Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live

Waziri Dkt. Augustine Mahiga ziarani Norway

$
0
0
Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akipokea taarifa ya kazi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake Stockholm Sweden, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa, katika Hoteli ya Grand Oslo iliyopo kwenye mji wa Oslo, Norway.  

Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akiwa kwenye kikao cha kazi na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Mjini Oslo, Norway kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Kwenye ziara hiyo Waziri Mahiga ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Adolf Mkenda (kulia kwa Waziri), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani Bw. Jestus Nyamanga, Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati Bw. Adamu Zuberi, pamoja na maafisa waandamizi wa Mambo ya Nje. 

IN LOVING MEMORY OF THE LATE MZEE MATTHEW GORDON KAYUZA

$
0
0
It is exactly one year today since the morning of 21st of June 2017 when you were called by God to depart from this world at The H.H. Agakhan Hospital, Dar Es Salaam.

To us (your wife, Children and grandchildren) it is just like yesterday, we still mourn you and things have not been the same without you DAD.

We thank God for the years granted us to live with you; we miss your kindness love and all the caring you showered us.It is still difficult to accept that you are no longer with us. But we believe that you are at a much safer place than this world.

You are much remembered by your beloved wife Mrs. Jill Mum (Mama Vero as you used to call her), your children Veronica, Mickey, Michael, Errovil, grandson Jacob, your brothers, sisters, cousins, Church & Work colleagues, all relatives, neighbours and friends.

There will be a requiem Mass for his remembrance on 23rd of June 2018 at 9.a.m at St Albans Anglican Cathedral Upanga Posta Mpya, Opposite YWCA and Adjacent to EXIM Bank in Dar es salaam.

Please come all to CELEBRATE & CHERISH THE LIFE OF OUR BELOVED DAD MZEE MATTHEW GORDON KAYUZA,

BELOVED DAD, REST IN PEACE.
YOU WILL LIVE IN OUR HEARTS FOREVER

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 21, 2018

MTAZAMO WA WADAU KUHUSIANA NA Infinix HOT 6

$
0
0

Baada ya ujio wa Infinix HOT 6 na kufanya vizuri sokoni kutoka na muonekano na uwezo wake lakini pia wadau wameweza kuongelea upande wake wa pili na kuweza kuyawasilisha kama ifuatavyo. 


Infinix HOT 6 ni simu iliyoboreshwa zaidi katika vionjo vya muziki kama vile spika mbili ikiwa na maana imemlenga zaidi mpenzi wa muziki hivyo basi tulitegemea Infinix HOT 6 kuja ikiwa na headphone kama ilivyo kwa TECNO BOOM J8 na si vi earphone.

Na kulingana na teknolojia kuendelea kukuwa tulitegemea Infinix HOT 6 yenye kasi ya 4G lakini hapa tumeona kampuni ya simu ya Infinix wameturudisha kwenye mfumo wa 3G tunategemea mabadiliko ya mtandao katika matoleo yanayokuja.

Sifa nyengine ambayo ni kijivunia ni uwezo wa kamera simu inakamera nzuri sana ya megapixel 13 nyumba ikiwa na flashi mbili na megapixel 5 mbele ikiwa na flashi. Infinix HOT 6 inakupa uhakika wa picha nzuri wakati wowote ule hata katika mwanga hafifu. Lakini pia muonekano wake unavutia sana ikiwa na wigo mpana wa kioo cha 18:9 kwa nchi 6.0.

Katika upande wa Android ipo vizuri sana Infinix HOT 6 imekuja na Android 8.1 yenye kuzuiya uishaji wa chaji katika simu kwa haraka lakini pia imesaidia simu kuwa na ‘application’ mpya kama vile face id lakini pia imeongeza ufanisi katika simu.
Kuhusiana na uwezo wa processor sio kama vile tulivyotegemea tumeona simu nyingi zikija na Qualcomm spandragon kama ilivyo kwa toleo la  awali la Infinix HOT S3 lakini kampuni imeturudisha nyuma na MTK6580 processor ya 1.3 ghz quard core.
 Na uhakika wa kudumu na chaji ni mkubwa inabetri ya ujazo wa 4000mAh inaweza kuhimili matumizi ndani ya siku mbili pasipo kuzima.

PASS YATAMBULISHA FURSA MPYA YA MIKOPO KWA WADAU WA SEKTA YA KILIMO NCHINI.

$
0
0
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .

Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo nchini (PASS) imeingia makubaliano na Mfuko wa uwekezaji wa biashara na kilimo Afrika (AATIF) kusaidia wadau wa sekta ya Kilimo nchini kwa kutoa mikopo mikubwa itakayowezesha utekelezwaji wa miradi mikubwa ya kilimo.

Makubaliano haya baina ya PASS na AATIF yanatajwa kuwa mkombozi wa changamoto za muda mrefu za wadau wa sekta ya Kilimo ambao wamekuwa wakipitia kwa kushindwa kupata mikopo ya muda mrefu kutoka kwa taasisi za kifedha hapa nchini kutokana na ufinyu wa muda wa urejeshwaji wa mikopo hiyo. 

Kwa kiasi kikubwa hali hii imekuwa ikitajwa kama sababu ya sekta hii kushindwa kuwa na maendeleo makubwa kutokana na mipango mingi kujikita katika uwekezaji wa muda mfupi. 

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutambulisha fursa hiyo kwa wadau wa kilimo na baadhi ya taasisi za fedha iliyofanyika mapema leo asubuhi katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Bwana Nicomed Bohay amesema.hatua ya upatikanaji wa mikopo mikubwa na ya muda mrefu kwa wadau wakubwa wa kilimo utachochea ukuaji wa sekta ya kilimo. 

“Malengo yetu sisi ni kutengeneza mashirikiano baina ya taasisi hizi ili ziweze kupata mikopo hii, imani yetu kama PASS nikuwa itachochea uwekezaji mkubwa katika maeneo mbalimbali ya kilimo na hivyo kuifanya sekta ya kilimo nchini kuwa mdau mkubwa wa falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya kuziwezesha sekta binafsi na hasa kilimo katika kushiriki katika uchumi wa viwanda” Amesema Bwana Nicomed Bohay. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Binafsi ya kusaidia sekta ya kilimo nchini (PASS) Bw,Nicomed Bohay akizungumza wakati wa kutambulisha fursa mpya kwa Wadau wa sekta ya Kilimo. 
Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Kilimo wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya PASS wakati wa utambulishaji wa fursa mpya kwa wadau wa sekta ya Kilimo.
Mwakilishi wa AATIF, Bwana Samuel Ndonga akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam .
Meneja uwekezaji Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Mfuko wa UGEAP,Sonja Riedke akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya PASS. 

WAZEE WA MILA MARA WAENDELEA KUPINGA UKEKETAJI KWA MTOTO WA KIKE.

$
0
0
Na Frankius Cleophace, BUTIAMA

Wazee wa Mila Muungano wa koo 12 kabila la Wakurya kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga Tarime, wameendelea kutoa Elimu ya Kupinga suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike kwa lengo la Kumnusuru ili atimize ndoto yake ya kupata Elimu na kutimiza Serikali ya Viwanda.

Wazee hao Muungano wa Koo 12 wamezungukia Koo 12 Wilayani Tarime kwa Kutoa Elimu ya kupinga Ukeketaji huku wakitoa Matamko ya Kuondoa Miiko ambayo imekuwa ikikandamiza Mtoto wa kike ambaye hajakeketwa kupitia Mikutano ya hadhara lengo  ikiwa ni kufikisha Ujumbe.

Licha ya kutoa Elimu hiyo sasa wazee hao wameamua kwenda Wilaya ya Butiama kwa lengo la kufikisha ujumbe huo uliokusudiwa, lengo ni kunusuru Mtoto wa kike.

Akitoa Elimu hiyo Mwita Nyasibora ambaye ni Katibu Msaidizi wa koo hiyo amesema kuwa ,Koo ya Bukenye ni kubwa imesambaa mpaka Wilaya ya  jirani ya Butiama, hivyo wameona ni vyema kufikisha Elimu hiyo ili wasije kukiuka na kukeketa Mtoto wa kike kwa kuwa wazee tayari wamekataa Ukeketaji.

“Sisi kama Wazee Muungano wa Koo12 tumeisha kataa Ukeketaji na Koo itakayokiuka iwajibishwe yenyewe” alisema Mwita.

Mmoja wa wazee wa Mila ametoa ushuhudi jinsi gani Mwanamke zamani alivyokuwa akinyanyaswa wakati mwingine kukeketwa wakati akijifungua jambo ambalo lilikuwa linamwongezea Uchungu mara mbili na kuendeleaza Ukatili lakini kwa sasa wazee hao wameona hakuna faida ya kukeketaji bali hasara ndo nyingi kuliko faida.

Mwenyekiti wa kijiji cha Buswahili Wilaya ya Butiama,Wambura Mwema amesema kuwa kuna haja kubwa ya Wazee hao wa Mila kula kiapo kuhusu Matamko yao ili atakayekiuka ka kukeketa Mtoto wa kike achukuliwe hatua peke yake huku akisema kuwa Serikali inaungana na wazee hao kutokomeza Ukeketaji.
Picha ya Pamoja Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Marea na Koo ya Bukenye Wilayani Butiama baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika kijiji cha Kongoto Kata ya Buswahili Wilayani Butiama lengo ni kuzungumzia Mikakati ya Kupiga Vita Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
Katibu Msaidizi wazee wa Mila Muungano wa Koo12 ,
Mwita Nyasibora 
akitoa Elimu kwa wazee hao juu ya madhara ya Ukeketaji kwa Mtoto wa kike, ambapo amesema kuwa Wilaya ya Tarime wamezunguka na kutoa Elimu hiyo kwa jamii,hivyo wameamua kufikia Koo ya Bukenye ambayo inaenda mpaka Wilaya ya Butiama.
Mwenyekiti wa Muungano wa wazee wa Mila kabila la Wakurya Wilayani Tarime Mkoani Mara,Nchagwa Mtongori  akijibu baadhi ya Maswali katika kikao hicho likiwemo suala la kutokomeza Wizi wa Mifugo na Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
wazee wa Mila wakiwa katika Kikao cha pamoja

 Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukenye Wilaya ya Butiama 
Werema Osombe 
akiomba aWazee hao kupiga Vita suala la Wizi wa Mifugo ambayo inaibiwa kutoka Wilayani humo na kupelekwa Tarime.
Baadhi ya Wazee wa Mila  wakiwa katika Kikao cha pamoja.

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT.MAGUFULI AKIWA DODOMA,IRINGA HADI MOROGORO. MEI 2018

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAONYA WANAOFANYA BIASHARA YA UTALII KINYUME CHA SHERIA


TAZAMA MATANGAZO LIVE RAIS MAGUFULI AKIPOKEA GAWIO LA SERIKALI KUTOKA TTCL.

MMILIKI WA IPTL ARUHUSIWA KUZUNGUMZA NA MKEWE MAHAKAMANI

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth kuongea na mke wake mahakamani hapo baada ya kutukumuona kwa muda wa miezi mitatu.

Ruhusa hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi hilo kutokana na kutokuwa na kibali cha kumuona mumewe gerezani.

Kabla ya kutolewa kwa ruhusa hiyo, Wakili wa utetezi, John Chuma ameiomba mshtakiwa aweze kuonana na mkewe ambaye hajaweza kumuona kwa kipindi cha miaka mitatu sababu kipindi chote hicho alikuwa amefiwa na mama mkwe wake( mama wa mkewe).

"Mheshimia tunaomba mshtakiwa namba moja (Sethi) aweze kuzungumza na mke wake ikiwezekana hata kumkumbatia ili aweze kumpa pole ya kufiwa na mama yake kwa sababu bado hajapata kibali cha kuruhusiwa kwenda kumuona gerezani,"amesema. 

Akijibu ombi hilo Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai, alidai, " kwa sababu ni ombi anaomba kusalimiana na mkewe hapa mahakamani sina pingamizi lakini kwa magereza kuna taratibu zake na mkewe alizivuruga yeye mwenyewe."

Kutokana na majibu hayo, Hakimu Shahidi aliruhusu mshtakiwa kuzungumza na mkewe mahakamani hapo chini ya uangalizi wa askari magereza.Kesi hiyo ambayo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, imeahirishwa hadi Julai 5, mwaka huu.

Mbali na Seth mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Rugemalira ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka kumi na mawili ya uhujumu uchumi ,utakatishaji fedha na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni mia tatu.
Pichani kushoto ni mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth ambaye ameruhusiwa kuongea na mke wake mahakamani hapo baada ya kutokumuona kwa muda wa miezi mitatu.

WAZIRI WA FEDHA AWASILISHA BAJETI YA SERIKALI YA ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed akionesha mkoba wenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019 wakati alipowasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Wilaya ya Magharibi ‘B’ jana.(PICHA NA HAROUB HUSSEIN). 
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed akisoma hutuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019 katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi uliopo Chukwani Wilaya ya Magharibi ‘B’ jana.

WAKIMBIZI KIGOMA WAMETAKIWA KUREJEA KATIKA NCHI ZAO

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

WAKIMBIZI mkoani Kigoma wametakiwa kurejea nchini kwao, ili waanze kujishughulisha na masuala ya maendeleo kwani kwa sasa nchi zao ziko salama na amani imerejea.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala katika kambi ya Mtendeli wakati wa Siku ya Wakimbikiz Duniani.

Amesema sasa ni wakati wa wakimbizi waliko chini kurudi katika nchi zao kuendelea na majukumu mengine.Amefafanua mkapa sasa baadhi ya wakimbizi 6000 wamerejea nchini mwao kwa hiyari. "Wapo wengine bado wapo nchini kwetu kutokana na kushawishiwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi,"amesema.

Amewaambia wakimbizi hao ni vema wakarejea nchini kwao na kuendelea na maisha yao badala ya kubaki Tanzania kwasababu kuna watu wanawashawishi.Aidha amesema Serikali haitawavumilia wakimbizi wanaoishi katika kambi zilizopo wilayani hapo ambao watabainika kujihusisha na vitendo vya kiualifu.

"Serikali imewahakikishia kuishi kwa amani na usalama wao pamoja na mali katika kambi yao na sambamba na kuilinda amani hiyo ambayo waliikuta nchini," amesema Ndagala Amefafanua kila mkimbizi anatakiwa kufata taratibu na sheria za nchi na kwa kila atakayekiuka taratibu hizo sheria haitamuacha salama lazima itafata mkondo wake.Pia amesema kuna changamoto ya uhalifu, kwani kuna baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakitoka kambini na kwekuharibu mazao katika mashamba ya watanzania.

Awali akisoma hotuba Mwenyekiti wa kambi hiyo Mtena Nizigiyumukiza ameiomba Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi(UNHCR), kufanya mahojiano na wakimbizi ambao hawako tayari kurudi nchini kwako ili wasikilizwe matatizo yao. "Tunaomba pia mtuongezee sabuni pamoja na chakula ikiwa sambamba na kubadilishiwa chakula kwani tumekuwa tukila ugali na imetufanya kutamani wali,"amesema Nizigiyumukiza.

Mkuu wa kambi hiyo Lulu Malima, amewataka wakimbizi hao kutunza mazingira ndani na nje ya kambi na kuacha tabia ya kukata miti ovyo.
Baadhi ya Wakimbizi wa kambi ya Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiadhimisha  katika siku ya wakimbizi duniani,
 Shughuli za burudani hapa na pale zilitolewa katika maadhimisho hayo hapo jana
 Baadhi ya Wakimbizi wa kambi ya Mtendeli iliyopo wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wakiadhimisha  katika siku ya wakimbizi duniani,
 

NAIBU WAZIRI NDITIYE AITAKA TAA KULIPA FIDIA

$
0
0
 Mkurugenzi Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba (NHC), Hakimeni Mlekio, akieleza hatua ya upanuzi wa jengo la abiria katika kiwanja cha ndege cha Dodoma kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia), wakati Naibu Waziri huyo alipokagua maendeleo ya mradi huo. Kukamilika kwa upanuzi wa jengo hilo kutaongeza idadi ya namba ya abiria 35 mpaka 145.
 Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), mkoani Dodoma, Ludovick Ndumbaro akimweleza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia), matumizi ya taa za kuongozea ndege kiwanjani hapo, wakati Naibu Waziri huyo alipokagua maendeleo ya mradi huo. Katikati ni Meneja wa Kiwanja hicho, Bertha Bankwa.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza na  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Bw. Richard Mayongela (kulia), pamoja na uongozi wa TAA, TCAA na TMA mkoa wa Dodoma, mara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa jengo la abiria katika kiwanja cha Ndege cha Dodoma.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akitoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), mkoa wa Dodoma, mara baada ya kukagua karakana ya shirika hilo jijini hapo. Kushoto ni Mkuu wa Stesheni, Bi. Rose Ngauga.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza na watumishi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) mkoa wa Dodoma, mara baada ya kukagua karakana ya shirika hilo jijini humo.
 Watumishi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani), wakati Naibu Waziri huyo alipozumgumza nao mara baada ya kukagua karakana ya shirika hilo jijini Dodoma.Kushoto ni Stesheni masta, Bi. Rose Ngauga.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, akizungumza na Maafisa  wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) mkoani Dodoma, mara baada ya kutembelea ofisi ya mamlaka hiyo. Kushoto ni Afisa Mfawidhi Konrad Shio.

Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akikabidhi zawadi ya kikombe kwa Idara ya upasuaji ambayo imekuwa mshindi wa kwanza kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yalianza tarehe 18 hadi 20 Juni, 2018 kwenye viwanja vya Muhimbili.  Idara hiyo imepatiwa zawadi ya kikombe, fedha na cheti cha ushiriki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akishuhudia shughuli ya kukabidhi zawadi kwa washiriki mbalimbali. Mwenyekiti huyo amefunga maonesho ya siku tatu yalioanza tarehe 18 hadi 20, Juni 2018 kwenye viwanja vya Muhimbili. Wengi walijitokeza kupima afya BURE, kupata elimu na ushauri kuhusu afya zao.
 Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dkt. Juma Mfinanga akipokea zawadi ya kikombe kutoka kwa Prof. Majinge. Pia, Idara hiyo imepatiwa fedha na cheti cha ushiriki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru.
 Wananchi wakitembelea banda la Magonjwa ya Damu na Saratani za Damu katika maonesho yaliofanyika Muhimbili.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akikabidhi zawadi ya fedha na kikombe kwa Idara meno.
 Idara ya macho nayo haikuwa nyuma katika kutoa huduma bora kwa wananchi waliofika kwenye banda lao kwani walishinda kikombe pamoja na feda taslimu.
 Wananchi wakisubiri kuhudumiwa katika banda la lishe kwenye maonesho hayo

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAGONJWA 11 KATI YA 20 WAFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE

$
0
0
Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita  inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa kushirikiana na Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India .

Wagonjwa hao wamefanyiwa upasuaji wa   kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve Replacement).

Wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na wanne kati yao wameruhusiwa kutoka  katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kwa ajili ya kuendelea na matibabu.

Katika kambi hiyo iliyoanza tarehe 18 hadi tarehe 23 mwezi huu  inaenda sambamba na utoaji wa elimu pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa madaktari wetu pamoja na wauguzi. Jumla ya wagonjwa 20  ambao ni watu wazima  wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji.
 Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India  Ali Ascar Beliranwalwa akivuna mshipa wa damu ndani ya kifua na kuunganisha kwenye misuli ya moyo ili kuuongezea moyo damu katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo ya siku sita inayofanywa na Hospitali hiyo kwa kushirikiana na  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Tangu kuanza kwa kambi hiyo jumla ya wagonjwa 11 kati ya  wagonjwa 20 waliopangwa kufanyiwa  upasuaji  wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na  kubadili milango miwili hadi mitatu ya  moyo (Valve Replacement) wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri. 
  Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa  Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India wakimfanyia mgonjwa  upasuaji  wa  kubadili milango ya moyo  (Valve Replacement) ambayo haipitishi damu vizuri kwenye moyo katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa  20 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kambi hiyo.
 Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa  Hospitali ya Saifee ya mjini Mumbai nchini India wakimfanyia mgonjwa  upasuaji  wa  kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku sita inayoendelea katika Taasisi hiyo. Kwa kipindi cha siku tatu tangu kuanza kwa kambi hiyo jumla ya wagonjwa  11 wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.
Picha na JKCI

USAID and Coca-Cola Partner to Improve Water Access for 70,000 Tanzanians

$
0
0
*Rural Water System to benefit remote areas through solar-powered project
The United States Agency for International Development (USAID) and The Coca Cola Foundation (TCCF), through their Water and Development Alliance (WADA) global partnership, commemorated the launch of activities that will transform the lives of more than 70,000 rural Tanzanians. The Coca-Cola Foundation and USAID are supporting project activities with a combined investment of more than US$1 million, primarily focused on an innovative water access project.

“USAID is pleased to contribute to this enterprising approach to use clean technology to access safe water,” said USAID Tanzania Director of Economic Growth Randall Chester. “The project brings opportunity and know-how to villages to manage their own resilient water system. USAID is proud to join international and Tanzanian public and private partners in a worthwhile investment that can transform lives.”

Tanzania has been facing unprecedented water stress. Rural villages often rely on out-of-date and inefficient water point technology for their water systems, resulting in expensive fuel costs, breakdowns, and consequently, a lack of access to safe water for the community. The WADA Tanzania project will install or upgrade solar-powered water systems in 36 villages identified by the Tanzanian Ministry of Water and Irrigation across theDodoma, Kilimanjaro, Mara, Mwanza, Singida, and Tabora regions.

The WADA project will enhance the technical knowledge held in Tanzania’s workforce, through field work and capacity-building collaboration with the University of Dodoma. “The WADA project is a key link for the University of Dodoma academia and students to provide the much needed community service in ensuring sustainability of the village water supplies.” said Professor Flora Fabian, the University of Dodoma’s Director of Research and Publications, Innovations, Consultancy, and Institutional Collaboration.

“For over a decade, The Coca-Cola Company and its Foundation have partnered with USAID, bringing shared opportunity to communities. We are pleased to launch this innovating new project to rural communities in Tanzania, building healthy and resilient villages through improved access to water and sanitation,” said Ahmed Rady, General Manager for Coca-Cola East & Central Franchise.

The sustainability of these systems will be ensured through WADA’s provision of two years of technical support to train and develop water service entrepreneurs in performing basic operations and maintenance tasks. This training will increase the self-reliance of the rural villages, enabling sustained access to a safe water supply. In addition, this project will collaborate with the Ministry of Water and Irrigation, theirRegional and District Water Engineers, and staff and students at the University of Dodoma to improve management of groundwater suppliers across the nation. This will include installing a solar-powered water systemtraining program at the University of Dodoma.

According to Marty Kress, Executive Director of the Global Water Institute at Ohio State, "The Ohio State model for sustainable water systems being deployed through this WADA project is focused not just on the installation of wells but also on the deployment of sustainable operating systems – enabling communities to thrive long after this project ends, rather than becoming reliant on its presence in the region."

WADA Tanzania is being implemented by a consortium of partners led by The Ohio State University and managed inTanzania byWorldServe International. Together, WorldServe International andWaterboys, an American charity founded by US National Football League (NFL) athlete Chris Long, are contributing U.S. $1 million in co-financing to scale project activities.
Mr. Randall Chester, Director of Economic Growth, USAID Tanzania (first left) explains a point during the launch of Resilient Village Water Systems in Dodoma. Looking on is (second left) Catherine Bamwenzaki, Assistant Director, Rural Water Supply Division, Ministry of Water and Irrigation, David Karamagi, Coca-Cola Tanzania Country Manager ( center), UDOM Deputy Vice Chancellor Prof. Peter Msofee (second right) and Haji Ally from Kwanza Bottlers Ltd.

Veteran wa Liverpool atua Dar kwa mwaliko wa Standard Chartered

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Sami Hyypia veteran wa timu ya Liverpool yupo nchini kwa mwaliko wa benki ya Standard Chartered.
Mchezaji huyo mwenye haiba ya aina yake aliwasili nchini Jumanne, kuhudhuria michuano ya kombe la Standard Chartered inayotarajiwa kuanza jumamosi wiki hii.
Akizungumza klatika mkutano na waandishi wa habari Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema benki yake imefurahjishwa sana na ujio wa mchezaji huyo wa zamani.
“Tumefurahi sana kuwa na Sami nchini na kumshirikisha katika michuano ya tatu ya kombe la Standard Chartered . Sami pia atatumia uwepo wake kufanya kazi na timu ya vijana chini ya miaka 17– Serengeti Boys”
Sami Hyypia ni mmoja wa viungo hatari ambao walivaa fulana nyekundu wakati wa utawala wa makocha Gerard Houllier na Rafael Benitez na kumfanya kuwa mmoja wa walinzi hodari barani Ulaya.
Mchango wa Hyypia katika soka la England kulimfanya atambuliwe kwao (Finland) kwa kupewa tuzo za mwanasoka bora wa mwaka kwa miaka saba. (1999, 2001, 2002, 2003, 2005, 2006 na 2008).
Baada ya kusaidia timu yake dhidi ya Sheffield Wednesday  hapo Agosti 7, 1999, Hyypia akawa katika mahusiano mazuri ya kisoka na Stephane Henchoz na kuwa na viungo bora wa ulinzi 2000-01.
Aidha uchezaji wake na Jamie Carragher ulitengeneza kitu kilichokubalika kuwa ngome thabiti  baada ya Liverpool baada ya kutwaa Champions League katika viwanja vya Ataturk.
Hyypia ndiye aliyefunga goli la kukumbukwa sana wakati alipofunga goli dhidi ya Juve katika robo fainali.
Historia ya soka, alisema mtendaji huyo wa Benki, itamweka katika eneo zuri kabisa la kibiashara mchezaji huyo ambaye wapenzi walimweka katika orodha ya kuwa mtu wa 38 kati ya watu 100 waliofanya vyema katika klabu hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akiwa ameongozana na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Gwiji huyo wa Liverpool nchini. Wengine katika picha nyuma kutoka kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika na Tanzania ikiwa ni nchi yake ya kwanza kutembelea huku wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akifurahi jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika na Tanzania ikiwa ni nchi yake ya kwanza kutembelea huku wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro.Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
 Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na ujio wa Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (katikati) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) akipeana mkono na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia mara baada ya mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.
Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akipeana mkono na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (kulia) mara baada ya kumalizika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency-The Kilimanjaro. Katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MKAPA AVUNJA UKIMYA WANAOSUBIRI KUMWAGIWA FEDHA KWA AJILI YA MAENDELEO

$
0
0
*Asema heshima ya nchi ni kujitegemea

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amesema hakuna Mtu wa kutumwagia fedha kwa ajili ya maendeleo yetu, bali yataletwa kwa watu kufanya kazi na heshima ya nchi ni kujitegemea .

Mkapa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua kitabu cha Hali ya umasikini hasa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na Afrika kwa ujumla.

Kitabu hicho kimeandikwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Balozi Martin Lumbanga. Kitabu hicho kimepewa jina la Global Poverty(The Case for Sab-Sahara Afrika)

Kabla ya kuzindua Kitabu hicho Mkapa amesema "Huu utamaduni wa kusubiri kumwambiwa fedha sijui umetoka wapi.Haipo hata katika Chama tawala ya kumwagia pesa."

Akasisistiza kwa kuhoji tena kwa Dunia hii ya Trump? "Lazima tufanye kazi kwa maendeleo yetu badala ya kusubiri fedha kutoka nje,"amefafanua Mkapa.

Mkapa anasema inashangaza unaposikia wapo wanaosubiri kumwagiwa fedha tena utasikia "Neema yaja .Haipo, heshima ya nchi ni kujitambua na kujitegemea."
Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akizundua kitabu cha Global Poverty (The Case For Sub- Sahara Africa) pamoja na Mtunzi wa kitabu hicho Balozi Martine Lumbanga (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuchapisha vitabu ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya(kulia), uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
 Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa  akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Global Poverty (The Case For Sub- Sahara Africa) uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
 Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akionyesha kitabu cha Global Poverty (The Case For Sub- Sahara Africa) mara baada ya kukizindua kushoto ni Mtunzi wa kitabu hicho Balozi Martine Lumbanga na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuchapisha vitabu ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya, Uzinduzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akipokea zawadi ya kitabu cha Global Poverty (The Case For Sub- Sahara Africa) na Balozi Martine Lumbanga mara baada ya Uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
 Mtunzi wa kitabu hicho Balozi Martine Lumbanga (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuchapisha vitabu ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya, katika uzinduzi uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa JNICC jijini Dar es salaam leo.
Balozi Martine Lumbanga(kulia) akisaini kitabu cha mmoja wa wageni waliofika kwenye uzinduzi huo baada ya kukinunua.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

'KUNA ONGEZEKO KUBWA LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA'

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

SERIKALI imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni hali inayotishia afya ya mama na mtoto wakati wa kijifungua pindi wanapofika hospitalini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maedeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Sara Maongezi wakati akifungua Programu ya AstraZeneca ya Healthy Heart Africa (HHA).

Programu hiyo inatokana na ushirikiano wa Touch Foundation na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Lengo ni  kupunguza maradhi ya shinikizo la damu wakati wa mimba.

Maongezi amefafanua ubia uliozinduliwa leo katika mradi huo utakaoongeza utekelezaji wa programu hiyo nchini Tanzania.  

"Ubia huo unakusudia kwa kiasi kikubwa kupunguza kuenea kwa maradhi ya shinikizo la damu, hasa miongoni mwa wanawake wajawazito ikiwa ni kuunga mkono mpango mkakati wa Serikali wa kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza,"amesema Dk. Maongezi.

Ameongeza kupanda kwa shinikizo la damu ni moja ya vihatarishi vikubwa vya ugonjwa wa moyo hali ambayo msukumo wa damu katika moyo  huzuizwa au kukatizwa na chembe chembe za mafuta kwenye mishipa ya koronari  na mwishowe huenda ikasababisha kiharusi.

Amefafanua kwa bahati mbaya, ugonjwa wa moyo ni moja ya vyanzo vikubwa vya kifo nchini Tanzania hasa kwa wajawazito wakati wa kujifungua.

Amesema  kupitia ufadhili wa AstraZeneca, shirika la Touch Foundation litaendeleza mpango wa Healthy Heart Africa  ambao tayari unatekelezwa huko Kenya na Ethiopia, kwa kufuata mazingira halisi ya Tanzania kama linavyotekelezwa mpango wake wa Mobilizing Maternal Health (MMH) katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza.

 "Serikali tunaukaribisha ubia huu mpya kwa vile unakwenda sambamba na azma yetu inayolenga kinga kwa jamii, kuboresha afya, kupima, na kutoa matibabu mapema, na kuwasaidia waathirika. 

NSSF YAVUNA WANACHAMA ELFU80 KAMPENI YA 'ZAMU YAKO'

$
0
0
KAMPENI ya kitaifa ya kuhamasisha watu binafsi pamoja na walioko kwenye sekta isiyorasmi kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) ya 'zamu yako', imeanza kutoa matokeo chanya baada ya zaidi ya watu elfu 80 kujiunga na mfuko huo hadi sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye kikao na viongozi wa vikundi vya wajasiriliamali na vyama vya ushirika mkoa wa Arusha, Mwenyekiti  wa kamati ya kuratibisha sera ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, Maryam Muhaji alisema kampeni hiyo ilianza Juni mosi mwaka huu katika Jiji la Dar es salaam.

Alisema  tangu kuanza kwa kampeni hiyo iliyoanzia katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Kagera, Mara na Arusha, tayari wanachama elfu 80 wamejiunga na mfuko wa NSSF na wameanza kupata huduma.

“Hii kampeni ya ‘Zamu Yako’ ni kampeni maalum ya kuhamasisha watu walioko katika sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko wa NSSF kwa kuwa katiba inamtaka kila mwananchi kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ni haki yake, hivyo baada ya kugawanywa kwa mifuko hii tumeanzisha kampeni hiui ili kutoa fursa kwa watu wote,”alisema.

Alisema  kwa kuwa lengo la Serikali ni kuwafikia wananchi wenye kipato cha chini kuweza kupata huduma muhimu, mfuko wa NSSF utaendelea na kampeni hiyo katika mikoa mbalimbali nchini na imepanga hadi kufikia Juni 2019 iwe imeshaandikisha wanachama laki 3.

Mwenyekiti wa kamati ya kuratibisha sera ya hifadhi ya jamii katika sekta isiyorasmi  kupitia mfuko wa NSSF, Maryam Muhaji akizungumza na viongozi wa vikundi vya ujasiriamali na saccos mkoa wa Arusha katika ukumbi wa NSSF Arusha kuhamasisha kujiunga na mfuko huo.

Washiriki wa kikao cha semina kwa viongozi wa vikundi vya wajasiriamali na  vyama vya  ushirika mkoa wa Arusha wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya kuratibisha sera ya hifadhi ya jamii katika sekta isiyorasmi kupitia mfuko wa NSSF Maryam Muhaji (hayuko pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110087 articles
Browse latest View live




Latest Images