Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110149 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli amteua Jaji Mstaafu Damian Lubuva kuwa Mwenyekiti wa Baraza UDSM


MAAJABU YA KIKOSI CHA ACELAND KINACHOTIKISA KOMBE LA DUNIA

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

KIKOSI cha Timu ya Taifa cha Iceland kinachoshiriki Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi, kimekuwa gumzo kubwa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji wake kuwa madaktari.Kwa kukumbusha tu idadi ya watu katika Taifa hilo la Iceland haizidi 350,000. Idadi hiyo haiwezi kuipita Wilaya yoyote ya nchini Tanzania.

Kikosi hicho chenye idadi kubwa ya madaktari katika michuano hiyo mchezo wake wa kwanza kimetoa sare ya 1-1 dhidi ya timu ya Argentina.

Katika mchezo wa kwanza kati ya kikosi hicho na Argentina nyota wa Bacelona Lionel Messi alikosa penati baada ya mkwaju wake kupanguliwa na kipa Hannes Halldorsson ambaye kitaaluma ni Mkurugenzi Mkaazi wa masuala ya filamu.

Kikosi cha Iceland ambacho kimesheheni madaktari hadi kinaingia fainali ya kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kimecheza michezo saba ,kikishinda sita na kutoka sare mchezo mmoja.

Inaelezwa mbali ya kuwa na wachezaji madaktari pia kila mchezaji anayo taaluma nyingine inayompatia mshahara mnono tofauti na soka.Pia kocha wa kikosi hicho Heimir Hallgrimsson naye ni daktari wa meno.

Cha kufurahisha zaidi pia kikosi hicho kuna mchezaji ambaye ni wanasiasa, kuna Muoka mikate na mwingine ni Mtangazaji.Kutokana na hali hiyo kikosi hicho kimekuwa fahari kubwa kwa taifa la nchi hiyo.

Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Yafana Muhimbili

$
0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanafaniyika kwa siku tatu mfulilizo. Wananchi mbalimbali wamefika kwa wingi katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo pamoja na kupima afya bure. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Muhimbili, Bw. Juma Muhimbi na Mkurugenzi wa Tiba katika wizara hiyo, Dkt. Doroth Gwajima..
Bw. Paul Mayengo akipima dawa ya methadone kwa watu wenye tatizo la uraibu wa heroin katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Dawa hiyo inatumiwa na wataalamu wa afya kwa ajili ya kutibu uraibu.
Waziri Ummy Mwalimu akiwa kwenye banda la lishe ambako ampatiwa maelezo kuhusu lishe bora. Kushoto ni mmoja wa watu akipimwa afya baada ya kutembelea banda hilo leo.
Mkuu wa Idara ya Afya ya Akili, Dkt. Frank Masao akieleza shughuli mbalimbali za tiba zinazofanywa na idara hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI - JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizinduaTaarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada  ya kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada  ya kuizindua  katika Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mhandisi, Salome Kabunda  kutoka TANROADS  Tuzo ya Uwezeshaji Kiuchumi, baada ya TANROADS kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara, Wakala na Idara za Serikali kwenye  Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofunguliwa na Waziri Mkuu katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na baadhi ya viongozi walioshiriki katika Ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakipiga makaofi baada ya Waziri Mkuu kufungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa, Faustine Kamuzora, Meya wa jiji la Dodoma,Profesa Davis Mwamfupe, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mku, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama  (katikati) Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mku, Profesa Faustine Kamuzora baada ya kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018.

MEYA MSTAAFU KINONDONI AISHAURI JAMII KUDUMISHA AMANI, UPENDO

$
0
0
MEYA Mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Yusuph Mwenda ameishauri jamii kuendelea kudumisha amani na upendo hasa kipindi hiki ambacho Taifa linapopiga hatua za kimaendeleo chini ya Uongozi wa Rais Dk.John Magufuli.

Mwenda aliyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kuandaa Chakula maalumu kwa ajili ya watoto wanaoishi katika Mazingira magumu wanaolelewa katika Kituo cha Malaika.Amesema katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaendelea 'kujengwa' kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo, kuna kila sababu kwa wananchi wote kudumisha amani iliyopo nchini, kama hatua ya kuungana mkono maendeleo hayo.

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano, Taifa limeshuhudia likitekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo.Ametaja baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Reli ya Kisasa(Standard Gauge),Bwawa la kuzalisha umeme la Mto Rufiji(Stiggler's George) na kuiunganisha mikoa mbalimbali kwa barabara za lami.

"Sote tunashuhudia namna ambavyo Taifa letu linazidi kupiga hatua kuelekea mikakati ya Serikali ya ujenzi wa uchumi wa viwanda ifikapo 2025."Ambayo kimsingi kama watanzania tunapaswa kuipongeza,lakini ili hayo yafanyike kwa ufasaha tunapaswa kwanza kudumisha amani yetu tuliyonayo,"amesema Mwenda.


Aidha Mwenda ameiomba jamii kuwa na upendo kwa watoto wadogo hasa yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili kujiona kuwa sehemu ya familia zingine ambazo hazipo katika maisha wanayoyapitia.Amesema watoto hao ambao wengi wao wamepoteza wazazi wao wana kila sababu ya kuoneshwa upendo ili kuwajenga kisaikolojia wakati wote wanapokuwa katika maeneo wanayoelelewa.

"Hiyo itasaidia kuwapa nguvu ya kuwafikisha katika malengo yao mbalimbali ya kimaisha.Tuwapende ili wajione na wao ni sehemu ya jamii kama ilivyo kwa watoto wengine,"amesema.

JAFO ATOA WIKI MBILI KWA WAKURUGENZI KUBAINISHA MAENEO YA UJENZI WA MADARASA

$
0
0
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo ametoa wiki mbili kuanzia leo kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanabainisha maeneo ya ujenzi na mafundi watakaojenga madarasa 478 na mabweni 269.

Ameayasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yanayofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo alisema kuwa tayari Serikali imetenga shilingi bilioni 29 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 478 mapya na Mabweni 269 ili kuhakikisha wananfunzi wote waliokosa nafasi ya kupangiwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya kwanza wanapata katika uchaguzi wa awamu ya pili.

Mhe. Jafo amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanatumia muda mdogo kubainisha maeneo yatakayojengwa madarasa na mabweni kwa kutumia njia ya “Force Account” ili uchaguzi wa wanafunzi awamu ya pili uatakapofanyika na ujenzi huo uwe umekamilika. 

Mhe. Jafo aliwaagiza Wakurugenzi hao kusimamia ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika tarehe 30/08/2018 ili wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya kwanza wanachaguliwa katika awamu ya pili na kutimiza ndoto za wanafunzi hao .

Mhe Jafo aliwaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanasimamia kwa weledi ujenzi wa miradi mbalimbali katika Halmashauri zao ikiwemo ya ujenzi wa madarasa na Mabweni ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa madarasa nchini.

“Ninawaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa madarasa na mabweni kwa umakini wa hali ya juu ili dhamani ya fedha inayotolewa na Serikali iendane na majengo yatakayojengwa. Alisema Jafo

Aidha Mhe. Jafo alisema sambamba na ujenzi huo Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vingine 98 na kuwataka kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi na umakini wa hali ya juu hasa katika suala zima la usimamizi wa miradi mbalimbali ili dhamani ya fedha zinazotolewa iendane na majengo yatakayojengwa. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akitoa maagizo kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Dkt. Charles Mhina akiongea na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma

VOA SWAHILI: Duniani Leo 18th June 2018

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO JUNI 18, 2018


MAKAMU MKUU WA CHUO ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA PROF. LEONARD LEMA

MICHUZI TV: MAULID KITENGE NA ZARI, CHIDIBENZ ADAKWA TENA..

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 19, 2018

RATIBA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA RAIS WA TCCIA NDIBALEMA MAYANJA

VOA Swahili: Ulimwengu wa michezo hivi leo

HABARI ZA UN: Mwigizaji Angelina Jolie azuru Mosul kuwajulia hali waathirika wa vita

Mufindi, PELUM kutoa Hatimiliki za kimila 700

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa kushirikiana na Shirika la PELUM Tanzania imeanza zoezi la kutoa hatimiliki za kimila zipatazo 747 kwa wananchi wa vijiji vitano vikiwemo vya Usokami, Ugesa, Magunguli, Isaula na Makungu.

Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Mufindi, Simon Mbago ameyazungumza hayo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa Habari hii ofisini kwake ambapo amesema kuwa hatimiliki hizo zimeanza kutolewa baada ya wananchi wa vijiji hivyo kufanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi kupitia mradi wa Ushiriki wa Wananchi katika Kusimamia Sekta ya Kilimo unaofadhiliwa na watu wa Marekani.

“Tunalishkuru Shirika la PELUM kwa kufanya kazi nasi kwani limetusaidia kutekeleza moja ya majukumu yetu ya upimaji ardhi na utoaji hatimiliki ambapo hatimiliki hizo zinatarajia kunufaisha wanawake 250, wanaume 385, wenza wenye ushiriki wa pamoja 97 pamoja na maeneo ya Taasisi 15”, alisema Mbago.

Mbago ameongeza kuwa ni jukumu la kila Halmashauri kuhakikisha inatenga fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ili kuvifanyia vijiji vyake mpango wa matumizi ya ardhi hivyo uwepo wa mashirika binafsi likiwemo la PELUM husaidia kwa kiwango kikubwa kuchochea maendeleo katika Halmashauri mbalimbali.

Pia Mbago amefafanua umuhimu wa hatimiliki hizo kuwa zitasaidia wananchi wa Halmashauri hiyo kuzitumia katika kuomba mikopo kwenye Taasisi za fedha kwa kuweka dhamana maeneo yao pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi kwenye vijiji husika hasa kwa wananchi waliopo mipakani mwa wilaya ya Kilolo na Mufindi.
 Asafu Mgelekwa na Mkewe Atuganule Lunyungu wakiwa wameshikilia hati zao za pamoja.
Simon Mbago Afisa Ardhi Mufindi akimsaidia mwananchi kuweka saini kwenye fomu kama uthibitisho ya kuwa amepokea hati.
 Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ugesa wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa na hatimiliki zao za kimila.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KILIMO CHA PAMBA KUNOGESHA MAPINDUZI YA VIWANDA

$
0
0
 *Ni kutokana na juhudi za Serikali za kuhamasisha kilimo cha pamba 

ZAO la pamba ni miongoni mwa mazao makubwa ya biashara yaliyokuwa yakiliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni na kuchangia kukuza uchumi wa wananchi miaka ya 1970.

Kwenye miaka ya 1970 kulisheheni vyama vingi vya ushirika wa zao la Pamba na viwanda vya kuchambua nyuzi na kukamua mafuta, ambavyo vilibadili  hali halisi ya kipato cha wananchi wa eneo linalolimwa zao hilo na kulifanya kujulikana kama dhahabu nyeupe.

Kilimo hicho kilianza kudorora miaka ya hivi karibuni kutokana na kulegalega kwa vyama vya ushirika na matokeo yake pamba iliuzwa ikiwa chafu bila kuzingatia ubora  na madaraja yaliyopo.

Kutokana na sababu hizo Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, iliamua kufufua zao hilo ili kuhakikisha upatikanaji wa malighafi ya viwanda vya nguo na mafuta yatokanayo na mbegu za pamba zinapatikana pamoja na kuinua uchumi wa wakulima nchini.
 Katika kufanikisha suala hilo Serikali ilianza kwa kuwaagiza viongozi wa mikoa yote inayolima pamba kuhakikisha wanawahamasisha wakulima kufufua mashamba yao na ilihakikisha inafuatilia jambo hilo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa mashamba, ugawaji wa pembejeo hadi utafutaji wa masoko.

Baada ya kutoa agizo hilo ambalo lilifanyiwa kazi na tayari mafanikio yameanza kuonekana katika msimu wa mwaka huu, kwa wakulima  kuanza kuvuna na kuuza kwa mafanikio.

Akizungumzia kuhusu hali ya zao hilo mwaka huu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella, anasema msimu wa mwaka huu umekuwa na mafanikio makubwa kutokana na hamasa iliyotolewa na viongozi wakuu wa Serikali.
 Bw. Mongella anasema kutokana na hamasa hiyo, mwaka huu wanatarajia kupata mavuno makubwa kutoka katika kilimo  hicho kwa sababu wakulima wengi wamelima na baadhi yao tayari wameshaanza kuvuna.

Anasema Rais Dk. Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, walitoa maelekezo mahususi na walifanya ufuatiliaji wa karibu wa kilimo cha mazao makuu matano ya biashara nchini, likiwamo na zao la pamba.

Akizungumza kuhusu maendeleo ya zao hilo jijini Mwanza hivi karibuni, Bw. Mongella amesema zao la pamba litasaidia kufufua viwanda vya mafuta ya kula, nguo pamoja na kuongeza ajira.

Amesema baada ya Rais Dkt. Magufuli kuhamasisha kilimo cha zao hilo, ambacho kilianza kusuasua nchini, viongozi waliitikia na kuwahimiza wakulima wachangamkie fursa hiyo, ambao walikubali.
 “Tunashukuru kwa hamasa na miongozo iliyotolewa na viongozi wetu kwa sababu iliongeza ari kwa wakulima kulima zao la pamba kwa wingi na mwamko kwa wananchi kulima mazao mengine, likiwamo la mpunga,” anasema.

Hata hivyo, kiongozi huyo ameishukuru Serikali kwa kuagiza pamba itakayovunwa iuzwe kupitia minada itakayosimamiwa na Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) katika kila eneo, jambo ambalo limesaidia  kufufuka kwa vyama hivyo.
“Tunashukuru kwa maelekezo na miongozo iliyokuwa inatolewa na viongozi wetu wakuu. Sasa AMCOS zetu zimefufuka na huu ni mwanzo tu mapinduzi makubwa katika biashara ya zao la pamba na yajayo yanafurahisha zaidi,” anasisitiza Bw. Mongella.

Bw. Mongella anatarajia kuwahamasisha wakulima wote wa mkoa huo pamoja na wafugaji na wavuvi wajiunge katika AMCOS zilizoko katika maeneo yao, ili kuweza kuirahisishia Serikali kufanyanao kazi.

Mkuu huyo wa mkoa pia anatumia fursa hiyo kuwapongeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maofisa Kilimo kuanzia ngazi ya wilaya hadi kijiji na wakulima kwa kuhakikisha kilimo cha zao la pamba kinapata mafanikio.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KALEMANI AFURAHISHWA NA WENYE NIA YA KUTENGENEZA VIFAA VINAVYOZUIA UPOTEVU WA UMEME

$
0
0
Na Veronica Simba – Dodoma
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, amefurahishwa na maombi ya wawekezaji wa Kampuni ya CTC Power Equipment Co. Ltd, kutoka China, wenye nia ya kujenga Kiwanda cha kutengeneza vifaa maalum vinavyotumika kuzuia upotevu wa umeme vijulikanavyo kitaalam kama ‘Insulators.’
Wawekezaji hao ambao wameingia ubia na Kampuni ya kizalendo iitwayo Interbest Investment Co. Ltd, waliambatana na Mkurugenzi wake, Augustine Masonga na kuwasilisha maombi hayo kwa Waziri, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma, Juni 18, 2018.
Waziri Kalemani alisema kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha vifaa vyote vinavyotumika kuunganisha umeme vinanunuliwa hapa nchini na tayari imekwishapiga marufuku kuagiza vifaa kama transfoma, nguzo na nyaya mbalimbali, ambavyo vinapatikana hapa nchini.
“Kwa upande wa ‘insulators’, tumeshindwa kutoa zuio hilo kwakuwa, hazipatikani nchini na hivyo tunalazimika kuziagiza kutoka nje ya nchi,” alisema Waziri na kuongeza kuwa, itakuwa ni faraja kubwa kwa Serikali endapo wawekezaji hao watafanikiwa kuanzisha Kiwanda husika ili kuepusha gharama kubwa zinazotumika kuagiza vifaa hivyo nje na pia kupunguza muda mrefu unaotumika katika kuvisafirisha.
Aliwataka wawekezaji hao kukutana na wataalam wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili kujadiliana nao kuhusu suala la viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya vifaa husika. Pia, aliwataka kukutana na wataalam kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), ili waweze kufahamishwa viwango vinavyotakiwa nchini.
Waziri aliwapongeza wawekezaji hao kuingia ubia na mzalendo kwani ni moja ya vigezo vya kisera vinavyohitajika katika uwekezaji wa aina hiyo nchini.
Alisema kuwa, mbali na kuwapatia ajira wananchi lakini pia itasaidia kuwapa fursa ya kujifunza teknolojia husika ili baadaye waweze wao wenyewe kuanzisha aina hiyo ya uwekezaji na kuisimamia kikamilifu.
Wawekezaji hao waliahidi kutekeleza yale yote waliyoelekezwa na Waziri na kusema kwamba wanatarajia kukamilisha kazi zote za maandalizi ndani ya kipindi cha miezi zita kutoka sasa, na hivyo Kiwanda kuanza kazi ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu au Januari mwakani.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akiwa katika mazungumzo na Ujumbe kutoka Kampuni ya CTC Power Equipment ya China, waliwasilisha maombi ya kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kuzuia upotevu wa umeme (Insulators), Juni 18, 2018, Makao Makuu ya Wizara Dodoma. Wengine pichani ni wataalam wa Nishati wa Wizara.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiagana na Augustine Masonga, ambaye kampuni yake imeingia ubia na Kampuni ya CTC Power Equipment kutoka China waliowasilisha maombi ya kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kuzuia upotevu wa umeme (Insulators) nchini, Juni 18, 2018, Makao Makuu ya Wizara Dodoma.
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Salum Inegeja (wa pili kutoka kulia), Sebastian Shana (wa tatu kutoka kulia) na Mhandisi Ahmed Chinemba (wa pili kutoka kushoto), wakijadiliana na Ujumbe kutoka Kampuni ya CTC Power Equipment kutoka China, baada ya kikao chao na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) ambapo waliwasilisha maombi ya kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya kuzuia upotevu wa umeme (Insulators) nchini. Kikao hicho kilifanyika Juni 18, 2018 Makao Makuu ya Wizara Dodoma.

MAFUNZO KWA WAUZAJI, WASAMBAZAJI NA WAMILIKI WA VITUO VYA MAFUTA YA PETROLI KATIKA MIKOA YA DODOMA NA MOROGORO KUHUSU MAOMBI YA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO

CALL FOR APPLICATIONS TO VARIOUS PROGRAMS FOR 2018/2019 ACADEMIC YEAR

$
0
0



Basic Technician Certificate Programs - NTA Level 4


1.     Social Work

2.     Business Administration

3.     Labour Relations and Public Management

4.     Human Resources Management

5.     Community Work with Children and Youth



Minimum Entry Qualifications


(i)       The applicant must have at least four (4) passes of Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) - (Excluding Religious Subjects).

OR

(ii)     The applicant who holds at least six (6) months certificate from any institution recognized

by NACTE or NTVA Level 3. In addition, the applicant must have at least four (4) passes from Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) - (Excluding Religious Subjects).



Ordinary Diploma programs -NTA Level 5 & 6


1.     Social Work

2.     Business Administration

3.     Labour Relations and Public Management

4.     Human Resources Management


WAJASIRIAMALI MKOA WA KIGOMA WAHIMIZWA KUYATUMIA VEMA MAFUNZO YA STADI ZA BIASHARA

$
0
0
Na Abel Daud,Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kigoma, Samson Anga ametoa mwito kwa wajasiriamali mkoani Kigoma kuyatumia kwa vitendo mafunzo wanayopata ya stadi za biashara na ujasirimali kwani ndiyo njia pekee itakayowawezesha kukua katika shughuli zao.

 Anga ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wajasirimali kutoka Wilaya hiyo yanayoendeshwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC).

Anga amesema kuwa mafunzo yanayotolewa kuhusiana na kukuza mitaji,utafutaji wa masoko, uboreshaji wa bidhaa na biashara za kuvuka mipaka ya nchi ni mambo ambayo wajasiriamali wakiyatumia ni wazi shughuli zao zitakuwa na mafanikio makubwa.

Pia amesema kuwa bado wajasiriamali wengi wanazalisha bidhaa zao katika viwango visivyozingatia ubora vikiwa na uzalishaji mdogo mambo ambayo yanakwaza wajasilmrimali wengi kukuwa katika shughuli zao.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo Meneja wa TIC Kanda ya Magharibi, Innocent Kahwa amesema lengo la mafunzo yanayotolewa kwa wajasirimali yanalenga kuwafanya wapate faida kwa bidhaa wanazozalisha lakini pia kuwafanya wapanue shughuli zao na kuwa  na mafanikio zaidi katika shughuli wanazozifanya.

Kahwa amesema kuwa msingi mkubwa wa mafunzo yanayotolewa kwa wajasiriamali ni kuwafanya kujua sheria na taratibu zinazoongoza shughuli zao, kujua teknolojia kuwarahisishia shughuli zao lakini pia kujua utawala wa miradi na biashara hasa inapoanza kuwa mikubwa.
Meneja wa Kanda ya Magharibi Innocent Kahwa akitoa mada kwa wajasiriamali mkoani Kigoma.
Baadhi ya wajasiriamali wa Mkoa wa kigoma wakisikiliza mafunzo kutoka kwa Meneja wa TIC Kanda ya magharibi.
Afisa ufundi wa Sido Kigoma Alexander Mpuya akitoa mada kwa wajasiriamali wa Mkoa wa kigoma

Viewing all 110149 articles
Browse latest View live




Latest Images