Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Dkt. Abaasi Awataka Wanahabari Kutumia Kalamu Zao Kupunguza Ajali

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amewataka waandishiwa habari nchini kutumia taaluma ya habari kuielemisha jamii juu ya usalama barabarini ili kupunguza ajali ambazo zimeendelea kusababisha vifo visivyo vya lazima na ulemavu wa maisha.

Dkt. Abbasi ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo maalumu ya miezi sita juu ya uandishi bora wa habari zinazohusu usalama barabarani, kwa waandishi wa habari 17 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Ameeleza kuwa ajali za barabarani zitapungua kwa kiwango kikubwa endapo waandishi wa habari watatumia taaluma yao kuielemisha jamii juu ya usalama barababrani, kupaza sauti za wananchi pale palipo na changamoto zinazohitaji usimamizi wa Serikali na pia kuwa sehemu ya mageuzi yanayofanywa na Serikali kuwaondolea wananchi changamoto za ajali.

“Zaidi ya watu milioni moja na laki mbili hufariki kila mwaka duniani kutokana na ajali za barabarani na kati ya vifo hivyo asilimia 90 hutokea katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Wengi wanaofariki kwa ajali ni watu wenye umri wa kati ya miaka 15-29 na hivyo kuwa na atahari kubwa kiuchumi na kijamii,” alieleza Dkt. Abbasi.

Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia kwa umakini mafunzo watakayopata ili watumie maarifa watakayoyapata kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na wadau wa usalama barabarani. Nae Mkurugenzi wa Uhakiki na Ubora kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mohamed Mohamed, amesema kuwa Wizara pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) wameona ni muhimu waandishi wa habari kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya masuala ya usalama barabarani kwa kuwa wao wana nafasi kubwa ya kufikisha elimu hiyo kwa jamii kubwa zaidi.

Dkt. Mohamed ameeleza kuwa watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha katika ajali kutokana na sababu nyingi ikiwemo majeruhi kukosa huduma za haraka pindi ajali inapotokea kutokana na hospitali kuwa mbali. Amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya majeruhi kukosa huduma za haraka wakati wa ajali, Wizara ipo katika hatua za mwisho kuweka vituo vya kutolea huduma za dharua (Emergency Medicine Services Centre) katika barabarani kuu ziendazo mikoani ambapo vitarahisisha kuwapatia huduma za haraka majeruhi wa ajali.

Waandishi wanaoshiriki mafunzo haya ni pamoja na Abadallah Msuya kutoka Daily News, Evance Ng’ingo na Adam Ruta kutoka Habarileo, Agness Mbapu kutoka TBC, Beaty Tesha kutoka TBC Taifa, Aisia Rweyemamu na Chrispin Gerald kutoka The Guardian, Dickson Kanyika kutoka Star Tv na Radio Free Africa, Herrieth Makweta kutoka Mwananchi na Jasmin Shamweku kutoka Redio ABM ya Dodoma.

Waandishi wengine ni Juhudi Felix kutoka FADECO Wilayani Karagwe, Margaret Malisa kutoka Nipashe, Renatus Mutabuzi kutoka ITV, Sylvanus Kayela kutoma Mlimani TV, Veronica Mrema kutoka Mtanzania na Vumilia Kondo kutoka Abood Media ya Morogoro. Mafunzo haya usalama barabarani kwa waandishi wa habari ni ya tangu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016 kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, na Shirika la Afya Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo maalum kuhusu uandishi wa habari za usalama barabarani jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali akimkabidhi vitendea kazi mwandishi wa Gazeti la Habarileo, Evance Ng’ingo ambaye anashiriki mafunzo maalum ya miezi sita kuhusu usalama barabarani.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 15 TANGU KUANZISHWA KWA MFUKO WA DHARURA WA RAIS WA MAREKANI WA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI (PEPFAR)

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018.Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia) na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson kabla ya Kuzindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuzindua Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR), Mei 30, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana baadhi ya viongozi walioshiriki katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 15 Tangu Kuanzishwa kwa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (PEPFAR) Kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 30, 2018. Kutoka kulia ni Dkt. Janet Mwambona wa Taasisi HIV/AIDS Treatment Advisor,Walter Reed Army Institute Of Research, Brian Rettmann ambaye ni Mratibu wa PEPFAR nchini, Dkt. Leonard Maboko, Mkurugenzi Mtendaji wa Tume yaTaifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania na wanne kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WANAFUNZI ZAIDI YA 600 WA DARASA LA TATU WASOMA KWENYE CHUMBA KIMOJA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma, 

WANAFUNZI zaidi ya 600 wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kumkambati Kata ya Nyamidaho wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wanalazimika kusoma katika chumba kimoja kutokana na uhaba wa madarasa na wingi wa wanafunzi.

Hali hiyo imewalazimu wazazi kuanzisha ujenzi wa shule nyingine Katika vijiji jirani vya Kumtundu na Mkuyuni.Hayo yalibainika jana wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marco Gaguti wakati akitembelea miradi ya Wilaya hiyo ilioanzishwa na wananchi na inayofadhiliwa na Serikali.
Ambapo alifika katika Shule ya Msingi Kumtundu iliyoanza kujengwa kwa juhudi za wananchi wa kijiji hicho ili kupunguza wingi wa wanafunzi katika shule iliyopo katika Kijiji jirani cha Mvungwe.

Akitoa taarifa ya shule hiyo Mkuu wa Shule ya Msingi Kumkumbati Falesi Lugati amesema hhule hiyo inajumla ya wanafunzi 2024 na jumla ya walimu 14 na darasa la tatu ndilo lina wanafunzi 600, ambapo wanalazimika kuwagawa awamu mbili ya asubuhi na mchana kwa lengo a kuwaweze kuwafundisha na kumpunguzia mzigo mwalimu anaefundisha darasa hilo .

Amesema shule hiyo inahudumia wanafunzi wa vijiji viwili na wameanza kutatua tatizo la mrundikano wa wanafunzi kwa kujenga vyumba viwili vya madarasa, na wananchi wa Kijiji cha Mkumtundu wameanza ujenzi wa shule mpya itakayo saidia kupunguza wanafunzi waliopo katika shule hiyo kuhamia katika shule jirani inayojengwa.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Shule hiyo Katibu wa kamati ya ujenzi wa Shule ya Msingi Kumtundu Raphael Zacharia amesema wameanza ujenzi wa madarasa manne na ofisi moja na ujenzi wa msingi na ukuta pamoja na upauaji umekalika na jumla ya ghalama ni Sh. milioni 14 na Sh.milioni 11 zimechangwa na wananchi na Waziri wa Elimu alichangia Sh. milioni tatu. 

Amesema changamoto ni upungufu wa vifaa vya ujenzi uhaba wa kifungu cha fedha kuwalipa mafundi na kuomba Serikali kuunga mkono kuchangia vifaa vya ujenzi ili kukamilisha ujenzi pamoja na upatikanaji huduma za maji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Brigedia Jenerali Marco Gaguti aliwapongeza wananchi kwa hatua hiyo waliyoichukua ya kuona upungufu wa vyumba vya madarasa na kuona wanafunzi wanavyoteseka na kuamua kutafuta shule nyingine ili kutatua tatizo la wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya shule.

Amesema ataendelea kuhimiza fedha inayotakiwa kutolewa kwa ajili ya kumalizia shule hiyo ianze, na kuahidi kuchangia Sh.milioni mbili kutoka katika Mfuko wa Mkuu wa Wilaya ili kuiongezea kwenye vifaa ambavyo bado havija nunuluwa.

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Godfrey Kasekenya amesema wamejipanga shule hiyo inakamilika Januari mwaka 2019 wanafunzi wanaanza kusoma na wao kama halmashauri wamejiandaa kukamilisha matundu 10 ya vyoo kupitia mfuko wa EPFORR kiasi cha Sh. milioni nane zimetengwa kwaajili ya shughuli hiyo.

Brigedia Jenerali Gaguti alitembelea vituo viwili vya Afya vya Nyamidaho na Nyakitonto Vituo vya Afya vinavyo jengwa kwa fedha za Serikali Kuu kwa kutuma uraratibu wa Force Account ambapo aliwapongeza viongozi wa vijiji na wananchi kwa kujitolea kukamilisha ujenzi huo kwa gharama nafuu na kazi inaendelea vizuri na kuwataka Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli za maendeleo.

WATUMISHI WATATU WA HALMASHAURI YA KALIUA MATATANI KWA KUSHINDWA KUONYESHA ZILIPO MILIONI TATU ZA UJENZI WA MADARASA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT, TABORA

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameagiza kuchukuliwa hatua kwa watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa tuhuma za kukiuka taratibu za manunuzi wakati wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya  Msingi Susitila na hivyo kusababisha upotevu wa milioni tatu za nguvu za wananchi. Hatua hiyo ilitokana na taarifa ya Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri hiyo  kubaini ukiukwaji wa taratibu mbalimbali zilisababisha shilingi milioni tatu kutokuwa na maelezo juu ya matumizi yake.

Alisema jengo hilo ambalo bado halijakamilika linaoonyesha kutumia milioni 6  ambazo hazilinganisha na hali halisi lilipofikia jengo wakati katika shule za jirani ya Imalampaka imetumia milioni mbili kujenga vyumba viwili vya madarasa hadi kufikia hatua ya kuezekwa. Mkuu huyo wa Mkoa alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua kuhakikisha anawachukulia hatua ikiwemo kurudisha shilingi milioni tatu ambazo hazionekana matumizi yake, kushushwa vyeo na kuondolewa katika nafasi zao kwa wale ambao watabainika kutenda kosa.

Alisema hatua isipochukuliwa inawakatisha tamaa wananchi ambao wanajitolea nguvu zao katika kuchangia miradi ya maendeleo huku fedha zikiishia mifukoni mwa wachache. Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Dkt. John Pima akitoa taarifa ya ukaguzi maalumu alisema Mkaguzi amebaini ukiukaji wa Sheria, taratibu, kanuni na utoaji wa taarifa za uongo kwa viongozi na umma.

Alisema Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Mtakuja  Josephine Benjamin alishindwa kutimiza wajibu na hivyo kutozingatia sheria, taratibu na kanuni wakati wa ukusanyaji na matumizi ya fedha zilizotokana na michango ya wananchi.

Dkt. Pima alisema kwa upande naye Kaimu Mkuu wa Shule ya Susitila Juma Kitwama alitoa taarifa za uongo kwa Mkuu wa Mkoa na umma kwa kutoa taarifa ambayo hakuwa na uhakika nayo  juu matumizi ya milioni sita zilizotokana na michango ya wananchi.

Dkt. Pima aliongeza mtuhumiwa huyo pia alishindwa kutoa viambatanisho vinavyothibitisha  matumizi ya fedha hizo  na kusema kuwa hana viambatisho vya matumizi ya fedha hizo  kwa kuwa alipewa taarifa hiyo kutoka kwa aliyekuwa Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Susutila Mussa Elias.

Mapema wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa wa Tabora akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Wilaya mbalimbali alisimamisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa baada ya kutoridhishwa na taarifa ya matumizi ya fedha katika mradi huo na kuagiza Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri kupitia na kisha kutoa taarifa kwake.

Alichukua uamuzi huo ikiwa ni sehemu ya kutaka kuzuia ubadhirifu ambao ungeweza kutokana na fedha nyingine milioni 24 walizopatiwa na Serikali kupitia Equip T ili kukamilisha mradi huo.

MBUNGE RITTA KABATI ATOA SADAKA YA TENDE KWA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM MANISPAA YA IRINGA

$
0
0
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa sadaka ya tende kwa waumini wa dini ya kiislamu wa manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuadhimisha mfungo wa ramadhan kwa waislamu wa wote wa manispaa ya Iringa

Akizungumza wakati wa kukabidhi sadaka hiyo katika msikiti wa Dhinureyn Gangilonga Kabati alisema kuwa kila mwaka amekuwa akifutulisha katika maeneo mbalimbali hivyo mwaka huu ameamua kununua tende na kugawa kwenye misikiti yote ya manispaa ya Iringa.

“Unajua mwaka huu tende ni tunda ambalo linahitajika katika kipindi hiki cha mfungo na kuna watu ambao hawana uwezo wa kununua tende hizi na ukiangalia mwaka huu tende zimepanda bei sana hivyo kwa kiasa ambacho nakipata nimeamua kutoa sadaka hii kwa waumini wa kiislam” alisema Kabati

Kabati aliwataka wananchi wengine kuendelea kumuabudu mwenyezi mungu pale ambapo tunapata nafasi ili kupunguza maovu ambayo tumekuwa tukiyatenda kwa kukusudia au bila kukusudia na kufanya hivyo basi mwenyezi mungu atatuongezea pale ambapo tumepunguza kwa ajili ya kumtumiaka mungu.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM)  Ritta Kabati akiongea na viongozi wa misikiti yote ya manispaa ya Iringa wakati wa utoaji sadaka ya tende kwa waumini wa dini ya kiislamu wa manispaa ya Iringa kwa ajili ya kuadhimisha mfungo wa ramadhan kwa waislamu wa wote wa manispaa ya Iringa. 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amemshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka ya tunda la tende kwa waiislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akikabidhi tende alizokabidhiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa kutoa sadaka kwa waiislamu katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhan.
Mkuu wa walimu na msimamizi wa misikiti ya Dhinureyn Tanzania Abdul Salam Ahmad Ayub akimshukuru mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati kwa sadaka aliyoitoa kwa waislam katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan.
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na viongozi wa misiki ya  manispaa ya Iringa walipohudhulia zoezi la utoaji wa sadaka ya tende ilitolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati.

MAKAMU WA RAIS AFUTARISHA TUNGUU ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kufutari kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Tunguu Zanzibar jana jioni tarehe 29 Mei 2018.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi Mdogo wa Ujerumani nchini  Mhe. Jens Dominic Warth mara baada ya kufutari kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Tunguu Zanzibar jana jioni tarehe 29 Mei 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi Mdogo wa India nchini Mhe. T.C. Barubai mara baada ya kufutari kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Tunguu Zanzibar jana jioni tarehe 29 Mei 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi wa Dini kutoka madhehebu mbali mbali  waliojumuika nae kwenye futari , Tunguu Zanzibar jana jioni tarehe 29 Mei 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Sister Maria Gaspara wa Kanisa Katoliki Zanzibar mara baada ya kufutari kwenye Makazi ya Makamu wa Rais, Tunguu Zanzibar jana jioni tarehe 29 Mei 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Katibu Tawala Morogoro awataka Maafisa Kilimo kuongeza Uzalishaji

$
0
0
Na Andrew Chimesela – Morogoro

Maafisa Kilimo wa Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Morogoro wametakiwa kusimamia na kutoa utalaama wao kwa wakulima kupitia maafisa Ugani ili kuongeza uzalishaji wa mazao Mkoani humo.
Agizo hilo limetolewa Mei 29 mwaka huu na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari alipofanya Kikao na Maafisa wa Kilimo huo kilicholenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kilimo za kila Halmashauri na kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji kwa mwaka 2018/2019.
Akifungua Kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Tandaria amesema, kila Afisa kilimo ahakikishe anasimamia Maafisa Ugani wake kwenda kwa wakulima kuwafundisha kilimo cha kisasa kwa kuwa wengi wao bado wanalima kilimo cha mazoea jambo linalowakosesha tija katika kilimo.
“sio wakulima waendelee na utaratibu ule ule wa zamani, tuhakikishe wakulima tunaweleza mbegu mpya zilizojitokeza na kuwasimamia kufanya palizi kwa wakati alisema ” alisema Tandari
Tandari amesema endapo watajipanga vizuri katika kuwasimamia Maafisa Ugani kuwafundisha wakulima kilimo cha kisasa na kuondoa kabisa upotevu wa mazao yanayopotea wakati wa kuvuna, upo uhakika wa kuongeza uzalisha wa mazao mara mbili ya matarajio ya mavuno ya mwaka huu ya kupata tani 2,800,000 katika Mkoa.
Aidha, amewataka Maafisa hao kuongeza uzalishaji wa kilimo cha mboga mboga ili kutumia vema fursa iliyojitokeza sasa ya kuwa katikati ya Jiji la Dar es Salaa na Makao Makuu ya Serikali Jiji la Dodoma  ili kuongeza mapato kupitia kilimo hicho hususan Halmashauri za Morogoro, Mvomero na Gairo ambazo ziko kando ya Barabara kuu ya Dar es Salaam – Dodoma.

“Kwa hiyo tunayo fursa, Dodoma sasa hivi mboga mboga zimeisha pale sokoni, inabidi waje watafute huku Morogoro ndio fursa zenyewe hizo, kuna uhaba wa mboga mboga kule Dodoma, sasa sisi tuitumie hii fursa ili tuongeze uzallishaji” alisema Tandari.

Katika hatua nyingine Clifford Tandari amewataka Maafisa hao wa kilimo kutilia mkazo Mkakati ya Pamba, Kahawa na Korosho yanayostawi Mkoani Morogoro ili kuongeza uzalishaji mapato ya Halmashauri kwa kuwa wawekezaji watavutiwa na uwepo wa mazao hayo ambayo ndiyo mali ghafi ya viwanda.
Kuhusu Maafisa Ugani ambao walipata mafunzo muda mrefu wa nyuma na hivyo kukosa Utalaamu ambao unakwenda na wakati (mafunzo rejea) Bw. Tandari amesema yuko katika mazungumzo na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine - SUA ili Maafisa hao waende kupata mafunzo yanayokwenda na wakati ili kuongeza tija kwa wakulima wa maeneo yao.
Mmoja wa Maafisa Kilimo katika kikao hicho Bw. Mohamed Ramadhani ambaye ni Afisa kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero  amesema Halmashauri yao imejipanga kupunguza upotevu wa mavuno wa kati ya asilimia 5 – 40 yanayopotea, kwa kuwa wametambua chanzo cha upotevu huo.
Bw. Mohamed ametaja baadhi ya sababu za upotevu  wa mazao hayo kuwa ni pamoja na wakulima kutopanda mbegu sahihi za mpunga, kutovuna kwa wakati, kuchelewa kutoa mazao shambani baada ya mavuno na kutotumia njia sahihi za kuvuna zao la mpunga. 
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rozaria Rwegasira, amezungumzia changamoto ya viwavi jeshi vamizi waliojitokeza katika msimu huu na kuwahakikishia wakulima kuwa wamejipanga vizuri kukabiliana na tatizo hilo kwa kuwa tayari mafunzo kuhusu kuwazuia wadudu hao yametolewa kupitia ufadhiri wa Benki ya Dunia na sasa yanaendelea kutolewa kwa Maafisa ugani wa ngazi za chini.

Ilala watakiwa kuanzisha klabu za mazingira

$
0
0
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imeshauriwa kuanzisha klabu za mazingira katika shule zake za msingi za manispaa hiyo ili wanafunzi wafundishwe umuhimu wa utunzaji mazingira. 

Ushauri huo umetolewa Dar es Salaam jana na Ofisa Tawala wa Wilaya ya Ilala Jabiri Makame wakati wa kampeni ya  upandaji miti shule msingi Yongwe iliyopo Chanika Ilala.

"Naomba Idara ya Mazingira manispaa ya Ilala muunde vilabu vya mazingira katika shule zenu za msingi ili wanafunzi wafundishwe umuhimu wa utunzaji wa mazingira"amesema Makame. Makame amesema suala la utunzaji wa mazingira ni letu sote hivyo inatakiwa tuweke mikakati mbalimbali jinsi ya uendelezaji na utunzaji wa mazingara. 

Afafanua ikiwekwa mikakati endelevu ya kuanzisha vilabu mashuleni wanafunzi wakafahamu jinsi  utunzaji mazingira serikali itakuwa imefaidika jamii nzima itapata elimu hiyo. Amewapongeza Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa juhudi zao kwa kuwekeza shule za msingi hasa upande wa mazingira na kuwataka wadau wengine Kushirikia na serikali. 

 Amesema utunzaji wa mazingira unafaida nyingi nchi yetu ikiwemo ya kuepuka jangwa,faida nyingine miti huleta kivuli na miti mingine ya matunda. Kwa upande wake Ofisa Elimu Msingi Ilala Elzabeth Thomas amesema Standard Chartered wameanza kampeni ya kusaidia shule za Msingi Ilala toka mwaka 2014  mpaka sasa wameweza kupanda miti 3300.

Amesema kuanzia mwaka 2014 hadi sasa wamekuwa wakishirikiana katika utunzaji wa mazingira  katika shule mbalimbali. Amesema awali kabla kupanda miti shule ya Yongwe kampeni hiyo ilianzia shule ya msingi Majani ya Chai, Pugu Kajiungeni, Buyuni, Kigogo Freshi, Viwege na Uhuru Mchanganyiko. 

Kwa upande wake Ofisa wa Benki hiyo  Isema Bilali amesema benki hiyo ilianza shughuli zake nchini mwaka 1917  na kwamba upandaji miti una faida nyingi ikiwemo kutuwezesha kupata mvua,ujenzi,inatupa chakula inazuia mmomonyoko wa udongo.  
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yongwe Kata ya Chanika wakiwa katika wiki ya mazingira na upandaji miti shuleni kwao Dar es Salaam jana Picha na Heri Shaaban

WATAALAMU WA MASUALA YA MAABARA WAAGIZWA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA SERIKALI

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Serikali imewaagiza wamiliki wa maabara binafsi kote nchini kuzingatia na kufuata tartibu zilizoweka katika kutoa huduma hili kufikia viwango vinavyohitajika katika sera ya utoaji huduma za afya.

Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Msajili wa Mabara binafsi za Afya, Dikson Majige alipokuwa akifungua mafunzo ya kuelimisha wataalamu wa maabara kuhusu utaratibu na mikakati ya urasimishwaji.

Majige amesema kuwa mafunzo hayo yatumike kutekeleza mikakati mipya na ya kudumu ya huduma za maabara za afya katika nafasi zao za kazi.“mafunzo haya yatumike kutekeleza kazi kwa juhudi ,maarifa na uaminifu mkubwa kufanikisha usimamiaji mzuri wa maabara za afya nchini na kutoa huduma zenye ubora na viwango vya kimataifa” amesema Majige.

Amewataka kila mmoja kufanya tathmini ya huduma anayotoa ili kujijua kuwa kama anawajibika ipasavyo katika utendaji wake wa kazi.Amesema kuwa wamiliki na wasimamizi wa huduma za maabara wajiweke tayari kutoa huduma bora Zaidi ambazo zitakuwa mfano kwa wengine.
Mkufunzi wa Masuala ya Uongozi na Menejimenti katika Maabara, Mayala Lushina akitoa mafunzo kwa wataalamu wa Maabara za afya juu ya utaratibu na mikakati ya Urasimishwaji katika Chuo cha Maabara Muhimbili
Mwenyekiti wa Institute ofa Laboratory (EA) Limited , Sabas Mrina akizungumza na Wataalamu wa Maabara za afya umuhimu wa wao kurasimishwa mamlaka za serikali
Mkufunzi wa utambuzi wa bidhaa na vifaa bora vya Maabara Colman Msuya , akiwaeleza wataalamu hao wa Maabara za Afya umuhimu wa kukagua vifaa vyao kabla ya kuanza kutumia ili kuepuka kupata majibu yasiyo sahihi kwa kutumia vifaa visivyo na ubora.
Wataalamu wa Maabara wakifuatilia somo Kuhusu utaratibu na mikakati ya urasimishwaji wa maabara za afya katika Shule ya Maabara Muhimbili-- 

MAOFISA ELIMU WAPIGWA MARUFUKU KUINGIZA MAMLUKI MASHINDANO YA UMISSETA DAR

$
0
0
Na Heri Shaaban .

MAOFISA Elimu Sekondari wa Manispaa tano katika Mkoa wa Dar es Salaam ambao wanafunzi wao wanashiriki Mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari (UMISSETA) wameshauriwa katika mashindano hayo wasiweke wachezaji mamruki. 

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana katika ufunguzi wa mashindano hayo  ya Mkoa Dar es  Salaam na Ofisa Elimu wa Mkoa huo Khamis Lissu. Lissu alisema katika mkoa wake wachezaji 750 wameshiriki mashindano hayo ya mkoa ambapo inatafutwa timu moja itakayoshiriki mashindano ya ngazi ya UMISSETA Taifa. 

"Kila mwaka mkoa wangu wa Dar es Salaam unafanya vizuri  mwaka jana tumechukua kombe ngazi ya Taifa Mwanza na mwaka huu tutafanya vizuri tutaleta vikombe vyote"alisema Lissu. Aliwataka  maofisa elimu wake wa ngazi za manispaa katika kufanya usaili waweke wachezaji ambao wana sifa na wasiopitiliza umri ili wasitie doa katika mashindano ya ngazi ya TAIFA. 

Alisema mwaka huu wachezaji wake wapo vizuri  katika kambi Jitegemee wanamichezo 750 wakiwemo wanafunzi 650  na walimu, makocha na viongozi 100."Wakurugenzi wa manispaa zote wamejitahidi na wameakikisha wilaya zao zinakuwa na timu bora ambazo kwa pamoja zinashindana katika michezo mbalimbali ili kuweza kupata wachezaji wa mkoa na wachezaji mahiri"alisema

Aidha alisema kwa mwaka 2018 michezo inayoshindaniwa ni, mpira wa Wavulana na wasichana, netiboli kwa wasichana,mpira wa mikono kwa wasichana na Wavulana, mpira wa wavu kwa Wasichana na Wavulana,mpira kikapu kwa wasichana na wavulana, riadhaa kwa wanafunzi wa kawaida na wenye mahitaji Maalum,Tenis,Bao,na fani za ndani, pamoja na ngoma, kwaya, ngonjera na Mashairi. 

Alisema mkoa wa Dar es Salaam mwaka 2017ulikuwa Bingwa wa umisseta Kitaifa kwa kushinda mikoa yote iliyoshiriki mashindano hayo na mwaka huu mkoa Dar es Salaam umejipanga kufanya vizuri zaidi kuchukua vikombe vingi kwa mshindi wa kwanza kama ilivyokuwa mwaka 2017.

Lissu alisema kupitia michezo hiyo watapatikana wanamichezo bora zaidi ambao watapambana kuhakikisha ushindi haupotei kwani dhamira wanayo, Nguvu wanayo na uwezo wa kutosha pia wanao.Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Jumaane Ndayigeze alisema Ofisi ya Rais TAMISEMI imetoa mwongozo wa uendeshaji michezo hii ya umisseta ambapo michezo uanzia katika ngazi ya shule, kata Klasta, Wilaya, mkoa na hatimaye TAIFA. 
 Wanafunzi wa Shule za Sekondari mkoa Dar Es Salaam wakiwa katika ufunguzi wa Mashindano ya Umoja wa SHULE za Sekondari UMISSETA Dar Es Salaam jana Picha na Heri Shaaban

ALICHOKISEMA WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA KATIKA MAADHIMISHO YA MFUKO WA RAIS WA MAREKANI KUDHIBIRI UKIMWI

Rais Dk.Shein akutana na ujumbe wa Saudi Arabia

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na  Waziri wa Mamlaka ya Saudi Arabia anayeshuhulikia Mambo ya Kiislamu, Misaada, Daawa na Miongozo Mhe. Dk.Sheikh Saleh bin Abdul Aziz bin Muhammad bin Ibrahim Al Sheikh, akifuatana na Ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Waziri wa Mamlaka ya Saudi Arabia  anayeshuhulikia Mambo ya Kiislamu, Misaada, Daawa,na Miongozo Mhe,Dk.Sheikh Saleh bin Abdul Aziz bin Muhammad bin Ibrahim Al Sheikh,(wa tatu kulia)  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Ujumbe wake.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Waziri wa Mamlaka ya Saudi Arabia anayeshuhulikia Mambo ya Kiislamu,Daawa,Misaada na Miongozo  Mhe. Dk.Sheikh Saleh bin Abdul Aziz bin Muhammad bin Ibrahim Al Sheikh,(kushoto) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na Ujumbe wake,(katikati) Mkalimani wa lugha) Sheikh Khalid Mohammed Mrisho.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) alipofuatana na Waziri wa Mamlaka ya Saudi Arabia anayeshuhulikia Mambo ya Kiislamu, Daawa, Misaada na Miongozo  Mhe. Dk.Sheikh Saleh bin Abdul Aziz bin Muhammad bin Ibrahim Al Sheikh,(kushoto) baada ya mazungumzo yao leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar  akifuatana na Ujumbe wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na  Waziri wa Mamlaka ya Saudi Arabia anayeshuhulikia Mambo ya Kiislamu, Daawa, Misaada na Miongozo  Mhe. Dk.Sheikh Saleh bin Abdul Aziz bin Muhammad bin Ibrahim Al Sheikh,(kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo baada ya mazungumzo yao akifuatana na Ujumbe wake,(hawapo pichani) (Picha na Ikulu)

DKT. ASHATU KIJAJI AZIPONGEZA BENKI KUSHUSHA RIBA ZA MIKOPO

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Uamuzi wa Serikali wa kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na benki za biashara  nchini, umechochea taasisi za fedha yakiwemo mabenki kuanza kupunguza viwango vya riba ya mikopo hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi.

Hayo yalisemwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha uliowashirikisha wabunge, washirika wa Maendeleo, wakuu wa Taasisi za fedha na Wizara ya Fedha na Mipango.

Dkt. Kijaji, alisema kuwa Serikali kupitia Benki Kuu imeshusha riba ya mikopo kwa taasisi za fedha kutoka asilimia 16.0 hadi  asilimia 9.0 na  kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa katika Benki hiyo na benki za biashara kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0  kuanzia mwezi Aprili 2017, jambo ambalo limeleta matokeo chanya katika kuimarisha uwezo wa taasisi kukopesha wateja wao.

Miongoni mwa Benki zilizoshusha viwango vyao vya riba za mikopo ni CRDB ambayo imetangaza kushusha riba kutoka asilimia 22 hadi 16 na kuongeza kiasi cha kukopa kwa wafanyakazi kutoka Sh. milioni 50 hadi Sh. milioni 100 huku muda wa kurejesha ukiongezwa kutoka miaka mitano hadi saba.

Benki  nyingine ni NMB ambayo imeongeza muda wa marejesho ya mikopo kwa wafanyakazi, wajasiriamali wadogo na wakubwa kutoka miezi 60 hadi 72, na  imepunguza riba ya mikopo kwa wafanyakazi kutoka asilimia 21 hadi 19 na wajasiriamali wadogo kutoka asilimia 23 hadi 21.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akifunga  warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akizungumza wakati wa  kufunga warsha  ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma. 
 Mbunge wa Jango’mbe Mhe. Ally Hassan King akizungumza  wakati wa  kufunga warsha ya wadau wa Sekta ya Fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Honest Ngowi akiongoza mjadala wakati wa warsha  ya wadau wa sekta ya fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.
 Mmoja wa wadau wa Sekta ya Fedha  akizungumzia umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta hiyo katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo hapa nchini ili kuchochea maendeleo.
 Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA), Dkt. Boghayo Saqware  akizungumzia hoja mbalimbali zilizoibuliwa na wajumbe wa   warsha  ya wadau wa sekta ya fedha iliyolenga kujadili mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa viwanda leo Jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAKAZI MKURANGA WAPIGWA MARUFUKU KUVUKA KATIKA MTO

$
0
0
Na  Emmanuel  Massaka wa Globu ya jamii,Mkuranga

HALMASHAURI ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imepiga marufuku  wakazi wa Wilaya hiyo na wanafunzi kutovuka katika mito,na badala yake watumie njia za barabara ili kuepuka kuzama katika maji ikiwamo kuumizwa na wanyama katika mito hiyo.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Filbeto Sanga,katika kikao cha robo mwaka cha Baraza la madiwani  wilayani hapo."Kutokana na mvua kunyesha katika kipindi cha mwezi wa nne  na mwezi huu,miundombinu imeharibika na watu wamekuwa wakitumia mito kuvuka kwenda Shule na wengine kwenda kutafuta mahitaji.

" Sasa naomba wanafunzi na wananchi,wasitumie mito kuvuka kwani kuna baadhi ya watu walipoteza maisha pia kuna wanyama wakati katika mito hiyo," amesema.Amesema wanafunzi watano walipoteza maisha katika mvua na kuna watu makubwa ambao wamepoteza maisha,lakini wanawafuatilia ili baraza lijalo idadi yake itajulikana na kuambiwa walipoteza maisha.

Amesema kutokana na mvua kunyesha miundombinu imeharibika na baadhi ya kaya nyumbani zao zimejaa maji na  hari hiyo ilisababisha kuyahama makazi.Wakati huo huo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Juma Abeid amesema  halmashauri hiyo imefanikiwa kupata hati safi kutokana na kusimamia  vizuri miradi ya maendeleo ambayo imekamilika kwa wakati.

Akizungumza katika baraza la madiwani alisema kuwa,Serikali kila mwaka wanafanya ukaguzi katika halmashauri zote nchini na kama halmashauri itakuwa haikufanya vizuri inapata hati chafu.Amesema kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wakuu wa idara na madiwani,wameweza kufanya kazi kwa pamoja na kufanikisha fedha za miradi ya maendeleo kutumika kama ilivyokusudiwa,kukaa vikao kwa wakati na kusimamia fedha vizuri za halmashauri.

"Yote hayo tumeyafanya kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani na tukafanikiwa kupata hati safi," amesema Juma Abeid.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Dk Stephen Mwandambo (wapili kutoka kushoto) akiwa na watendaji wa wilaya hiyo katika mkutano wa robo mwaka wa baraza la Madiwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbeto Sanga akizungumza Michuzi juu ya kupiga marufuku kwa wananchi na wanafunzi kutokuvuka mito badala yake watumie njia za barabara ili kuepuka kuzama katika maji na  kuumizwa na wanyama katika mito hiyo (kushoto)  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde akizungumza katika mkutano wa robo mwaka wa baraza la madiwani.

RAIS MAGUFULI ALIPOPOKEA RIPOTI YA UHAKIKI WA MALI ZA CCM, KATIBU MKUU MPYA WA CCM ALIPOTANGAZWA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein wakiwa na 'mlima' wa makabrasha ya ripoti ya uhakiki wa mali za chama baada ya kukabidhiwa na tume aliyounda kuchunguza mali hizo ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam Mei 29, 2018
 Wa kwanza kushoto ni Dkt Bashiru Ali Kakurwa ni Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli kuchunguza na kuhakiki mali za CCM akiwa na wajumbe wa tume hiyo mara tu baada ya jina lake kupendekezwa kuchukua nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam Mei 29, 2018
 Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya  CCM wakisamama na kuunga mkono kwa kauli moja pendekezo la Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam Mei 29, 2018
Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli kuchunguza na kuhakiki mali za CCM  Dkt. Bashiru Ali Kakurwa akipongezwa  na wajumbe wa tume hiyo mara tu baada ya jina lake kupendekezwa kuchukua nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam Mei 29, 2018

PICHA NA IKULU

ULEGA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MADARAJA MKURANGA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

NAIBU  Waziri Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga, Abdalah Ulega ameweka jiwe la msingi  kwa ajili ya  ujenzi wa madaraja matatu wilayani Mkuranga mkoani Pwani

Akizungumzia ujenzi wa madaraja hayo ,Ulega ameeleza  madaraja hayo matatu yatajengwa katika vijiji vitatu ambavyo ni  Tamabani Mwanabilatu, na Kifaurongo.

Amesema ujenzi wa madaraja hayo hadi kukamilika kwake Julai mwaka huu utagharimu kiasi cha takribani Sh.bilioni 1.5.Aidha Ulega amemuagiza mkandarasi anayejenga madaraja hayo asichukue vibarua wa kutoka sehemu nyingine bali wachukuliwe katika vijiji ambavyo mradi huo wa ujenzi wa madaraja unafanyika ili wakazi wa maeneo hayo wapate vipato.

Pia Ulega  amewaomba wananchi wa Wilaya ya Mkuranga kushirikiana na wakandarasi wa ujenzi ili kuweza kurahisisha kazi hiyo na kufanya mradi huo kuisha kwa wakati.Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini(TARULA) Wilaya ya  Mkuranga, Mhandisi Emmanuel Mubofu amesema miradi hiyo ita kamilika ndani ya miezi miwili tu, yaani kuanzia mwezi Mei hadi Julai mwaka huu.

Mubofu ameeleza  mradi huo umeanza na kufikia Agosti wananchi wataanza kutumia madaraja hayo licha ya kuikamilisha Julai.Kuhusu  fedha za ujenzi Mubofu ameeleza kuwa zimetoka mfuko wa barabara kwa ajili ya kero hizo za kimiundombinu zilizokuwa zinawakabili wakazi hao.

Aidha ameeleza wakandarasi wawili wameshaanza kazi na kwa asilimia 20 tayari ujenzi umekamilika.
 Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga  Abdallah Ulega (watatu kutoka kulia) akiweka  jiwe la msingi  kwa ajili ya  ujenzi wa madalaja mitatu yatakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5
 Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi, Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wanaichi wa kijiji cha Kifaurongo kabla katika hafla ya kuweka  jiwe la msingi  kwaajili ya  ujenzi wa madalaja mitatu yatakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.5(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
 Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega  akimsikiliza Kaimu Mejeneja Tarula Mkuranga Muhandisi Emmanuel  Mubofu alienyosha mkono alipo tembelea mradi wa ujenzi wa madaraja.
 Naibu Waziri Mifungo na Uvuvi,Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa ameambatana na  viongozi wa (CCM) wa Wilaya Mkuranga  wakivuka Mto Mzinga.
Wananichi wa kijiji cha Kifaurongo wakivuka Mto Mzinga.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akijibu swali kuhusu utaratibu unaotumika kutoa ajira kwa wananchi katika sekta za Muungano leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki  na Naibu Waziri Mhe. Dotto Biteko leo Bungeni  Jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali  na majibu.
 Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Tate Ole Nasha akieleza mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa inajenga vyuo vya ufundi stadi kila Wilaya hapa nchini leo  Bungeni  Jijini Dodoma.
  Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi ( kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Sera,  Bunge, Uratibu,   Kazi,  Vijana,  Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.   Jenista Mhagama wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni  Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Welezo  Mhe. Saada Salum  Mkuya akiuliza swali kuhusu utaratibu unaotumika katika kutoa ajira katika sekta za Muungano.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  (JKT) Dkt. Hussein   Mwinyi akieleza hatua zinazochukuliwa na Serikali  katika kutatua migogoro ya mipaka kati ya wananchi na Jeshi  la Ulinzi  la Wananachi wa Tanzania ( JWTZ) wakati wa kipindi cha maswali na majibu  leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Wanafunzi wa Shule ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni kwa ziara ya mafunzo  wakati wa kipindi cha maswali na majibu, leo Jjijini Dodoma.

(Picha na Frank Mvungi- MAELEZO)

EFM REDIO YATUA RASMI DODOMA

$
0
0
KITUO cha Utangazaji cha Efm redio katika kuhakikisha kinaenda sanjari na maendeleo pamoja na mpango wa serikali wa kuhamia Jijini Dodoma, imewasha rasmi masafa yake leo Jijini humo ambapo inasikika kupitia masafa ya 92.5 fm. 

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Efm Radio na TV E, Bwana Dennis Busulwa, wameelekeza matangazo ya kituo hicho Jiji la Dodoma kwa kuangalia uhitaji wa jamii pamoja na maendeleo ya jiji katika kuhabarisha, kuburudisha pamoja na kuelimisha.

Bwana Busulwa amesema Vilevile Efm redio inatarajia kuwasha masafa yake katika mkoa wa Morogoro, Tabora, na Kigoma pamoja na mikoa mingine ili kuhakikisha watanzania wote wanapata matangazo yake.

Aidha, Efm redio inazidi kuishukuru serikali na wadau wake wote hususani wasikilizaji wake kwa kuendelea kuwaunga mkono pamoja na kuwaahidi wasikilizaji wake kutimiza wajibu wake uliojiwekea kama chombo cha habari pamoja na kufikisha matamasha yake hususani ya uwezeshaji katika kuendeleza uchumi pamoja na elimu katika jamii.

AIRTEL NA ITEL WAZINDUA SIMU AINA YA A32F, WATUMIAJI KUNUFAIKA NA BANDO LA MIEZI SITA BUREE.

NEWS ALERT: Serikali yashinda kesi iliyofunguliwa na wadau wa habari juu ya kanuni za mitandaoni

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images