Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

DIRA YA DUNIA IJUMAA 22.06.2018


Tanzanian Youth Focus Group Diaspora meet in massachusetts

$
0
0
Tanzanian youth from Western MA, came together in Downtown Springfield, MA, inside Make-it Springfield, and held a focus group. The purpose was to brainstorm ideas on how to resolve issues and provide resources to help strengthen their community. The focus group was organized by Cecelela Tomi, Zulfiqar Manzi, Abdul Kibodya, and Mimi Mgawe.  This was also an opportunity for youths to have open dialogue on questions that were conducted by the organizers. A lot of positivity came out from the focus group.  

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MISS MBEYA 2018 WATEMBELEA SHIRIKA LA TTCL ,WAVUTIWA NA TENDAJI WAKE.

$
0
0
Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa shirika la mawasiliano Tanzania TTCL ,Juvenal Utafu amewataka washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2018 ngazi ya mkoa wa Mbeya (Dream Miss Mbeya 2018), kuhakikisha wanatumia urembo wao kama nguzo ya kuzifikia ndoto zao.

Meneja huyo amebainisha hayo baada ya Walimwende hao waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora ya mashindano hayo, kutembelea afisi za shirika hilo kanda ya nyanda za juu kusini kwa lengo la kutambua mambo mbalimbali yanayo husu TTCL, ikiwa ni pamoja na namna ya uhifadhi wa taarifa za watumiaji wa huduma za mawasiliano. 

Utafu amesema kwamba Ulimbwende ni moja ya njia za kuonesha mchango katika jamii, lakini hilo litafanikiwa ikiwa walimbwende hao watajitambua na kusimama vema katika nafasi zao. “Ni lazima mtambue ya kwamba mna deni kubwa kwa taifa, la kutoa mchango chanya katika nyanja mbalimbali, hasa katika hali ya sasa ya dunia ya utandawazi na mapinduzi ya sekta ya mawasiliano”, aliongeza Utafu. 

Kwa upande wake Meneja msaidizi biashara wa TTCL mkoa wa Mbeya Charles Mwita, alisema kuwa amefarijika sana kwa kauli mbiu ya mashindano hayo isemayo “urembo na kazi kwa maendeleo ya jamii”, na kuwapa changamoto walimbwende hao kwamba hawana budi kuitekeleza kauli mbiu hiyo kwa vitendo. 

Juni 29 mwaka huu ni fainali za mashindano ya Dream Miss Mbeya 2018 yenye lengo la kumpata mlimbwende atakayevikwa taji la Mrembo wa mkoa wa Mbeya (Miss Mbeya 2018). Aidha mshindi huyo wa kwanza ataungana na washindi wengine akiwemo mshindni wa Pili na tatu kuuwakilisha mkoa wa Mbeya katika mashindano ya ngazi ya kanda yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao, kuwatafuta wawakilishi wa kanda ya nyanda za juu kusini katika mashindano ya urembo ngazi ya taifa. 

Mashindano ya Dream Miss Mbeya 2018 yameandaliwa na redio Dream FM ya jijini Mbeya kwa udhamini wa TTCL Corporation, PII Limited, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Ally Rich Sanaa Arts Limited, Kalulu Safari’s Tours Co. Limited, Pepsi, Paradise Inn Hotel, Michuzi Blog, Michuzi Tv, na Dorcus Beauty Point.
Afisa huduma kwa wateja wa TTCL Corporation Bi Niva Mkwe akiwaelezea washiriki wa Dream Miss Mbeya 2018 huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo.

Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa TTCL Corporation Juvenal Utafu akizungumza na washirki wa Dream Miss Mbeya 2018 walipomtembelea ofisini kwake Jijini MbeyaMeneja msaidizi-biashara wa TTCL Corporation Mkoa wa Mbeya Charles Mwita akiwaelezea washiriki wa Dream Miss Mbeya 2018 huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo


RC PWANI ALIAGIZA SHIRIKA LA VIWANGO NCHINI KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI KUDHIBITI UBORA

$
0
0
NA Linda  Shebby, Kibaha Pwani

MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Everist Ndikilo amewataka uongozi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), kutokukaa maofisini na kusubiri wafanya biashara wawapelekee bidhaa zao wanazozizalisha kwani wanaweza kufanya udanganyifu hivyo kuweza kujipatia sifa ya ubora ambao hawakustahili.

Ndikilo amesema kuwa anategemea kuona bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Mkoa wa Pwani na nchi nzima kwa ujumla ziwe zinakidhi viwango vya ubora unaostahiki,kuzalisha bidhaa bora na zitakazoweza kuleta ushindani kwenye masoko yetu yote ya ndani na nje ya nchi.

Amesema kuwa ili kuitekeleza azma ya Uchumi wa Viwanda kwa ukamilifu ametoa rai kwa wenye viwanda na wazalishaji nchini kote kuzalisha bidhaa kwa kutumia vipimo stahiki ili kuweza kukidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa na kuweza kungia kwenye ushindani wa masoko ya Kimataifa.

 Ndikilo amesema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) bado kunachangamoto nyingi kama vile umbali mrefu kutoka ofisi za Kanda hadi Mkoa na hivyo kusababisha baadhi ya wafanyabiashara kushindwa kupata huduma kwa urahisi, huku upimaji huo umekuwa ukichukua muda mrefu hali inayosababisha kuendelea kuzalisha bidhaa zisizo na uthibitisho.

Hivyo amewataka TBS kufungua matawi ya ofisi zao kwenye Mikoa ikiwa ni katika kurahisisha huduma zao kwani zitasaidia kupunguza gharama kwa wafanyabiashara kwa lengo la kuongeza ubora wa bidhaa.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani amesema hayo wakati alipokua akifungua ,mafunzo ya vipimo ya siku moja yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani ambayo yameadhimishwa Mkoani Pwani leo.

Huku katika historia siku hii ya Vpimo Duniani huadhimishwa kila ifikapo Mei 20 kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kusainiwa kwa makubaliano ya kutumia vipimo vinavyofanana duniani kote ambayo yalifanywa kutoka mataifa 17 duniani, tarehe 20 Mei 1875.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Everist Ndikilo aakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Viwango nchini (TBS),mara baada ya kumaliza kikao chao mkaoni humo. 

Askari wapya 2,081 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wahitimu mafunzo ya awali ya kijeshi

$
0
0
Na Ripota Wetu, Arusha 
 MKUU wa Mafunzo na Utendaji wa kivita wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Meja Jenerali Alfredy Kapinga amewataka askari wapya 2,081 kuhakikisha wanakuwa na utii, uaminifu na uhodari kwani huo ndio msingi wa jeshi. 
 Hayo aliyasema mjini Arusha wakati wa kufunga mafunzo ya kundi la 38 B la mwaka 2017 lenye askari wapatao 2,081 waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya kijeshi katika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha ambapo mafunzo hayo yalifungwa Juni 22, mwaka huu. 
 Akizungumza kwenye sherehe hizo Meja Jenerali Kapinga amewataka vijana hao kutambua tayari wameiva kuwa askari na hivyo wapo tayari kutumika mahali popote na masuala ya longolongo kwa sasa hayapo tena. 
 “Jukumu kubwa mbele yenu ni kulinda nchi dhidi ya maadui wan je na ndani, kulinda mipaka na shughuli za kijamii mtakazokuwa mmepangiwa endapo mtahitajika,” amesema Meja Jenerali Kapinga. 
Katika hotuba yake hiyo amewataka pia wazazi nchini kuwaacha vijana hao wafanye kazi ya jeshi kwani wamekabidhiwa dhamana kubwa kwa taifa hivyo kitendo cha kuendelea kuwachukulia kama watoto si sahihi. 
 “Hawa tayari ni askari, tumewapokea tutawatunza na kuwafundisha maadili mema kwa taifa, ile mbereko ya kuwabeba sasa mziache hawa ni askari,” amesema Meja Jenerali Kapinga. 
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya awali ya kijeshi Kihangaiko (RTS), iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani Kanali Sijaona Myala akizungumza kwenye sherehe hizo aliwataka wazazi kuacha kusikitika pindi watoto wao wanapopangwa kwenda nje ya nchi. 
Naye Mkuu wa Kikosi cha 883 KJ Oljoro Luteni Kanal i Christopher Kavalambi alisema miongoni mwa wahitmu hao wamo pia wanariadhara 10 na wanamichezo mingine ya mpira wa pete na ngumi. Amewataja baadhi ya wanartiadhara waliomaliza mafunzo hayo ya awali ya kijeshi ni pamoja na Alphonce Simbu na Emmanuel Giniki. 
Sherehe hizo za kuhitimu mafunzo zilishereheshwa na kwa gwaride la kuhitimu mafunzo na maonyesho ya vikundi mbalimbali yaliyoandaliwa na kuruta waliohitimu mafunzo yao na kuwa askari.
 Askari wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakitoa heshima wakati wa Gwaride lao la kumaliza mafunzo ya wali ya kijeshi yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha
 Askari wakionyesha moja ya maonyesho ya ukakamavu wakati wa kufunga mafunzo yao ya awali ya kijeshi yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha
 Askari hao wakionyesha sehemu ya maoezi ya ukakamavu wakati wa Gwaride la kumaliza mafunzo yao ya awali yaliyokuwa yakifanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha 
 Askari wapya wakionyesha sarakasi wakati wa gwaride la kufunga mafunzo yao yaliyofanyika Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha 
Mkuu wa mafunzo na utendaji wa kivita Jeshini Meja Jenerali Alfredy Kapinga akikagua Gwaride la askari 2,081 la askari wapya wa JWTZ waliomaliza mafunzo yao Shule ya Mafunzo ya awali ya Kijeshi Kihangaiko (RTS), iliyoko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo mafunzo hayo yalikuwa yakitolewa Kikosi cha 833 KJ Oljoro mkoani Arusha.

IGP SIRRO AFANYA UKAGUZI POLISI OYERSTEBAY

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na baadhi ya wananchi nje ya Kituo cha Polisi cha Oyesterbay jijini Dar es Salaam leo, wakati alipofanya ukaguzi katika kituo hicho. Picha na jeshi la Polisi.

MABAO YA AHMED MUSSA YAIPELEKA NIGERIA NAFASI YA PILI KUNDI D MICHUANO KOMBE LA DUNIA

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 
 KAMA noma na iwe noma !Ndivyo unavyoweza kuuelezea mchezo kati ya Nigeria dhidi ya Iceland ambapo mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji machachari wa Nigeria 'Nigeria Super Eagles' Ahmed Mussa kuwafanya mashabiki wa soka Afrika kuungana na kushangalia ushindi mnono ambao wameupata. 
Katika mchezo huo ambao Nigeria wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Iceland wanaotoka katika taifa ambalo idadi yake ya watu ni 350,000.Mechi imechezwa katika Uwanja wa Volgograd Arena.Kwa sasa Nigeria inajipanga kwa mchezo wake ujao dhidi ya Argentina ambayo juzi ilipoteza mchezo wake kwa kufungwa mabao matatu. 
Yote kwa yote ukweli utabaki kuwa ushindi wa jana wa Nigeria ni kama vile umeifanya kikosi hicho na Bara la Afrika kuamka kutoka usingizini na kutambua nini ambacho kimewapeleka kwenye michuano ya Kombe la Dunia ambayo inaendelea nchini Urusi. 
 Ufundi, umaridadi na matumizi ya akili nyingi yaliyotosha kuifanya Nigeria kuonekana kutawala licha ya mchezo kuwa na ushndani wa hali ya juu hasa kwa kuzingatia kikosi cha Iceland ambacho kwa sehemu kubwa wachezaji wake kuwa ni madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu hakuwa nyuma kwani walionesha soka la uhakika. 
Kasi ya mchezo huo ulikuwa kibwa na takwimu za kosoka zinaelezea iwapo wangekuwa ni kukimbia basi hadi dakika ya 80 ya mchezo wachezaji walikuwa wamekimbia kilometa 47.Hivyo unaweza kupata picha ya kasi ya mchezo huo ambapo pamoja na kila aina ya ufundi kwa kila mchezaji hadi unalizika shangwe zikawaka kwa Afrika. 
Unajua mshambuali wa Nigeria Ahmed Mussa kafanya nini cha ziada? Iko hivi mabao yake mawili yamesababisha kubadilsha muundo wa kundi D ambapo sasa yanaonesha Nigeria iko nafasi ya pili ikiwa na alama tatu. Katika mchezo huo kikosi cha Iceland kilipata penati dakika ya 83 lakini kiungo na mshambualiji wake Gylfi Sigurdsson alipaisha mkwaju wa penati hiyo.Hivyo hadi mchezo umalizika Nigeria 2-1. 
Michuzi TV kwa kukumbusha tu kikosi cha Nigeria ambacho kimeshinda mchezo wa jana kilikuwa ni tofauti kidogo na kile kilichocheza katika mchezo wa kwanza na matokeo yakawa ni kwa Nigeria kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Croatia.
Jana wafungaji wanaoichezea Leicester City Ahmed Musa na Kelechi Iheanacho walianza kuchezeshwa kwa mara ya kwanza katika mechi ya kombe hilo na uwepo wao umeifanya timu yao kuonekana mahiri kwa kutawala soka. 
Wakati huo huo kivuti katika mchezo kati ya Brazil dhidi ya Costa Rica, kivutio kilikuwa kwa mshambuliaji wa Brazil Neymar ambaye aliamua kuangalia kilio uwanjani baada ya mchezo kumalizika. Brazil iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kati ya mabao hayo ya Brazil moja limetiwa wavuni na Neymar bao lake la ufundi likaibua shangwe kwa mashabiki wa soka wa nchi hiyo. Hata hivyo kitendo cha kulia uwanjani ndicho kilioneka
na kuvutia zaidi na watu kutaka kufahamu nini ambacho kimemliza. Alipoulizwa kwanini amelia uwanjani amejibu hiyo inatokana na hisi alizonazo baada ya kuwa majeruhi kwa miezi mitatu akiwa nje ya uwanja.

Tuzo ya Kiswahili ya Heshima ya Shaaban Robert kuanza kutolewa mwakani

$
0
0
                   Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Tuzo ya Kiswahili ya Heshima ya Shaaban Robert inategemea kuanza kutolewa mwaka 2019 na Kampuni ya Maendeleo ya Kiswahili (KIDE - MAKI) kwa watu mbalimbali wanaoendelea kuienzi na kuikuza lugha ya Kiswahili.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amethibitisha hayo leo kwenye uzinduzi wa kumbukizi ya Shaaban Robert na Tamasha la Ustaarabu wa Mswahili uliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Chuo cha Mt. John jijini Dodoma.
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa tuzo hizo zitatolewa katika tamasha Kubwa la ‘Ustaarabu wa Mswahili’ litakalokuwa likifanyika kwa siku tatu za mwezi Januari kila mwaka. 
“Tuzo hizo zitatolewa katika kilele cha tamasha hilo ambapo watu na taasisi mbalimbali zilizojipambanua kipekee katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili zitatunukiwa”, alisema Dkt. Mwakyembe. 
Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau wa lugha ikiwemo Kampuni hiyo katika mambo yanayolenga kukuza, kueneza na kuendeleza lugha nchini. Pia amefafanua kuwa juhudi hizo ni moja ya utekelezaji wa sera hivyo kinachotakiwa sasa ni ubidhaishaji wa lugha ya Kiswahili ili kiendelee kuleta manufaa na kuongeza tija kwa wananchi. 
Akiongelea kuhusu Kumbukizi ya Hayati Shaaban Suleimani Juma Ufukwe (Shaaban Robert), Dkt. Mwakyembe amesema kuwa juhudi zake zimechangia sana kukua kwa lugha ya Kiswahili ambapo kwa hivi sasa ni lugha ya 10 kati ya lugha 6000 zinazozungumzwa duniani.
“Chemchem za mawazo yake, tifutifu za mielekeo yake, mboji za maarifa na mafunzo ya nguli na jabali wa Fasihi ya Kiswahili bado yanatuongoza vema hata leo katika maono ya nchi yetu ya kuwa na uchumi wa kati kupitia Tanzania ya viwanda”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha katika kumbukizi hiyo, Waziri Mwakyembe amezindua kitabu cha “Historia ya Kiswahili kwa Mtazamo Mpya” kilichotungwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo ambaye amebobea katika uandishi wa vitabu vya kifasihi, Prof. David Massamba.
Kitabu hicho kinatoa ufafanuzi wa kina kuhusu historia na asili/chimbuko la lugha ya Kiswahili na Waswahili na kuziba mapengo ya kuwepo kwa mkanganyiko au ukinzani wa wanazuoni mbalimbali kuhusu historia na asili  ya lugha ya Kiswahili na Mswahili ambao umedumu kwa muda mrefu sana. 
Shaaban Robert alikuwa ni mwandishi nguli wa vitabu vyenye maudhui mbalimbali vikiwemo vya Kusadikika, Kufikirika pamoja na Adili na Nduguze, alizaliwa Januari Mosi, 1909 na kufariki June 22,1962.

DK. KIGWANGALLA ATIMUA WAVAMIZI KWENYE PORI LA AKIBA SWAGASWAGA

$
0
0


Video
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga. 

Na Hamza Temba-WMU-Chemba, Dodoma

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wananchi waliovamia Pori la Akiba Swagaswaga na kuendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, makazi na ufugaji ndani ya pori hilo kinyume cha Sheria waondoke mara moja kwa hiari yao kabla ya kuondolewa kwa nguvu.

Ametoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Handa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutatua mgogoro wa ardhi kwenye hifadhi hiyo wilayani humo.


"Tunawapa siku 30 muanze kutoka wenyewe, baada ya siku 30 tunatoa notisi ya siku nyingine 30 za kutumia nguvu, kwahiyo kuanzia sasa hivi anzeni kujipanga wenyewe na kuondoka wakati Halmashauri ikifanya tathmini ya maeneo ya vijiji ambavyo ni halali ya kuwagawia kwa wale watakaopenda kupewa maeneo huko", alisisitiza Dk. Kigwangalla.


Alisema sheria za uhifadhi haziruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya maeneo ya hifadhi na kuendesha shughuli za kibinadamu na kwamba kufanya hivyo ni kudharau Sheria na Malmlaka zilizopo.


Alisema kwa upande wa wananchi wa kijiji cha Handa ambacho kilianzishwa kimakosa ndani ya pori hilo wataendelea kubaki mpaka pale wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Tamisemi na Ardhi zitakapoamua hatma yao ikiwemo ama kulipwa fidia kupisha eneo hilo au waendelee kubaki na mipaka ya hifadhi isogezwe.


Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kujenga miundombinu ya kuvuta maji kutoka katika chemchem iliyopo ndani ya hifadhi hiyo na kuyasogeza kwenye makazi ya wananchi ili kulinda chanzo hicho kwa kuzuia uharibifu unaofanywa na wananchi wanaofuata huduma katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Handa katika wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana, alipotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kutatua mgogoro kati yake na Pori la Akiba Swagaswaga.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga akizungumza katika mkutano huo.
Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia akizungumza katika mkutano huo katika kijiji cha Handa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma jana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MINISTER MAHIGA’S DAY VISIT TO ROMANIA; SIGNS AN MOU FOR BILATERAL CONSULTATIONS

$
0
0
Tanzania’s foreign minister Hon. Dr. Augustine Mahiga, and his Romanian counterpart Hon. Teodor Melescanu have signed a Memorandum of Understanding, redefining bilateral relations that exist between Tanzania and Romania in Bucharest. 
The two leaders held extensive talks prior to the signing ceremony which was held at Ministry of Foreign Affairs in Bucharest in front of members of the press. The timely signing came at a time when the two parties are working to establish strong economic ties, with different nations around the world.  
The signed MoU between the two countries’ Foreign Ministries provides a platform to hold regular strategic consultations on political, economic, commercial, scientific, technical and cultural aspects of bilateral relations, regional and international matters.
The platform is envisaged to further develop and strengthen friendly relations while increase mutual understanding and cooperation between Tanzania and Romania.
“During the liberation struggle of Africa, many Tanzanian students came to Romania to study medicine and pharmaceutical. With the signing of this MoU, now Romania and Tanzania are strategic partners. We anticipate diversification in the area of training and capacity building to include new sectors such as agronomy for Tanzanian students” Hon. Mahiga remarked. 
Hon. Melescanu explained that ever since the new Government of Romania came into leadership one year ago, the focus has been to re establish relations and partnerships with countries outside Europe. 
“But Tanzania and Romania have been friends for the longest time, and we witnessed many of your colleagues receiving education in Romania. The number kept decreasing year after year due to the closing of our embassy in the 90’s. I believe now things will be better, for our people” announced Foreign Minister Melescanu. 
Diplomatic relations between the two countries were established on 5th May 1964. The relations were very active until 18th November, 1999, when the government of Romania closed its embassy in Dar es Salaam, due to financial difficulties. The relations were mainly based on education particularly scholarship to Tanzania students. 
The platform for political discussions will provide an opportunity to discuss both priority issues, including migration issues, business opportunities, investments, various development projects, capacity building and tourism promotion.
Hon. Mahiga and his delegation, made a one-day visit to Bucharest on their way back to Tanzania after concluding another working visit in the region. Permanent Secretary of Romania Foreign Ministry is also expected to visit Tanzania as a follow up of this signed MoU within the coming month. 

 Tanzania’s foreign minister Hon. Dr. Augustine Mahiga, and his Romanian counterpart Hon. Teodor Melescanu have signed a Memorandum of Understanding, redefining bilateral relations that exist between Tanzania and Romania in Bucharest. 
 Tanzania’s foreign minister Hon. Dr. Augustine Mahiga, and his Romanian counterpart Hon. Teodor Melescanu after signing the Memorandum of Understanding, redefining bilateral relations that exist between Tanzania and Romania. 
 Tanzania’s foreign minister Hon. Dr. Augustine Mahiga, and his Romanian counterpart Hon. Teodor Melescanu have signed a Memorandum of Understanding.
Tanzania’s foreign minister Hon. Dr. Augustine Mahiga, and his Romanian counterpart Hon. Teodor Melescanu shake hands after signing the  Memorandum of Understanding

TRC RELI TV: Zoezi la Kuhamisha Makaburi kupisha Ujenzi wa Reli ya SG

WAKAZI MKOA WA PWANI WATAKIWA KULINDA MIRADI INAYOJENGWA

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

WAKAZI wa Rufiji mkoani Pwani wametakiwa kulinda miradi inayojengwa ili kupata wataalam wengi watakaoisaidia Serikali.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana baada ya kukagua majengo ya kisasa yaliyojengwa Kijiji cha Dohatul Khayr kupitia Taasisi ya Alat'a Chartable Foundation Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema mradi huo utasaidia kupata wataalamu mbalimbali.

"Mradi huu ni mkubwa kwa wilaya ya Rufiji utasaidia kupata wataalamu na wengi watakaoisaidia Serikali kwenye kazi mbalimbali za kimaendeleo," amesema Ulega.Ameongeza kuwa Wilaya za Mkuranga, Rufiji na Kibiti ziko nyuma kimaendeleo hivyo miradi inayoanzishwa itawawezesha kuhimiza maendeleo na kuzalisha wataalamu.

Mfadhili wa mradi huo kutoka Qata Nusser Al Khal amesema miradi huo ni miradi kwanza kwa Tanzania kujengwa kwa ufadhili ambapo umehusisha nyumba 32,kituo cha afya na msikiti.

"Miradi huu wa kwanza umegarimu Sh.bilioni 1.3 ambapo umehusisha nyumba ya ibada,hospital na nyumba 32 ambapo miradi utakaofuata utajenga majengo ya taaluma," amesema All Khal.

Kwa upande wa Shekh wa Wilaya ya Rufiji Othmani Kaporwa amesema kujengwa kwa miradi hiyo itawasaidi wakazi wa maeneo hayo.Wafadhili hao pia wanajenga mradi mkubwa katika jimbo la Mkuranga ambapo itakuwa na nyumba zaidi ya 30, shule ya msingi, sekondari na chuo cha ufundi.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Rufiji kwa niaba ya Waziri Mkuu katika hafla ya ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (alievaa koti) kwa niaba ya Waziri Mkuu akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega akikagua bweni la kulala watoto yatima na wanaoIshi katika mazingira magumU kwa niaba ya Waziri Mkuu katika ufunguzi wa kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wa pili kulia alievaa koti akiwa pamoja na waumini wengine katika ibada ya Ijumaa katika msikiti uliopo ndani ya kijiji hicho.
Muomekano wa wa majengo pamoja yaliyopo katika kijiji cha Dohatl Khayr.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abdallah Ulega akiwa ameambatana na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa kukagua majengo yaliyo jengwa katika kijiji cha Dohatl Khayr jana mkoa wa pwani.

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK

KAMPUNI YA MINET GROUP YAZINDUA JH MINET TANZANIA,YAAHIDI HUDUMA BORA ZA BIMA

$
0
0
KAMPUNI ya Aon kupitia Minet imezindua rasmi JH Minet Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa safari iliyoanza 1998 ikiwa inatoa huduma za bima pamoja na mafao.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Minet Group Joe Onsando amesema kuwa kampuni hiyo mpya itakuwa chini Aon na hakuna kazi itakayopotezwa baada ya mabadiliko hayo.

Amesema  kuwa Minet  ni kampuni inayoaminika  kote Afrika na nje ya bara hilo na wafanyakazi wa Aon ambayo sasa itajukulikana Minet katika nchi hizo na viongozi wao ambao wana ujuzi katika masuala ya viwanda wataendelea kuwa nafasi kama watendaji katika utoaji wa huduma.Onsando ameeleza kuwa mwaka 1997  kampuni hiyo ya  JH Minet ilibadilishwa na kuwa Aon Minet na wanaendelea kujenga uchumi imara Afrika na itaendelea kuwa sehemu ya Aon katika utendaji kazi wao.

Onsando amefafanua kuwa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo hazitabadilika katika sekta zote kama vile kilimo, madini na mawasiliano.Pia amesema wanafurahishwa na namna uwekezaji unavyoendelea na kukua barani Afrika na wataendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao kwa sasa na baadaye.

Viongozi wa kampuni ya Minet wakizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa kufanya mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
Baadhi ya viongozi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya bima na mafao ya MINET wakisalimiana na baadhi wageni waalikwa waliofika kushuhudia mabadiliko ya jina la kampuni hiyo. 
Baadhi ya viongozi wa kampuni inayojihusisha na masuala ya bima na mafao ya MINET wakisalimiana na baadhi wageni waalikwa waliofika kushuhudia mabadiliko ya jina la kampuni hiyo.
Wageni waalikwa walioshiriki uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET wakifuatilia tukio hilo ambalo limefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Mwanamuziki maarufu barani Afrika Vyone Chaka Chaka akisakata rumba na baadhi ya wageni waalikwa kwenye tukio la uzinduzi wa jina jipya la Kampuni ya MINET.

WANAWAKE CHEMBA WAHIMIZWA KUTUMIA VEMA FURSA WANAZOZIPATA KATIKA JAMII

$
0
0

Na Shani Amanzi, Chemba.

OFIS Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chemba mkoani Singida Mwatumu Doso amewataka wanawake watumie vema fursa wanazozipata kwa kuwa wao ndiyo kioo katika jamii hasa katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo za uongozi wanazopewa katika jamii.

Doso ametoa kauli hiyo kwenye ufungaji wa Mafunzo ya Uongozi yaliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Juni 19 hadi Juni ,mwaka huu wilayani Chemba.Mwatumu amesema "kwa muda wa miongo kadhaa iliyopita,wanawake wametokea kuwa wenye juhudi nyingi katika masuala ya jamii zao.

"Lakini kumekuwepo na changamoto mbalimbali zinazowakwamisha ndiyo maana Serikali pamoja na Sekta Binafsi zinajitahidi kuwashika mikono wanawake ili wapate maendeleo."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la UFUNDIKO (Ufundi na Uhandisi Kongwa) Saidi Panga amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanawake katika uongozi bora na kujua majukumu yao ya msingi katika Uongozi na kuweza kujua uhusiano uliopo kati ya Viongozi na Wanaongozwa.

"Uongozi usio rasmi mahali popote una umuhimu wake na viongozi wanapotenda shughuli zao hivyo kiongozi anawajibu wa kutambua kuwepo kwa taasisi zisizo rasmi."Na kufanya kila njia kuzitumia katika kufanikisha malengo yake au ya Halmashauri kwa hiyo ni wajibu wa Viongozi kutumia njia sahihi za Uongozi,"amesema Panga.

Katika mafunzo hayo yalishirikisha vijiji 12 ambavyo ni Tandala,Kidoka,Mondo,Goima ,Kilema Balai,Lahoda,Lalta,Jangalo,Kwamtoro,Gwandi,Mrijo Chini na Makorongo ambapo katika kila kijiji kilileta wahusika wanawake watano ambapo wapo kwenye makundi matatu likiwemo kundi la kwanza wahusika watatu kutoka kamati ya maji ya kijiji ,kundi la pili ni Muuguzi wa Zahanati na kundi la tatu Kiongozi mmoja wa kijiji.
Picha ya pamoja ya Washiriki wa Mafunzo wakiwa na Mwezeshaji wao Mkurugenzi wa Shirika la UFUNDIKO (Ufundi na Uhandisi Kongwa) Saidi Panga .



MANISPAA YA ILALA YAZIFUNGA MAABARA BUBU,MADUKA YA DAWA

$
0
0
Na Heri Shaaban .

MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imezifungia maabara bubu na maduka ya dawa yasio na sifa ambayo yanatoa huduma kinyume cha sheria. Oparesheni ya kuzifungia maabara hizo pamoja na maduka ya dawa imeanza Dar es Salaam jana katika Jimbo la Segerea, Ukonga na Ilala.

Akizungumza jana kuhusu operesheni hiyo Mratibu wa Vituo Binafsi Manispaa ya Ilala Dk.Wille Sangu amesema maduka ya dawa ambayo wanayafungia ni ambayo wahudumu wake hawana sifa za kuendesha huduma hiyo na wengine wanatoa huduma za kuwachoma sindano wateja tofauti na kibali chao.

"Ofisi ya Mganga Mkuu Ilala imeweka utaratibu wake kila mwaka kufanya ziara ya ukaguzi wa kuzikagua maabara bubu ambazo hazina vibali na duka za dawa mara baaada kuwakamata kuwataka wafuate taratibu za usajili ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Ilala,"amesema Dk.Sangu.Amefafanua katika oparesheni hiyo pia wameyanga maduka ya dawa waliyoyakuta watoa huduma hawana sifa na maduka mengine yakijiusisha na upimaji VVV, utoaji mimba na uchomaji sindano.

Amewataka watoa huduma wote ambao wamekamatwa kwenda ofisi za Manispaa ya Ilala kwa ajili ya taratibu .Dk.Sangu amewataka wananchi watumie vituo vya tiba kwa ajili ya matibabu ya maabara kwa ajili ya vipimo na maduka ya dawa kwa ajili ya kununua dawa."Ukikuta duka la dawa linatoa tiba au huduma za maabara ni hatari kwa afya yako na toa taarifa kwetu,"amesisitiza.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dk. Emily Lihawa amewataka wamiliki wa vituo vya kutolea huduma katika wilaya hiyo, wafuate miongozo yote ya hutoaji huduma ya afya. Pia amewataka wamiliki watoe huduma kulingana na vibali vyao wasikiuke kanuni,kikubwa wafuate miongozo ya kukinga na kuthibiti maambukizi wakati wa utoaji huduma za afya. Katika ziara hiyo ilifungia maabara bubu na Zahanati Kiwalani, Tabata, Kivule na Minazi Mirefu.

 Mratibu wa vituo Binafsi MANISPAA ILALA ,Dkt Wile Sangu akifungia Maabara Bubu na vituo  bubu Kijiwe Samri Kiwalani kwa kosa la kutoa huduma bila kibali, katika oparesheni endelevu ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam jana (PICHA NA HERI SHAABAN)

TRA YAWAPIGA MSASA WATENDAJI WA HALMASHAURI NA WAFANYABIASHARA WADOGO MKOANI NJOMBE

$
0
0
Na Mariam Mwayela,Njombe

Watendaji wa Halmashauri pamoja na wafanyabiashara wadogo wa Mkoa wa Njombe wameelimishwa juu ya urasimishaji wa wafanyabiashara hao ili waweze kutambulika rasmi na kuchangia pato la taifa ikiwa ni katika muendelezo wa Kampeni ya utoaji wa Huduma, Elimu na usajili wa walipakodi wapya.

Akizungumza wakati wa semina kwa watendaji na wafanyabiashara hao wilayani Njombe na Makambako, Mkuu wa Wilaya ya hiyo Bi. Ruth Msafiri amewataka wafanyabiashara hao kuchangia mapato ya Serikali kwa kulipa kiasi cha kodi watakachopangiwa ili kuweza kusaidia kuboresha miundombinu pamoja na huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo shule, huduma za afya, maji safi na salama, umeme pamoja na barabara.

“Tukumbuke kuwa, kila kitu tunachokifanya kinahitaji fedha kwa mfano kuwa na miundombinu na wataalam wa kutoa huduma za afya ni gharama, kuwa na shule pamoja na sehemu safi za kufanyia biashara ni gharama pia. Hivyo basi, kila mmoja achangie kwa kulipa kodi ili kuweza kuendeleza huduma hizi muhimu”. Alisema Ruth.

Aliongeza kuwa, katika kutafuta maendeleo kitu kikubwa ambacho kila mwananchi anatakiwa kuwa nacho ni uzalendo, utayari na kuelewa kwamba kila mmoja ana mchango wake katika maendeleo husika.

KAMPUNI YA Infinix KUSHIRIKIANA NA GOOGLE KATIKA UZINDUZI WA SIMU MPYA BARANI AFRIKA

$
0
0
KAMPUNI ya simu ya Infinix kuzindua simu mpya ikiwa ni muendelezo wa Infinix NOTE 4 kwa kushirikiana na GOOGLE. Uzinduzi huo unategemewa kufanyika mnamo mwezi huu wa Juni barani Afrika nchini Dubai katika jengo la Burj Khalifa.

Kwa pamoja ikishirikiana na GOOGLE kampuni ya simu ya Infinix imeweka nia ya kuzindua simu iliyo na ubora zaidi ya matarajio ya wengi na inasemekana kupitia ushirika wake na GOOGLE ujio wa simu zote za NOTE kutumia mfumo wa Android 1 (A1) wenye ufanisi zaidi ya Android Oreo.


Zaidi ya watu 200 mpaka sasa wameshapata mwaliko kutoka katika kampuni hizo mbili kwenda kushuhudia uzinduzi huo pamoja na kushuhudia namna Android 1 (A1) inavyofanya kazi kupitia GOOGLE Assistant na GOOGLE Lens.


 Akiongelea mafanikio ya kampuni, muongeaji wa kampuni ya Infinix Bwana Erick Mkomoye alisema kwamba, “tangu kutambulishwa kwa kampuni ya Infinix mwaka 2013, kampuni imeweza kudhihirisha ubora wake na kuweza kupenya katika masoko ya Afrika na tuko mbioni kuwaletea teknolojia mpya kupitia simu mpya itakayozinduliwa wiki ijayo.

Muhimbili ya Kwanza Afrika Mashariki Tiba ya Kuondoa Mawe Kwenye Ini na Kogosho

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza kufanya uchunguzi na tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini na kwenye kongosho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya hadubini.

Mbali na Muhimbili kuanza kutoa huduma ya uchunguzi na kutibu wagonjwa, Kenya inatarajia kuanza kutoa huduma kama hiyo Agosti, mwaka huu.

Mpaka sasa wataalamu wa magonjwa ya tumbo na ini, wamefanikiwa kuchunguza na kutibu wagonjwa 40.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Tumbo na Ini kutoka idara ya tiba, Dkt. John Rwegasha amesema mfumo wa njia ya hadubini ni wa kisasa na kwamba unafanywa bila kufungua tumbo la mgonjwa.

Amesema kwamba mfumo wa hadibini umekuwa ukitumiwa kuchunguza na kutibu matatizo ya vivimbe na mawe kwenye ini ikiwa ni miongoni mwa mikakati wa hatua za awali wa kuelekea kwenye upasuaji wa kupandikiza ini nchini.

Pia, amesema wataalamu wa Muhimbili kwa kushirikiana na Mtalaamu Bingwa wa Upasuaji na Upandikizaji wa Ini kutoka Hospitali ya BLK India wamefanikiwa kurepea ini la mgonjwa lililopasuka ikiwa ni hatua ya msingi wa  kujenga uwezo kwa watalaamu wetu wa upasuaji.

“Tayari wataalamu wetu wa upasuaji wamefanikiwa kurepea ini lililopasuka baada ya mgonjwa kupata ajali ikiwa ni hatua ya awali kuwajengea uwezo watalaamu wetu kuelekea kwenye upasuaji mkubwa wa ini,” amesema Rwegasha.  

Akizungumzia gharama, Dkt. Rwegasha amesema kuwa gharama za kumfanyia uchunguzi na tiba kwa mgonjwa mmoja kwa matumizi ya vifaa tiba pekee ni milioni mbili na kwamba mgonjwa akitibiwa nje ya nchi ni Shs. milioni sita kwa uchunguzi na tiba ya aina hiyo kwa mgonjwa mmoja.

Amesema gharama za kupandikiza ini ni kubwa kuliko kupandikiza figo na kwamba mgonjwa mmoja anahitaji lita 20 za damu ili kufanikisha upasuaji huo.
 Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Tumbo na Ini, Dkt. John Rwegasha akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuanza mchakato wa uchunguzi na tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini na kongosho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya hadubini. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Tumbo na Ini, Dkt. Yogesh Batra kutoka Hospitali ya BLK nchini India, katikati ni Manju Sharma ambaye ni Meneja wa Uhusiano wa Kimtaifa kutoka Hospitali ya BLK. Wengine ni wataalamu wa magonjwa ya tumbo na ini.
Mmoja wa wagonjwa akipatiwa tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  tarehe 21 Juni, 2018.

BENKI YA NBC YAZINDUA MTANDAO WA NBC WAKALA KWA WATEJA WAO

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya jamii
BENKI ya NBC  imezindua ramsi mtandao wa NBC Wakala kwa wateja wao wote  na  wale wasiotumia huduma ya benki  hiyo.

NBC Wakala ni fursa  inayolenga kutoa huduma za kibenki nje ya mtandao wa matawi na mashine za kutolea fedha za ATM kwa mawakala wenye mikataba.

Akizungumza wakati wa kuzindua huduma hiyo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa benki NBC Theobald Sabi amesema benki hiyo imedhamiria kutoa huduma za kibenki kwa Watanzania na wateja wao  kuwataka kufika kwenye matawi hayo.

"Kwa Kupitia NBC Wakala wateja wetu wataweza kupata huduma za kibenki katika maeneo ambayo yako karibu zaidi kwao Kupitia mtandao wa matawi 50 na ATM zaidi ya 2000 zilizosambaa nchi nzima,  lakini kupitia NBC Wakala benki yetu inazidi kuwa karibu na wateja wake," amesema Sabi.

Sabi amesema kuwa Uzinduzi wa NBC Wakala ni moja ya mpango mkakati wa kuongeza tija na ufanisi katika kuwahudumia wateja kwa njia rafiki na kwa ukaribu zaidi ambayo ni kati ya mifumo yetu ya ugavi tunayoiwekea mkazo kwa maana inapanua wigo na mtandao wa utoaji wa huduma kwa wateja wao.

Aidha Sabi amesema kuwa huduma hiyo ya  NBC Wakala ni fursa ya kipekee kwa wajasiriamali wanaotaka kushiriki katika biashara ya utoaji huduma za kibenki,ambapo pia ametoa mwito kwa wajasiriamali wanaohitaji kushiriki katika fursa hiyo wajitokeze bila kuhofia.

Mkurugenzi huyo  ameongezea kuwa ili kuwa Wakala wa NBC, mjasiriamali atatakiwa kuwa na leseni ya biashara, sehemu ya biashara ya kudumu na awe anaendesha biashara ya kwa muda usiopungua miaka miwili.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NBC Theobald Sabi kulia na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Filbert Mponzi wakionyesha bango baada ya kuzindua huduma ya NBC Wakala jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa huduma za NBC Wakala Jacqueline Sindano (kulia) akimkabidhi  mmoja wa wakala wa NBC Wakala Humud Ali Salum mashine maalum ya POS baada ya uzinduzi wa NBC Wakala  jijini Dar es Salaam, Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi
Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki ya NBC Filbert Mponzi (kulia) akimueleza mmoja wa wakala wa NBC Humud Ali Salum(kushoto) jinsi ya kutumia mashine maalum za POS wakati wa kuzindua huduma na NBC Wakala leo jijini Dar es Salaam, Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Theobald Sabi.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images