Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110004 articles
Browse latest View live

BITEKO AELEKEZA TUME YA MADINI KUPELEKA TIMU YA WAKAGUZI WA MADINI WILAYANI ULANGA

$
0
0
NA FREDY MGUNDA,MOROGORO.

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amesema kuwa ataunda timu maalum ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza migodi yote nchini ikiwa ni pamoja na utambuzi wa aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika sekta ya madini.

Akizungumza wakati wa ziara ya siku mbili Mkoani Morogoro Mh Biteko alisema kuwa madini yote yaliyopo katika ardhi ya Tanzania ni mali ya watanzania hivyo yanapaswa kuwanufaisha watanzania kwanza ndipo watu wengine wafuate.

“Naombeni watanzania wote mjue kuwa madini haya ni mali ya watanzania wote hivyo tunapaswa kuyalinda na kutoa taarifa sahihi kwa serikali kama kuna mtu anaiibia serikali kwa namna moja au nyingine ili serikali iweze kuchukua hatua za kisheria dhidi yake, Na mimi nawaambieni watanzania tuache uoga tuseme ukweli kama Rais wetu Mhe Dkt John Pombe Magufuli anavyosisitiza utendaji wa uwazi na uwajibikaji katika serikali” Alikaririwa Mhe Biteko

Biteko amepiga marufuku wawekezaji kutumia fedha zao kuwanyanyasa wananchi waliopo kwenye maeneo ambayo kuna migodi kwa ajili ya kuwaibia watanzania ambao bado wana kipato cha chini katika maeneo yanapopatikana madini.

“Najua hawa wawekezaji wanapesa nyingi sana hivyo isiwe sababu ya kuwarubuni baadhi ya wananchi na kuwatesa wananchi wengi hususani waliopo kwenye maeneo ya madini na leo nataka niwaambie ukweli wawekezaji wote nchini najua ambavyo mnatumia pesa zenu kuwanyanyasa wananchi, sasa ndio mwisho wenu maana serikali ya awamu ya tano inataka haki kwa kila mwananchi” Alisisitiza Biteko

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Bitoke alifanya ziara ya kikazi katika kijiji cha Ipanko kilichopo katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kugundua kuwa kuna wawekezaji wanaidanganya serikali na wananchi kwa kutoweka wazi kiasi gani ambacho wanakipata kwenye migodi iliyopo katika kijiji hicho.


Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko akiongea na wananchi wa kijiji cha Ipanko juu ya changamoto ambazo wanakabiliwa nazo na kuunda timu maalum ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza migodi yote na aina ya madini yanayopatika katika migodi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania haiendelei kuibiwa na wawekezaji katika seckta ya madini. 

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Naibu waziri wa madini mheshimiwa Doto Bitoke alifanya ziara ya kutatua mgogoro baina ya wawekezaji na wananchi kwenye sekta ya madini.


BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA UCHANGISHAJI DAMU NCHI NZIMA.

$
0
0
Afisa uhamasishaji wa mpango wa taifa wa Damu salama, Mariam Juma akimpima damu mfanyakazi wa Exim Bank Daniel Lukuba wakati wa kampeni ya uhamasishaji watu kuchangia damu kwa hiari kwa kushirikiana na Damu Salama iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, posta mjini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya watoaji damu duniania (World Blood Donors Day 2018). 
Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama akimtoa damu mfanyakazi wa Exim Bank Patrick Masawe wakati wa kampeni ya uhamasishaji watu kuchangia damu kwa hiari kwa kushirikiana na Damu Salama iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, posta mjini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya watoaji damu duniani (World Blood Donors Day 2018). 
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim waitoa damu.

KUFIKIA 14 Juni, 2018 benki ya Exim Tanzania ilifikia kilele cha kampeni inayoenda kwa jina la "Kupata damu katika benki ya damu kesho, leo" ambayo imejikita kuwahamasisha wananchi kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu inayofanyika kila tarehe 14 Juni duniani kote.

Lengo kuu la kampeni hiyo ambayo iliendana sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo inayosema “Exim kazini leo kwa ajili ya kesho” ni kuchangisha damu na kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu katika mpango wa taifa. Kampeni hiyo inaonyesha kuwa benki ya Exim iko makini kutafuta njia za ubunifu za kuhudumia wateja wake na muhimu zaidi, inajitolea kuhakikisha inashirki kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mpango huu kila mwaka unalenga kukusanya damu kwa ajili ya benki ya taifa chini ya usimamizi wa Mpango wa Taifa wa uchangiaji damu nchini [NBTS].

Kampeni hii ilianza rasmi katika tawi la Exim mkoani Arusha tarehe 4 Juni na kuendelea katika mikoa ya Mbeya, Dodoma na Mwanza. Tukio kuu limefanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi 200 , wateja na jamii chini ya kauli mbiu ya kimataifa: "“Jitoe kwa ajili ya mwingine. Changia damu." Kampeni hii inakumbusha jukumu la kila mtu kujitolea katika kuwasaidia wengine katika hali ya dharura kwa kutoa zawadi ya thamani ya damu. Pia inasisitiza juu ya ukweli kwamba ni muhimu kutoa damu mara kwa mara ili kuhakikisha kuwepo na damu ya kutosha kabla ya dharura kujitokeza. Kampeni hii ni sehemu ya programu ya majukumu ya shirika la kijamii ya benki ya Exim Tanzania iitwayo, Exim Cares. 

mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard Visa’ akwea pipa

$
0
0
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (wa pili kushoto), akiagana na mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard Visa’, Mohamed Kinjenge, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, kabla ya kwenda nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (wa pili kushoto), akiagana na mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard Visa’, Mohamed Kinjenge, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, kabla ya kwenda nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia. Wengine wanaoshuhudia ni maofisa wa benki ya CRDB.
Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard visa’, Mohamed Kinjenge (kulia), akisindikizwa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Willy Kamwela (kushoto), wakati akielekea nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 
Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard visa’ Mohamed, akifurahia safari yake ya kwenda nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia la Fifa 2018. 
Mshindi wa Wiki ya Kwanza ya Kampeni ya ‘Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCard Visa’ Mohamed Kinjenge (kulia), akiwapungia mkono maofisa wa Benki ya CRDB (hawapo pichani), waliomsindikiza kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, wakati akielekea nchini Urusi kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia la Fifa 2018. Kushoto ni Meneja Huduma za Kibenki kwa Njia ya Kielektroniki, Mangire Kibanda ambaye anaambatana na mshindi huyo.

NEWZ ALERT:WAZIRI WA MAJI AMTUMBUA KAIMU AFISA MTENDAJI WA DAWASA NA BODI YA WAKURUGENZI

$
0
0
Na Cathbert Kajuna-Kajunason/MMG.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Isack Kamwelwe ametengua uteuzi wa aliyekuA kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Eng. Romanus Mwang'ingo na kuvunja bodi ya wakurugenzi wa DAWASA.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Eng. Kamwelwe amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kupisha uchunguzi wa taarifa ya kuwepo kwa udanganyifu na ubadhirifu katika utekelezaji wa mradi wa kuchimba visima vya maji Kimbiji na Mpera huko Kigamboni jijini Dar es Salaam. 

"Wakati jambo hilo linafanyiwa uchunguzi na TAKUKURU serikali imechukua hatua za kutengua uteuzi wa huyo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Bodi yake kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki ili kuunusuru mradi mapema," amesema Eng. Kamwelwe.

Taarifa hizi zinaonyesha pamoja na mambo mengine udanganyifu uliofanyika kuhusu idadi ya visima vilivyokamilika kama ambavyo zimewasilishwa wizarani na DAWASA na uhalisia katika eneo la utekelezaji wa mradi.

Aidha Waziri Eng. Kamwelwe amemteua Dkt. Sufian Masasi kukaimu nafasi hiyo mpaka utaratibu mwingine utakapokamilika.

KAMISHNA MKUU WA TRA APONGEZA UTUMIAJI WA MASHINE ZA EFD IRINGA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Iringa

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere amewapongeza Wafanyabiashara mkoani Iringa kwa kuwa na mwitikio mkubwa wa kutumia Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFD) ambazo husaidia kutunza kumbukumbu za mauzo ya wafanyabiashara hao na kurahisisha ukusanyaji mapato ya Serikali.

Akizungumza leo mara baada ya kutembelea baadhi ya maduka na vituo vya mafuta mkoani hapa, Kichere amesema kwamba, mwamko wa matumizi ya Mashine za EFD umeongezeka kwa kiasi kikubwa na wafanyabiashara wengi wanatumia mashine hizo kwa ufasaha.

"Nichukue nafasi hii kuwapongeza wafanyabiashra wa Iringa mjini kwa mwitikio wao mkubwa wa kutumia Mashine hizi za EFD. Nimeona maduka mengi na wafanyabiashara wengi sana wakitumia mashine za EFD katika maduka na vituo mbalimbali vya mafuta hapa mjini," alisema Kichere.

Aidha, Kamishna Mkuu Kichere amewahimiza wafanyabiashara hao na wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa na kudai risiti kila wanapofanya mauzo na kununua bidhaa na huduma mbalimbali.Kwa upande wake mfanyabiashara maarufu wa Kampuni ya ASAS iliyopo mkoani hapa, Feisal Abri amesema kuwa, ujio wa Kamishna Mkuu wa TRA ni wa muhimu kwa wafanyabiashara hao kwani huwasaidia kutambua Sheria mbalimbali za Kodi zikiwemo zile zinazohusiana na matumizi ya Mashine za EFD.

"Ujio wa Kamishna Mkuu unatupa nguvu sisi wafanyabiashara na kuona kwamba hatuko peke yetu ila kuna watu wanatufuatilia kwa maana ya kutusaidia kujua Sheria mbalimbali za Kodi. Hivyo, ninaomba utamaduni huu uendelee na uwe wa mara kwa mara," alieleza Abri.Naye, Rehema Shabani mfanyabiasha wa duka la nguo lililopo katika soko la Miyomboni alisema kuwa amefurahishwa sana na ziara ya Kamshina Mkuu wa TRA katika soko hilo kwa sababu amepata fursa ya kumueleza kero na malalamiko yake.

"Nimefurahi sana kumuona Kamishna Mkuu wa TRA kwa sababu nimetoa kero zangu na nimemueleza malalamiko yangu na amewaagiza viongozi wa TRA hapa mkoani kuyafanyia kazi," alisema Rehema.Kamishna Mkuu Charles Kichere amehitimisha ziara yake mkoani Iringa ambapo amefanikiwa kutembelea jumla ya maduka ya bidhaa mbalimbali 36 pamoja na vituo vya mafuta vinne.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akisikiliza maoni kutoka kwa mfanyabiasha wa duka la nguo lililopo katika soko la Miyomboni mkoani Iringa Bi. Rehema Shabani wakati alipofanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta leo mkoani hapo.
Mfanyabiashara wa Kampuni ya ASAS iliyopo mkoani Iringa Feisal Abri akitoa maelezo kuhusu namna Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) inavyofanya kazi katika kituo chake cha mafuta wakati Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere alipofanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za EFD kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta leo mkoani Iringa.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa kofia kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa moja ya kituo cha mafuta mkoani Iringa wakati alipofanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta leo mkoani hapo. (PICHA NA TRA).

WAKULIMA, WAWEKEZAJI ZAO LA KOROSHO WAPONGEZA UFUFUAJI WA VIWANDA, WATOA MAOMBI KWA RAIS MAGUFULI

UTARATIBU MPYA WA USAJILI WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

NCHI ZA KENYA, TANZANIA ZAOMBWA KUSHIRIKIANA KUPINGA UKEKETAJI

$
0
0
Na Frankius Cleophace, Tarime

NCHI za Kenya na Tanzania zimeshauriwa kuendelea kushirikiana vema katika kupinga na kulaani vitendo vya ukeketaji kwa mtoto wa kike huku zikitakiwa kumthamini na kumpa kipaumbele katika elimu.

Ushauri huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Wazee wa Mila kutoka nchini Kenya Zacharia Ghati wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na wazee wa Mila Kijiji cha Pemba kwa kushirikiana na Shirika la ATFGM Masanga ambao wanapiga vita ukeketaji.Zacharia amesema kuna koo ambazo zinapatikana Tarime kwa upande wa Tanzania pia zinapatikana nchini Kenya, hivyo wote wanatamaduni moja.

" kama ni suala la ukeketaji wengine wanaenda Kenya ili kutimiza azma yao na wengine kutoka Kenya na kuja Tanzana, hivyo sasa kuna haja kubwa ya kushirikiana baina ya nchi zote mbili ili kukomesha ukeketeji,"amesema.

Kwa upande wa Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukenye Elias Maganya anasema wao kama wazee wa mila tayari wamepaza sauti zao na kudai kuwa mwaka huu hapatakuwa na ukeketaji kwa mtoto wa kike.

"Na suala la kupaka unga tutapaka watoto kuanzia miaka 15 si watoto wadogo na lengo ni kutimiza mila na ili suala litamalizika polepole kama zamani tulikuwa tunatoboa masikio."Wajaruo wanangoa Meno lakini Vyote kwa sasa vimeisha na suala la Ukeketaji litaisha lenyewe,"amesema Elias.
Zacharia Ghati Mzee wa Mila kutoka Nchini Kenya akitoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Pemba .
Wazee wa Mila Muungano wa Koo12 Kabila la Wakurya na Wazee wa Mila kutoaka Nchini Kenya wakiwa katika Mkutano huo wa kutoa Elimu ya Kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.
Abel Gichaine ambaye ni Mratibu wa Huduma ya Afya na Ustawi wa Jamii Wilaya ya Tarime akitoa Elimu kwa Wananchi hao na kutaja madhara yanayompata Mwanamke aliyekeketwa wakati wa kijifungua na kufafanua sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.
Wangubo Mtongori Mzee wa Mila kutoka Koo ya Bukira Tanzania na Kenya akitoa Elimu kwa Wananchi wa kata ya Pemba.


DKT TIZEBA ASHTUSHWA WANAWAKE PEKEE KUVUNA PAMBA

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Igunga-Tabora

Waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba ameshtushwa na wanawake pekee kuwa kwenye mashamba wakivuna pamba ilihali waume zao wakiwa kwenye Chang’aa (Pombe za kienyeji) ama kwenye vijiwe kupiga soga.

Dkt Tizeba ameshtushwa na wanawake wengi kuwa shambani wakivuna pamba ilihali waume zao wakiwa kwenye vijiwe vya pombe za kienyeji mara baada ya jana 18 Juni 2018 kutembelea katika Kijiji cha Bukama na Mwakipoleja vilivyopo katika kata ya Mbutu Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora kujionea hali ya mavuno ya zao la pamba.

Waziri wa Kilimo Mhe Tizeba amesema kuwa kwa muda mrefu imekuwa kama utamaduni wa kawaida kwa wanaume katika maeneo mengi nchi kuwatelekeza wake zao wakati wa kuvuna pamba lakini wakati wa mauzo wanawake hao huachwa nyumbani pasina kujua kiasi kilichopatikana baada ya mauzo.

Hata hivyo wananchi wengi ambao ni wakulima wa pamba kijijini hapo wameishukuru Serikari kwa kuweka mfumo mzuri wa ununuzi wa zao hilo, ambalo kwa mwaka huu linauzwa kupitia katika minada inayosimamiwa na Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS).

Pia wakulima hao wameiomba Serikali kuziwezesha AMCOS kuwa na maghala makubwa na ya kisasa ya kuhifadhia pamba, lengo likiwa ni kuhakikisha pamba inahifadhiwa kwenye maeneo salama na kuifanya isipoteze ubora.

Mkulima wa pamba Ndg Elius Bushia kutoka kijiji cha Bukama alimueleza waziri wa kilimo kuwa awali kabla pamba kuanza kuuzwa kupitia AMCOS suala la ubora lilikuwa halizingatiwi na wakulima wengi kwani pamba yake ikikataliwa na kampuni moja alikuwa na uhuru wa kuipeleka kwenye kampuni nyingine hivyo jambo hilo lilichangia kupunguza ama kuisha thamani ya zao hilo.

Hata hivyo ameiomba Serikali kuwajengea uwezo viongozi wa Ushirika ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu na pia isaidie kutoa elimu kwa wanachama juu ya umuhimu na faida za AMCOS ili wakulima wengi waweze kujiunga.

Dkt Tizeba aliwaahidi wananchi hao kuwa changamoto zilizojitokeza kwenye kilimo mwaka huu serikali itazifanyia kazi ili kuzipunguza au kuzitokomeza kabisa huku akiwatangazia neema wakulima hao kuwa serikali itatoa mbegu na dawa za pamba bure ili wakulima wanufaike na matunda ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akishiriki uvunaji wa zao la Pamba, wakati alipotembelea Kijiji cha Mwakipoleja kilichopo kata ya Mbutu Wilayani Igunga Mkoani Tabora akiwa safarini kuelekea Mjini Dodoma, Jana 17 Juni 2018. Picha zote Na Mathias Canal-WK
Waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba akimkabidhi Felista Elius pamba aliyovuna, wakati alipotembelea Kijiji cha Bukama kilichopo kata ya Mbutu Wilayani Igunga Mkoani Tabora akiwa safarini kuelekea Mjini Dodoma, Jana 17 Juni 2018.

GERALD MWANILWA AIBUKA MSHINDI KAMPENI YA BENKI YA CRDB YA SHUHUDIA KOMBE LA DUNIA LA FIFA 2018 NA TEMBOCARDVISA

$
0
0


Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akimkabidhi mshindi wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa, Gerlad Mwanilwa, Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi tiketi yake mshindi wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa 2018 na TemboCardVisa Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa wiki ya sita, Gerald Mwanilwa.
Mshindi wa wiki ya sita wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa na TemboCardVisa, Gerald Mwanilwa, akitoa neno la shukrani baada ya kupokea tiketi ya kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia la Fifa 2018.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (kulia), akifafanua jambo kuhusu utaratibu wa kusafiri mshindi wa wiki ya sita wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia la Fifa na TemboCardVisa, Gerald Mwanilwa (kushoto).

HELPAGE TANZANIA, JB GERIATRIC WATOA ELIMU YA AFYA KWA VIJIJI 10 KIBAHA

$
0
0
VIJIJI 1O vya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ikiwemo cha Kongowe wamepatiwa elimu ya afya na vizazi rika pamoja na kupatiwa mafunzo mbalimbali kuhusu magonjwa yasiyo ambukiza.

Elimu na mafunzo hayo yametolewa na Shirika la HelpAge Tanzania kwa kushirikiana na asasi ya Jb Geriatric pamoja na HIV Center.

Mkurugenzi wa Asasi ya Jb Geriatric Judith Bagachwa amesema elimu na mafunzo hayo yametokana kupitia nguvu ya kijiji katika tekelezaji.Amesema lengo ni kuwawezesha wanakijiji kutumia rasilimali walizo nazo pasipo kutegemea kupata msaada wowote ule kutoka vyanzo vya nje.  

"Mradi huu ulichaguliwa na wanakijiji wenyewe wa Kongowe ambao kwa busara zao waliona ni kitu ambacho kingeweza kunufaisha wanakijiji wote,"amesema. Pia ameongeza kwa muda mrefu toka mradi huo uanze Kongowe imekuwa ikisuasua hasa katika utekelezeji. 

"Wanakijiji walikubaliana kuanzisha shamba la bustani ya kulima mbogamboga ili kuwasaidia wazee na pia watu mbalimbali kupata lishe bora,"amema.Pia wanakijiji walikubaliana kutoa elimu ya dawa ya kulevya ili kuwasaidia vijana ambao walionekana kuathirika na janga hilo. 

 Akieleza kwa undani kuhusu jitihada zilizofanyika Mzee Gadi Salumu Matitu amesema haikuwa rahisi kwani kila mtu alitegemea wangewezeshwa katika kuufanya  mradi huu. "Wengi walisahau kuwa ilitupasa kutumia rasilimali tulizonazo ili kufanikisha mradi huu,"amesema. 

Mmoja wa walioshiriki  kutekeleza mradi huo Shaha Iddi amesema rasilimali waliyokuwa nayo ilikuwa nguvu tosha ya kufanikisha mradi wa kijiji ila watu wengi wamekuwa wakitaka kuwezeshwa kwanza ili kuweza kufanya kitu.Naye Mariam Ally anasema penye nia pana njia. Hiyo imejidhihirisha sasa kwani pamoja na changamoto zilizopo wamefanikiwa kufanikisha lengo lao.

Mshiriki mwingine katika mradi huu wa Kongowe Salma Hamadi Salum amesema mradi huo umekuwa wa manufaa kwao kama washiriki na hata pia jamii. 
Mahindi kutoka shamba lo kongowe baada ya kuvunwa na sasa yanapikwa kwa ajili ya kuuzwa kwa wateja ambao ni wana kongowe. 

Baadhi ya washiriki wa Mradi wa kijiji Kongowe

TASAF YAIVUTIA NIGERIA NA SUDAN KUSINI,WAJA NCHINI KUJIFUNZA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI.

$
0
0
Na.Estom Sanga-TASAF. 

Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF yameanza kuvutia Mataifa mbalimbali ya kiafrika kuja nchini kujifunza namna Mpango huo unavyotekelezwa. 

Miongoni mwa nchi ambazo zimetuma wataalamu kujifunza namna serikali ya Tanzania kupitia TASAF inavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaohudumia takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja ni pamoja na Sudan Kusini na Nigeria. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa Ujumbe huo ambao umeanza ziara katika Ofisi za TASAF jijini Dar es salaam,wamepongeza hatua ya Serikali ya Tanzania kutekeleza Mpango huo ambao wamesema unawagusa moja kwa moja wananchi wanaokabiliwa na umaskini. 

Wamesema mkakati huo wa kupunguza umaskini kwa njia ya hifadhi ya jamii unaonyesha mafanikio makubwa nchini Tanzania na hivyo kuvutia nchi nyingine kuja kujifunza namna Mpango huo uliyofanikiwa. 

Aidha wajumbe hao kutoka Sudan Kusini na Nigeria wamesema utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutokana na dhamira ya dhati inayoonyeshwa na serikali katika kupambana na umaskini kwa kuwashirikisha wananchi. 

Akitoa maelezo kwa Wageni hao,Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga amesema mafanikio ya shughuli za Mpango yametokana kwa kiasi kikubwa na ushirikishaji wa Wananchi tangu katika hatua za awali hadi sasa,huku akiipongeza Serikali kwa kuratibu kwa ufanisi utekelezaji wa shughuli za Mpango huo. 

Ametaja baadhi ya mafanikio ya Mpango kuwa ni kuhamaisha walengwa wa Mpango kufanya kazi za uzalishaji mali kwa kutumia ruzuku wanayoipata na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora, huku msisitizo pia ukiwekwa katiamsekta za elimu, afya na lishe hususani kwa watoto na mama wajawazito. 

Ujumbe huo utapata fursa ya kutembelea mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambako utakutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini na kujionea namna wanavyonufaika na Mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akizungumza na wageni kutoka Sudan Kusini na Nigeria (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijijini Dar es salaam,wageni hao wako nchini kujifunza namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Mmoja wa wageni kutoka Sudan Kusini akizungumza kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam juu ya azma ya serikali yao kujifunza utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kwenda kuutekeleza nchini kwao.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga (wa pili kushoto) akimsikiliza mgeni kutoka Nigeria aliyesimama kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijijini Dar es salaam,wageni hao wako nchini kujifunza namna TASAF inavyotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
Wajumbe kutoka Sudan Kusini,Nigeria,na baadhi ya Watumishi wa TASAF makao makuu wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI TANO KWA MTOTO LATIFA KADOGOSA ALIYEPOOZA MWILI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Katibu wa Rais Ngusa Samike akimkabidhi Rehema Kadogosa ambaye ni Mama wa Mtoto Latifa Kadogosa (13) aliyelala kitandani kiasi cha Shilingi milioni tano (5,000,000/-) fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo ambaye ana matatizo ya kiafya jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Rais Ngusa Samike akimuangalia mtoto huyo Latifa Kadogosa(13) ambaye amepakatwa na Mama yake Rehema Kadogosa Mwenge jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Tawi la Benki ya CRDB Mikocheni Rehema Moyo akimkabidhi Kadi ya Benki Rehema Kadogosa mama mzazi wa Latifa Kadogosa mara baada ya kufungua Akaunti katika tawi hilo kwa ajili ya kutunza fedha hizo alizopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na fedha nyingine atakazosaidiwa na wadau wengine. PICHA NA IKULU

STRENGTH OF COMMUNITY LIFE COMPETENCE (CLCP) AT MWENDAPOLE A

$
0
0
HelpAge International in partnership with Jb Geriatrics and HIV Center, Pwani DPA and GSST have been implementing a project on Measuring Healthy Aging and Co Designing Health in Tanzania. The project is being implemented in Kibaha township and Kibaha Municipal council.

Judith Bagachwa director of Jb geriatrics says Mwendapole A is one of the communities that has successfully been engaged in the implementation of the project. The beginning was really tough because the practice of community life competence requires members to use/utilize their own resources so as to solve their problems. 

The process of using their own resources took a very long time before community members realized they were capable of doing something by themselves. CLCP has helped Mwendapole A community members learn to appreciate their strengths and take actions towards challenges that they face.

So as to live a healthy living style Mwendapole A started a vegetable garden where community members could grow vegetables to improve on their nutrition. Community members worked together and through the help of their local leader they managed to secure a piece of land where they could grow their vegetables. 

 Mr Desdery Masawe who works at the Local government office, confirmed that a piece of land was secured for community members to implement on their project. Community members immediately took actions and started to work on their project.

Salum Chambuli a group chairperson explained that the steps taken gave community members a sense of progress and believed that anything is possible. Before the land was secured people had lost hope and others left. But now that the land is available people have put all their strengths in making sure that the community project becomes a success. 
 

Community members at their new farm
Elizabeth Nkwela at the community farm 

TIMU 49 ZAJIANDIKISHA KUSHIRIKI MSIMU MPYA WA MICHUANO YA SPRITE BBALL KINGS

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Timu 49 kutoka Jijini Dar es Salaam zimefanikiwa kufanya usaili wa ushiriki wa michuano ya Sprite inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings msimu wa pili yalizinduliwa mapema wiki iliyopita na kuzitaka timu kufanya usaili siku ya Jumanosi ikiwa ni zoezi la siku moja kwenye Viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya zoezi la usaili kwa timu shiriki likiendelea Afisa Masoko wa East Africa Television Basilisa Biseko alisema kuwa zoezi limeenda vizuri na mwitikio umekuwa mkubwa sana na timu zilizoshiriki mwaka jana nazo ziliweza kujitokeza na kufanya usaili.Basilisa amesema kuwa, michuano ya mwaka huu yatakuwa ya kuvutia zaidi kwani timu nyingi zimejipanga na zimejiandaa kwa ajili ya kuleta ushindani kwa msimu huu wa pili.

"Michuano ya mwaka huu yatakuwa na ushindano mkubwa sana kwani timu zimejiandaa pamoja na zile zilizoweza kushiriki msimu wa kwanza wa Sprite BBall Kings ," amesema Basilisa."Kwa mwaka huu timu zimejipanga kuondoka na milioni 10 za ushindi na kombe, na Mchezaji bora wa michuano (MVP) ataondoka na Milioni 2 na kikombe ukiachilia mbali mshindi wa pili akijinyakulia Milioni 3," amesema.

Kwenye msimu wa kwanza wa Sprite BBall Kings timu ya Mchenga BBall Stars iliweza kuibuka na ubingwa wa Sprite BBall Kings 2017 akijinyakulia milioni 10 na kombe huku TMT wakishika nafasi ya pili na kujipatia milioni 3 huku mchezajj bora (MVP) Barongo akiondoka na milioni 2.

Baadhi ya timu zilizoweza kujiandikisha kwa msimu huu wa pili ni pamoja na Mchenga BBall Stars, TMT,Flying Dribblera, Ardhi University na Kurasini Heat ikija na jina jipya la Temeke Heroes baada ya kugawanyika kwa baadhi ya wachezaji wake.
Afisa Masoko wa East Africa Television Basilisa Biseko akizungumzia zoezi zima la usaili kwa zitakazoshiriki michuano ya Sprite BBall Kings msimu wa pili unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Juni.
Usaili wa washiriki wa Mashindano Sprite BBall Kings wakiendelea kujisajili kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo yanayotarajiwa kutimua vumbi Juni 23 mwaka huu uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Mlimani City Mall , Jumla ya timu 49 ziliiweza kujisajili kwa ajili ya simu kwa msimu wa pili wa Sprite BBall Kings.

OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YAWATUNUKU WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI MASOMO YA KEMIA NA BAIOLOJIA KITAIFA

$
0
0
 Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Mohamed Bakari akizungumza katika hafla ya kuwatunukia wanafunzi Kidato cha Nne na cha Tano waliofanya vizuri kitaifa katika masomo ya Sayansi, Baioloji na Kemia iliyofanyika kwenye makao makuu ya Wakala wa Maabara ya  Mkemia Mkuu wa Serikali barabara ya Barack Obama jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Maabara  ya Mkemia mkuu wa Serikali Elen Hellen Jason akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es salaam.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Maabara  ya Mkemia mkuu wa Serikali Elen Hellen Jason akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es salaam.
 Dk Fidelice Mafumiko  Mkemia Mkuu wa Serikali akizungumza na kutoa maelezo kadhaa wakati wa kuwatunikia zawadi wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi, Kemia na Baioloji katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam.
 Picha mbalimbali zikionyesha wanafunzi wakipokea vyeti na zawadi katika hafla hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA UHOLANZI NCHINI TANZANIA

$
0
0

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul alipomtembelea leo tarehe 18 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul alipomtembelea leo tarehe 18 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul alipomtembelea leo tarehe 18 Juni, 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jeroen Verheul alipomtembelea leo tarehe 18 Juni, 2018 ​fisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA DEONISIUS SIMBA – OFISI YA BUNGE)

TANZANIA INAONGOZA KWA UCHUMI KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA-WAZIRI MKUU MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema taarifa ya Kongamano la Uchumi la Dunia la mwaka 2018 inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kuwa na uchumi jumuishi miongoni mwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Amesema hali hiyo, imetokana na Tanzania kufungua fursa za ujasiriamali ambapo kuna zaidi ya biashara milioni tatu zinazokuwepo kila mwaka, lengo la nchi ni kuhakikisha kuwa uchumi unakua na unamgusa kila Mtanzania hususan mwananchi wa kawaida.

Waziri Mkuu ameyasena hayo leo (Jumatatu, Juni 18, 2018) wakati akifunguaKongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa LAPF, jijini dodoma.

“Pia, huduma za fedha jumuishi ni kigezo ambacho kimeiweka Tanzania mahala pazuri kwenye uchumi jumuishi ambapo zaidi ya Watanzania milioni 30 wamekuwa wakifanya miamala mbalimbali ya fedha kupitia simu za mkononi na hivyo kuongeza huduma za fedha kufikia asilimia 65,” amesema. 

Amesema huduma za msingi za kijamii kama vile elimu, afya na kupungua kwa rushwa katika utoaji huduma za umma pamoja namtandao wa miundombinu ya barabara ambayo huwezesha wananchi wengi kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ni kigezo kingine kilichozingatiwa katika kuipatia Tanzania nafasi hiyo. 

Waziri Mkuu ameongeza kwamba Serikali inaamini kuwa uchumi wa viwanda ukiimarika uchumi utakuwa kwa kasi kubwa na matokeo yake yataonekana wazi kwa kupanua wigo wa ajira, soko la huduma na shughuli nyingine za kiuchumi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 9 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu  Jenista Mhagama akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. 
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizinduaTaarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada ya kufungua Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Taarifa ya Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mei 2017 Mpaka Mei 2018  baada ya kuizindua  katika Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mhandisi, Salome Kabunda  kutoka TANROADS  Tuzo ya Uwezeshaji Kiuchumi, baada ya TANROADS kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Wizara, Wakala na Idara za Serikali kwenye  Kongamano la Tatu la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofunguliwa na Waziri Mkuu katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma Juni 18, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. John Jingu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMPUNI YA EY YAWAKUTANISHA WADAU KUCHAMBUA BAJETI 2018/ 19

$
0
0
 KAMPUNI ya EY imewakutanisha wadau wakiwamo wachambuzi wa bajeti ambapo pamoja na kuipongeza bajeti ya fedha ya mwaka 2018/2019 wameishauri Serikali kuwekeza zaidi kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza viwanda na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Wakizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kujadili bejeti ya Serikali iliyowasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango wadau hao kila mmoja aliyepata nafasi ya kutoa maoni yake wameipongeza lakini wakatoa ushauri kwa baadhi ya maeneo ambayo wanaamini yakitiliwa mkazo italeta tija katika maendeleo ya nchi.

Miongoni mwa waliochangia na kuichambua bajeti ya mwaka huu ni Mtalaam na Mchambuzi wa bajeti Profesa Prosper Ngowi ambaye amesema Serikali inatakiwa kuwekeza zaidi kwenye sekta ya kilimo ambayo itaongeza ukuaji wa viwanda na kuchochea ajira kwa wananchi.

Amefafanua katika sekta ya kilimo, Serikali ya Tanzania imeridhia makubaliano yaliyoingiwa na nchi mbalimbali za kuongeza sekta ya kilimo kwa asilimia 10 lakini ukifuatilia utabaini kilimo kinakuwa kati ya asilimia 3 hadi asilimia 5.
 Mtalaam na Mchambuzi wa bajeti Profesa Prosper Ngowi akizungumza jambo wakati wa kujadili bejeti ya Serikali, katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam leo.

"Bajeti ya Serikali ya mwaka huu ni nzuri na unapotaka kuchambua bajeti lazima uangalie na bajeti za mwaka uliopita.

"Unapoangalia bajeti imekuwa na maendeleo kila mwaka lakini kikubwa ambacho tunataka kuona ni utekelezaji wa bejeti yenyewe,"amesema Profesa Ngowi.
 Hata hivyo bajeti kwa ujumla iko vizuri na kufafanua ni wakati muafaka pia kwa Serikali kuhakikisha inatoa fursa zaidi katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati ambao wakijengewa uwezo kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza wigo wa ajira

Mtoa mada na mchambuzi mwingine kwenye mjadala huo Felix Mlaki amesema kuwa kuna baadhi ya mambo lazima yaangaliwe vizuri ambapo amesema kwa upande wake hakubaliani na kutengwa fedha kwa ajili ya kutoa kwa wananchi.

"Kuna utaratibu ambao unafanyika wa kutengwa fedha kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na vijana.Kwangu sioni kama hili linatija na ushauri wangu badala ya kutoa fedha.
 Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mokasi Medical Systems, Monica Joseph akizungumza jambo wakati wa kujadili bejeti ya Serikali, katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es salaam leo.

"Ni vema Serikali ikatengeneza mazingira ya kuwadhamini wananchi katika kuanzisha miradi ya kimaendeleo.Pia lazima watu walipe kodi kikamilifu,"amesema Mlaki.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mkazi wa Ernest &Young Joseph Sheffu amesema lengo la kuandaa mjadala huo wa kuichambua bajeti ni kupata maoni ya wateja wao hasa kwa kuzingatia bajeti husaidia wafanyabiashara kupanga mikakati yao na kuangalia namna ya kuitekeleza.

Sheffu amesema bajeti iliyowalishwa na Waziri wa Fedha kwa mwaka huu ni nzuri."Tunaamini mjadala huu wa kuichambua bejeti unatoa fursa kwa wafanyabiashara kuweka malengo yao ya kibiashara,"amesisitiza Sheffu.

Mtoa mada mwingine kwenye mjadala huo Monica Joseph ameipongeza bajeti ya mwaka huu kutokana na namna ambavyo imejikita katika kuimarisha sekta ya kilimo, kusaidia wajasiriamali pamona na makundi mbalimbali yakiwamo ya wanawake na vijana.
Sehemu ya Wadau waliohudhulia majadiliano hayo.

Upinzani Wapongeza Juhudi za Serikali Kukuza Uchumi

$
0
0
Na Jonas Kamaleki-MAELEZO, Dodoma
Mbunge wa Viti Maalum, Chama cha Wananchi (CUF), Mhe.Rukia Kassim amepongeza juhudi za Serikali katika kukuza uchumi ikiwemo kuongezeka kwa pato la Taifa.

Mhe. Rukia ameyasema hayo leo Bungeni, Jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2018/19.

“Naipongeza Serikali kwa hatua za kukuza uchumi  hasa ukuaji wa Pato la Taifa unaotarajiwa kuwa asilimia 7.2”, alisema Rukia.

Naye Mbunge wa Urambo, Mhe. Margreth Sitta ameipongeza Serikali kwa kupendekeza kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye taulo za kike.

“Mheshimiwa Spika hatua hii ya kusamehe kodi hiyo itapunguza bei ya taulo hizo ambayo itawafanya wanafunzi wa kike kuzipata kwa bei nafuu na kuwawezesha kuhudhuria masomo kwa muda wote wa masomo ikilinganishwa walivyokuwa wakishindwa kufanya hivyo wakiwa katika siku zao kwa kukosa taulo”,alisema Mama Sitta.

Akichangia kwenye bajeti kuu ya Serikali, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa anampongeza saa Rais John Pombe Magufuli kwa kujenga miradi mikubwa miwili ya Standard Gauge naye Umeme wa Stiegler’s Gorge.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (Mb), akizungumza wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 1 leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hawa Ghasia akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu Bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 11 leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akijibu swali wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 11 leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Missungwi mkoani Mwanza, Mhe. Charles Kitwanga akichangia hoja kuhusu taarifa ya hali ya uchumi na mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2018/19 wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 11 leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Singida, Martha Mlacha wakati wa kikao cha 52 cha Bunge la 11 leo tarehe 18 Juni, 2018 Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110004 articles
Browse latest View live


Latest Images