Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 231 | 232 | (Page 233) | 234 | 235 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wakiwa katika msiba wa binti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe Phillip Mangula nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013. Marehemu Nemela amafariki Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari. mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 21, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Nemela Phillip Mangula, binti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe Phillip Mangula nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013. Marehemu Nemela amafariki Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari. mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 21, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakitoa pole kwa familia ya marehemu baada ya kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Nemela Phillip Mangula, binti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mhe Phillip Mangula nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013. Marehemu Nemela amafariki Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari. mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Njombe kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Agosti 21, 2013. PICHA NA IKULU

  0 0
 • 08/19/13--20:00: ngoma azipendazo ankla
 • The Whispers walitamba na ngoma ya 'Rock Steady'

  0 0

  Uncle michuzi asante kwa kuweka ile habari juzi ya kukamatwa mtu na madawa ya kulevya mwenye pasipoti ya Tanzania. 
  Sasa after the incident ya watu ambao kwa 100% tuna uhakika ni wanigeria kukamatwa na sembe na wengine kua involved kwenye cases tofauti zikiwemo human traficking and prostitution sasa wamilik wa condominiums (aina ya hosteli) mbali mbali zinazomilikiwa na Ridzuan Properties wamepitisha utaratibu huu ya kwamba hawataki tena waafrika kukaa kwenye nyumba zao. 
  Hivyo mzazi mwenye mpango wa kumleta mtoto wake huku au mwanafunzi mwenye mpango wa kukaa na  kusoma huku especially Taylors university, Sunway university, Inti university na Segi college Subang tunawashauri ku-book hostel za chuo mapema wasitegemee kukaa nje ya hostel. 

  0 0

  Pamoja na kumuwezesha mtu anayesafiri ndani ya Tanzania kulipia huduma za malazi katika hoteli 142 zilizopo katika Mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa njia ya mtandao, Vinjari (www.vinjari.co.tz) imeanzisha huduma mpya ya kununua tiketi za ndege mtandaoni.

  Kwa kushirikiana na kampuni ya Coastal Aviation, sasa mtu yeyote anayetarajia kusafiri kwa njia ya ndege, anaweza kulipia tiketi yake kwenda katika Mikoa mbalimbali Nchini Tanzania pamoja na Nchi za jirani za Uganda, Rwanda na Msumbiji kwa kupitia Vinjari.

  Huduma za malipo zinafanyika kwa kupitia Mpesa, Tigo Pesa, pamoja na kadi za Benki za Visa na MasterCard. Tembelea https://vinjari.co.tz/v.php?listing=coastalkwa maelezo zaidi.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makzi, Prof. Anna Tibaijuka. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi. Kongamano hilo limefunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Ukumbi wa Bunge la Afrika Mashariki, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha
   
   Baadhi ya wabunge na wageni waliohudhuria ufunguzi wa Kongamano hilo leo, jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Tree Ltd ya Arusha, Magdalena Ayo, kuhusu utengenezaji wa Majiko Bomba, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, lililofunguliwa leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Kongamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuadhimisha Siku ya Mabunge Duniani, kuhusu suala la Makazi, leo Agosti 19, 2013 jijini Arusha. 
  Picha  ya pamoja

  0 0
 • 08/19/13--21:49: Article 8


 • 0 0

   Balozi wa China nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing (kushoto), akikata utepe kuzindua huduma mpya ya kifedha kwa kutumia fedha ya China (Yuan) ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi
  Mtendaji wa benki hiyo, Mizinga Melu.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam.

   Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha NBC, William Kallaghe (kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wenzake katika hafla ya uzinduzi wa huduma za kifedha za NBC kwa kutumia fedha ya kichina. Mgeni rasmi
  alikuwa Balozi wa China nchini, Dk. Yu Youqing.
   Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Maharage Chande (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha benki hiyo, Jane Dogani (kushoto), wakifurahia wakati mmoja wa wateja wao, Amin Juma (katikati) akijibiwa swali alilouliza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo. 
    Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Benki ya NBC, Jane Dogani akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Hotline Service inayomwezesha mteja wa NBC kuuliza maswali yake moja kwa moja kwa ofisa wa benki hiyo awapo ndani ya tawi la benki.
   Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, Eddie Mhina akiongoza shughuli za uzinduzi wa huduma ya Hotline Service ya Benki ya NBC katika Tawi la Corporate jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo pia kwa sasa inaweza kupatikana katikan matawi ya……


  0 0

    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizindua maabara ya mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano     { Tehama } ya chuo Kikuu huria cha Tanzania katika kituo cha Uratibu cha Chuo hicho kiliopo Zanzibar hapo Beit El- Ras Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
   Balozi Seif akiwapongeza wanafunzi wa Kituo cha uratibu cha chuo kikuu Huria Tanzania kiliopo Beit El Ras kwa uamuzi wao wa kujipatia mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano { Tehama }.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza mara baada ya kuizindua maabara ya mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  { Tehama } ya chuo Kikuu huria cha Tanzania katika kituo cha Uratibu cha Chuo hicho kiliopo Zanzibar hapo Beit El- Ras.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania mara baada ya uzinduzi wa maabara ya mafunzo ya { Tehama } ya chuo Kikuu huria cha Tanzania katika kituo cha Uratibu cha Chuo hicho kiliopo Zanzibar.
  Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.

  Vijana Nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za elimu zinazotolewa na vyuo mbali mbali nchini ili kupanda daraja la kitaaluma pamoja na kuwa na uwezo wa uchanganuzi wa mambo tofauti yatakayosaidia Kitaifa katika kupanga na kutekeleza mipango ya kimaendeleo kwa ustadi.
  Wito huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akizindua maabara ya mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano { Tehama } ya chuo Kikuu huria cha Tanzania katika kituo cha Uratibu cha Chuo hicho cha Zanzibar hapo Beit El- Ras Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  Balozi Seif alisema jamii imeshuhudia mabadiliko makubwa ya haraka ya sayansi na teknolojia yaliyosababisha baadhi ya wafanyakazi katika taasisi tofauti za umma na hata zile za kibinafsi kuachwa nyuma kwa kutofahamu matumizi ya taaluma hiyo.
  Ameuomba uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania uendelee kusogeza fursa hiyo karibu zaidi na wananchi kama ilivyo dhamira ya Chuo hicho katika miaka kumi ijayo ambapo Vituo vya Uratibu kama cha Zanzibar vitabahatika kuwa Chuo kwa kushirikiana na Mikoa husika. 
  “ Sote tunafahamu kuwa katika miaka ya hivi karibuni, dunia imeshuhudia mabadiliko ya haraka katika matumizi ya Sayansi na Teknolojia.  Hii imesababisha baadhi ya wafanyakazi waachwe nyuma kutokana na kutofahamu matumizi ya TEHAMA vizuri “. Alieleza Balozi Seif.
  Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua kuwa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimewakomboa wananchi wengi Nchini kwa kuwafikishia elimu ya Cheti, Stashahada, Shahada ya Kwanza pamoja na Shahada za Uzamili na Uzamivu popote pale walipo. 
  Aliupongeza uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Tolly Mbwette kwa azma yao njema ya kuanzisha mafunzo ya TEHAMA hapa Zanzibar kwa ajili ya kusaidia jamii kuendana na kasi ya haraka katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alifahamisha kwamba huo ni mpango mzuri utakaowasaidia vijana waliowengi pamoja na wananchi wa kawaida wa Zanzibar kwenda na wakati.
  Alielezea matumaini yake makubwa kuwa kwa bidii hii iliyoonyeshwa na chuo hicho, itaweza kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kipindi kifupi kijacho kama yalivyoainishwa katika mpango wa mkakati wa Chuo hicho.
  “Bila shaka wengi tumeshasikia kuhusu mkongo wa Taifa wa mawasiliano kwa kutumia kompyuta ambao ujenzi wake unaendelea nchini kote.  Mkongo huu unalenga kuunganisha Wilaya zote za Unguja na Pemba na pia kuunganishwa na mtandao wa Kimataifa ambao huunganisha nchi zote duniani.  Zoezi hili litakapokamilika thamani na manufaa yake yataonekana endapo tutajua jinsi ya kutumia TEHAMA “. Alifafanua Balozi Seif.
  Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika mpango wake huo kinatarajia   kutoa mafunzo ya awali ya matumizi ya kompyuta, Cheti cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano { Tehama } mwaka mmoja na Stashahada ya TEHAMA miaka miwili. 
  Mapema Mkurugenzi, Kituo cha uratibu cha Chuo Kikuu Huria Tanzania kiliopo Zanzibar Bw. Yussuf Mhangwa alisema kituo hicho kina wanafunzi 451, kati ya hao wanafunzik 267 tayari wameshahitimu masomo yao tokea kuanzishwa kwake.
  Bw. Yussuf alisema kazi kubwa iliyopo hivi sasa kwa wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho ni kuwawezesha kupata taarifa mbali mbali zitakazowasaidia kuwapa nguvu na uwezo zaidi wa kukabiliana na masomo yao ya kila siku.
  Alisema Kituo cha chuo Kikuu Huria cha Tanzania hapa Zanzibar kikiwa niongoni mwa vituo vya mwanzo kuanzishwa na chuo hicho nchini Tanzania kimekuwa kikitoa mafunzo ya sayansi, sheria, utalii na uchumi katika kiwango cha shahada ya kwanza na  ya pili.
  Alitoa wito kwa wananchi mbali mbali wa Zanzibar na hasa wale wanafunzi waliomaliza masomo yao ya sekondari kuitumia fgursa hiyo ili kupata taaluma zaidi ya chuo kikuu kwa vile kituo hicho hivi sasa kina uwezo wa kuhudumia wanafunzi 120 kwa wakati mmoja.
  Akimkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo wa maabara ya mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwenye kituo cha chuo Kikuu Huria Tanzania Beit El Ras Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Tolly Mbwette alisema lengo lao ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2014 Mikoa Yote Tanzania iwe na Mfumo huo wa Tehama.
  Profesa Tolly aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jitihada zake za kuikubali Taaluma hii ya Tehama ambayo pia itasaidia watumishi wa Umma kulingana na muda wao watavyoamua kujipangia.
  “ Tumeanzisha kituo cha Jamii katika njia ya kuwawezesha hata wananchi wa kawaida katika sehemu mbali mbali Nchini. Tunba mfano hai kwa wafanyabiashara wadogo wadogo { Maarufu Wamachinga } wanapata mafunzo ya Tehama kwa wakati walioamua kujipangia kuanzia saa 3.00 za usiku hadi saa 6.00 usiku na kwa gharama wanazozimudu “. Alifafanua Profesa Tolly Mbwette.
  Makamu Mkuu huyo wa chuo kikuu huria cha Tanzania alifahamisha kwamba jumla ya wanafunzi 67,103 wamepata taaluma na kufaulu mafunzo yao tokea kuanzishwa kwake mwaka 1993 katika ngazi za stashahada na shahada.

  Na Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar


  0 0


  0 0

   Balozi wa Malaria ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


   Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika uzinduzi huo.  


   Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo.
   Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika uzinduzi huo.  


   Balozi wa Malaria ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga akipeana mkono naMeneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


   Meneja wa Mafao ya Matibabu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ali Mtulia akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) pamoja na NSSF.  0 0

  Globally there are lots of advancements in ways ICT is used to improve accessibility, timely and best matched health services according to the patients conditions. With available technology todate, failure to locate a doctor best-matched to your illness, not being able to make an appointment based on doctors availability but also patient's convenient times and long waiting lines, are all very out-fashioned.
  Caring Tanzanians in the diaspora should also be able search and book an appointment for their loved ones at home. See an example of a doc who has put his profile available and also included clinic times and location;

  As a means to keep up to speed with digital health support systems, an initiative called Daktari Konnect is to be launched in Tanzania and East Africa very soon. All disciplines are included, but the phase 1 of the initiative includes doctors/clinicians-vs.-patients interaction

  Therefore, interested doctors/clinicians are invited to register. Currently more than 40 have done so, but before the service is public announced to Tanzanians, qualified doctors must register first;
   
  Registration requires only 4 steps listed below
  STEP 1: Go to our web [www.daktarikonnect.co.tz]
  STEP 2: Register [on “I am a Doctor” tab]
  STEP 3: Login [username= your valid email address & password emailed to you instantly]
  STEP 4: Complete your profile!
  Obviously this forum may sound more profitable for those in private clinics, but you are strongly encouraged to also enter your clinic locations and availability times for government hospital too, be it you are seeing fast track patients or normal track.

  Above is an example of how the site looks like 

  Best regards,
  Support Team  0 0

  Wafanyakazi wa Airtel wanategemea  kuiingiza rasmi promosheni ya Airtel money, Hakatwi mtu hapa kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kuanzia jumatano wiki hii.
  wafanyakazi wa kampuni ya mitandao ya simu za mkononi Airtel wanafanya hivyo kwa dhumuni la kuelimisha na kuikaribisha rasmi promosheni ya Airtel money, Hakatwi mtu hapa kwa watanzania.
  Airtel imechukua maamuzi hayo katika muendelezo wa kuhakikisha inajenga mahusiano mazuri kati ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wateja wake na kuwapatia huduma bora kwa kuwatembelea maeneo walipo.
  Akizungumza juu ya ziara hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema dhumuni la ziara hiyo ni kuhamasisha na kuwaelewesha wateja mbalimbali wa Airtel juu ya huduma mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na kampuni hiyo ya mitandao ya simu za mkononi hususani promosheni mpya ya Airtel money, hakatwi mtu hapa.
  “Tumeamua kuingia mtaani kuwahamasisha wateja wetu juu ya huduma ya Airtel Money Yatosha kwamba inamuwezesha mteja yeyote wa Airtel kutuma na kupokea pesa bure katika Mtandao wowote hapa Tanzania,” alisema Mmbando.
  Kwa mwaka huu ziara hii inakuwa ni ziara ya tatu kufanywa na kampuni hiyo ya simu za mkononi baada ya ziara nyingine mbili zilizofanywa hapo awali mwaka huu kuwa na mafanikio makubwa sana kwa kuweza kupata nafasi ya kuweza kukutana na wateja wao kwa kutoa Elimu  na kuweza kuwasaidia katika  maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

  0 0

  Globu ya Jamii ina furaha na fahari kutangaza kwamba hatimaye wazazi wa mtoto wa kike Manka wamepatikana na tayari wamemchukua binti yao tokea jana usiku.
  Manka, mwenye umri kati ya miaka 3-4 ambaye jana jioni tulimtangaza kuwa ameokotwa maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam na kuhifadhiwa kituo kidogo cha Polisi cha Salender, ameungana na wazazi wake ambao waliiona taarifa hii mara moja.
  Msamaria mwema aliyetuma habari hii anasema amefurahi sana wazazi wa Manka kupatikana kwani kama mzazi alijihisi vibaya sana kuona mtoto kapotea. Anawashukuru pia askari wa kituo cha Salender kwa kufanikisha hilo. Anamtakia Manka maisha mema na ya fanaka.

  0 0
 • 08/20/13--00:52: KIJIWE CHA UGHAIBUNI


 • 0 0

   Kijana Ramadhani Rajabu akionesha sehemu ambazo amenyofoka nyama kwa kemikali hizo.
  Kijana Said Omari akionesha sehemu za vidole vyake vilivyoathirika kwa kemikali hizo

  Na Mashaka Mhando,Handeni
  VIJANA 12 wa kijiji cha Manga kilichopo kata ya Mkata wilayani hapa, wameanza kunyofoka nyama kutokana na madai ya kubeba magunia yenye kemikali baada ya lori lililokuwa limebeba mzigo huo, kupinduka katika eneo la dajani la kitongoji cha Tengwe kijijini.

  Vijana hao wamepata athari hizo baada ya kupewa kibarua cha muda mfupi wa kubeba maguni yaliyokuwa na uzito wa kilo 25 kuyafaulisha kwenye gari jingine na kulipwa ujira wa sh. 95,000 ambazo waligawana sh. 11,500 kila mmoja baada ya kumaliza kazi hiyo.

  Ofisa Tarafa ya Mazingara Bw Hashim Msagati alisema kuwa tukio hilo limetokea Julai 26 mwaka huu majira ya saa 11:00 jioni katika eneo hilo baada ya lori lenye namba za usajili T 787 CBT lililokuwa na tela lenye namba T 101 BTB kupinduka kisha watu waliokuwa kwenye gari hilo, kuwapa kazi vijana hao kubeba mizigo hiyo.

  Alisema lori linadaiwa kumilikiwa na kiwanda cha soda cha Bonite kilichopo mjini Moshi, lilipata ajali hiyo iliyothibitishwa na polisi wa kituo cha Mkata, lilikuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda mkoani Kilimanjaro, likiwa limebeba mifuko yenye kemikali hizo.

  Wakizungumza na gazeti hili, wakiwa nyumbani kwao katika kijiji hicho cha Manga, mmoja ya waathirika hao Bw. Said Omari alisema walipata kazi hiyo kutoka kwa mtu mmoja aliyekuwa na asili ya Kihindi kupakia mifuko hiyo bila kuelezwa kwamba kilichomo ndani yake ni madawa makali.

  Aliwataja wenzake waliokuwa pamoja ni Omari Bahorela, Khatib Juma, kassim Bakari, Hamis Chilo, Ramadhani Rajab, Ramadhani Mbelwa na Omari Mbuji kutoka katika mji wa Manga na Lazaro Jackson, Aweso Mussa, Mkombozi Mussa na Mohamedi Shabani waliotokea kitongoji cha Tengwe.

  Alisema baada ya kufika kwenye eneo hilo, walianza kubeba mizigo hiyo na kuipakia kwenye gari jingine lakini ghafla mwezao mmoja Kasimu alianza kuanguka chini akawa hawezi kusimama baada ya madawa hayo kuanza kumuunguza miguuni na kwenye shingo hatua ambayo walianza kuogopa kuendelea na zoezi hilo.

  "Mwenzetu alipokuwa ameanguka chini akawa hawezi kuinuka huku akilia miguu kumchoma kwa ndani na huku akishindwa kuinuka pale chini, tulianza kuogopa tukamwagia maji tukazidisha maumivu, tulikataa kuendelea na zoezi lile lakini yule Mhindi akasema hapana endeleeni mifuko iliyobaki, vinginevyo hatatulipa," alisema Bw Said.

  Alisema hata hivyo, waliendelea kubeba na walipomaliza wakalipwa fedha hiyo ingawa walikuwa wamekubaliana ujira wa sh. 100,000 wakapewa sh. 95,000, lakini mwenzao yule hakuweza kutembea hadi wakambeba pamoja na Mhindi huyo kumrudisha nyumbani kwao kisha wakaondoka kuendelea na safari.

  Bw Said alisema kesho yake walianza kunyofoka nyama kila mmoja aliyebeba mizigo hiyo na ngozi kuwa nyeupe huku wakipata maumivu kwenye uti wa mgongo na maeneo mengine ya miili yao hatua ambayo wanashindwa kupata matibabu sahihi kutokana na kukosa fedha.

  Akizungumzia zaidi tukio hilo Bw. Msagati alisema kuwa wamepeleka taarifa hizo kwa viongozi wa wilaya ili waweze kuchukua hatua ya kuwatafuta waliohusika kwa ajili ya kuwasaidia matibabu vijana hao na kusafisha eneo lililopata ajali hiyo amba[po wanahofu kwamba endapo mvua itanyesha, inaweza kusombwa na kuingia katika visima vya maji na kuleta madhara makubwa kwa jamii.

  Mkuu wa wilaya ya Handeni, Bw Muhingo Rweyemamu alisema atafika katika kijiji hicho kuwatembelea vijana hao kisha kuona eneo lililopata ajali kabla ya kuchukua hatua nyingine.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal wakiwa katika picha ya pamoja na na wakuu wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki  vilivyotunukiwa hati ya idhini leo katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam


   Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi Hati Idhini ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Nelson Mandera, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni Mkuu wa Chuo hicho, wakati wa hafla ya kuvitunuku Hati Idhini Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Agosti 20, 2013.
   Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, akimkabidhi Hati Idhini ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Nelson Mandera, Makamu wake, Prof. Burton Mwamila, wakati wa hafla ya kuvitunuku Hati Idhini Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Agosti 20, 2013. Katikati ni Rais Jakaya Kikwete, akishuhudia.
   Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo.
   Rais Jakaya Kikwete, akihutubia baada ya kutunuku Hati Idhini kwa Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. 
   Rais Jakaya Kikwete, akihutubia baada ya kutunuku Hati Idhini kwa Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. 
   Picha ya pamoja kwa kumbukumbu baada ya shughuli ya kutunuku Hati Idhini kwa Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Picha ya pamoja kwa kumbukumbu baada ya shughuli ya kutunuku Hati Idhini kwa Vyuo Vikuu Vishiriki nane vya nchini vilivyotimiza vigezo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR
  0 0

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Windhoek Namibia.

  Hatimaye michezo ya nane kwa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) yamefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Namibia Dk Hage Geingob katika uwanja wa Taifa wa Namibia na kupambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma, nyimbo sarakasi na maonyesho ya helkopta.

  Ufunguzi wa mashindano hayo ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi wanachama wa SARPCCO akiwemo IGP Said Mwema.

  Akizungumza katika ufunguzi huo Dk Geingob alizitaka timu zinazoshiriki mashindano hayo kushindana kwa nidhamu na kudumisha urafiki uliopo ili kuweza kukabiliana na uhalifu kwa kubadilishana mbinu na mikakati kutoka katika mataifa yao kwa lengo la kuwa na ukanda salama wa Kusini mwa Afrika.

  Alisema nchi zinashiriki zinahitaji ushindi lakini ni vyema zikatambua kuwa timu moja na bora ndiyo itakayonyakua ushindi kwa kuwa mshindi ni mmoja tu kati ya mataifa yote yaliyoshiriki.

  Wakati huohuo Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema amewataka wachezaji wa Tanzania kuhakikisha kuwa wanarejea na ushindi ili kupata zawadi nono ambazo amewaaandalia endapo wataibuka na ushindi katika michezo hiyo.

  IGP Mwema aliyasema hayo wakati alipowatembelea na kuzungumza na wachezaji wa Tanzania katika hoteli waliyofikia ili kuwapa hamasa na morali wakati wote wa michezo hiyo.

  Alisema kitu kikubwa ambacho wachezaji hao wamekifuata nchini Namibia ni ushindi hivyo wahakikishe kuwa wanacheza michezo yote kwa morali na kuibuka na ushindi jambo ambalo litalitea taifa na Jeshi la Polisi sifa.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,IGP Said Mwema (mwenye suti) akizungumza na baadhi ya wachezaji wa timu ya Jeshi la Polisi wanaoshiriki Mashindano ya michezo ya nane kwa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO GAMES) yaliyofunguliwa rasmi leo,nchini Namibia.
  Timu ya Jeshi la Polisi la Tanzania.
  Michezo ikiendelea.


  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akimshukuru Bw. R. de Roon, mmoja wa wabunge wa Bunge la Uholanzi waliofika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya kupata ufahamu zaidi kuhusu sekta ndogo ya gesi na mafuta.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe.Jaap Frederiks (kulia) pamoja na Bw. R. de Roon (Mb.) mara walipomtembelea ofisini kwake.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na ujumbe kutoka Uholanzi ulioongozwa na Balozi mteule wa Uholanzi nchini Tanzania Mhe.Jaap Frederiks (wa tatu kutoka kulia) pamoja na wabunge wa Bunge la Uholanzi wakati walipomtembelea ofisini kwake.

  Balozi mteule wa Uholanzi hapa nchini, Mhe.Jaap Frederiks akiongozana na ujumbe wa wabunge 7 kutoka Bunge la Uholanzi wamemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa nia ya kupata ufahamu zaidi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ndogo ya mafuta na gesi nchini.

  Akiongea katika mkutano huo, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alieleza kuwa shughuli za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia zinaendelea katika maeneo ya kina kirefu cha bahari, mwambao wa bahari, katika maziwa na nchi kavu na kiasi cha gesi asilia kilichogundulika mpaka sasa ni futi za ujazo trilioni 43.1 hivyo inatarajiwa kuwa baada ya miaka miwili Tanzania itakuwa na gesi ya kiasi cha futi za ujazo trilioni 200.

  Kuhusu sera ya gesi Waziri Muhongo alisema kuwa kwa sasa Serikali imeshaandaa rasimu ya sera ya gesi ambayo imeshajadiliwa na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi, Taasisi za Elimu ya Juu, sekta binafsi, Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na mwishoni mwa mwaka huu inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge la Tanzania ili ikajadiliwe na baadaye kutungiwa sheria itakayoendana na shughuli za utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi nchini.

  0 0

  Sehemu ya Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani cha Msamvu, mjini Morogoro kikionekana kutoka angani, Augosti 20, mwaka huu. ( Picha na John Nditi).

  0 0

  Mama Tunu Pinda
  MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amesema kuna haja ya kuweka juhudi za makusudi za kuwawezesha wasichana wote nchini kuondokana na aibu zinazowazuia kuhudhuria masomo yao kila siku.

  Amesema kukosekana kwa vifaa vya kujisetiri miongoni mwa wasichana waliofikia balehe, ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wakose masomo kati ya siku 30 hadi 70 kwa mwaka jambo ambalo linachangia kudorora kwa elimu miongoni mwao.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Agosti 20, 2013) wakati akizindua Mradi wa Hakuna Wasichoweza katika Shule ya Msingi Chilongola, iliyoko Manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara. Mradi huo unafadhiliwa na Taasisi ya T-MARC inayojihusisha na Masuala ya Afya na Maendeleo, umelenga kuwafikia wasichana 10,000 katika wilaya mbili za mkoa wa Mtwara, yaani Manispaa ya Mtwara Mikindani na Wilaya ya Mtwara Vijijini.

  “Wasichana wengi wanapopata siku zao, hushindwa kuhudhuria masomo yao kati ya siku tatu hadi saba kwa mwezi au siku kati ya siku 30 hadi 70 kwa mwaka. Hii husababishwa na wasichana hawa kukosa nyenzo za uhakika za kujisitiri wakiwa shuleni. Wengi wao huamua kubaki nyumbani hadi pale mizinguko yao itakapokwisha ili kuepuka kuaibika...,” alisema.


older | 1 | .... | 231 | 232 | (Page 233) | 234 | 235 | .... | 3272 | newer