Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA ZIARA YA WAZIRI MAHIGA NCHINI NORWAY

$
0
0
  
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeihakikishia Serikali ya Norway kuwa inaendelea kuelekeza nguvu zake kwenye kuweka mikakati sahihi ya kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi, ikiwemo nchi ya Norway, ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Hayo yamesemwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania alipokutana na Bw. Jon Lamoy, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Norway lijulikanalo kwa kifupi kama NORAD mwanzoni mwa ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mjini Oslo, makao makuu ya Norway.

Katika mazungumzo yao, Mkurugenzi Lamoy alimueleza Waziri Mahiga kuwa shirika hilo limekuwa na uhusiano wa karibu na wa kindugu kwa zaidi ya miongo mitano na nchi ya Tanzania. Yeye binafsi na washirika wengi wa Tanzania nchini humo wanasifu utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli hususan kwenye mapambano dhidi ya rushwa. 

Rushwa inarudisha nyuma maendeleo kwa kuikosesha nchi mapato, hivyo jitihada za Tanzania za kupambana na rushwa, hususan kwenye ukusanyaji kodi, zitawawezesha wananchi wa Tanzania kunufaika na huduma za kijamii na hatimaye kupata maendeleo kwa haraka.

Hata hivyo mkurugenzi huyo alitoa angalizo kuwa nia nzuri ya Serikali ya Tanzania ya kuweka mifumo thabiti ya uwekezaji wenye faida  ukiwemo ule wa sekta ya madini, ni muhimu ikakamilika mapema ili kutoa fursa kwa wawekezaji wapya kuwekeza kwenye sekta hiyo kwa wakati.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Mahiga alielezea kuwa suala hilo tayari linafanyiwa kazi ambapo pamoja na Serikali kuweka mazingira rafiki  kwa wawekezaji, uwekezaji huo ni lazima uwe na faida kwa Watanzania na kwa maendeleo ya nchi.


WANAWAKE WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAUME ZAO KATIKA KUJILETEA MAENDELEO NA TAIFA KWA UJUMLA.

$
0
0
Na Frankius Cleophace Tarime

Wanawake wametakiwa kujenga Umoja na Ushirikiano na Waume zao pamoja nakuwa waaminifu katika kutunza mali zao ikiwemo fedha ili kujiinua na kuongeza Uchumi wa Nchi kwa Ujumla.

Hayo yamebainishwa na Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mara Conference George Ezekiel katika Uzinduzi wa Nyumba ya Kulala wageni iliyojengwa na Kampuni ya SOJEMA Mjini Tarime Mkoani Mara.

Askofu huyo amesema kuwa Wanawake wengi siyo waaminifu katika suala zima la fedha jambo ambalo linapelekea waume zao kushindwa kuwaamini na kuwapa Miradi Mikubwa ili waweze kusimamia hivyo amezidi kusisitiza suala la Uaminifu kwa waume zao ili waweze kupewa Mitata na kusimamia Miradi yao kwa lengo la kujikomboa Kiuchumi.

Askofu ameshukuru Kampuni ya SOJEMA kwa kushirikisha Viongozi wa Dini na Serikali katika ufunguzi wa Nyumba ya Kulala Wagenzi iliyopo Mtaa wa Mwangaza Mjini Tarime huku akisihi jamii kuiga Mfano huo wa kufanyia Maombezi Nyumba zao za biashara ili Mwenyezi Mungu azidi kuzibariki na kuepuka Majaribu.

“Wengi waliobarikiwa na Mwenyezi Mungu wamekuwa wakijenga Nyumba zaao ata za kuishi lakini hawashirikishi Mwenyezi Mungu hivyo sasa huu ni mfano mzuri wa Kuigwa” alisema Askofu.

Eziekieli amezungumzia Pia suala la Jamii kuendelea Kutumikia Mwenyezi Mungu na siyo kukumbatia Mila potofu ambzo zinanyima Mwanamke uhuru katika Jamii inayomzunguka likiwemo suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.

Angela Godfrey kutoka kampuni ya SOJEMA anazidi kusisitiza suala la Mwanamke kudhubutu na kudai kuwa wanawake wanaweza hivyo sasa wanaume waweze kuwapa Mitaji na kuwaamini ili kuendesha Biashara zao

“Mimi nimeweza kushirikiana vyema katika Ujenzi wa Nyumba hii ya kulala wageni na mme wangu ameniamini nimekuja kuifungua hayupo yote ni kwa sababu ya uaminifu” alisema Angela.

Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mara Conference George Ezikiel Ojwang akikata Utepe kama ishara ya uzinduzi rasmi Nyumba ya Kulala wageni iliyojengwa na Kampuni ya SOJEMA Katika Mtaa wa Mwangaza Mjini Tarime Mkoani Mara.
 Sehemu ya jengo hilo kama lionekanavyo nje
Baadhi ya Wageni mbalimbali walioshiriki kwenye hafla hiyo 

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA SWEDEN NCHINI ANAYEMALIZA MUDA WAKE

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzana Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt ambaye amemaliza muda wake wa kazi .Balozi Katarina Rangnitt alifika ofisi kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga rasmi Makamu wa Rais. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt ambaye amemaliza muda wake wa kazi .Balozi Katarina Rangnitt alifika ofisi kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga rasmi Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kumuaga baada ya muda wake wa kazi nchini kumalizika. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt ambaye amemaliza muda wake wa kazi .Balozi Katarina Rangnitt alifika ofisi kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumuaga rasmi Makamu wa Rais 

ZFDA YAKAMATA BIDHA MBALIMBALI ZISIZOFAA KWA MATUMIZI YA BINADAMU

$
0
0
Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Wakala wa Chakula na Dawa  Zanzibar (ZFDA) imezuia kusambazwa bidhaa za chakula na vipodozi zilizoingizwa nchini kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na siku kuu ya Idd el Fitri kinyume na taratibu na zilizokuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Burhan Othman Simai alisema bidhaa hizo zilikamatwa kufuatia operesheni maalumu waliyoifanya katika kipindi cha miezi miwili kwenye maghala ya wafanyabiashara na baadhi ziligundulika zimetupwa katika jaa la Kibele na eneo la Migombani.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mombasa Dkt. Burhani alizitaja bidhaa zilizokamatwa na zilizotupwa kuwa ni mchele tani 40, unga wa sembe tani 75,  sukari tani 25 na lita 15,000 za mafuta ya kula.

Alisema dawa na vipodozi vilivyokamatwa ni vichupa 4000 vya chanjo aina ya ATS kutoka China zilizoingizwa nchini kinyume na miongozo ya uingizaji na utoaji wa dawa nchini, na tani tisa za vipodozi vyenye viambata vya sumu kali inayosababisha saratani ya ngozi.

Dkt. Burhan alieleza masikitiko yako kwa baadhi ya wafanyabiashara kutoa sadaka bidhaa hizo bila kuangalia athari inayoweza kuwapata wananchi wenzao baada ya kuzitumia.
MKURUGENZI Mtendaji Bodi ya Chakula na Dawa Zanzibar, Dkt. Burhan Othman Simai (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi la Kukamata bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya Binaadamu miezi miwili iliyopita. 
 Mkuu wa Ukaguzi wa Chakula Mohammed Shadhil (kushoto) na Muangalizi wa Ofisi Mussa Bakar Othman wakionesha  vipodozi vyenye chemicali za sumu zilizoingizwa kwa ajili ya siku kuu
Aina za Bidhaa za Mchele, Unga wa Ngano,Mafuta ya Kula na vipodozi zilizokamatwa na ZFDA ambazo  hazifai kwa  matumizi ya Binaadamu.
Picha na Abdalla omar Maelezo – Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JAJI WA MAHAKAMA KUU YA NCHINI UGANDA ATEMBELEA JENGO JIPYA LA KISASA LA MAHAKAMA YA MWANZO NA MAHAKAMA YA WILAYA –KIGAMBONI

$
0
0
 Jaji wa Mahakama Kuu ya Uganda, Mhe. Paul Gadenya akitia saini kitabu cha wageni pindi alipowasili katika Mahakama ya Wilaya Kigamboni kujionea jengo hilo la kisasa lililojengwa kwa teknolojia ya ujenzi ya Moladi, mbali na kutembelea jengo hilo Jaji Gadenya ametembelea Ofisi za Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ‘JDU’ kupata taarifa ya maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama kwa lengo la kuboresha huduma za utoaji haki nchini, aliyesimama kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo, akimpitisha Mhe. Jaji Gadenya kukagua sehemu mbalimbali za jengo hilo la kisasa, aliyepo nyuma ya Mhe. Gadenya ni Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Tathmini, Mahakama, Bw. Sebastian Lacha. 
 Mhe. Jaji Gadenya (kushoto) akijadili jambo na wenzake, kulia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Sundi Fimbo na katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Tathmini, Mahakama, Bw. Sebastian Lacha.
Picha ya pamoja nje ya jengo jipya la kisasa la Mahakama ya Mwanzo na Mahakama ya Wilaya Kigamboni, Mhe. Gadenya ameisifu Mahakama kwa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika na ambayo tayari ameshafanyika kwa ustawi wa Wananchi.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)


WASAFI TV RASMI NDANI STARTIMES

$
0
0
 KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imetangaza rasmi uwepo masafa ya Wasafi TV katika king'amuzi cha Startimes kupitia king’amuzi chake, uzinduzi huo umefanyika leo June 19 katika Hotel ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa ameeleza kuwa  chaneli hiyo mpya ya burudani itaweza kutazamwa na watu wengi zaidi Tanzania kwa sababu StarTimes ndicho king’amuzi chenye watumiaji wengi zaidi nchini.

Malisa  ameeleza kuwa kuanzia sasa Wasafi TV itapatikana pia katika ving’amuzi vyao vya Antenna, hivyo watumiaji wa Antenna wanaweza kutazama chaneli hiyo mpya ikiwa na vipindi vipya ambavyo vitatangazwa baadaye. Pia wateja wanaweza kulipia kifurushi chochote cha Antenna na kuipata Wasafi TV na malipo hayo yanafanywa unaweza kulipia NYOTA kwa 7000 tu mwezi mzima, MAMBO Tsh 13,000 tu kwa mwezi na UHURU kwa 24,000 tu. 

imeelezwa kuwa Wasafi TV imekuja na lengo kubwa la kuwainua vijana tofauti na ambavyo watu wengi wanafikiria. Ndoto kubwa walizonazo vijana huko mtaani sasa wanaelekea kuzitimiza. Pia Wasafi TV kitakuwa chombo cha kukuza sanaa nchini, kwa sababu wasanii wanajuana  na wana uwezo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.

Mbali na kutazama chaneli ya Wasafi TV wateja wa StarTimes wanaweza kuendelea kutazama mechi zote za Kombe la Dunia katika kiwango safi kabisa cha picha, HD t kwa lugha ya Kiswahili. 

Naye msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul ambaye ni mmiliki wa Wasafi Tv amefurahi kuingia makubaliano na Startimes na kwa sasa chaneli ya Wasafi itaonekana kupitia chaneli 444.

Aidha ameeleza kuwa kupitia chaneli hiyo watazamaji wajiandae kupata burudani na waendelee kutoa ushirikiano katika kukuza na kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia sanaa.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wasafi TV kuunganishwa kwenye king’amuzi  cha Startimes katika ukumbi wa Hotel ya Slipway jijini Dar es  Salaam.
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' (kushoto) akisaini mpira wa Startimes Tanzania bara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa Wasafi TV kwenye king'amuzi cha Startimes. Katikati ni Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Maudhui ya Startimes, Zamarad Nzowa.

Article 4

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI ya Rasilimali Tanzania TIB Corporate imewataka wateja wake kutoa maoni yao juu ya huduma wanazopatiwa katika benki hizo ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma.

TIB wamewataka wateja wa benki hiyo kuelezea changamoto wanazokutana pindi wanapokuja kupata huduma ili waweze kuzifanyia kazi.

Akizungumza na wateja wa benki ya TIB Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa TIB Corporate Bank , Frank Nyabundege amesema kuwa wiki hii ya utumiashi wa umma wataitumia kwa ajili kupokea maoni ya wateja wao kuhusiana na huduma wanazozipata.

Nyabundege amesema kuwa wiki hii ni muhimu sana kwa uongozi wa TIB kufahamu na kupata maoni kutoka kwa wateja wao ambapo itawasaidia kuzitatua na kuona wapi walikosea ili kuweza kufanyia marekebisho.
Wakielezea huduma wanazozipata katika benki ya TIB Denis Kabogo kutoka Mbeya amesema kuwa benkk hiyo ina huduma nzuri ila anawaomba waongeze matawi sehemu mbalimbali za nchini ikiwemo mkoa wao wa Mbeya, Naye Mteja wa muda mrefu na Mbunge Ahmed Salum amesema kuwa anafurahia sana huduma za benki ya TIB na amewataka waongeze ufanisi hususani katika kutumia huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu kwani ni njia rahisi sana pale unapokua na hela nyingi inakua rahisi kuziamishia kwenye akaunti moja kwa moja.

Wiki ya maadhimisho ya utumishi wa umma imeanza Juni 19 hadi Juni 22 nchini ambapo mashirika na taasisi mbalimbali nchini zimekuwa zikiadhimisha kwa kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wateja wao.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Rasilimali Tanzania TIB Corporate Frank Nyabundege akizungumza na wateja wa benki hiyo katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma na kuwataka kusema changamoto zao ili waweze kuzifanyia kazi.
Mteja na mbunge Ahmed Salum akizungumza mbele ya uongozi wa Benki ya Rasilimali Tanzania TIB Corporate leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Matawi na Masoko Benki ya Rasilimali Tanzania TIB Corporate Theresia Soka akizungumza na wateja katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya Rasilimali Tanznaia TIB Corporate.
Wateja wa Benki ya Rasilimali Tanznaia TIB Corporate.

VYUO VIKUU VYATAKIWA KUJIKITA KATIKA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
Vyuo Vikuu nchini vimetakiwa kuhakikisha vinafundisha kozi zitakazozalisha wataalamu wengi  watakaoendana na Sera ya Serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.

Rai hiyo imetolewa leo  na Mkuu wa Chuo kinachotoa mafunzo ya Tehama cha Power Computer LTD (PCTL), Avelin Malamsha, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kozi mpya wanaotarajia kuitoa yenye lengo la kuwajenga vijana kiajiliwa katika hadhi ya kimataifa na viwanda.

Amesema, wadau wa sekta ya elimu wanapaswa kujitafakari kwa kuanzisha kozi zitakazozalisha wataalamu katika sekta ya viwanda na uwekezaji nchini kwani elimu ni jambo kubwa kwa sasa na linashika kasi nchini ambayo tunategemea itazalisha wasomi wengi watakaokuja kusaidia nchi.

Malamsha ameongeza kuwa, ili kuendana na Sera hiyo ya Tanzania ya viwanda na upatikanaji wa ajira chuo hicho cha PCTL kimeanzisha kozi mpya ya kimataifa ya Tehama (ICDL) itakayowajengea uwezo vijana kidigitali na kuajiria sehemu yoyote duniani.

Amesema, Tanzania ya viwanda na ajira itakuwepo pale ambapo kila mmoja akielewa mchango wake katika hili, pia itakuwepo kama tutakuwa na rasilimali watu wa kutosha na sahihi, “PCTL kama chuo tukaona kwamba tuna wajibu kuijenga Tanzania ya hiyo viwanda na kupunguza tatizo la ajira kupitia kozi yetu mpya ya ICDL," alisema.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa linalotoa Cheti cha kozi hiyo ya ICDL, Edwin Masanta alisema baada ya kuona mapungufu yaliyopo nchini wameona ni vema kuileta kozi hiyo.

"ICDL inaongeza nafasi ya ajira kwa vijana kwani inatoa wataalamu wengi katika masuala ya komputa kwenye vigezo vya kuajiliwa popote duniani," alisema.
Mkuu wa Chuo cha mafunzo cha PCTL, Avelin Malamsha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu program za kompyuta zinavyoweza kusaidia Tanzania kuimarika na kukua katika viwanda na kuongeza ajira kwa vijana. Kulia ni mkuu wa Itifaki kwa wanafunzi, Daniel Ngumbuke na Mkurugenzi wa PCTL nchini, Edwin Masanta.

SANGA APIGA MARUFUKU MALORI KUPITA KATIKA MIUNDOMBINU INAYOTENGENEZWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.
MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amemshukuru Rais na viongozi wote ambao wanashiriki katika ujenzi wa taifa.

Pia amehaidi kutoa ushirikiano wakandarasi ili waweze kutekeleza miradi na amezuia malori kupita katika kijiji cha Kitoga kwa muda wa miezi miwili hadi ujenzi wa daraja hilo utakapokamilika. 

Akizungumza leo Sanga pia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Julai 12 kuupokea Mwenge wa uhuru ambao utafungua miradi mingi ya kimaendeleo.

Kwa upande wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika ziara yake katika jimbo la Mkuranga ameendelea kukagua ujenzi wa barabara katika kata za Tambani, Mipeko, Mkuranga, Kimanzichana, Mkamba na kata ya Kisegese.

Ulega ameeleza kuwa ziara hiyo imelenga kukagua ukarabati wa barabara mara baada ya mvua kunyesha, na amesema kuwa wamekagua katika kata mbalimbali na wameridhishwa na utendaji kazi unaofanywa na wakandarasi katika kutekeleza mradi huo kwani fedha iliyotolewa na kinachofanyika vinawiana.

Aidha Ulega amemshukuru Rais Magufuli kwa kuangalia mahitaji ya wananchi na kuyafanyia kazi na kuahidi kuwa kama wasaidizi wake watamuunga mkono katika kulipeleka taifa katika hali nzuri ya uchumi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote muhimu.

Amewataka wananchi kutunza miundombinu hiyo ili kuwarahisishia shughuli mbalimbali na kuweza kudumu kwa matumizi ya kizazi kijacho.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega akishiriki unjenzi wa daraja katika kijiji cha Mipeko katika ziara ya kukangua mirandi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akishiliki ujenzi wa daraja katika kijiji cha Mipeko katika ziara ya kukangua mirandi mbalimbali iliyo fanyika leo mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi Abu na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mihekela alipo tembelea na kukangua barabara ya kijiji hicho na kumuomba meneja TARURA kujenga barabara hiyo Kwa kiwango ubora na na kuhakiksha sehemu korofi zinaimarika.

Ufuta wa wafanyabiashara uliokamatwa Kibiti kuuzwa kwa mnada

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Ufuta uliokamatwa Halmashauri ya Kibiti kutokana na kukosa nyaraka ya mnada kutoka Halmashauri ya Rufiji unapigwa mnada ikiwa ni agizo la serikali ya kutaka mazao ya Kahawa, Pamba na Ufuta kuuzwa kwa stakabadhi ghalani.

Uamuzi huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Gulam Hussein Kifu wakati wa kikao cha pamoja kati ya Halmashauri ya Kibiti na Rufiji wakiongozwa na wataalam Kutoka Wizara Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kifu alisema maamuzi ya kikao kuhusiana na ufuta uliokamatwa hauwezi kutenguliwa na mtu yeyote kutokana na Agizo la Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa kutaka mazao ya ufuta, Kahawa na pamba kwa mfumo wa Sitakabadhi Ghalani ili kuweza kumuinua Mkulima.

Amesema kuwa wafanyabiashara wanatakiwa kufuata utekelezaji wa maamuzi yanayotokana na serikali hivyo ufuta uliokamatwa upigwe mnada.

Kifu amesema kuwa hakuna mtu mwenye matatizo na wafanyabiashara isipokuwa ni kuwataka wafanyabiashara hao kufuata utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni.

Mkuu wa Wilaya hiyo amesema kuwa baada ya ufuta kuuzwa kwa njia ya mnada watarudishiwa fedha zao walizonunulia ufuta kutokana na kilo zitakazouzwa.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo amesema kuwa maamuzi yaliyotolewa ni kutekeleza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa mnada.

Hivi karibuni Mkurugenzi  Mtendaji wa  Halmashauri ya Kibiti, Alvera Ngabagoye aliwaambia waandishi wa habari  kuhusiana ufuta kukamatwa katika wilaya ya kibiti ikiwa ni kutekeleza agizo la serikali la kuuza katika mfumo wa stakabadhi ghalani  kwa kuhusisha mnada.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibiti , Gulam Hussein Kifu akizungumza katika kikao cha pamoja kuhusiana na Ufuta uliokamatwa katika Wilaya ya Kibiti ukitokea Wilaya ya Rufiji na kumualiwa kuuzwa kwa njia ya mnada  
 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji , Juma Njwayo akizungumza juu ya utekelaji wa agizo la kuuza ufuta kutoka kwa wakulima kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania wa Wizara ya Fedha na Mipango, Godfrey Malekano akizungumza kuhusiana na maamzu ya kikao kuhusiana na Ufuta.
Sehemu ya watendaji , wafanyabiashara pamoja na madiwani wa wilaya ya Rufiji waliokuwepo katika mkutano uliofanyika Kibiti.

ANZISHENI KAMPENI ZA KUHAMASISHA UPIMAJI WA VVU-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa yote nchini washirikiane na wadau wa mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kuanzisha kampeni ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema.

Kadhalika, amewaagiza Wakuu hao wa Mikoa na Wilaya kwa kusaidiana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wasimamie kwa uzito unaostahili kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa muda wa miezi sita mfululizo.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumanne, Juni 19, 2018) wakati akizindua kampeni ya Kitaifa ya kuhamasisha wananchi hususani wanaume kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema, iliyofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri, jijini Dodoma.

“Kwa vile tunazindua kampeni ya kupima na kuanza ARV mara moja (Test and Treat) natoa rai kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI, mhakikishe vitendanishi na dawa za ARV zipo za kutosheleza katika kila kituo kinachotoa huduma katika kila Mkoa na Wilaya,” amesema. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahamasisha watu wote watakaogundulika na maambukizo ya VVU waelewe kuwa utaratibu wa sasa ni kuanza dawa mara moja pasipo kujali kiwango cha kinga mwilini, yaani CD4.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea tuzo ya kutambua kukubali kuwa Balozi wa kuhamasisha wanaume kupima VVU nchini, kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Flora Kamwela, wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU  na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihamasisha upimaji wa Virusi vya  Ukimwi hususani kwa wanaume, wakati alipozindua Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kulia ni Sajenti Deogratius Peter. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipewa maelezo na kapteni Geofrey Mwajombe katika Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, katikati ni Sajenti Deogratius Peter.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo, akihamasisha pimaji wa VVU hususan kwa wanaume, wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Kuhamasisha Upimaji wa VVU na kuanza dawa mapema, kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 19, 2018, kulia ni Sajenti Deogratius Peter. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HUKUMU KESI YA WEMA SEPETU MATUMIZI DAWA ZA KULEVYA KUTOLEWA JULAI 16

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 16 mwaka 2018 inatarajia kusoma hukumu ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii maaruifu wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Sepetu na wafanyakazi wake wawili.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa upande wa utetezi, Albert Msando kuwasilisha hoja za majumuisho katika kesi hiyo za kushawishi Mahakama iwaone wateja wake hawana hatia.

Wakati Wakili wa upande wa mashtaka Costantine Kakula akiwasilisha hoja za majumuisho ili Mahakama iwaone washtakiwa wana hatia.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wema na wafanyakazi wake kumaliza kujitetea na upande huo wa utetezi kufunga kesi yao.

Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.

Akijitetea katika kesi hiyo, Wema alikubali kuwa nyumbani kwake palikutwa na msokoto unaodhaniwa kuwa ni bangi jikoni na katika chumba cha kuhifadhia nguo zake.Pia walikuta kiberiti katika chumba wanacholala wanamuziki hao wawili Jodarn na Mila.

Akiongozwa na Wakili Msando alidai Februari 3 mwaka 2017 alitakiwa kuripoti polisi kwa tamko la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Ambapo akiwa na watu wengine, walifika pale saa tano asubuhi na kusubiri hadi saa 10 jioni, ambapo Makonda alifika na kuwaita mmoja mmoja katika chumba ambacho alikuwepo na Afande Sirro" Ameeleza Wema.
Amedai moja kati ya maswali waliyomuuliza ni kama alikuwa akitumia au kuuza dawa za kulevya lakini aliwajibu hapana.

Aliendelea kudai kuwa baada ya mahojiano hayo walipelekwa mahabusu ambapo walikaa kwa siku saba na kati ya siku hizo, Februari 5 mwaka 2017 Jumapili polisi, akiwamo afande Mery,OCID Denis, Hassani walimpeleka kwake kufanya upekuzi.

Alidai hajui hizo bangi ni za nani ingawa polisi walizikuta nyumbani kwake, kwa sababu yeye kwa asili ya kazi yake ya usanii nyumbani kwake wanaingia watu tofauti tofauti pia huwa anafanya pati mara kwa mara na kualika marafiki zake.

“Nyumba yangu inaingia watu wengi tofauti tofauti, siwezi kujua hivyo, vitu viliingizwa na kina nani maana kila anayefika kwangu anauhuru wa kuingia katika chumba chochote kasoro chumbani kwangu tu,”ameeleza Wema

Ameongeza kuwa, muda wote walipokuwa njiani kwenda kwa kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake hawakuzungumza chochote na afande Mery.

Bali baada ya kurudishwa kituoni alichukuliwa sampuli ya mkojo pale pale Polisi na kwamba alimkabidhi afande Mery.

Wakijitetea wafanyakazi wa Wema, Angelinana Matrida wao walieleza kuwa wakati askari walipoenda kufanza upekuzi kwa Wema wao walikuwa wamekaa nje.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februar 4 mwaka 2017 huko Kunduchi Ununio washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februari Mosi mwaka 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Bangi.

Only 18 Days To Go For The Biggest Concert In Chicago By Diamond Platnumz

$
0
0
Yeeeeeesssss....!!!
July 6th At Alhambra palace 1240 W Randolph..
The Question Is!!...Have you Purchased your Ticket??
If Not Then Hurry Up And Purchase Your Tickets Now...
FYI:Tickets Price Goes Up By Wednesday...
Let's Support Our Own!!...
Cheers Can't Wait To See You Jul 6th 
It's Going To Be Massive...
You Know How I do!!!... 
Love You...xoxo Twi!!!

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA JUMAPILI Julai 8, 2018 mjini MAMLING, AUSTRIA

$
0
0
  Baada ya kuwadatisha washabiki katika maonyesho mawili makubwa kule Regensburg Festival  na Birkenreid festival Ujerumani sasa kamanda Ras Makunja anakipeleka kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni katika onyesho kubwa la Mamling Festival   nchini Austria ,onyesho hilo litafanyika siku ya  jumapili Julai 8, 2018.
Akiongea na vyombo vya habari kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Kamanda wa FFU Ughaibuni Ras Makunja alisema Ngoma Africa band ni mali ya washabiki na ina kazi moja tu nayo kudatisha washabiki katika kila onyesho bila kuremba remba.
Bendi hiyo iliyojizolea umaarufu na maelfu ya washabiki kila kona duniani imejiwekea rekodi ya aina yake kuwa ni bendi ya mwanzo ya kiafrika kuimiri vishindo,na kudumu kwa miaka 24  ughaibuni na kufanikiwa kuwanasa washabiki wa kimataifa.
ungana nao at www.ngoma-africa.com



BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 19/06/2018


VOA SWAHILI: Duniani Leo Juni 18, 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa azindua kampeni ya kitaifa ya kupima VVU

$
0
0

Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa akikata utepe katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. 


Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa (wa pili toka kulia) akipokea ngao ya heshima kutoka kwa mawaziri kuanzia kushoto, Selemani Jafo (TAMISEMI), Jenista Mhagama (Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu) na Ummy Mwalimu (Afya) kulia kabisa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa akimkabidhi cheti mojawapo ya mabalozi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu katika uzinduzi uliofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma


Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt Leonard Maboko akihutubia wageni waalikwa katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe Jenista Mhagama akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kupima VVU na kuanza kutumia dawa mapema ijulikanayo kama Furaha Yangu iliyofanfyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

TECNO SPARK 2, ANGAZA NYAKATI ZA MAISHA YAKO

$
0
0
TECNO SPARK 2, Angaza Nyakati za Maisha yako.
TECNO inafanya vizuri kwenye soko la ‘smartphone’ Tanzania.

 Hii inajidhihirisha kutokana na jinsi simu ya Spark ilivyofanya vyema mwaka jana. Mwaka huu TECNO wamekuja na Spark 2 ambayo imeboreshwa zaidi maalum kabisa kwa ajili yako wewe.

Imekuja na umbo jembamba pia ni nyepesi yenye nchi 6.0 HD+ na wigo mpana wa kioo chenye uwiano wa 18:9 kwa kuweza kuona vizuri zaidi na kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja kwenye skrini yako.

Kamera ya Spark 2 ni ‘megapixel’ 13 nyuma ikisindikizwa na flash tatu zilizokaa pamoja sehemu moja na ‘megapixel’ 8 mbele yenye flash mbili zilizokaa pamoja. Hivi vionjo vyote vinafanya kazi kwa pamoja ikiwa ni kung’aza picha na kupiga picha yenye uhalisia hata katika mwanga hafifu.
Uwezo wa ‘Portrait mode’ umeongezwa kwenye kamera ya mbele ili pale unapopiga selfie yako, sura yako inakua inaonekana vizuri kabisa. Pia kwa mfumo wa mixed flash 2.0, mwanga wa flash ya mbele umeongezwa kwa 40% na ule wa flash ya nyuma kwa 70%.

Spark 2 ina aina mpya ya ‘security’ yenye ulinzi madhubutu ambayo ni ‘face id’. Kupitia ‘face id’ una uwezo wa kufungua simu yako haraka zaidi kwa kuitazamanisha sambamba na paji la uso. Lakini pia ina ‘fingerprint’ yenye kufungua simu yako kupitia alama za vidole.

Pamoja ya kua kifaa hiki kinaendeshwa na Android 8.1 pamoja na processor ya 1.3Ghz quad core yenye kuipa simu kasi ya kufanya kazi kwa haraka zaidi na kupunguza uishaji wa chaji kwa haraka, lakini bado Spark 2 ina betri lenye ujazo wa 3500mAh. Kupitia Spark 2 unapata uhuru wa kusikiliza mziki, kupiga picha na kufanya kazi mbalimbali pasipo kikomo.
Kwa wale wapenzi wa simu nzuri, hakika hiki ni kifaa kwa ajili yako.
Kwa maelezo zaidi tembelea http://bbs.tecno-mobile.com

NIGERIA YAVUTIWA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI UNAOTEKELEZWA NA SERIKALI KUPITIA TASAF.

$
0
0

Na Estom Sanga- TASAF

Maafisa kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza namna Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF unavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameipongeza serikali ya Tanzania kwa kutekeleza kwa mafanikio Mpango huo wenye lengo la kupambana na umaskini.

Wakizungumza baada ya kutembelea eneo la Nzasa A katika halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam, Wataalamu hao kutoka Nigeria pamoja na mambo mengine wameshuhudia Walengwa wa TASAF wakijishughulisha na uzalishaji wa bidhaa kama mikeka, vikapu ,vyungu kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.

Aidha maafisa hao kutoka Nigeria wameshuhudia namna Walengwa walivyoboresha makazi yao kwa kujenga nyumba huku wakielezwa kuwa suala la elimu na afya limepewa kipaumbele kwa Kaya za Walengwa ikiwa ni mkakati maalum wa Mpango huo kujenga rasilimali watu .Wakiwa katika eneo hilo la Nzasa A wageni hao walioko nchini pamoja na wageni wengine kutoka Sudan Kusini wamejionea namna walengwa wanavyopata ruzuku kwa njia ya simu ikiwa ni mkakati maalum wa kuboresha huduma hiyo kupitia TASAF.

Hata hivyo katika ziara hiyo kilio cha Walengwa juu ya upatikanaji wa soko la bidhaa wanazozalisha baada ya kupata ruzuku kutoka TASAF kimeendelea kusikika huku walengwa hao wakiomba mfumo bora zaidi wa kutafuta masoko ya bidhaa wanazozalisha ili waweze kunufaika vizuri zaidi.Hii leo (Jumatano)maafisa hao kutoka Nigeria na Sudan Kusini wanatembelea na kukuitana na Walengwa wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Bagamoyo kujifunza namna Mpango huo unavyowanufaisha Walengwa hao.

Serikali kupitia TASAF imefanikiwa kuandikisha zaidi ya Kaya Milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote katika Mpango huo ambao pamoja na kupata ruzuku ya fedha ya kilamwezi, lakini pia wamekuwa wakipewa mafunzo ya namna ya kukuza kipato chao kwa kuanzisha miradi midogo midogo kwenye maeneo yao.
 Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF moja ya malengo yake ni kuihamasisha Walengwa wa Mpango huo kufanya shughuli za uzalishaji mali ikiwemo ususi wa vikapo,mikeka na kuuza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato. Pichani hapo juu wageni kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza na TASAF inavyotekeleza majukumu yake wakiangali bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa Mpango huo.
 Mmoja wa Wageni kutoka Nigeria akiwa ameshika kikapo alichokinunua kutoka kwa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF katika eneo la Nzasa B katika kata ya Charambe wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam.
 Baadhi ya maafisa kutoka nchini Nigeria walioko nchini kujifunza namna Mfuko wa Maendeleo  ya Jamii TASAF unavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini  wakiangalia bidhaa zinazouzwa na Wanufaika wa Mpango huo  katika eneo la Nzasa B wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
 Wageni kutoka nchini Nigeria wakiangalia baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- katika  mtaa wa Nzasa B kata ya Charambe wilaya ya Temeke mkoani Dar es salaam.

 Maafisa kutoka Nigeria wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke na TASAF baada ya kupata maelezo ya namna halmashauri hiyo inavyotekeleza  Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini .

Tanzania sasa mwanachama wa mataifa yanayokataa taka

$
0
0
Na Nelson Nchobe wa LITA

Duniani kote taka ni kero au adha ndogo katika familia kwa sababu moja tu: katika ngazi ya kaya watu ni wachache na taka ni adha ambayo watu hao wachache wanaweza kuimudu. Ili kuondokana na kero hiyo, kwa desturi, wanakaya hukusanya taka na kuziweka eneo moja.

Lakini kaya nyingi katika mtaa au kijiji zinapokusanya taka nakuzirundika eneo moja, ubaya wa taka unapanda daraja; taka inakuwa siyo adha au changamoto ndogo tena bali taka inageuka nakuwa ni tatizo KUBWA; rundo hilo la ataka linakuwa ni jambo la hatari. Hivyo ndivyo ilivyo duniani kote.

Kwa hiyo katika nchi zote duniani ukusanyaji na uhifadhi salama wa taka vimekuwa ni tatizo sugu kwa sababu kila siku taka huzalishwa majumbani, ofisini na viwandani. Taka hizo sasa zimekuwa ni kitu cha hatari kwa uhayi wa mwanadamu na viumbe wengine. Taka zimekuwa jambo la hatari kwa sababu kimsingi taka ni uchafu na uchafu ni chanzo cha magonjwa karibu yote. Lakini si hayo tu, taka zingine ni sumu inayoharibu mazingira na kuangamiza viumbe hai, wakiwemo wanadamu.

Kwa kuwa ukusanyaji na uhifadhi salama wa taka ni tatizo la kidunia, mataifa yote yamekuwa yakihangaika ili kushinda tatizo hilo. Sasa dalili za kupambana vilivyo na tatizo hili kidunia zinaanza kuonekana mwisho wa upeo wa macho kwa sababu kuna juhudi zinazoratibika zikiongozwa na asasi ijukanayo kama Let’s Do It World chini ya taasisi iitwayo Let’s Do It Global Foundation. 

Japo ukusanyaji na uhifadhi salama wa taka nchini Tanzania bado ni ndoto, Tanzania tayari imesajiliwa na taasisi ya Let’s Do It Global Foundation kuwa ni kati ya nchi zenye dhamira ya kweli katika kupambana na taka na kulinda mazingira. Lakini kusajilika tu hakutoshi; kikubwa ni bidii ya kweli ya kukusanya na kuhifadhi salama taka zizalishwazo nchini kwa mujibu wa sheria. Afrika ina nchi 42 ambazo zimesajiliwa katika zoezi hili wanachi wan chi hizo tayari wameishapata mafunzo.

Kihistoria msukumo wa hiari wa kupambana na taka ulianzia katika nchi ndogo ya Estonia huko Ulaya mwaka 2008. Msisimko huu sasa umesambaa duniani na nchi 133 and watu takribani milioni 20 wanashiriki katika ukusanyaji wa hiari wa taka zinazozagaa sehemu zisizo rasmi au taka zilizo nje ya madapo yanayotambuliwa na mamlaka husika katika nchi.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images