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Africana Kinzudi jana jijini Dar as Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi naMeya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta wakiwasili eneo la Africana kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo jana jijini Dar as Salaam.
Sehemu ya wanachi wa Africana na Kinzudi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda( hayupo pichani),alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa hadhara

Muonekano wa barabara hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya Kinondoni,Ally Hapi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Africana Kinzudi jana jijini Dar as Salaam.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 24, 2018

NAIBU WAZIRI SHONZA AZINDUA ONESHO LA ADORABLE WEDDING TRADE FAIR 2018 JIJINI DAR

$
0
0
Uzinduzi rasmi wa onesho la Adorableweddingtradefair2018  umefanyika  jana jumamosi ndani ya ukumbi wa King Solomon,Namanga jijini  Dar,ambapo Mgeni rasmi alikuwa  ni Naibu waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Juliana Shonza.

Aidha katika muendelezo wa onesho hilo leo Usisite kupita pale katika ukumbi wa King Solomon, Namanga mkabala na Best Bite leo na kujionea wadau mbalimbali wa sherehe kama wapambaji, Cake,Ma-Mc,Wauzaji wa nguo,Chakula,Picha na wengineo lukuki wakionesha bidhaa zao,bila kusahau Vyakula mbalimbali vitakuwepoo kwa bei nafuu tuu,Ni Onesho la bure kabisa na hakuna kingilio. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza   akizungumza  mbele ya washiriki na waandaaji wakati wa uzinduzi wa onesho la Adorableweddingtradefair2018,lililofanyika ndani ya ukumbi wa King Solom jana,Namanga jijini Dar

Muandaaji wa Onesho la 
Adorableweddingtradefair2018, Anna Lema akizungumza jambo wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza kabla ya uzinduzi wa onesho la Adorableweddingtradefair2018.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza (wa tatu kushoto ) akitazama bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikiuzwa katika onesho hilo laAdorableweddingtradefair2018,lililofanyika ndani ya ukumbi wa King Solom jana,Namanga jijini Dar

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa onesho hilo la Adorableweddingtradefair2018

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe .Juliana Shonza (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waandaaji wa onesho hilo la Adorableweddingtradefair2018 sambamba na washiriki wengine mbalimbali waliohakikisha onesho hilo linafana kwa kiasi kikubwa

SPIKA NDUGAI AONGOZA HARAMBEE YA UZINDUZI MAALUM YA UJENZI WA VYOO BORA KWA MAENDELEO YA MTOTO WA KIKE NCHINI

$
0
0

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa hafla Maalum ya Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
 Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan(kushoto) na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) wakifurahia maonyesho ya Waheshimiwa Wabunge (hawapo kwenye picha) ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
 Waheshimiwa Wabunge wakiingia kwa kuimba wakati wa Maonyesho yao ikiwa ni njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
 Mgeni rasmi Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia), Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) wakishikilia hundi ya sh. Millioni 100 waliopewa na kampuni ya Uchimbaji Madini ya GEITA GOLD MINING mchango wao kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana
Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Lucy Mayenga akiwapungia mkono wageni waalikwa wakati wa Maonyesho ya mavazi yaliyotolewa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kama njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangisha fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Ambapo kiasi cha Shillingi Billioni 1. 4 ziliweza kupatikana kwa siku ya jana 
 Mbunge wa Viti Maalum CCM, Mhe. Vicky Kamata na Waheshimiwa wenzake wakiwaburudisha wageni waalikwa na Wabunge katika onyesho la kuimba lililoandaliwa na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge kama njia ya kuhamasisha Ujenzi wa Vyoo Bora kwa Maendeleo ya Mtoto wa kike nchini ya Kuchangish​​a fedha iliyofanyika jana katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MWENYEKITI WA MTAA MJINI TARIME AVAMIWA,APIGWA MAPANGA, APORWA FEDHA

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime

MWENYEKITI wa Mtaa wa Mtaa wa Bugosi Kata ya Nyamisangura Mjini Tarime mkoani Mara Zacharia Ghati amevamiwa akiwa njiani na watu wanaodhaniwa kuwa vibaka na kumshambulia kwa kutumia vitu vyenye ncha kali.

Pia vibaka hao walikuwa na nondo na marungu ambayo waliyatumia kumshambulia nayo,hivyo kumsababishia maumivu makali na kisha wakampora fedha Sh.320,000.

Akizungumza na Michuzi Blog akiwa amelazwa katika Hospitlai ya Mji wa Tarime Mwenyekiti huyo amedai tukio hilo limetokea Saa Nne ambapo ameporwa pia kitamburisho chake cha kazi na cha mpiga kura pamoja na kumsababisha maumivu.“Nilikuwa nimesindikiza mmoja wa wananchi wangu alienda kwenye harusi kwa ajili ya kuchinjia mama mkwe sasa kipindi tunarudi nilipofika mtaani kwangu nilipigiwa simu na mwenyekiti wa Mtaa.

"Hivyo wananchi tukaachana na kipindi naenda nilikutana na watu wawili wakanisimamisha wakaanza kunishambulia na panga na kisha wengine kama wanne wakaongezeka ndio wakaanza kunishambulia kwa virungu na nondo,” amesema . Mmoja wa wananchi Chacha Masero aliyekuwa ameambatana na Mwenyekiti huyo kabla ya kutokea kwa tukio hilo amesema saa tatu wakiwa nyumbani baada ya kutoka kwenye harusi Mwenyekiti huyo alipigiwa Simu na Mjumbe wa Mtaa.

Ameongeza hivyo alimua kuondoka peke yake na baada ya muda alipokea taarifa za Mwenyekiti huyo kuvamiwa na vibaka. “Mie nilipopata taarifa hizo nilikwenda Polisi na kisha tukafanya utaratibu wa kumleta hospitali mpaka sasa anaendelea na matibabu japo ameumizwa sana Mwenyekiti wetu,” amesema Chacha.

Nao wananchi wa Mtaa wa Bugosi Kata ya Nyamisangura wameiomba Serikali likiwemo Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia ulinzi huku wakichukuliwa hatua kali vibaka wanakamatwa na kufaamika katika mitaa huska.“Kuna vibaka wanafaamika kabisa lakini wanalindwa na baadhi ya viongozi kwa sababu ya undugu, tunaomba washughulikiwe,” amesema mmoja wa Wananchi.

Aidha Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashir Abdallah amethibitisha kushambuliwa kwa mwenyekiti huyo. Hivyo ameliomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi maeoneo yote na kuwahi kwa wakati pindi tukio linapotokea popote. Abdallah amesema kuwa Polisi wamekuwa wakichelewa katika eneo la tukio pale wanapopigiwa simu za haraka hivyo kuna haja kubwa ya jeshi hilo kulifanyia kazi suala hilo.

“Ndo Maana kukaundwa kanada Maalumu Tarime Rorya siyo kwa sababu ya vita vya koo ni pamoja na kulinda wananchi na mali zao ili wananchi wasiishi kwa hofu,” amesema Diwani.

Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashir Abdallah akiwa katika Hospitali ya Mji wa Tarime akijulia hali ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugosi Zacharia Chacha Ghati aliyevamiwa na Vibaka na kushambuliwa na Vitu Vyenye Ncha kali zikiwemo Nondo na Vilungu na kumsababishia Maumivu Makali.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugosi kata ya Nyamisangura Zacharia Chacha Ghati akiwa amelazwa katiko Hospitali ya Mji wa Tarime Mkoani Mara kwa ajili ya Matibabu.
Chacha Masero Mkazi wa Bugosi akisimulia juu ya tukio hilo kwani alikuwa na Mwenyekiti kabla ya kutokea kwa tukio hilo.
Diwani wa kata ya Nyamisangura Bashiri Abdallah akidhibitisha uwepo wa Tukio hilo katika kaya yake huku akiomba jeshi la Polisi kujimalisha ulinzi.

Prof. Kamuzora Akagua Ujenzi wa chumba kitakacho toa huduma za Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa taarifa za ardhi (ILMIS) Kinondoni

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora (Sera na Uratibu) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni wakati wa ziara fupi kukagua ujenzi wa chumba kitakachokuwa kinatoa huduma za Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa taarifa za Ardhi (ILMIS)  katika Mradi wa Mfano Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Katibu  Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora (Sera na Uratibu) akizungumza na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta wakati wa ziara fupi  kukagua ujenzi wa chumba kitakachotumia Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa taarifa za Ardhi (ILMIS) katika Mradi wa Mfano Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora (Sera na Uratibu) akioneshwa namna jalada ambalo taarifa zake tayari zimeshafanyiwa kazi na mfumo huo linavyoonekana katika Mradi wa Mfano unaotekelezwa katika Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Picha na Ofis ya Waziri Mkuu

BALOZI WA TANZANIA NCHINI AFRIKA KUSINI AKUTANISHA WATANZANIA WAISHIO HUKO, AWAONGOZA KUUNDA JUMUIYA YAO

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Sylvester Mwakinyuke Ambokile Jumamosi Juni 23, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Watanzania wanaoishi nchini humo, na kuwaongoza katika kuunda umoja wao kwa mara ya kwanza, kwenye mkutano uliofanyika ubalozini jijini Pretoria.
"Sisi leo tulikuwa tunakutana na watanzania wa Afrika kusini. Ndugu zetu hawa walikuwa hawana umoja wao wa kuwaunganisha. Na ndiyo tunakutana kuujadili umoja huo ambao nimesaidia  kuaandikishwa rasmi serikalini. Umoja huo unaitwa Tanzanian  community in South Africa  (TACOSA)", Balozi Ambokile aliiambia Globu ya Jamii kwa njia ya mtandao usiku wa kuamkia leo.
Amesema ubalozi uliamua kuchukua hatua hiyo kwa kuzingatia kwamba Watanzania wengi wanaishi nchini Afrika Kusini, wengi wao wakiwa wanafunzi, wafanyabiashara na wafanya kazi lakini walikuwa hawana umoja wa kuwaunganisha  kwenye masuala mbalimbali yanayopaswa kufanywa na wana-Diaspora. 
Balozi Ambokile amesema kwamba kwa umoja huo, sasa Watanzania waishio Afrika Kusini watakuwa na fursa ya kuwa pamoja na kusaidiana katika shida na raha, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kila mmoja wao alikuwa akifanya mambo yake kivyake.
"Hii itaturahihishia pia kuwakusanya  pamoja katika masuala ya misiba, harusi, sherehe za Kitaifa na mengineyo kama wafanyavyo Watanzania walio katika nchi zingine" alisema Mhe. Balozi.

 Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Sylvester Mwakinyuke Ambokile Jumamosi akizungumza na Watanzania waishio nchini humo kwenye mkutano uliofanyika Jumamosi Juni 23, 2018 ubalozini jijini Pretoria. Pamoja naye ni viongozi walioteuliwa kuongoza Tanzanian community in South AfrCoica (TACOSA)
 Sehemu ya watanzania waishio nchini nchini Afrika Kusini wakiwa kwenye mkutano uliofanyika Jumamosi Juni 23, 2018 ubalozini jijini Pretoria.
Watanzania waishio nchini nchini Afrika Kusini wakiwa kwenye mkutano wao na balozi uliofanyika Jumamosi Juni 23, 2018 ubalozini jijini Pretoria.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Sylvester Mwakinyuke Ambokile Jumamosi akiendelea kuzungumza na Watanzania waishio nchini humo kwenye mkutano uliofanyika Jumamosi Juni 23, 2018 ubalozini jijini Pretoria.

MICHUZI TV: WATANZANIA WATAKIWA KUTOBAKI NYUMA KUSHUHUDIA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA

Viewing all 109978 articles
Browse latest View live




Latest Images