Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

DCB WAJITOSA UDHAMINI NDONDO CUP, YAAHIDI KUTOA ELIMU YA HUDUMA ZA KIBENKI

$
0
0
Meneja Masoko wa Benki ya DCB Boyd Mwaisame akielezea namba watakavyokuwa wanawafungulia akaunti wachezaji na timu shiriki kupitia zawadi wakatazokuwa wanazitoa.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uzinduzi wa Michuano ya Ndondo Cup iliweza kufunguliwa rasmi jana kwa timu ya Mabibo Market kuchuana na Keko Furniture uliofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi Jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa kwanza Mabibo Market waliweza kuondoka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Keko ukiwa ni katika hatua ya makundi ya 32 bora.

Kwenye michuano ya mwaka huu, Benki ya DCB imeweza kudhamini kwa mwaka huu na kuahidi kutoa hela za washindi wa kila mchezo sambamba na mchezaji bora wa mechi.

Akuzungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Meneja Masoko wa DCB Boyd  Mwaisame amesema kuwa kwa mwaka huu wameamua kuja kudhamini michuano hiyo ya Ndondo Cup ikiwa ni pamoja na kutoa hamasa kwa wachezaji na timu kuweza kufungua akaunti za benki ili kuhifadhi fedha zao kwa usalama zaidi.

Boyd amesema kuwa katika zawadi wakatazokuwa wanatoa kwa timu itakayokuwa inashinda kwenye michuano ambapo ni sawa na kiasi cha shillingi laki mbili (200,000) moja kwa moja fedha hizo zitafunguliwa akaunti ya timu sambamba na mchezaji bora wa mechi yeye fedha yake atafunguliwa akaunti binafsi.

"Sisi kama DCB tumeonelea sana kuwa timu zote pamoja na wachezaj kuwa na akaunti za benki maana hata fedha za ushindi  watakazokuwa wanazipata ziwe zinapitia kwenye akaunti kitu ambacho kitakuwa ni kizuri zaidi, na kwa kuanzia leo tunaanza timu ya Mabibo Market iliyoshinda pamoja na mchezaji bora wa mechi wote kwa pamoja watafunguliwa akaunti zao hapa hapa,"amesema Boyd.

Pia, Boyd ameema kuwa pamoja na udhamini huo wanataka kutoa elimu ya huduma za kibenki kwa vijana wengi na timu zinazoshiriki mashindano hayo ya Ndondo Cup ili wazitumie na kuwanufaisha kiuchumi huku wakiwa na lengo la kusaidia kuendeleza mpira wa soka nchini.
Msanii Nikki Wa Pili akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup iliyozinduliwa jana katika Uwanja wa Kinesi Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Meneja Masoko wa benko ya DCB Boyd Mwaisame.

Mbali na hilo DCB waliweza kumtambulisha Balozi wao msanii Nikki wa Pili  ambaye aliweza kuwashauri vijana hususani wachezaji kuweza kufungua akaunti ya benki ambapo wanaweza kupata hadi mikopo pindi pale wanapokwama.

Uzinduzi huo uliweza kuhudhuriwa na wachezaji mbalimbali akiwemo mchezaji wa Kimataifa wa Kenya Victor Wanyama  anayekipiga ligi ya Uingereza katika timu ya Tottenham Spurs, Mshambuliaji wa Genk Mbwana Samatta, Mrisho Ngasa na wachezaji wengine mbalimbali.
Wachezaji wa Kimataifa Victor Wanyama na Mbwana Samatta wakiwa wanafuatilia mtanange wa uzinduzi baina Ya Mabibo Market na Keko Furniture.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF Wallace Karia akimkabidhi fedha kiasi cha Shilling Elfu Hamisini (50,000) mchezaji bora wa mechi kutoka timu ya Mabibo Market Nassor Kapama baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Aidha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Wallace Karia aliweza kutoa neno kwa waandaji wa michuano hiyo kuendelea kuibia vipaji vya wachezaji wachanga kwani wengi wao wanatokea katika timu za kawaida.


KONGWA WAFANYA ZIARA MKOANI SIMIYU KUTEMBELEA MIRADI YA VIJANA ILI KUJIFUNZA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Viongozi kutoka Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Deo Ndejembi pamoja na baadhi ya viongozi wa vikundi vya vijana wilayani humo wamefanya ziara Mkoani Simiyu ili kujifunza namna vikundi vya vijana vinavyotekeleza miradi yake.

Timu hiyo imefanya ziara ya siku mbili hadi Juni 08, 2018  katika miradi inayotekelezwa na vijana kwa kushirikiana na Halmashauri ambayo ni Kiwanda cha Chaki,  Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi wilayani Maswa na Mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu.

Mkuu wa wilaya ya Kongwa amesema wameamua kuja Simiyu kwa kuwa vikundi vyake vimeonekana vikifanya vizuri katika miradi yake, hivyo wamewaleta vijana wao ili wapate uzoefu na ari itawasukuma kubuni miradi yao na kujua namna bora ya kuiendesha.

"Tumeona tuje tujifunze kutoka Simiyu maana mkoa wa Simiyu umeonesha mfano wa namna vikundi vya vijana vinavyotakiwa kutekeleza miradi yake, tumeona kwenye vyombo vya habari na kwingineko mkipata sifa nyingi kutokana na miradi yenu kuonesha matokeo, nia yetu vijana waje waone wajifunze wapate hasira ya kufanya kitu cha kwao" alisema Ndejembi.
 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi (wa tatu kulia) na baadhi ya vijana kutoka Kongwa waliofika kutembelea kiwanda cha chaki wilayani humo, wakati wa ziara yao ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe(kulia) akimuonesha  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi kiatu kilichotengenezwa na Kikundi cha Vijana Senani wilayani Maswa, wakati wa ziara ya Viongozi na Vijana wa Wilaya ya Kongwa kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi (kushoto) akiangalia chupa ya maziwa yanayosindikwa wilayani Meatu, baada ya kutembelea Kiwanda cha kusindika maziwa ‘Meatu Milk’ wakati wa Ziara yake na vijana wa Wilaya ya Kongwa ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Meatu, Bw. Fabian Manoza akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi zawadi ya maziwa, mara baada ya kutembelea Kiwanda cha Kusindika Maziwa wilayani humo,  wakati wa Ziara yake na vijana wa Wilaya ya Kongwa ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mmoja wa Vijana kutoka kikundi cha Maswa Family akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi na baadhi ya vijana kutoka Kongwa (wa tatu kulia) waliofika kutembelea kiwanda cha chaki wilayani humo, wakati wa ziara yao ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deo Ndejembi (wa pili kulia) akiuliza jambo wakati alipotembea eneo la kufungashia chaki wakati alipotembelea kiwanda cha chaki wilayani Maswa, wakati wa ziara yao ya kutembelea miradi ya vijana Mkoani Simiyu kwa lengo la kujifunza.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MWAKYEMBE AFUNGUA WARSHA YA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI MKOANI MOROGORO

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Siku mbili ya Wahariri wa Vyombo vya Habari iliyofanyika mkoani Morogoro. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuwajengea wahariri wa vyombo vya Habari uwezo wa kuripoti taarifa mbalimbali za Kitakwimu.
 Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mr. Irenius Ruyobya akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Siku mbili ya Wahariri wa Vyombo vya Habari iliyofanyika mkoani Morogoro. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuwajengea wahariri wa vyombo vya Habari uwezo wa kuripoti taarifa mbalimbali za Kitakwimu.
 Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari walioshiriki katika warsha ya siku mbili ya Wahariri wa Vyombo vya Habari iliyofanyika mkoani Morogoro. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuwajengea wahariri wa vyombo vya Habari uwezo wa kuripoti taarifa mbalimbali za Kitakwimu.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari walioshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya Wahariri wa Vyombo vya Habari iliyofanyika mkoani Morogoro. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuwajengea wahariri wa vyombo vya Habari uwezo wa kuripoti taarifa mbalimbali za Kitakwimu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kufungua warsha ya siku mbili ya Wahariri wa Vyombo vya Habari iliyofanyika mkoani Morogoro.
(Picha Na Emmanuel Ghula)

LIVE: SHEREHE YA HARUSI REUBEN & JENISTA UKUMBI WA PRIME ROSE - MBEZI BEACH DSM

SPIKA NDUGAI AOSHA MAGARI KUHAMASISHA UCHANGIAJI WA FEDHA ZA UJENZI WA VYOO

$
0
0
 
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akiosha magari tofauti tofauti wakati wa shughui ya kuosha Magari kwa ajili ya kuchangia fedha za kujengea Vyoo vya mfano kwa ajili ya watoto wa Kike na wenye mahitaji maalum. Shughuli hiyo imefanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. PICHA NA BUNGE

Mtanzania atamba mpira wa meza Kenya

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Mchezaji wa mpira meza wa Tanzania, Sara Alidina ameingia hatua ya mashindano ya mikoa ya Kenya iliyopangwa kuanza wiki ijayo baada ya kushinda medali ya fedha katika hatua ya awali.
Sara  aambaye anasoma katika shule ya  Aga Khan Academy Mombasa, amejumuishwa katika timu ya Mvita ambayo pia inaundwa na wachezaji wawili kwa ajili ya mashindano mkoa.

Sara alianza michuano hiyo kwa vishindo baada ya kumchapa Rachel Thomas kwa seti 2-0 (11-4, 11-6) na baadaye kupata ushindani mgumu kutoka kwa Elizabeth Ochieng ambaye alianza kwa kushinda kwa 15-14 kabla ya kumbadilishia kibao na kuibuka na ushindi kwa seti mbili zilizobaki kwa  11-5 na 11-4).

Sara aliendelea kutamba katika mashindano kwa kumchapa  Christine Augustine kwa 2-0 (11-4, 11-6) na baadaye kushinda dhidi ya Maliha Haji kwa  2-0 (11-4, 11-5) na kupoteza kwa 2-0 dhidi ya Rachel Simon kwa 8-11 na 9-11.

Pamoja na kushindwa dhidi ya Rechal, Sara alifuzu hatua ya robo fainali na kushinda mechi dhidi ya Eliza Wanjiru kwa  2-0 (11-4, 11-4) na kushinda tena kwa 2-0 katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Catherine Okoth  kwa 11-4 na 11-6. Hata hivyo alikumbana na kigindi katika fainali kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Krupa Vyas kwa 11-8, 9-11 na 11-7.

Akizungumza kwa njia ya simu, Sara alisema kuwa mashindano hayo yalikuwa magumu sana na kushukuru Mungu kwa kufuzu hatua ya mashindano ya mikoa.

“Lengo ni kutwaa ubingwa pamoja na kupata ushindani mkubwa, mechi nyingi zilikuwa ngumu na hasa ukingatia kuwa nacheza na wachezaji wakubwa zaidi yangu. Hii imesababisha kuchoka na kufungwa katika hatua ya fainali,” alisema Sara.

TEAM SAMATTA WAIPAPASA TEAM KIBA KWA 4-2 MBELE YA WAZIRI DKT MWAKYEMBE

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Ali Kiba  na Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva  katika mchezo wa hisani uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo , Katika mchezo huo Team Samatta imeifunga Team Kiba magoli 4-2 na kuibuka washindi wa mchezo huo mbele ya mashabiki wao waliojitokeza kwenye uwanja wa Taifa leo, Mchezo huo ulikuwa unadhaminiwa na Kiwanda cha Maziwa ya ASAS DAIRIERS cha Iringa

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Mechi ya hisani baina ya marafiki wa Ali Kiba na marafiki wa Samatta imechezwa leo Jijini Dar es Salaam huku mamia ya wananchi wakijitokeza kwa wingi wakiongozwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe.


Mechi hiyo mahususi kwa ajili ya uchangiaji wa fedha zitakazotumika kukarabati miundo mbinu ya mashuleni iliweza kukutanisha wachezaji kutoka timu mbalimbali za ligi kuu na nje ya nchi.


Mchezo huo uliomalizika kwa Marafiki wa Samatta kuondoka na ushindi wa goli 4-2 dhidi ya Marafiki wa Ali kiba ulikuwa ni wa ushindani kwa kila upande wakitaka ushindi.


Timu ya marafiki wa Ali Kiba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib akifunga goli la kwanza na la pili ila mpaka mapumziko timu ya marafiki wa Samatta waliweza kupata goli moja na matokeo kuwa 2-1.


Katika kipindi cha pili,Marafiki wa Samatta waliingia kwa kasi na kupata goli la pili kwa mkwaju wa penati na Haruna Moshi Boban na Mbwana Samatta kukandamiza msumari wa moto na kuleta matokeo kuwa 4-2 ila ndani ya kipindi cha pili Marafiki wa Ali Kiba walipata mkwaju wa penati ila Ali Kiba alikosa kwa kupaisha juu.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Samatta na mchezaji wa kimataifa anayecheza Genk Ubelgiji Mbwana Samatta  katika mchezo wa hisani uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo , Katika mchezo huo Team Samatta imeifunga Team Kiba magoli 4-2 na kuibuka washindi wa mchezo huo mbele ya mashabiki wao waliojitokeza kwenye uwanja wa Taifa leo, Mchezo huo ulikuwa unadhaminiwa na Kiwanda cha Maziwa ya ASAS DAIRIERS cha Iringa

Mchezo huo ulikua na burudani yake hasa kwa upande wa marafiki wa Samatta kupitia kwa msemaji wa Joti ambaye aliweza kufanya mbwembwe uwanjani ikiwemo kuingia uwanjani wakati mpira ukiwa unaendelea.

Baada ya matokeo hayo,wachezaji wote wa timu mbili walionesha kufurahishwa sana na hatua hiyo kubwa waliyoifanya ya kufanikisha kuchezwa kwa mchezo huo kwa ajili ya uchangiaji wa fedha zitakazofanikisha ukarabati wa shule hususani za msingi.

Mbali na hao, wadau wengine walioweza kuhamasisha na kufanikisha mechi hiyo ni kampuni ya maziwa ya Asasi Diaries ambapo waliweza kutoa jezi kwa pande zote mbili pamoja na mahitaji mengine muhimu kwa wachezaji.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh, Harisson Mwakyembe akitambulishwa wachezaji wa Team Kiba na Mwanamuziki Ali Kiba kwenye mchezo wa hisani uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa kati ya timu ya mwanamuziki Ali Kiba na Mbwana Samata Mchezaji wa timu ya Genk ya Ubeligiji
Kikosi cha Team Samatta.
 Kikosi cha Team Kiba.

MABULA AHAKIKI UHAWILISHAJI ARDHI KATIKA VIJIJI VYA NAKAWALE NA LILAHI PERAMIHO HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA RUVUMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akihakiki majina katika kijiji cha Nakawale halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kuhakiki uhawilishaji ardhi katika vijiji vya Nakawale na Lilahi Peramiho mkoa wa Ruvuma. Aliyevaa kofia ni mwenyekiti wa kijiji cha Nakawale Ally Paswere na kulia ni Mtendaji wa Kata ya Muhukuru halmashauri ya Songea Rajabu Issa Ajida
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha  Nakawale halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kuhakiki uhawilishaji ardhi katika vijiji vya Nakawale na Lilahi Peramiho mkoa wa Ruvuma.
 Kaimu Kamishna wa ardhi vijijini kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Kokula Shenkumba akitoa elimu ya uhawilishaji ardhi kwa wananchi wa kijiji cha Nakawale Peramiho wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Songea Rajabu Kiula akizungumza wakati naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula alipokwenda kuhakiki uhawilishaji ardhi katika kijiji  Nakawale Peramiho mkoani Ruvuma.
 Baadhi ya wananchi wa wa kijiji cha Nakawale Peramiho wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula (hayupo pichani)  wakati wa uhakiki wa uhawilishaji ardhi ya kijiji hicho.
 Wajumbe wa halmashauri ya Kijiji cha Lilahi Peramiho Wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma wakitambulishwa kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati ziara ya uhakiki wa uhawilishaji ardhi ya kijiji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HII NDIO HISTORIA YA MUZIKI WA DISCO TANZANIA

$
0
0
Image may contain: 12 people, indoor
Na Mwandishi wetu, Washington, DC
Nimeona nikae chini niipitie maandiko ya mhenga moja aliyeandika habari ya DISCO iliyokua na kichwa cha habari "WAHENGA TULITESA SANA ENZI ZETU DISCO LA MCHANA (BOOGIE) NA MA-DJ WAKALI!!!" mwandishi wa habari hiyo amejitahidi sana kuelezea kwa mapana ya ufahamu wake jinsi gani alivyoujua muziki wa Disco wa enzi zile waliwemo maDj wake.

Mimi nimeamua kuweka sawa baadhi ya mambo Dj Kalikali yeye alishapiga muziki YMCA wakishirikiana na Dj Niga Jay na kuna wakati pia walipiga pamoja na Dj John Peter Pantalakisi na muda mwingi John Peter Pantalakis walikua wakishirikiana na Dj Chogy Sly Dico la Born City na kuna kipindi fulani Dj Kalikali alikua Dj wa Disco la RSVP ambalo Mbowe walianzisha tawi la DICO  katika hotel ya New Africa ghorofa ya saba.
Image may contain: 5 people, including Richie Dillon, people smiling, people standing and outdoor
Muziki wa Disco unasafari ndefu maDj wengi wa zamani walikua wanamuziki wa bendi na baadae kubadili mwelekeo na kuwa maDj kwa mfano Dj Sweet Francis na Dj Addy Sally chimbuko lao walitokea kwenye bendi na baadae miaka ya 1970 wakahamisha mawazo yao na kuwa maDj wakati huo kukiwa na Disco la Banda Beach, Sea View na madisco mengine Kilimanjaro Hotel Summit

Nataka nikupe historia ya musiki na disco theque.Africana Gogo Disco lilianza mwaka 1971 na aliyeanza kupiga disco hapo ni Bhoka Wilson (Mzimbabwe) wakati ule ikiitwa Southern Rhodesia naye alikuwa cabbaret singer Simba Grill Kilimanjaro hotel. August 1972 Dj Sweet Fransis akawa Dj hapo mpaka Nov.1973 kisha akawa Dj. Judy Kingui (Msouth Africa ambaye alikuwa mkewe Kingui aliyekuwa mwenye The Rifters Band. Judy alikuwa Dj.hapo Gogo Disco mpaka 1975.

Katika historia ya muziki wa disco Tanzania ambayo inabeba Madj wengi wengine wakiwa wametangulia mbele ya haki 
Disco la XTC ambalo maDj hawa wamepitia David , Lawrance , Pailonga, TNT Jackson

Disco la Valentinos/Continental haliwezi kutajwa bila ya watu hawa Ibrahim G ,Camal, Mr A, Salai, Meb, Guru, Sabry Kube

Disco la Rungwe 110 halijakamilika bila ya watu hawa Chogy Sly JP Pantelakis, Roma Pop Juice, Amon Washington, Agib Show, Ibony, Ntimizi, Bhester, Kim and the boyz, John Bure na wengineo
Image may contain: 5 people, including Muhidin Issa Michuzi, people smiling, people standing, stripes, beard and outdoor
Dj Sweet Francis jina kamaili ni Francis James Bundala,mwaka 1964 alianzisha bendi iliyoitwa The Screemers na Dj Sweet Francis akiwa mwimbaji(singer) hapo ndipo alipopewa jina la SWEET baada ya kusikia sauti yake na jinsi alivyokuwa akiimba iliwakuna sana na wakawa wanasema "YOUR VOICE IS SO SWEET " na ndiyo hapa akawa anaitwa Sweet. Hiyo ni hapa Dar.Bendi The Screamers ilidumu muda mfupi. Mwaka 1965 alianzish a bendi nyingine ya watu 5 wakaiita The Hot Five wakawa wanapiga bugi kila Jumapili mchana hapo Arnatoglo hall Mnazi mmoja. Wakawa wanashindana na bendi ilikuwa inaitwa The Flamming Star.

 Mwaka 1967 June The Hot Five ikavunjika. 1967 Sept. Dj Sweet Francis na aliyekuwa Solo guitarist wakaanzisha bendi nyingine wakapata watu wengine 3 ambao walianza kuwafundisha ambao walikuwa mpiga bass, mpiga rythym na drummer. Bendi wakaiita The TONICS. Mwimbaji- Sweet, Solo- Michael Jackson, Rythym- Green Jackson. Bass- John Morand na Drums- Charles Alowasa. 

Baada ya mazoezi makali mwezi November1967 wakaapata mkataba wa kupiga muziki kila siku hapo Splendid Hotel iliyokuwa inamilikiwa na mtaliano aliyeitwa MOSKA mtaa wa Samora zamani ukiitwa Independence Ave.

Siku moja wakati wanapiga muziki jamaa mmoja ambaye hawakuwa na mazoea naye akaja kwenye stage akaomba apige bongos wakamruhusu, wakati Dj Sweet Francis anaimba na yule jamaa akawa amapiga bongos vizuri sana Dj Sweet Francis akawaambia wenzake kuwa anafaa kuwa drummer lakini wenzake walimkatalia na baada ya kuwasihi sana walikubali kwa sharti kuwa amfundishe kupiga drums mpaka ajue. 
Image may contain: 10 people, including Ahmed Chande and Peter Moe, people smiling, people standing and outdoor
Baada ya kumfundisha kwa muda mfupi akaona ameelewa na baada ya kumpa nafasi kwenye stage alipiga drums na wenzangu wakamfurahia, huyo alikuwa anaitwa Adam Salehe Mwambile (R.I.P.) na tangu siku hiyo Dj Swett Francis akamwambia kuazia leo utaitwa ADDY SALLY,  ilikuwa mwezi April 1968, hilo ndiyo lilikuwa chimbuko la ADDY SALLY. 

May 1968 mkataba ulimalizika hapo Splendid  wakaamua kwenda mikoani.Wakati wote huo Dj Sweet Francis alikuwa mfanyakazi wa NPF sasa ni NSSF.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

VOA Swahili: Zulia Jekundu June 8th 2018

TBF YAOMBA WADAU KUSAIDIA KUFANIKISHA MICHUANO YA KANDA YA TANO YA VIJANA

$
0
0

Let's walk the talk members ...


Naomba kuwashirikisha wadau wote katika matukio yetu yajayo ya kikapu, naomba mjumuike nasi kufanikisha mashindano ya kimataifa ya kikapu ya kanda ya tano kwa timu za Taifa za vijana chini ya miaka 18 (FIBA ZoneV U18) 17-22 June 2018, yatakayofanyika hapa Dar es Salaam.
Kanda ya tano ina nchi 12 ; Egypt, Sudan, South Sudan, Eritrea , Ethiopia, Somalia, Djibouti, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania. Bingwa wa mashindano haya atapata tiketi ya kushiriki mashindano ya kutafuta bingwa wa Kikapu Mataifa ya Afrika (Afrobasket 2018). 
Tunahitaji fedha za kusaidia mashindano na kusaidia timu zetu za wanawake na wanaume kukaa kambini, jumla tunahitaji 100M. Corporate Sponsors karibuni na wachangiaji binafsi pia karibuni.
Makundi mbali mbali ya kijamii eg. WhatsApp groups, Telegram groups, Facebook groups, Google groups etc mnakaribishwa kuratibu na kuchanga kimakundi na mnakabidhi pamoja, Admins watakabidhi kwa niaba ya kila kikundi. 
Pamoja tunaweza, ahsanteni na Mungu awabariki wote kwa moyo wa upendo kwa vijana wetu na Taifa letu. 



Kwa mawasiliano na michango :
0713 /0784 /0767 618320. 
Phares Magesa, 
Rais, 
Tanzania Basketball Federation,

JESHI LA POLISI PWANI LATOA ZAWADI ZA IDDI NA KUFUTURISHA WATOTO YATIMA KITUO CHA KULELEA WATOTO FADHILA MISUGUSUGU

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
KAMANDA wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna,amewataka wananchi wenye uwezo kimaisha kutumia sehemu ya vipato vyao kuwezesha watoto yatima badala ya kuwaachia jukumu hilo wamiliki wa vituo vya kulelea watoto hao pekee.
Aliyasema hayo wakati jeshi hilo lilipojumuika katika Iftar ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Fadhila kilichopo eneo la Misugusugu Kibaha na kutoa zawadi ya sikukuu ya Eid el Fitr kwa watoto hao.
Alisema hakuna mtoto aliyependa kuwa yatima katika maisha yake ila kwa kuwa kifo ni wajibu kwa binadamu watoto hao wamejikuta wakiondokewa na wazazi wao.
"Hakuna ajuaye kesho yake ,watoto hawa hawakujua kama wangekuwa katika maisha haya ,ila ni kutokana na wazazi wao kufariki kwa sababu mbalimbali na kujikuta wamekuwa yatima" alisema kamanda Shanna.

Kamanda Shanna alieleza moja ya sababu zinazosababisha vifo ni ajali za barabarani ambazo nyingi hutokana na uzembe wa madereva kuyapita magari mengi bila ya kuchukua tahadhari na mwendo kasi.Alisema ajali hizo husababisha vifo na majeruhi hali inayopelekea tegemezi kupoteza wazazi wao jambo ambalo linaweza kudhibitiwa iwapo kila mmoja atashirikiana na jeshi la polisi kwenye kuwafichua madereva wasiotii sheria za usalama barabarani kwa makusudi. 
Kamanda huyo alisema, jeshi hilo kama chombo cha wananchi, limesukumwa kwa kurudisha fadhila za ushirikiano wanaopatiwa na wananchi katika kutanzua na kuzuia uhalifu .
"Tumeguswa kwa kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan kuja kufturisha watoto yatima ambao ni sehemu ya jamii yenye kuhitaji kutazamwa kwa karibu ili nao kujiona hawajatengwa na jamii inayowazunguka" alisisitiza. Aidha kamanda Shanna alitoa mbuzi, mafuta ya kula, sabuni za kufulia, unga, sukari na Mchele.
Kwa upande wake katibu wa kituo hicho Suraiya Mohammed, alilishukuru jeshi la polisi mkoa wa Pwani kwa kufuturu nao pamoja na zawadi ya sikukuu ya Eid el Fitr kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho .

Aliomba wasiishie katika mwezi mtukufu pekee bali wapatapo nafasi wafanye hivyo na kwa kipindi kingine kwani uhitaji wa msaada katika kuendesha kituo hicho kilicho na idadi ya watoto zaidi ya 150 ni mkubwa.
 Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna  akiongea machache kabla ya kukabidhi vitu mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Idd el Fitr kwa katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Fadhila kilichopo Misugusugu Kibaha, Suraiya Mohammed, wakati jeshi hilo lilipokwenda kufturu pamoja na watoto 150 wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna akikabidhi vitu mbalimbali kwa ajili ya sikukuu ya Idd el Fitr kwa katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Fadhila kilichopo Misugusugu Kibaha, Suraiya Mohammed, wakati jeshi hilo lilipokwenda kufturu pamoja na watoto 150 wanaolelewa kwenye kituo hicho.

MAFUNZO YA WISN NA POA YALIYOSHIRIKISHA MIKOA MINNE YAHITIMISHWA KWA MAFANIKIO.

$
0
0
Na. Andrew Chimesela, Morogoro

Mafunzo ya kubaini mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo unaojulikana kwa jina la kitaalamuWorkload Indicators of Staffing Needs - WISN na Prioritaization and Optimization analysis – POA (WISN plus POA)  yaliyoanza Juni 4 mwaka huu katika ukumbi wa ICE wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne– SUA Mkoani Morogoro yamehitimishwa Juni 8 kwa mafanikio makubwa.
Akiongea na washiriki wenzake wakati wa Kufunga mafunzo hayo Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu  Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Sebastian Masanja amewapongeza wakufunzi wa mafunzo hayo kwa kujitahidi kuwapa kile walicholenga kutoa hadi wao kuelewa  kwa ufanisi na kwa niaba ya wenzake ameahidi kwenda kuyafanyia kazi mafunzo hayo katika Halmashauri zao.
Bw. Masanja ambaye alikuwa mgeni rasimi katika kufunga mafunzo hayo amewataka washiriki wenzake kutambua kuwa hadi sasa watumishi wa Serikali hususan wa kada ya Afya bado hawatoshelezi kwenye vituo vya kutolea huduma, hivyo ni wajibu wao kutumia mafunzo waliyoyapata kuisaidia Serikali kuwapanga vizuri watumishi waliopo kulingana na uzinto wa kazi.
“Washiriki wenzangu, tumeshajifunza kuwa kituo cha Afya kilichopo Mjini hakiwezi kulingana majukumu yake na uzito wake wa kazi na kituo cha Afya cha kijijini, kwa sababu hata idadi ya wagonjwa inatofautiana, kwa hiyo tuisaidie Serikali kuondoa malalamiko  kwa kuwapanga vizuri watumishi waliopo kulingana na uzito wa kazi zinazopatikana kwenye maeneo husika” alisema Bw. Masanja.
Baadhi ya timu ya  viongoi wa mafunzo ya WISN PLUS POA wakiwa tayari kukabidhi vitabu vilivyoandaliwa kwa ajili ya kutekeleza kile walichojifunza washiriki wa mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Gracian Makota, Renatus Mashauri na Bw. Sebastian Masanja. Wengine ni wenyekiti wa washiriki wakati wa mafunzo na David Laput Mratibu wa PS 3 Mkoa wa Morogoro.
Bw. Sebastian Masanja ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala, Mkoa wa Kilimanjaro aliyefunga mafunzo hayo akimkabidhi vitabu Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya WISN PLUS POA SUA Mkoani Morogoro.  DSCN1936
Mgeni Ramsi aliyefungua mafunzo ya WISN PLUS POA Dkt. Frank Jacob (katikati waliokaa) ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mikoa ya Morogoro na Dodoma yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

MBWANA SAMATTA AIPONGEZA KAMPUNI YA MAZIWA YA ASA

$
0
0
MCM_8385
Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta anayecheza soka lake nchini Ubeligiji katika klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta ameipongeza kampuni ya kuuza maziwa ya Asas Dairies kwa kujitokeza kudhamini kampeni yake ya “Nifuate”.
Kampeni hiyo ilikutanisha timu mbili, timu Samatta na timu-Kiba ambazo ziliwajumuisha mastaa wengine wengi wa soka la Tanzania, muziki na waigizaji.
Aizungumza jijini, Samatta alisema kuwa wazo la kuanzisha kampeni hiyo alilichukulia kama utani tu, lakini kampuni hiyo na wadau wengine wameamua kuunga mkono na kuwa suala la Kitaifa.Samatta alisema kuwa kampuni hiyo na wadau wengine wameonyesha jinsi gani wanavyojali maslahi ya Taifa na kuahidi kushirikiana nayo katika kampeni nyingine mbalimbali.
MCM_8448
“Kwa kweli nawashukuru wadhamini kwa sapoti yao kubwa katika kampeni hii ambayo lengo lake kubwa ni kutatua changamoto za elimu nchini, huu ni mwanzo tu, kwani natarajia kufanya mambo mengine makubwa kwa jamii hapo baadaye,” alisema Samatta.
Alisema kuwa anatarajia kupata mafanikio makubwa katika kampeni hiyo ambayo ilifanyika kwa mara ya kwanza katika historia.
“Lengo si kupata fedha, lengo ni kuchangia na tupo tayari kupokea chochote kutoka kwa wadau ambacho kitaisaidia maendeleo ya elimu hapa nchini. Tutaendelea kupokea misaada hata baada ya mechi,” alisema.

Waziri Mkuu atoa maelekezo kufufua michezo nchini

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG 
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema hali ya kiwango cha michezo nchini si ya kuridhisha hivyo lazima wanamichezo kuanzia shule za awali, msingi, sekondari pamoja na vyuo waandaliwe vyema. 
 Waziri Majaliwa aliyasema hayo jana katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza wakati akifungua rasmi Mashindano ya Umoja wa Michezo kwa shule za Sekondari nchini UMISSETA, ulioambatana na pia na ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za Msingi UMITASHUMTA. 
 Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella alitoa pongezi kwa viongozi na wadau wote wakiwemo wadhamini wakuu kampuni ya Cocacola kwa kufanikisha maandalizi ya michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA inayofanyika kwa mwaka wa tatu mfululizo Jijini Mwanza ambapo mwakani michezo hiyo itafanyika Jijini Dodoma.

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AFUTURISHA JIJINI MWANZA, AWATAKA WATANZANIA WASIKUBALI KUCHONGANISHWA

$
0
0
 Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasikubali kuchonganishwa na kwamba Serikali haiongozwi kwa misingi ya kidini bali imeziachia taasisi za kidini zifanye kazi kwa kuzingatia Katiba , Sheria za nchi na malengo yaliyokusudiwa katika uanzishwaji wake. 
 Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Juni 9, 2018) alipozungumza na viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mwanza baada ya kushirikiana nao katika futari aliyowaandalia. Shughuli hiyo ilihudhuriwa na waumini wa dini mbalimbali. 
 Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa amani na utulivu, jambo litakalowawezesha kufanya shughuli zao kikamilifu, hivyo wasikubali kuchonganishwa kwa misingi yoyote. 
 “Nawaasa viongozi wa dini msikubali kutumia makundi mengine nje ya taasisi zenu kwa ajili ya kuwazungumzia masuala yenu kwa sababu watawachonganisha na Serikali ambayo haipo kwa ajili ya kugombana na taasisi yoyote,” alisisitiza. 
 Waziri Mkuu alisema jukumu kubwa la taasisi za kidini ni kuhakikisha wanawalinda waumini wao pamoja na kuwaongoza kwa kuwapa mafundisho mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu, ambayo yatawawezesha kuishi kwa amani . 
 Alisema misingi ya amani na utulivu ikiwa pamoja na mshikamano walionao wananchi umesababisha Tanzania kupata heshima kubwa dunia kote, hivyo ni vema kila mwananchi ahakikishe suala la kudumisha amani linapewa kipaumbele. 
 Pia Waziri Mkuu alisema amefurahi sana kujumuika na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika futari hiyo, ambapo aliwapongeza kwa kukamilisha uundaji wa kamani za amani kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa.
 Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella amlishukuru Waziri Mkuu kwa ukarimu wake kwa kuwaalika wakazi wa Mwanza katika hafla hiyo, ambapo alisema Mwanza ni kitovu cha amani kwa kanda ya Ziwa na nchi za Maziwa Makuu. T
 “Mwanza tumejipanga na tunashirikiana na taasisi zote kwenye njanja zote , tupo pamoja na tunashirikiana katika kuimarisha amani na utulivu. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli kwa kutuamini na tunamuahidi tutafuata falsafa zake katika utendaji wetu,”. 
 Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza na Askofu wa Kanisa la Charismatic Episcopal Church of Tanzania (CECT), Charles Sekelwa alisema wao wanaiunga mkono Serikali katika kudumisha amani na wataendelea kushirikiana nayo. 
 Alisema awali kulikuwa na changamoto ya matabaka ya kidini iliyobabisha na kutoelewana baina ya waislamu na wakiristo, ambapo kamati yao ilifanya kazi ya kuyasulisha na sasa hali ni shwari. “Matabaka ya kiimani yameisha na watu wa dini zote wanashirikiana vizuri,”
Askofu Sekelwa alisema wao kama viongozi wa pande hizo mbili hawawezi kukubali kuona kunakuwa na matabaka ya kiimani miongoni mwa waumini, hivyo watakikisha wanaendelea kuwafundisha waumini wao umuhimu wa amani. 
 Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Akson, Naibu Waziri waNchi, OR – TAMISEMI, Joseph Kakunda, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mwanza
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha wakati alipowasili kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza kushiriki katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Juni 9, 2018. 
 Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika futari aliyoiandaa kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofuturisha kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika dua iliyoongozwa na Sheikh Khamis Almasi (wanne kushoto) baada ya kufuturisha kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI, Joseph Kakunda, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Jamal Abdul Babu na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani inayojumuisha  viongozi wa dini zote ya mkoa wa Mwanza, Askofu Charles Sekelwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akigana na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani inayojumuisha viongozi wa dini zote ya mkoa wa Mwanza, Askofu Charles Sekela baada ya kufuturisha kwenye viwanja vya Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri TAMISEMI, Charles Kakunda na  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Sheikh Khamisi Almasi. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu baada ya kufuturisha kwenye viwanja vya  Benki Kuu jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa atembelea kampuni ya Tanzanice Agrofood ltd ya Mkoani Njombe

$
0
0
 Makamu wenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo,Mifugo na Maji Dkt.Christine Ishengoma(kushoto) akiangalia kwa makini kifungashio cha parachichi zinazozalishwa na kupakiwa na kampuni ya Tanzanice Agrofood Ltd.  ya Mkoani Njombe. walipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya ziara ya kamati hiyo kutembelea na kujifunza maeneo ya kilimo yanaratibiwa na Kituo ch Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania(SAGCOT). Kulia ni Contract farming Manager wa Kampuni hiyo Bw.Noel Lugenge
 Naibu Waziri wa Kilimo Dkt.Mary Mwanjelwa(wapili kulia) akiwa ameshika parachichi pamoja na Makamu wenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo,Mifugo na Maji Dkt.Christine Ishengoma(wapili kushoto)
walipotembelea Kampuni ya Tanzanice Agrofood Ltd. Mkoani Njombe inayokusanya na kupatia zao hilo kwa kusafirisha katika masoko ya nje ikiwa ni sehemu ya ziara ya kamati hiyo kutembelea na kujifunza maeneo ya kilimo yanaratibiwa na Kituo ch Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania(SAGCOT). kushoto ni Contract farming Manager wa Kampuni hiyo Bi.Rebeca Hepelwa
 Naibu Waziri wa Kilimo Dkt.Mary Mwanjelwa(wapili kulia) akiwa ameshika mche wa parachichi akiwa  na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo,Mifugo na Maji Dkt.Christine Ishengoma walipotembelea Kampuni ya Tanzanice Agrofood  Ltd. Mkoani Njombe inayokusanya na kupakia zao hilo kwa kusafirisha katika masoko ya nje.

JAFO AKERWA NA KUSUASUA KWA UJENZI WA KITUO CHA MABASI MJI WA NJOMBE

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameonyesha kukerwa kutokamilika kwa ujenzi wa kituo cha mabasi cha mji wa Njombe licha ya serikali fedha zote za gharama ya ujenzi huo  zaidi ya  Sh. bilioni 10.  


Ujenzi wa kituo hicho ulianza tangu Desemba 2013 lakini hadi sasa haijakamilika.

Kufuatia hali hiyo, Waziri Jafo amemjia juu mkandarasi aliyepewa kazi hiyo pamoja na upande wa usimamizi wa ujenzi huo na kudai kuwa umechelewa kukamilika kutokana na uzembe wao. 


“Hapo awali kazi hiyo ilikuwa ikifanywa na MASASI CONSTRUCTION kwa kujenga awamu ya kwanza na ya pili ambapo katika awamu hizo  zimekamilika lakini kwa kuchelewa sana na kulazimika kutafutwa mkandarasi mwingine ili akamilishe awamu ya tatu ambayo ni ya mwisho kwa mradi huo,”amesema.



 Amebainisha kuwa awamu ya tatu Halmashauri ya mji wa Njombe wamempata mkandarasi mpya ambaye ni kampuni ya HAINAN INTERNATIONAL na amesaini mkataba mwezi Mei 2018 na anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo mwezi Februari 2019.



Jafo amewaonya wakandarasi ambao wanachukua kazi lakini wanapopewa kazi wanaleta ubabaishaji katika kukamilisha kazi hizo. 



Amemuagiza mkandarasi huyo mpya kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma bora kama serikali ilivyokusudia.



Waziri Jafo, kabla ya kutembelea kituo hicho, alisimamia harambee ya kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule ya sekondari Makoga iliyopo wikayani Wanging’ombe ili iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano hapo mwezi Julai 2018.


Katika harambe hiyo kiasi cha sh.Milioni 137 zilichangwa na wananchi wa Wanging'ombe na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Mkoa wa Njombe.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo   akisisitiza jambo kwa wakandarasi wapya wanaojenga Kituo cha mabasi cha Mji wa Njombe.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo  akitoa maelekezo kwa viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha mabasi.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo  akisikiliza taarifa ya ujenzi wa Kituo cha mabasi.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo   akipanda mti wa Matumaini kabla ya Harambee ya shule ya Makoga mkoani Njombe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo  akiendesha zoezi la Harambee katika wilaya ya wanging'ombe kwa ajili ya sekondari ya Makoga.

ULEGA AWAASA WANA-CCM MKURANGA KUUSEMEA UTEKELEZAJI WA ILANI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga 
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ,Abdallah Ulega, amesema anaandaa mpango mkakati utakaowezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda kwa kishindo katika chaguzi za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020. 
 Aidha amewatoa shaka wanaCCM wilayani hapo kwa kudai ushindi utapatikana kwani ahadi na ilani ya CCM inatekelezwa hivyo wapinzani hawana pa kupenya. Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, aliyasema hayo wakati akiongea na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Mkuranga . 
 Alisema, chama kipo imara na halmashauri kuu ya CCM wilaya ndiyo jeshi namba moja la kuhakikisha ushindi huo unapatikana katika chaguzi hizo. 
 "Msikae kimya ,kila mwanachama na kiongozi kuanzia ngazi za chini ni jukumu letu kushirikiana kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali yetu na utekelezaji wa ilani"alisema. 
 Ulega alisisitiza umoja na ushikamano na kuacha kuyapa nafasi makundi ambayo hayana tija katika mustakabali wa kukiimarisha chama hicho. Alieleza anatambua changamoto ambazo bado zinalikabili jimbo hilo hivyo ataendelea kupambana nazo . 
 Ulega alisema kuwa, yapo maeneo yenye changamoto kama za miundombinu ya barabara kukatika baada ya mvua kupita ambapo tayari zipo fedha za baadhi ya maeneo ,na kinachosubiriwa ni utekelezaji wa wakandarasi. 
 Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo alisema ,ataendelea na jitihada zake na kushirikiana na wadau wa maendeleo kupunguza kama sio kumaliza kero ambazo bado zipo katika baadhi ya maeneo ikiwemo elimu ,afya na masuala ya kijamii. Pia kwa kuzingatia mwezi mtukufu wa Ramadan na unakaribia kumalizika alikabidhi zakatulfitry kwa wajumbe waliohudhuria.
 Mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza jambo na wajumbe wa halmashauri kuu CCM Wilaya ya Mkuranga
Mbunge wa jimbo la Mkuranga  na Naibu Waziri wa Mifugo Mhe. Abdallah Ulega akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ,Ally Msikamo kwa niaba ya wajumbe wa halmashauri kuu CCM Wilaya katika muendelezo wake wa kutambua thamani ya Chama kwa kugawana na wana CCM wenzake kidogo anachopata. Picha na Mwamvua Mwinyi

TUPENDE VYA NYUMBANI VILIVYO HALISI NA VYENYE UBORA WA KIMATAIFA

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images