Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Mfumuko wa bei wapungua hadi kufikia asilimia 3.6

0
0


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MFUMUKO  wa bei wa Taifa  wa Mei 2018  umepungua  hadi kufikia asilimia 3.6 ikilinganishwa na asilimia 3.8 ilivyokuwa Mwezi Aprili 2018 mwaka huu .

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa bei kumechangiwa sana na kupungua kwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula.

Amesema  baadhi ya bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mahindi kwa asilimia 10.3, unga wa mahindi kwa asilimia 12.5, mtama kwa asilimia 13.8, unga wa mihogo kwa asilimia 15.2, viazi mviringo kwa asilimia 9.0 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.6, alisema bwana Kwesigabo.

Ameongeza kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili 2018.

Hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 nchini Uganda umepungua hadi asilimia 1.7 kutoka asilimia 1.8 kwa mwaka ulioishia mwezi aprili 2018.

Aidha kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2018 umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.95 kutoka asilimia 3.73 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2018.

Mfumuko wa bei unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mfumko wa bei wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, Mfumuko wa bei umeshuka toka asilimia 3.8 mwezi Aprili hadi kufikia 3.6 Mei. Kushoto ni Meneja wa Ajira na Bei toka NBS, Ruth Minja.

RUTA KUFANYA MAANDAMANO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DK. MAGUFULI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

UMOJA wa wananchi ujulikanao kama Rudisha Uzalendo Tanzania (RUTA) unatarajia kufanya maandamano ya amani ya kumuunga mkono Rais John Magufuli kutokana na juhudi na uthubutu anaoonesha katika utendaji wake wa kazi yatakayofanyika jijini Dar es salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari Mwenyekiti wa Kamati ya maandamo hayo Charles Maselle ameeleza kuwa Juni 21, mwaka huu watafanya maandamano ya amani yasiyohusisha itikadi za vyama vya kisiasa wala dini ila wananchi wa kada zote jijini wataandamana kutoka Karume na kumalizikia katika viwanja vya mnazi mmoja na wanategemea mgeni rasmi atakuwa Rais.

Aidha amesema kuwa kama wananchi wameona ni bora kumpongeza Rais kwa sasa ili kumpa nguvu na kumtia moyo katika kazi anazofanya hasa dhamira yake ya dhati, ukweli na uthubutu katika kuleta maendeleo na wameanza kwa mkoa wa Dar es salaam na baadaye yataendelea nchini kote.

Pia Maselle ameeleza kama wananchi wameamua kurudisha uzalendo kutokana na mambo yanayofanywa na Rais kama kuboresha huduma za afya, elimu na miundombinu.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya maandamano Kigoro Athumani hayo ameeleza kuwa wanamuunga mkono Rais kutokana na juhudi na dhamira yake ya dhati katika kulipeleka taifa katika maendeleo zaidi hasa katika kuziba mianya ya rushwa  na kusimamia uadilifu katika taasisi za umma na binafsi  na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo.

Pia amewaomba wananchi kujitokeza siku hiyo kumuunga mkono Rais kutokana na mapinduzi anayoleta bila kujali vyama wala dini.

Hali kadharika RUTA wamezindua nembo maalumu itakochapishwa katika tisheti zitakazovaliwa siku hiyo na wameomba wadau mbalimbali kutumia nembo hizo kwa kuchapa fulana na kugawa kwa wananchi siku hiyo.
 Mwenyekiti wa maandamano ya Rudisha Uzalendo Tanzania(RUTA) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya maandamano ya amani yasiyohusisha itikadi za vya vya siasa yatakayo fanyika Juni 21 mwaka huu jijini Dar as Salaam.picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii.
Mwenyekiti wa kamati ya maandamano ya Rudisha Uzalendo  Tanzania  (RUTA) Charles Maselle(kulia)akiwa na wajumbe wameonesha   ya umoja huo.

DK. KIKWETE AISHAURI CMSA KUTOA ELIMU KUHUSIANA NA FAIDA ZA HISA

0
0
CMSA yairudisha NICOL soko la hisa

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne , Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameishauriwa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) kutoa elimu kwa watanzania kuhusiana na ununuaji wa hisa katika soko la hisa.

Kikwete ameyasema wakati hafla ya Kampuni ya NICOL kurudishwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE) baada ya kukidhi vigezo vya kisheria kuongia katika soko hilo, amesema CMSA ikitoa elimu kwa wananchi kutafanya kuongeza hamasa ya ununuaji hisa kuliko ilivyo sasa.

Dk.Kikwete amesema kuwa CMSA ikitoa elimu kutafanya kampuni nyingi kuorodheshwa katika soko la hisa na kufanya uwekezaji wa miradi mingine.Aidha amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia katika masoko CMSA imeshauriwa kuboresha zaidi manada wa soko la Hisa wakati wa kufungua na kufunga.Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete alisema kwamba lengo la kuisajili Nocol ilikuwa ni kuwasaidia .

"Nakumbuka wakati serikali inauza hisa zake NMB kulikuwa na mjadala mkali wa kuhoji kwanini nicol wapewe asilimia tano, lakini kwa imani kwamba hii ni kampuni ya wazalendo, basi tukachukua uamuzi kuwapa wazalendo," alisema.Kikwete kwamba hakuwahi kuusikia mgogoro wa NICOL wakati wa utawala wake.

"Lengo lilikuwa kusaidia wazawa kujijenga kuichumi na kukuza maendeleo, nimesikia leo (jana) hadithi ya Nicol katika uongozi wangu sikusikia kabisa mgogoro wao," alisema Kikwete.Aidha aliipongeza CMSA kwa utendaji kazi wake, ikiwemo kusimamia kwa madhubuti masoko ya mitaji.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akigonga kengele kwa ajili ya kufungua soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kuingia kampuni ya NICOL.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na kuingia NICOL katika Soko la Hisa la Dar es Salaam , jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti bodi ya NICOL, Dk. Gideon Kaunda akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na kuingia NICOL katika soko hisa na changamoto walizoweza kukabiliana nazo .
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine.

JWTZ YATOA TAARIFA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU PT.NSEVILWE NZOWA

WANAWAKE WASHIRIKI KUJENGA WODI YA MAMA NA MTOTO CHEMBA

0
0

Wanawake washiriki kujenga Wodi ya mama na mtoto - Chemba

Wanawake wa Kata ya Songolo, katika Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma wamejitoa katika ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto lililojengwa katika kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya hiyo kwa lengo la kuchangia nguvukazi ili kupunguza changamoto za kutembea muda mrefu kutafuta huduma za afya.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo hicho Bw. Saidi Msigwa mbele ya timu ya ukaguzi wa ujenzi wa vituo vya afya katika Mkoa wa Dodoma walipokuwa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya mkoani Dodoma.

Amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake wa Kata ya Songolo walijitokeza katika ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa ndicho kilikuwa kilio chao cha muda mrefu cha kujengewa Wodi ya mama na Mtoto jambo lililopelekea wanawake wengi hasa wajawazito kwenda kujifungulia katika Hospitali ya Wialaya ya Kondoa.

Amesema kukamilika kwa Kituo cha afya cha Hamai kutasaidia wananchi wengi kupata huduma ya afya hasa vijiji vya jirani ambavyo ni Murongia, Itolwa , Jangalo, Jinjo, Kinkima na Kirerechangombena ambao wote hupata huduma katika kituo hicho.

Bw. Msigwa amesema mwaka 2015 wanawake wa Kata ya Songolo waliamua kijutolea kujenga jengo la Wodi ya Mama na mtoto kutokana na kuwepo kwa jengo moja la wodi ya Mama na Mtoto jambo ambalo lilikuwa likisababisha msongamano wa wamama wajawazito sababu hii ilipelekea wanawake kuamua kuchimba msingi na kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa wodi hiyo ndipo serikali ilipoamua kujenga jengo hilo mwaka 2018.

Bw. Msigwa ameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga kituo cha afya cha Hamai ambacho kitasaidia wananchi maskini ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.Amesema kituo hicho kimejengewa wodi ya mama na mtoto, jengo la upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi ambapo mpaka sasa tayari zimetumika zaidi ya shilingi milioni 291.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Charles Kiologwe ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya chemba kwa usimamizi mzuri wa majengo yaliyojengwa ambayo yanaonyesha uhalisia wa matumizi ya fedha zilizotumika ukilinganisha na ubora wa majengo.

Aidha ameutaka uongozi wahuo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma za afya katika maeneo ya karibu na wanapoishi.Naye Bi Martha Mariki Afisa afya Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ameutaka uongozi wa Halamashauri ya Wilaya ya Chemba kuhakikisha maeneo ya taasisi yanapimwa na kuwa na hati miliki, pia kuhakikisha wanaweka kwenye bajeti kama kipaombele cha kuweka uzio wa maeneo ya taasisi ili kuepusha maeneo mengi kuvamiwa na wananchi.
Jengo la Mama na Mtoto liliojengwa katika Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe akitoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Hamai kilichopo katika Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma.
Timu ya ufuatiliaji na ukarabari wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Charles Kiologwe wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Bw.Jofrey Shima wakati walipotembelea Kituo cha afya cha Hamai, kilichopo katika Kata ya Songolo Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA MADINI NA KUZINDUA MAABARA YA KISASA YA MADINI

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa 38 wa Mawaziri wa Madini  kutoka nchi wananchama wa Ukanda wa  Maziwa Makuu kwenye   Kituo cha Utafiti  na uendelezaji wa sekta ya Madini, Kundichi jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Meneja wa Maabara ya Kemia na Mazingira wa Kituo cha Utafiti na Uendelezaji wa Sekta  ya Madini, Bw.  Charles Butete baada ya kuzindua maabara hiyo , kunduchi jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Madini, Angela Kairuki. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi  kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa   Maziwa Makuu baada ya kufungua Mkutano 38 wa  Mawaziri wa Madini kutoka nchi hizo kwenye Kituo cha utafiti na uendelezaji wa sekta ya Madini, Kunduchi jijini Dar es salam, Juni 8, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Madini, Angela Kairuki. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua Mkutano wa 38 wa  Mawaziri wa Madini kutoka nchi wanachama wa Ukanda wa  Maziwa Makuu kwenye Kituo cha utafiti na uendelezaji wa sekta ya Madini, Kunduchi jijini Dar es salam, Juni 8, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA DK MNDOLWA AANZA ZIARA MIKOA YA KANDA YA ZIWA NA SINGIDA, LEO.

0
0

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimiana na viongozi wa Jumuia hiyo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo kuanza ziara katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza na Singida.

SERIKALI YASHAURIWA KUJENGA MAHABUSU ZA WATOTO KWENYE MIKOA NA WILAYA HAPA NCHINI

0
0
SERIKALI imeshauriwa kujenga mahabusu za watoto kwenye mikoa na wilaya hapa nchini ili kuwaweka watoto waliokuwa katika ukinzani wa kisheria ambao wamekuwa wakifanya vitendo viovu. 

Hatua hiyo itakuwa sehemu ya kuwaweka watoto happy wakiwa wanasubiri kesi zao kusikilizwa badala ya ilivyokuwa hivi sasa watoto hao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na uhaba uliopo. 

Hayo yalisemwa juzi na Mratibu wa Chama cha Wanasheria wanawake mkoani Tanga (TAWLA) Latifa Ayoub wakati wa warsha ya siku moja iliyokuwa na lengo la kujaribu kujadili changamoto kwenye sheria za mtoto na kanunuzi zake hususani waliopo kwenye ukinzani nazo wakiwemo kama wadau iliyofanyika mjini hapa 

Alisema kutokana na uhaba wa mahabusu za watoto wamekuwa wakati mwengine wakikumbana na changamoto kadhaa wakati wakisubiri utaratibu wa kusikilizwa kesi zao wanazokabiliana nazo kabla ya kutolewa hukumu. 
 Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga Latiba Ayoub akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya siku moja iliyokuwa na lengo la kujaribu kujadili changamoto kwenye sheria za mtoto na kanunuzi zake hususani waliopo kwenye ukinzani nazo wakiwemo kama wadau iliyofanyika mjini hapa .
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (Tawla) Mwanaidi Kombo akizungumza wakati wa warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa YDCP Jijini Tanga
Afisa wa Dawati Jeshi la Magereza mkoani Tanga ASP Halima Mswagilla akichangia jambo kwenye warsha hiyo 
Wakili wa Serikali Rebbeca Msalangi akisisistiza jambo kwenye warsha hiyo wakati akiwasilisha mada 


MAAFISA UUGUZI CHUO KIKUU CHA NEW YORK NCHINI MAREKANI KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KATIKA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA WAGONJWA

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akimkabidhi zawadi ya kinyago Afisa Muuguzi wa Chuo Kikuu cha New York cha nchini Marekani Linda Herrmann wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Maafisa uuguzi wawili kutoka chuo hicho walifika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Delila Kimambo akimkabidhi zawadi Afisa Muuguzi wa Chuo Kikuu cha New York cha nchini Marekani Mary Brennan wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Maafisa uuguzi wawili kutoka chuo hicho walifika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi Robert ally pamoja na Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Uuguzi wa Chuo Kikuu cha New York cha nchini Marekani Mary Brennan mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Maafisa uuguzi wawili kutoka chuo hicho walifika katika Taasisi hiyo kwaajili ya kuangalia namna ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.Picha na JKCI

MAKAMU WA RAIS BENKI YA DUNIA ATEMBELEA MAHAKAMA YA WILAYA KIGAMBONI,AISIFU MAHAKAMA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA MOLADI KTK UJENZI

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro ameipongeza mahakama ya Tanzania kwa utekelezaji wa miradi ya mahakama kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya ujenzi wa bei nafuu ya mradi wa Molandi.

Pia Okoro ameipongeza mahakama kwa kuzingatia uwiano wa jinsia mahakamani katika utekelezaji wa majukumu kwani ameona kutoka ngazi za juu hadi ya chini wanawake wako wengi, 

Okiro amesema hayo leo Juni 8,2018 wakati anatembelea Mahakama ya Mwanzo na ile ya Wilaya ya Kigamboni iliyopo katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambapo alishuhudia majengo na kupewa maelezo mbali mbali yanayofanywa na mahakama za Tanzania. Ikiwemo mahakama inayotembea (Mobile Court).

Amesema taarifa za ujenzi wa majengo hayo ni za mfano wa kuigwa na zinapaswa kuwa mfano wa nchi nyingi za Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla kwani majengo hayo ni mazuri na yanakidhi thamani ya fedha.Amesema, taarifa ya namna ya mfumo wa mawasilisho na ujenzi na jinsi miradi hiyo inavyofanya kazi,ni mfumo mzuri na ni kitu cha kuigwa kwani inaonyesha wazi ni jinsi gani jengo lilivyo na mfumo mzuri.

"Nimefurahi sana, miradi imejengwa kwa mfumo mzuri, majengo nilikuwa nikiyaona kwenye documents tu lakini sasa hivi nimeyaona, yanakidhi vigezo na thamani ya pesa", amesema Okiro.

Kabla ya kuongea hayo, makamu wa rais huyo, alipata nafasi ya kusikikiza taarifa (Presentation) kutoka kwa Mhadhiri Mwandamizi wa Mfumo (Court Mapping) kutoka chuo cha Ardhi Job Chaula amesema, katika mahakama hiyo, wameweka mifumo ya mawasiliano ya kutoa taarifa mbali mbali za mahakama itakayomuwezesha mwananchi kufuatilia kesi bila ya kufika mahakamani, na vile vile ramani ya kufika mahakamani hapo kutokea mahali popote.
Mhadhiri Mwandamizi wa Mfumo: Court Mapping kutoka chuo cha Ardhi Job Chaula, akieleza jinsi mfumo wa kutoa taarifa mbali mbali za mahakama una vyofanya kazi katika Mahakama ya Mwanzo na Wilaya ya Kigamboni kupitia mradi wa Court Mapping. 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Dk. Daniel Mbisso, akieleza jinsi teknolojia ya Moladi ilivyotumika kujenga majengo mbalimbali ya Mahakama na kufanikisha kwa mafaniko makubwa mahakama zaidi ya tano zilizojengwa kwa muda mfupi na garama nafuu.
Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro (katikati) aliyevaa miwani akiwa katika Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mara baada ya kupokea taarifa (presentation) juu ya utekelezwaji wa miradi wa Court Mapping na mradi wa ujenzi wa mahakama kwa garama nafuu wa kupitia mladi wa Moladi.
Makamu wa rais wa Benki ya dunia, Sandie Okoro kulia akizungumza na wadau mbali mbali wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni na Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mara baada ya kupokea taarifa (presentation) juu ya utekelezwaji wa miradi wa Court Mapping na mradi wa ujenzi wa mahakama kwa garama nafuu wa kupitia mladi wa Moladi. Pembeni yake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga.


NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALU, ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MITA ZA LUKU ZA KISASA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

NA K-VIS BLOG/KhalfanSaid

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, ametembelea kiwanda cha kutengeneza mita za LUKU kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam leo Juni 8, 2018 na kuridhishwa na ubora wa mita hizo.

Alisema tatizo la mita lilikuwa ni changamoto kubwa iliyopelekea kasi ya kuwafikishia umeme Watanzania kuwa na kikwazo kwani TANESCO iliagiza mita hizo kutoka nje.

Kampuni ya Baobab Engineering System Tanzania ndiyo watengenezaji wa mita hizo za kisasa za LUKU (Smart Meters) na uongozi wa kiwanda umeahidi kuzalisha mita za kutosha ili kutatua changamoto iliyokuwa ikiikabili TANESCO kuhusu upatikanaji wa mita.

“Sisi katika kutaka shirika letu la TANESCO lifanye vizuri tumewapa maelekezo yako ndani ya Sera na mipango yetu lazima waunganishie umeme wateja wengi na moja ya component inayotakiwa ni mita, kumekuwa na changamoto ya mita kama mlivyosema, na hasa inatokana na utaratibu wa uagizaji na hata kufika kwa vifaa hivyo ilichukua muda sana, sasa uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mita hapa nyumbani ninaamini tatizo hili sasa halitakuwepo.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Mgalu.

NAIBU Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, akiwa ameshika moja ya mita ya kisasa ya LUKU, (Smart Meter), iliyotengenezwa na kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam, wakati alipokitembelea kujionea mita hizo leo Juni 8, 2018.


Mheshimiwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizunguzma jambo baada ya kujionea mita hizo.
Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.
Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

ALIKIBA NA SAMATTA WATAMBIANA, ZARI NA MILIONI 4.

KATIBU MKUU WA UWT,NDUGU QUEEN MLOZI,AMEAHIDI KUFANYA KAZI KWA WELEDI,UAMINIFU NA UZALENDO NDANI YA CCM

0
0

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndugu Queen Mlozi ameahidi kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uzalendo uliotukuka ili CCM ishinde katika uchaguzi mkuu wa dola mwaka 2020.

Hayo ameyasema wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa ngazi mbali mbali za UWT Zanzibar hapo Afisi Kuu CCM Kisiwandui katika ziara yake ya kwanza kujitambulisha kwa viongozi na watendaji hao.

Alisema atatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kwa lengo la kuimarisha taasisi hiyo ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ndani ya Umoja huo na Chama kwa ujumla.Ameeleza kwamba wanawake wa UWT wanatakiwa kuelekeza nguvu zao katika kulinda maslahi ya CCM ili ishinde kwa ngazi zote kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar katika uchaguzi Mkuu ujao.

Katibu Mkuu huyo amewashukuru viongozi viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi waliomuamini na kumteuwa kushika nafasi hiyo ya ngazi ya juu ya kiutendaji kupitia Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilichofanyika hivi karibuni Jijini Dar es saalam.

“ Viongozi na wanachama wote nakuahidini kwamba nitatumia weledi na uzoefu wangu wote kwa kuhakikisha UWT inaendelea kuwa imara na mkombozi na mtetezi mkubwa wa maslahi ya wanawake wote nchini”, alisema Queen.Akizungumza Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndugu Gaudencia Kabaka alisema ushirikiano anaoupata kutoka kwa viongozi mbali mbali wa Umoja huo na Chama unampa nguvu na imani ya kusimamia maslahi ya taasisi hiyo bila hofu.


KATIBU Mkuu wa UWT Taifa Ndugu Queen Mlozi akizungumza na viongozi na watendaji wa Umoja huo ngazi za Mikoa na Wilaya Zanzibar, Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar katika ziara yake ya kujitambulisha.
BAADHI ya Wenyeviti na Makatibu wa UWT wa Mikoa na Wilaya wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja huo Taifa.


VIONGOZI wakuu wa UWT Taifa wakiomba dua katika kaburi la Mwasisi wa Mapinduzi ya mwaka 1964 ambaye pia alikuwa ni Rais wa kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Abeid Amani Karume.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza na viongozi wakuu wa UWT Taifa waliofika Ofisini kwake, Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid(kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Gaudencia Kabaka(kulia) alipofika katika Baraza hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na Wawakilishi wanawake katika Baraza hilo.
NAIBU Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Mgeni Hassan Juma (kulia) akimkabidhi Katiba ya Jumuiya ya wawakilishi wanawake katika Baraza hilo Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Bi. Queen Mlozi (kushoto).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMBI YA UPASUAJI KISARAWE YATARAJIA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 350

0
0
NA WAMJW-KISARAWE.

KAMBI ya upasuaji wa mabusha na matende katika hospitali ya Wilaya ya Kisarawe inatarajia kufanya upasuaji kwa wagonjwa wapatao 350 katika mkoa wa Pwani ili kuondoa kabisa watu wenye ugonjwa huo.

Hayo yamezungumzwa na Mratibu wa Taifa wa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD) kutoka Wizara ya Afya Dkt. Upendo Mwingira wakati alipotembelea kambi hiyo katika kufikia tamati wa mkutano wa mwaka wa kupitia,kujadili na kupanga mikakati ya kupambana na magonjwa hayo leo Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

“Mpaka leo hii wagonjwa 100 wamefanyiwa upasuaji katika kambi hii ya upasuaji ya kisarawe na lengo letu ni kuwafikia wagonjwa 350 mpaka mwisho wa kambi hii itapofikia tamati kwa muda wa wiki mbili kuanzia jumatatu iliyoisha” alisema Dkt. Mwingira.

Aidha Dkt. Mwingira amesema kuwa zoezi hilo limeanza kufanywa kwenye mikoa ya lindi,Pangani na Tanga kwa kuweka kambi za upasuaji kwa wagonjwa hao na kujenga uwezo kwa wataalam wa upasuaji wa mabusha na matende wa ndani na nje ya mkoa.

Mbali na hayo Dkt. Mwingira amewataka wananchi wajitokeze kupata huduma hiyo kwani ugonjwa huo sio wa kurogwa hivyo unatibika hospitali bila ya gharama zozote na kuwaomba wajitokeze kwenye zoezi la kumeza kingatiba ya magonjwa hayo litakaloanza mwezi wa tisa mwaka huu.

Kwa upande wake Mtaalam wa upasuaji na msimamizi wa kambi hiyo Dkt. Alexander Mwerange amesema kuwa katika kufanikisha zoezi hilo wameamua kila siku kufanyia upasuaji angalau kuanzi wagonjwa 25 kwa siku ili kuendana na kasi ya kuwanusuru wagonjwa hao.

“Katika kufanikisha zoezi hili wakati mwingine wataalam inatubidi tuwafuate wagonjwa huko walipo kwani wanashindwa kufika kambini hapa kwa sababu ya usafiri hivyo tukiwapima basi tunawaleta hapa kwa ajili ya uapsuaji” alisema Dkt. Mwerange.

Aidha, Dkt. Mwerange ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa kufanikisha kambi za namna hiyo katika mikoa mbalimbali na kuwataka wananchi kutowaficha wagonjwa wa matende na mabusha bali wajitokeze ili waweze kupata matibabu hayo .

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AWAVISHWA VYEO MAOFISA WAANDAMIZI TISAWA JESHI LA MAGEREZA JIJINI DAR

0
0
KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu Rais John Magufuli amewavisha vyeo maafisa wa ngazi ya juu 9 wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Miongoni mwa maafisa 9 waliovishwa vyeo ni manaibu kamishna wa magereza – DCP wanne wa Jeshi hilo ambao wamepandishwa vyeo na kuwa Makamishna wa magereza, huku makamishna wasaidizi waandamizi wa Magereza -SACP watano wakipandishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna – DCP wa Jeshi hilo.

Waliovishwa vyeo kuwa Makamishna wa Magereza ni Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila, Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza Augustine Mboje, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Naibu Kamishna wa Magereza Gideon Nkana ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam.

Wengine waliovishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Julius Sang’udi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Phaustine Kasike, Mkuu wa Kitengo cha Parole pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Jeremiah Katungu ambaye ni Katibu Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo akimvalisha cheo Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila kuwa Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga kuwa Naibu wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.
Makamishina na Manaibu Kamishna wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2018. 
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt Juma Malewa akikagua gwaride maalum katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.


DKT. ABBASI ATOA MAFUNZO KWA MAAFISA HABARI NA TEHAMA KUTOKA TAASISI ZA SERIKALI

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kutangaza huduma na shughuli mbalimbali za Serikali kwa Maafisa Habari na Maafisa Tehama kutoka Taasisi mbalimbali Serikalini pwakati wa mafunzo maalum yaliyofanyika leo Ijumaa Juni 8, 2018 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA MAELEZO)

MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI CHA MKOA WA ILALA, ENEO LA FIRE JIJINI DAR

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye wakati alipotembelea Kituo cha Zimamoto za na Uokoaji cha Mkoa wa Ilala eneo la Fire jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipotembelea Kituo cha jeshi hilo cha mkoa wa Ilala eneo la Fire jijini Dar es salaam, Juni 8, 2018. Kushoto ni Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua baadhi ya vifaa, magari na mitambo inayotumiwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipotembelea Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Mkoa wa Ilala, eneo la Fire jijini Dar es salaam. Juni 8, 2018. Kushoto kwake ni Kamishina Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye. 

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATENDAJI WAKUU KUTOKA BOT, MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA NA UMOJA WA WACHIMBAJI MADINI TANZANIA

0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma wakiongozwa na Gavana wa Benki hiyo, Prof. Florens Luoga (kushoto kwa Spika). Kulia kwa Spika ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (kulia) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kushoto chini) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) walioongozwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof. Florens Luoga (watatu kulia) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kushoto chini ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele (kulia) ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Shinyanga Mjini, Mhe. Stephen Masele (kulia) ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Watendaji Wakuu kutoka Umoja wa Wachimba Madini Tanzania walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wakiongozwa na Katibu Mtendaji wa Umoja huo, Ndg. Gerald Mturi (kushoto kwa Spika) 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu kutoka Umoja wa Wachimba Madini Tanzania walioongozwa na Katibu Mtendaji wa Umoja huo, Ndg. Gerald Mturi (wa pili kulia) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


(PICHA NA DEONISIUS SIMBA – OFISI YA BUNGE)

WANANCHI WA KIGOMBE WATAKIWA KUACHANA NA BIASHARA ZA MAGENDO

0
0
WANANCHI wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga wametakiwa kuacha kushiriki kwenye biashara za magendo badala yake watumie maeneo yaliyorasmi kwa kisheria kwa ajili ya upitishaji wa bidhaa. 

Wito huo ulitolewa leo na Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo wakati akizungumza na wananchi hao kwenye mkutano uliofanyika kwenye eneo la sokoni akiwa ameambatana na maafisa wa TRA mkoa wa Tanga. 

Alisema kitendo cha wananchi kuacha kutumia bandari ya Pangani ambayo ipo kusheria wanafanya makosa makubwa na kuwataka kuitumia kupitisha bidhaa badala ya kutumia zile ambazo hazitambuliki ambazo watakapokamatwa watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria. 

“Tumefika hapa kigombe kutoa elimu kwa kuzungumza na wananchi kutokana na changamoto za mara kwa mara biashara za magendo ambazo zimekuwa zikipitishwa eneo hilo na kuona kutumia muda huo kuzungumza na wananchi kuwaambia madhara yake ni yapi”Alisema. 
 MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza umuhimu wa kulipa kodi na kuacha kujihusisha na uingizaji wa bidhaa kwa njia za magendo.
 MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza ambao hawapo pichani juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kuacha kujihusisha na uingizaji wa bidhaa kwa njia za magendo kulia ni Kaimu Meneja wa TRA Mkoani Tanga Nazarius Mfikwa kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigombe Bakari Akida Ally.
 Kaimu Meneja wa TRA Mkoani Tanga Nazarius Mfikwa akizngumza wakati wa mkutano huo kushoto ni MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.
AFISA Mfawidhi wa Forodha Bandari ya Tanga Zahor Makame akizungumza katika mkutano huo 
Mkazi wa Kijiji cha Kigombe Kata ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga Tajiri Twaha akiuliza swali kwenye mkutano
 Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kigombe kata ya Kigombe wilayani Muheza wakimsikiliza kwa umakini MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo ambaye hayupo pichani wakati alipokwenda kuzungumza nao kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na na kuacha kujihusisha na uingizaji wa bidhaa kwa njia za magendo.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images