Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

SERIKALI MKOANI SIMIYU YAITAKA JAMII KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUPINGA MIMBA ZA UTOTONI

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Serikali Mkoani Simiyu imeitaka jamii kushiriki kikamilifu katika suala la kupinga mimba za utotoni ili kukabiliana na ongezeko la mimba lililofikia 195  kwa wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari katika kipindi cha miaka mitatu  mkoani humo.

 Wito  huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.  Benson Kilangi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa  wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Afrika, yaliyofanyika Kimkoa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nanga B wilayani humo na kuhudhuriwa na wananchi na wadau wa maendeleo lengo likiwa ni kuikumbusha jamii haki za Mtoto.


Kilangi amesema Serikali haitawafumbia macho wale wote watakaowapa mimba wanafunzi hivyo akawataka wananchi kuungana na Serikali katika kulaani na kufichua wale wote wanaojihusisha na suala hilo ambalo linasababisha watoto wa kike kukatisha masomo yao.

“ Mpaka kufikia  mwaka 2016/2017 watoto 195 kati yao 25  wa shule za msingi na sekondari 170 wamepata mimba ndani ya mkoa wetu, hili ni tatizo na sisi hatutamfumbia macho wala kumlea mtu yeyote atakayempa mimba mtoto wa shule, niwaombe wananchi wote muungane na Serikali kulaani kwa nguvu zote mimba kwa watoto wetu wa kike” alisisitiza Kilangi
 Wanafunzi  wa shule za Msingi za kata ya Chinamili wilayani Itilima Mkoani Simiyu wakipita na mabango yenye jumbe mbalimbali mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Kimkoa yaliyofanyika katika Viwanja vya shule ya msingi Nanga B wilayani humo. 
 Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.  Benson Kilangi (wa tatu kulia) na viongozi wengine wakipokea maandamano ya watoto(Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu) katika maadhimisho ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa wilayani Itilima katika viwanja vya Shule ya Msingi Nanga B.
 Kwaya ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Senani wilaya ya Itilima mkoani Simiyu wakitoa burudani ya wimbo katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Shule ya Msingi Nanga B wilayani humo.
 Mtoto Luhangija Maduhu kutoka Shule ya Msingi Nanga B wilayani Itilima akisoma risala mbele ya Mkuu wa Wilaya  hiyo, Mhe. Benson Kilangi (ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka )kwa niaba ya watoto wa Mkoa wa Simiyu, katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika kimkoa wilayani Itilima katika viwanja vya Shule ya Nanga B. 
Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Bw. Mariano Mwanyigu akitoa taarifa fupi kuhusu Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika, ambayo yamefanyika kimkoa wilayani humo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Nanga B. 


Introducing New Single from Balozi Dola "Kombora" (worlwide exclusive )

TCRA YAONGEZA MUDA WA USAJILI WA WATOA HUDUMA ZA MAUDHUI KWA NJIA YA MTANDAO

99 Names Of Allah by R.NAme

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 17, 2018

UNICEF Tanzania celebrates Father’s Day with renowned footballer, Ivo Mapunda

0
0
Former Taifa Stars goalkeeper calls upon fathers to play an effective role in parenting during their children’s early years.

UNICEF Tanzania celebrated Father’s Day with renowned footballer and former Taifa Stars goalkeeper, Ivo Mapunda, who called on fathers to step up their game in parenting, especially in the early years of their children’s lives.

UNICEF celebrity supporter and father-of-four, Mapunda, shared a video message for all Tanzanian fathers – urging them to be more involved in their children’s lives, especially in the early years.

Evidence suggests that when fathers bond with their babies from the beginning of life, they are more likely to play a more active role in their child’s development. Research also suggests that when children positively interact with their fathers, they have better psychological health, self-esteem and life-satisfaction in the long-term.

Advances in neuroscience have proven that when children spend their earliest years – particularly the first 1,000 days – in a nurturing and stimulating environment, new neural connections form at an optimal speed. These neural connections help determine a child’s cognitive ability, how they learn and think, their ability to deal with stress, and can even influence how much they will earn as adults.

“I read to my two-year-old every day, and encourage her to ask questions. And I play football with my older three on a daily basis. It’s our time to bond, and talk. On Father’s Day, I would like to encourage all dads to make sure they don’t miss out on this precious phase of their children’s lives. I am very happy to collaborate with UNICEF on this day,” said Mapunda. UNICEF is using Father’s Day to renew its call to break down cultural and financial barriers preventing fathers from spending quality time with their young children.


SERIKALI YAPIGA VITA AJIRA KWA WATOTO WILAYANI TARIME, YAHIMIZA KUWAPELEKA SHULE

0
0
Na Frankius Cleophacee Tarime.

Serikali imepiga vita suala la Ajira kwa watoto wadogo ikiwemo kufanya biashara ndogondogo kwa watoto hao, badala yake wapelekwe shuleni na kuahidi kuwachukulia hatua kali wazazi na walezi watakaokiuka.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashari ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo kiwilaya Wilaya ya Tarime Maadhimisho hayo yuamefanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Nyamongo katika Kata ya Matongo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Apoo Castro Tindwa amepiga vita suala la ajira kwa watoto hususani kufanya biashara ndogo katika Maeneo ya Stendi huku akipiga vita pia suala la Walimu Wa Shule za Sekondari na Msingi kufanya biashara katika Maeneo hayo.

Katika Maadhimisho hayo zimeweza kushiriki Tasisi mbalimbali Likiwemo Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime, ATFGM Masanga, Plan International,Muungano wa Jamii Tanzania MUJATA, Acacia North Mara pamoja na Viongozi wa Dini

Kambibi Kamugisha kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto na Valerian Mgani kutoka Shirika la ATFGM Masanga wanazidi kupaza sauti zao kwa jamii ili kutokomeza Suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike Wilayani Tarime huku wakiomba serikali Kuungana na Mashirika hayo kwa lengo la kupiga Vita suala la Ukeketaji kwa Mtoto wa kike.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Apoo Castro Tindwa akizungumza mbele ye Wananchi (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika,ndani ya viwanya vya shule ya sekondari Nyamongo wilayani Tarime .
Muwakilishi Kutoka Shirika la ATFGM Masanga,Valerian Mgani ambao wamekuwa wakipiga vita Ukatili katika jamii akiongea na Wananchi kwenye Maadhimisho hayo.
Muwakilishi Kutoka Shirika la Plan International , Shaban Shaban akizungumza mbele ya Wananchi katika Maadhimisho hayo.
Wanafunzi kutoka Shule za Msingi zinazozunguka Mgodi wa Uchimbaji wa Mawe ya Dhahabu ACACIA North Mara wakiwa katika Maadhimisho hayo ya Siku ya Mtoto wa Afrika,ndani ya viwanya vya shule ya sekondari Nyamongo wilayani Tarime .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TTCL CORPORATION YAENDELEZA UTARATIBU WAKE WAKUSAIDIA WAHITAJI

0
0
Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa Mamamlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwana, Saada Omar Ally (kushoto) kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada huo.


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, limetoa msaada wa vyakula na mahitaji muhimu kwa watoto waishio katika mazingira magumu ili kuwawezesha kufurahia Sikukuu ya Eid.

Msaada huo umetolewa kwa Vituo vya DMI kilichopo Kibamba Kibwegere chenye watoto 60 na Kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti chenye watoto 85 vyote vikiwa jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi misaada hiyo kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba, Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi amesema, Shirika lake linatekeleza kikamilifu wajibu wa Taasisi za Umma na Binafsi wa kutoa sehemu ya mapato yake kwa ajili ya ustawi wa Jamii na kuleta unafuu kwa maisha ya watu wanao wazunguka.

“Huu ni utaratibu wetu wa kila mara hali inaporuhusu, tunajitoa kwa ajili ya wahitaji na hasa watoto wa naoishi katika mazingira magumu ili kuwapa matumaini ya kujiendeleza ki-elimu na kujitegemea ili kuwa raia wema wasiku za baadae. Tuna waomba Watanzania watuunge mkono kwa kutumia huduma zetu ili kutupa nguvu ya kuendelea kusaidia jamii kwa matendo mema kama haya,” alisema Ndugu Thom Mushi.

Wakishukuru kwa misaada hiyo, Viongozi wa vituo vyote viwili wameiomba TTCL na Taasisi nyingine kuendelea kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu na hasa watoto wenye ndoto nyingi za kubadili hali zao za maisha na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi sehemu ya msaada mmoja wa watoto (kushoto) wa kituo cha DMI inachosimamiwa na Shirika la Mabinti Immakulata cha Kibamba, jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia), akikabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa Sista Makrina Kapinga (kushoto) mlezi wa Kituo cha watoto yatima cha DMI kinachosimamiwa na Shirika la Mabinti Immakulata cha Kibamba, jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa TTCL Tanzania, Ndugu Nicodemus Thom Mushi (kulia),
akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na mahitaji mengine kwa niaba ya Mkugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba kwa Mamamlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwana, Saada Omar Ally (kushoto) kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada huo.

TGNP MTANDAO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA NJIA HII

0
0
Watoto kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali mapema jana katika kilele cha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Elimu bure inatakiwa iende sambamba na huduma muhimu kwa watoto ikiwemo upatikanaji wa maji, vyoo vya kutosha, vyumba vya kujihifadhia watoto wa kike, Mabweni pamoja na chakula kwa wanafunzi wawapo mashuleni.

Hayo yamesemwa mapema jana jijjini Dar es salaam na Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Anna Sangai katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambapo yamekuwa yakifanyika kila mwaka ifikapo tarehe 16 mwezi juni.
Afisa Programu ya Harakati na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja wa TGNP Mtandao Anna Sangai akiongea na waandishi wa habari baada ya maandamano ya amani yaliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam.

Afisa huyo alisema kuwa lengo kuu la kukutana pamoja na watoto hao ni kutathmini sera na mipango ya nchi iliyowekwa katika kulinda, kutetea haki na maslahi ya mtoto kulingana na sharia na mikataba ya kimataifa ambayo taifa letu limeingia.

Aliendelea kusisitiza kuwa jambo hili liende sambamba na ulinzi wa watoto wawapo ndani na nje shule, lakini pia kuwalinda dhidi ya mila na desturi zinazowakandamiza watoto hasa wa kike kama vitendo vya ukeketaji, ndoa pamoja na mimba za utotoni.

Lakini pia katika kukuza na kuendeleza uchumi wa viwanda watoto wasiachwe nyuma kwani wao ndio wanaotarajiwa kuja kuviendesha viwanda hivyo tarajiwa katika nchi yetu kwa kuwakuza kwa elimu ya vitendo ikiwemo masomo kilimo.
Mwenyekiti wa vituo vya Taarifa na Maarifa Taifa Janeth Mawinza akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Mwananyamara jijini Dar es salaam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata Makumbusho Dada Janeth Mawinza alisema kuwa wameamua kufanya maadhimisho hayo katika eneno la Mwananyamara Kisiwani kutokana ni eneo ambalo waligundua matukio mengi ya ukatili wa watoto ikiwemo kupigwa kunakopitiliza pamoja na matukio ya watoto kuchomwa moto.

“Eneo la Mwananyamara Kisiwani lina watoto wengi sana waliofanyiwa ukatili na ndio maana tumekuja na ujumbe unaowataka wazazi na walezi kuacha vitendo hivyo mara moja, kwani mtoto ana haki zake na anastahili kulindwa na kuendelezwa ili aweze kufikia malengo yake”. Alisisitiza Dada Mawinza
Watoto kutoka kata mbalimbali wakiwa katika maandamano ya amani Siku ya Mtoto wa Afrika mapema jana jijini Dar es salaam.

KIVUKO KIPYA CHA MV. MWANZA CHASHUSHWA KWENYE MAJI TAYARI KWA MAJARIBIO

0
0
NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)

Wakazi wa jiji la Mwanza mapema leo wameshuhudia tukio la kushushwa kwenye maji kwa Kivuko kipya cha MV. Mwanza baada ya kufikia hatua za mwisho za kukamilika kwa ujenzi wake. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ametoa pongezi kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa kusimamia mradi huo kwa mafanikio makubwa. Aidha, ameipongeza Kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Boatyard Ltd ya jijini Mwanza kwa kujenga kivuko hicho kwa ubora wake.

Kaimu Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za vivuko kutoka TEMESA, Mhandisi Lukombe King’ombe ambaye alimuwakilisha Mtendaji Mkuu wa TEMESA alisema ni faraja kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza kupata kivuko kipya kwani kitapunguza adha ya foleni ndefu kwa watumiaji wa vivuko vinavyotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi. 

Mhandisi King’ombe aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kuhakikisha kuwa wakazi wa mkoa huo wanapata huduma ya usafiri yenye uhakika na kuwataka wakazi hao kukitunza kivuko hicho kitakapoanza kutoa huduma ya uvushaji wa abiria na magari. Alisema, hatua inayofuata baada ya kivuko hicho kushushwa kwenye maji ni ukamilishaji wa kazi chache zilizobaki na hatimaye kukifanyia majaribio ili kuhakikisha abiria na mali zao wanakuwa salama pindi watumiapo kivuko hicho.

Naye Meneja wa TEMESA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Alex William aliwaomba wakazi wa Mwanza kujivunia kivuko hicho kwa kuwa kimepewa jina la mkoa huo na hii ikiwa ni heshima kubwa kwa wakazi hao.Kivuko hicho cha tani 250 kina uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma kati ya Kigongo na Busisi mkoani Mwanza hivi karibuni.
Kivuko cha MV. Mwanza kikisubiri kutoswa kwa mara ya kwanza kwenye maji kufanyiwa ukaguzi wa mwisho, kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250. Kivuko hicho kitafanya idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vinne
Muonekano wa kivuko kipya cha MV. Mwanza mara baada ya kutoswa kwenye maji kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250 na kitafanya idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vinne.
Muonekano wa Kivuko cha MV MWANZA mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.
Kaimu Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuhudia kutoswa kwenye maji kwa kivuko cha MV.Mwanza ambacho kitakua kikitoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza, kivuko hicho kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushuhudia kutoswa kwenye maji kwa kivuko cha MV.Mwanza ambacho kitakua kikitoa huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza, kivuko hicho kitakua na uwezo wa kubeba abiria 1000 na magari 36 sawa na tani 250.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO

KIBITI YATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI KWA KUUZA UFUTA KWA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI KWA MKOA WA PWANI

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii, Kibiti
Ufuta ni miongoni mwa mazao ya biashara katika Mkoa wa Pwani ambapo wakulima wamekuwa wanauza kwa wachuuzi na kufanya zao hilo kudumaa kutokana na kuuza kwa bei ya chini.

Wilaya ya Kibiti imekuwa ya kwanza kwa Wilaya za Mkoa wa Pwani kuuza zao la Ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibiti,  Alvera Ndabagoye amesema kuwa kutokana  na zao hilo kuwa na soko kwa  ndani na nje serikali imeagiza zao hilo kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuweza kuwanufaisha wakulima wa zao hilo ikiwa ni pamoja na serikali kupata mapato ya uhakika ambapo Kibiti imeweza kufanikiwa kuuza ufuta kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.

Amesema kuwa mara tu baada ya kupata maagizo waliweza kutekeleza na kuweza kufanya minada miwili kwa bei ya sh.2700 kwa kilo moja na kuwa  tofauti na bei ya wachuuzi ambao walikuwa wakinunua kwa sh.1200 kwa kilo.

Ndabagoye amesema kuwa mfumo wa stakabadhi ghalani wametumia ule wa korosho kupitia vyama vya Ushirika ikiwa ni kuhamasisha wananchi kuuza katika mfumo huo.

Amesema kuwa zao hilo lilikuwa likilimwa na wakulima wachache kutokana na baadhi ya wakulima kukata tamaa kwa bei waliokuwa wakiuza ya hasara 

Aidha  Ndabagoye amesema kuwa ni ya serikali ni kuwanyanyua wakulima wasipate hasara na kuamua kuja na mfumo wa sitakabadhi ghalani katika mazao ya Ufuta , Pamba pamoja na kahawa.

Amesema kuwa wemekamata  magari   nane aina ya Fuso yakiwa  na ufuta kutoka wilaya ya jirani wakazikamata Kibiti na kukagua na kubaini wenye ufuta katika magari hayo hawana nyaraka hali ambayo inawapa shaka kuwa baadhi ya wakulima wamezunguka na kwenda kuuza katika wilaya ambayo inapakana nayo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibiti,  Alvera Ndabagoye akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zao la Ufuta na  hatua walizozichukua baada ya serikali kuagiza uzwaji mazao ya Korosho, Kahawa na Ufuta kuuza kwa mfumo wa stakabadhi ghalani katika wilaya ya Kibiti mkoaani Pwani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kibiti,  Alvera Ndabagoye akionesha zao la Ufuta kwa waandishi habari
 Afisa Kilimo wa Wilaya ya Bwenda  Bahinda akionesha zao la Ufuta na jinsi linavyoandaliwa kwa ajili ya soko
Sehemu ya magari walioyakamata yakiwa na ufuta na hakuna nyaraka

CHADEMA YAWAVUA UWANACHAMA VIONGOZI WAKE TARIME,WAPOTEZA SIFA YA KUWA VIONGOZI

0
0


Na Frankius Cleophace Tarime.

Viongozi watatu Wanaotokan ana Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyamwaga Wilayani Tarime Mkoani Mara wamevuliwa wanachama na kupoteza sifa ya kuwa Viongozi kwa kukiuka Maadili ya uongozi pamoja na Katiba za Chama chao.

Mkutano Mkuu wa CHADEMA Kata ya Nyamwaga umewavua uanachama Viongozi hao akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Nyamwaga Getende Sagirai, Mjumbe wa Serikai ya Kijiji Koroso Sasi na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mchanchara Mniko Chacha

Lukas Ngoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Tarime Mkoani Mara akiongea na Waandishi wa habari amesema kuwa Mkutano Mkuu wa Chama ulioshirikisha Viongozi wa Wilaya umewasimamisha Viongozi hao kwa tuhuma mbalimbali.

Ngoto amesema kuwa Mwenyekiti wa serikalia ya Kijiji cha Nyamwaga natuhumiwa kwa kutumia vibaya madaraka yake huku baadhi ya Fedha zinazotokana na Mnara pamoja na Maji hazijulikani zimeenda wapi

Pia Ngoto ameongeza kuwa Mwenyekiti huyo amekuwa akikashifu chama hicho katika Vijiwe suala ambalo ni kukiuka kanuni ya Chama hicho.

“Sasa viongozi hawa watatu wamevuliwa uanachama na watapoteza sifa ya kuwa viongozi na tayari tumewateua baadhi ya vuongozi wa Muda wakati huo tukisubiri kufanya uchaguzi wa kuziba pengo na tunaenda kuandika barua kwa ajili ya kutaarifa Maofisa watendaji wa kata ili wasiwatambue” alisema Ngoto.

Jitiada za Kumtafuta Mwenyekiti huyo ili kuongelea juu ya kuvuliwa wanahama zimegonga Mwamba baada ya Simu yake ya Mkononi kuita bila kupokelewa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Lukas Ngoto akiongea na Waandishi wa habari kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Viongozi hao.

WAZIRI JAFO ATOA AGIZO KWA WAKUU WA MIKOA WOTE NCHINI

0
0
Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo ametoa muda wa miezi miwili kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini kuanza kusimamia ujenzi wa miundombinu ya shule katika Mikoa yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, Mhe. Jafo amesema miundombunu hiyo itahusisha ujenzi wa vyumba vya Madarasa 478 na mabweni 269 ambapo kila bweni moja litachukua wanafunzi 80.

Mhe. Jafo alisema kuwa ni wajibu wa kila Mkuu wa Mkoa kusimamia kusimamia kwa dhati kazi ya ujenzi wa miundombinu ya Madarasa na Mabweni na kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali zinaendana na majengo yatakayojengwa kama walivyokuwa wakifanya katika miradi ya afya na Elimu.

Aliendelea kusema kuwa Serikali imeweza kuchagua shule 119 ambazo orodha itatolewa wakuu wa Mikoa hiyo wahakikishe wanasimamia kwa haraka zoezi la kubaini maeneo ya yatakapojengwa madarasa na mabweni, pia kusimamia uteuzi wa Kamati za Ujenzi na kuanza mchakato wa kuwatafuta wajenzi wa majengo hayo.

Alisema kuwa Serikali itatoa fedha kukamilisha haraka ujenzi wa miundombinu ya mabweni 269 na madarasa 478 kwa ajili ya wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano kwa kipindi hiki na kuagiza fedha hizo zikasimamiwe kwa weledi.

Mhe Jafo alisema ujenzi wa miundombinu hiyo utatumika kwa njia ya “Force Accont” utaratibu unaotumika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na ambao umetuika katika ujenzi wa shule na vituo vya afya Nchini.Aliwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Halmashauri zao kazi ya Ujenzi wa Miundombinu ya Shule inaenda kufanyika kusimamia kwa nguvu mchakato wa kutafuta mafundi wa ujenzi wa majengo na kuhakikisha wanapatikana haraka ili kazi ianze mara moja baada ya kubainisha maeneo.

Aliwataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wamekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni ifikapo tarehe 30/8/2018 ili kuhakikisha wanafunzi walio na sifa ya kujiunga na kidato cha Tano watapata fursa ya kujiunga na kidato cha tano.Wakati huohuo aliwaagiza Wakurugenzi ambao watasuasua katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa na mabwebi pamoja na miradi mingine hatasita kuwachukulia hatua na kuwataka watakapopata fedha wahakikishe kazi hiyo inakamilika mapema.

“Niwatake Wakurugenzi ambao wanatabia ya kusuasua utekelezaji wa mradi mbalimbali kuacha mara moja na katika jambo hili sihitaji masiahara hata kidogo, Mamlaka za Serikali za Mitaa itakapo pokea fedha ihakikishe inakamilisha ujenzi huo haraka.” Alisema Jafo.Aliendelea kusema kuwa Serikali haiwezi kukubali kuona watoto wa maskini wanakosa nafasi ya kujiunga na kidato cha Tano wakati wanasifa, hivyo amewataka nawata Wakuu wa Mikoa kusimamia kazi hiyo haraka kwa lengo la watanzania kuweza kupata fursa ya elimu katika nchi yao.

Aidha alisema Serikali imetenga shilingi bilioni 29 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha vijana wa Tanzania wanapata Elimu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea na Waandishi wa Habari wakati akitoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa wote nchini kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa na Mabweni leo ofisini kwake, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo wakati akitoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa wote nchini kuhusu ujenzi wa vyumba vya madarasa na Mabweni leo Ofisini kwa Jijini Dodoma.

WAHAMIAJI HARAMU SITA WAKAMATWA PWANI

0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

JESHI la polisi mkoa wa Pwani, limewakamata wahamiaji haramu sita ,raia wa nchi ya Ethiopia na Somalia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Aidha mkoa huo umemaliza kusheherekea sikukuu ya Eid Ul Fitr kwa salama na utulivu kwani hakukuwa na tukio lolote la uvunjifu wa amani.

Kamanda wa polisi mkoani humo (ACP) Jonathan Shanna ,alithibitisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao ambao wamekamatwa maeneo ya Msalabani kata ya Dunda wilayani Bagamoyo .

"Katika misako inayoendelea tumefanikiwa kuwakamata raia hao usiku wa kuamkia leo ambao wameingia nchini kinyume na sheria na taratibu zinazotakiwa " alifafanua kamanda Shanna.

Kamanda Shanna aliwataja wahamiaji haramu waliokamatwa kuwa ni Ahamed Mohamed (26) ,Mahad Ahmad (14) ,Abshir Aboulah wote raia wa Somalia .Wengine ni Beyene Abute (25),Abete Eramo (23), Abraham Adoise (24) wote raia wa Ethiopia.

Kwa mujibu wa kamanda huyo alisema ,watuhumiwa wote watawakabidhi idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.Akizungumzia juu ya kumaliza kwa amani sherehe za Eid Ul Fitr alibainisha mkoa huo hauna tukio lolote la uvunjifu wa amani lililojitokeza .

Kamanda Shanna alisema ,licha ya kumaliza salama sikukuu hiyo ,wanaendelea na misako na doria mbalimbali katika mkoa huo ambayo ni endelevu.

TCRA YATOA UFAFANUZI KUHUSU USAJILI WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII.


'BAKWATA HAITAKUBALI KUONEWA NA WATU WACHACHE,TUMEDHAMIRIA KUREJESHA MALI ZA WAISLAMU'

0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema halitakubali kuonewa na watu wachache na limedhamiria kurejesha mali za Waislamu zilizohodhiwa kwa maslahi ya wachache.

Pia limesema waumini wa dini Kiislamu wameridhia kuwa chini ya kiongozi mmoja Sheikh Mkuu wa Tanzania na kuwataka wengine wote kufuata Katiba ya BAKWATA ili kuepusha vurugu.

Kauli hiyo ilitolewa ja juzi jijini Mwanza kwenye Baraza la Idd El Fitri na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Taifa Sheikh Hassan Kabeke ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuendeleza Quraan na Suna Tanzania (JUQUSUTA).

Alisema BAKWATA hitakubali kuporwa mali za Waislamu na kuwanufaisha wachache ambao wamelifanya baraza hilo kuwa ombaomba wakati lina mtandao mkubwa kuliko taasisi nyingi za dini nchini kwa kuwa lina mtandao wa uongozi hadi vijijini.

Sheikh Kabeke alisema kuwa wamejipanga kurejesha mali za waislamu na kuwataka waumini na viongozi wa dini hiyo kuwa imara na wahakikishe mali zote za Waislamu zinarudishwa lakini wakilegea zote zitakwisha.“Tunataka BAKWATA yenye nguvu itakayopambana na watu wanaopuuza maelekezo ya baraza hilo na hatuna sababu ya kuwa ombaomba wakati tumeweka mizizi hadi vijijini, isipokuwa tunazidiwa na CCM tu.
Sheikh Hassan Kabeke akizungumza kwenye Baraza la Idd jijini Mwanza ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Makutano wa New Mwanza Hotel juzi.Picha na Baltazar Mashaka.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Bima ya afya na eneo la kutosha, changamoto kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga

0
0
Na Jumia Food Tanzania

Kikiwa kimeanzishwa takribani miaka 10 iliyopita, kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam kinakumbwa na changamoto kadhaa zikiwemo eneo la kutosha kuwalea na kuwahifadhi watoto pamoja na bima ya afya.
Kituo hiki ambacho mpaka hivi sasa kina jumla ya watoto 48 wakiwemo wavulana 26 huku 22 ni wasichana. Watoto hao wanaolelewa na Bi. Zainab Bakari ambaye ndiye mwanzilishi na mlezi wa watoto hao, anawahudumia kwa mahitaji yao yote muhimu yakiwemo malazi, chakula, mavazi, shule, afya na mengineyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile serikali, sekta na watu binafsi kupitia misaada inayopelekwa kituoni hapo.

Akizungumza wakati akipokea msaada wa chakula na mahitaji ya shule kutoka kampuni ya Jumia Food, Bi. Bakari ameelezea kuwa watoto wanazidi kuongezeka kituoni kwake hali inayopelekea kuwa ni changamoto kuwahifadhi na kuwalea katika eneo moja kama inavyotakiwa.
“Kituo hiki nilikianzisha takribani miaka 10 iliyopita nikiwa na watoto wachache hapa kwenye hii nyumba yetu. Na kwa kipindi chote hiko nimekuwa nikipokea watoto na kuwalea hapahapa. Hivyo, kadri miaka inavyozidi kwenda ndivyo ninavyozidi kupokea watoto, wakizidi kukua na mahitaji kuongezeka.

 Hali hiyo imepelekea suala la kuwalea wote kwa pamoja kuwa ni changamoto kwasababu kituo hiki hakina uzio na kimezungukwa na nyumba za watu wengine,” alielezea Mwanzilishi na Mlezi wa Kituo cha Maunga.

Jumia Food, kampuni inayojihusisha na huduma ya chakula kwa njia ya mtandao ilikuwa ikiendesha kampeni iliyokwenda kwa jina la “STAND BY ME” katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kampeni hii iliwashirikisha wateja wake kwa kuwataka kuagiza chakula kwa kutumia nenosiri ‘ASANTE’ ili kuchangia mahitaji ya chakula kituoni hapo.

KIVUKO KIPYA CHA MV MWANZA TAYARI KUANZA KAZI

Wasichana 40 Tarime wapewa Elimu ya kupinga Ukeketaji.

0
0
Na Frankius Cleophace Tarime.

Wasichana 40 kutoka katika kata tofauti Wilayani Tarime Mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya uelimishaji rika katika Maeneo wanayotoka kwa lengo la kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto zake ikiwemo kupata Elimu.

Sarah Bedah ni Afisa Mawasiliano kutoka Shirika la Msihana Initiative lililopo Jijini Dar Es Salaam, amesema kuwa wao kama Shirika kwa kushirikiana na Shirila la ATFGM Masanga lililopo Tarime wameamua kutoa Elimu hiyo kwa lengo la kuwajengea Uwezo wasichana hao ili kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha Elimu ya kupinga Ukeketaji kwa Mtoto wa Kike.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ATFGM Masanga Sister Stella Mgaya amesema kuwa wao kama shirika wameamua kutoa Pia Mafunzo hayo kwa wasichana ambao wamekeketwa tayari na ambao hawajakeketwa ili kuzidi kuwaelimisha Wasicha ambao hawajakeketwa ili wasikeketwe.

Pia Mgaya ameongeza kuwa licha ya kutoa Elimukwa Wasichana hao bado wanazunguka na wazee wa Mila Muungano wa Koo12 kwa lengo la kutoa Elimu kwa jamii ili kuondoa Ukeketaji ikiwa ni pamoja na Kupiga Vita Miiko ambayo inakandamiza Mtoto wa kike ambaye hajakeketwa ili asitengwe Kwenye Jamii.

Aidha Washiriki wa Semina hiyo ya Siku mbili wamesema kuwa Elimu watakayopewa itakuwa chachu kwao na kuitumia Vyema kwa lengo la kukomboa Mtoto wa Kike Wilayani Tarime Mkoani Mara.

Naye Mratibu wa Huduma ya Afya ambaye pia ni Mwezeshaji katika Mafunzo hayo Abel Gichaine amesema kuwa baada ya kutoa Elimu kwa jamii endepo itakiuka lazima Sheria itumike ili kuwatia hatiani wale ambao watakao keketa Msichana kwani Mwaka huu unaogawanyika Kwa Mbili wenda koo Nyingi za kabila la Wakurya Wilayani Tarime zikakeketa ili kutimiza Mila zao.

Meneja Miradi Shirika la ATFGM Masanga Tarime ambao wanapiga Vita Ukatili wa kijinsia akitoa Somo kwa Mabinti hao ambao baadhi yao wamekeketwa na kuolewa katika Umri Mdogo wakipewa Elimu ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuopiga Vita Ukaili Maeneoo wanayotoka.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 18, 2018

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images