Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

VOA SWAHILI: DUNIANI LEO JUNI 12, 2018


DKT FAUSTINE NDUGULILE ALIPOKUTANA NA BARAZA LA WATOTO JIJINI ARUSHA

ZIARA YA KITALII MUENDESHA PIKIPIKI KUTOKA NCHI YA OMAN

$
0
0
 MUENDESHA Pikipiki kutoka Oman Maher Al Barwany akiingia katika Viwanja vya Wizara Ya Habari Utalii na Mambo ya Kale zilizopo Kikwajuni Mjini Zanzibar kwaajili ya ziara ya kitalii kwa kutumia pikipiki na kufanya mazungumzo na Waziri wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo.
 WAZIRI wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Maher Al Barwany muendesha Pikipiki kutoka Oman alipofanya ziara ya kitalii katikati ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.
 MSHAURI wa Waziri Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Maalim Abdalla Mwinyi akibadilishana mawazo na Maher Al Barwany  alipofanya ziara ya kitalii katikati ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.
 WAZIRI wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Maher Al Barwany muendesha Pikipiki kutoka Oman katika ukumbi wa Wizara ya Habari uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar alipofanya ziara ya kitalii Visiwani Zanzibar,  katikati ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.
  WAZIRI wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akimvisha Skafu inayotangaza Utalii wa Visiwa Vya Zanzibar Maher Al Barwany muendesha Pikipiki kutoka Oman katika ukumbi wa Wizara ya Habari uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar alipofanya ziara ya kitalii kushoto ni Balozi Mdogo wa Oman Zanzibar Dkt. Ahmed Hamoud Al Habsy.


WAZIRI wa  Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akijaribu kuendesha Pikipiki linalotumiwa na Maher Al Barwany kutoka Oman katika safari zake za kitalii Nchi mbalimbali Duniani (Picha na Abdalla Omar Maelezo - Zanzibar).

WAZIRI UMMY KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LA TIKA WAGAWA VYAKULA VYA SIKUKUU YA EID EL FITRI KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA

$
0
0
  Na Assenga Oscar, Tanga 
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi vyakula mkazi wa Jiji la Tanga vyenye thamani ya sh.milioni 29.9 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Fitri kwa kaya 500 za wakazi  Jiji la Tanga ambavyo ni Mchele Kg 5,Maharage Kg 5,Sukari Kg 5,Unga wa Ugali kg 5,Unga wa Ngano Kg 5,Chumvi Kg 1 na Mafuta ya kupikia lita 5 vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo la Uturuki(TIKA) baada ya kuwapa maombi ya mahitaji hayo kwa wakazi hao kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella katika halfa iliyofanyika kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga.
  WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia Mbunge wa Viti Maalumu (CCM)Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto wakiwa na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) Hikmet Ozdenoglu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo ya ugawaji wa vyakula ambavyo ni Mchele Kg 5,Maharage Kg 5,Sukari Kg 5,Unga wa Ugali kg 5,Unga wa Ngano Kg 5,Chumvi Kg 1 na Mafuta ya kupikia lita 5
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa halfa hiyo.
 Sehemu ya vyakula vikishushwa kwenye gari tayari kwa ajili ya kugawiwa wakazi 500 wa Jiji la Tanga ambavyo vimetolewa na Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA). Kwa habari zaidi BOFYA HAPA





BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 12.06.2018

TANZIA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

EID FETE

KUMBUKUMBU YA MAMA YETU MPENDWA MRS. ELIPINA MSANGI SEMKURUTO

$
0
0


Sisi familia tunatoa shukrani za pekee kwa Mungu kwa jinsi alivyoweza kutulinda na kutupa faraja ya pekee katika kipindi chote cha majonzi na hadi sasa unatimiza mwaka bila kuwa nawe. Tunakukumbuka sana mama yetu japo kimwili haupo nasi pengo lako daima haliwezi kuzibika. 

Tunakumbuka upendo wako, ushauri wako, upole na ucheshi wako pamoja na ukarimu wako ambao ulimfanyia kila aliyekufahamu kuguswa kipekee.  Kipekee unakumbukwa sana na mumeo  Mzee Vincent William Semkuruto watoto wako Naomi, Jane, Caroline, Samweli, Dolly, Diana pamoja na wajukuu wako, ndugu,  jamaa na marafiki.

‘Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda, nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana atanipa siku ile.” 2 Timotheo 4:7-8              

Pumzika kwa Amani Mama    

Amen



UJUMBE WA EID EL FITR TOKA KWA MUFTI NA SHEKHE MKUU WA TANZANIA

UZI MPYA WA BWAWA LA MAINI KWA MSIMU WA 2018/18

UBA-TANZANIA MEETS LEGENDARY INSPIRATIONAL FIGURE AND PROFFESIONAL ATHLETE JOHN STEVEN AKHWARI.

$
0
0
On 29th May 2018, Lucky United Bank for Africa - Tanzania staff were visited by a legendary figure from the summer Olympics of 1968, Mr. John Steven Akwari who is famous for his quote "My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race."

Executive Director Emeke E. Iweriebor was pleased to host Mr. Akhwari,s as he always referred to his story to motivate the team to making success stories through resilience and commitment.The ED/RCEO charged all staff members to be strongly committed and positively inclined to creating a difference.

He urged staff to become believers, be resilient and always go the extra miles to achieve exceptional results.During his dialogue, the ED/RCEO largely used the example of John Steven Akhwari a marathon runner during the 1968 Olympic games in Mexico City. Akhwari was a world class runner of the 1960’s and 1970’s where he participated in different Olympic games across the world. His 1968’s Olympics in Mexico is regarded the most heroic story to date.

This is because during his 42 Kilometre marathon mission Akhwari was Cramped up due to the high altitude of the city. He had not trained at such an altitude back in his country. At the 30 -kilometre point there was jockeying for position between some runners and he was hit. He fell badly wounding his knee and dislocating that joint plus his shoulder hit hard against the pavement.
From Left Mr. Mathias Ninga, HR Business Partner East and Southern Africa UBA Group, next is Mr. Emeke Iweriebor, Executive Director East and Southern Africa UBA Group, next is the Renowned Olympian Mr.John Akhwari and Right is Mr.Usman Isiaka the Managing Director UBA Tanzania.
Mr. John Akhwari stressing a point during his visit to UBA Tanzania. On his right hand is Mr. Emeke Iweriebor the Executive Director East and Southern Africa UBA Group.
UBA Staff members pose with Mr. John Akhwari during his visit to UBA Tanzania Head Office.

RAIS DK.SHEIN AWAFUTARISHA WANANCHI MKOA WA MJINI MAGHARIBI UNGUJA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Viongozi na Wananchi wa  Mkoa wa Mjini Magharibi  katika Futari aliyowaandalia jana katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar  ikiwa ni mwendelezo wake wa kufutarisha kila ifikapo kipindi kama hichi,(kulia) Rais mstaafu wa Zanzibar Dkt.Amani Abeid Karume
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akijumuika na Viongozi Wanawake na Wananchi wengine katika Futari aliyoandaliwa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar jana
  Baadhi ya Akinamama wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar katika  mwendelezo wake wa kuwafutarisha Wananchi hao kila ifikapo Mwezi 27 wa Mfungo wa Ramadhan
 Wananchi na Waislamu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakiwa katika Futari iliyoandaliwa jana na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar ikiwa ni mwendeleo wake kila ifikapo mwezi 2y ya Mfungo wa Ramadhan kuwafutarisha Wananchi 
 Kadhi Mkuu wa Zanzibar  Sheikh Khamis Haji (kulia) alipokuwa akisoma Dua kumuombea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) baada ya futari aliyoiandaa kwa Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi jana katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar, ikiwa ni mwendelezo wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa Mikoa huo 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na Wananchi mbali mbali  waliohudhuria katika Futari iliyowaandalia Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi jana  katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar ikiwa ni katika mpangilio wake wa kuwafutarisha Wananchi na Waislamu wa  Mikoa huo kila ifikapo mwezi 27 ya Mfungo wa Ramadhan


VODACOM NA KWESE INFILIX KUTOA BURUDANI YA KOMBE LA DUNIA 2018 KIGANJANI

$
0
0
MASHABIKI wa soka wanatarajia kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia inayoanza leo nchini Russia kupitia simu zao za mkononi kwa ushirikiano wa kampuni ya Vodacom Tanzania na Inflix.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Nandy Mwiyombella, alisema wateja wa Vodacom wataweza kushuhudia fainali hizo kwa kupakua App ya Kwese Inflix na kununua bando kupitia menu ya *149*01# na kuchagua vifurushi vya siku au wiki.

“Tunazindua kampeni yetu hii ya wateja wa Vodacom kushuhudia Kombe la Dunia tukiwa na Inflix, lengo letu ni kuwapa fursa wateja wetu kufurahia fainali hizi, tumeona tuungane kuwarahisishia wateja wetu kama ilivyo kauli mbiu yetu ya Yajayo yanafurahisha,” alisema.

Alisema kuwa kwa ushirikiano wa Vodacom na Inflix wamejipanga kuwaletea wateja wao kuangalia Kombe la Dunia kupitia Kwese Inflix bando kupitia simu ya kiganjani.

Naye Mkurugenzi wa Inflix, Mgope Kiwanga alisema kuwa wamejipanga kuleta mambo tofauti na sit u Fainali za Kombe la dunia bali kuna burudani za aina mbalimbali.

“Huu ni mwanzo tu wa kuwaletea mashabiki wetu kushuhudia Fainali za Kombe la Dunia, tukiwa na Vodacom, mashabiki watashudia mechi zote katika fainali hizo pamoja na matukio na burudani mbalimbali,” alisema.
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Nandy Mwiyombella (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu makubaliano walioingia kati ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Kwese Infix kwa wateja wa Vodacom wataweza kushuhudia fainali hizo kwa kupakua App ya Kwese Inflix na kununua bando kupitia menu ya *149*01# na kuchagua vifurushi vya siku au wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa Kwese TV Tanzania, Mgope Kiwanga na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Digitali Huduma za Ziada wa Vodacom, Paulina Shao.
Mkurugenzi wa Kwese TV Tanzania, Mgope Kiwanga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kwese TV walivyijipanga kurusha michuano ya Kombe la Dunia kupitia  App ya Kwese Inflix kwa wateja wa Vodacom Tanzania. Kulia ni  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Nandy Mwiyombella.

MADEREVA WALEVI KUKIONA

$
0
0
JOSEPH MPANGALA,MTWARA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya amewaonya Madereva wa Magari na Pikipiki Kuacha Kutumia Kilevi na baadaye Kuendesha Hasa katika Sikukuu ijayo ya Idd El Fitri.

Akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda Mkondya amewataka watu woote wanaotumia Kilevi kuhakikisha wanatafuta madereva watakao wandesha kwa lengo la kuepuka Ajali.

“Tukikumata umelewa na unaendesha gari Utakaa mahabusu ya Polisi Mpaka Sikukuu itakapokwisha ndio tutakupeleka Mahakamani,Kwa hiyo Tukikukamata siku ya Iddi Utakuja kupelekwa Mahakaman siku ya Jumatatu lakini kama unaona Huwezi Sikumbili haziwez kupita Bila kunywa Pombe ni Bora Utafute Dereva aweze kukuendesha”

Aidha ameongeza kuwa katika siku ya Idi Watu woote wanaopenda kukaa maeneo ya ufukweni wahakikishe wanaondoka na kurudi majumbani Pindi inapofika Mida ya saa 12 Jioni.

“Inapofika Saa12 jioni hatutaruhusu watu kuendelea kuogelea baharini kwa hiyo tunawaomba waende mapema na itakapofika saa12 jioni werejee majumbani”

KAMISHNA MKUU WA TRA AWASHUKURU WAFANYABIASHARA JIJINI DODOMA

$
0
0
Na Veronica Kazimoto,Dodoma 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewashukuru wafanyabiashara jijini Dodoma kwa mchango wao wa kulipa kodi na kuiwezesha Serikali kutekeleza wajibu wake wa kukuza uchumi na kutoa huduma mbalimbali za jamii hapa nchini. 

Akizungumza wakati akifuturisha wafanyabiashara na wafanyakazi wa TRA katika ukumbi wa LAPF jijini hapa, Kichere alisifia uhusiano mzuri uliopo kati ya wafanyabiashara hao na ofisi ya TRA Mkoa wa Dodoma. 

"Nachukua nafasi hii kuwashukuru wafanyabiashara wa Dodoma kwa kuwa walipakodi wazuri na kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na ofisi yetu ya TRA hapa mkoani Dodoma ambapo kutokana na uhusiano huu uliopo, tunapata urahisi wa kutekeleza jukumu letu la kukusanya mapato ya Serikali kwa manufaa ya watanzania wote," alisema Kichere. 

Kichere amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa, TRA itaendelea kudumisha ushirikiano huo na kukaribisha mazungumzo ya pamoja na viongozi wa TRA mkoani hapa ili kufikia muafaka wa masuala mbalimbali yanayohusu kodi badala ya kulalamika mitaani bila kupata suluhisho. 

Aidha, Kamishna Mkuu Kichere amewahimiza wafanyabiashara hao kuendelea kulipa kodi mbalimbali kwa wakati kwani kodi hizo hutumika katika kujenga uchumi wa nchi na kutoa huduma mbalimbali za jamii ikiwa ni pamoja na huduma za afya, maji safi na salama, elimu, kulipa mishahara ya watumishi wa Umma, miundombinu ya barabara na umeme. 

"Nachukua fursa hii kutoa rai kwenu wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi zote kwa wakati ikiwa ni pamoja na Kodi ya Majengo na Kodi ya Mapato awamu ya pili ambapo mwisho wa kulipa kodi hizi ni tarehe 30 Juni, mwaka huu. Kodi nyingine ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo hulipwa tarehe 20 ya kila mwezi. Hivyo, uhiari wenu wa kulipa kodi hizi kwa wakati ndio chachu ya kujenga uchumi wetu na kuharakisha kutoa huduma za jamii kwa watanzania wote", alisema Kichere. 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akitoa hotuba fupi kwa Wafanyabiashara wa Jijini Dodoma wakati wa hafla fupi ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara hao ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa miwani) akiwekewa futari wakati wa hafla fupi ya Iftar aliyowaandalia wafanyabiashara wa Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Jijini Dodoma wakichukua futari wakati wa hafla fupi ya Iftar iliyoandaliwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere kwa wafanyabiashara hao ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (aliyevaa kofia kulia) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara na watumishi wa TRA wakifuturu wakati wa hafla fupi ya Iftar iliyoandaliwa na Kamishna Mkuu huyo ikiwa ni sehemu ya kuwathamini walipakodi nchini.


MKURUGENZI MKUU TCAA ATHIBITISHWA KUWA MWENYEKITI WA CANSO KANDA YA AFRIKA

$
0
0
Shirikisho  la Kimataifa  la Huduma za Anga na uongozaji Ndege, maarufu kama (CANSO), katika mkutano wake mkuu wa 22 wa mwaka uliofanyika tarehe 12/06/2018 huko Bangkok, Thailand, limemthibitisha, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza S. Johari, kuwa Mwenyekiti mpya wa CANSO kanda ya Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Hii inafuatia uteuzi wa Bwana Johari kuwa Mwenyekiti wa CANSO Afrika Machi 2018 huko Madrid, Hispania. Kwa wadhifa huo Bwana Johari anakuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji (EXCOM) ya shirikisho hilo muhimu la kimataifa katika usafiri wa anga.
Bi Terri Bristol, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Marekani anaendelea kuwa Mwenyekiti wa CANSO  ambapo, Bwana Rudy Keller kutoka Canada ameteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti
Wajumbe wengine wa EXCOM ni Martin Rolfe -Uingereza,Klaus Dieter Scheurle -Ujerumani,  Hamza S. Johari - Tanzania, Mark Cooper- Uingereza, Augustin Rodrigues Grellet - Agentina, Jan Klas - Jamhuri ya Czech, Don Thoma - Marekani, Dr Saleh Al Ghamdi - Saudi Arabia, Kevin Shum - Singapore and Captain Gilbert Kibe - Kenya.
Wajumbe wa EXCOM wanakutana mara nne kwa mwaka kupanga mikakati ya uongozaji safari za ndege na masuala mengine ya kisera kuhakikisha usalama na ufanisi wa usafiri wa anga duniani.
Menejimenti ya Shirikisho la CANSO inaongozwa chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wake Mkuu Jeff Poole akishirikiana na wafanyakazi wengine wa sekretariati ambayo inahakikisha utekelezaji wa maagizo na mikakati ya kamati kuu ya EXCOM
Tunamtakia Mkurugenzi Mkuu Hamza Johari Heri na Mafanikio katika majukumu yake mapya katika jumuiya hii ya kimataifa.
Imetolewa  na Kitengo cha Habari -TCAA

MASAUNI AFANYA ZIARA MKOANI GEITA, AKAGUA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA POLISI, GEREZA NA UJENZI WA NYUMBA 100 ZA ASKARI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akionyeshwa na Mkuu wa Gereza Chato, Joseph Busumabu, maeneo mbalimbali ya Gereza hilo ambalo tayari linahifadhi wafungwa na mahabusu na pia linaendelea kupanuliwa kwa kujengwa majengo mapya zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Shabaan Ntarambe. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulamboakimuonyesha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), Kituo kipya cha Polisi mjini Chato ambacho kipo katika hatua ya mwisho kukamilika. . Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitoka kukagua ujenzi wa Gereza Chato, mkoani Geita, ambalo licha ya kua tayari Gereza hilo jipya limenza kuhifadhi wafungwa na mahabusu lakini linaendelea kupanuliwa kwa kuongezwa majengo zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaaban Ntarambe, na kulia alyevaa sare, ni Mkuu wa Gereza hilo, Joseph Busumabu. Masauni alifanya ziara katika Mkoa wa Geita kwa kukagua ujenzi wa Kituo cha Polisi Chato, ujenzi wa Gereza Chato na baadaye kukagua ujenzi wa nyumba 100 za askari polisi ambazo zimeanza kujengwa mjini Geita.

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMONDO YA UMOJA WA MATAIFA KUFANYIKA JUNI 30, 2018

WANAFUNZI WATEMBELEA BUNGE KWA LENGO LA KUJIFUNZA SHUGHULI ZA BUNGE

$
0
0
 Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mount Kibo ya Jijini Dar es salaam wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.
 Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Angelico Lipani ya Jijini Arusha wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.
Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Martin Luther ya Jijini Dodoma wakiongozwa na Walimu wao wakiwa katika Majukwaa ya Wageni Bungeni kufuatilia Shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna linavyoendeshwa.PICHA NA BUNGE

HOSPITALI YA TAALUMA NA TIBA MAMC, MLOGANZILA WAADHIMISHA SIKU YA KUCHANGIA DAMU

$
0
0
Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili MAMC, Mloganzila imeanza maadhimisho ya siku ya kuchangia damu kwa kufanya zoezi la uchangishaji damu kwa wafanyakazi wa Mkombozi Commercial Bank, tawi la Msimbazi Center ili kukidhi mahitaji ya huduma hiyo kwa wagonjwa wanaohitaji. 

Katika zoezi hili la uchangizaji damu Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Mkombozi Bw.George R. Shumbusho alitoa msaada wa kitanda kimoja kwa hospitali ya MAMC kwa ajili ya kusaidia wakati wa zoezi la utoaji damu kwa watu mbalimbali wanaojitolea na mabox 20 (cooler boxes) za kuhifadhia damu wakati wa kupeleka damu wodini kwa wagonjwa. Msaada huu wa vifaa unagharimu pesa ya kitanzania shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000).

Akiongea wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Shumbusho “Kama taasisi ya benki kwa kuona umuhimu wa mahitaji ya damu ndiyo maana tumeadhimisha siku hii ya leo kwa kuwaamasisha wafanyakazi wetu wachangie damu ili tuweze kuokoa maisha ya watanzania na kutoa msaada ya vifaa vitakavyoweza kusaidia zoezi la uchangishaji damu”, alisema Vile Vile aliwapongeza wafanyakazi waliojitokeza kuchangia damu, “Ni jambo la umuhimu mmefanya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa”, aliongeza. 

Naye Mkuu wa kitengo cha kuchangia damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba MAMC, Mloganzila Dkt. Ivan Nyamhanga amewashukuru uongozi mzima wa Benki ya Mkombozi kwa kuhamasisha zoezi hili la kuchangia damu na pia kwa vifaa walivyotoa ambavyo vitasaidia wakati wa zoezi la uchangishaji damu. Pia aliwashukuru wafanyakazi wote wa benki ya Mkombozi kwa kujitolea kuchangia damu kwa wahitaji. 

"Kama mnavyojua mahitaji ya damu ni makubwa hasa katika hospitali yetu ambayo bado ni changa na hivyo tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kuhamasika kuchangia damu", alisema Dkt. Nyamhanga. Zoezi hili la maadhimisho ya siku ya kuchangia damu lilifanyika katika Benki ya Mkombozi, tawi la Msimbazi center na vile vile baadhi ya maaskari kutoka SUMA JKT, Mloganzila waliweza kuchangia damu.
Mtaalamu kutoka kitengo cha kuchangia Damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) akielezea faida za kuchangia damu na sifa za mtu anayetakiwa kuchangia damu kwa wafanyakazi ya Benki ya Mkombozi waliojitolea kuchangia damu katika kuadhimisha siku ya kuchangia damu duniani. 
Wataalamu kutoka kitengo cha cha kuchangia Damu katika Hospitali ya Taaluma na Tiba (MAMC) wakiwa wanapima vipimo mbalimbali kwa wachangiaji kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi, Bw. George R. Shumbusho (kulia) akishiriki katika maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani.

Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images