Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


KIGWANGALLA AFUTURISHA WABUNGE DODOMA, ASISITIZA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO WA KITAIFA

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefuturisha wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika makazi yake yaliyopo Area D Jijini Dodoma.

Futari hiyo ilihudhauriwa na wabunge mbalimbali wa chama tawala CCM na wa vyama vya upinzani wakiongozwa na Spika, Job Ndugai na Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson.

Dkt. Kigwangalla aliwashukuru wabunge wote waliohudhuria hafla hiyo na kusema kuwa imelenga kudumisha upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa uliopo baina ya wabunge hao bila ya kujali mipaka ya vyama vyao hususan katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

"Nimefarijika sana kuwapokea waheshimiwa wabunge wenzangu hapa nyumbani kwangu, ninawashukuru sana kwa kuja maana shughuli ni watu, tuliandaa futari nyingi kwa ajili ya wabunge wote, sasa msingefika tungepata mtihani ni wapi pa kuipeleka. "Hafla kama hii ya Iftar inatuunganisha sisi sote bila kujali dini zetu, inajenga na kudumisha upendo, mshikamano na umoja wetu wa kitaifa bila kujali mipaka ya vyama vyetu" alisisitiza Dkt. Kigwangalla. 

Alisema zamani kulikuwa na utamaduni wa watu kufuturu nje ya nyumba zao ili wapita njia au majirani wakikuta wanafuturu nao wanajumuika, "Siku hizi tumeanza kufuturia ndani kila mtu na familia yake, basi siku moja moja kama hivi inatokea tunaamua kuukumbuka utamaduni wetu na kualikana kufuturu pamoja" alisema. 

Kwa upande Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikua mgeni rasmi kwenye hafla hiyo, Job Ndugai alimpongeza na kumshukuru Dkt. Kigwangalla kwa kuandaa hafla hiyo na kusema kuwa inajenga mshikamano baina ya wabunge bila kujali itikadi za vyama na dini zao. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai nyumbani kwake kwa ajili ya kujumuika na wabunge wengine kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili yao nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum, Janeth Massaburi akimuombea dua Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla katika hafla ya futari aliyoiandaa jana kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson kwanye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mama Salma Kikwete kwenye hafla ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya wabunge nyumbani kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (wa tatu kulia) akizungumza na baadhi ya wabunge kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla nyumbani kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao aliwaalika kwenye futari ya pamoja nyumbani kwake Jijini Dodoma.

WAZIRI MWIGULU ASEMA KWA SIMBA ILIPOFIKA ANAIPA BARAKA ZA USHINDI FAINALI YA SPORT PESA ILA...

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.Mwigulu amesema kwa sasa anachoweza kukielezea kwa timu ya Simba anamuomba Mungu aifanikishe timu hiyo kuhsinda mchezo wa fainali wa michuano ya Sport pesa dhidi ya timu ya Gor Mahia ya nchini Kenya.

Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wametinga fainali ya michuano hiyo na kesho Jumapili watacheza mchezo wa fainali ya michuano hiyo na timu ya Gor Mahia ya Kenya.

Akizungumza na Michuzi Blog jijini Dar es Saalam jana Dk.Mwigulu amesema amefurahi Simba kuingia fainali na sasa anatoa baraka ili ishinde kombe la michuano hiyo.

Michuzi Blog baada ya kukutana na Waziri Mwigulu pamoja na mambo mengine ilitaka kufahamu nini kauli yake kwa Simba inayosubiri kucheza fainali hiyo."Kwangu niseme tu naipa baraka zote timu ya Simba ili ishinde kombe la michuano hiyo.Hiki ndicho nachoweza kukielezea kwa sasa.

"Mashabiki wa soka nchini Kenya baada ya mwaka jana moja ya timu yao kuchukua kikombe hicho walitoa maneno ya kutubeza sana lakini tunaka kuonesha tupo vizuri.Hata hivyo nilitamani sana Simba icheze fainali na Singida United lakini imeshndikana,"amesema.

Alipoulizwa kwanini alitamani Simba icheze fainali hiyo na Singida United akafafanua maana yake ni moja tu kombe la michuano hiyo lingebaki Tanzania kwa asilimia 100.

"Fainali ingekuwa kati ya Singida United na Simba tungekuwa na uhakika tayari kombe la michuano hiyo ni la kwetu maana timu yoyote ambayo ingelichukua ilikuwa inaleta kombe nyumba,"amesema Dk.Mwigulu.

Mashabiki wa soka nchini Tanzania na hasa mashabiki wa Simba wameonesha matumaini makubwa na timu yao kuwa itaibuka mshindi na kuchukua kombe hilo.

WAZIRI MKUU ATAKA WANAOTOA TAARIFA ZA UONGO WADHIBITIWE

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wawachukulie hatua kali wananchi wote wanaotumia vibaya namba za mawasiliano za jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu matukio ya majanga ya moto.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kuendelea kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na kupambana na majanga ya moto pindi yanapotokea katika maeneo yao.

Pia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuwa na magari ya zimamoto pamoja na magari ya kubeba wagonjwa kwenye vituo vyote vya Zimamoto na Uokoaji katika maeneo yao.Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Juni 8, 2018) wakati alipofanya ziara katika Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura ya Maafa pamoja na Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha mkoa wa Ilala.

Amesema ili kudhibiti wananchi wanaopiga simu za kuomba msaada wa kutaka kuokolewa, huku kukiwa hakuna tukio lolote la janga la moto lililotokea kwenye maeneo yao, ni vema watu hao wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye kumweleza baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na wananchi kupiga simu wakidai kuna ajali ya moto imetokea katika maeneo yao na baada watu wa uokoaji kufika wanabaini ni uongo.

Muogeleaji Natalia atamba kushinda mashindano ya kuogelea ya Marekani

$
0
0
Dar es Salaam. Muogeleaji wa Tanzania, Natalia Ladha ametamba kufanya vyema katika mashindano ya kuogelea ya kutafuta tiketi ya kufuzu kwa mashindano ya Olimpiki ya jimbo la Florida nchini Marekani yajulikanayo kwa jina la Florida Gold Coast Junior Olympic.

Natalia aliondoka nchini jana tayari kwa mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika Martin County Juni 16 ambapo atajiunga na waogeleaji wa klabu ya Swimfast.

Muogeleaji huyo ambaye ni nyota kwa waogeleaji wa Tanzania wenye umri kati ya miaka tisa na 10, anashindana katika mashindano hayo makubwa matano Marekani kwa mara ya pili mfulilizo.

“Nimejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na natarajia kufanya vyema kwa waogeleaji wenye umri kama wangu, nimejiandaa vyema katika nikiwa na makocha wangu wa klabu ya Taliss,” alisema Natalia.

Katika mashindano yam waka jana ya Miami, Natalia alishinda medali ya shaba kwa mita 50 na 100 kwa upande wa staili ya backstroke.

Natalia pia alitamba katika mashindano ya staili nyingine ambapo alitwaa medali ya dhahabu kwa mita 200 freestyle, 200 ( individual medley), 100m (backstroke),50m (butterfly) na medali ya fedha kwa mita 100 katika staili ya butterfly. Pia alishinda medali ya dhahabu kwa mita 100 katika freestyle.

Mbali ya mashindano hayo, Natalia pia atashiriki katika mashindano ya umri ya Coral Spring ambayo yataanza Juni 15 na kumalizika Juni 17 na vile vile mashindano ya Fort Lauderdale yaliyopangwa kuanza Juni 22 mpaka 24.

Vile vile atashiriki katika mashindano ya Sectionals, yaliyopangwa kuanza Julai 6 mpaka 9 ma Area championships yaliyopangwa kuanza Julai 13 mpaka 15, mjini Sunrise.

MAJALIWA ATEMBELEA OFISI ZA MPIGA CHAPA WA SERIKALI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

PMO_5761
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mitambo ya kwanza ya Mpiga  Chapa wa Serikali uitwao  Original Heidelberg wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam Juni 8, 2018. Mtambo huo wenye zaidi ya miaka 100 bado unafanya kazi vizuri.
PMO_5776
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa Bw. Mohammed  S. Mohammed (kulia) ambaye ni Mtalaam na mwendeshaji  mkongwe wa mitambo ya uchapaji kuhusu jarada lililochapwa na mtambo uitwao Original Heidelberg wenye umri wa zaidi ya miaka 100 wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018
PMO_5823
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kuhusu mtambo unaochapa majarada ya serikali kutoka kwa Kaimu Mpiga Chapa wa Serikali, Bw. John Kaswalala (kushoto) wakati alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Der es salaam, Juni 8, 2018. Mtambo huo wenye zaidi ya miaka 100 bado unafanya kazi vizuri . Kulia ni mwendeshaji wa mtambo huo, Dismas Shayo.
PMO_5863
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akikagua moja ya karatasi zenye nembo na maadishi yasioonekana kwa macho ya kawaida  kwenye  Kitengo cha Digitali wakati  alipotembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018.  Katikati ni Kaimu Mpiga Chapa wa Serikali, John Kaswalala na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Digitali, Ali Machupa.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

HAJI MANARA AZUNGUMZIA MCHEZO WA SIMBA NA GOR MAHIA FAINALI ZA SPORTPESA KESHO

SERIKALI YASHAURIWA KUKABILIANA NA UKOSEFU WA USAWA KATIKA ULIPAJI KODI

$
0
0

Sehemu ya washiriki toka vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia makundi ya wanafunzi na vijana uliofanyika Tarehe 7 hadi 8 jijini Dar es Salaam wakifuatilia matukio wakati wa warsha iliyojadili maswala ya usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma. 
Mmoja wa washiriki akitoa mchango wake katika warsha iliyojadili maswala ya usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU), Rashid Mtima (wa tatu kulia) akiwaongoza wajumbe wa warsha ya siku mbili iliyojadili usawa katika ulipaji wa kodi na manufaa yake katika kuboresha huduma za umma wakiimba wimbo wa ‘Mshikamano Daima’ wakati wa ufungaji wa warsha hiyo jijini Dar es Salaam. Walipendekeza serikali kupitia upya misamaha na mikataba ya kodi, kuwepo uwazi wa umiliki na faida wanazopata makampuni mbalimbali kuongeza uwezo wa TRA ili ikusanye mapato na fedha zitakazowezesha kujenga miundombinu na kuboresha huduma kwa umma. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs).

HABARI ZAIDI SOMA HAPA

POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro

POLISI mkoani Morogoro inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu mwanamke aliyejifungua mtoto wakati akiwa njiani kupelekwa Kituo cha Afya Mang’ula, wilaya ya Kilombero mkoani humo mara baada ya kutolewa mahabusu ili kubaini kama kuna uzembe wowote umefanywa na watendaji ama askari na ikibainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Mugabo Wekwe alisema hayo katika taarifa yake kwa waandishi wa habari juu ya tukio la kujifungua mtoto njiani mwanamke Amina Rafael Mbunda (27) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa , Tarafa ya Mang’ula , wilayani Kilombero , mkoa wa Morogoro.
Alisema , Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio la mwanamke huyo aliyefikishwa katika kituo cha Polisi Mang’ula kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi kisha kujifungua akiwa njiani kuelekea katika Kituo cha Afya Mang’ula.
Alisema , Mei 31, mwaka huu ilifunguliwa kesi ya wizi wa samani mbalimbali zenye thamani ya Sh 1,040,000 katika kituo cha Polisi Mang’ula kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro zilizoibwa kwa vipindi tofauti katika karakana ya Joseph Mdee iliyopo maeneo ya Posta Mang’ula .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huyo alisema, baada ya tukio uchunguzi ulianza mara moja na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja alitwaje Ridhiwani Athuman na kukiri kuiba kisha kuwauzia watu mbalimbali akiwemo Abdallah Mohamed Mrisho (40) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa Tarafa ya Mang’ula.

RC MAKONDA AFUTURISHA MAMIA YA WANANCHI DAR, AOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKUU wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini kuendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli kwani anafanya kazi ngumu na kitu pekee ni kuendelea kumuombea. 
Amesema kwa nafasi ya Rais wapo ambao wanampenda na wapo ambao wanakasirishwa lakini cha msingi ni kuongeza maombi na Dia kwa Rais wetu huku akihimiza umoja na mshikamano. Makonda ametoa kauli hiyo leo jioni hii katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam kabla ya futari maalum ambayo ameiandaa kwa mamia ya wakazi wa Mkoa huo. 
Amesema viongozi wa dini wana nguvu kubwa na ndio maana watu wanakwenda Kanisani, watu wanakwenda Msikiti na kueleza nguvu hiyo itumike kushirikiana na Serikali. Hivyo ameomba viongozi wa dini kuendelea kumuombea Rais Dk.John Magufuli ili aweze kulitumikia Taifa na kusisitiza nafasi anayoitumikia Rais ni kubwa na inahitaji maombi. 

"Rais wetu anafanya kazi kubwa, na dua za viongozi wa dini ni muhimu ili aweze kulitumikia vema taifa letu. Kama mimi kwa nafasi yangu napigwa mawe hivi je kwenye nafasi ya Rais itakuaje? "Rais wetu anapongezwa na mataifa mengi kwa kazi nzuri anayoifanya na kwa hapa nchini wapo wanaopongeza kwa nguvu zao zote na wapo wanaomkasirikia. 

"Sishangai wakitokea wa kubeza na ukwel ni kwamba wabadharifu wa fedha za umma hawawezi kufurahia, "amesema Makonda. Akizungumza siku ya leo kutokana na kuandaa futari hiyo Makonda amesema wapo viongozi wa dini mbalimbali, viongozi wa vyama vya siasa na makundi mbalimbali. 
 Amesema anamshukuru Mungu kwa wananchi wote bila kujali dini zao wanaungana katika mwezi wa Ramadhan kuuheshimu.Amesema hakuna imani ya dini ambayo ameihasau kwani wote wamejumuika kwenye futar hiyo na kubwa zaidi ni kwamba hiyo inaonesha umoja na mshikamano Katika Mkoa wa Dar es Salaam. 

Amefafanua ktika futari hiyo kuna makundi mbalimbali wakiwamo wacheza mpira,wasanii wa Bongo Fleva, watu mashuhuri, na kila aina ya makundi ya wananchi. Makonda amesema kumewepo na tofauti katika baadhi ya watu ambapo amefafanua jambo kubwa kwa Mkoa wa Dar es Salaam viongozi wa dini zote na waumini wote wamebaki kuwa wamoja. 

Amesema wakazi wa Dar es Salaam hawana muda wa kulumbana katika mambo ya kidini kwasababu wameamua kuwa wamoja.Ameongeza katika kuhakikisha watoto waishio kwenye mazingira magumu nao kupata futari ameamua kuwapelekea huko huko wanakolelewa. 
"Leo hii kwenye futar hii wote tumependeza kutokana na mavazi nadhifu na kwa umoja uliopo huwezi kujua kati ya Sheikh na ambaye si Sheikh. Hili ni jambo jema na kwangu linanifariji. Ameeleza Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa umefikia watu milioni sita na Wilaya ya Temeke ndio inaongoza kwa idadi ya watu. 
Amefafanua idadi ya watu iliyopo inachangamoto zake kwani ongezeko la watu linachangia kuibuka kwa changamoto nyingine za kijamii.

MICHUZI TV: DKT. MWIGULU AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI IDARA YA SHERIA NA MSAJILI WA JUMUIYA ZA KIDINI

BALOZI MUHIDINI ALLY MBOWETO AKABIDHI HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS BUHARI WA NIGERIA JIJINI ABUJA

$
0
0
Mnamo Juni 7, 2018 Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Muhidini Ally Mboweto, alikabidhi Hati za Utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria Mhe. Muhammadu Buhari katika Ikulu ya nchi hiyo Jijini Abuja na kuhudhuriwa na mke wa Mhe. Balozi Hajat Ashura Ally Mboweto, Maafisa wa Ubalozi na viongozi mbalimbali wa serikali ya Nigeria.
C:\Users\Elias\Desktop\Mhe. Kukabidhi Hati\Amb Tan (4).JPG
Mhe. Balozi akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wa jeshi la Nigeria kabla ya kukabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria Mhe. Muhammadu Buhari katika Ikulu ya nchi hiyo Jijini Abuja

C:\Users\Elias\Desktop\Mhe. Kukabidhi Hati\Amb Tan (5).JPG
                            Mhe. Balozi Mboweto akikagua gwaride kabla ya kukabidhi hati Hati za Utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria Mhe. Muhammadu Buhari katika Ikulu ya nchi hiyo Jijini Abuja
C:\Users\Elias\Desktop\HC Tanzania\Amb Tan (27).JPG
Mhe. Balozi akielekea kwenye ukumbi wa Ikulu baada ya kukagua gwaride.Mhe. Rais Buhari akiwa na Waziri wa nchi (Mambo ya Nje) na Katibu wa Rais akimsubiri Mhe. Balozi.
C:\Users\Elias\Desktop\HC Tanzania\Tan  (1).jpg
  Mhe. Balozi akikabidhi Hati kwa Mhe Rais Buhari
C:\Users\Elias\Desktop\HC Tanzania\Tan  (4).jpg
Mhe. Balozi  akiwa katika mazungumzo ya falagha na Mhe. Rais Buhari baada ya kukabidhi hati za utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria Mhe. Muhammadu Buhari katika Ikulu ya nchi hiyo Jijini Abuja.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

UZINDUZI WA PASIPOTI YA KIELEKTRONIKI MKOA WA KAGERA WAFANA

$
0
0
Na Abdullatif Yunus wa  Globu ya Jamii, Kagera
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  wa Kagera kupitia Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kagera imezindua rasmi pasipoti ya kielektroniki kwa wananchi na wakazi wa Mkoa huo. Tayari pasipoti hizo zimeanza kutolewa tarehe Junin7, 2018 katika hafla  iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya, maafisa kutoka jeshi la Uhamiaji, viongozi wa dini, wananchi na wadau wa Idara ya Uhamiaji katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.
Katika hotuba yake Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu iliyotolewa na mwakilishi wake Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Mh. Deodatus Kinawiro, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma hii ya pasipoti huku akitaja faida lukuki za kuwa na pasipoti ya aina hii. miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kukidhi matakwa ya usalama wa Nchi, na pia kukidhi viwango vinavyopendekezwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia mambo ya anga.
Kwa mujibu wa idara ya Uhamiaji mpaka sasa tayari Jeshi la Uhamiaji limekwishatoa jumla ya pasipoti 17,598 zikiwemo pasipoti za kawaida, Utumishi, Diplomasia, na Diplomasia maalum tangu zoezi hili lilipozinduliwa Rasmi mapema Januari 31 mwaka huu, na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
​Muonekano wa viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga, katika uzinduzi wa pasipoti ya kielektroniki Mkoani Kagera m ​apema Juni 8, 2018.
Kamishna wa pasipoti na Uraia afande Gerlad Kihiga amesema katika hafla hiyo kwamba pasipoti hiyo imetengenezwa kwa viwango na ubora wa hali ya juu na haiwezi kugushiwa kitrahisi kwani ina kifaa maalumu ndani yake hivyo itamsaidia msafiri  kutumia E-gates pasipo kuweka msongamano, ikiwa na mfanano wa pasipoti nyingine za Afrika mashariki hivyo unaweza kupata usaidizi ubalozi wowote  katika nchi wanachama, na huku tahadhari ikitolewa kwa wale ambao huwasaidia raia ambao si watanzania kupata pasipoti, kwa atakaebainika pasina kujali ni atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa wale wanaotumia simu janja tayari ipo app ya pasipoti ambayo mwananchi yeyote anaweza kupakua app hiyo katika simu yake na kujaza taarifa zake, au kuangalia taarifa zake.
 ​Sheikh wa Mkoa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta akiomba dua wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.
 Askofu Msaidizi Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini akiomba sala wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.

  Kamishna wa pasipoti na Uraia afande Gerlad Kihiga akikabidhi pasipoti ya kwanza Kagera kwa Mkuu wa Wilaya Mh. Deodatus Kinawiro kwa niaba ya mgeni rasmi katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Mh. Deodatus Kinawiro akimkabidhi pasiposti Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bukoba Ndg. Zachwa katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba akikabidhi Pasipoti kwa Askofu Mkuu wa jimbo la Bukoba Desderius Lwoma katika viwanja vya Uhuru platform maarufu kwa Mayunga mjini Bukoba. 
Picha na Abdullatif Yunus wa  Globu ya Jamii, Kagera

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA: Wajumbe wapya watano wachaguliwa Baraza la Usalama UN

VOA Swahili: mkutano wa kampuni ya Facebook, wawekezaji wakielezea jinsi wanavyotaka mambo yatendeke


RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEINA ZUNGUMZA NA VYAMA VYA UPINZANI LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na viongozi wa Vyama vya Upinzani katika mkutano wa ushauriano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar(wa nne kushoto) Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe.Ibrahim Haruna Lipumba
 Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Mhe.Magalie John P.Shibuda alipokuwa akitoa mchango wake katika Mkutano wa kushauriana na Vyama vya Upinzani pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) uliofanyika leo  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) katika  picha ya pamoja na  Vyama vya Upinzani baada ya  mkutano wa pamoja wa ushauriano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na  Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania Mhe.Magalie John P.Shibuda   wakati wa  Mkutano wa kushauriana na Vyama vya Upinzani  uliofanyika leo  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na  Mwenyekiti wa CUF Taifa Mhe.Ibrahim Haruna Lipumba,  wakati wa  Mkutano wa kushauriana na Vyama vya Upinzani  uliofanyika leo  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. 
Picha na IKULU.

MICHUZI TV: MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHA MKOA WA ILALA, ENEO LA FIRE JIJINI DAR

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wawachukulie hatua kali wananchi wote wanaotumia vibaya namba za mawasiliano za jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu matukio ya majanga ya moto. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini kuendelea kutoa mafunzo kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na kupambana na majanga ya moto pindi yanapotokea katika maeneo yao. Pia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuwa na magari ya zimamoto pamoja na magari ya kubeba wagonjwa kwenye vituo vyote vya Zimamoto na Uokoaji katika maeneo yao.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Juni 8, 2018) wakati alipofanya ziara katika Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura ya Maafa pamoja na Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha mkoa wa Ilala. Amesema ili kudhibiti wananchi wanaopiga simu za kuomba msaada wa kutaka kuokolewa, huku kukiwa hakuna tukio lolote la janga la moto lililotokea kwenye maeneo yao, ni vema watu hao wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,  Thobias Andengenye kumweleza baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na wananchi kupiga simu wakidai kuna ajali ya moto imetokea katika maeneo yao na baada watu wa uokoaji kufika wanabaini ni uongo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aziagiza Halmashauri zote nchini kuwa na magari ya zimamoto pamoja na ya kubebea wagonjwa kwa ajili ya kutoa huduma pindi majanga yanapotokea kwenye maeneo yao ili kuharakisha utoaji wa huduma za dharura.

Pia amelitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kila Mtanzania aweze kuwa na uelewa wa kutoa huduma za awali pindi majanga ya moto yanapotokea katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutumia vifaa vya kuzima moto.

Waziri Mkuu ambaye alitembelea kituo cha Jeshi la Zimamoto cha Ilala amejionea magari ya kuzimia moto likiwemo la aina ya Bronto Sky Lift lenye uwezo wa kufika futi 54 na kuzunguka nyuzi 360. Alielezwa kuwa katika Bara la Afrika, magari ya aina hiyo yapo matatu tu, ambayo yapo nchini Tanzania, Misri na Afrika Kusini. Kwa upande wa Tanzania, gari hilo lilinunuliwa miaka 10 iliyopita kwa sh. bilioni 1.5.  

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitembelea Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura ya Maafa, ambapo aliwasisitiza viongozi wa kituo hicho kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara yatokanayo na kuishi kwenye maeneo hatarishi hususan mabondeni.

Waziri Mkuu alisema licha ya kuwapa elimu, pia wanatakiwa kuwashawishi wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya kutokea kwa maafa badala ya kusubiri majanga yatokee. Pia aliwataka wawe na mpango wa kuonesha eneo lenye maafa na kuujulisha umma. Pia aliwataka watendaji wanaohusika na kamati za maafa waimarishe mawasiliano katika ngazi zote kuanzia ya kijiji hadi Taifa na wafanye kazi kwa ushirikiano ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi pindi maafa yanapotokea.

Awali, Waziri Mkuualitembelea Ofisi za Mpiga Chapa wa Serikali jijini Dar es salaam ambapo mbali na mambo mengine alijionea moja kati ya mitambo ya kwanza ya Mpiga  Chapa wa Serikali uitwao  Original Heidelberg wenye zaidi ya miaka 100 ambao bado unafanya kazi vizuri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya vifaa, magari na mitambo inayotumiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipotembelea Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Mkoa wa Ilala, eneo la Fire jijini Dar es salaam. Juni 8, 2018. Kushoto kwake ni Kamishina Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye wakati alipotembelea Kituo cha Zimamoto za na Uokoaji cha Mkoa wa Ilala eneo la Fire jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipotembelea Kituo cha jeshi hilo cha mkoa wa Ilala eneo la Fire jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018. Kushoto ni Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

VODACOM TANZANIA YAFUTURISHA WATEJA WAKE JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Wateja wa Mikataba (Business Enterprise Unit) Vodacom Tanzania, Arjun Dhillon akitoa neno la shukrani kwa baadhi ya wateja wa Vodacom Tanzania walioudhuria kwenye futari hiyo iliyoandaliwa na mtandao huo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja kutoka Vodacom Tanzania, Bakari Kamenge akizungumza na baadhi ya wateja wa Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati mtandao huo ulipoandaa futari mahsusi kwa wateje hao ili kuongeza ukaribu na  wateja wao.

Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa mtandao wa simu wa Vodacom Tanzania wakichukua futari, wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na mtandao huo jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuturu wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na mtandao huo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakibadilishana mawazo mara baada ya kufuturu pamoja kwenye futari iliyoandaliwa na mtandao huo jijini Dar es Salaam

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MLOGANZILA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema ufumbuzi umepatikana wa changamoto kubwa ya umeme inayoikabili hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila na kuahidi kusimamia utendaji ili umeme upatikane muda wote.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila. Makamu wa Rais amesema kwa vifaa vya kisasa vya umeme vilivyopo hospitalini hapo havipaswi kupata umeme wa mashaka .

Makamu wa Rais amesema kuwa wananchi wengi hawajajua umuhimu wa kuwa na bima ya afya hivyo elimu zaidi itolewe ili wananchi wengi wachangie huduma ya afya kwa kupitia bima zao hii itawapunguzia gharama sana wakati wa matibabu.

Makamu wa Rais aliutaka uongozi wa Mloganzila kutangaza kwa wananchi huduma zinazopatikana hospitalini hapo ambapo wana vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya uchunguzi wa afya, Makamu wa Rais alisema huduma ya kupima saratani ya matiti katika hospitali ya Mloganzila ni shilingi elfu 30 tu. Akiongea na Watumishi wa hospitali hiyo Makamu wa Rais amesema “ Mnaofanya kazi sekta ya afya mnafanya kazi ya Uungu”

Makamu wa Rais pia aliwasikiliza wananchi waliofika kwenye kupata huduma hospitalini hapo na kusema kuwa Serikali itajitahidi kushughulikia changamoto zinazojitokeza lakini aliwahimiza wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima ya afya.

Mapema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alimuambia Makamu wa Rais kuwa (MAMC) Mloganzila ni kati ya hospitali saba zinazomilikiwa na serikali ambazo zinatoa huduma za matibabu ya kibingwa ngazi ya juu pia alimpongeza Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kuweka msukumo wake katika huduma ya mama na mtoto ambapo juhudi za Makamu wa Rais zimezaa matunda ambapo leo hii kuna vituo 208 vimeboreshwa na kutoa huduma.

Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Ole Nasha amesema wanafunzi 350 wa shahada ya kwanza wameanza kupata mafunzo ya udaktari na udaktari bingwa na kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuona umuhimu wa maendeleo ya upanuzi wa kamapsi hii ili kuruhusu udahili wa wanafunzi wengi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Lulu Sakafu juu ya mashine ya kupimia saratani ya matiti wakati wa ziara yake katika hospitali yaTaaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu na Mwalimu wa masuala ya Meno Dkt. Elison Simon wakati wa ziara yake katika hospitali yaTaaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mtoto Amani Ahmada mwenye umri ya miaka 6, wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
  Muonekano wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila wakati wa ziara yake iliyofanyika leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wanaopata huduma ya matibabu Mloganzila wakati wa ziara yake katika hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Mradi Mhandisi Elly Kisoreka juu ya maendeleo ya ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi wakati wa ziara yake katika hospitali yaTaaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MAMC), Kampasi ya Mloganzila.

WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Elimu wahakikishe wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo ni wale waliovuka katika ngazi ya shule, kata, wilaya na mkoa, ambao wote ni wanafunzi halali wa shule na marufuku kuchezesha mamluki. 

“Endapo itabainika yupo mchezaji aliyeletwa kushiriki michezo hii ambaye si mwanafunzi (yaani mamluki) naagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahusika kwa kuzingatia kanuni na sheria za mashindano haya,” amesisitiza.
Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 9, 2018) wakati akifunguaMashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania yanayofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Pia, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa na wilaya zote nchini wahakikishe kuwa masomo ya haiba, michezo na stadi za kazi yanafundishwa kikamilifu kwenye shule zote za msingi. 

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema somo la elimu ya michezo kwa Shule za Sekondari nalo lifundishwe kikamilifu na vyuo vya michezo kama Malya viendelee kuwaendeleza walimu wa michezo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipuliza kipenga  kuamuru ipigwe penati wakati alipofungua  Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Unguja wakati alipofungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Kagera wakati alipofungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  (wasita kushoto) wakitazama mechi ya  mpira wa Kikapu  kwa wanawake baada ya kufungua mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM  Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018.  Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza na watano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. Pichani, Aisha Nasoro wa Dodoma (kulia) akimtoka  Zurfa Maulid wa Singida.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji timu ya mpira wa Kikapu ya wanawake kutoka mkoa wa  Singida wakati alipofungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mashindano  ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kabla ya kufungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Bwiru ya jijini Mwanza wakionyesha halaiki kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018.  

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images