Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WANAMUZIKI NCHINI KUTEMBELEA BUNGE WIKI IJAYO KUPITIA TAMUFO

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

WANAMUZI walio wanachama wa Umoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) wiki ijayo watatembelea Bunge kwa ajili ya kuona mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Bunge hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa Umoja huo, Dk.Donald Kisanga alisema kwa umoja huo kwao ni fursa kubwa ya kutembelea Bunge."Kwetu sisi Tamufo kutembelea Bunge ni fursa kubwa na tunaenda kuona jinsi Bunge linavyofanya kazi yake" alisema Kisanga.

Kisanga alisema msafara wao utaondoka jijini Dar es Salaam Juni 23 na Bungeni watakuwepo Juni 25 mwaka huu na mwenyeji wao ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harrison Mwakyembe.

Kisanga aliyataja baadhi ya makundi ya wanamuziki watakaokuwepo kwenye msafara huo kuwa ni wanamuziki wa dansi ambalo litaongozwa na Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kik na Hamza Kalala.

Alitaja kundi la muziki wa Injili kuwa litaongozwa na Stella Joel na Emanuel Mbasha wakati Bongo Fleva litaongozwa na Witness Kibonge Mwepesi huko taarabu likiongozwa na Sizer Masogelo na Muziki wa Asili likiongozwa na Grace Kayinga.Katibu wa Tamufo, Stellah Joel alisema wanamuziki kutoka mikoa yote waliotayari watakuwepo kwenye msafara huo.
Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk. Donald Kisanga, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tamufo, Morocco Dar es Salaam jana wakati wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja huo pamoja na safari ya baadhi ya wanachama wa Tamufo kwenda Bungeni Dodoma.
Mhandisi Abdallah Ally kutoka Kampuni ya CogsNet ambayo inasimia kazi za wasanii akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.
Mwanamuzi mahiri Kitenzogu Makassy, akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Mwanamuziki Hamza Kalala.
Mwanamuziki mkongwe Boniface Kikumbi Mwanza Mpango au King Kiki akichangia jambo kwenye mkutano huo.


BENKI YA BARCLAYS YAANDA SEMINA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI

$
0
0
Na  Agness Francis, Globu ya Jamii
BENKI ya Barclays Tanzania  imeandaa semina ya siku moja kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wakati na lengo kuu ni kuwajengea uwezo na kuwaongezea ujuzi wa kufanya biashara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na wakati wa benki Ahmed Khamis amesema kuwa semina hiyo ni moja ya mpango wa benki ya Barclays kurudisha baadhi ya faida yake kwa jamii.

"Barclays tunaamini kwenye mpango wa kukua pamoja kwa wateja wafanya biashara wetu.Wateja wetu wameweza kuongeza ujuzi wao jinsi ya kuandaa mpango wa biashara, jinsi ya kutangaza biashara zao, jinsi ya kutunza kumbukumbu na njia bora ya kuomba na kutumia mikopo," amesema Khamis.

Kamesema wamengundua na kutambua njia bora ya kufundisha na kuwaongoza wateja wao hasa wale ambao wanaochukua mikopo na kwamba mafunzo hayo yamekuwa muhimu kwao.
 kwani wameweza kuongeza na kupata ujuzi jinsi ya kutengeneza mpango wa biashara, kukuza biashara zao na kukopa kwa kuongeza kukuza biashara.

Amefafanua semina kama hizo zitaendelea kufanyika nchi nzima na nia ni kuongeza ujuzi kwa wateja wao ikiwa tayari zishafanyika Zanzibar na Arusha.

Khamis amesema taasisi nne za Serikali zimekuwa na fursa ya kutoa mada jinsi wanavyofanya shughuli zao na jinsi ya kuwasaidia wafanya biashara hao.

Akizungumza kwenye semina hiyo Mkuu wa Kitengo cha Kampuni kutoka BRELA Rehema Kitambi amesema usajili wa kampuni umekuwa rahisi kwani kwa sasa inasajili kampuni kupitia kwa njia ya mtandao bila mteja kufika katika ofisi zao.


"Kuna changamoto za kusajili kwa njia ya mtandao kwani kuna baadhi ya watu hawana elimu hiyo huku wengine wakipata changamoto za huduma ya mtandao kulingana na maeneo yao wanavyoishi.

"Ni lazima Mtanzania awe na kitambulisho cha uraia ili kusajili kampuni wakati wengine bado hawajapata vitambulisho.Nawamba wote tuwe pamoja kukubaliana na changamoto hizo  na kwa wale ambao sio raia wanatakiwa kuwa na hati zao za kusafiria,"amesema.
 Afisa Mwandizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Maternus Mallya akitoa mada wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya Barclays Tanzania kwa wajasiriamali wadogo na wa kati 50 kwa lengo ya kuwaongezea ujuzi wa kufanya na kuendesha biashara zao kwa faidi zaidi na pia kuwaongezea ujuzi wa biashara Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha makampuni kutoka BRELA Rehema Kitambi akitoa mada wakati wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya Barclays Tanzania kwa wajasiriamali wadogo na wa kati 50 kwa lengo  la kuwaongezea ujuzi wa kufanya na kuendesha biashara zao kwa faidi zaidi na pia kuwaongezea ujuzi wa biashara Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha makampuni kutoka BRELA, Rehema Kitambi (kushoto) akijadiliana na Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wa kati, Ahmed Khamis wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na benki ya Barclays Tanzania kwa wajasiriamali wadogo na wa kati 50 kwa lengo ya kuwaongezea ujuzi wa kufanya na kuendesha biashara zao kwa faida zaidi na pia kuwaongezea ujuzi wa biashara Jijini Dar es Salaam.

NHIF, HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA WAJADILIANA NAMNA YA KUBORESHA HUDUMA KWA WANACHAMA

$
0
0

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

UONGOZI wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bernard Konga umekutana na uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kujadili namna ya kuboresha huduma kwa wanachama wakati wanapofika kupata huduma za matibabu hosptalini hapo.

Majadiliano ya huduma kati ya watoa huduma na Mfuko yamekuwa yakifanyika kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wanachama wa Mfuko.

Akizungumza leo kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa NHIF  Bw.Konga amesema kuwa suala la huduma bora kwa wanachama ni kipaumbele cha Mfuko kwa kuwa wamelipia huduma hizo kabla ya kuugua.

"NHIF na watoa huduma lazima tuwe na lugha moja ya kuwapa huduma bora wanachama wetu na kama kuna tatizo linajitokeza tulishughulikie wenyewe na sio kuwahusisha wanachama wetu.

"Na kwa kufanya hivi mwanachama atapata huduma bila usumbufu wowote na itavutia wengine kujiunga na huduma zetu," amesema Bwa.Konga.
Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Bernard Konga umekutana na uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kujadili namna ya kuboresha huduma kwa wanachama wakati wanapofika kupata huduma za matibabu hospitalini hapo.

BODI YA PSPTB: SOMO LA HESABU LATAJWA KUWA CHANGAMOTO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
BODI ya wataalumu wa Manunuzi  na Ugavi (PSPTB)nchini imesema ni vema somo la hisabati likatiliwa mkazo kuanzia shule ya msingi  ili kuwezesha kupatikana kwa wahitimu wanaostahili kukabidhiwa ofisiM

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya PSPTB,  Godfred Mbanyi amesema hayo leo jijini  Dar es Salaam na wakati wa kutangaza matokeo ya 16 ya mitihani ya bodi hiyo.

Amesema licha ya jitihada zote ambazo zimekuwa zikichukuliwa na bodi hiyo kuhakikisha kuwa wahitimu wa fani hiyo wanafanya vizuri kwenye somo la hesabu lakini bado ufaulu umeendele kuwa hafifu jambo ambalo linaleta shaka kwa wataalamu hao kukabidhiwa ofisi.

Amesema ingawa katika matokeo haya ya 16 ya mitihani ya bodi ufaulu umeongezeka kwa asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka jana, lakini bado kuna ufaulu hafifu kwenye masomo yanayohusisha hesabu.

“ Somo la hesabu bado ni changamoto kubwa katika Jamii, wahitimu wengi wamekuwa hawana msingi mzuri wa somo la hesabuheh wakiwa chini, jambo ambalo linaongeza changamoto, ni vigumu kwa muhitimu wa aina hii kumkabidhi Ofisi kutokana na kushindwa kumudu sawasawa mahesabu,

Amesema kuwa pamoja na matokeo hayo kama bodi wataendelea kubuni mbinu nyingine ambazo zitasaidia kurahisisha ufaulu kwenye somo hilo.

Mbanyi amevitaja vyuo vilivyofanya vizuri kwenye mitihani hiyo kuwa ni Chuo cha Ushirika Moshi, Chuo cha Biashara CBE na Chuo cha Mtakatifu Augustine cha Mwanza katika ngazi ya nne.

 Aidha amesema, bodi imeanzisha utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wahitimu ili waweze kufanya vema katika mitihani yao, "mtu yeyote anayetaka kuja kufanya mitihani ya bodi ni vema awe tayari kuhudhuria mafunzo ya kujitayarisha ili kuongeza idadi ya watahiniwa wanaofaulu" amesema Mbanyi.

“Kwa sasa tunaweka mikakati ya kuboresha ufundishaji ili kuweza kuongeza ufaulu kwa wahitimu kwani licha ya kuongezeka ufaulu kwa asilimia 11 matokeo bado siyo mazuri sana, hata hivyo ni lazima kuwe na mkakati bora Zaidi wa kutilia mkazo somo hili kuanzia chini,” amesema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa bodi hiyo, Amani Ngonyani amesema  bodi itahakikisha inaendelea kufanya ziara za mafunzo katika vyuo vinavyotoa taaluma hiyo nchini ili kuwakumbusha wanafunzi juu ya kutilia mkazo taaluma hiyo.

“Tutatembela vituo vyote nchini ili kuona kama vina sifa na uwezo w akufundisha ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo kwa ajili ya kupika na kutoa wanafunzi wenye sifa na uwezo unaohitajika katika taaluma hii,” amesema.

Pamoja na kutunukiwa cheti cha Bodi, wahitimu 809 kati ya 1549 waliofanya mitihani hiyo Mei Mwaka huu ikihusisha vituo tisa wahitimu hao pia wanatarajiwa kutunukiwa vyeti vya kimataifa kwenya maafali itakayofanyika Oktoba mwaka huu, 
 Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi  na Ugavi, PSPTB akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa kutangaza matokeo ya 16 ya mitihani ya bodi hiyo. Iliyofanyika Mei mwaka huu ambayo mahafali yake yatafanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa bodi hiyo, Amani Ngonyani
Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa bodi  ya wataalumu wa Manunuzi  na Ugavi, PSPTB , Amani Ngonyani akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari juu ya mikakati inayowekwa na bodi hiyo ya kuboresha ufundishaji ili kuweza kuongeza ufaulu kwa wahitimu wakati wa utangazwaji wa matokeo ya 16 ya mitihani ya bodi hiyo. Iliyofanyika Mei mwaka huu ambayo mahafali yake yatafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA UPANUZI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO ZA TTCL NCHI NZIMA, APOKEA GAWIO LAO LA BILIONI 1.5

$
0
0


 


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakitumia mawasiliano ya Video Conference wakati baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.5 kwa serikali  toka kwa viongozi wa TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 21, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kupokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi Bilioni 1.5 kwa serikali  toka kwa viongozi wa TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 21, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akipokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi Bilioni 1.5 kwa serikali  toka kwa viongozi wa TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 21, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.5 kwa serikali toka kwa viongozi wa  TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo  Juni 21, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za mawasiliano za kampuni ya TTCL nchi nzima baada ya kupokea gawio la shilingi Bilioni 1.5 toka kwa viongozi wa TTCL Corporation kwenye hafla iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 21, 2018. 

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZINDUA MAJENGO YA TAASISI YA ELIMU YA AFYA MVUMI MKOANI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wa nne kulia akikata utepe kuzindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma na wanne kutoka kushoto ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  wa Tatu kulia akizindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma, wa pili kulia ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kulia akipokea cheti cha umalizaji wa ujenzi wa majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi kutoka kwa Waziri wa Afya,Maendeleo ya amii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa majengo hayo uliofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mwenye suti ya bluu akikagua baadhi ya sehemu za majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi baada ya kuzindua majengo hayo yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) yaliyozinduliwa leo jijini Dodoma.
 aadhi ya viongozi na wananchi  wa Mvumi wilayani Chamwino waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uzinduzi wa Majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanya na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo jijini Dodoma.PICHA NA WIZARA YA AFYA. 

WANAFUNZI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA UOMBAJI WA MIKOPO-BODI YA MIKOPO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Wanafunzi wanaoomba Mikopo ya  Elimu ya Juu wametakiwa kufuata taratibu zilizowekwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu Juu (HESLB) ili kuweza kurahisisha katika uchambuzi.

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi ya Elimu Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru wakati wa tathimini na changamoto za waombaji wa Mikopo ya Elimu Juu kwa kushirikiana Shirika laPosta , Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wakala Usajili Udhamini na Ufilisi (RITA) pamoja na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), amesema kuwa wanafunzi wakifuata taratibu zilizowekwa kunapunguza changamoto katika uchambuzi wa mikopo.

Amesema kuwa nyaraka zote zinazohitajika na bodi ni muhumu hivyo waombaji lazima wazingatie wanaweka vigezo vilivyowekwa na bodi ya mikopo na wasipoweka vigezo hivyo fomu inakuwa haijakamilika.

Aidha amesema kuwa wanafunzi ambao hawajaomba waendelee kuomba katika kipindi hiki kilichobaki ili wasiweze kuachwa katika utaratibu huo.

Wakala Usajili Udhamini na Ufilisi (RITA)  imesema kuwa wanafunzi waliomba vyeti vya kuzaliwa 41573 tangu walipoanza utaratibu wa kutoa vyeti kuzaliwa na vifo kwa wanafunzi hao na utaratibu huo vyeti 25676 uko tayari  vimepitishwa.

Akizungumzia changamoto za uombaji Mkurugenzi Tehama, Cuthbert Simalenga amesema kuwa wanafunzi wengine wamekuwa na weka picha ambazo haziko katika taratibu za uombaji  uliowekwa.

Shirika la Posta Nchini (TPC) limesema kuwa jumla ya fomu za maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu 14440 ambayo yaliombwa na wanafunzi hao, fomu 12823 wameziwasilisha bodi ya Mikopo na fomu 1619 ziko katika mchakato wa kuzisafirisha.

Akizunguma katika tathimini ya waombaji wa mikopo, Meneja Mkuu wa Uendesha wa Shirika la Posta (TPC)Mwanaisha Said amesema kuwa wazazi wawape fedha mapema wanafunzi wanaomba mikopo katika bodi katika kuondoa changamoto.
 Mkurugenzi Mtendaji HESLB,  Abdul-Razaq Badru akizungumza  katika tathimini ya waombaji wa mikopo katika bodi hiyo na changamoto ambazo wanakumbana nazo na taasisi zinazohusika katika maombi hayo.
 Mkurugezi  wa Tehama wa RITA, Cuthbert Simalenga akizungumza kuhusiana na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa waombaji wa katika bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya Juu.
 Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa Shirika la Posta  Nchini (TPC) , Mwanaisha Said akizungumza  kuhusiana na usafirishaji wa fomu za wanafunzi wanaomaba mikopo katika bodi ya mikopo.
 Picha pamoja kwa watendaji wa taasisi zinazohusiana na katika uombaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Picha pamoja kwa watendaji wa taasisi zinazohusiana na katika uombaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na wanafunzi waombaji wa mikopo

Michuzi TV: TECNO SPARK2 YAZINDULIWA RASMI DAR ES SALAAM


RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMIN MKAPA AZINDUA KITABU CHA KUZUNGUMZIA HALI YA UMASKINI

WAZIRI MAHIGA AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI NORWAY, ASISITIZA UWEKEZAJI WENYE TIJA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini Norway kwa mazungumzo na wafanyabiashara huku akiwapa ujumbe mkuu wa kuwekeza Tanzania ambapo tayari kuna mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwenye hotuba yake kwa wanachama wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Norway na Afrika (NABA), Mhe. Mahiga ameelezea ushirikiano uliopo kati ya Serikali za Norway na Afrika kwa ujumla hususan Tanzania, ambapo Norway inasaidiana na nchi nyingi za kiafrika  ikiwemo Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo. Hii ni ishara nzuri kwa ukuaji wa biashara na mahusiano.
Akitolea mfano wa Tanzania, Mhe. Mahiga alisema kuwa miaka ya hivi karibuni Serikali ya Norway imebadilisha ushirikiano wake na Tanzania kutoka kwenye kutoa misaada kwenda kwenye udhamini wa pamoja wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kuinua uchumi.
“Ushiriki wa Serikali ya Norway nchini kwetu ni wa kipekee, kwani unazingatia vipaumbele na sera za Tanzania na pale wanaongeza nguvu kwa kudhamini mafunzo na hatimaye ujenzi wa mifumo sahihi ya utekelezaji wa sera hizo” Waziri Mahiga alisema.
Waziri Mahiga aliongeza kuwa, kwenye awamu ya tano ya uongozi nchini Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mambo mengine, amejenga mifumo bora ya ukusanyaji kodi, usimamizi wa rasilimali za umma pamoja na uendelezwaji wa rasilimali ya mafuta kwa maendeleo. “Serikali ya Norway inadhamini maeneo yote hayo na mengine mengi, kama mdau wa maendeleo ya Watanzania. Hivyo ni vyema na nyie wafanyabiashara muwekeze pale ambapo Serikali yenu ipo. Kwa sababu hapo ndio mahali salama kwa uwekezaji wenye tija” alihimiza Mhe. Mahiga.
Mkutano huo uliojumuisha taasisi takriban 25, ulifanyika chini ya mwamvuli wa Norfund, Taasisi inayojenga uwezo kwa wafanyabiashara kuendesha biashara kwenye nchi zinazoendelea.
Akielezea mikakati ya taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wake, Bw. Kjell Roland alisema Norfund inajikita zaidi kwenye nchi ambazo upatikanaji wa mitaji ni mgumu kutokana na uchanga wa sekta binafsi.
Kwa upande wake, Mratibu wa umoja huo wa Wafanyabiashara wa NABA, amesema kuwa wapo kwenye maandalizi ya ziara ya biashara Tanzania kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Waziri Mahiga alitumia fursa ya mkutano huo kumtambulisha Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa ambaye anatarajiwa kukabidhi hati zake  za utambulisho tarehe 21 Juni, 2018.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 21 Juni, 2018

Veteran wa Liverpool Sami Hyypia atua Dar kwa mwaliko wa Standard Chartered

$
0
0

Sami Hyypia veteran wa timu ya Liverpool yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered. Mchezaji huyo mwenye haiba ya aina yake aliwasili nchini Jumanne, kuhudhuria michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kuanza jumamosi wiki hii. Akizungumza klatika mkutano na waandishi wa habari Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema benki yake imefurahjishwa sana na ujio wa mchezaji huyo wa zamani. 

“Tumefurahi sana kuwa na Sami nchini na kumshirikisha katika michuano ya tatu ya kombe la Standard Chartered . Sami pia atatumia uwepo wake kufanya kazi na timu ya vijana chini ya miaka 17– Serengeti Boys” Sami Hyypia ni mmoja wa viungo hatari ambao walivaa fulana nyekundu wakati wa utawala wa makocha Gerard Houllier na Rafael Benitez na kumfanya kuwa mmoja wa walinzi hodari barani Ulaya. 

Mchango wa Hyypia katika soka la England kulimfanya atambuliwe kwao (Finland) kwa kupewa tuzo za mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka saba. (1999, 2001, 2002, 2003, 2005, 2006 na 2008). Baada ya kusaidia timu yake dhidi ya Sheffield Wednesday hapo Agosti 7, 1999, Hyypia akawa katika mahusiano mazuri ya kisoka na Stephane Henchoz na kuwa na viungo bora wa ulinzi 2000-01. 

Aidha uchezaji wake na Jamie Carragher ulitengeneza kitu kilichokubalika kuwa ngome thabiti baada ya Liverpool baada ya kutwaa Champions League katika viwanja vya Ataturk. Hyypia ndiye aliyefunga goli la kukumbukwa sana wakati alipofunga goli dhidi ya Juve katika robo fainali. Historia ya soka, alisema mtendaji huyo wa Benki, itamweka katika eneo zuri kabisa la kibiashara mchezaji huyo ambaye wapenzi walimweka katika orodha ya kuwa mtu wa 38 kati ya watu 100 waliofanya vyema katika klabu hiyo. 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akiwa ameongozana na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Gwiji huyo wa Liverpool nchini. Wengine katika picha nyuma kutoka kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akipeana mkono na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia mara baada ya mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika na Tanzania ikiwa ni nchi yake ya kwanza kutembelea huku wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi. 
Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ujio wa Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (katikati) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani 

Polisi Mbeya yakamata vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Aidha kumekuwa mafanikio katika misako kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 20.06.2018 majira ya saa 22:30 Usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko maeneo ya Gerezani, Kata ya Ndandalo, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kukamata vipande tisa [09] vya meno ya Tembo na jino moja [01] la Kiboko vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa kilogram 30.
Thamani halisi ya meno hayo bado haijafahamika, jitihada za kuwasiliana na Idara ya Wanyama pori zinafanyika. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na msako mkali kuwatafuta watuhumiwa ambao walikimbia mara baada ya kuwaona askari. Aidha watuhumiwa wawili waliokimbia mmoja ametambulika kwa jina [Linahifadhiwa] Mkazi wa eneo la Magereza.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi MUSSA A. TAIBU anatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za siri kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi. Aidha Kamanda TAIBU anatoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na ujangiri na badala yake kujihusisha na shughuli halali pamoja na kulinda maliasili za nchi.

Imesainiwa na:
[MUSSA A. TAIBU - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

 Vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko vilivyokamatwa Mbeya
 Vipande tisa vya meno ya Tembo na jino moja la Kiboko vilivyokamatwa Mbeya

ACP MUSSA A. TAIBU -KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Introducing "NAUMWA" by Kisamaki of mkubwa na wanawe

ALIYOYAZUNGUMZA MSAJILI WA NGOs ALIPO KUTANA NA WADAU WA NDANI YA SERIKALI WANAOFANYA KAZI NA NGOs

MWANAMKE AUAWA MANYARA, CHANZO CHA KIFO BADO HAKIJAFAHAMIKA, MMOJA ASHIKILIWA NA POLISI

$
0
0
Na. Vero Ignatus , Manyara.

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jila la Josephine Peter (51)mkazi wa Mrara kata ya Mamire wilayani Babati ameuawa na watu wasiofahamika huku shingo yake ikikatwa na kitu chenye ncha kali.

Akizungumza leo Juni  21 Kamanda wa polisi mkoani Manyara Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema mwanamke huyo alifariki dunia juni 19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake na mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kutokana na mauaji hayo.

Kamanda amesema kuwa hadi sasa chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika kwani mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi nakubainika kuwa hajabakwa kama watu wanavyozusha bali jeshi la polisi unaendelea na upelelezi wa tukio hilo la mauaji amesema kuwa ukikamilika taarifa kamili itatolewa

Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara)

Kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara Augustino Senga.
 

WANANCHI MKOANI NJOMBE WAITIKIA KWA WINGI KAMPENI YA ELIMU, HUDUMA NA USAJILI WA WALIPAKODI WAPYA

$
0
0
Na Mariam Mwayela,Njombe

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kutoa huduma, elimu na kusajili walipakodi wapya katika maeneo ya Ludewa, Matamba, Ilembula, Mlangali, Ikonda na Makete Mkoani Njombe ambapo mpaka sasa jumla ya walipakodi 351 wamesajiliwa.

Zoezi hili limekuwa na muitikio mkubwa kutoka kwa wananchi ambao kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kupatiwa elimu ya kodi na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Akizungumza wakati wa kampeni hiyo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Bw. Richard Kayombo amewashukuru wakazi wa maeneo hayo kwa kuitikia wito na kuonyesha shauku ya kutaka kujua mambo mbalimbali yanayohusu kodi hususani usajili wa biashara, kuhakiki TIN na kusajili walipakodi wapya.

“Tunashukuru sana kwa muitikio huu ulioonyeshwa katika zoezi hili hapa mkoani Njombe ambao unaonyesha uzalendo wa kuchangia mapato ya Serikali kwa kujisajili na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi ambayo ni mwanzo wa kutimiza wajibu wa kulipa kodi”, Alisema Kayombo.

Kayombo amewaambia wafanyabiashara waliofika katika kampeni hiyo, kuwa na ukaribu na maafisa wa TRA ili kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika kila hatua ya ulipaji wa kodi na kutoa maoni yao ambayo yataboresha huduma zitolewazo na Mamlaka.

Aidha, Kayombo aliwakumbusha kulipa kodi sahihi na kwa wakati ili kuepuka faini na adhabu zinazoambatana na ucheleweshaji huo. Vilevile, aliwasisitiza umuhimu wa kutunza kumbukumbu sahihi za biashara, kutoa risiti pindi wanapouza bidhaa au huduma na kudai risiti kila wanapofanya manunuzi mbalimbali.

Naye William Kabupa ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wa duka la Nguo eneo la Ilembula, ameishukuru TRA na kusisitiza kuwa, zoezi hili ni zuri na litasaidia wafanyabiashara kutokuwa na sababu ya kukosa TIN au kukataa kulipa kodi.

“Nimefurahi sana kupata TIN yangu leo hapa Ilembula kwani ilikuwa inanibidi kusafiri kwenda Njombe mjini kupata TIN. Aidha, nashauri wafanyabiashara wenzangu wa Ilembula wajitokeze kwa wingi ili waweze kupata elimu na kusajiliwa ili waweze kulipa kodi na kujivunia kuwa mmoja wa wachangiaji wa mapato ya Serikali” alisema Kabupa.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea na kampeni ya kutoa Elimu, Huduma na kusajili walipakodi wapya Mkoani Njombe ambapo hadi sasa Walipakodi wa Wilaya za Makete, Ludewa, Wanging’ombe na Njombe wanaendelea kupata huduma, elimu na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

MSHINDI WA GARI KUTOKA BE FORWARD ATIMIZA NDOTO ZAKE JIJINI MWANZA

$
0
0
 Mnamo Desemba 2013 Dr.Marko Hingi ambaye alikuwa mwanafunzi wa udaktari katika chuo kikuu cha afya na sayansi alishinda gari kupitia kampuni ya kuagiza magari ya Be Forward ambapo alikabidhiwa mnano Februari 25, 2014. Makabidhio hayo yalifanyika katika bustani ya palm residency karibu na hospitali ya Ocean Road Dar es salaam.
(BOFYA HAPA KUONA KUMBUKUMBU HIYO)
Katika kufuatilia, Michuzi Blog imefanikiwa kumtafuta na kumpata Dr. Marko Hingi na kufanya mahojiano nae miaka minne baada ya kushinda gari aina ya Toyota-Noah ambapo katika mahojiano na vyombo vya habari aliahidi kulitumia gari hilo kubeba wagonjwa hasa kinamama wajawazito na watoto wanapopata dharura.





KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT.MAGUFULI AKIWA DODOMA,IRINGA HADI MOROGORO. MEI 2018

Vodacom Tanzania yakabidhi gari la kwanza jijini Mwanza

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) akimkabidhi ufunguo wa gari mkazi wa Geita Pasquina Ignas, baada ya kuibuka mshindi wa matumizi ya Mpesa wakati wa hafla ya kuadhimisha mika 10 ya Mpesa,Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Mworia Rosalynn(kushoto) akishuhudia.
 Mshindi wa kutumia huduma za Mpesa mkazi wa Geita  Pasquina Ignas, akionyesha namba ya gari baada ya kukabidhiwa kwenye hafla ya kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa Mpesa, kushoto ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Mworia Rosalynn na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella(kulia) wakishuhudia.
 Mshindi wa kutumia huduma za Mpesa mkazi wa Geita  Pasquina Ignas,akipanda kwenye gari yake baada ya kukabidhiwa jijini Mwanza kwenye hafla ya miaka 10 ya Mpesa.
 Wasanii wa kikundi cha Bujora wa mkoani Mwanza wakitumbuiza.
 Wasanii wa kikundi cha The Happy center, wakitumbuiza kwenye hafla iliyofanyika jijini Mwanza ya kuadhimisha miaka 10 ya Mpesa.


 Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali jijini Mwanza, wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 10 ya Mpesa.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella(kushoto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia, wakati wa hafla ya miaka 10 ya Mpesa iliyofanyika jijini Mwanza.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 22, 2018

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images