Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA JAMII KUCHANGIA DAMU

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
SERIKALI mkoani Mwanza imezindua klabu ya wachangiaji damu wa kundi maalumu (RH Nagative) na kuahidi kuendelea kuhamasisha jamii iweze kuchangia damu itakayosaidia kuokoa maisha ya watu na kuipongeza Taasisi ya The Desk & Chair Foundation kwa mchango wake wa kujitoa kuhamasisha jamii kuchangia damu.

Klabu hiyo ilizinduliwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wachangiaji Damu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.

Akizungumza baada ya kuzindua klabu hiyo Mongela alisema uhaba wa damu ni changamoto kubwa kwa Mkoa wa Mwanza ambapo mahitaji yake ya damu ni chupa 30,000 na hivyo jamii isisubiri hadi iuguliwe ndugu ndipo ichangie damu.

“Wachangiaji damu waenzie lakini niwapongeze The Desk & Chair Foundation, wamejitoa sana mkoani kwetu na taifa kwa ujumla lakini pia wanafunzi wamekuwa msaada mkubwa kwa kubeba jukumu la kukusanya damu.Hivyo kwa uhaba wa damu mkoani kwetu kila mmoja atambue umuhimu wa kuchangia damu ili wagonjwa waongezwe damu iliyo salama,”alisema Mongela.
 Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary tesha aliyemwalikisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza na wadau wa damu kwenye maadhimisho ya siku ya Wachangiaji Damu jijini humo.
 Mfadhili Mkuu wa Kituo cha Damu Salama Kanda ya Ziwa, Mwenyekiti wa Desk & Chair Foundation akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wachangiaji Damu Duniani iliyofanyika jijini Mwanza kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou Toure.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akichangia damu wakati wa maadhimisho ya Siku ya wachangiaji Damu Duniani wakati wa maadhimisho hayo jana yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure ya Mkoa wa Mwanza, Tesha alimwakilisha Mkuu wa Mkoa John Mongela ambaye alijuwa mgeni rasmi.

 Wadau wa damu wakichangia damu kwenye maadhimisho ya Siku ya wachangiaji Damu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya sekou Toure. Picha zote na Baltazar Mashaka

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AKABIDHI ZAWADI MASHINDANO YA MASAUNI-JAZEERA VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
 Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James (wapili kulia), Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassoro Salim Jazeera (wakwanza kulia) na Mbunge wa jimbo hilo wakiwakabidhi kombe wachezaji wa timu ya Miembeni baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa fainali ya Mashindano ya Masauni-Jazeera kwa kuifunga timu ya Kilimani bao 1-0.Mchezo huo umefanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Kikwajuni visiwani Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM), Kheri James  (kulia),akimkabidhi nahodha wa timu ya Kilimani, zawadi ya mipira baada ya kuibuka washindi wa pili  katika mchezo wa fainali ya Mashindano ya Masauni-Jazeera .Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni. Mchezo huo umefanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Kikwajuni visiwani Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM), Kheri James, akionyesha fedha  kabla ya kuwakabidhi washindi wa Fainali ya Mashindano ya Masauni-Jazeera ambapo timu ya Miembeni iliibuka na ushindi wa bao 1-0.Wakwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Nassoro Salim Jazeera na watatu ni Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni. Mchezo huo umefanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Kikwajuni visiwani Zanzibar.
 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wachezaji na mashabiki waliofika kushuhudia mchezo wa fainali ya Mashindano ya Masauni- Jazeera uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Kikwajuni Visiwani Zanzibar, ambapo timu ya Miembeni walibuka mabingwa baada ya kuifunga timu ya Kilimani bao 1-0.
 Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar, Dk. Abdulla Juma Saadalla, akizungumza na wachezaji na mashabiki waliofika kushuhudia mchezo wa fainali ya Mashindano ya Masauni- Jazeera uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Kikwajuni Visiwani Zanzibar, ambapo timu ya Miembeni walibuka mabingwa baada ya kuifunga timu ya Kilimani bao 1-0.Wengine meza kuu ni Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM), Kheri James na Mbunge wa Jimbo la Kiwajuni,Mhandisi Hamad Masauni.  
Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James(kulia) na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mhandisi Hamad Masauni, wakiteta jambo wakati wa fainali ya Mashindano ya Masauni- Jazeera iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

TAARIFA YA TUKIO LA MOTO KARIAKOO

VOA SWAHILI: Duniani Leo Mei 15, 2018

MZEE MWINYI AHIMIZA UMOJA, MSHIKAMANO NA KUVUMILIANA

$
0
0


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

*Asisitiza umuhimu wa kumuombea Rais Magufuli ili atekeleze yale anayoyafanya kwa maslahi ya Taifa

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesisitiza umuhimu wa Watanzania kudumisha umoja, amani na mshikamano huku akitoa rai ya kuendelea kumuombea Rais Dk. John Magufuli ili aendelee kulitumikia Taifa. 

Alhaj Mwinyi ametoa kauli hiyo leo mbele ya mamia ya waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kumalizika kwa ibada ya swala ya Eid ambayo kitaifa ilifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dr es Salaam. "Niwaombe ndugu zangu na watanzania wote tuendelee kudumisha umoja na mshikamano.

"Tuvumiliane kwa kila jambo na kubwa zaidi tuhakikishe tunaendelea kuitunza amani yetu ili tubaki kuwa salama,"amesema Alhaj Mwinyi. Aidha amewaomba Watanzania kuhakikisha wanaendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli ili aendelee kuwatumikia Watanzania hasa katika kuleta maendeleo. Amefafanua kuna mambo ambayo Rais Magufuli amekuwa akiyafanya kwa maslahi ya chini, hivyo ni kujukumu la kila mwananchi kuombea mwa Mwenyezi Mungu aendelee kuyafanikisha yote aliyoyaanzisha. 

Awali Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza na waumini waliokuwa kwenye viwanja hivyo amehimiza waumini wa dini ya Kiislamu kuzingatia mafunzo ambayo wameyapata wakati wa mfungo wa Ramadhan. Pia amehimiza Watanzania kuendelea kudumisha umoja na mshikamano huku akielezea umuhimu wa kushirikiana.

Ametumia nafasi hiyo kuzungumzia Hijja ambapo amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)limeanza kupokea waumini wa dini ya Kiislamu ambao wanataka kwenda Hijja mwaka huu. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein ahutubia Baraza la IDD-EL-FITRI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  na Waziri wa Katiba,Sheria.Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman (katikati) wakifuatana mara alipowasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, leo akihudhuria katika Baraza la  IDD-EL-FITRI lililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya IDD baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud na Kamishana wa Polisi Zanzibar (CP) Mohamed Hassani Haji
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (mbele) akipokea salamu ya Heshma ya Gwaride la Kikosi cha Polisi FFU leo mara alipowasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, katika Baraza la  IDD-EL-FITRI   lililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya Eid baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Askari wa Kikosi cha Polisi (FFU) wakitoa salamu ya Heshma kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipowasili katika Viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar, katika Baraza la  IDD-EL-FITRI  lililofanyika leo  katika kusheherekea Sikukuu ya Eid baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
 Sehemu ya Viongozi na Wananchi wakiwa katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar katika Sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI lililofanyika  katika kusheherekea Sikukuu ya Idd baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan  lililofanyika leo Mgeni rasmi akiwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiwahutubia  viongozi,Mabalozi,Wananchi na Waislamu mbali mbali katika sherehe za Baraza la  IDD-EL-FITRI  baada ya kumalizika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan,zilizofanyika leo katika  Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar. 


MICHEZO YA PIKIPIKI YAWA KIVUTIO TAMASHA LA SPORT MUSIC FESTIVAL KANDA YA ZIWA

$
0
0
Na Agnes Francis,Glob ya jamii
WAKAZI wa Kanda ya Ziwa wamejikuta wakishuhudia burudani ya aina yake kutokana na kushuhudia mchezo wa mashindano ya pikipiki. 

Burudani hiyo ya aina yake ambayo ni sehemu ya kusheherekea Sikukuu ya Eid imeandaliwa na Tamasha la Sport Music Festival.

Hivyo kwa leo tamasha hilo kinaendelea kufanyika katika Mkoa wa Geita wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Eid.

Wananchi wa Mkoa huo tangu mapema wamejitokeza kwenye tamasha hilo na mchezo wa pikipiki ilikuwa kivutio kikubwa kutokana na umahiri waliokuwa wanaendesha pikipiki hizo. 

Wengi wao waliwathibitishia wakazi waliofika kwenye tamasha hilo kuwa wanajua vema kuchezea pikipiki hali iliyosababisha kuibua shangwe.

Baada ya michezo ya pikipiki usiku huu wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaaanda kupanda jukwaani kutoa burudani kwa mashabiki wa muziki huo. 

Ambapo pia   wasanii wa kizazi kipya watakuwepo kutoa katika  kuendeleza sherehe hizo.
 Wakati wa kusherekea sikukuu ya Idd kwa wakazi wa Geita walishuhudia michezo ya pikipiki iliyokuwa ikitoa burudani uwanjani hapo.

 Mmoja wa vijana akionesha umahili wa kuchezesha baiskeli wakati wa sherehe za Idd zilizofanyika Geita
 Baadhi ya wananchi wa Geita wakifuatilia burudani  ya baiskeli, pikipiki na magari  ikiwa ni sehemu ya kusheherekea Sikukuu ya Eid imeandaliwa na Tamasha la Sport Music Festiva

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 16, 2018


TANZIA: RAIS WA TCCIA NDIBALEMA JOHN MAYANJA AFARIKI DUNIA

DK. MNDOLWA AMALIZA ZIARA YAKE KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA NA MKOA WA SINGIDA

$
0
0

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Edmund Mndolwa akipata maelezo kuhusu eneo lenye madini la Jumuiya hiyo lililopo katika Kijiji cha Bigigi, alipokagua eneo hilo akiwa katika ziara ya kikazo mkoani Singida, jana. Anayempa maelezo ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Singida Mjini Ali Balo (Wapili kushoto) na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kati Sosthenes Masola. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa NEC- CCM Christina Joramu na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa upande wa Zanzibar Haidar Haji abdallah. Dk. Mndolwa ameagiza uongozi wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Singida kuharakisha kulitafutia leseni na kuliwekea vigingi vya mipaka eneo hilo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Singida, kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, jana. 
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Singida Mashigani Kija akisoma taarifa ya jumuiya hiyo mbele ya Dk. Mndolwa
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Dk. Edmund Mndolwa akipata maelezo kuhusu eneo lenye madini la Jumuiya hiyo lililopo katika Kijiji cha Bigigi, alipokagua eneo hilo akiwa katika ziara ya kikazo mkoani Singida, jana. Anayempa maelezo ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Singida Mjini Ali Balo.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

TRA YATAIFISHA BOKSI 41 ZA MVINYO NA POMBE KALI DODOMA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dodoma

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata na kutaifisha boksi 41 za mvinyo na pombe kali zilizokutwa katika duka la jumla jijini Dodoma zikiwa hazina Stempu za Kodi.

Boksi hizo zenye thamani ya shilingi milioni tatu ambazo ni mali ya Anthony George, zimekamatwa na kutaifishwa leo wakati Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere akikagua matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) Jijini hapa kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.Akizungumza mara baada ya kutaifisha boksi hizo, Kichere amesema kuwa, ni wajibu wa muuzaji kuhakikisha kwamba, vinjwaji vinavyostahili kuwekewa Stempu za Kodi vinakuwa na stempu hizo ili kuisaidia Mamlaka kutoza kodi stahiki.

"Inatakiwa Stempu za Kodi ziwekwe kwenye mzigo kabla mzigo huo haujanunuliwa na wauzaji wa rejareja. Hii itaisaidia TRA kukusanya kodi halali na hatimaye kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali," alisema Kichere.Mvinyo na pombe kali zilizokamatwa na kutaifishwa ni pamoja na boksi 27 za Robertson, boksi 7 za Jameson, boksi 5 za Drostdy Hof na boksi 2 za Alko Dompo.

Wakati huo huo, Kamishna Mkuu Kichere amemkamata Dereva wa Bodaboda Issa Athumani na kumtoza faini ya shilingi 30,000 baada ya kununua mafuta ya bodaboda hiyo bila kudai wala kuchukua Risiti ya Kielektroniki ya EFD.Kichere ameeleza kuwa, wananchi ambao hawadai risiti wanatakiwa kutozwa faini ya shilingi 30,000 hadi 1,500,00 au kuhukumiwa kifungo kisichozidi miezi sita kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015.

"Kuna watu ambao hawadai risiti na kuna mwingine nimemkamata leo ambaye nimemtoza faini ya shilingi 30,000 ili iwe fundisho kwa watu wote wanaonunua bidhaa na huduma mbalimbali bila kudai wala kuchukua risiti", aliongeza Kichere.Aidha, Kamishna Mkuu Kichere ametoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kutoa risiti kila wanapofanya mauzo na wananchi kuhakikisha wanadai risiti kila wanapofanya manunuzi mbalimbali.

"Natoa wito kwa wafanyabiashara wote waendelee kutoa risti lakini pia wanunuaji wadai na kuchukua risiti. Tunataka kujenga utamaduni wa kutoa na kudai risiti ili tuweze kukusanya kodi stahiki," alisema Kichere.Naye, Mfanyabiashara wa mafuta jijini hapa Faustine Mwakalinga amemshukuru Kamishna Mkuu wa TRA kwa kutembelea kituo chake cha mafuta na kusema kuwa, zoezi hilo analolifanya litaongeza mapato ya Serikali kwasababu linajenga ukaribu na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.

"Namshukuru sana Kamishna Mkuu wa TRA kwa kutembelea kituo changu cha mafuta na nimefurahishwa sana na jinsi anavyofanya kazi yake ukizingatia leo ni sikukuu. Ukaguzi huu anaoufanya Kamishna Mkuu, utasaidia kuongeza mapato ya Serikali na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili sisi wafanyabiashara," alifafanua Mwakalinga.

Kamishna Mkuu Kichere ametembelea jumla ya Vituo vya Mafuta vinane na maduka 15 ikiwa ni moja ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni Dodoma hivi karibuni.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akifungua boksi katika duka la jumla Jijini Dodoma kuangalia kama vinywaji vilivyomo kwenye boksi hilo vina Stepu za Kodi wakati akifanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akiangalia chupa ya pombe kali aina ya Jameson katika duka la jumla Jijini Dodoma kuangalia kama chupa hiyo ina Stepu ya Kodi wakati akifanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza na Dereva wa Bodaboda Issa Athumani ambaye amekamatwa na Kamishna huyo na kumtoza faini ya shilingi 30,000 kwa kosa la kununua mafuta bila kudai wala kuchukua risiti Jijini Dodoma wakati akifanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akiangalia risiti ya kielektroniki ya EFD wakati akifanya ukaguzi wa matumizi ya Mashine za Kielektroniki za Kutolea Risiti (EFDs) kwenye maduka na vituo mbalimbali vya mafuta Jijini Dodoma. Mwenye Kanzu nyeupe ni Msimamizi wa Kituo cha Mafuta cha Camel Oil kilichopo maeneno ya Kisasa. (PICHA NA TRA).

WAFANYAKAZI TPA TANGA WATOA MSAADA WA SIKUKUU YA IDDI KWA KAMBI YA WAZEE MWANZANGE

$
0
0
Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani y ash.milioni 1.5kwa kituo cha wazee wasiojiweza kilichopo eneo la Mwanzange Jijini Tanga.

Msaada wa vitu hivyo ni vyakula mbalimbali ambavyo vitatumika kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitri ambapo halfa ya makabidhiano ilifanyika juzi kwenye kambi hiyo. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo,Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Bandari ya Tanga Hassan Senkole alisema waliona ni busara kupunguza sehemu ya mapato yao katika mwezi mtukufu wa ramadhani kuwasaidia wazee hao. 

Alisema waliamua kutoa msaada huo ili kuwa sehemu ya jamii iliyowasaidia wazee hao katika sikukuu ya Eid EL Fitri ili nao waweze kusheherekea sikukuu hiyo bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ile.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga Ally Senkole kulia akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha kulea wazee wasiojiweza cha Mwanzange Jijini Tanga ambapo walikabidhi vitu vyenye thamani ya sh.milioni 1.5
 Sehemu ya watumishi wa Bandari ya Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na wazee hao mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri
 Sehemu ya watumishi wa Bandari ya Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na vitu mbalimbali walivyonunua kabla ya kuwakabidhi wazee hao
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga Ally Senkole akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vitu hivyo
sehemu ya vitu ambavyo vilikabidhiwa

TFDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE ZAIDI YA 3000 KIDATO CHA NNE WALIOPIGA KAMBI ZA KITAALUMA SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetoa msaada wa taulo za kike katoni 210 zenye thamani ya shilingi milioni tano na kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaalum mkoani humo, ambao wanajiandaa na mtihani wa Taifa kwa mwaka 2018.

Akizungumza na viongozi, walimu na wanafunzi wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Bariadi Mjini Bariadi, Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa, Bw. Moses Mbambe amesema msaada huo umetolewa kujibu ombi la Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alilolitoa kwa Mamlaka hiyo kuwasaidia watoto wa kike wa kidato cha nne walio kwenye kambi ya Kitaalum mkoani humo ili wawapo kambini wasome kwa utulivu na kujiamini hususani wakati wa hedhi.

“Tunakabidhi taulo hizi za kike kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TFDA, Bi. Agnes Sitta Kijo ambazo Mkuu Mkoa wa Simiyu alimuomba ili ziweze kuwasaidia watoto wa kike wa kidato cha nne walioko kwenye kambi za kitaaluma katika maeneo mabalimbali hapa mkoani katika kuwawekea mazingira mazuri ya kusoma kuwa utulivu na kujiamini wakati wa siku zao za hedhi” alisema

Aidha, Mbambe ameupongeza uongozi wa Mkoa kwa kuanzisha utaratibu wa kambi za kitaaluma na akawataka wanafunzi kuwa na ndoto, kusoma kwa bidii na kuweka mikakati ya kuwawezesha kufikia ndoto zao; huku akiwaasa kufanya vizuri katika mitihani yao ili kutoa nafasi kwa walio nyuma yao kuwekewa utaratibu endelevu wa kambi za kitaaluma katika kuuwezesha mkoa huo kufanya vizuri kielimu.
Kutoka kulia Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe na Meneja Mawasiliano wa TFDA Guadencia Simwanza wakimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka taulo za kike zilizotolewa Mamlaka hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa kidato cha nne zaidi ya 3000 walio katika kambi za kitaaluma mkoani humo, kushoto ni baadhi ya wananfunzi hao wakipokea kwa niaba ya wenzao, katika Shue ya Sekondari Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa saba kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kike walio katika Kambi ya kitaaluma Shule ya Sekondari Bariadi baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za Kitaaluma ambao umetolewa na wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) .Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa saba kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa kike walio katika Kambi ya kitaaluma Shule ya Sekondari Bariadi baada ya kupokea msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 3000 wa kidato cha nne walio katika kambi za Kitaaluma ambao umetolewa na wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) .
Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa, Moses Mbambe akizungumza na wanafunzi wa Shule za Sekondari Bariadi, Somada, Chenge na Gudui kabla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike uliotolewa na Mamlaka hiyo kwa wanafunzi wa kike wa kidato cha nne walio katika kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, katika Shule ya Sekondari ya Bariadi Mjini Bariadi.

WAZIRI JAFO ATANGAZA UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO.

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 70,904 wakiwemo wasichana 31,884 na wavulana 39,020 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu kati kwa mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, Mhe. Jafo alisema wanafunzi waliochaguliwa ni kati ya wanafunzi 95, 337 walifaulu kwa kupata daraja la I-III na walikuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano na vyuo vya ufundi.

Mhe. Jafo kati ya wanafunzi waliochaguliwa wanafunzi 30,317 watajiunga tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 28,610 watajiunga na taasusi za masomo ya Sanaa na biashara.Alisema kuwa wanafunzi 885 watajiunga na vyuo vya ufundi ambavyo ni vyuo vya ufundi vya Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar-Es-Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kiukuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)

Mhe. Jafo alisema jumla ya wanafunzi 11,977 wamechaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali za ngazi za Astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada katika vyo vya elimu ya kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akitoa taarifa kwa umma kuhusu zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vyuo vya elimu ya kati kwa mwaka 2018 kwa vyombo vya Habari..




TAMCO YANDAA SHEREHE ZA EID EL FITR DMV

$
0
0

Mwenyekiti wa TAMCO Ally Mohamed (kushoto) akiwa pamoja nae Balozi mstaafu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani,Mhe. Mustafa Nyang'anyi katika sherehe ya Eid el Fitr iliyofanyika siku ya Ijumaa June 15, 2018 Silver Spring, Maryalnd. Jumuiya hiyo ya Kiislam DMV ilisherehekea sherehe hiyo sambamba na Waislam wengine, Duniani. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza production kwa hisani ya Kilimanjaro Studio

WaTanzania DMV wakijumuika pamoja kusherehekea sikukuu ya Eid el Fitr iliyofanyika siku ya Ijumaa June 15, 2018 Silver Spring, Marland.

Makamu wa Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bi. Joha Nyang;anyi akihudhuria sherehe hizo kulia ni mama yake mama Nyang'anyi.

WaTanzania wakijumuika pamoja kusherehekea sikukuu ya Eid el Fitr DMV, kulia ni Mikidadi Ally Mweka hazina msaidizi wa Jumuiya ya waTanzania DMV.

Kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
 

Maafisa TEHAMA Wakamilisha Mafunzo ya Mfumo Mpya wa Malipo (Epicor 10.2) Jijini Dodoma

$
0
0
Afisa TEHAMA, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bw. Robert Dudu (aliyesimama) akitoa maelekezo ya namna gani Afisa TEHAMA anatakiwa kutatua matatizo katika mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) wakati wa mafunzo ya mfumo huo kwa Maafisa TEHAMA kutoka Halmashauri za Mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha, Shinyanga, Kigoma na Manyara, leo Jijini Dodoma.
Maafisa TEHAMA kutoka Halmashauri za Mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha, Shinyanga, Kigoma na Manyara wakifuatilia mafunzo ya mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) leo, Jijini Dodoma.
Maafisa TEHAMA kutoka Halmashauri za Wilaya ya Kiteto, Hanang’ na Babati wakifanya mazoezi ya namna mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) unavyofanya kazi na namna gani ya kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza katika mfumo huo pindi utakapoanza kutumika Julai 1 mwaka huu katika Halmashauri zote za wilaya, miji na majiji hapa nchini.
Maafisa TEHAMA kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mpwawa na Bahi wakifuatilia mafunzo ya mfumo wa malipo (epicor 10.2) ambayo yametolewa kwa Maafisa TEHAMA kutoka Mamlaka zote za Serikali za Mitaa ili kuwapa uelewa wa namna gani ya kutatua changamoto katika mfumo huo mara utakapoanza kutumika na Mamlaka hizo kuanzia Julai 1 mwaka huu.
Afisa TEHAMA kutoka Halmashauri ya Mji Shinyanga, Bw. Stanley Manyonyi na Afisa TEHAMA kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bi. Swaumu Hamza wakiendelea na mafunzo ya mfumo mpya wa malipo (epicor 10.2) leo, Jijini Dodoma.

KIKUNDI CHA BEAUTY WITH BRAIN,SERENA HOTEL WAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUTOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KURASINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Katika kuadhimisha  ya siku ya mtoto wa Afrika leo kikundi cha Beauty with Brain kwa kushirikiana naSerena Hotel  wamemtoa msaada wa vitu mbalimbali kwa kituo cha watoto wanaoishi  kwenye mazingira cha serikali kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam. 

Beauty with Brain pamoja na Serena waliweza kukabidhi vyakula, mafuta ya kupikia, masweta ya watoto, rangi na gypsum kwa ajili ya ukarabati wa sehemu ya kulia chakula, vitabu, nguo na baadhi ya vitu vingine.

Akizungumza ma wanahabari baada ya kukabidhi kwa vitu hivyo, Mwenyekiti wa Beauty With Brain Teddy Mapunda alisema kuwa lengo kuu la kuwasaidia watoto hao ni kuwafanya wajisikie wanafamilia zinazowapendà  na kuwajali pia.

Teddy amesema, katika siku ya leo wamekuja na zawadi mbalimbali kwa watoto hao ikiwemo vitabi vya kujisomea, masweta 71 kwa watoto wote na pia  nguo na viatu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.

Kikundi hicho kimeweza kushirikiana bega kwa bega na Serena Hotel na kufanikisha kupatiwa kwa zawadi hizo kwa watoto hao ambapo Mkurugenzi wa Rasilimali Wa Serena Hotel Sophia Mketo amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu wameamua kujumuika pamoja na watoto wa kituo cha Kurasini na wameona wanahitaji sana mchango wao.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja wa wanawake cha Beauty with Brain cha jijini Dar es Salaam,Teddy Mapunda (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitabu mmoja kati ya watoto wanaolelewa katika Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Serikali kilichopo Kurasini,jijini Dar es Salaam,wakati kinamama hao kwa kushirikiana na Hoteli ya Serena, walipotembelea kituo hicho leo asubuhi na kukabidhi Vyakula, Ndoo za rangi, Gipsum Board, Masweta ya watoto wote 71, nguo na viatu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Picha Zote na Nasma Mafoto
Mazungumzo kabla ya kukabidhi msaada huo
Kina mama wa Beauty With Brain wakikabidhi sehemu ya msaada huo kwa watoto wa kituo chaWatoto Yatima ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Umoja wa wanawake cha Beauty with Brain cha jijini Dar es Salaam,Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima Kurasini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Hoteli ya Serena, Sophiaakizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima Kurasini ikiwa ni maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika leo Jijini Dar es Salaam
Msimamizi wa Kituo ya Yatima cha Kurasni Beatrice Mgumiro, akiwashukuru kikundi cha Beauty with Brain pamoja Serena Hotel kwa kuwakumbuka watoto hao wanaoishi katika kituo cha watoto yatima Kurasini.
Baadhi ya wafanyakazi wa Hotel  Serena Hotel wakiwa katika picha ya pamoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mwalimu Mwingine Aongelea Kitabu Changu

$
0
0
Na Profesa Joseph Mbele

Ni jadi yangu kuwatambua wasomaji wanaosema neno kuhusu vitabu vyangu. Ni namna ya kuwashukuru kwa kutumia muda wao kukisoma kitabu na kutumia tena muda kuandika maoni yao. Ninatambua kwamba wanafanya hivyo kwa hiari, na wangeweza kutumia muda wao kwa namna nyingine. Ninawashukuru.

Wiki hii amejitokeza mwalimu Khalid Kitito, ambaye amekitumia kitabu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences katika ufundishaji wake hapa Marekani, akaandka maoni kwenye mtandao wa PublicReputation:

Africans and Americans written by Joseph Mbele is an excellent book to read about cultural differences between Americans and Africans. He examined the deep culture and not surface culture. It brings out clearly the understanding as to why Americans and Africans have different perspective of time, relationships, work, family, love, respect among others. I used it to teach in my Culture and Identity Class and found it useful. The book provided a forum for insightful discussions and at the end of the course students were able to view other cultures as different and not weird. It is also easy to read and understand, thus suitable for general readers.
Napenda kugusia tathmini yake kuwa ninaibua "deep culture." Wanataaluma wa tamaduni wanasisitiza suala hili la "deep culture." Tunapokutana na utamaduni wowote, tunaona mambo mengi, lakini ili kuyaelewa yale tunayoyaona, tunatakiwa kuelewa msingi wake. Hii ndio "deep culture." Inachukua muda sana kuuelewa utamaduni kwa maana hiyo. Ndivyo ilivyokuwa kwangu, katika kutafakari utamaduni wa wa-Marekani. Ilinichukua miaka karibu ishirini ya kuishi na wa-Marekani kabla sijathubutu kuandika kitabu changu. Kwa upande mwingine, kwa kuwa mimi ni mtafiti na mwalimu wa fasihi na "folklore" na ni mw-Afrika, haikuwa shida kwangu kuelezea "deep culture" kwa upande wa wa-Afrika.
Pamoja na kumshukuru mwalimu Kitito, kwa kuandika maoni yake, ninatoa mwaliko kwa yeyote mwingine aliyesoma au kutumia kitabu changu chochote kuandika maoni yake katika ukurasa huu wa PublicReputation.

TARIMBA: 'Usajili wa YANGA, tunafukuza Mwizi Kimya Kimya'

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images