Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAPIGA VITA WANANCHI KUMALIZA KESI ZA UKATILI KIENYEJI.

$
0
0
Na Frankius Cleophace Rorya

Serikali Wilayani Rorya Mkoani Mara imepiga Marufuku Jamii kumaliza kesi zinazohusu Ukatili wa Kijinsia Ukiwemo Ubakaji, Utelekezaji wa watoto wadogo, Kuchomwa Moto na Kuwatenga kwa watoto wenye Ulemavu bila kuripoti Kwenye Vyombo vya Sheria ili kuchukua hatua kali kwa wanaotenda Ukatili huo na kumaliza kiundugu jambo ambalo linazidi kunyima Mtoto haki zake za Msingi na hawatalifumbia Macho Kamwe.

Hayo yamebainishwa na Gabriel Paul ambaye ni Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya kwa niamba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.

Gabriel amesema kuwa katika Maeneo mengi vitendo vya Ukatili dhidi ya mtoto vimekuwa vikifanyika lakini jamii wanamaliza Matatizo hayo kiundugu bila kushirikisha Vyombo vya Sheria ili kulinda Mtoto dhidi ya Ukatili huo.Pia Gabriel amezitaka idara zote ikiwemo idara ya Maendeleo ya Jamii pamoja na Mashirika Mbalimbali kuendelea kutoa Elimu kwa Jamii juu ya Madhara ya Ukatili wa kijinsia ikiwa nipamoja na kujua Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.

Wilaya ya Rorya Imekuwa ikikumbwa na Changamoto ya Mimba kwa Watoto wa Shule za Msingi na Sekondari ambapo Afisa Elimu Sekondari Gabriel Paul anaeleza Mikakati ya Serikali ili kunusuru Mabinti hao huku akisema kuwa tayari watumiwa saba wamefikishwa Mahakani na wamejenga Mabweni saba na wanaendelea kuhamasisha jamii kujenga Mabweni kwa lengo la kuwapunguzia Umbali mrefu mabinti kwa ajili ya kutafuta Elimu na wakati Mwingine kushawishika na kujiingiza kwenye Mapenzi na kupata Mimba zisizojarajiwa.

Ossoro Siris ambaye ni Mwenyekiti Shirika la Shirika la Tanzaia Education Aid (TEA) amesemakuwa Shirika hilo limekuwa likiwasaidia Watoto hususani mabinti wanaotoka katika Mazingira Magumu kwa kuwalipia ada katika Shule za Serikali na Binafsi kabla ya Elimu bure lakini wa shule binafsi bado wanalipiwa.

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma ya Mtoto TZ 704 Wilayani Rorya Justin Lugoye Nyanswede ameiomba Serikali kutoa bure Tauro za Watoto wa Kike Mashuleni ili kutatua Chnagamoto inayowakabili na kushindwa kuudhulia Masomo pale mabadiliko ya Mwili yanapotokea.

Aidha Watoto hao wamesema kuwa kupitia Kauli mbiu ya Mwaka huu kuwa Kuelekea Uchumi wa Viwanda Usimwache Mtoto Nyuma hivyo wameomba Wazazi kuendelea kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo Elimu na kupiga Vita Mimba za Utoto ambazo zinakatisha ndoto zao.
  Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akizungumza  katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.
 Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akipata maaelezo kwa mmoja wa Watoto Mbunifu katika sanaa ya Uchoraji na Uchingaji  katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.
 Afisa elimu Sekondari Wilayani Rorya Gabriel Paul kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Simon Chacha akipata maaelezo kwa baadhi ya Wajasiriamali kuhusua bidhaa zao mbalimbali katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Kwenye Viwanja vya Obwere Mji Mdogo wa Shirati.


Watanzania kumjua Mengi kupitia uzinduzi wake wa kitabu kuhusu maisha yake

$
0
0
KUNA maswali mengi sana yanayoulizwa na watu mbalimbali kuhusu mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Dk. Reginald Mengi, alivyoweza kufikia nafasi aliyonayo kwa sasa akimiliki makampuni kadhaa na mengine kuwa na hisa hapa nchini na ughaibuni.

Majibu ya maswali hayo na maelezo mengine yatapatikana katika kitabu chake cha kumbukumbu kuelekea utajiri ambacho kitazinduliwa Juni 30 mwaka huu. Kitabu hicho chenye taarifa muhimu kwanza za kumfahamu Mengi ni nani kisha safari yake ndefu kufikia ustawi alionao leo akiwa na makampuni yaliyotawanyika nchini na katika nchi za majirani na mataifa tajiri duniani. 

Ndani ya kitabu hiki ambapo wakali wa tafakari kimataifa wameandikia maelezo yao ya kukiafiki kama kitabu bora kinachostahili hata kufundishia. Kitabu hicho ambacho kinaelezea safari ya maisha ya Dk. Mengi kutoka kwenye maisha ya kimaskini mpaka kufikia kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa hapa nchini kitafanyiwa uzinduzi Dar es salaam na kinatarajiwa kuwa mwongozo kwa wasomaji, hususan vijana wanaotaka kuwa wajasiriamali. 

Kitabu hiki ambacho kinaitwa “I Can, I Will, I Must…The Spirit of Success” (Naweza, Nitaweza, Nitafanya na Moyo wa Mafanikio”, na kinaelezea kwa undani mambo aliyoyapitia Dk. Mengi mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata. Mambo ambayo yanaelezewa kwenye kitabu hicho yamekuwa yakichambua kiini cha msongo kwani majaribu, matatizo, changamoto pamoja na maeneo aliyoshindwa lakini hakukata tamaa kutokana na nia madhubuti na malengo ya kutaka kufanikiwa. 

Mpaka hivi sasa kitabu hicho kimeshapongezwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, ambaye amekielezea kuwa ni simulizi ya mafanikio ya hali ya juu na ni cha kwanza cha aina yake barani Afrika. Ameongeza kuwa simulizi ya kitabu hicho imeweza kuelezea kwa ufasaha na kiufundi jinsi mifumo ya kiuchumi na kisiasa iliyokuwa ikibadilika kwa miongo minne iliyopita ilivyoweza kuathiri jitihada za ujasiriamali nchini Tanzania na kuelezea nini kinahitajika katika kutafuta mafanikio. 

Pia kitabu kimepongezwa na wanazuoni wastaafu wa Chuo Kikuu Cha Harvard, Profesa Daniel Isenberg na Profesa Sujata Bhatia. 

Kwa taarifa zaidi kuelekea uzinduzi wa kitabu chake ‘like’ na ‘follow’ akaunti zake za mitandao ya kijamii kupitia twitter @regmengi na instagram @regmengi

MKAPA ATAKA WATAALAM WOTE, TAASISI ZINAZOHUSIKA NA UMEME-JUA KUPANUA WIGO MATUMIZI YA NISHATI HIYO

$
0
0
*Azindua kitabu cha Mafunzo ya umeme wa jua 
*Atashauri kisambazwe kwa wataalam ,mafundi mitambo 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa amewataka watalaam wote na taasisi zinazohusika na nishati ya umeme-jua kuangalia namna ya kupanua wigo wa matumizi ya nishati hiyo ya jua ambayo ipo kwa wingi katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwamo Tanzania. 

Amefafanua katika kiwango cha Gigawatt 400 za umeme jua zinazotumika duniani kwa sasa bado ni Gigawatt moja tu ndio zimefungwa na kutumika katika nchi za Afrika ,Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa namna mbili. 

Mkapa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua Kitabu cha Mafunzo ya Umeme wa Jua ambacho mtunzi na mwandishi wake ni Godwin Msigwa.Kitabu hicho ambacho kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kitasaidia kusambaza taaluma na maarifa katika eneo la nishati ya umeme wa jua nchini. 

Akizungumza kabla ya kuzindua kitabu hicho ambacho ameomba kisambazwe kwa watalaamu wa nishati ya umeme jua na mafundi mitambo wa umeme jua, amesema pamoja na duniani kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme unaotokana na jua bado nchi za Afrika zipo chini kwenye matumizi. 

Mkapa amefafanua kwa mujibu wa taarifa za Mtandao wa jarida la kimataifa la nishati Jadidifu linaloitwa REN 21 ya 2018 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2017 jumla ya zaidi ya Gigawatt 400 za umeme jua zimefungwa duniani kote kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme ambayo sote tunaifahamu kuwa ni nishati muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Aidha amesema ongezeko la uzalishaji wa umeme duniani kote linatokana na uzalishaji kwa kutumia umeme-jua lilifikia Gigawatt 380 katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2017. "Ongezeko hilo ni la kasi sana, jambo ambalo linaashiria kuwa kuna mwelekezo mkubwa duniani wa matumizi ya nishati ya umeme unaozalishwa kwa kutumia nishati ya jua. 
Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akizungumza katika uzinduzi wa Kitabu cha Mafunzo ya Umeme Jua Kilichoandikwa na Godwin Msigwa katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Costech jijini Dar es Salaam.
.Mwenyekiti wa Bodi ya Costech, Profesa Makenya Maboko akitoa shukrani kwa Mgeni Rasmi Benjamin Mkapa.
Rais wa Awamu ya Tatu akitoa kitabu baada ya kukata utepe.
Rais wa Awamu ya Tatu akitoa kitabu baada ya kukata utepe.
Mtunzi wa Kitabu cha Mafunzo ya Umeme Jua, Godwin Msigwa akieleza malengo ya kitabu hicho na hatua alizozipitia, hafla ilifanyika katika ukumbi wa Costech kijiji Dar es Salaam.

Baadhi ya Wadau waliohudhuria hafla hiyo

Introducing "TATIZO NI CHAKULA" by BASSAT

$
0
0
City Music present to you Bassat na wimbo wake mpya unao kwenda kwa la TATIZO NI CHAKULA. Bassat ni kati ya wasanii wanao fanya katika industry ya music Tanzania kwa sasa...

WAMISRI WAOMBA KUWEKEZA KATIKA MIRADI YA UMEME NCHINI

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma

Ujumbe kutoka Kampuni ya ORASCOM ya Misri, wamemtembelea Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani na kuzungumza naye kuhusu nia yao ya kuwekeza katika miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe pamoja na maporomoko ya maji.

Mazungumzo hayo yalifanyika Juni 19, 2018 Makao Makuu ya Wizara, jijini Dodoma na kuwashirikisha pia Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka.

Wakizungumzia uwezo wao katika kutekeleza nia waliyowasilisha, walieleza kuwa wana uzoefu wa miaka mingi katika kazi hiyo na kwamba wanatumia teknolojia ya kisasa. Pia, waliongeza kuwa wanazo fedha za kutosha kuweza kutekeleza miradi husika.

Aidha, waliutaja Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe wa Kiwira wenye megawati 200 pamoja na Ruhudji wenye megawati 358, kuwa ndiyo hasa ambayo wangependa kuwekeza.

Waziri Kalemani aliyapokea mapendekezo ya Kampuni hiyo na kuwataka waendelee kufanya majadiliano na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na TANESCO kuhusu uwekezaji huo, wakati Serikali ikikamilisha utaratibu wa kuitangaza miradi husika.

Hata hivyo, Waziri alieleza bayana kuwa, Kampuni hiyo itatakiwa kushiriki katika ushindani na wawekezaji wengine wenye nia ya kuwekeza katika miradi husika, baada ya miradi hiyo kutangazwa rasmi.

Dkt. Kalemani aliishukuru Kampuni ya ORASCOM kwa kuonesha nia ya kuwekeza Tanzania na aliwahakikishia kuwa Serikali itawapa ushirikiano stahiki.

 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (katikati), akizungumza na Ujumbe kutoka Kampuni ya ORASCOM ya Misri (kulia), waliofika ofisini kwake Dodoma, Juni 19 2018 na kuwasilisha nia ya kuwekeza katika miradi ya kuzalisha umeme nchini. Kushoto ni Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.

 Mmoja wa wawekezaji kutoka Kampuni ya ORASCOM ya Misri, akimkabidhi Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, Kabrasha lenye maombi ya kuwekeza katika miradi ya umeme nchini. Ujumbe kutoka Kampuni hiyo ulimtembelea Waziri ofisini kwake jijini Dodoma, Juni 19, 2018.

 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Kampuni ya ORASCOM ya Misri, waliofika ofisini kwake Dodoma, Juni 19, 2018 na kuwasilisha nia ya kuwekeza katika miradi ya umeme nchini. Wengine pichani ni Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka (wa tatu kutoka kushoto).


Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akiagana na Ujumbe kutoka Kampuni ya ORASCOM ya Misri, waliofika ofisini kwake Dodoma, Juni 19, 2018 na kuwasilisha nia ya kuwekeza katika miradi ya umeme nchini.


MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 20, 2018

Watanzania kumjua Mengi kupitia uzinduzi wake wa kitabu kuhusu maisha yake

$
0
0
KUNA maswali mengi sana yanayoulizwa na watu mbalimbali kuhusu mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Dk. Reginald Mengi, alivyoweza kufikia nafasi aliyonayo kwa sasa akimiliki makampuni kadhaa na mengine kuwa na hisa hapa nchini na ughaibuni.

Majibu ya maswali hayo na maelezo mengine yatapatikana katika kitabu chake cha kumbukumbu kuelekea utajiri ambacho kitazinduliwa Juni 30 mwaka huu.

Kitabu hicho chenye taarifa muhimu kwanza za kumfahamu Mengi ni nani kisha safari yake ndefu kufikia ustawi alionao leo akiwa na makampuni yaliyotawanyika nchini na katika nchi za majirani na mataifa tajiri duniani.

Ndani ya kitabu hiki ambapo wakali wa tafakari kimataifa wameandikia maelezo yao ya kukiafiki kama kitabu bora kinachostahili hata kufundishia.

Kitabu hicho ambacho kinaelezea safari ya maisha ya Dk. Mengi kutoka kwenye maisha ya kimaskini mpaka kufikia kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa hapa nchini kitafanyiwa uzinduzi Dar es salaam na kinatarajiwa kuwa mwongozo kwa wasomaji, hususan vijana wanaotaka kuwa wajasiriamali.

Kitabu hiki ambacho kinaitwa “I Can, I Will, I Must…The Spirit of Success” (Naweza, Nitaweza, Nitafanya na Moyo wa Mafanikio”, na kinaelezea kwa undani mambo aliyoyapitia Dk. Mengi mpaka kufikia mafanikio aliyoyapata.

Mambo ambayo yanaelezewa kwenye kitabu hicho yamekuwa yakichambua kiini cha msongo kwani majaribu, matatizo, changamoto pamoja na maeneo aliyoshindwa lakini hakukata tamaa kutokana na nia madhubuti na malengo ya kutaka kufanikiwa.

Mpaka hivi sasa kitabu hicho kimeshapongezwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, ambaye amekielezea kuwa ni simulizi ya mafanikio ya hali ya juu na ni cha kwanza cha aina yake barani Afrika.

Ameongeza kuwa simulizi ya kitabu hicho imeweza kuelezea kwa ufasaha na kiufundi jinsi mifumo ya kiuchumi na kisiasa iliyokuwa ikibadilika kwa miongo minne iliyopita ilivyoweza kuathiri jitihada za ujasiriamali nchini Tanzania na kuelezea nini kinahitajika katika kutafuta mafanikio.

Pia kitabu kimepongezwa na wanazuoni wastaafu wa Chuo Kikuu Cha Harvard, Profesa Daniel Isenberg na Profesa Sujata Bhatia.


Kwa taarifa zaidi kuelekea uzinduzi wa kitabu chake ‘like’ na ‘follow’ akaunti zake za mitandao ya kijamii kupitia twitter @regmengi na instagram @regmengi

MAFUNZO KWA WAUZAJI, WASAMBAZAJI NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA YA PETROLI KATIKA MIKOA YA DODOMA NA MOROGORO KUHUSU MAOMBI YA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO


Washindi wa Mawakala wa Tigo Pesa kanda kaskazini wapatikana

$
0
0
 Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Tigo kanda ya Kaskazini, Aidan Komba akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Milioni moja kwa mshindi wa Pili, Kanda ya Kaskazini wa Promosheni iliyowahusisha Mawakala mtandao wa Tigo kupitia Tigo Pesa, Justin Mbazi kutoka wilaya ya Same.
 Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi Tigo kanda ya Kaska,zini, Aidan Komba akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh Laki tano kwa mshindi wa tatu. Kanda ya Kaskazini wa Promosheni iliyowahusisha Mawakala mtandao wa Tigo kupitia Tigo Pesa, Vaileth Mkala.
Washindi wa Promosehni ya Mawakala wa Mtandao wa Simu za Mkononi ya Tigo kupitia Tigo Pesa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Tigo mara baada ya kukabidhiwa mifano ya Hundi baada ya kujishindia zawadi za Pesa katika Promosehini hiyo.

WALIMU WASTAAFU KUANZISHA SHULE YA MFANO SONGEA

$
0
0
 Walimu wastaafu katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wanatarajia kuanzisha shule ya Sekondari ya mfano katika manispaa hiyo.

Wakiongea kwenye kikao chao cha Taasisi ya walimu wastaafu Songea (TAWASO) walimu hao walisema kuwa ipo haja ya walimu kuanzisha shule ya mfano ambayo itamwandaa mwanafunzi kujikita katika kujitegemea baada ya kutegemea ajira za serikali.

Mwenyekiti wa Tasisi ya walimu Wastaafu Songea bwana Rashidi Maulidi Ngerangera alibainisha sababu ya kuanzisha shule ambayo itakuwa ya mfano na itawaandaa vijana katika maisha ya kujitegemea baada ya kutegemea ajira serikalini.
 Bwana Ngerangera alidai kuwa walimu hao wamedhamiria kuanzisha sekondari hiyo ambapo itachukua masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na masomo ya ufundi ili kumwezesha kijana amalizapo kidato cha nne aweze kwenda kujitegemea badala ya kusubiri ajira za serikali pekee.

Aidha katibu wa Taasisi hiyo bwana James Kaupunda aliwaambia wanachama wenzake kuwa ili waweze kufanikisha hilo ni lazima michango waliyokubaliana kwa kila mwaka ambayo ni 1,500,000 kwa kila mwanachama aweze kutolewa kwa wakati ili adhima yao ya kujenga sekondari hiyo iweze kukamilika .

Bwana kaupunda aliwasomea gharama ya ujenzi wa darasa lililojengwa na Taasisi hiyo kuwa limegharimu milioni 12 na ili kuweza kukamilisha uwekaji wa milango na madirisha nilazima wachangie kwa wakati na kazi ifanyike kwa wakati.
Hata hivyo kwa mwaka 2017 wanataasisi 9 walifanikiwa kuchangia milioni 1,500,000 kila mmoja na kupata 13,500,000 ambazo ziliweza kujenga darasa moja la Taasisi hiyo ya TAWASO.

Kwa mwaka huu 2018 taasisi hiyo imepanga kujenga darasa la pili kwa kutumia michango yao binafsi na wamejipanga kuanza kuandika maandiko kuweza kuomba wafadhili watakao wasaidia waweze kukamilisha wazo lao la kujenga shule hiyo.

Taasisi ya Wastaafu hao ilianza na walimu 3mwaka 2012 na sasa taasisi hiyo inajumla ya wanachama 9 na wameweza kujenga darasa moja katika eneo la Shule ya Tanga kwa Bubu na kumiliki zaidi ya ekari 100.

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA ABBOTT FUND

$
0
0
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akisalimiana na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini.
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sihaba Nkinga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja  na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson (wa pili kushoto) mara baada ya mazungumzo wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini kushoto ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt Naftali Ng’ondi na kulia ni Meneja Programu wa Abbott Fund Bw. Alfred Magalla. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

DATA ANALYSIS TRAINING

MBUNGE KUBENEA ATOA USHAURI KWA SERIKALI KUBORESHA MRADI WA MABASI YA MWENDO KASI

$
0
0
*Uchache wa mabasi wasababisha mlundikano wa abiria vituoni

Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MBUNGE wa Ubungo jijini Dar es Salaam Saed Kubenea ameishauri Serikali kuifuta kodi kwa mabasi ya mwendokasi 70 yanayotarajiwa kuingia nchini kwa lengo la kurahisisha usafiri katika mradi huo ambao kwa sasa unasua kutokana na kuzidiwa na wingi wa abiria.

Kubenea ametoa ushauri huo leo baada ya kutembelea Kituo cha mabasi ya Mwendokasi cha Kimara Mwisho ili kuangalia changamoto zilizopo katika mradi wa mabasi yaendayo Haraka (Udart).

Akiwa katika kituo hicho Kubenea ameambiwa changamoto kubwa iliyopo ni uhaba wa wa mabasi hayo ukilinganisha na wingi wa abiria wanaotumia usafiri huo.

"Niishauri Serikali ifute kodi ili haya mabasi yaweze kuingia au itoe muda fulani wa kulipa kodi angalau miezi sita hivi huku usafiri ukiendelea kutumika.

"Inawezekana mabasi hayo yanashindwa kuingia kwasababu mhusika amekosa kodi ya kulipa ndio maana yanachelewa na matokeo yake kusababisha adha ya usafiri kwa abiria kurundikana kwenye vituo kutokana na uhaba wa mabasi hayo,"amesema Kubenea.

Kubenea amesema wao kama wabunge wa Dar es Salaam pamoja na madiwani watahakikisha wanaulinda mradi huo ili udumu kwa ajili ya kizazi kijacho.

"Dar es Salaam ni kitovu cha nchi kibiashara, hivyo usafiri unapokuwa wa shida unaathiri mambo mengine. Sisi kama wabunge tunaowajibu wa kuulinda mradi huu na tutahakikisha tunaulinda,".

Ameongeza atazungumza na wabunge pamoja na Waziri wa Tamisemi kujua wanafanyaje kuulinda mradi huo pamoja na kupata eneo kwa ajili ya karakana.

Aidha Kubenea amesema mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo serikalini (GePG) ni mzuri na utasaidia katika kuokoa wanaokwepa kodi na upotevu wa fedha.

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Maofisa wa kitengo cha habari cha mradi wa mabasi yaendayo kasi (UDART) mara baad ya kutembelea mradi wa huo na kujionea mapungufu yaliyojitokeza na kusisitiza kuwa kila mbia ahakikishe changamoto zilizopo zinamalizika haraka.
 Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akimsikiliza mmoja wa Watendaji wa kitengo cha habari katika mradi wa UDART , Joel Beda wakati alipofika  makao makuu ya ofisi hizo Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akiwa ndani ya moja ya mabasi yaendayo kasi mara kuchanganyika na wananchi.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja ya watendaji wa UDART Katika kituo cha Kimara ambapo alikwenda kujionea msongamano wa abiria katika eneo hilo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE

$
0
0
JIOGRAFIA/MAHALI LILIPO SOKO.

Soko la Katengele linapatikana katika vilele vya milima yenye msitu ujulikanao kama Iyondo - Mswima wenye miti ya asili na ile ya kupandwa ukizungukwa na Kata za Kalembo, Sange, Ibaba, Ngulugulu na Kufule.

Pia soko hili hupitiwa na Barabara ya Mkoa ya Ibungu - Ileje hadi KKK Wilayani Rungwe ikiligawa katikati na kuacha upande mmoja kuwa Kata ya Sange na upande mwingine Kata za Kafule na Sange.

HISTORIA YA SOKO:

Soko hili limekuwepo kwa muda mrefu likianzia kabla ya wakoloni, wakati wa ukoloni na baada ya Uhuru wa wetu mnamo 1961 hadi sasa.

Katengele awali palijulikana kama Katengele Bhalindu (yaani mabinti) ikielezwa kuwa ndipo palikutanisha vijana waliotaka kuoa au kuolewa kwa kabila la Wandali ambalo ni kubwa kwa Wilaya hii na maarufu kwa Mkoa wa Songwe na Mbeya kutokana na uchapaji kazi hususani zile za kutumia nguvu.

Kuhusu “Katengele Bhalindu” (yaani mabinti) hapa ndipo palipokuwa soko la awali pakiwa na msitu mdogo ambapo inasemekana kuwa mabinti wawili walipotea bila kupatikana katika mazingira ya kutatanisha kwa muda mrefu na imebaki kuwa simulizi inayoendelea kila linapotajwa neno katengele.

Awali lilikutanisha watu wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ileje na Wilaya za Mbozi, Rungwe na Kyela wakiuza bidhaa kwa fedha tasilimu pamoja na biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa. 

Kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa maarufu sana kwa biashara ya ng’ombe, bidhaa za asili pamoja na zile za viwandani likiwavutia hata raia wa Nchi jirani ya Malawi.

KUANZISHWA KWA MRADI WA SHAMBA LA MITI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Misitu (TFS) imeamua kuanzisha Shamba la Miti la Iyondo - Mswima ukiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2015/2020 ibara ya 31 vifungu vya b,c,d,e na f kuhusiana sekta ya Maliasili.

Kwa mujibu wa Meneja wa Mradi wa Iyondo – Mswima Ndg. Deograsian Kavishe upandaji miti utaanza rasmi katika mwaka wa Fedha 2018/2019 ikiwa baadhi ya kazi zilianza kutekelezwa na Mradi katika mwaka wa fedha 2017/2018.

Kuanzishwa kwa shamba hili la Katengele kunaifanya Tanzania kuwa na mashamba ya miti ya kupandwa 23 yakiwa yanapatikana katika Kanda mbalimbali kati ya hayo manne yapo katika hatua ya uanzishwaji likiwemo hilo la Iyondo – Mswima (Ileje).

Eneo la Mnada wa Katengele Wilayani Ileje mkoani Songwe unaotakiwa kuhamishwa ili kupisha Mradi wa Upandaji Miti.
Askari Jeshi USU (ambalo ni jina geni kwa wengi ) Deograsian Kavishe Meneja Mradiwa Upandaji Miti wa Iyondo-Mswima akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mhe.Ubatizo Songa akiongoza Wahe. Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje walipotembelea eneo la Mradiwa Upandaji Miti la Iyondo-Mswima.
Kitalu cha miti kilichopo Katengele-Ileje kikitarajiwa kubadilisha sura ya msitu wa Iyondo-Mswima wiyani Ileje
Eneo la Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala panapotarajiwa kuhamishiwa Mnada wa Katengele.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ndugu Haji Mnasi (aliyesimama) akizungumza kwenye Baraza Maalum kuhusu Mnada wa Katengele.

BENKI YA CRDB YAIPIGA TAFU VIFAA VYA MICHEZO TIMU YA MAGEREZA DAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akikabidhi jezi kwa Afisa Mipango wa Magereza Dar FC, Insp. William Mkamba (wa pili kushoto) ikiwa ni sehemu ya udhamiwa wa Benki hiyo kwa timu ya Magereza Dar FC. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu pamoja na Koplo Jaffar kutoka Mageteza.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu akizungumza jambo na Afisa Mipango wa Magereza Dar FC, Insp. William Mkamba pamoja na Koplo Jaffar kutoka Mageteza, baada ya kuwakabidhi jezi ya timu ya timu ya Magereza Dar FC.

'KUNA ONGEZEKO KUBWA LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA'

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

SERIKALI imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni hali inayotishia afya ya mama na mtoto wakati wa kijifungua pindi wanapofika hospitalini.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maedeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk . Sara Maongezi wakati akifungua Programu ya AstraZeneca ya Healthy Heart Africa (HHA).
 Programu hiyo inatokana na ushirikiano wa Touch Foundation na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Lengo ni  kupunguza maradhi ya shinikizo la damu wakati wa mimba.Maongezi amefafanua ubia uliozinduliwa leo katika mradi huo utakaoongeza utekelezaji wa programu hiyo nchini Tanzania.  
"Ubia huo unakusudia kwa kiasi kikubwa kupunguza kuenea kwa maradhi ya shinikizo la damu, hasa miongoni mwa wanawake wajawazito ikiwa ni kuunga mkono mpango mkakati wa Serikali wa kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza,"amesema Dk. Maongezi.

  Ameongeza kupanda kwa shinikizo la damu ni moja ya vihatarishi vikubwa vya ugonjwa wa moyo hali ambayo msukumo wa damu katika moyo  huzuizwa au kukatizwa na chembe chembe za mafuta kwenye mishipa ya koronari  na mwishowe huenda ikasababisha kiharusi.Amefafanua kwa bahati mbaya, ugonjwa wa moyo ni moja ya vyanzo vikubwa vya kifo nchini Tanzania hasa kwa wajawazito wakati wa kujifungua.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya DK. Sara Maongezi akizungumza kwa niaba ya serikali wakati wa mkutano wa wadau wa Afya uliozungumzia mstakabali wa sekta hiyo katika bara la Afrika.
Mkuu wa Masuala ya Madawa kutoka Tasisi ya Touch Afrika ,Steve Justus akizungumza wakati kujibu maswali kwa wadau na Waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Tasisi ya Healthy Heart Afrika (HHA),Ashling Mulvaney akizungumza wakati w aufunguzi wa Mradi wa kupunguza shinikizo la damu wakati wa ujauzito.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Rashid Said Mfaume akizungumza wakati kuchangia uzoefu wake kwa mradi huo katika mkoa anaotoka.

UNFPA ITAENDELEA KUTOA MASHIRIKIANO KUENDELEZA UZAZI SALAMA ZANZIBAR

$
0
0

Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar 

Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa linaloshuhulikia Idadi ya watu Duniani UNFPA Jaqline Mohan amesema Shirika lake litaendelea kutoa mashirikiano katika sekta ya afya hasa katika uzazi salama ili kuweza kuyanusuru maisha ya mama na mtoto.

Hayo ameyasema huko katika ofisi ya Wizara ya Afya Mnazi Mmoja wakati alipokuwa akielezea lengo la matarajio yao katika kusaidia mpango wa uzazi salama wa mama na mtoto.

Alisema afya na mama na mtoto ni muhimu katika jamii hivyo wataendelea kusaidia sekta hiyo ya afya ili kuhakikisha kuwa kinamama wanapata huduma bora wakati wa kujifungua pamoja na watoto kupata makuzi yaliyo salama ili kupunguza vifo wakati wa uzazi.

Alisema vifo vingi vya akinamama na watoto hutokea wakati wa kujifungua hivyo huduma hiyo itaweza kupunguza vifo na kusaidia kuwapa uzazi salama kwa kujenga afya bora na makuzi mazuri wa watoto.

“Tuna mpango wa kusaidia Wizara ya Afya katika mambo ya kijamii , uzazi salama kwa mama na mtoto na kushuhulikia vijana katika kujua afya zao” alisema mwakilishi huyo.
   MWAKILISHI wa UNFPA Tanzania Jacguline Mahon akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kuhusu kuongeza ushirikiano juu ya uzazi salama na kuimarisha afya ya Mama na Mtoto, (kulia kwake)  ni Mwakilishi wa (UNICEF) Maniza Zaman 
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed katika akipiga picha ya pamoja na Wawakilisi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania, (kushoto) Mania Zaman wa UNICEF na  Jacguline Mahon wa UNFPA (Picha na Abdalla Omar  Maelezo - Zanzibar).

KATIBU MKUU SIHABA NKINGA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA ABBOTT FUND

$
0
0
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi. Sihaba Nkinga (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Abbott Fund kutoka Marekani Bw. Andy Wilson (wa pili kushoto) mara baada ya mazungumzo wakati Makamu wa Rais wa Mfuko huo alipomtembelea leo Ofisi kwake Jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yahusuyo utoaji wa huduma kwa watoto waishio katika mazingira magumu nchini kushoto ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt Naftali Ng’ondi na kulia ni Meneja Programu wa Abbott Fund Bw. Alfred Magalla.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YAKUTANA NA WABUNGE KUTOKA GAUTENG AFRIKA YA KUSINI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Mussa Zungu (katikati) akizungumza na Waheshimiwa Wabunge (hawapo kwenye picha) kutoka Jimbo la Gauteng lililopo Afika kusini ambao ni Wajumbe wa kamati ya Usalama wa Jamii walipowatembelea leo katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. 
 Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (kulia) wakizungumza na Wajumbe wa kamati ya Usalama wa Jamii ambao ni Waheshimiwa Wabunge kutoka Jimbo la Gauteng lililopo Afika kusini walipokutana leo katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
 Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Usalama wa Jamii ambao ni Waheshimiwa Wabunge kutoka Jimbo la Gauteng lililopo Afika kusini walipokutana leo katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Mbunge wa IIala  Mhe. Mussa Zungu (kulia) akisalimiana na Kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Jimbo la Gauteng lililopo Afika kusini ambao ni Wajumbe wa kamati ya Usalama wa Jamii, Mhe.  Sochayile Khanyile

 (PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NCHINI WATAKIWA KUFUATA SHERIA , KANUNI

$
0
0
Na Emmauel Masaka, Globu ya jamii

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini na wanachama kutekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa kufuata na kuzingatia Sheria na kanuni za vyama vya Siasa.

Taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Jaji Mutungi amesema lazima sheria za nchi kwa ujumla zifuatwe na vyama vyote vya siasa.

Amefafanua kumeibuka tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia vibaya vyombo vya habari, hususani mitandao ya kijamii kufanya vitendo au kutoa kauli ambazo zinavunja sheria za nchi.

Hivyo ametoa mwito kwa wenye tabia hiyo kuacha tabia hiyo mara moja. "Ninasisitiza kuwa viongozi wa Vyama vya Siasa wasitumie vibaya dhana ya demokrasia na uhuru wa habari."Amesema ieleweke kwamba mtu yeyote anapokiuka sheria za nchi, sheria itachukua mkondo wake bila kujali wadhifa wa mhusika katika chama cha siasa.

Amesisitiza rai yake kwa viongozi wote wa vyama vya siasa na wanachama wote wa vyama vya siasa nchini, ni wajibu wa kila mmoja wao kuelewa katika kutekeleza majukumu yao ya kisiasa wanapaswa kuheshimu sheria za nchi wakati wote ili kudumisha na kukuza demokrasia ya vyama vingi nchini. 

"Kwa kufanya hivyo pia, Viongozi hawa watalinda na kuimarisha Amani ya nchi yetu,"amesema Jaji Mutungi.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images