Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WALIOISHIA VETA SASA WANAWEZA KUSOMA ELIMU YA JUU

$
0
0
Filbert Rweyemamu.

Arusha.Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) imethibitisha matumizi ya mtaala unganishi wa masomo ya ufundi nchini utakaowawezesha wahitimu wa vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi(Veta) kuendelea na elimu ya juu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtaala huo,Mkurugenzi wa Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini,Dk Noel Mbonde amesema utasaidia kuwapa fursa vijana wengi waliotamani kuendelea na masomo ya ufundi ya juu kunufaika.Amesema serikali inathamini maboresho hayo yanayotoa nafasi ya kuwanoa wataalamu wa kutosha inayoenda sambamba na sera ya serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa viwanda.

"Kulikua na tatizo la wanafunzi wetu wanaohitimu Veta kuendelea na kozi za juu za ufundi na sababu kubwa ilikua ni kukosekana kwa sifa za kuwawezesha kujiunga na kozi za ufundi katika ngazi ya Stashahada na kuendelea mtaala unganishi umekua jibu,"alisema Dk Mbonde

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Erick Mgaya amesema mtaala huo ni matokeo ya mahitaji ya wahitimu wengi wa vyuo vya Veta nchini kuwa na shauku ya kuendelea na masomo ya juu ya ufundi.

Amesema kwa ushirikiano wa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sault nchini Canada walikamilisha mtaala huo unawapa sifa wanaotaka kuendelea na masomo kwa kuhudhuria kozi maalumu kwa muda mwa miezi mitatu.Naye Mratibu wa NACTE Kanda ya Kaskazini,Godfrey Komba amesema mtaala huo umekuja kwa wakati muafaka ambao serikali inahimiza matumizi ya teknolojia katika kusukuma ajenda ya uchumi wa viwanda nchini.

Aliwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo ya kupata elimu unganishi inayowapa nafasi ya kuendelea na elimu ya juu ya ufundi itakayofungua milango zaidi kwa kutoa nafasi ya kupata ajira kwenye makampuni makubwa na kujiajiri wenyewe.


Kwa upande wake Mshauri wa Elimu ya Ufundi kutoka nchini Canada,Dk Allan Copeland amesema jumla ya wanafunzi 72 wameanza kozi unganishi katika Chuo cha Ufundi Arusha kutoka mikoa mbalimbali ambao ni wahitimu wa vyuo vya Veta.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Standi nchini,Dk Noel Mbonde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtaala Unganishi katika Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)jijini Arusha ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi(ATC),Dk Erick Mgaya. 
Mkurugenzi wa Ufundi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Standi nchini,Dk Noel Mbonde akizinduzi wa Mtaala Unganishi unaowawezesha wahitimu wa Veta kuendelea na elimu ya juu ya ufundi,kushoto ni Mshauri wa Ufundi kutoka Canada,Dk Allan Copeland na kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi(ATC),Dk Erick Mgaya. 
Mkurugenzi wa Ufundi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Standi nchini,Dk Noel Mbonde akionesha Mtaala Unganishi uliozinduliwa katika Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) jijini Arusha,kushoto ni Mshauri wa Ufundi kutoka Canada,Dk Allan Copeland na kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Erick Mgaya 


WAHITIMU MAFUNZO YA AWALI YA KIJESHI KAMBI YA 821 KJ WAHIMIZWA KUWA MFANO WA KUIGWA KATIKA JAMII

$
0
0
Na Rhoda EZEKIEL kigoma,

VIJANA wanaohitimu mafunzo ya awali ya kujitolea ya oparesheni Mererani ya Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)Kambi ya Bulombola 821KJ kuwa mfano wa kuigwa na jamii wanayoenda kuishinayo pamoja na kujikita katika shughuli za uzalishaji mali ili kufikia azma ya Rais wa Serikali ya Awamu ya tano Dk.John Magufulu kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kuwa Tanzania ya viwanda.

Mwito huo ulitolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia General Marko Gaguti katika sherehe za kuhitimu mafunzo ya awali ya kijeshi katika kambi hiyo wilayani Uvinza mkoani Kigoma na kuwataka kutumia stadi za kazi wanazofundishwa, na kuwa mfano kwa vijana wengine na kusaidia Serikali kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Brigeda Jenerali Gaguti amesema mafunzo waliyoyapata vijana yanawafanya kuwa wazalendo na vijana wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleo na kutoa mwito kuwa mafunzo hayo waliyoyapata wayatumie kujijenga kiuchumi na kujiajiri wenyewe ili kuanzisha viwanda na kuwa na uchumi wa kati.

"Nitoe rai vijana mliohitimu mafunzo haya muwe vijana mnaowaza mtaifanyia nini Tanzania na si Tanzania iwafanyie nini, na vijana wenye uthubutu mtakaosaidia kutoa suluhu kwa changamoto ya vijana nchini na si sehemu ya matatizo ya vurugu na mtoe darasa kwa vijana wengine kufanya matendo mema,"amesema Jenerali Gaguti.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha 821KJ kambi ya Bulombola Luteni Kanali Rashidi Kanole amesema vijana waliohitimu mafunzo hayo ya oparesheni Mererani ni vijana 839 ambapo wavulana 55 na wasichana 284 ambao wamehitimu mafunzo ya awali ya kijeshi na watatakiwa kuendelea kuwepo katika kambi hiyo kujifunza stadi za maisha .
Aidha amewataka vijana hao kuzingati nidhamu waliyoelekezwa na wakufunzi wao na kuendelea kushiriki katika shughuili za maendeleo katika kambi hiyo kwani kambi hiyo inajishughulishana shughuli za kilimo cha michikichi na alizeti kwa ajili ya kuwajenga vijana wanaoingia katika mafunzo kambini hapo kujiajiri wenyewe baada ya mafunzo.

Wakati huohuo Mwakilishi Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Kanali Juliusi Kadawi amesema vijana wanatakiwa kuisaidia Serikali katika masuala ya ulinzi na usalama na kuwa vielelezo kwa vijana wengine ambao bado hawajapata mafunzo hayo, kwani wakufunzi waliowafundisha vijana hao wamefanya kazi kubwa na kutokana na maonyesho walionesha yanaonesha jinsi gani walivyopikwa ipasavyo.

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKURUGENZI MTENDAJI MTANDAO WA JAMII RORUMS

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na Mwanahisa wa  mtandao wa Jamii Forums, Micke William baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu.

Max na Micke wameachiwa huru leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi  Godfrey Mwambapa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kuona kuwa ushahidi uĺiotolewa na mashahidi hao dhidi ya washtakiwa umeshindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha na kuongeza kuwa hauna mashiko. 

Katika kesi hiyo namba 457 ya mwaka 2017 washtakiwa wanatuhumiwa kuwazuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi.

Kabla ya uamuzi huuo kutolewa leo, awali washtakiwa hao walisomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali  Mutalemwa Kishenyi ambae alidai  Melo na William  ni wamiliki na waanzilishi wa mtandao wa Jamii  Media Co Ltd ambao umesajiliwa Brela Julai 2 mwaka 2008 na kupewa namba ya usajili 66333 

Alidai baada ya usajili, hupatiwa taarifa za siri ambazo huwezesha mtu kuingia katika mtandao huo husika hivyo washtakiwa hao walikuwa na uwezo wa kuona taarifa kwenye mfumo wao.

Aidha katika maelezo hayo, Kishenyi  alidai Mei 10 mwaka 2016, ZCO aliwaandika barua washtakiwa akiwafahamisha ofisi yake inafanya upelelezi kuhusu taarifa ya uongo dhidi ya Cusna Investment na Ocean Link iliyochapishwa na  mwanachama wao Kwayu JF senior Expert member na Amrishipuri. ZCO pia aliwafahamisha  kwa kifupi taarifa ambayo anaihitaji kutoka kwao  na maelezo binafsi ya mtu aliyechapisha  ili aweze kufanya upelelezi.

Alibainisha kuwa Mei 11mwaka  2016 mfanyakazi wa Jamii Media, Chrispin Mganyizi aliipokea na kuiwasilisha kwa washtakiwa  lakini walikwamisha polisi kufanya upelelezi kwa kuficha taarifa za wanachama wao Kwayu JF senior Expert member na Amrishipuri.

Kishenyi alidai kuwa kufuatia jitihada hizo za ZCO za kuwataka washtakiwa kutoa taarifa muhimu na wao kukataa walikamatwa na kufikishwa mahakamani.

WAFANYAKAZI WANNE MAMLAKA YA BANDARI,WENZAO WAWILI SASA WASUBIRI KUSOMEWA MAELEZO YA AWALI JUNI 18,2018

$
0
0
*Ni katika kesi ya kudaiwa kuhujumu uchumi inayowakabili, yupo Masoud Suleiman Kova

 Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

WAFANYAKAZI wanne wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na wenzao wawili wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia TPA hasara ya Sh.26,041,782.73,ambapo Juni 18 mwaka huu watasomewa maelezo ya awali (PH).

Washtakiwa ambao watasomewa PH katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Thomas Simba ni  Masoud Suleiman Kova (36) mhasibu wa TPA washtakiwa wengine ni Lydia Kimaro (52) mhasibu TPA, Ally Mkango (54)  Oparesheni ofisa wa TPA na Aron Luisinga (35) mhasibu TPA. Wengine ni wafanyakazi wa benki ya CRDB,  Grace Komba (41) na Juma Ng'oka (41).

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya washtakiwa kusomewa PH lakini bado hajamaliza kuiandaa.Hivyo taarifa hiyo,  kesi imeahirishwa hadi Juni 18 mwaka huu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kushindwa kuzuia kutendeka kwa kosa na kusababisha hasara.

MKURUGENZI MPYA UNITED BANK FOR AFRICA AAHIDI BENKI YAO KUENDELEA KUISAIDIA SERIKALI KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

UONGOZI wa United Bank for Africa(UBA) Tawi la Tanzania umeweka wazi moja ya mkakati wake ni kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano kutekeleza mipango ya maendeleo huku ukisisitiza kutoa huduma bora za kibenki nchini.

Pia umesema unajivunia mafanikio yake katika kutoa huduma bora za kibenki na uwepo wake nchini Tanzania umetoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuendelea kueleza namna ambavyo wamekuwa wakitoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo, wakubwa na wakati.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam wakati wa kutambulishwa kwa Mkurugenzi mpya wa Benki hiyo nchini Usman Isiaka ambapo uongozi wa UBA umetumia nafasi hiyo kuelezea mipango mbalimbali na hatua ambazo wanazoendelea kuchukua katika kutoa huduma bora kwa wateja wao.

Akizungumza kuhusu ushirikiano kati yao na Serikali mbele ya waandishi wa habari Isiaka amesisitiza umelenga katika kusaidia miundombinu ya barabara, nishati, elimu na kukuza mitaji ya wajasiriamali.

"Tunajivunia kuwepo nchini Tanzania na kwetu ni fahari kubwa tunapoona tunatoa huduma za kibenki lakini wakati huo huo tunashiriki katika kusaidia ukuaji wa maendeleo katika nyanja mbalimbali.Hivyo tutaendelea na mkakati huo kwani UBA ipo kwa ajili ya Bara la Afrika ikiwemo na Tanzania,"amefafanua.

Ameongeza kwa kuzingatia taratibu na misingi ya uendeshaji wa huduma za kibenki nchini, UBA imejipanga kuhakikisha inawasimamia wajasriamali wadogo na wakubwa pamoja na kampuni kwa kuwapa mikopo yenye riba nafuu, ili kukuze mitaji na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi ambao umeendelea kuwa imara siku hadi siku .

Kuhusu benki hiyo amesema inafanya shughuli zake katika nchi 20 za Bara la Afrika na kubwa zaidi wamejiimarisha katika utoaji wa huduma bora za kifedha nchini huku ikikusudia kuendeleza mikakati katika maendeleo ya sekta za kilimo,nishati, barabara pamoja na uzalishaji wa bidhaa za viwanda.

Wakati kwa Tanzania, amesema tangu ianzishwe miaka tisa iliyopita UBA imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali na kusaidia kusukuma kasi ya ukuaji wa maendeleo ya nchi, hatua inayowafanya wao waaamini wanatekeleza wajibu wao.Isiaka ameipongeza Tanzania kwa namna inavyozisimamia taasisi za kibenki licha ya uwingi wa taasisi hizo hapa nchini.

Wakati huohuo Ofisa Mtendaji Mkuu wa UBA Kanda ya Afrika Mashariki Emeke Iweriebor, amesema pamoja na maboresho ya huduma mbalimbali yanayofanywa na benki hiyo kwa wateja wake, wamekusudia kuendelea kufungua matawi maeneo mbalimbali hapa nchini ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wateja wake.

Pia wamewaomba watanzania kuendelea kujiunga na UBA ili nao wawe sehemu ya watakaofurahia huduma ambazo za kifedha zinazotolewa na benki hiyo ambayo kwa sehemu kubwa imejikita kutoa huduma kiteknolojia zaidi.

RC TABORA : WATENDAJI KUANZA ZOEZI LA UHAKIKI WA WATOTO WA KIKE WALIOHAMIA MIKOA MINGINE

$
0
0
Na Tiganya Vincent
WAKUU wa Wilaya na  Watendaji mkoani Tabora wametakiwa kuanza uhakiki  wa uhamisho wa  wanafunzi wote wa kike waliohama kutoka mkoani humo kwenda kwingine ili kujiridhisha kama kweli wanaendelea na masomo au walihamishwa ili wakaolewe.
Hatua hiyo inalenga kupata taarifa sahihi za watoto wa kike waliohamisha wakiwa darasa la nne na kuendelea hadi sekondari  kama kweli wanaendelea na masomo yao au walihamishwa ili wakawe wake za watu.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kwenye ziara yake katika maeneo mbalimbali mkoani humo wakati akiendelea na kampeni ya operesheni komesha utoro, mimba  na ndoa za utotoni.
Alisema baadhi ya wazazi wakiona mtoto wao ambaye yuko shuleni amechumbiwa wamekuwa wakitumia mbinu hiyo chafu ya kudai wanahamishia mikoa mingine kwa ndugu zao ili wamuoze na kumkatisha masomo yake.
 “Nawaagiza anzeni kufuatilia watoto wote wa kike waliohama kuanzia mwaka 2015 walipokwenda kama kweli wanasomo…kama hawasomi warudisheni hapa ili nianze kufutilia nani aliyepata mpango huo ili nipambane naye…kama kuna mtumishi au mzazi alihusika nitamsomba mzima ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye kutaka kupanga mbinu hizo chafu” alisema Mwanri.
Alisema kuna wazazi au walezi kwa sababu wanajua kuwa hawawezi kwenda shule kusema kuwa wanamuomba mtoto wao akaolewe kwa sababu amepata mchumba wanachodai anahamia Kahama au Katavi kwa Shangazi yake au baba yake mtoto ili kuhalalisha uhamisho kumbe anaishia hapa katikati.
Mwanri aliwataka kutumia mifumo ya kiserikali iliyopo kuwasiliana na watendaji wa Mikoa au maeneo mengine ambayo wazazi wa watoto hao wanadai wamehamia ili kujua ukweli wa uhamisho huo isije ikiwa ni udanganyifu.
“Wewe Ofisa Elimu au Mkuu wa Shule unajua ni shule gani ambayo mzazi au mlezi wa mtoto alidai anamuhamishia mtoto wake…piga simu kwa Ofisa mwezako au Mkuu wa Shule ambayo mtoto alidaiwa kuhamisha ili kujua kama kweli yuko shuleni…kama hayupo peleka taarifa kwa Mtendaji wa Kata au Mkuu wa Wilaya ili mhusika akamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake” alisema.
Alisema anataka ifikapo mwakani Mkoa wa Tabora uwe wa kwanza kwa watoto ambao wanahudhuria shuleni na sio kwa utoro.
 Baadhi ya wakazi wa Miguwa wilayani Nzega wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora ( hayupo katika picha) jana wakati akiendelea na kampeni yake ya kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya na kukomesha utoro shuleni.
  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Tabora Vedastus Kalungwani akitoa maelezo kwa wanaushurika wa Miguwa wilayani Nzega jana jinsi ya kujiunga na aina ya Bima ijulikanayo Ushirika Afya.
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula akitoa maelezo jana wakati wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kupambana na utoro ambayo inaoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiendesha kampeni katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Nzega juu ya kupambana na utoro mashuleni na kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya. Picha na Tiganya Vincent

SUMA JKT YAINGIA MAKUBALIANO KULINDA MAJENGO NA MIUNDOMBINU YA TTCL NCHI NZIMA

$
0
0
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania - TTCL Corporation limeikabidhi kandarasi ya Ulinzi wa Majengo, mali na Miundo mbinu yake kwa SUMA JKT, Kampuni Tanzu ya Jeshi la kujenga Taifa kwa mkataba wa mwaka mmoja kuanzia Juni 01 2018. 

Hafla ya utiaji saini Makubaliano hayo imefanyika leo katika Makao Makuu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania- TTCL Corporation na kuhudhuriwa na Viongozi waandamizi wa taasisi hizo mbili na watendaji wa Idara mbali mbali.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation Bw. Waziri Kindamba amesema, TTCL ina furaha kubwa kushirikiana na SUMA JKT katika jukumu hili nyeti la Ulinzi na Usalama wa Majengo, Mali na Miundo mbinu yake.

“Tuliwapa SUMA JKT kazi ya Ulinzi katika Makao Makuu ya Shirika letu na katika Kituo cha Kimataifa cha kutunzia Kumbukumbu(NIDC) kilichopo Kijitionyama Dar Es salaam. SUMA JKT wamefanya kazi yao kwa Weledi, nidhamu na ufanisi mkubwa, ndio maana leo tunayo furaha kuwakabidhi jukumu kubwa zaidi la kutulinda katika Ofisi zetu Nchi nzima.”

Bw. Kindamba amesema, TTCL Corporation ni Shirika jipya la Mawasiliano Tanzania ambalo limechukua nafasi ya iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL LTD. Miongoni mwa majukumu mahsusi ya TTCL Corporation ni kuchochea kasi ya ukuaji wa Uchumi, kusimamia maendeleo ya Sekta ya Mawasiliano kwa kuwaunganisha Wananchi wote, kusimamia ufanisi wa Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano kwa niaba ya Serikali, kusaidia shughuli za Ulinzi na Usalama wa Nchi, Huduma za Jamii na ukuaji wa Sekta nyingine zote.

“Hii ni TTCL mpya ambayo imedhamiria kuwahudumia Wananchi kwa Viwango vya hali ya juu. Tutaweza kutimiza vyema wajibu huo tukiwa na uhakika katika ulinzi na usalama wa Watendaji wetu, mali zetu na Miundombinu yetu ambayo ni muhimu sana kwa Ulinzi na Usalama wa Nchi, amesema.”

Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT, Kanali Aristides Rutta amesema, licha ya Nidhamu na Ujuzi wa Kijeshi walio nao vijana wake, Kampuni hiyo inajivunia mafunzo na vifaa vya kisasa vya kufanyia kazi, rekodi iliyotukuka katika utekelezaji wa miradi ya Wananchi na nyenzo za Ulinzi na Usalama walizonazo.

“Tunalishukuru sana Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa Imani kubwa waliyotupa, tunawakikishia utendaji uliotukuka kwa uzalendo wa hali ya juu wakati wote wa kutimiza majukumu yetu katika kandarasi hii. SUMA JKT imepata umaarufu mkubwa Nchini hasa baada ya kutekeleza kwa mafanikio kandarasi mbali mbali katika Sekta za Ulinzi na Ujenzi wa Miundombinu katika maeneo mengi Nchini.
Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (kulia) pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT,Kanali Aristides Rutta (kushoto) wakisaini mkataba wakampuni ya SUMA JKT kulinda Majengo, mali na Miundombinu ya kampuni ya TTCL Corporation. SUMA JKT ambao ni Kampuni Tanzu ya Jeshi la kujenga Taifa itafanya kazi hiyokwa muda wa mwaka mmoja, kuanzia Juni Mosi, 2018. 
Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (kulia) pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT,Kanali Aristides Rutta (kushoto) wakibadilishana nyaraka zamkataba wa kampuni ya SUMA JKT kulinda Majengo, mali naMiundo mbinu ya kampuni ya TTCL Corporation mara baada ya kusaini. SUMA JKT ambao ni Kampuni Tanzu ya Jeshi la kujenga Taifa itafanya kazi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja,kuanzia Juni Mosi, 2018. Nyuma yao ni wanasheria wa TTCL na Suma JKT wakishuhudia zoezi hilo.
Picha ya pamoja ya maofisa wa TTCL Corporation na SUMA JKT mara baada ya hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu yaTTCL Corporation jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kutiliana saini na kampuni ya SUMA JKT kuingia makubaliano ya kulinda Majengo, mali na Miundo mbinu ya kampuni ya TTCL Corporation. Kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa -JKT, Kanali Aristides Rutta akifuatilia mazungumzo hayo. Kwa mujibu wa makubaliano hayo SUMA JKT ambao ni Kampuni Tanzu ya Jeshi la kujenga Taifa itafanya kazi hiyo kwa muda wa mwaka mmoja, kuanzia Juni Mosi, 2018. 

WAJUMBE WA BODI YA NSSF WARIDHISHWA NA UKUAJI WA MIWA KATIKA MRADI WA MIWA WA KIWANDA CHA MKULAZI II- MBIGIRI

$
0
0
 Wajumbe wa Bodi ya NSSF wakipata maelezo kuhusu shamba la miwa la Mradi wa Kiwanda  cha Sukari cha Mkulazi  II kilichopo Mbigiri kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi Eng Robert Kabudi baada ya Bodi hiyo kutembelea na kujua maendeleo ya Mradi huo.
Wajumbe wa Bodi ya NSSFwakifurahia ukuaji wa Miwa katika shamba la miwa la Mradi wa Kiwanda  cha Sukari cha Mkulazi  II kilichopo Mbigiri walipotembelea na kujua maendeleo ya Mradi huo.

Introducing "MARUKUTU" by Catrima ft. Sokomoko @ Mkubwa Na Wanae Music

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKABIDHI RIPOTI MAALUMU ZA UVUVI WA BAHARI KUU NA GESI ASILIA

MAFUNZO KWA KAMATI YA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO SHINYANGA YAFUNGWA

$
0
0
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo,Katibu tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga alisema ili kukomesha vitendo hivyo ni lazima kila mmoja ashiriki kwa nafasi yake. 

“Ni lazima wadau wote waweke nguvu ya pamoja kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto,hivyo mafunzo haya mliyopata yawe chachu ya kuleta mabadiliko katika jamii yetu ili wanawake na watoto waishi salama”,alieleza Msovela. 

Aidha alisema kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga ni kamati ya kwanza nchini kuundwa na kupatiwa mafunzo na tayari uundaji wa kamati katika ngazi ya halmashauri,kata na vijiji unaendelea. 

Mafunzo hayo yaliyoanza Mei 30,2018 yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kukutanisha wajumbe wa kamati hiyo ambao kwa pamoja watashiriki katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga. 

Kupitia mafunzo hayo,wajumbe wa kamati hiyo wamejifunza kuhusu dhana ya masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto lakini pia wamejifunza maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifunga mafunzo hayo.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisisitiza jambo ukumbini.
Afisa Mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto kutoka shirika la ICS mkoa wa Shinyanga,ambao ndiyo wafadhili wa mafunzo hayo,Shadia Nurdin akiwashukuru wajumbe kuhudhuria mafunzo hayo na kuwaomba kwenda kufanyia kazi mambo waliyojifunza kwa muda wa siku tatu ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga Glory Mbia akiwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuendelea kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Picha ya pamoja wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga.
Picha ya pamoja wajumbe wa kamati ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

KATIBU MKUU MPYA JUMUIYA YA WAZAZI AKABIDHIWA RASMI OFISI, LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima (kushoto) akipokea vitendekazi kutoka kwa Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed katika makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika leo jijini Dae es Salama
  Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi, Erasto Sima (kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed wakati akizungumza katika makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika leo jijini Dae es Salama
  Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima (kushoto) akipokea vitendekazi kutoka kwa Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed katika makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika leo jijini Dae es Salama
  Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima akizungumza na waandishi wa habari baada ya makabidhiano ya ofisi
 Katibu Mkuu Mstaafu, wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Seif Shaaban Mohamed akimkaribisha kuzungumza na  Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Erasto Sima na baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo, mwishoni mwa  makabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika leo jijini Dae es Salama. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

MKUU WA MAGEREZA NCHINI SHELISHELI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA JIJINI DAR

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa akisalimiana na Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange ofisini kwake alipowasili Makao Makuu ya Magereza leo Juni 1, 2018 katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili.
 Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongoza mazungumzo Ofisini kwake  na Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange(hayupo pichani), leo Juni 1, 2018 alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza.
 Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange akitambulisha ujumbe wake alioongozananao(hawapo piachani) kabla ya utilianaji saini makubaliano ya ushirikiano na Jeshi la Magereza.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akisaini Mkataba  wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Magereza nchini SheliSheli na Jeshi la Magereza Tanzania Bara. Kushoto ni Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli hiyo Raymond St Ange akisaini mkataba huo.  Hafla fupi ya  utilianaji saini Mkataba huo umefanyika leo Juni, 2018 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) na Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange wakionesha nyaraka za Mkataba wa makubaliano mara baada ya utiliananji wa mkataba huo ambapo Jeshi la Magereza linatarajia kupeleka baadhi ya Maofisa wa Jeshi hilo kwenda nchini SheliSheli kusaidia kuwajengea uwezo wa Uendeshaji wa Magereza nchini humo.
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiliananji saini wa mkataba huo (Kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(katikati) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila Kushoto ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Charles Novart.
  Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange(kushoto) akiwa pamoja na ujumbe wake  kabla ya kusainiana Mkataba wa makubaliano hayo,(kulia) ni Balozi wa Heshima wa SheliSheli nchini Tanzania, Maryvonne Pool akifuatilia mazungumzo hayo kama inavyoonekana katika picha.
 Mkuu wa Magereza nchini Shelisheli Raymond St Ange pamoja na ujumbe wake na Maofisa wa Jeshi la Magereza wakitembezwa ndani ya Kiwanda cha USeremala  Gereza Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.
 Kamishna Jenerali wa Maagereza, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Magereza nchini SheliSheli, Raymond St Ange(wa tatu kushoto) walioketi, (wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga, (wa pili toka kushoto) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila,(wa tatu toka kulia) ni Balozi wa Heshima wa SheliSheli nchini Tanzania, Maryvonne Pool. Wengine waliosimama mstari wa nyuma ni Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Maofisa kutoka nchini SheliSheli(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA NGAZI ZA JUU LA MABADILIKO YA TABIA NCHI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema kuwa ongezeko la watu katika miji mikubwa kuna changia sana katika uharibifu wa mazingira na matumizi makubwa ya mkaa.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa.
Makamu wa Rais amesema “Mkaa ni Ghali Tutumie Nishati Mbadala”, kwani kiwango cha miti inayokatwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa ni kikubwa na kinatisha.
“ Dar es Salaam peke yake inakadiriwa kutumia kati ya magunia kati ya 200,000 mpaka 300,000 yenye uzito wa kilo 50 kila moja ya mkaa kwa mwezi na inategemewa itaongezeka zaidi kutokana na kasi ya ongezeko la watu hasa kwenye miji ” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amewata Watanzania, Makampuni pamoja na Taasisi mbalimbali kuungana na Serikali kubadilisha jamii yetu kuanza kutumia nishati ya majani kwa namna ya mkaa na kuni kama vyanzo mbadala vya nishati endelevu.
Makamu wa Rais amesema kuwa kilele cha Siku ya Mazingira ni tarehe 5 Juni, 2018 ambapo dhima ya Kimataifa ni Kupiga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini Tanzania imelekeza nguvu zake katika kuadhimisha siku hiyo kwa kuwataka Wananchi wake wabadilike badala ya kutumia mkaa ambao unasababisha ukataji mkubwa wa miti ni vyema kuanza kutumia nishati mbadala.
Mapema; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba alisema kutokana na uhitaji na umuhimu wa kutunza mazingira Serikali, Wadau wa Maendeleo, Taasisi mbali mbali, Sekta Binafsi na Watungaji wa Sera kutafakari kwa pamoja na kuja na majawabu yatakayosaidia katika utunzaji wa mazingira na kuilinda miti.
Wakati huo huo;  Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Katarina Rangnitt amesema tangu mwaka 1972 changamoto za uharibifu wa mazingira hazikuwa za Kikanda tu bali ni kwa dunia nzima hivyo hili jambo linahitaji ushiriki wa Dunia nzima katika kupambana na uharibifu wa mazingira.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshukuru Profesa Mark Mwandosya kwa zawadi ya kitabu mara baada ya ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
 Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  akihutubia wakati wa ufunguzi wa  Kongamano la Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mazingira na Uchumi wa Taifa  lililoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na kufanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU MGENI RASMI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA KUHIFADHI QURAN YATAKAYOFANYIKA JUNI 3 ,2018 JIJINI DAR

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Fainali ya Mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi Quran yanayotarajiwa kufanyika Juni 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo mataifa zaidi ya 20 yameshiriki.

Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania.Mbali ya kuwepo kwa Waziri Mkuu Majaliwa viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo wastaafu nao watakuwa miongoni mwa watakaohudhuria kushuhudia mashindano hayo yenye hadhi ya kimataifa.

Viongozi wastaafu watakaohudhuria siku hiyo ni Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne mzee Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais mstaafu Dk.Mohammed Ghalib Bilal pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa Mashindano hayo kutoka Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Nasoro amesema tayari washiriki karibu wote wamewasili chini Tanzania ambapo waliopo sasa ni washiriki kutoka mataifa 18 kati ya mataifa 20 ambayo yamealikwa.

Mratibu wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qur an Tanzania, Shekh Mohammed Nassor (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mashindano ya kuhifadhi Qur an Kimataifa yanayotarajia kufayika kesho katika ukumbi wa Diamond Jubilee June 3, 2018. Kulia ni Katibu wa Jumuiya hiyo, Shekh. Mohamed Ali Hassan na Jaji wa mashindano hayo, Dk. Abbas Hamza Mohammad.

Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Ali Hassan(kulia) akielezea kwa kina kuhusu mashindano hao yanayotarajia kufanyika Juni 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa majaji kutoka nchini Somalia (wa pili kushoto) akizungumzia namna ambavyo wamejiandaa kuchuja washiriki kwenye mashindano hayo.Wa kwanza kulia ni Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Tanzania Sheikh Mohamed Ali Hassan na anayefuatia ni Mratibu wa mashindano hayo Sheikh Mohamed Nasoro.

 

Rais Magufuli amteua Prof. Andrew Pembe kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS

Benki ya CRDB yawazawadia washindi wa kampeni ya “Shuhudia Kombe la Dunia FIFA 2018 na TemboCard Visa”

$
0
0
 Benki ya CRDB imetoa zawadi za kwanza kwa washindi wa kampeni yake ya TemboCardVisa ijulikanayo kama “Shuhudia Kombe la Dunia FIFA 2018 na TemboCardVisa” katika hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Ramada Encore iliyopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo jumla ya washindi 15 wamekabidhiwa zawadi zao ikiwamo zawadi ya tiketi kwenda kushuhudia mechi za Kombe la Dunia nchini Urusi kwa washindi wa 3 wa kwanza kwa wiki tatu za mwanzo za kampeni. Wakati washindi wengine 12 walioshika nafasi ya pili hadi tano wamekabidhiwa zawadi za seti ya luninga na king’amuzi cha Dstv kilicholipiwa kwa miezi miwili ya Kombe la Dunia. 

Akizungumza katika hafla hiyo ya utoaji zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dokta Charles Kimei alisema kampeni hiyo ina lengo la kuwahamasisha wateja wa Benki ya CRDB kufanya malipo na manunuzi kwa kutumia kadi zao za TemboCardVisa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa baadhi ya washindi wa kampeni ya TemboCardVisa ijulikanayo kama “Shuhudia Kombe la Dunia FIFA 2018 na TemboCardVisa” iliyofanyika katika hoteli ya Ramada Encore, jijini Dar es salaam.

“Lengo letu ni kuwajengea wateja wetu utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya malipo na manunuzi mitandaoni ‘online shopping’ na kupitia vifaa vya manunuzi vilivyopo sehemu mbalimbali kama supermarkets, maduka ya rejareja, mahotelini, mahospitalini na taasisi nyingine mbalimbali binafsi na za serikali,” alisema Dokta Kimei. Kampeni ya “Shuhudia Kombe la Dunia FIFA 2018 na TemboCardVisa” ilizinduliwa rasmi mapema mwezi wa nne kwa Benki ya CRDB kushirikiana na Visa International ambao pia ni moja ya wadhamini wa Kombe la Dunia mwaka huu.

 Dokta Kimei pia aliwapongeza washindi wote walioibuka kidedea katika shindano hilo huku akiwasihi wateja wengine wa Benki hiyo kuendelea kushiriki katika Shindano hilo linalotarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa mwezi wa saba. “Mshindi ni mteja ambaye atafanikiwa kufanya miamala mingi zaidi ya manunuzi kupitia kadi yake ya TemboCardVisa,” alisema Dkt. Kimei.
Akizungumza katika hafla hiyo Meneja Mkuu wa Visa Afrika Mashariki Ndugu Sunny Walia aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha wateja kutumia kadi zao kufanya malipo huku akiwataka wateja kuendelea na utamaduni huo kwani sasa dunia inaondokana na matumizi ya pesa taslimu hivyo ni vizuri kujiweka tayari.

“Niwapongeze pia washindi wetu, na niwaombe waendelee kutumia kadi zao za TemboCardVisa na wakawe mabalozi pia kwa ndugu jamaa na rafiki zao ili siku nyingine nao tuwaone wakishinda,” alisema Ndugu Sunny Walia Kwa upande wake Mkuu wa Uendeshaji Multichoice Tanzania ambao pia ni washirika wa kampeni hiyo Ndugu Ronald Shelukindo, alisema imekuwa ni fahari kwao kushirikiana na Benki ya CRDB katika kampeni hiyo ya “Shuhudia Kombe la Dunia FIFA 2018 na TemboCardVisa” huku akisema Multichoice itahakikisha washindi hao wanapata fursa ya kushuhudia Kombe la Dunia mubashara kupitia ving’amuzi vyao ambavyo vitakuwa na ofa maalum katika msimu wa Kombe la Dunia.

 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifafanua jambo, katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa baadhi ya washindi wa kampeni ya TemboCardVisa ijulikanayo kama “Shuhudia Kombe la Dunia FIFA 2018 na TemboCardVisa” iliyofanyika katika hoteli ya Ramada Encore, jijini Dar es salaam.

“Niwakumbushe pia huduma ya malipo ya Dstv inapatikana katika SimBanking, hivyo basi hamna sababu ya kuhangaika kulipia ving’amuzi vyenu vinapokaribia kuisha,” alisema Ndugu Shelukindo.

Kampeni ya “TemboCardVisa” pia imekuwa ikiendeshwa kupitia mitandao ya kijamii ya Instagram, Facebook na Twitter kwa hashtag maalum ya #TwenzetuRussia2018, ambapo watu wamekuwa wakishiriki na kushinda zawadi mbalimbali ikiwamo fedha taslimu.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

RC DKT. KEBWE ATAKA WALIOKULA FEDHA YA UJENZI WA MAABARA YA SEKONDARI YA IDIBO WAKAMATWE, AUSIFIA UONGOZI WA WILAYA GAIRO

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amemuagiza mkuu wa Kituo Cha Polisi Gairo kuwakamata wale wote waliokula fedha za ujenzi wa maabara ya shule sekondari ya Idibo iliyiyopo katika Kata ya Idibo wilayani Gairo. 

 Akizungumza katika mkutano wa hadhara hizi karibuni Dkt. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amesema kuwa hawezi kuvumilia kuona shilingi Milioni 12 fedha za ujenzi wa maabara zilizotokana na nguvu ya wananchi zinaliwa na watu wachache tena bila kufanikisha malengo.

 "Hivi kuna watu bado hawaelewi umuhimu wa kutunza fedha za umma??? Haiwezekani wananchi wajichange harafu nyie viongozi wa kijiji mle hela zao za maendeleo bila aibu, siwezi kuvumilia... Nakuagiza OCD Gairo na TAKUKURU kufanya msako watu hawa wapelekwe mbele ya sheria haijalishi walishastaafu au la!," amesema. Amesema kuwa ni vyema kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waendelee kuchangia maendeleo ya kijiji chao ila wanapotokea viongozi ambao si waaminifu ni vyema kuwaondoa haraka.

 "Haiwezekani tokea mwaka 2014 maabara haijakamilika imeishia kujengwa msingi na kupandisha matofali kidogo huku fedha na nguvu za kujitolea wanachi ziwe zimepotea bure, naagiza viongozi waliokuwepo kipindi hicho wajisalimishe wenyewe huu ujinga hauwezi kuvumilika," amesema.

 Aidha mbali na madudu hayo aliyoyakuta Dkt. Kebwe alitoa pongezi zake za pekee kwa uongozi wa wilaya ya Gairo ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe kwa kuweza kusimamia vyema maendeleo ya wilaya na kuona inavyokuwa kwa haraka. 

 Amesema wilaya ya Gairo ilianzishwa mwaka 2013 lakini imeonyesha kuwa na miradi mingi ya maendeleo ambayo iko hai jambo linalompa faraja sana kwa kuona viongozi wanachapa kazi. "Wanawake wanaweza kweli, wilaya yenu inaongozwa na akina mama na wanachapa kazi vizuri sana, kwa hili lazima niliseme bila hata kificho... mpe mtu sifa zake akiwa hai maana hawa ndiyo wasaidizi wangu najua wanapitia changamoto nyingi ila wanazipangua na kusonga mbele,' amesema. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (Katikati) akiwahutubia wakati kijiji cha Chakwale mara baada ya kufanya usafi katika Soko la Chakwale katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akipokea zawadi ya mahindi mara baada ya kuwahutubia (katikati) wananchi wa kijiji cha Chakwale mara baada ya kufanya usafi katika Soko la Chakwale katika ziara yake aliyoifanya hivi karibuni kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Mchembe (mwenye kilemba), Diwani Kata ya Idibo Mhe. Rajabu Mguhi pamoja na pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya kijiji wakiwa katika ziara kwa ajili ya kuhamasisha miradi ya maendeleo wiyani humo.

HIMID MAO MKAMI AAGA RASMI AZAM FC

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Aliyekuwa Nahodha wa Azam FC, Himid Mao Mkami ameiaga rasmi timu hiyo, baada yakupata nafasi kwenda kucheza Soka la kulipwa nchini Misri kwenye Klabu ya Petrojet inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo inayofundishwa na Aliyekuwa Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Hassan Shehata.

Himid maarufu kwa jina la Ninja aliyekuwa na Azam FC tangu mwaka 2009, katika ukurasa wake wa Instagram ametumia nafasi hiyo kuaga Benchi la Ufundi, Makocha, Viongozi na Wafanyakazi wote wa timu hiyo iliyomaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL).
‘Nashukuru kufanya kazi pamoja kila siku kwa ushirikiano na timu ya Azam katika kupanda na kushuka, huzuni na furaha na bado mlikua bega kwa bega na mimi miaka yote, ni huzuni kusema kwa heri lakini haikuwa na jinsi’, ameandika Himid Mao.

Himid amesema alifanya maamuzi kwa kushirikiana na uongozi wa timu hiyo na kumruhusu alipoomba ruhusa yakutafuta changamoto mpya.

KAMPUNI YA MAGARI YA KOREA YA TATA DAEWOO YAZINDUA TRUCK YA KISASA

$
0
0
Kampuni ya magari ya Korea ya TATA Daewoo yazindua Truck ya kisasa inayohimili barabara zisizo na lami vijijini. Wafanyabiashara wa usafirishaji sasa kutumia gharama ndogo kuendesha biashara hiyo.
Mkuu wa usambazaji wa magari ya Daewoo Truck kwa bara la Afrika, leo Brand akizungumzia jinsi wafanyabiashara wanavyoweza kutumia magari hayo kusafirisha bidhaa za vyakula kutoka mashambani ambako barabara zake hazina lami na kumrahishia kufika sokoni kwa wakati kwa kuwa magari hayo yanahimili changamoto za barabara zisizo na lami.
Kampuni ya magari ya Korea ya TATA Daewoo yazindua Truck ya kisasa inayohimili barabara zisizo na lami vijijini. Wafanyabiashara wa usafirishaji sasa kutumia gharama ndogo kuendesha biashara hiyo.
Mtunishi misuli akionehsa umahiri wake katika fani hiyo wakati wa uzinduzi wa gari ngumu ya kubebea mizigo ya Truck Daewoo jijini Dar es Salaam.
Daewoo Truck iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images