Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live

SUDAN KUSINI NA NIGERIA WAPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUANZISHA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI KUPITIA TASAF.

$
0
0

Na Estom Sanga- TASAF.


Wataalam wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka nchini Sudan Kusini na Nigeria wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa uamuzi wake wa kukuza sekta hiyo inayolenga kuzikwamua kaya za wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na umaskini mkubwa wa kipato.


Wataalamu hao ambao wako nchini kuona namna sekta hiyo inavyotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF-ambayo inatekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini –PSSN-wamesema Mpango huo unawagusa moja kwa moja wananchi hususani wanaoishi katika mazingira ya umaskini uliokithiri.


Wamesema hamasa waliyoiona baada ya kuwatembelea baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Wilaya za Temeke,Ilala jijini Dar es salaam na Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani katika kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa zilizoko kwenye Mpango huo zimeonyesha kuwa katika kipindi kifupi cha utekelezaji wa Mpango huo maisha yao yameanza kuboreshwa.


Miongoni mwa mambo yaliyowavutia Wataalam hao ni namna TASAF inavyoshirikisha Sekta nyingine za serikali kuwafikia Walengwa na uwezo  wa Watumishi wa Taasisi hiyo katika kuwatembelea Walengwa na kuwahamasisha kufanya kazi za uzalishaji mali ili kufikia malengo na kuboresha maisha ya Walengwa hao.


Aidha suala la ujenzi wa makazi ya Walengwa kwa kutumia ruzuku wanayopata kutoka TASAF limewashangaza Wataalamu hao kwani katika maeneo waliyotembelea wamebaini kuwa Sehemu kubwa ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wamekuwa wakidunduliza fedha na kisha kununua vifaa vya ujenzi wa nyumba hususani mabati,na saruji ili kuboresha makazi yao.
 Baadhi ya Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Disunyala wilaya ya Kibaha wakiwa katika kitalu cha miche ya mboga (nyanya,pilipili hoho) wanazozalisha kwa lengo la kujiongezea kipato.
 Baadhi ya Wataalam wa sekta ya hifadhi ya Jamii kutoka Sudan Kusini wakiangalia matuta yaliyolimwa na Walengwa wa TASAF yanayotarajiwa kupangwa miche ya mboga mboga ikiwa ni mojawapo ya shughuli za uzalishaji mali ili kujiongezea kipato.
 Mmoja wa Walengwa wa TASAF akiwa amebeba sehemu ya kuku wa kienyeji anaowafuga kwa kutumia sehemu ya ruzuku anayoipata kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya maskini.
 Baadhi wageni kutoka Sudan Kusini wakiangalia tanki lililojengwa na TASAF katika kijiji cha Disunyala wilaya ya Kibaha kwa lengo la kuvuna maji ya mvua yanayotumika kumwagilia bustani ya mboga mboga ikiwa ni mojawapo ya miradi ya kuwaongezea kipato Walengwa wake. 
 Pichani ni baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka nchini Sudan Kusini wakiwa katika eneo la Shamba darasa la Muhogo lililoanzishwa na TASAF kwa lengo la kuhamasisha walengwa na wananchi wa eneo hilo kuzalisha muhogo kwa wingi kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. 
Mkuu wa wilaya ya Kibaha,Bi. Assumpta Mshama(Watatu  kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalam wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kutoka Sudan Kusini walimtembelea ofisini kwake kabla ya kwenda kukutana na Walengwa wa Mpango huo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

DKT TIZEBA ATOA SIKU 4 WAKULIMA WA MKONGE MKOANI TANGA KULIPWA FEDHA ZAO

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Tanga

Wakulima wa Mkonge Mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kupitia agizo lake alilolitoa kwa Kampuni ya Katani Limited kuhusu kulipa madeni ya wakulima ndani ya siku nne kuanzia 21 Juni 2018 hadi 26 Juni 2018 Kwa madeni ya muda mrefu ya wakulima wa zao hilo jambo lililopelekea kupunguza ufanisi na tija ya Kilimo Kwa wakulima hao.

Dkt Tizeba ametoa agizo hilo leo 21 Juni 2018 akiwa kwenye mkutano na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) unaotekelezwa kwenye mashamba matano ya Hale, Magunga, Magoma, Mwelya na Ngombezi yaliyo chini ya miliki ya Bodi ya Mkonge Tanzania. 

Katika Mkutano huu uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Martin Shigela sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe, Msajili wa Hazina, Mtendaji wa BRELA, Muwakilishi wa mwanasheria Mkuu wa serikali, Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge na wataalamu wengine; Waziri wa Kilimo Mhe Tizeba ametoa agizo hilo Kwa Uongozi wa mfumo wa Kilimo cha wakulima wadogo wa kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO), Kampuni ya Katani ltd ambayo ndio mnunuzi pekee wa Mkonge wa mkulima na Bodi ya Mkonge Tanzania.

Sambamba na agizo hilo pia Mhe Waziri ameiagiza Bodi ya Mkonge Tanzania kupitia upya mikataba yote iliyopo Kwa kushirikisha Bodi yenyewe, Kampuni ya Katani na wadau wa zao hilo haraka iwezekanavyo ili kurekebisha makosa yaliyopo.

Aidha, ameitaka Bodi hiyo ya Mkonge Tanzania kuitisha kikao na wadau wote wa zao hilo ili kupitia upya utaratibu wa makato ya mgawanyo wa mapato katika kusindika zao la Mkonge.Mhe Dkt Tizeba aliongeza kuwa hati za miliki ya mashamba zitapaswa kutolewa Kwa wahusika Mara baada ya kujiridhisha na mchakato utakapokamilika huku akiwataka wakulima kulipa malimbikizo ya kodi ya ardhi.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemaliza ziara ya siku moja ya kikazi mkoani Tanga huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela Kwa umakini na uwajibikaji katika kusimamia sekta ya Kilimo hususani zao la Mkonge mkoani humo.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akitoa maelekezo ya serikali wakati wa kikao cha pamoja na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) kabla ya mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela akizungumza jambo kabla ya kumaribisha mgeni rasmi Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kuongoza mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.
Viongozi mbalimbali Mkoani Tanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela wakiagana na Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.
Wadau wa zao la Mkonge wakichangia mada wakati wa mkutano wa wadau wa zao la Mkonge Uliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Jana 21 Juni 2018.

ROSE MBAGA ATAKA WATANZANIA KUSAIDIANA NA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA AJIRA KWA VIJANA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWEZESHAJI wa Vijana katika masuala ya maendeleo endelevu nchini Rose Mbaga amesema ikitokea akapata nafasi ya kukutana na Rais Dk.John Magufuli atamuelezea kuhusu changamoto ya ajira kwa vijana nchini.

Pia amesema katika kutatua changamoto ya ajira ametoa rai kwa Watanzania wote kushirikiana na Serikali katika kuitatua huku akisisitiza ipo haja kwa vijana kuwa na uthubutu wa kufanya mambo yanayohusu maendeleo.

Mbaga ametoa kauli hiyo jana usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akijiandaa na safari ya kwenda nchini Uingereza baada ya kutambulika kuwa miongoni mwa wanawake 100 wanaosaidia kuwainua wengine kwenye kazi za kijamii .Akiwa huko atakabidhiwa tuzo ya STAR AWARD.

"Ikitokea siku nikapata nafasi ya kukutana na Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli kikubwa nitakachomwambia ni kuhusu kuwasadia vijana na hasa wanaohitimu elimu ya juu."Kuna idadi kubwa ya vijana ambao wanahitimu elimu ya juu na changamoto yao kubwa ni ajira.Hivyo namatamani kumwambia umuhimu wa kukutana na vijana na kisha kwa pamoja tujadiliane namna ya kutatua changamoto hiyo,"amesma Mbaga.

Pia Mwanadad huyo ambaye amekuwa akijihusisha na kuhamasisha makundi ya rika mbalimbali yakiwamo ya vijana amesema anaamini kuthubutu ni jambo muhimu na hata yeye amefika hapo kwasababu ya kuthubutu na kutoa mchango wake kwa ajili ya nchi yake na nchi nyingine mbalimbali duniani.


Ametoa rai kwa vijana wa Tanzania kuhakikisha wanashiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kufafanua baada ya kumaliza chuo mwaka 2010 alikaa nyumbani kwa miaka mitatu na baadae aliamua kuanza kufanya kazi za kujitolea na sasa amekuwa mfano wa kuigwa na vijana wengine

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MSAADA WA KISHERIA BURE BILA MALIPO YOYOTE.

$
0
0
Na Bashir Yakub. 

Wapo watu wana matatizo na wanahangaika kupata msaada wa bure wa kisheria lakini hawajui waanzie wapi,wafanye nini ili kupata huduma hii. Taratibu zipo, na unaweza kupata wakili wa kusimamia kesi yako bure bila malipo kupitia utaratibu wa msaada wa kisheria. Unaweza kupata uwakilishi huu katika kesi zote yaani zile za jinai pamoja na zile za madai. 

Tunapoongelea za jinai tunamaanisha zile kesi za kuua,kubaka, kupiga,kutukana nk, na tunapoongelea kesi za madai tunamaanisha zile za ardhi kugombea mali, mirathi, ndoa, mikopo,watoto malezi, talaka, nk. 

Kwahiyo pote kwenye jinai na madai unaweza kupata uwakilishi wa bure wa Wakili. Utasimamiwa kesi yako mwanzo hadi mwisho bila kuhitaji kulipa gharama yoyote. Na msaada wa kisheria unaweza kuwa wa uwakilishi kwa maana kuwa wakili utakusimamia mahakamani au unaweza kuwa wa ushauri tu bila kuhusisha mahakama au vyote kwa pamoja. 

Lakini yafaa tufahamu kuwa sio watu wote wanaweza kupata msaada huu. Makala yataeleza utaratibu wa kupata msaada wa kisheria bure halikadhalika ni watu wa aina gani wanaweza kupata msaada huu.

1.WANAOSTAHILI KUPATA MSAADA WA KISHERIA BURE. 

i)Watu wasiojiweza kabisa kifedha. 
ii) Wanawake. 

NAIBU SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI MKAZI SHIRIKA LA VOLUNTARY SERVICES OVERSEA BUNGENI JIJINI DODOMA.

$
0
0
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Voluntary Services Oversea (VSO) Tanzania, Ndg. Dawn Hoyle alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Shirika la Voluntary Services Oversea (VSO) Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Voluntary Services Oversea (VSO) Tanzania, Ndg. Dawn Hoyle (wa pili kushoto) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Shirika la Voluntary Services Oversea (VSO) Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI MWIGULU ATOA WIKI MOJA KWA POLISI DODOMA, OFISI YA MKURUGENZI BAHI KUMPA TATHMINI MAREKEBISHO UJENZI KITUO CHA POLISI CHA CHIPANGA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba (aliyevaa skafu shingoni) akiingia katika Kituo cha Polisi Chipanga, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, wakati alipofanya ziara ya kukikagua kituo hicho ambacho kilijengwa na wananchi lakini hakikufunguliwa tangu mwaka 2005 kutokana na sababu mbalimbali. Hata hivyo, Dk. Mwigulu ametoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani humo, kufanya tahmini ya makadirio ya marekebisho ya ujenzi wa Kituo hicho, ili kiweze kufunguliwa kwa uharaka haraka. Kulia aliyevaa kaunda suti ni Mbunge wa Jimbo la Bahi, Omary Badueli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Bahi, Omary Badueli, wakati walipokua ndani ya Kituo cha Polisi Chipanga ambacho kilijengwa na wananchi lakini hakikufunguliwa tangu mwaka 2005 kutokana na sababu mbalimbali. Hata hivyo, Dk. Mwigulu ametoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani humo, kufanya tahmini ya makadirio ya marekebisho ya ujenzi wa Kituo hicho, ili kiweze kufunguliwa kwa uharaka haraka

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chipanga, wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma, leo, wakati alipofanya ziara ya kukikagua Kituo cha Polisi Chipanga ambacho kilijengwa na wananchi hao lakini hakikufunguliwa tangu mwaka 2005 kutokana na sababu mbalimbali. Hata hivyo, Dk. Mwigulu ametoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani humo, kufanya tahmini ya makadirio ya marekebisho ya ujenzi wa Kituo hicho, ili kiweze kufunguliwa kwa uharaka haraka. 
Mbunge wa Jimbo la Bahi, Omary Badueli, akimpa taarifa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba (watatu kulia), kuhusu historia ya Kituo cha Polisi Chipanga ambacho kilijengwa na wananchi lakini hakikufunguliwa tangu mwaka 2005 kutokana na sababu mbalimbali. Hata hivyo, Dk. Mwigulu ametoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani humo, kufanya tahmini ya makadirio ya marekebisho ya ujenzi wa Kituo hicho ili kiweze kufunguliwa kwa uharaka haraka
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chipanga (hawapo pichani), wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma, leo, wakati alipofanya ziara ya kukikagua Kituo cha Polisi Chipanga ambacho kilijengwa na wananchi hao lakini hakikufunguliwa tangu mwaka 2005 kutokana na sababu mbalimbali. Hata hivyo, Dk. Mwigulu ametoa wiki moja kwa Jeshi la Polisi Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani humo, kufanya tahmini ya makadirio ya marekebisho ya ujenzi wa Kituo hicho, ili kiweze kufunguliwa kwa uharaka haraka. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bahi, Omary Badueli, na kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Chipanga A, Ologa Masaulwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi, Wilaya ya Bahi wakati alipofanya ziara ya kukikagua kituo cha Polisi Chipanga. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SSP Maxi Muhindi, Kulia ni Mkuu wa Jeshi hilo Wilaya ya Bahi, SP Mahemba Kavalambi, na wapili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bahi, Omary Badueli.

Muhimbili ya Kwanza Afrika Mashariki Tiba ya Kuondoa Mawe Kwenye Ini na Kogosho

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza kufanya uchunguzi na tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini na kwenye kongosho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya hadubini.

Mbali na Muhimbili kuanza kutoa huduma ya uchunguzi na kutibu wagonjwa, Kenya inatarajia kuanza kutoa huduma kama hiyo Agosti, mwaka huu.

Mpaka sasa wataalamu wa magonjwa ya tumbo na ini, wamefanikiwa kuchunguza na kutibu wagonjwa 40.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Tumbo na Ini kutoka idara ya tiba, Dkt. John Rwegasha amesema mfumo wa njia ya hadubini ni wa kisasa na kwamba unafanywa bila kufungua tumbo la mgonjwa.

Amesema kwamba mfumo wa hadibini umekuwa ukitumiwa kuchunguza na kutibu matatizo ya vivimbe na mawe kwenye ini ikiwa ni miongoni mwa mikakati wa hatua za awali wa kuelekea kwenye upasuaji wa kupandikiza ini nchini.

Pia, amesema wataalamu wa Muhimbili kwa kushirikiana na Mtalaamu Bingwa wa Upasuaji na Upandikizaji wa Ini kutoka Hospitali ya BLK India wamefanikiwa kurepea ini la mgonjwa lililopasuka ikiwa ni hatua ya msingi wa  kujenga uwezo kwa watalaamu wetu wa upasuaji.

“Tayari wataalamu wetu wa upasuaji wamefanikiwa kurepea ini lililopasuka baada ya mgonjwa kupata ajali ikiwa ni hatua ya awali kuwajengea uwezo watalaamu wetu kuelekea kwenye upasuaji mkubwa wa ini,” amesema Rwegasha.  

Akizungumzia gharama, Dkt. Rwegasha amesema kuwa gharama za kumfanyia uchunguzi na tiba kwa mgonjwa mmoja kwa matumizi ya vifaa tiba pekee ni milioni mbili na kwamba mgonjwa akitibiwa nje ya nchi ni Shs. milioni sita kwa uchunguzi na tiba ya aina hiyo kwa mgonjwa mmoja.

Amesema gharama za kupandikiza ini ni kubwa kuliko kupandikiza figo na kwamba mgonjwa mmoja anahitaji lita 20 za damu ili kufanikisha upasuaji huo.
 Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Tumbo na Ini, Dkt. John Rwegasha akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuanza mchakato wa uchunguzi na tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini na kongosho kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya hadubini. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Tumbo na Ini, Dkt. Yogesh Batra kutoka Hospitali ya BLK nchini India, katikati ni Manju Sharma ambaye ni Meneja wa Uhusiano wa Kimtaifa kutoka Hospitali ya BLK. Wengine ni wataalamu wa magonjwa ya tumbo na ini.
Mmoja wa wagonjwa akipatiwa tiba ya vivimbe pamoja na kuondoa mawe kwenye ini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)  tarehe 21 Juni, 2018.

TAKUKURU WAWANOA VIONGOZI WA ARU KUEPUKA VIASHIRIA VYA RUSHWA

$
0
0
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akitoa nasaha zake kwa viongozi na wafanyakazi wa ARU wakati wa semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuazuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda) 
Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa ARU wakishiriki semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. 
Mmoja wa watoa mada kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kinondoni Elly Makalla akiwasilisha hoja kwa viongozi na wafanyakazi wa ARU walioshiriki semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na taasisi hiyo chuoni hapo Juni 21 2018. 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU), Profesa Evaristo Liwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari kuwaelezea umuhimu wa mafunzo ya kupambana na kuzuia Rushwa chuoni hapo. 
Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa ARU wakishiriki semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. 
Sehemu ya viongozi na wafanyakazi wa ARU wakifuatilia mada kwenye semina ya maswala ya rushwa iliyoendeshwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) chuoni hapo Juni 21 2018. 

SEMINA YA MAFUNZO KWA MAHAKIMU,WAKUU WA MAGEREZA NA WAENDESHA MASHITAKA YAFANYIKA MKOANI KIGOMA

$
0
0
Na Abel Daud,KIGOMA,

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga amewataka Mahakimu wa Mkoa wa Kigoma kufanya kazi kwa Weredi pamoja na kutoa haki kikamilifu bila upendeleo ili kudumisha uaminifu kwa vyombo vya maamuzi.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema vyombo vya ulinzi na usalama nguvu yake kubwa vinategemea maamuzi kutoka kwa mahakama,nakuongeza kuwa nchi nyingi zilizo katika machafuko sehemu kubwa ni ukosefu was haki,pamoja na kutoa angalizo kuwa haki isipotolewa kikamilifu wananchi wanaweza kuchoka na kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi.

Hayo ameyasema  leo alipokuwa akifungua semina ya mafunzo ya siku moja kwa mahakimu wote wa mkoa wa kigoma, kuanzia ngazi ya mahakama ya mwanzo mpaka mahakama ya hakimu mkazi na waendesha mashtaka pamoja na Magereza.

MKURUGENZI msaidizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Nsanze amesema kuanzishwa kwa sheria hii kumepunguza mrundikano wa wafungwa katika magereza na kuongeza pato la Taifa kupitia shughuli zinazofanywa na wafungwa wenye vifungo vya nje katika taasisi za serikali ambazo zingetumia kuajili raia wengine.

Amesema hadi sasa zaidi ya wafungwa elfu kumi na sita (16) wametumikia na wanaendelea kutumikia kifungo hicho cha nje,ikitajwa kuwa wafungwa wenye vifungo vifupi kuacha kuchangamana na wafungwa wenye makosa sugu,hiyo itasaidia kupunguza uhalifu kwani pindi wawapo pamoja hujifunza tabia za waharifu hao sugu taratibu.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Manspaa ya Kigoma Ujiji Agnes Punjila amesema kuwa pamoja na sheria hii kuwa nzuri ila bado kuna changamoto kubwa hasa kwa jamii kuona kuwa sheria hiyo ni yakuwabeba baadhi ya watu na kuomba taasisi zote zinazohusika katika sheria hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii hasa kupitia vyombo vya habari.
MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga  akizungumza mbele ya Washiriki wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wa tatu kulia akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo

RAIS DK. SHEIN AWAAPISHA WAJUMBE WA TUME MPYA YA UCHAGUZI ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha  Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)  katika hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuapisha  Bw.Mabrouk Jabu Makame kuwa Mjumbe wa Tume Mpya ya Uchaguzi Zanzibar  (ZEC)  katika hafla iliyofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuapisha  Bw.Feteh Saad Mgeni kuwa Mjumbe wa Tume Mpya ya Uchaguzi Zanzibar  (ZEC)  katika hafla iliyofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuapisha  Bw.Makame Juma Pandu kuwa Mjumbe wa Tume Mpya ya Uchaguzi Zanzibar  (ZEC)  katika hafla iliyofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuapisha  Dk.Kombo Khamis Hassan kuwa Mjumbe wa Tume Mpya ya Uchaguzi Zanzibar  (ZEC)  katika hafla iliyofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar, ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuapisha   Jaji Khamis Ramadhan Abdalla  kuwa Mjumbe wa Tume Mpya ya Uchaguzi Zanzibar  (ZEC)  katika hafla iliyofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akimuapisha  Bibi Jokha  Khamis Makame kuwa Mjumbe wa Tume Mpya ya Uchaguzi Zanzibar  (ZEC)  katika hafla iliyofanyika  leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati)akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi,Wajumbe wa Tume mpya ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)  katika hafla iliyofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria
Baadhi ya Viongozi na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Wajumbe wa  Tume mpya ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)  katika hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,ambapo Viongozi mbali mbali walihudhuria.
 Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe, Said Hassan Said akisalimiana na Wajumbe wa  Tume mpya ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)  kabla ya kuapishwa leo katika hafla iliyofanyika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
(Picha na Ikulu)

KUMBUKUMBU YA MPENDWA WETU EDMUND LAWRENCE MUSHI

$
0
0
Kuzaliwa:07/12/1973 Kufariki:22/06/2015 


Leo 22/06/2018 Umetimiza miaka Mitatu tangu umefariki Huko Houston,TX,USA. Sisi ndugu zako umetuachia Huzuni na pengo ambalo halitazibika.Unakumbukwa sana na watoto zako Luis(Anwar) na Jermaine.

Unakumbukwa na Baba yako Mzazi mzee Lawrence Mushi Kimbori,Wadogo zako Rudolf(dofu),Gaudence,Fulgence,Renatus(Kulwa),Claudia,Martha(Dotto/Manka) na Mary(Mkakeni).

Unakumbukwa na Ukoo wote wa Kimbori na Massawe.Unakumbukwa na ndugu Jamaa na marafiki zako wote.
Pia Unakumbukwa na wanajumuiya wa Tanzania Houston Community (THC) Houston TX, USA.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa 
Jina lake Lihimidiwe,
Amen.

Timu ya Madaktari Kutoa Hudumza Kitabibu Muhimbili, MOI, JKCI na Hospitali ya Mbeya

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makani Makwaia akikaribisha timu ya wataalamu kutoka China ambao wamekuja kujenga uwezo kwa wataalamu wa hapa nchini na kusaidia maeneo ambayo yana upungu wa wataalamu Muhimbili, Taasisi ya Mifupa MOI, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.  Kutoka kushoto ni viongozi wa watalaamu hao na kulia ni Mkurungezi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi na anayefuatia ni mwakilishi wa MOI, Dkt. Swai. Leo Muhimbili, MOI na JKCI imewaaga wataalamu watatu ambao walikuwa hapa nchini. Tanzania na China imekuwa ikishinikiana kwa zaidi ya miaka 50 katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwamo sekta ya afya.
 Wataalamu kutoka China ambao watashirikiana na wataalamu wetu wa MNH, MOI, JKCI na Hospitali ta Rufaa ya Mkoa Mbeya katika kutoa huduma za kitabibu. Miongoni mwa kundi hilo wamo wataalamu watatu; Dkt. Zhu Jian, Dkt.Wang Qiang na Song Tao ambao wameagwa leo baada ya kumaliza muda wao.
 Mwakilishi kutoka MOI akizungumza na wataalamu kutoka China
ambao wamekuja kujenga uwezo kwa wataalamu wa hapa nchini na kusaidia maeneo ambayo yana upungu wa wataalamu Muhimbili
 Mkurungezi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi akiwakaribisha watalaamu hao kutoka China ambao wamekuja kujenga uwezo kwa wataalamu wa hapa nchini na kusaidia maeneo ambayo yana upungu wa wataalamu Muhimbili
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Makani Makwaia akimpatia cheti Dkt. Zhu Jian ambaye amemaliza muda wake.
 Dkt. Wang Qiang akionyesha cheti chake baada ya kupewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji.
 Mwakilishi wa MOI, Dkt. Swai akimuaga Song Tao ambaye pia amemaliza muda wake nchini.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Bw. Makwaia akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu hao na watumishi wa taasisi tatu ambazo ni  MOI, JKCI na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

MKUTANO WA WADAU KUPINGA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Separatus Fella, akizungumza na wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na biashara hiyo, ambapo maadhimisho ya mwaka huu ya kupinga biashara hiyo yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi wa sita.Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwenyekiti   wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Adatus Magere, akizungumza na wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupambana na biashara hiyo.Kikao hicho kimefanyika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
Mshiriki wa Kikao cha Kujadili mikakati ya kupambana na biashara haramu ya binadamu kutoka Shirika la Utangazaji Tanzani(TBC), Prudence Constantine, akichangia hoja wakati wa kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
Mshiriki wa Kikao cha Kujadili mikakati ya kupambana na biashara haramu ya binadamu kutoka Jeshi la Polisi , ACP Rogathe Mlasani, akichangia hoja wakati wa kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Masuala ya Ongezeko la Watu (UNFPA), Jacqueline Mahon, akizungumza wakati wa Kikao cha Kujadili mikakati ya kupambana na biashara haramu ya binadamu wakati wa kikao kilichofanyika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Msaidizi wa mwakilishi huyo, Anna Holmstrom.
Mshiriki wa Kikao cha Kujadili mikakati ya kupambana na biashara haramu ya binadamu kutoka Vyombo vya Habari vya Azam,Yahya Mohamed , akichangia hoja wakati wa kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Sami Hyypia asisitiza kujituma kufanikiwa

$
0
0
Sami Hyypia veterani wa timu ya Liverpool ambaye yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered amesema kuwa mwanasoka wa mafanikio kunahitaji kazi ngumu na kujituma.

Alisema tangu utoto wake amekuwa akijituma na anaamini katika kujituma katika shughuli zinazokuinua.

Alisema hayo katika hafla ya kukabidhiana vifaa kwa timu zitakazoshiriki michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kufanyika jumamosi wiki hii, iliofanyika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.

Alisema kwamba kuwa juu katika soko kunatokana na mambo mawili makubwa ambayo ni kujituma na kuwa na kipaji.

Alisema hata ukiwa na kipaji ukibweteka katika mazoezi na kujituma katika kuhakikisha uko fiti katika maisha ya mwanasoka huwezi kufikia ngazi za juu za uchezaji wenye kuheshimika.

Alisema pamoja na kuja kuangalia michuano hiyo amepata nafasi ya kuzungumza haja ya kukua katika soka kwa kutengeneza nidhamu inayotakiwa ya kujituma, kufanya mazoezi na kutumia kipaji katika kuimarisha usakataji soka.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akizungumza kwenye hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kulia).
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na timu (hazipo pichani) zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ gwiji huyo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kushoto) na Meneja Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered nchini, Mariam Sezinga wakipitia ratiba ya hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani).
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia wakikabidhi vifaa vya michezo kwa Afisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Mubaraka Kibarabara (katikati) ambapo Airtel ni moja kati ya washiriki 32 wa mashindano ya ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki kutoka kampuni mbalimbali wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (hayupo pichani) wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaa. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakibadilishana mawazo wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani).
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisaini ‘Autograph’ kwa baadhi ya timu zitakazoshiriki mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisalimiana na baadhi ya timu kutoka makampuni mbalimbali zitakazoshiriki mashindano ya Kombe la Standard Chartered yatakayofanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam wakati wa hafla mchapalo uliyoambatana na tukio la kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yatakayofanyika siku ya Jumamosi. Hafla hiyo imefanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wachezaji wa timu shiriki na makapteni walipata fursa ya kupiga picha na kusainiwa ‘Autograph’ Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VIONGOZI WA TIMU ZA NDONDO 2018 WATEMBELEA OFISI ZA BENKI YA DCB LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha biashara wa DCB Benki James Ngaluko akizungumza na viongozi wa timu zinazoshiriki Ndondo Cup 2018 walipotembelea Benki hiyo kujifunza huduma mbalimbali za kibenki na kufungua akaunti za timu zao. DCB Benki ndiyo mdhamini wa Ndondo cup 2018.  
 Moja ya waratibu wa mashindano ya Ndondo Cup Yahya Mohamed akizungumza na viongozi wa timu za Ndondo Cup wakati walipotembelea ofisi za benki ya DCB ambaye ni mdhamini wa michuano hiyo kwa mwaka 2018.
Moja ya viongozi wa timu shiriki za michuano ya  Ndondo Cup akizungumza mbele ya  viongozi wa benki ya DCB na waandaaji wa Ndondo Cup  wakati walipotembelea benki hiyo ambao ni wadhamini wa mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.

MAHAKAMA KUWASOMEA MAELEZO YA AWALI MBOWE, WENZAKE JUNI 25 HADI 29

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itawasomea maelezo ya awali (PH) na kesi kuanza kuisikiliza kesi ya jinai inayowakabili viongozi wa juu wa tisa wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kwa mfululizo kuanzia Juni 25 hadi 29 mwaka 2018.

Hati hiyo imekuja baada ya mawakili wa upande wa Serikali wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na Wakili Paul Kadushi, Wankyo Simon na Jackline Nyantori kuieleza mahakama kuwa, kesi ilikuja kwa ajili ya Ph .

Hata hivyo, Mahakama haikuweza kusoma PH kwa sababu mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Freeman Mbowe amefiwa na kaka yake na amesafiri jana kwenda kuzika Moshi.

Pia Mahakama imemtaka mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo, Mbunge wa Tarime mjini Estherher Matiko ambaye amekuwa akiripotiwa kuwa mgonjwa mara kadhaa, kuhudhuria mahakamani bila ya kukosa na asipofanya hivyo hatua dhidi yake zitachukuliwa.

Pia kesi hiyo imeshindwa kuendelea kusikilizwa ysikilizwaji wa PH leo sababu mawakili wanaowatetea washtakiwa hao Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya hawakuwepo walikuwa na kesi zingine, Kibatala ana kesi mahakama kuu. Huku Mtobesy alikuwa amehudhuria kesi Mahakama ya Afrika Mashariki Arusha na wamewakilishwa mahakamani hapo na mawakili Nashon Nkungu, Frederick Kihwelo na Hekima Mwesigwa.

Mbowe aliwakakilishwa mahakamani hapo na mdhamini wake Grayson Celestine ambaye aliwasilisha nakala ya cheti cha kifo mahakamani ili kuithibitishia mahakama, huku akiwasilishwa na mdhamini wake Patrick John ambaye alidai Matiko bado anaumwa na akawasilisha nyaraka ya mapumziko kutoka kituo cha afya ambayo inamapumziko ya siku saba kuanzia juni 21,2018 mpaka Juni 28,2018.

Hata hivyo nyaraka hiyo ilipingwa na Wakili Nchimbi kwa madai kuwa ni batili haina maelezo yanayojitosheleza ambayo yanaweza kuishawishi mahakama kuamini Matiko ni mgonjwa na anapaswa kupumzika kwa siku saba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HOSPITALI MLOGANZILA WAJIANDAA KUTIBU SELIMUNDU KWA KUPANDIKIZA UTE WA MIFUPA

$
0
0
*Wazungumzia namna wanavyofanya tafiti, kutoa huduma bora

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MKUU wa Idara ya Hematolojia, Uwekaji wa Damu na Mtafiti Mkuu wa Program ya Selimundu katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili(MUHAS) Profesa Jullie Makani amesema wapo katika mchakato wa kutoa huduma ya kutibu Selimundu kwa Kupandikiza ute wa Mifupa

Prof.Makani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Selimundu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Mlaganzila ambapo amesema kwa sasa wapo katika mchakato wa mazungumzo na yakikamilika wanatarajia kuanza kutibu Selimundu kwa kutumia tiba ya Kupandikiza Ute wa mifupa kwa mgonjwa.

"Zipo njia mbili zinazotumika kutibu Selimundu.Njia ya kwanza ni kwa kutumia Hydroxyurea na ndio ambayo tunaitumia hapa nchini.Njia ya pili ni ya kutibu kwa kupandikiza ute wa mifupa ambayo kitalaam inafahamika Bone Marrow Transplant,"amefafanua.

Alipoulizwa ni lini wataanza kupandikiza ute wa mifupa kwa mgonjwa wa Selimundu katika hospitali hiyo amejibu wanatarajia kuanza mwakani iwapo mchakato utakwenda vizuri hata.Pia amesema haijafahamika gharama ya kutibu kwa kupandikiza ute wa mifupa itakuwa kiasi gani na ndio mazungumzo ambayo wanaendelea nayo kufanya.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MuHAS) Profesa Appolinary Kamuhabwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Ugonjwa wa Seli Mundu yaliyofanyika kwenye Chuo Kikuu hicho Kampasi ya Mloganzila leo na kushirikisha Madaktari Bingwa, Watafiti wa Magonjwa na Tiba mbalimbali na wauguzi, Profesa Kamuhabwa amesema chuo hicho mpaka sasa ina miradi ya utafiti wa magonjwa mbalimbali pamoja na tiba inayofikia 92.
Profesa Julie Makani Mkuu wa Idara ya Hematolojia , Uwekaji wa Damu na Mtafiti Mkuu wa Programu ya Seli Mundu (MuHAS)akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Seli Mundu yaliyofanyika katika Chuo hicho Kampasi ya Moganzila leo.Profesa Julie Makani Mkuu wa Idara ya Hematolojia , Uwekaji wa Damu na Mtafiti Mkuu wa Programu ya Seli Mundu (MuHAS) akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Seli Mundu yaliyofanyika katika Chuo hicho Kampasi ya Moganzila leo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MuHAS) Profesa Appolinary Kamuhabwa katikati ,Profesa Julie Makani Mkuu wa Idara ya Hematolojia , Uwekaji wa Damu na Mtafiti Mkuu wa Programu ya Seli Mundu (MuHAS) kushoto na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma za Hospitali Profesa Said Aboud wakifuatilia baadhi ya taarifa za tafiti zilizokuwa zikionyeshwa kwenye Projekta. 
Baadhi ya wataalamu na madaktari mbalimbali wakiwa katika maadhimisho hayo. 
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma za Hospitali Profesa Said Aboud akitoa shukurani zake wakati wa maadhimisho hayo mara baada ya kutolewa kwa taarifa mbalimbali za kiutafiti katika chuo hicho.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MuHAS) Profesa Appolinary Kamuhabwa katikati ,Profesa Julie Makani Mkuu wa Idara ya Hematolojia , Uwekaji wa Damu na Mtafiti Mkuu wa Programu ya Seli Mundu (MuHAS) kushoto na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Huduma za Hospitali Profesa Said Aboud wa pili kutoka kushoto pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Udahili na Uzamivu (MuHAS) Emmanuel Balondya kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Madaktari Bingwa, Wataalam na Watafiti wa chuo hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA CRDB

$
0
0

 Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi (kulia) akizungumza na baadhi wa wafanyakazi wa Benki ya CRDB walioongozwa na Meneja Uhusiano wa Benki hiyo, Godwin Semunyu (nguo nyekundu) walipofika kuzungumza naye kuhusiana na maswala ya kibenki kwa watu wa Diaspora, kwenye Makazi ya Balozi, 51 Ulitsa Bolshaya Nikitskaya, Jijini Moscow, nchini Urusi.
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB walioongozwa na Meneja Uhusiano wa Benki hiyo, Godwin Semunyu (wa pili kushoto). wengine pichani kutoka kulia ni Mshauri wa Balozi, George Lengeju, mmoja wa washindi wa Promosheni ya Shuhudia Kombe la Dunia na TemboCard Visa ya Benki ya CRDB, Nuru Kisome, Meneja Masoko wa Benki ya CRDB, Jadi Ngwale.
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi akiagana na Meneja Uhusiano wa Benki hiyo, Godwin Semunyu baada ya mazungumzoa yako, leo jijini Moscow, nchini Urusi.

MICHUZI TV: UBONGO TIME

Viewing all 110095 articles
Browse latest View live




Latest Images