Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AZIONYA ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka asasi zisizokuwa za Serikali (NGOs) zitekeleze majukumu yake kama ambavyo zimesajiliwa na ziache kufanya shughuli zilizo nje ya makubaliano.

Amesema Serikali itaendelea kuzichukulia hatua NGOs zote zinazokiuka taratibu kwa kufanya majukumu mengine kinyume na malengo yake.Ametoa onyo hilo leo (Alhamisi, Juni 7, 2018) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Longido, Dkt. Stephen Lemomo Kiruswa kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

“Serikali itaendelea kuzifuatilia NGOs zote zinazokiuka taratibu na kufanya majukumu mengine yanayozua mitafaruku kwenye jamii na Serikali,” amesema.Dkt. Kiruswa alitaka kufahamu ni lini Serikali itazifutia usajili NGOs zote ambazo kwa muda mrefu zimeacha kutekeleza majukumu yake na badala yake zinafanya shughuli za uchochezi.

Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ina utaratibu wa kufuatilia taasisi hizo kubaini endapo zinafanya kazi kama zilivyojieleza kwenye usajili wake.Amesema mara inapobainika kwamba kuna NGOs ambazo zimeacha majukumu yake na zinafanya shughuli zingine nje ya mikataba yao, hatua stahiki huchukuliwa, hivyo alizitaka zijikite katika utoaji wa huduma bora kwa jamii.

“Kwa hiyo nitoe wito kwa NGO’s zote ambazo Serikali imeridhia na tumezisajili ili ziweze kufanya kazi ya kutoa huduma za jamii, zijikite kutoa huduma za jamii kama ambavyo tumekubaliana, ili tuweze kufikia malengo ya pamoja kati ya Serikali na taasisi zisizo za kiserikali katika kutoa huduma kwa Watanzania wote,” amesema.


MJADALA KUHUSU UKIMWI KUFANYIKA UDSM LEO

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 07.06.2018

HALMASHAURI YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA YA MIUNDOMBINU KATIKA SEKTA YA ELIMU

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
HALMASHAURI ya wilaya ya Bagamoyo ,Pwani inakabiliwa na upungufu mkubwa wa miundombinu katika sekta ya elimu ikiwemo vyumba vya madarasa 367 ambapo shule za msingi kuna upungufu 329 huku shule za sekondari upungufu ni 38. Aidha kuna upungufu wa matundu ya vyoo 770 huku nyumba za walimu zipo pungufu 634.
Akitoa taarifa ya masuala ya elimu katika maadhimisho ya Juma la elimu wilayani Bagamoyo ,kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo, ofisa elimu msingi ,Peter Fussi alisema upungufu huo unasababisha kero ya mlundikano wa wanafunzi madarasani. Alisema ,shule za msingi zina mahitaji ya madarasa 621 ,yaliyopo 292 na mapungufu ni 329.
Alitaja mahitaji ya matundu ya vyoo kuwa ni 1,133, yaliyopo 363 ,upungufu 770 ,nyumba za walimu mahitaji 707, zilizopo 73 upungufu 634, maktaba 32 ,zilizopo 25 na pungufu saba. Kwa mujibu wa ofisa elimu msingi huyo ,kwa upande wa elimu msingi wanaendelea na jitihada kwa kushirikiana na wananchi na wadau kujenga vyumba vya madarasa 74 katika kata mbalimbali. Fussi alisema, pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali na wadau bado upo upungufu huo.
"Kwa upande wa elimu sekondari ,alisema ipo miradi inayotekelezwa ni ujenzi ikiwemo ujenzi wa madarasa manne shule mpya ya sekondari Mapinga. Miradi mingine ni umaliziaji wa ujenzi wa maabara mbili shule ya sekondari Kingani ,ujenzi wa nyumba mbili ,ofisi shule ya sekondari Hassanal Damji ,bweni shule ya sekondari Dunda na jengo la utawala shule ya sekondari Kerege" alisema.
Fussi alisema kukamilika na kutumika kwa miradi hiyo kutasaidia kuboresha mazingira ya kusomea na kufundishia kuwa bora na hivyo kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Hata hivyo ,alielezea wananchi kupitia madiwani wameelimika vya kutosha ambapo kila kata ina mpango kazi wake wa ujenzi wa miundombinu yake ya elimu na huduma nyingine za jamii.
Pamoja na hayo alisema kuwa limekuwepo tatizo kwa baadhi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na wale wanaojiunga na kidato cha kwanza kutokujua kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK).Fussi alibainisha ,tafiti zinaonyesha upo ukweli wa jambo hilo ,linalosababishwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi unatokana na upungufu wa madarasa.
Alisema wapo walimu wasio na mafunzo ya KKK ambao kutokana na upungufu wa walimu wanapewa kufundisha madarasa ya chini yenye kuhitaji walimu wenye mafunzo na waliobobea katika utumiaji wa mbinu na zana za KKK.
Akizungumzia suala la mdondoko ,Fussi alisema idadi ya wanafunzi wanaokatisha masomo kwasababu mbalimbali( mdondoko) imepungua.Alisema kuwa mwaka 2016/2017 katika shule za msingi kulikuwa na mdondoko 23 na shule za sekondari utoro 29,mimba 7 jumla mdondoko 43.
Aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Bw. Alphonce Amuli  aliwataka wananchi kushirikiana na walimu kuangalia namna ya kutatua changamoto za miundombinu na kuinua ufaulu mashuleni. Alisema serikali ama walimu pekee hawawezi kupambana na changamoto hizo hivyo kuna kila sababu ya kuungana pamoja kumaliza kero hizo.
 Mgeni rasmi Bw. Alphonce Amuli akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu wilayani humo yaliyofanyika shule ya msingi Majengo.


Ofisa elimu ya msingi halmashauri ya Bagamoyo Bw. Peter Fussi akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Fatuma Latu wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu kiwilaya iliyofanyika shule ya msingi Majengo. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Katibu Mkuu mpya UWT akabidhiwa Ofisi rasmi,awataka wanawake kushikamana kujiletea maendeleo.

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Gaudencia Kabaka akizungumza wakati wa hafla ya utambulisho wa Katibu Mkuu mpya wa Umoja huo Mwalimu Queen Mlozi pamoja na kukabidhiwa Ofisi rasmi  jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa UWT aliemaliza muda wake Amina Makilagi akimuelekeza jambo Katibu Mkuu mpya UWT Mwalimu Queen Mlozi wakati wa mabdhiano ya Ofisi hapo jana Jijini Dar es salam,Mlozi ,amewataka wanawake kuwa wamoja na kushikamana katika mambo mbalimbali ya kujiletea maendeleo.
Katibu Mkuu UWT aliemaliza muda wake Amina Makilagi pichani kulia akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu Mpya Mwalimu Queen Mlozi hapo Jana katika ofisi za Umoja huo Jijini Dar es salam.
Wakiwa katika picha ya pamoja Uongozi wa sasa na Uliopita wa UWT

MWANAHABARI NYOTA NCHINI MILLARD AYO AKANUSHA UZUSHI WA KIFO CHAKE ULIOSAMBAA KILA KONA

INTRODUCING Galaxy - ONA (Official Video)

JAMII ISHIRIKISHWE MABADILIKO TABIA NCHI KUWA NA KILIMO CHENYE TIJA

$
0
0
JAMII inayojitambua ndiyo inayoweza kutumika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha kushindikana kwa mipango mingi ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira kunatokana na uelewa duni na mipangilio isiyozingatia mahitaji halisi ya wananchi wa maeneo husika.

Kauli hiyo imo katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ofisi za ESRF.Katika mdahalo huo uliowezeshwa na Shirika la Kimataifa la Care kwa kushirikiana na taasisi ya FANRPAN na ESRF imeelezwa kuwa kuna changamoto kubwa kwa maendeleo ya kilimo na ukuaji wake kutokana na n chi nyingi Kusini mwa Afrika kutegemea mvua.

Aidha ilielezwa kuwa changamoto nyingine ni umaskini uliokithiri, upungufu nmkubwa wa raslimali watu, maandalizi hafifu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na miundombinu dhaifu.Mmoja wa watoa mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko alisema kwamba kumekuwa na kulegalega kwa matumizi ya teknolojia katika kusaidia kuhifadhi mazingira miongoni mwa wananchi na uwezeshaji kwa watendaji kiasi cha kuharibu muitikio unaonekana wakati wa mafunzo.

Chinoko alisema kwamba kutokana na hali hiyo walibuni kanuni ambazo wao wanaziita SUPER kanuni ambazo zikifuatwa vyema zinajibu matatizo yaliyopo sasa. Alisema kwamba Super ni mfumo wa uchakataji wa taarifa na utekelezaji wake unaolenga kuwafikia wananchi wa pembezoni ambao ndio washiriki wakubwa wa utunzaji wa mazingira na uzalishaji wa chakula.

Alisema kwa kutumia kanuni hizo wananchi wanaweza kutambua mwendelezo wa rasilimali ardhi na misitu waliyonayo, wakawezesha kuitumia kwa faida kutokana na uadimu wake.Aidha kanuni hizo zinahitaji mipango kuzingatia usawa wa kijinsia ili kuteketeleza sera katika uchumi.

Alisema mfumo wa masoko unazungumzwa ikiwa ni pamoja na ushiriki wa sekta binafsi katika kilimo ili kuipaisha na kuifanya kuwa na tija zaidi.Alisema kwa sasa kuna tatizo kubwa sana la kuwasilisha taarifa huku watengeneza sera wakiwa pekee yao bila kushirikisha wananchi ambao ndio watendaji wenyewe.

Mshehereshaji wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi, Mtafiti mshiriki wa ESRF, Abdallah Henku akitoa utambulisho wa wanenaji wa mdahalo huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ESRF.

Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida wakati wa Mdahalo  wa Kitaifa wa Kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Menejimenti ya Mazingira Wizara ya Kilimo Bi. Shakwaanande Natai akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa sera ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa Kilimo cha Kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Muwasilishaji mada kutoka Taasisi ya CARE International nchini Malawi, Vitumbo Chinoko (wa pili kushoto) akifafanua kanuni za kufauta katika kuhifadhi mazingira na kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Tafiti zilizoanishwa ESRF, Bi. Vivian Kazi (kulia), Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale (wa tatu kulia), Meneja ushirikiano, uragibishi wa sera kutoka taasisi ya Food, Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) Bw. Lufingo Mwamakamba (wan ne kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango (kushoto)  akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida.
Mkurugenzi wa Sera, Mawasiliano na Uragibishi FANRPAN, Francis Hale akifafanua jambo wakati majadiliano kwenye mdahalo wa kitaifa wa kilimo cha kisasa kinachozingatia mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.


Benki ya CRDB na Jeshi la Polisi nchini kudumisha mahusiano ya kibiashara

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kulia) akizungumza wakati uongozi wa Benki ya CRDB ulipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kudumisha mahusiano ya kibiashara kati ya CRDB na Jeshi hilo. Huku akisikilizwa kwa makini na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro pamoja na Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii kwa Jeshi la Polisi, CP Mussa Ali Mussa. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Benki ya CRDB Bi. Esther Kitoka.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akieleza jambo kwa baadhi ya Maafisa wa juu wa Jeshi la Polini pamoja na Wafanyakazi wa Benki ya CRDB (hawapo pichani) katika Mkutano maalum wa kudumisha mahusiano ya kibiashara kati ya CRDB na Jeshi hilo, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei na Kushoto ni Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii kwa Jeshi la Polisi, CP Mussa Ali Mussa. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, akionyesha Kadi ya TemboCard Visa Infinite, aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), wakati uongozi wa Benki ya CRDB ulipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kudumisha mahusiano ya kibiashara. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Viva Tower, Naomi Mwamfupe.
Picha ya pamoja.

MTANAGE NA KIKAPU KUPIGIWA WASHINGTON, DC OLD SCHOOL REUNIOUN DMV USIPIME

$
0
0

Its all About Fun, Food, Drinks, Fashion,Sports and Nyama choma

From Fri JULY 6 to Sun JULY 8, 2018
Oxford Center
9700 Martin L King Jr Hwy,
Lanham, MD 20706

Friday July 6, 2018
from 9pm DMV International VIBE
Music by DMV DJ's
$50 Cover Charge plus OPEN BAR all night (Driks included)

Saturday July 7, 2018
From 10 am Basketball Bonanza
830 Ridge Rd, SE
Washington, DC 20019

From 4 Pm Simba vs Yanga
830 Ridge Rd, SE
Washington, DC 20019

From 9pm OLD SCHOOL REUNION PARTY Like never before!
Music by the best DJs in North America Dj Luke Joe
Dj Dennis the Funkhouse

$80 Cover Charge Dinner plus OPEN BAR all night (Dinner and Drinks Included)

Friday and Saturday all together for $110

NO TICKETS AT THE DOOR CashhAaap 336 214 0218 or online tickets CLICK HERE

RAIS DK.SHEIN AFUTARISHA MKANYAGENI PEMBA

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akisalimiana na Viongozi mara alipowasili katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani katika futari aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Eneo hilo jana akiwa katika utaratibu wa kuwafutarisha Wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba
 Wananchi wa Jimbomla Mkanyageni wakisubi wakati wa Swala ya Magharibi jana katika Futari iliyotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipojumuika na Viongozi na Wananchi wa Mkanyageni katika Swala ya Mgaharibi kabla ya Futari aliyowaandalia Wananchi wa Eneo hilo  katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni utaratibu wake wa kufutarisha kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali katika Futari aliyoiandaa kwa Wananchi wa Mkanyageni   katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni utaratibu wake wa kuwafutarisha Wananchi wa Jimbo hilo kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
 Baadhi ya Viongozi na Wananchi wa Jimbo la Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkowa Kusini Pemba wakiwa katika Futari iliyoaandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni utaratibu wake wa kuwafutarisha Wananchi wa Jimbo hilo kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akijumuika na Viongozi Wanawake katika Futari iliyoaandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni utaratibu wake wa kuwafutarisha Wananchi wa Jimbo hilo kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,(kulia) Mshauri wa Rais Pemba Bi.Mauwa Abeid Daftari  na Mshauri wa  Rais Mambo ya Jamii Bi Zainab Omar Mohamed.
 Sheikh Abdalla Yussuf Ali alipokuwa akitoa shukurani na kuomba dua kwa niaba ya  Wananchi wa Jimbo la Mkanyageni jana baada ya Futari uiliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani,Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni utaratibu wake wa kuwafutarisha Wananchi wa Jimbo hilo kila mwaka katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiagana na Viongozi mara baada ya kumalizika kwa futari  aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkanyageni jana katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani ikiwa ni  utaratibu wake wa  kuwafutarisha Wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba kila ifikapo Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akiagana na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika futari  aliyowaandalia Wananchi na Waislamu wa Mkanyageni jana katika viwanja vya Skuli ya  Sekondari ya Mkanyageni Wilaya ya Mkoani ikiwa ni  utaratibu wake wa  kuwafutarisha Wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba kila ifikapo Mwezi Mtukufu wa Ramadhan(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemedi Suleiman(Picha na Ikulu).

BREAKING NEWS:: WAZIRI DK. MWIGULU NCHEMBA AMSIMAMISHA KAZI MSAJILI WA TAASISI ZA KIDINI WIZARANI

$
0
0
*Wizara yake yaanza kumchunguza aliyesambaza nyaraka na matamko mitandaoni 

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba ametangaza kumsimamisha kazi Msajili wa Taasisi za kidini Maryline Komba, huku akiwaomba viongozi wa dini kuendelea na shughuli zao za kutoa huduma za kiroho.

Pia amesema kwa sasa Wizara yake inaendelea kuchunguza aliyeandika na kusambaza nyaraka katika mitandao ya kijamii ambayo imeibua sintofahamu kwa viongozi wa dini mbalimbali na Watanzania kwa ujumla ili sheria ichukue mkondo wake.

Ameongeza kuwa viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla wafahamu kuwa nyaraka na matamko ambayo yamesambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina baraka za Wizara husika wala Serikali na hivyo ni vema zikapuuzwa tu.

"Tuwaombe viongozi wa dini kupuuza nyaraka ambazo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Endeleeni na shughuli zenu kama kawaida kwani nchi hii inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba na hivyo msiwe na hofu.

"Serikali na viongozi wa dini wamekuwa na ushirikiano mkubwa na hakuna mahali ambapo wanaonekana kutoaminiana. Hivyo aliyesambaza nyaraka hizo tunachunguza na kisha tutachukua hatua zinazostahili,"amesema Dk. Mwigulu.

Akizungumza leo wizarani hapo Dk. Mwigulu amesema msajili huyo amesimamishwa kupisha uchungu wa kina na iwapo atabainika kutohusika na matamko hayo au nyaraka ambazo zinasambaa mtandaoni basi atarudi kwenye majukumu yake.

Amesisitiza kuwa Serikali inaheshimu viongozi wa dini zote huku akionya wanaotaka kutumia dini kama kigezo cha kufanya siasa au kuigawa nchini.

"Wale ambao wanataka kutugawa kwa misingi ya kidini ni vema wakaacha kwani haitakuwa na tija kwao wala kwa Taifa letu. Hivyo tusiwe sehemu ya kushabikia mambo yanayohusu dini,"amesema.

IGP SIRRO AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KIKOSI CHA POLISI RELI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati), akizungumza na Maofisa wa Jeshi hilo kikosi cha Polisi Reli Dar es salaam leo wakati alipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika kikosi hicho kwa lengo la kujionea utayari wao katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. Picha na Jeshi la Polisi.

Airtel kuendelea kuboresha huduma zake kwenda na teknolojia

$
0
0
Airtel yatangaza huduma mpya mbili, yatamba kuendelea kuboresha huduma zake kwendana na teknolojia

Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania imehaidi kuendelea kutoa huduma bora na za kisasa kwa wateja wake. Hii ni kutatua kero na changamoto ambazo zimekuwa zikiikumba sekta ya mawasiliano hapa nchini.

Akiongea jijini Dar es Salaam jioni baada ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja na washirika wake, Mkurugenzi wa Biashara kwa wateja maalum Airtel Tanzania Boniface Bwambo alisema kampuni hiyo itaendelea kutoa huduma bora na za kisasa ili kukidhi matakwa ya wateja wake pamoja na kuongeza pato kutoka na huduma zake kwenye kipindi hiki ambacho ushindani umekuwa mkubwa kwenye sekta ya mawasiliano.

Bwambo alisema baadhi ya bidhaa mpya zinazotolewa na kampuni hiyo ili kwenda na wakati ni fixed portfolio ambayo huwapa wateja nafasi ya kufurahia huduma ya mtandao ya kasi ya Fiber Solutions, Line Solutions na Co-Location Solutions. Huduma hizi ni suluhisho kwa biashara za mtandaoni, inapatikana kwa gharama nafuu katika vifurushi zinazotolewa na Airtel.

Bwambo alisema hayo wakati wa futari iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam. ‘Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kipindi muhimu sana kwa waumini wa dini ya Kislam duniani kote. Kwa kutambua umuhimu huo, sisi Airtel tumeona ni Faraja kukutana hapa siku ya leo na kufuturu kwa pamoja. Hii ni moja ya njia nzuri pia kukutana na wateja na kuonyesha tunawajali. Vile vile, kwa kukutana pamoja hapa inatoa fursa ya kuzungumza na kuonyesha baadhi ya bidhaa zetu kwa wateja wetu, aliongeza  Bwambo.

‘Ni furaha sana kuwa nasi zote hapa. Ni furaha zaidi kuweza kutambua kuwa sisi Airtel tunatoa huduma zaidi ya mawasiliano. Kwa kuongea tu ni kwamba wengi wanajua huduma yetu ya Airtel Money ni kutuma na kupokea fedha na kununua au kulipia bidhaa. Lakini vile vile imeenda zaidi kwa kuweza kukusanya mauzo au mapato kwa wateja na kupeleka moja kwa moja kwenye akaunti yake ya benki. Kwa sasa mfanya biashara hana haja ya kutoka kukusanya mauzo ua mapato kwa sisi kupitia Airtel Money tufanya kazi hio na ndio sababu tunasema Airtel Money ni salama na njia nafuu ya kuweka na kutunza fedha. Alisema Bwambo .

Kwenye tukio la futari hiyo alikuwepo pia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Tanzania Sanjay Rughani. Alipongeza kampuni ya Airtel kwa kutambua umuhimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na pia kwa kutoa huduma bora na nafuu kwa wateja wake.

 ‘Airtel inafanya vizuri kwa kuboresha huduma zake kila siku ili kwenda na wakati kitu ambacho ni muhimu kwa wateja na washirika wake kama sisi. Kuja kwangu hapa leo kumeweza kunipa na kutambua huduma na bidhaa mpya kutoka Airtel ambazo nilikuwa sina taarifa nazo hapa awali. Hii ni jambo la kupongezwa sana, alisema Rughani.

On her side the Administration and Project Manager of the National Industrial and Commercial (NIC) Bank, MsBadriaLema, said out of enjoying sharing iftar with the Airtel staffs and other people, she gets a chance to know other services offered by the company especially Airtel Money profit distribution.

Kwa upande, Meneja Utawala na miradi wa benki ya NIC Tanzania Badrial Lema alisema ni furaha kubwa kuungana na wafanya kazi wa Airtel Tanzania kushiriki futari ya leo. ‘Nimefurahi sana kukutana na wafanyakazi wa Airtel na wageni wengine waalikwa. Ni tukio la iana yake kwani nimeweza kupata marafiki wapya na kuongeza ufahamu juu ya huduma zinazotolewa na Kampuni ya Airtel Tanzania.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel Tanzania akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Tanzania Sanjay Rughani wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam. Kati kati ni Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel Tanzania akimkaribisha moja ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam. Kati kati ni Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon
 Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na wafanya kazi wa kampuni hiyo, wateja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Tanzania Sanjay Rughani akiongea na moja ya wageni waalikwa wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam. Kati kati ni Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso.

 Mkurugenzi wa Biashara kwa wateja maalum Boniface Bwambo akiongea na wafanyakazi wa kampuni hiyo, wateja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Tanzania Sanjay Rughani akiongea na Mkurugenzi wa Biashara Airtel Tanzania Rohit Tandon wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja na washirika wake jijini Dar es Salaam.

MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.

Jenerali Mabeyo ametoa ushauri huo wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Juni 07, 2018.

Mabeyo amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri na hivyo waondokane na dhana ya kuajiriwa  .

“Vijana tunaowachukua JKT ni kwa ajili ya kuwapa elimu na stadi za kazi ili hata kijana akikosa nafasi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama anaweza kurudi kijijini akafanya vitu vya maendeleo, mimi nadhani watu wanahamasishana vibaya kuwa kila anayekwenda JKT lazima aajiriwe,  ipo haja ya kubadili mtazamo” alisema Jenerali Mabeyo

“Jeshi linachukua vijana elfu ishirini kwa mafunzo, wanaochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama hawazidi vijana 2000 sasa hawa wengine 18,000 wanaenda wapi, kama mawazo yatakuwa ni kwenda JKT ili kuajiriwa hatutafanikiwa lakini kama watakwenda JKT kujifunza stadi za kazi kuwasaidia ili ziwasaidie kujiajiri na kubadili maisha yao tutafanikiwa sana” alisisitiza.
 Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Ofisini kwake Juni 07, Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akitoa taarifa fupi ya mkoa kwa Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo(kulia)  wakati alipomtembelea ofisini kwakeJuni 07, 2018 Mjini Bariadi na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi  walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa mkoa wa   Simiyu, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi  walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka  Mjini Bariadi, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
 Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kumaliza mazungumzo  na viongozi hao , Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  wakiteta jambo baada ya Mkuu huyo wa Majeshi kuzungumza na viongozi Mkoani humo Juni 07, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TPA TANGA YAIBUKA MSHINDI KWA TAASISI ZA KISERIKALI ZILIZOSHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI TANGA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasilia na Utalii Japhet Hasunga kushoto akimkabidhi Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kombe la mshindi wa kwanza wa taasisi za serikali zilizoshiriki maonyesho ya biashara ya kimataifa yaliyokuwa yakifanyika Jijini Tanga na kumalizika hivi karibuni
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akiwa na kombe la mshindi wa kwanza wa taasisi za serikali zilizoshiriki maonyesho ya biashara ya kimataifa yaliyokuwa yakifanyika Jijini Tanga akiwa na watumishi wa Bandari hiyo

DKT. NZUKI AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA UNWTO-AFRIKA NCHINI NIGERIA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akisalimiana na Waziri wa Utalii wa Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa barani Afrika (UNWTO), Mhe. Najib Balala walipokutana kwenye semina wakati wa mkutano wa kimataifa wa kujadili takwimu za utalii kama kichocheo cha maendeleo barani Afrika jijini Abuja nchini Nigeria Juni 4-6,2108. Dkt. Nzuki amemuwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla katika mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akiwa na Waziri wa Utalii wa Zambia, Mhe. Charles Banda katika mkutano huo.

TABOA BADO WASUBIRI KUKUTANA NA WAZIRI MKUU,YAWAOMBA WAMILIKI WA MABASI KUENDELEA KUTOA HUDUMA BORA ZA USAFIRI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wasafirishaji wa Mabasi Tanzania(TABOA) Enea Mrutu amewaomba wamiliki wote wa mabasi nchini kuendelea kutoa huduma za kusafirisha abiria kwa umakini wa hali ya juu kwa kuhakikisha hawasababishi ajali wakati wakiendelea kusubiri kukuona na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili watoe kilio chao.

TABOA iliomba kuonana na Waziri Mkuu kwa ajili ya kutoa malalamiko yao kutokana kwa madai kuna sheria na kanuni za usalama barabarani ambazo  ni kandamizi kwao na zimekuwa zikiwaweka katika wakati mgumu katika kutoa huduma ya kusafirisha abiria nchii.

Hata hivyo TABOA bado hawajafanikiwa kuonana naye ingawa tayari ameshawapa maelekezo kuwa wakati wowote atakutana nao na kisha kuwasikiliza ili kupata muafaka kwa kushirikiana na wadau wengine wa usafiri wakiwamo Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra).

Akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam Mrutu amesema wanatambua majukumu aliyonayo Waziri Mkuu hivyo wana imani akipata muda watakutana naye na kisha kuzungumza kwa kina kuhusu changamoto ambazo wanakabiliana nazo watoa huduma ya usafiri nchini.

"Ombi letu kwa wanachama wa Taboa waendelee kutoa huduma bora ikiwa pamoja na kuwa makini barabarani ili kuepuka ajali.Tunamatumaini makubwa na Waziri Mkuu, hivyo tunajua akipata muda atatuita ,nasi tupo tunasubiri.Hivyo wakati tunaendelea kumsubiri tuendelee kutoa huduma ya usafiri bila kuchoka,"amesema Mrutu.

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MALAWI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Malawi ambalo litafanyika Julai 26 hadi Julai 27 mwaka huu mkoani Mbeya.

Kongamano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji  Tanzania(TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) pamoja na Taasisi ya Biashara na Uwekezaji ya Malawi(MITC).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika ofisi za TIC, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amesema kauli mbiu ya kongamano hilo ni "Kuimarisha Uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi" huku lengo la kongamano hilo likiwa kuwatanisha wafanyabiashara /wawekezaji  wa nchi hizo mbili ili kubaini fursa mbalimbali za kibiashara na uwekezaji.

Ambapo amefafanua zitawezesha kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta za viwanda ,usafirishaji,utalii, uvuvi, kilimo ,madini, elimu, afya, benki, mawasiliano, tehama na biashara kwa ujumla.

Pia amesema sambamba na kongamano hilo kutakuwapo na mikutano ya wafanyabiashara (B2B), mikutano ya watendaji wa Serikali(G2G) na mikutano kati ya Serikali na wafanyabiashara (B2G) kutoka nchi hizo mbili.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali.
 Baadhi ya watendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (hayupo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Godfrey Simbeye, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini, Godfrey Simbeye, kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi litakalofanyika Julai 26 na 27 jijini Mbeya, katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Amos Makalla na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NACTE IMEFUTA USAJII KWA VYUO 20 , TISA VYASIMAMISHWA KUDAHILI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)limetengaza kufuta usajili wa vyuo 20 baada ya kubaini vimeshindwa kufuata tararibu zinazoendana na matakwa ya usajili wa vyuo hivyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kaim Katibu Mtendaji wa NACTE Dk.Adolf Rutayunga amesema uamuzi huo umefikiwa kwa kuzingatia kifungu cha 20 cha kanuni za usajili wa vyuo vya ufundi 2001.

Amesema vyuo ambavyo vimefutiwa usajili tayari baraza limeshaviandikia barua vyuo husika kuvitaka vihakikishe kuwa wanafunzi waliko kwenye programu zinazotolewa na vyuo hivyo wanahamia kwenye vyuo vingine vilivyosajiliwa na baraza kutoa programu kama hizo.

Amevitaja vyuo vilivyofutiwa usajili ni Covenant College of Business Sdudies(Dar es Salaam), Mugerezi Spatial Technology College(Dar es Salaam),Techno Brain(Dar es Salaam), DACICO Institute of Business and Management(Sumbawanga) na Arusha Institute of Technology (Arusha).

Vyuo vingine ni Lisbon Business Collage(Dar es Salaam), PCTL Training Institute(Dar es Salaam), Royal College of Tanzania(Dar es Salam), Iringa RETCO Business College(Iringa) na Highlands Health Instutute(Njombe).

Vyuo vingine ni East African Institute of Entrepreneurship and Finacial Management(EAIEFM) (Arusha), Musoma Utali Collage (Shinyanga) na Mlimani School of Professional Studies(Dar es Salaam).

Pia kuna chuo cha Dinobb Institute of Science and Business Technology(Mbeya), Institute of Social Work(Mbeya), Regency School of Hygiene (Dar es Salaam), St.Peters College of Health Sciences(Dar es Salaam), Genesis Institute of Social Science(Dar es Salaam), Institute of Management and Information Technology(Dar es Salaam) na Boston City Campus of Business College(Dar es Salaam).

Pia Dk. Rutayunga amesema mbali ya kufuta usajili kwa vyuo hivyo wamesitisha program zisizoidhinishwa na baraza ambapo vyuo vitatu vimefutiwa programu.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Adolf Lutayunga akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya NACTE Mwenge jijini Dar es salaam wakati akitangaza kufuta vyuo 20 vya ufundi ambavyo havijakidhi viwango na taratibu za usajiri uendeshaji wa vyuo nchini vya ufundi nchini kutoka kulia ni Dk. Marcelina Aloyce Baitilwake na Dk. Gema Modu Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya Vyuo
Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Adolf Lutayunga akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya NACTE Mwenge jijini Dar es salaam wakati akitangaza kufuta vyuo 20 vya ufundi ambavyo havijakidhi viwango na taratibu za usajiri uendeshaji wa vyuo nchini vya ufundi nchini kutoka kulia ni Dk. Marcelina Aloyce Baitilwake na Dk. Gema Modu Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya Vyuo kulia ni Mr. Twaha A. Twaha Mkuu wa Kitengo cha Udahili NACTE.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images