Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

MWAKILISHI WA UNICEF AMUAGA RAIS DK.SHEIN

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la kusaidia Watoto Tanzania (UNICEF) Bibi Maniza S.Zaman alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Mwakilishi wa Shirika hilo Ofisi ya Zanzibar Bibi.Francesca Morandimi (kushoto) aliyefika kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa Kazi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la UNICEF anayefanyia kazi zake Zanzibar Bibi.Francesca Morandimi (kushoto) aliyefika kumuaga Rais alipofika Ikulu Mjini Zanzibar baada ya kumaliza muda wake wa Kazi akifuatana na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la kusaidia Watoto Tanzania (UNICEF) Bibi Maniza S.Zaman (katikati).
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la kusaidia Watoto Tanzania (UNICEF) Bibi Maniza S.Zaman alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Mwakilishi wa Shirika hilo Ofisi ya Zanzibar Bibi.Francesca Morandimi (hayupo pichani) aliyefika kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa Kazi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la kusaidia Watoto Tanzania (UNICEF) Bibi Maniza S.Zaman (katikati)alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Mwakilishi wa Shirika hilo Ofisi ya Zanzibar Bibi.Francesca Morandimi (kushoto) aliyefika kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa Kazi. (Picha na Ikulu)

PROFESA KAMUZORA ATEMBELEA NA KUONA UTENDAJI KAZI WA MFUMO UNGANISHI WA USIMAMIZI WA TAARIFA ZA ARDHI (ILMIS)

0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora amefurahishwa na utendajikazi wa Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia uliopo katika Wizara ya Ardhi Jijini Dar es Salaam.

Mradi huu utasaidia kupatikana kwa taarifa kwa urahisi na kuongeza ufanisi wa utunzaji wa taarifa za wananchi na kupunguza muda wa kutafuta taarifa kama ilivyokuwa hapo awali, alisema Prof. Kamuzora.

“Mfumo huu pia utaiwezesha Serikali kutambua walipajiwa wa ardhi, itasaidia kuboresha mazingira mazuri ya kufanya biashara na vilevile ukusanyaji wa mapato utaongezeka kwa wingi ambapo kwa sasa Mradi  huu unatekelezwa katika wilaya mbili za mfano Kinondoni na Ubungo”. Alisema Prof. Kamuzora.

Serikali imejipanga kuongeza wataalamu watakaoweza kuendesha mifumo hii pale wafadhili watakapoukabidhi ili tuumiliki na tuwezwe kuendeleza na hata kwenda kwenye mikoa mingine ili kuweza kutoa huduma za kisasa kwa wananchi.

Mapema: Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dr. Moses Kusiluka alisema, serikali imetenga fedha ili kuweza kuwajengea uwezo wataalamu wa Tehama ili kuwezo kutumia mfumo huo pale wafadhili watakapo ukabidhi rasmi katika Wizara ya Ardhi.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu  Prof. Faustin Kamuzora akizungumza baada ya kutembelea chumba kinachoanda Majadala ya usajili wa ardhi kupitia Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa taarifa za Ardhi ( ILMIS) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia katika Ofisi za Wizara ya Ardhi tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Makazi Dr. Moses Kusiluka akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora walipotembelea chumba kinachoandaa majalada ya Msajili wa ardhi kwa kupitia Mfumo Unganishi wa Usimamizi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS) katika Ofisi hiyo tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi  wa Mradi Erick Gies Kisai akimweleza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora namna chumba hicho kinavyoendesha kazi za usajili wa ardhi katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Kukuza Ushindani wa Sekta Binafsi (PC-PSCP) Barney Laseko akimwelezea Prof. Faustin Kamuzora namna mradi wa Mfumo Unganishi wa usimaizi wa Taarifa za Ardhi (ILMIS)  unavyofanyakazi katika Wizara ya Ardhi Tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam .
Baadhi ya wafanyakazi  katika chumba cha uandikishaji wa ardhi ngazi ya kamishna wakiendelea na kazi wakati Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora alipotembelea mradi huo tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.
Msimamizi  Uandikishaji wa Ardhi ngazi ya Kamishna Costa Chaula akimwelezea Prof. Faustin Kamuzora namna wanavyofanyakazi katika chumba hicho wakati wa ziara fupi iliyofanywa ofisini hapo tarehe 20 Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustin Kamuzora akipitia moja ya jalada linafanyiwa kazi katika chumba cha uandikishaji wa ardhi ngazi ya kamishna wakati wa ziara fupi iliyofanyika ofisi hapo tarehe 20Juni,2018 Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

USAID and Coca-Cola partner to improve Water Access for 70,000 Tanzanians

0
0
Representatives from the United States Agency for International Development (USAID), The Coca Cola Foundation, the University of Dodoma, and the Singida Regional Water Office pose for a group photo during an event on Tuesday, June 19 commemorating the launch of an innovative water access project. The program will introduce solar powered systems in 36 villages co-identified with the Tanzanian Ministry of Water and Irrigation, ensuring a safe, reliable water supply that can even be monitored via mobile phone. (Photo credit: U.S. Embassy Dar es Salaam).

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi, bungeni  jijini Dodoma Juni 20, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Joseph Kakunda, bungeni jijini Dodoma Juni 20, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mvomero  Suleiman Saddiq kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2018 YATENGA SIKU TATU KUPOKEA MALALAMIKO NA KERO.

KONGAMANO LA 6 LA KIMATAIFA LA MADAKTARI WA MIFUPA LAANZA MOI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

KONGAMANO la kimataifa la madaktari wa mifupa duniani limeanza kufanyika leo hadi Juni 23 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Ambapo linaratibiwa na Taasisi za IGOT, SIGN, OTA, OA ALLIANCE na Chuo Kikuu cha Calfonia San Fransisco cha Marekani na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.Akizungumza leo Dar es salaam Daktari bingwa wa mifupa Bill Aonga amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa na madaktari bingwa wa Mifupa wa MOI kwa kishirikiana na wakufunzi kutoka Marekani, Uingereza na Switzerland.

Amefafanua mafunzo hayo yatalenga mbinu mpya za matibabu ya mivunjiko mbalimbali ya Mifupa, magonjwa yatokanayo na ajali na namna ya kufidia kilande cha mfupa kilichopotea kutokana na ajali.Ameeleza washiriki sita kutoka Tanzania watapewa mafunzo hayo na baadaye watakuwa wakufunzi wa mafunzo hayo bila kutegemea wageni.

Pia daktari bingwa wa mifupa aliyebobea katika nyonga na kiuno Joseph Mwanga amesema idadi kubwa ya watanzania walioshiriki katika mafunzo hayo watanufaika na ujuzi waliopata utanufaisha na kuendeleza wengi.Mafunzo hayo wamelenga kuangalia namna ya kuunga mifupa na misuli mara baada ya kuchanika na kupoteza misuli.

Aidha imeelezwa taasisi ya MOI inatambulika kama kitovu cha weledi katika matibabu ya mifupa kwa muda mrefu wa paja kwa kutumia teknolojia ya kuweka chuma ndani ya mfupa.Na teknolojia hiyo hutumika zaidi duniani na hadi sasa taasisi ya MOI imefikisha wagonjwa zaidi ya 8,000 idadi ambayo haijafikiwa na hospitali yoyote duniani.

Pia mafunzo hayo hufanyika kila mwaka kwa miaka 6 mfululizo ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani na kuwapa mbinu mpya madaktari bingwa ili waweze kuendana na teknolojia ya matibabu duniani inayobadilika mara kwa mara.
Daktari Bingwa wa Uhamishaji wa ngozi Profesa kutoka Marekani,Profesa Michael Terry akizungumza na Madakri wa mifupa Duniani katika kongamano lililo fanyika leo jijini Dar as Salaam.
 Daktari Bingwa wa upasuaji Mifupa na Muhadhiri wa chuo Kikuu cha Afya Mhuhimbili,Bill Aonga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano lililo fanyika leo jijini Dar as Salaam.(picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Wadau mbalimbali wa afya wakiwa katika kongamano hilo.

WAZIRI UMMY MWALIMU AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA MDEMU

0
0
WAZIRI wa Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya Mdemu kilichopo Wilayani Bahi Jijini Dodoma baada ya kuridhishwa na ujenzi huo.

Akizungumza wakati wa kuweka jiwe hilo la msingi Waziri Ummy alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imefanya kipaumbele maboresho mbalimbali hususan katika sekta ya afya nchini.

“Nilipofika hapa mwaka 2016 niliona wanawake wajawazito wanalala kwa kubanana na wengine wanafariki kwa uzazi pingamizi hivyo nikaona tuanze kujenga vyumba vya upasuaji wa dharura nchini ikiwemo wodi ya wanawake wajawazito ili kuokoa Maisha ya mwanamke na mtoto anapojifungua ” alisisitiza Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa mpaka sasa wilaya ya Bahi imefikia asilimia 98 ya wanawake wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya amabapo Kitaifa inaonesha katika kila wanawake 100 wanawake 51 ndo hijifungilia kwenye vituo vya afya.Vilevile Waziri Ummy amesema kuwa Juhudi za Serikali katika kuokoa vifo vya wakina mama wajawazito Kijijini Mundemu atawapatia gari ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya rufaa kutoka kituo kituoni hapo kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Bi. Benadertha Januari amesema kuwa wamefanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 4 mwaka 2015 mpaka vifo 3 mwaka 2017 na vifo vya watoto chini ya miaka 5 kutoka 50 mwaka 2015 mpaka kufikia vifo 12 2017.Aidha Bi. Januari amesema kuwa wamefanikiwa kukusanya chupa za damu salama 1640 kati ya chupa 2216 ya malengo waliojiwekea ambayo ni sawa na asilimia 74 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Kata ya Mundemu Bw. Reuben Ntiruka amesema kuwa Kituo cha afya Cha Mundemu kinapokea rufaa ya kutoka Zahanati 21 za vijiji vitatu ambayo idadi ya walengwa wake ni wananchi 9103.Mbali na hayo Bw. Ntiruka ameiomba Serikali kuijengea Kituo hicho Uzio ,nyumba za watumishi, kuongeza idadi ya watumishi pamoja gari ya kubebea wagonjwa kwani ndio changamoto kubwa zinazoikumba Kituo hicho cha afya.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akiweka jiwe la msingi Mradi wa ukarabati na uboreshwaji katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma leo.kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mzee na Mbunge wa Bahi Bw. Omari Baduel.

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua majengo ya wodi ya wajawazito,jengo la upasuaji wa dharura ,Mochwari ,sehemu ya kuchomea taka na maabara katika Kituo Cha Afya Mdemu kilichopo Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi leo. 
 Mbunge wa Jimbo la Bahi Bw. Omari Baduel akiongea na wanakijiji wa kata ya Mdemu hawapo pichani wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kituo cha Afya Mdemu wilayani Bahi  jijini Dodoma, kushoto waliokaa ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Bi. Elizabeth Kitundu 

 Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo cha afya Mdemu uliofanywa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wilayani Bahi  jijini Dodoma.

 Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kumsikiliza na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi katika Kituo cha afya Mdemu uliofanywa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wilayani Bahi  jijini Dodoma.

Mafundi wakiwa katika hatua ya mwisho ya kumalizia jengo la Mochwari lilipo katika Kituo cha Afya Mdemu Wilayani Bahi Mkoa Dodoma .PICHA NA WIZARA YA AFYA -DODOMA



UJENZI WA DARAJA LA KIFAULONGO KUOKOA MAISHA YA WAKAZI WA KATA YA TAMBANI, MKURANGA


NEWZ ALERT:RAIS DKT SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein amemteua Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mheshimiwa Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Dkt. Shein amefanya uteuzi huo kwa kutumia uwezo aliopewa chini ya Kifungu 119 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 .

Aidha amewateua wajumbe sita wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambao ni Bwana Mabrouk Jabu Makame, Bwana Feteh Saad Mgeni, Bwana Makame Juma Pandu, Dkt. Kombo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhan Abdalla na Bibi Jokha Khamis Makame.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotiwa saini na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, uteuzi huo umeanza leo tarehe 20 Juni 2018.

Wajumbe wote wa Tume ya Uchaguzi walioteuliwa wataapishwa siku ya Ijumaa tarehe 22 Juni 2018 saa 4.00 asubuhi Ikulu Mjini Zanzibar.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

WAZIRI WA MIFUGO AOMBA RADHI BUNGENI...SPIKA ATOA MSIMAMO

0
0
*Ni kwa kitendo cha Wizara kuingia mgahawa wa Bunge kupima samaki
*Amwambia Waziri Mkuu kilichofanyika si uungwana, akubali kusamehe yaishe

Na Said Mwishehe,
wa Globu ya jamii

PAMOJA na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina kuliomba radhi Bunge kwa kitendo cha Wizara yake kuingia kwenye mgahawa wa Bunge bila kibali na kupima samaki waliopikwa kwa rula, Spika wa Bunge Job Ndugai amasema kitendo hicho ni udhalilishaji.

Juzi Waziri Mpina alitoa maagizo kwa watendaji wa Wizara yake kuingia kwenye Mgahawa wa Bunge na kisha kuingia jikoni kupima samaki ambao tayari walikuwa wamepikwa.Kitendo hicho kilisababisha wabunge kuchachama na kutoa hoja ili kujadili kitendo hicho.Mbunge Peter Serukamba ndio aliyeomba muongozo.
Hivyo leo Mpina akiwa bungeni mjini Dodoma ameomba radhi Bunge pamoja na Spika wa Bunge kwa kitendo hicho.Hata hivyo Spika Ndugai amemueleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa kitendo hicho ni udhalilishaji na si sahihi."Tunamshukuru Waziri kutokana na maelezo ambayo ameyatoa lakini niseme tu kwa Waziri Mkuu tumesikitishwa na kilichotokea.
"Sisi si Bunge pekee duniani bali ni sehemu ya mabunge mengine ya jumuiya ya madola.Ikisikika kuna Waziri amefanya kitendo hiki bungeni ni kosa. "Hata kama kuna kosa la jinai ambalo limefanyika ndani ya Bunge ni vema Spika akajulishwa badala ya watu kuingia tu,"amesema Spika Ndugai.

WABUNGE WA CCM WAMUAGA KINANA JIJINI DODOMA.

0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipeana Mkono na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana mara baada ya kumkabidhi zawadi mbalimbali alizotoa kwa niaba ya Kamati ya Wabunge wa CCM katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma  jana.
 Meza kuu
Wajumbe wa Sekretariet ya CCM wakiimba wimbo alipowasili Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Ndg Abdulrahman Kinana katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma jana .
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Kmati ya Wabunge wa CCM Mhe Majaliwa Kassim akimkabidhi zawadi mbalimbali Katibu Mkuu wa CCM  kwa niaba ya Kamati ya Wabunge wa CCM katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga Ndg Abdulrahman Kinana   na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma jana.


Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu Abdurahmani Kinana akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally.
 Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wabunge katika hafla aliyoandaliwa na wabunge wa CCM ya kumuaga  na kumkaribisha Katibu Mkuu mpya, Dk Bashiru Ally, jijini Dodoma jana.
 Sehemu ya wabunge wakifuatilia Hafla hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA CRDB YAIONGEZEA MTAJI WA SH. 3.2 BILIONI BENKI YA WANANCHI TANDAHIMBA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kulia), akifafanua jambo mbele ya waandhishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kusaini Mkataba wa kuiwezesha Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA) kimtaji iliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Benki ya CRDB imeipatia Benki ya Wananchi Tandahimba kiashi ya Sh. 3.2 Bilioni kuongeza mtaji wake. wengine pichani toka kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA), Rajabu Mmunda, Meneja Mkuu wa Benki ya Wananchi Tandahimba, Mugwagi Steven.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA), Rajabu Mmunda akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akibadilishana Mkataba na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA), Rajabu Mmunda  wa kuiwezesha Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA) kimtaji katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amteua Mohammed Ali Ahmed kuwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Zanzibar

MWANAMUZIKI NANDY KUNOGESHA SHINDANO LA MISS MWANZA 2018

WASHIRIKI WA MISS ARUSHA 2018 KUOSHA MAGARI KUCHANGISHA FEDHA KUBORESHA WODI YA KINAMAMA HOSPITALI YA MOUNT MERU


Shamba la Miti la Iyondo-Mswima wilayani Ileje Mkoani Songwe kuanzishwa mwaka huu

0
0
 Na Daniel J. Mwambene, Afisa Habari Ileje
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Misitu (TFS) imeamua kuanzisha Shamba la Miti la Iyondo - Mswima ukiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2015/2020 ibara ya 31 vifungu vya b,c,d,e na f kuhusiana sekta ya Maliasili. 
Kwa mujibu wa Meneja wa Mradi wa Iyondo-Mswima Ndg. Deograsian Kavishe upandaji miti utaanza rasmi katika mwaka wa Fedha 2018/2019 ikiwa baadhi ya kazi zilianza kutekelezwa na Mradi katika mwaka wa fedha 2017/2018. 
Kuanzishwa kwa shamba hili la Katengele kunaifanya Tanzania kuwa na mashamba ya miti ya kupandwa 23 yakiwa yanapatikana katika Kanda mbalimbali kati ya hayo manne yapo katika hatua ya uanzishwaji likiwemo hilo la Iyondo-Mswima wilayani Ileje. 
Kutokana na soko hili kuwa ndani ya msitu wa hifadhi na ili  kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa kufuata Kanuni, Sheria na taratibu za uanzishwaji na uendeshaji wa miradi ya upandaji miti hapa nchini, soko hilo halistahili kuendelea kuwepo mahali lilipo, hivyo linatakiwa kuhamishiwa sehemu nyingine nje ya hifadhi zikiwemo kaya 13 zinazoishi ndani ya eneo hilo. Ujenzi wa miundombinu katika eneo lililochaguliwa utafanywa na serikali kupitia wakala wa Misitu (TFS). 
 Ili kuendeleza mahusiano mazuri na wadau mbalimbali wa maendeleo TFS imeshirikisha Baraza la Madiwani, wataalam wa Halmashauri pamoja na Serikali Kuu. Michakato hiyo ilianzia kwenye vikao vya CMT, Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango pamoja na Baraza la Madiwani ambalo liliridhia kuhama kwa Mnada wa Soko hilo kutoka mahali lilipo na kwenda sehemu nyingine. 
 Baraza la Madiwani baada ya kujadili na kupitia mapendekezo ya vikao vilivyotangulia kisheria liliridhia juu ya kuhama kwa soko la Katengele kutoka mahali lilipo na kwenda Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala katika barabara ya Ibaba - Katengele ili kupisha uanzishwaji wa Mradi wa Shamba la Miti la Iyondo - Mswima. 
 Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya upigaji kura kufanyika ambapo Wah. Madiwani wane waliliridhia mnada wa Katengele uhamishiwe eneo la Ghala - Sange huku Madiwani 18 wakiridhia Mnada wa Katengele uhamishiwe Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ndugu Haji Mnasi (aliyesimama) akizungumza kwenye Baraza Maalum kuhusu Mnada wa Katengele
Eneo la Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala panapotarajiwa kuhamishiwa Mnada wa Katengele.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje  Mhe.Ubatizo Songa akiongoza Wahe. Madiwani na Wataalam  wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje walipotembelea eneo la Mradiwa Upandaji Miti la Iyondo-Mswima.Chini ni kitalu cha miti kilichopo Katengele-Ileje kikitarajiwa kubadilisha sura ya msitu wa Iyondo-Mswima wilayani Ileje.

Kusoma taarifa kamili BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 20.06.2018

LUDOVICK UTOUH ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA TAASISI YA TEITI

Vitabu Vinapobebana

0
0
Na Profesa Joseph Mbele

Nadhani kila msomaji wa vitabu anatambua manufaa na raha ya kusoma vitabu vya aina mbali mbali. Hivi ninavyoandika, ninakaribia kumaliza kusoma Riding the Waves of Culture: Understanding Diversity in Global Business, kitabu ambacho nilikitaja siku kadhaa katika blogu hii.

Nimekifurahia sana kitabu hiki, kwa jinsi kinavyoongelea masuala ya tofauti za tamaduni, mada ambayo ninashughulika nayo sana. Kinanifanya nielewe undani wa yale niliyoandika katika Africans and Americans: Embracing Cultural Differences.
Kwa mfano, sura ya kitabu hiki iitwayo "How We Manage Time," imenipa msamiati wa kuelezea yale niliyoelezea katika sura iitwayo "Time Flies But Not in Africa." Nimeelewa kwamba msimamo wetu wa-Afrika ni "synchronic" au "polychronic" na msimamo wa wa-Marekani ni "sequential." Tofauti zetu ambazo nimezielezea katika kitabu changu zimejengeka katika mitazamo hiyo miwili.
Nitoe mfano. Kama ninavyoeleza katika kitabu changu, sisi tunaonekana hatuna nidhamu ya kuchunga muda, katika mazingira yetu, wakati wa-Marekani wanachunga sana muda, katika mazingira yao. Hizi ni tofauti tu, wala si ishara kwamba utamaduni moja ni bora kuliko mwingine. Kila utamaduni una mantiki yake.
Dhana zilizomo katika Riding the Waves of Culture zimenipa mianya ya kufafanua yale niliyoandika katika kitabu changu. Tofauti kubwa kati ya vitabu hivi viwili ni kuwa Riding the Waves of Culture kimeandikwa kitaaluma na ni kikubwa, wakati Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kimeandikwa kiwe rahisi kusomwa na yeyote na ni kifupi sana.       Kusoma mengi zaidi BOFYA HAPA

JAJI WA MAHAKAMA KUU YA NCHINI UGANDA ATEMBELEA JENGO JIPYA LA KISASA LA MAHAKAMA YA MWANZO NA MAHAKAMA YA WILAYA YA KIGAMBONI

0
0

 Jaji wa Mahakama Kuu ya Uganda, Mhe. Paul Gadenya akitia saini kitabu cha wageni pindi alipowasili katika Mahakama ya Wilaya Kigamboni kujionea jengo hilo la kisasa lililojengwa kwa teknolojia ya ujenzi ya Moladi, mbali na kutembelea jengo hilo Jaji Gadenya ametembelea Ofisi za Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ‘JDU’ kupata taarifa ya maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama kwa lengo la kuboresha huduma za utoaji haki nchini, aliyesimama kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo, akimpitisha Mhe. Jaji Gadenya kukagua sehemu mbalimbali za jengo hilo la kisasa, aliyepo nyuma ya Mhe. Gadenya ni Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Tathmini, Mahakama, Bw. Sebastian Lacha. 
 Mhe. Jaji Gadenya (kushoto) akijadili jambo na wenzake, kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Tathmini, Mahakama, Bw. Sebastian Lacha.
Picha ya pamoja nje ya jengo jipya la kisasa la Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Gadenya ameisifu Mahakama kwa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika na ambayo tayari ameshafanyika kwa ustawi wa Wananchi.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images