Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

TaESA WAKANUSHA TAARIFA YA TANGAZO LA AJIRA LINALOSAMBAA MTANDAONI

0
0
WAKALA wa Huduma za Ajira Tanzania(TaEsa) umesema umesikitishwa na taarifa potofu ambazo zinasambazwa kupitia tangazo la ajira .

Imefahamika taarifa hiyo inayosambaa kupitia tangazo hilo inasomeka ‘’CHINI YA MH:RAIS WETU DKT JOHN POMBE MAGUFULI KUPITIA SHERIA YA UANDIKISHAJI VIZAZI NA VIFO SURA 108 YA MWAKA 2000’’ kwamba tunatangaza ajira kwa vijana wote waliomaliza mafunzo ya uwalimu ngazi ya cheti,stashahada na waliosoma vyuo vya utumishi wa umma ngazi ya cheti.

Taarifa hiyo ya upotoshaji inaendelea kueleza mchakato wa usajili ajira linaratibiwa na RITA kwa kushirikiana na TaESA na kwamba maombi yameanza kupokelewa Mei 5 mwaka 2018 hadi Julai 7 mwaka 2018 na hivyo waombaji wote watume maombi yao kupitia barua pepe, taesa.ritarecruitment.go.tz@outlook.com.

Taarifa ya TaESA imesema leo jijini Dar es Salaam imefafanua tangazo hilo ni uzushi na utapeli wa wazi kwani RITA haina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia utaratibu huo ulioainishwa hapo juu.

Imefafanuliwa badala yake ajira zote zinatangazwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kusimamiwa na Sekretarieti ya Ajira na siyo TaESA.Aidha wamesena wanachukua fursa hiyo kuwatahadharisha wananchi kuhusu watu wanaojifanya kuwa ni Mawakala wa RITA chini ya Kampuni yao ya Mtema Brokers Limited ambao wanafanya kazi za usajili wa vizazi na vifo katika Mikoa mbalimbali Tanzania Bara.

TaESA imeelezwa watu hao ni matapeli hivyo yeyote mwenye taarifa sahihi afike kituo cha Polisi kilichopo karibu naye au awapigie kwa namba za simu hapo juu.Kampuni hiyo imeshawatapeli wananchi katika maeneo ya Kipunguni B,Temeke,Kinondoni,Kigamboni Sinza Jijini Dar es salaam na Mlandizi mkoani Pwani ambapo zaidi ya wananchi 1000 wametapeliwa fedha zao.
 Afisa habari wa TaESA, Jamila Mbarouk akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo  jijini Dar es Salaam , kuhusu kukanusha na kuwaomba wananchi wasitume fedha katika Kampuni ya  Mtema Brokers Limited watatapeliwa pesa zao.
 Afisa habari wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Jafari Hamadi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kukanusha taarifa zilizo enea katika mitandao ya kijamii na kubandikwa katika semu mbalimbali unaosema kwamba wametangaza ajira, Tangazo hilo ni uzushi na utapeli wa wazi kwani RITA haina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia utaratibu huo.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Mkutano ukiendelea.

MAHAKAMA YAKWAMA KUANZA KUSIKILIZA UTETEZI KESI YA WEMA SEPETU

0
0
Ni baada ya mama Wema kudai mwanaye ameenda India kufanyia upasuaji

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuanza kusikiliza utetezi wa msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya sababu amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Taarifa hiyo imewasilishwa mahakamani hapo na Mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa Serikali, Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani.

Wakili Kakula alidai, kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya mshtakiwa Wema kuanza kujitetea lakini anashangaa kutokumuona mahakamani hapo kwani hata ahirisho la mwisho la kesi yake hakuwepo.

Kufuatia  hayo, Mama Wema alisimama na kutoa nyaraka za Wema za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Wakili Kakula alidai hakuna uthibitisho wowote wa kuonesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba Mahakama isimamie sheria.Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba amesema ni kweli hakuna uthibitisho, hivyo katika tarehe ijayo uthibitisho unapaswa kuwepo, na kesi  imeahirishwa  hadi June 13 mwaka 2018.

Mbali na Wema, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni wafanyakazi wa Wema, Angelina Msigwa na Matrida Abbas. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya.

Inadaiwa Februari 4 mwaka 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio, washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February Mosi mwaka 2017 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.

WIZARA YA ARDHI YAOMBA BILIONI 73 KWA MWAKA 2018/2019.

0
0
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maedeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwasilisha Bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo ameliomba Bunge kujadili na kuopitisha kiasi cha shilingi 73,071,273,632 iloi wizara iweze kutumiza majukumu yake.
 Waziri, Lukuvi ameliambia Bunge kuwa katika mwaka wa fedha wa 2018/19 wizara inataraji kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 120 kutokana na kodi, tozo, na ada mbalimbali za zinazotokana na shughuli za sekta ya ardhi kwa kutekeleza mikakati ambayo wamejiwekea. 
 Msemaji wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili na Utalii, Halima Bulembo akisoma taarifa ya Kamati Bungeni leo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akijadili jambo na Naibu Waziri wake, Dk. Angelina Mabula Bungeni leo. 
 Wabunge wakiwa Bungeni jijini Dodoma leo .

VIJANA 966 WAHITIMU MAFUNZO YA KIJESHI MLALE JKT

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akikagua Gwaride maalum la vijana wa kujitolea waliomaliza mafunzo ya miezi minne ya kijeshi katika kikosi cha 842 Kj Mlale wilayani Songea ambapo jumla ya vijana 966 walimaliza mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali katika kikosi hicho.
 Baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo ya kijeshi na ujasiriamali katika kikosi cha 842 Kj Mlale Operesheni Mererani wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme(hayupo pichani)wakati wa kuhitimu mafunzo yao ya miezi minne katika kikosi hicho.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiongea na vijana,wazazi,Askari na maafisa mbalimbali wa jeshi la kujenga Taifa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika kikosi cha 842 wakati wa kufunga mafunzo ya miezi minne ya kijeshi na Ujasiriamali kwa vijana 966 waliohitimu mafunzo yao jana,kushoto kwake ni mkuu wa kikosi cha 842 Kj Mlale Luten Kanal Absomlomon Shausi.Picha na Muhidin Amri
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiangalia Tikiti maji katika Bustani ya kikosi cha 842 Kj Mlale JKT mkoani Ruvuma alipokwenda kwa ajili ya kufunga mafunzo   ya vijana Operesheni Mererani jana.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akitoa kitambaa kama Ishara ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la mradi wa ufugaji Kuku katika kikosi cha 842 Kj Mlale mkoani Ruvuma,anayemsaidia  kuondoa kitambaa ni mkuu wa kikosi  hicho    Lutewn Kanali Absolomon Shausi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

EXIM BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE MWANZA

0
0
 Meneja wa Benki ya Exim tawi la Mwanza Deo Makwaia, akizungumza na wateja wa benki hiyo wa jijini Mwanza wakati wa hafla ya Futar iliyoandaliwa na benki hiyo.
 Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba,akichukua Futar, wakati wa hafla ya  kufuturu iliyoandaliwa na benki hiyo jijini humo. 
 Wateja wa Benki ya Exim Mwanza wakichukua Futar, wakati wa hafla ya  kufuturu iliyoandaliwa na benki hiyo juzi.
Wateja wa Benki ya Exim wakifuturu, wakati wa hafla ya  futar iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Mwanza juzi.

LIVE BUNGENI:KUAGWA KWA MBUNGE BILAGO MJINI DODOMA HIVI SASA

VODACOM M-PESA YASHEREHEKEA MIAKA KUMI YA KUBADILISHA MAISHA YA WATANZANIA

0
0
Vodacom Tanzania PLC leo imetimiza miaka kumi tangu kuzinduliwa kwa huduma ya M-Pesa. Kwa miaka hiyo kumi, Vodacom M-Pesa imejikita kwenye huduma mbali mbali kama kulipia huduma na bidhaa, huduma za kibenki, kuweka na kukopa pesa, kutuma pesa nje ya nchi na zingine nyingi. Huduma hizo zote zinatokana kwa njia rahisi sana ya huduma ya pesa kwa njia ya mtandao ambayo ilikuwepo tangu mwanzoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Vodacom Tanzania Ian Ferrao alisema, M-Pesa imeweza ajira za moja kwa moja na ambao sio za moja kwa moja zaidi ya 200,000- wengi wao wakiwa ndio wanaanza ujasiriamali – na kufanya zaidi ya Tzs 617 bilioni kulipwa kama kasmine kwa mawakala kila mahali Tanzania. 

Zaidi ya Tzs 120 bilioni zimetolewa kama mikopo tangu kuzinduliwa kwa M-Pawa (huduma ya kuweka na kukopa) mwaka 2014 na hivyo kufanya wajasiriamali kuanzisha biashara mpya na hivyo kubadilisha hali ya maisha yao ya kila siku. Mpaka sasa zaidi ya Tzs 99 bilioni zimetolewa kama faida kwa watumiaji wa M-Pesa milioni 8 na zaidi ya Tzs 355 bilioni zimewekezwa kwenye benki mbali mbali hapa Tanzania. Hii inaamanisha kuwa M-Pesa, pesa yako inaendelea kutengeneza faida kupitia kwenye akaunti yako.

Mafanikio ya M-Pesa kwa miaka kumi iliyopita inamaanisha mwanzo mpya wa malipo kwa njia ya kidijitali hapa Tanzania. M-Pesa imenguza na kubadilisha maisha ya mamilioni ya Watanzania pekee. Miaka kumi iliyopita, M-Pesa ilimaanisha kutuma na kupokea pesa kutoka kwa mteja mmoja kwenda kwa mwingine. 

Ian alipongeza juhudi za Vodacom kuboresha na kukuza huduma ya fedha kwa simu za mkononi hapa Tanzania na kuchangia kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutengeneza ajira, kukuza biashara na sana sana wajasiriamali wadogo na wa kati pamoja na kukuza uchumi wa nchi. Leo zaidi ya 35% uchumi wa nchi – GDP unachangiwa kwa kupitia M-Pesa huku kila mwezi ziaidi ya miamala yenye thamani ya 1.2 trilioni ikifanyika.

Kusherekea miaka kumi ya mafanikio ya Vodacom M-Pesa kuna kuja baada ya kuzawadiwa zawadi ya GSMA Mobile certification kwa usalama na utaalam uliotukuka na kuifanya Vodacom M-Pesa moja na bidhaa za kampuni za simu za mkononi kupata cheti cha kimataifa.


Ian Ferrao aliongeza kuwa maadhimisho ya kutimiza miaka kumi yatafanyika mikoa mbali mbali hapa Tanzania ikiwa ni kwa kampuni kuonyesha shukrani kwa wafanyakazi, mawakala wa M-Pesa, wafanyabiashara ambao kwa pamoja wameweza kuchangia safari hii ya mafanikio.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao (katikati) akizunguza na waandishi wa habari leo wakati wa maadhimisho ya miaka kumo ya kuanzishwa kwa huduma ya M-Pesa nchini Tanzania leo katika ukumbi wa Makao makuu ya Vodacom hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mwendelezo ya Biashara ya M-Pesa, Polycarp Ndekana  na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(kulia)  akitoa zawadi kwa mwandishi wa EATV, Njonanje Samwel (kushoto)   wa habari ambaye alikuwepo wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-Pesa 2008
Mkuu wa Kitengo cha Mwendelezo ya Biashara ya M-Pesa, Polycarp Ndekana akizungumzia namna walivyojiimarisha kwenye huduma ya M-Pesa hapa nchini pamoja na nje ya nchi wakati wa maadhimisho ya miaka Kumi ya kuanzishwa kwa huduma ya M-Pesa hapa nchini kupitia mtandao wa Vodacom.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Plc, Rosalynn Mworia akitoa ufafanuzi kuhusu huduma za Mpesa zinazotolewa na Mtandao wa Vodacom hapa nchini.

HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, MHE WILLIAM LUKUVI ALIOIWASILISHA MAPEMA LEO BUNGENI MJINI DODOMA

0
0
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maedeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwasilisha Bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo ameliomba Bunge kujadili na kuopitisha kiasi cha shilingi 73,071,273,632 iloi wizara iweze kutumiza majukumu yake.


MKANDARASI WA KITUO CHA AFYA GAIRO ATAKIWA KUMALIZA KAZI KWA WAKATI

0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameutaka uongozi wa wilaya ya Gairo unamsimamia mkandarasi na kuhakikisha upanuzi wa kituo cha afya na unakwisha kwa wakati.

Akizungumza na uongozi na mkandarasi wakati wa ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita ya kukagua maendeleo ya Wilaya ya Gairo, Mhe. Kebwe amesema kuwa hajaridhishwa na kasi wanayokwenda nayo katika upanuzi wa kituo cha afya unaofanyika hivi sasa licha ya kuwa fedha za kituo hizo zote zimeshatolewa.

"Ni nini kinakwamisha ujenzi kuisha wakati fedha mmeshapewa???? amemuuliza Mkandarasi na Uongozi unaosimamia jengo hilo ... nawaomba sana, hebu fanyeni haraka maana kuna baadhi ya huduma wananchi wanakwenda kuzipatia mbali," amesema.

Amesema kuwa ipo haja ya kila mtu kutimiza majukumu yake bila ya kusukumwa sukumwa maana hali ya sasa ni kazi tu.

Awali akitoa maelezo ya ujenzi, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba amesema kuwa ujenzi huo umeshagharimu zaidi ya milioni 139 na baada ya kukamilika jumla ya wananchi wapatao 218,000 wataweza kupatiwa huduma huku vipimo vyote vikipatikana.


 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (aliyeshika tofali na mwiko) na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Rachel Nyangasi (wa kwanza kulia) wakishirikiana kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (aliyebeba tofali) kumsaidia fundi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe kujenga ukuta wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akikagua ujenzi kwa ajili ya kupanua eneo la kulaza, na sehemu ya kuhifadhia maiti wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na Mkuu wa wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Mchembe (mwenye blauzi nyekundu) wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo, Dennis Ngaromba (wa kwanza kulia) wakati akitoa maelezo juu ya upanuzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Watanzania watakiwa kujenga utamaduni wa kunywa maziwa kila siku kujenga afya,kuongeza pato la taifa.

0
0

Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Daniel Daqarro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amesema katika kuadhimisha wiki ya maziwa Mkoani Arusha, wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Themi Njiro maalufu kama viwanja vya nanenane.

Amesema maonyesho hayo ya wiki ya maziwa yanatija kubwa sana kwa wafugaji,wasindikaji na wananchi kwa ujumla kwani wataweza kujifunza juu ya umuhimu wa unywaji maziwa na ufugaji wa kisasa.Aidha,amewataka maafisa mifigo wote kuhakikisha wanasambaza elimu hiyo mpaka ngazi za chini kwenye jamii hususani namna ya ufugaji wa Ngo’mbe wachache na wenye tija.

Mwenyekiti wa bodi ya maziwa bwana Charles Malunde, amesema unywaji wa maziwa kwa Mtanzania mmoja ni wastani wa lita 47 kwa mwaka ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo wastani upo juu,hasa nchi ya Kenya ni lita 63 kwa Mwaka.

Amesema maziwa ni mlo kamili kwani yamebeba virutubisho vya aina zote vinavyoitajika katika mwili wa binadamu.Akisisitiza zaidi,amesema Tanzania ina takribani Ng’ombe milioni 30.5 ambapo Ngo’mbe milioni 27 niwakienyeji na wanatoa lita 1 hadi 1.5 ya maziwa kwa siku na milioni 1 ndio Ngo’mbe wa kisasa.

Tanzania ina idadi kubwa ya Ngo’mbe na hawana tija katika uzalishaji wa maziwa kwani Ngo’mbe wa kisasa wanauwezo wakutoa lita 30 hadi 40 za maziwa kwa siku.Kaimu Mkurugenzi wa balaza la Kilimo Tanzania bwana Timothy Mbaga,amesema maonyesho hayo ya 21 hayatakuwa na kiingilio chochote ili kutoa fursa zaidi kwa wafugaji kushiriki kwa wingi.

Pia maonyesho hayo yatawasaidia wafugaji kupata maarifa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi na takribani makapuni 40 yameshathibitisha ushiriki.Maonyesho ya mifugo na wiki ya maziwa Kitaifa yatafanyika jijini Arusha kuanzia Mei 30 hadi Juni 1, 2018 katika viwanja vya Themi Njiro na yatafunguliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Luhanga Mpina na kufungwa na Waziri wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mheshimiwa Daniel Daqarro akiwa na wenyekiti wa bodi ya maziwa bwana Charles Malunde na Kaimu Mkurugenzi wa alaza la Kilimo Tanzania bwana Timothy Mbaga wakizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya wiki ya mifigo na maziwa,Jijini Arusha.

MFANO WA BARUA YA KUOMBA NAKALA YA HUKUMU HUU HAPA.

0
0
Na  Bashir Yakub.

Nakala ya hukumu ni haki yako ikiwa ulikuwa mhusika katika kesi au shauri. Unakuwa mhusika katika kesi au shauri pale unapokuwa mshitaki au mshitakiwa,  mlalamikaji au mlalamikiwa, au mhusika mwingine mwenye maslahi.  Hapa ndipo unapohesabika kuwa mhusika katika kesi au shauri na hapa ndipo unapokuwa na haki ya kuomba kupatiwa nakala ya hukumu.


Makala yaliyopita yalieleza kuwa nakala ya hukumu ni muhimu hasa ukitaka kukata rufaa au kuchukua hatua zaidi , lakini pia ni muhimu kama nyaraka ya kumbukumbu kwa ajili ya kesho, pia ni muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa kile kilichoamuliwa.  Leo tuone mfano halisi wa barua ya  maombi ya  nakala ya hukumu 

kama ulivyo hapa chini ;-




Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,                                                        24 / 5 / 2018

S.L.P..............................

Dar es salaam.

YAH ; MAOMBI YA KUPATIWA NAKALA YA HUKUMU.

Nilikuwa mlalamikiwa katika shauri namba  13 la mwaka 2018,  ambalo limetolewa hukumu tarehe 22 / 3 / 2018, mbele ya Mhe. Kijana Mponela. Ninaomba kupatiwa nakala ya hukumu  kwa kumbukumbu au hatua zaidi.

Wako

Mti Mkavu

( Aliyekuwa mlalamikiwa ).

0717600900

Sahihi...............................

               

Tanzania itaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani duniani, Balozi Mahiga

0
0
Siku ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa (UN Peacekeeping: 70 Years of Service and Sacrifice).

Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. 

Pia akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya uhakika. " Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga.

Aidha, Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari 3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao 2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika maadhimisho ya miaka 70 ya Siku ya Walinda Amani Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnanzi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Mei 2018. 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Walinda Amani Duniani ambapo alieleza pamoja na kuendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo, Umoja wa Mataifa utaendelea kuhakikisha Dunia inakuwa mahali salama pa kuishi ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu. 
Mhe. Waziri Mahiga akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa uliopo Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Walinda Amani Duniani. 
Wakitoa heshima kwa ajili ya kuwakumbuka Walinda Amani, waliosimama mbele kutoka kushoto ni Mhe. Waziri Mahiga akiwa na Mwakilishi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Maj. Gen. Henry Kamunde, Bw. Alvaro Rodriguez na Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Nsato Marijani. 
Mhe.Waziri Mahiga akisalimiana na Askari walioshiriki katika Misheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. 

Nsajigwa,Pondamali kukalia kuti kavu

0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

KIKOSI cha Timu ya Yanga kufanya mabadiliko ya bechi  la ufundi kwa baadhi ya makocha.

Ambapo Kocha msaidizi wa kikosi hicho Shadrack Nsajigwa pamoja na kocha wa makipa  Juma Pondamali ndio watakao ondolewa na kuongezwa wengine.

Huku wakibaki Mwinyi Zahera, Pamoja na Noeli Mwandila katika benchi hilo la ufundi.

Akiongezeka Kocha wa Kagera Sugar  Meck Mexime huku nafasi ya Juma Pondamali ikichukuliwa na Razack Siwa ambaye ni raia wa Nchini Kenya.

Baada ya Kikosi hicho kutokufanya vizuri katika msimu huu uliofikia Tamati jana Mei 28 Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.

Ambapo msimu huu umemlizika vibaya kwa upande wao kwa  kushika nafasi ya 3 wakiwa na alama 52 Azam wakiwatangulia mbele kwa pointi 6 na kushika nafasi ya Pili,Huku Mabingwa wapya wa ligi hiyo Simba Sc wakiwa mbele kwa alama 69.

KIKAO CHA KUJUANA CHAFANYIKA PEMBA KUTOKANA NA UGATUZI ULIOFANYWA NA SMZ

0
0
Na Masanja Mabula, Pemba
 KAIMU Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Bi Salma Abuu Hamad amewataka walimu wa wakuu wa skuli za msingi kuongeza uwabikaji katika kusimamia maendeleo ya elimu katika skuli zao ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Akizungumza na walimu wakuu wa skuli za msingi ambazo zimeinga kwenye mpango wa Serikali wa Ugatuzi , Kaimu Mkurugenzi amesema ni vyema walimu wakuu kuwa makini katika kuwasimamia walimu wao kwani kuongezeka ufaulu wa wanafunzi ni sifa kwa mwalimu.

Amefahamisha kwamba kazi ya uwalimu ni wito , hivyo wanatakiwa kuweka mbele maslahi ya taifa kwanza kwa kuhakikisha walimu wanaowasimamia wanatimiza wajibu  wao kwa wanafanzi.

’’ Pamoja na Serikali ya awamu ya saba kuoongeza mshahara kwa wafanyakazi wake ,lakini natambua walimu kuna malipo mengine huku tuendako , hivyo mnatakiwa kusimamia vyema suala la uwajibikaji sehemu za kazi kwa mnaowaongoza’’ alifahamisha.

Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Fundi Msingi Maulid Ali Salim amuomba uongozi wa Baraza la Mji Wete kuandaa utaratibu wa kuwalipa posho walimu wanaojitolea ili wasivunjike moyo na waendelea kuwasaidia  wanafunzi.

Ameeleza kwamba skuli nyingi zinakabiliwa na upungufu wa walimu na hivyo kulazimika kuwatumia walimu wa kujitolea , ili kuweza kusaidia wanafunzi kuhakikisha wanakamilisha vipindi vyao vya masomo.

‘’Baadhi ya skuli mwalimu akiumwa na wanafunzi wanaumwa , mwalimu akijifungua na wanafunzi wanajifungua , maana yangu ni kwamba mwalimu akiuumwa na wanafunzi hawaji skuli’’alieleza.

Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali Mkoa wa Kaskazini Pemba Mohammed Nassor Salim amesema dhamira ya Serikali wa kuzigatua baadhi ya taasisi ni kuleta usimamia imara wa utoaji wa huduma bora .

 ‘’Lengo la serikali ya kufanya ugatuzi ni kurahisisha kupatikana huduma bora kwa wananchi , na kwa upande wa Wizara ya elimu utoaji wa huduma bora umepatikana kwa kipindi hichi cha ugatuzi’’alifahamisha.

Hata hivyo wakichangia katika mkutano huo baadhi ya madiwani wameahidi kuendelea kufanya ufuatiliaji maskulini kwa lengo la kihimiza uwajibikaji wa walimu .
 Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Bi Salma Abuu Hamad akifungua kikao cha Madiwani na walimu wakuu wa skuli za msingi za Mkoa wa Kaskazini Pemba kilichofanyika katika Ofisi za Baraza la Mji Wete.
 Baadhi ya walimu wakuu wakimskiliza Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Bi Salma (hayupo pichani ) wakati wa mkutano wakujuana kufuatia mfumo uliopo wa ugatuzi.
 Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali Mkoa Kaskazini Pemba Muhammed Juma Ali akichangia kitu katika Mkutano wa kujuana katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Mji Wete Asaa Juma Ali (kusho) Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete Bi Salma Abuu Hamad.

Picha na Makame Mshenga Pemba.

SEKTA YA FEDHA YATAKIWA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA UTOAJI WA MIKOPO

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
SERIKALI imeitaka Sekta ndogo ya Benki kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda na kilimo pamoja na wajasiriamali wadogo.

Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, katika Mkutano wa wadau wa Sekta ya Fedha uliowashirikisha wabunge, washirika wa Maendeleo, wakuu wa Taasisi za fedha na Wizara ya Fedha na Mipango.

Prof. Luoga alitoa wito huo kufuatia kuwepo kwa changamoto katika Sekta hiyo ikiwemo  ukosefu wa uwekezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo katika viwanda, kilimo na miundombinu pia  ukosefu wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati.

“Kuna kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma za bima za kilimo, gharama kubwa za huduma za fedha, mifumo hafifu ya kuwalinda  watumiaji wa huduma za fedha, ukosefu wa elimu ya fedha kwa wananchi na wananchi wengi kutofikiwa na huduma za fedha ambapo ni asilimia 8.6 tu ya nguvu kazi ya wananchi waishio vijijini wanapata huduma za benki ikilinganishwa na asilimia 32.1 ya nguvu kazi kwa wanaoishi mijini” alisisitiza Prof Luoga

Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo, Serikali ilifanya maboresho ya Sekta ya Fedha  katika eneo la ubinafsishaji wa benki za Serikali kurekebisha na kutunga sera na sheria mbalimbali hadi kufikia Desemba, 2017 ili kuweka misingi imara ya kuwezesha ukuaji, ushindani na ufanisi katika sekta ya fedha.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisisitiza kuhusu sekta ya fedha kuwa na mikakakati yenye tija katika kukuza uchumi wa viwanda wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, akielezea kuwapo kwa changamoto ya kiwango cha chini cha upatikanaji wa huduma za bima za kilimo na   gharama kubwa za huduma za fedha wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Kaimu Kamishna wa Sera za Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Michael Nyagoga akielezea dhana ya Mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango  kuwa ni pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za kifedha za Sekta ya Viwanda nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei, akisikiliza kwa makini wito wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga (hayupo pichani) kuhusu Sekta ndogo ya Benki kuongeza ubunifu kwa kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu ambayo itawezesha ukuaji wa sekta za viwanda, Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wakurugenzi wa taasisi za fedha na maafisa waandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani) alipokua akieleza wajibu wa sekta ya fedha nchini katika kuwezesha viwanda vidogo vidogo, wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Wakuu wa taasisi za fedha wakiwa katika majadiliano na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma kuhusu mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa viwanda nchini. 
 Wakuu wa taasisi za fedha wakiwa katika  picha ya pamoja na meza kuu wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
 Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya Fedha na Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma ulioangazia mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa viwanda nchini.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizaya ya Fedha na Mipango)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


MUDA WA KUSHUGHULIKIA MIZIGO MPAKANI RUSUMO WAPUNGUA

0
0
Na Veronica Kazimoto
Serikali ya Tanzania na Rwanda kupitia Mamlaka zake za Mapato zimefanikiwa kupunguza muda wa kushughulikia mizigo mpakani Rusumo mkoani Kagera kwa asilimia 73.

Hayo yamesemwa leo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere wakati wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Zanzibar.

Kichere amesema kuwa, baadhi ya mafanikio muhimu ya  mradi huu ni pamoja na uendeshaji wa Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani kwenye mipaka ya Rusumo na Namanga na maendeleo ya uwezo wa utendaji kazi wa maofisa wa forodha na mawakala.

"Mafanikio ya mradi huu yanaonekana wazi, kwa mfano tukichukulia mpaka wa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo, muda wa kushughulikia mizigo mpakani hapo umepungua kwa asilimia 73% yaani kutoka masaa manane na dakika 42 hadi kufikia masaa mawili na dakika 20 tu," alisema Kichere.

Mradi huu wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ni wa miaka mitatu na nusu ambao unafadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) na ulizinduliwa rasmi mwezi Desemba, 2017.

Mradi huu unatekelezwa  na Mamlaka tano za Mapato  za nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki uliofanyika leo Zanzibar. Kushoto ni Mhe. Audace Niyonzima wa Mamlaka ya Mapato Burundi na kulia ni Bw. Toshio Nagase Mwakilishi Mkazi wa JICA.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna Wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki na wajumbe wa Mkutano wa kwanza wa Kamati ya Uratibu wa Pamoja wa Mradi wa Maendeleo wa Kuwezesha Biashara na Udhibiti wa Mipaka Afrika Mashariki ambao umefanyika leo Zanzibar.

BREAKING NEWS: DKT. BASHIRU ALLY APITISHWA NA NEC KUWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kumpendekeza  na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally kwenye meza kuu mara baada ya kumpendekeza  na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally wapili kutoka kulia kwenye meza kuu kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe wa NEC hawaonekani pichani, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwa meza kuu mara baada ya kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwashukuru Wajumbe wa NEC kwa kumpitisha kuwa Katibu Mkuu wa Chama Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wajumbe mara baada ya kikao cha NEC Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA AFYA RAHALEO NA MAKAAZI YA MADAKTARI WA CHINA NA CUBA

0
0
MUUGUZI wa Kitu cha Afya Rahaleo Wanu Amour akimuonyesha kichupa cha chanjo ya watoto Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (mwenye suti) alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho .

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed amesisitiza msimamo wake wa kufuatilia na kupambana na Wafanyakazi wakorofi  wenye tabia ya kuwatolea lugha chafu  wagonjwa wanapofika vituo vya afya kutafuta huduma.

Amesema Wafanyakazi wengi wa vituo vya afya ni wazuri na wanatekeleza wajibu wao kwa uadilifu mkubwa lakini bado wapo wafanyakazi wachache wenye tabia ya kuwanyanyasa wagonjwa na kuwaharibia sifa nzuri wenzao. Waziri Hamad Rashid ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha afya cha Rahaleo baada ya kufanya ziara ya ghafla katika kituo hicho.

Aliwakumbusha wafanyakazi wa sekta ya afya kuwa kilio kikubwa cha Wananchi kilikuwa ni upungufu wa dawa na lugha mbaya kwa wagonjwa lakini tatizo la dawa Serikali imelipatia ufumbuzi. Aliwataka wafanyakazi wa afya kubadilika na kuwafanyia wema na kuwapa upendo  wananchi wanapofika katika vituo vyao  kwa vile lugha nzuri inawapa nafuu wagonjwa .
WAZIRI wa Afya Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Madaktari wa Kichina wanaofanya kazi Zanzibar alipotembelea Makaazi yao Mtaaa wa Vuga Mjini Zanzibar.

Hata hivyo Waziri wa Afya amewataka wagonjwa na jamaa za wagonjwa wanapofika vituo vya afya kufuata taratibu zilizowekwa ili kujenga maelewano mazuri na wafanyakazi. Aidha Waziri Hamad Rashid ameziagiza Manispaa na Mabaraza ya Miji kuimarisha usafi katika vituo vya afya kufuatia uamuzi wa Serikali wa kufanya ugatuzi na vituo hivyo kuwa chini yao.

Mfanyakazi wa Maabara wa Kituo cha Rahaleo Ineneni Fadhil Abdalla alimueleza Waziri Hamad kuwa baadhi ya wananachi wanaopeleka wagonjwa vituo vya afya wamekuwa chanzo kikubwa cha kuvuruga uhusiano mwema baina yao na wagonjwa. Amewashauri wananchi kwa upande wao kuwa wavumilivu na kuwasaidia  wanapofika kupatiwa huduma ili kazi zao ziwe nyepesi zaidi.
KIONGOZI wa Madaktari kutoka Cuba Dkt. Katia Duany Baderas akizungumza na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed (alievaa suti) alipotembelea katika Makaazi yao Vuga (kulia) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman na wapili (kushoto) Mkurugenzi Utumishi Wizara ya Afya Ramadhani Khamis Juma .

Wakati huo huo Waziri wa Afya alitembelea makaazi ya Madaktari wa China na Cuba katika mtaa wa Vuga na kuwashukuru  kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwahudumia wananchi wa Zanzibar. Alitoa pongezi maalum kwa Serikali ya Cuba kwa msaada  mkubwa uliopelekea kuanzishwa shahada ya kwanza katika Chuo cha Taaluma za Sayansi za afya na kukubali kuwapokea wanafunzi wanaochuka shahada hiyo kwa masomo zaidi katika nchi yao.

Amewaomba wahadhiri wa Cuba wanaofundisha Chuo hicho kutoa ushauri kwa Wizara ya afya juu ya kuimarisha huduma ya afya ya msingi na mbinu zitakaosaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wa Zanzibar wanaopelekwa nje kwa ajili ya matibabu.
DAKTARI dhamana wa Kituo cha Afya cha Rahaleo Ashura Miraji Mpatani akizungumzia changamoto na mafanikio ya Kituo cha Afya cha Rahaleo wakati wa ziara ya Waziri wa Afya Hamad Rashid (hayupo pichani).
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akizungumza na Wafanyakazi wa Kituo cha Afya Rahaleo wakati wa ziara yake katika Kituo hicho. PICHA NA ABDALLA OMAR

SHEREKEA SANAA NA NAFASI ART SPACE JUMAMOSI HII

0
0
Sherekea Sanaa ni tamasha la kipekee linalosheherekea sanaa na tamaduni za Tanzania kwa njia ya mziki, miondoko, michoro na mengineyo. Nafasi Art Space inawaalika tarehe 2 Juni kuanzia saa 12.30 joini mpaka saa 5 usiku kwenye tamasha hili linalofanyika kwa ushirkiano wa Nordic Week.

Siku hio, ndani ya ukumbi wa Nafasi Art Space, kutakuwa na maonyesho ya sanaa ya “Silence (ukimya)” zilizoandaliwa na wasanii mbali mbali nchini. Na kwenye jukwaa makundi ya “Muda Dance” na “Nantea Dance” yameandaa maonyesho yao ya miondoko ya kisasa, yaani contemporary dance.

Aidha, kwaya maarufu kutoka Denmark inaojulikana kama Nordlys Choir wataburudisha wahudhuria. Pia dada Grace Matata atakuwepo kuwafuharisha mashabiki wa miziki wa kizazi kipya.
Hivyo kutakuwa na kitu kwa kila mmoja. Tamasha hili la SHEREKEA SANAA ni bure na wote mnaalikwa.

Tuma Barua pepe info@nafasiartspace.org kujua zaidi.

DC SANGA ATOA TATHMINI YA AWALI YA MAAFA YA MVUA MKURANGA

0
0
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mkuranga ,Juma Abeid akizungumza jambo katika kikao cha baraza la madiwani ,wa kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Mshamu Munde.

Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga

MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkuranga, Filberto Sanga, ametoa tathmini ya awali ya maafa yaliyotokea katika mvua zilizonyesha hivi karibuni ambapo wanafunzi watano wamepoteza maisha kwenye mvua hizo. Aidha ametoa tahadhari kwa watu na watoto kuacha kukatiza katika mito na maeneo hatarishi ili kuepukana na maafa yanayoweza kujitokeza.

Akitoa tathmini hiyo kwa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, Sanga alitaja kata walizopoteza watoto hao kuwa ni Tambani wanafunzi wawili ambao walizama, kata ya Mianzi, Mwarusembe,Mwandege mwanafunzi mmoja mmoja. Alieleza kuwa, pia ipo miundombinu ya barabara ambayo imeharibika vibaya na haipitiki. Sanga alisema ,wakati mvua ikiwa ni neema lakini mazingira yalishindwa kuhimili ,hivyo wamejipanga kuanza kukarabati baadhi ya miundombinu baada ya mvua kukoma. Alifafanua ,tathmini bado inaendelea na watatoa ukubwa wa maafa yaliyotokea baadae.
Diwani viti maalum Mkuranga, Daima Utanga akizungumza jambo wakati wa kikao cha baraza la madiwani wilayani humo .

WAKATI HUO HUO , Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mkuranga wamemtaka afisa elimu msingi wa halmashauri hiyo, kuweka wazi idadi ya shule zilizotumika kiasi cha fedha mil.29. Fedha hizo ni kati ya mil.151 iliyopangwa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa shule mbalimbali wilayani humo ambapo inadaiwa kutumika mil.29 .

Diwani wa kata ya Mwandege ,Kowero Edward na diwani wa viti maalum Daima Utanga waliibua hoja hiyo, katika kikao cha madiwani kilichofanyika wilayani hapo. Walitaka kujua zilizotumika kwenye ukarabati na ujenzi wa madarasa na shule ngapi kwani taarifa inaonyesha gharama bila idadi ya shule husika, zilizotumika fedha hiyo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images