Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

WATOTO TISA WENYE MATATIZO YA MOYO KWENDA KUTIBIWA NCHINI ISRAEL

0
0
Watoto tisa wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wanaondoka leo tarehe 28/5/2018 kwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. Katika safari yao ya matibabu nchini humo watoto wataambata na wauguzi pamoja na wazazi wao.

Safari hiyo ya matibabu nchini Israel inahusisha watoto wenye umri wa miezi tisa hadi miaka 14 imeratibiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini humo. 

Taasisi yetu inatibu magonjwa mengi ya moyo (kwa asilimia 90) kwa watoto kupitia wataalamu wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya wagonjwa wachache ambao ni asilimia 10 wanaohitaji utaalamu wa hali ya juu zaidi kuliko uliopo hapa nchini kwa sasa.

Tunaushirikiano mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa zinagharamiwa na SACH. Aidha tuna madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo sita na wauguzi wanne ambao wamesoma nchini Israel na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu. Daktari wetu mmoja na wauguzi wawili bado wanaendelea na masomo nchini humo hii itasaidia kwa siku za mbeleni zaidi ya asalimia 95 ya watoto watatibiwa hapa nchini.

Hili ni kundi la sita la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH) wa kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 56 wameshatibiwa nchini humo na wanaendelea vizuri.

Taasisi inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulikwa kuwa mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.

Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo au la. Kupitia kipimo hiki mtoto akigundulika kuwa na tatizo la moyo ataweza kupatiwa matibabu kwa wakati na hivyo kuwa na afya njema kama watoto wengine.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
28/05/2018

WAZIRI UMMY AMWAGA FUTARI KWA TAASISI 10 ZA KIDINI NA MAGEREZA JIJINI TANGA

0
0


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kupitia Taasisi yake ya Odo Ummy Foundation leo amegawa futari kwa taasisi za kiislamu na magereza zilizopo Jijini Tanga vyakula mbalimbali ili viweze kuwasaidia wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani. 

Vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi futari hizo mapema leo taasisi zenye wanafunzi waliotika maeneo mbalimbali na wakati mwengine wanakuwa hawana uhakika wa kufutari,watu wengine wajitoleza kulea taasisi hizo pamoja na alisema ameona atoe futari hiyo kwa kila taasisi badala ya kuwaita pamoja kufuturu nao maana wengine wanaweza kushindwa kupata fursa ya kuhudhuria lakini wakikabidhiwa wanaweza kuona namna nzuri ya kuweza kuitumia wakati wa mfungo mtukufu wa ramadhani. 

“Nimeona ni bora nitoe futari hii badala ya kwenda kufuturu kila mahali kwani tutakapofanya hivyo wanaweza kuja wachache na mimi kutokana na kuwa nimetoka kwenye familia ya watu wa kawaida maskini nimeona angalu hicho kidogo ambacho nimejaliwa nitoa kwa taasisi za dini na watoto kwenye mazingira magumu”Alisema. 
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akimkabidhi futari Mkurugenzi wa Taasisi ya kulea watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu ya Goodwill Sayyed Muhdhar Idarus ambapo futari hiyo ambapo taasisi 10 zilipewa futari hiyo kwa kila taasisi ni Unga wa ngano kg 50, mchele kg 100,unga wa ngano kg 50,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20na majani ya chai kilo 3,Maharage Kg 100 na Unga wa Dona Kg 25 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katikati akimkabidhi futari mmoja wa walezi wa vituo vinavyolelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu Jijini Tanga vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akigawa futari kwa wawakilishi wa vituo mbalimbali na taasisi za kidini tano zilizopo Jijini Tanga wakiwemo Magereza vyakula ambavyo vimetolewa na Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kwa kila taasisi ni Unga wa Ngano Kg 50, mchele kg 100,Sukari Kg 25,Tambi Mfuko miwili,Mafuta ya kula lita 20,Maharage kg 100, unga wa dona kg 25,na majani ya chai kilo 3 vyote vikiwa na thamani y ash.milioni 6.8 
 Sehemu ya vyakula mbalimbali vilivyotolewa kwa ajili ya Futari kwa Taasisi 10 wakiwemo Magareza na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM).



NINI UFANYE UNAPOCHELEWESHWA NA MAAFISA WA MAHAKAMA KUPATA NAKALA YA HUKUMU.

0
0

Na Bashir Yakub.

Nakala ya hukumu ya mahakama huhitajika pale kesi au shauri linapokuwa limefika mwisho. 

Kwa lugha nyingine maamuzi ya mahakama ndiyo hukumu ya mahakama. Hapa ndipo tunapojua nani ameshinda na nani ameshindwa. 

Nani anastahili kulipwa au kukabidhiwa mali fulani na nani hastahili. Kadhalika nani anastahili kufungwa na nani anastahili kuachiwa huru. Yote haya na mengine mengi ndiyo yanayojenga kitu kinachoitwa hukumu.

1.UMUHIMU WA NAKALA YA HUKUMU. 

Mara nyingi wale ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya mahakama kwenye hukumu hutaka kukata rufaa. Rufaa ni malalamiko yanayopelekwa mahakama ya juu zaidi yakilalamikia hukumu au maamuzi yaliyotolewa na mahakama ya chini. Rufaa hufunguliwa na mtu ambaye hakuridhika na kile kilichoamuliwa. Kwahiyo hata wewe kama unayo kesi ambayo tayari imetolewa hukumu na hukuridhishwa na kile kilichoamuliwa basi unayo haki ya msingi ya kukata rufaa.

Na huna haja ya kuhofu kama unazo sababu za msingi na za kisheria. Waweza kuwa umeshindwa mahakama ya chini lakini ukaibuka mshindi mahakama ya juu ambako umekata rufaa.

Hata hivyo, huwezi kukata rufaa bila kuwa na nakala ya hukumu. Na hapa ndipo linapojitokeza suala la kupata nakala ya hukumu kwa wakati na bila kucheleweshwa. Narudia huwezi kukata rufaa ikiwa hujapata nakala ya hukumu kutoka mahakama iliyotoa uamuzi.

                KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com 

NHIF TANGA YAHAMASISHA WAFANYABIASHARA KUJIUNGA NA MPANGO WA BIMA YA AFYA

0
0
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) umesema watatumia maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Jijini Tanga kuwahamasisha wafanyabiashara kujiunga nao ili waweze kunifaika na huduma za matibabu pindi wanakuwa wakikumbana na magonjwa mbalimbali. 

Hayo yalisemwa jana na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao kwenye ufunguzi wa maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa yanayofanyika eneo la Mwahako mjini hapa. 

Alisema watakapojiunga nao wataweza kuwa na uhakika wa matibabu wakati wanapougua lakini pia itawawezesha kuepukana na kutumia fedha nyingi pindi wanapokuwa wakiugua zinazotokana na kupanda kwa gharama. 

“Ndugu zangu maradhi yanakuja bila taarifa hivyo iwapo tutawekeza kujiunga na mpango wa Mfuko huu unaweza kufaidika na matibabu lakini pia utaepukana na gharama kubwa za matibabu utakazopaswa kulipia wakati unapokumbana na magonjwa mbalimbali “Alisema. 
 Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku kushoto akitoa elimu kwa mkazi wa barabara 20 Jijini Tanga aliyetembea Banda lao lililopo kwenye maonyesho ya kimataifa ya Biashara 
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku kushoto akimmkabidhi vipeperusi Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga,Lupakisyo Kapange mara baada ya kutembelea Banda leo
 Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) Sophia Kaku akisalimiana na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kuwasAili kwenye viwanja vya Mwahako alipokwenda kufungua maonyesho hayo
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiteta jambo watumishi wa NHIF Tanga kushoto ni Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga Sophia Kaku kulia ni Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Macrina Clemens
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akisalimiana na Afisa matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Macrina Clemens mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga 

Serikali yaandaa utaratibu wa Kuwatambua Wazee nchini

0
0

Na. Atley Kuni na Mathew Kwembe, OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia zoezi la kuwatambua wazee wote nchini katika mikoa yao na wahakikishe kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2018 Mikoa yao inawasilisha Ofisi ya Rais TAMISEMI orodha ya wazee katika mikoa yao.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo, Mhe. Jafo alisema kuwa tayari amekwishatoa maagizo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha kuwa zoezi hilo linashirikisha ngazi zote za Mamlaka ya Serikali za Mitaa.



Alisema ifikapo tarehe 15 juni 2018 anatarajia kuona kuwa zoezi hilo liwe limekamilika katika ngazi ya kata ambapo Mtendaji wa Kata atapaswa kuliwasilisha katika ngazi ya halmashauri kabla ya kufika ngazi ya Mkoa.



Pia alisema kuwa ifikapo tarehe 20 Juni, 2018 anatarajia kuwa zoezi hilo liwe limekamilika katika ngazi ya halmashauri ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri atapaswa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji katika ngazi ya mkoa tarehe 26 juni, 2018.



Waziri Jafo alieleza kuwa ifikapo tarehe 30 Juni, 2018 anatarajia kuwa ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa iwasilishe taarifa hiyo katika Ofisi ya Rais TAMISEMI.



Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa zoezi hilo Mhe.Jafo alisema kuwa serikali imeamua kuchukua hatua hiyo ya kuwatambua wazee wote nchini ili wasiendelee kupata manyanyaso kwa kukosa utambuzi rasmi.



Aliongeza kuwa wazee ni tunu ya taifa na hivyo hawana budi kuenziwa kwa serikali kuhakikisha kuwa wanatambuliwa na kupatiwa vitambulisho vitakavyowawezesha kupata huduma muhimu kama vile afya.



Kwa mujibu wa Waziri Jafo wazee wanaolengwa ni wale wa kuanzia miaka 60 ambapo inakadiriwa kuwa asilimia 75 ya wazee wote nchini wapo maeneo ya vijijini.


30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili

0
0
Hospitali ya Taifa Mhimbili (MNH) leo tarehe 28-05-2018 imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 200 vitakavyotumika kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya macho.

Msaada huo ambao unajumuisha kifaa maalum kinachotumika kupima uwezo wa kuona umetolewa na timu ya madaktari wa macho kutoka Japan ambao wamekuja MNH kwa ajili ya kambi maalum ya upasuaji wa macho.

Akikabidhi msaada huo Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida amesema kwa muda  mrefu Japan imekua ikishirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili katika masuala mbalimbali hivyo ujio wa madaktari hao unazidi kuimarisha ushirikiano wao, lakini pia watalaam wa pande zote mbili wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji MNH, Dkt. Julieth Magandi ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Prof.  Lawrence Museru amesema Japan na Muhimbili wamekua na ushirikiano  takribani miaka 11 sasa na kwamba wamekuwa wakipeleka watalaam wao MNH kwa ajili ya kufanya upasuaji wa macho wa kibingwa.

“Napenda kutoa shukrani za pekee kwa Ubalozi wa Japan kwa ushirikiano tuliokua nao katika nyanja tofauti, wenzetu wamekua wakileta watalaam hapa na tumekua tukifanya nao kazi na kuzidi kujengeana uwezo,” amesema Dkt. Magandi.

Kuhusu kambi ya upasuaji wa macho amesema kambi hiyo ya siku tatu  ambayo imeanza leo jumla ya wagonjwa 30 wenye tatizo la mtoto wa jicho watafanyiwa upasuaji.

Naye Daktari Bingwa wa upasuaji macho Neema Kanyaro amesema katika Kliniki ya macho Muhimbili wataalam huona wagonjwa 15 hadi 20 kwa siku ambao wanatatizo la mtoto wa jicho.

Amesema tatizo hilo ni kubwa hususani kwa watu wazima na lina chukua nafasi ya kwanza katika matatizo ya macho yanayosababisha upofu kwa asilimia kubwa. Hata hivyo tatizo hilo linatibika kwa asilimia 100.
 Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kushoto)  vifaa tiba-Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Julieth Magandi.Wengine ni Mkurungezi wa Hospitali ya Macho nchini Japan, Dkt. Takashi Yamasaki, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kojima nchini Japan, Dkt. Yoshihisa Kojima. Balozi huyo amekabidhi vifaa tiba kwa niaba ya timu ya madaktari wa Japan ambao wametoa msaada huo. Madaktari hao wameanza kambi ya siku tatu kwa ajili ya kufanya upasuaji wa mtoto wa jicho katika hospitali hiyo.
  Baadhi ya madaktari wakifuatilia tukio hilo leo tarehe 28-05-2018.
 Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo kwa uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Julieth Magandi na kushoto ni Mkurungezi wa Hospitali ya Macho nchini Japan, Dkt. Takashi Yamasaki.
 Baadhi ya madaktari wakifuatilia tukio hilo leo tarehe 28-05-2018.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ikiwamo timu ya madaktari kutoka Japan.

NBS Kukusanya Takwimu Kwa Njia ya Satelaiti na Vishikwambi

0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, Dodoma
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanzisha mfumo wa ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa ya kielektroniki kwa njia ya satelaiti  na Vishikwambi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Dodoma mrasimu ramani mwandamizi na msimamizi wa Sehemu ya mfumo wa Ukusanyaji na Usambazaji wa taarifa za Kijiografia (GIS) Benedict Mgambi amesema kuwa lengo la mfumo huo ni kuboresha ukusanyaji wa  taarifa na tafiti mbalimbali   kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Mgambi amesema kuwa teknolojia hii mpya imerahisisha kwa kiasi kikubwa ufanyaji kazi ikilinganishwa na taratibu zilizokuwa zikitumika awali.
“Awali tulikuwa tunatumia teknolojia ya duni ambapo mchakato wake ulihusisha watu wengi, gharama kubwa ila kwa sasa hivi kila kitu kinafanyika eneo husika la tafiti na kutumwa moja kwa moja makao makuu” amesema Mgambi
Aidha Mgambi amesema kuwa zoezi hilo limeshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo, TAMISEMI, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Wizara ya Maliasili na utalii pamoja na TAMISEMI.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Masuala ya Kijiografia (NBS) Martha Macha amesema kuwa mfumo huo umerahisisha utendaji kazi wao kwani unasaidia kutambua mipaka mbalimbali kati ya kitongoji kimoja na kingine.
“Vifaa hivi vinafanya kazi kubwa kwa muda mfupi na pia vinafanya kazi kwa ubora ule unaohitajika kwa kuona vielelezo mbalimbali vitakavyokuwezesha kufanya kazi kwa urahisi” amefafanu Bi. Macha.
Mpaka sasa vijii vitano vya Sasajila, Suli, Fufu, Champumba na Chiboli Wilaya ya Chamwino Mkoa wa Dodoma vimefanyiwa majaribio ya mfumo huo.
Mrasimu ramani Mwandamizi   kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Benedict Mgambi akieleza kwa waandishi wa habari  faida za kutumia mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia  wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.
Mtaalamu wa masuala ya Jiografia kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Matha Macha  akitoa maelezo kuhusu namna mfumo huo unavyofanya kazi.
Mrasimu ramani msaidizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Rahim  Mussa  akisisitiza kuhusu namna mfumo huo unavyochochea maendeleo.
Mrasimu ramani Mwandamizi   kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Benedict Mgambi  akiongoza ujumbe kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutembelea  kijiji cha  Sasa Wilaya ya Chamwino ambapo  ujumbe huo umeambatana na waandishi wa habari kujionea mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia  wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa.
Mwenyekiti   wa  kijiji cha  Sasa Wilaya ya Chamwino ambapo ni ujumbe wa NBS  na waandishi wa habari walitembelea  kujionea jinsi  mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za kijiografia  wakati wa ziara yao iliyonga kujionea jinsi Ofisi ya hiyo inavyotekeleza majukumu yake katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ikiwemo sense na tafiti zinazofanywa kwa kutumia mfumo huo wa kisasa. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

RC DKT. KEBWE ATAKA WANAFUNZI WOTE WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KUPATIWA CHAKULA MASHULENI

0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo. 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ameuagiza uongozi wa wilaya ya Gairo na mkoa wetu kwa ujumla kuhakikisha wanafunzi wa shule msingi mpaka sekondani wanapatiwa chakula mashuleni. Kauli hiyo ameitoa wishoni mwa wiki iliyopita wakati akiwa katika Ufunguzi wa madarasa ya shule ya sekondari Chagongwe katika ziara yake kwa siku ya tatu Wilayani Gairo kukagua miradi ya maendeleo.

 Ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Gairo kujiwekea mpango kazi ili kuwawezesha watoto wote kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari wanapatiwa chakula cha mchana na kuwawezesha waweze kufanya vizuri katika masomo yao. 

"Watoto wa shule za Morogoro kutokula chakula mashuleni ni aibu, sitaki kabisa kusikia hili suala watoto kunyimwa chakula, naomba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo, upitishe azimio kwenye baraza na shule ambayo hawatatoa chakula shuleni wachukuliwe hatua uongozi wa eneo hilo," amesema Dkt. Kebwe.

 "Mkoa wetu unaongozwa kwa uzalishaji wa chakula cha kutosha sasa inakuwaje watoto wetu tuwanyime chakula, tutakosa matokeo mazuri," amesema.Aidha amesema kuwa mtoto anatakiwa kula chakula mara mbili ya mtu mzima, unapomnyima chakula hata ukuaji wake unakuwa hafifu... "Ubongo unatakiwa kupata chakula gram 6 za grucose" Amesema kuwa kukosekana kwa chakula shuleni kumekuwa kukichangia matokeo mabaya kwa wanafunzi bila kujali ni shule ya msingi au sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akifungua majengo ya shule ya Chagongwe wakati wa ziaya yake ya kukagua miradi ya maendeleo. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG-Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwa na mkuu wa wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe  (wa pili kushoto) wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kumaliza ufunguzi wa majengo ya shule ya sekondari Chagongwe.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Chagongwe waliojitokeza kumpokea wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Gairo na vitongoji vyake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye kofia nyeupe) akikagua vyoo vya hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nongwe.


KAMISHNA MSAIDIZI WA ARDHI KANDA YA MAGHARIBI AKUTANA NA WATENDAJI WA KATA MANISPAA YA TABORA

0
0

Na Munir Shemwea, Tabora
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharibi Idrisa Keyera amesema manispaa ya Tabora pekee inadai zaidi ya shilingi bilioni sita kwa wamiliki wa ardhi na mashamba mkoani humo kama kodi ya ardhi. 
Kayera alisema hayo jana wakati akizungumza na watendaji kata wa Manispaa ya Tabora alipokutana na watendaji hao kuhamasisha ulipaji wa kodi ya ardhi na mashamba katika mkoa huo, mkutano uliofanyika ukumbi wa VETA Tabora.
Alisema, mpaka kufikia sasa katika manispaa ya Tabora zimekusanywa jumla ya shilingi bilioni 3.2 ikiwa ni pungufu ya malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi bilioni nne katika mwaka huu wa fedha unaoishia juni mwaka 2018.
Alisema, kanda yake inayohusisha mikoa ya Tabora, Shinyanga, Kigoma na Katavi imeanza kuchukua hatua kwa wadaiwa sugu wa kodi za ardhi kwa kuwapatia hati za madai ambapo wahusika watatakiwa kulipa madeni yao ndani ya wiki mbili na wasipofanya hivyo wanapelekwa mahakamani na huko vifaa vyao au nyumba zitauzwa kufidia deni huku umiliki nyumba ama shamba ukifutwa.
‘’Unapopelekwa mahakamani uwezekano wa kushinda haupo na pia itakulazimu kulipa gharama za madadlali kwa kushindwa kulipa’’ alisema Kamishana Msaidizi Kayera.
Kwa mujibu wa Kayera, kikao chake na watendaji wa kata za manispaa ya Tabora ni moja ya harakati za ofisi yake ya Kanda ya magharibi kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana sambamba na kuwashirikisha watendaji kuwatambua na kuwapelekea hati za madai wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi katika mitaa yao ili kuwabana waweze kulipa madeni yao.
Aidha, Kamishna Msaidizi wa ardhi Kanda ya Magharibi alisema, utaratibu wa kulipa kodi ya ardhi kwa sasa ni rahisi kwani unaweza kulipia kwa njia ya simu na malipo hayo yanafanywa na wananchi waliopimiwa maeneo yao ingawa serikali iko katika hatua za kuhakikisha maeneo yote ya mijini hata yale yasiyopimwa wamiliki wake wanalipa kodi ya ardhi.

Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharibi Idrisa Kayera akizungumza na watendaji wa Kata za Manispaa ya Tabora jana wakati wa kampeni ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya ardhi katika kanda hiyo mkoani Tabora, kampeni inayoendeshwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushoto ni Mwanasheria wa Kanda Ramadhani Jongo.

Watendaji wa Kata za Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda ya Magharibi Idrisa Kayera (hayupo pichani) wakati wa kampeni ya kuhamasisha ulipaji kodi ya ardhi katika kanda ya magharibi mkoani Tabora, kampeni inayoendeshwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Mmoja wa watendaji wa kata  za Manispaa ya Tabora akichangia maoni wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa kulipa kodi ya ardhi kanda ya magharibi ulioendeshwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Jamii yatambua umuhimu wa mwanamke kumiliki Ardhi

0
0
Jamii kwa sasa imeanza kutambua na kuthamini haki za mwanamke kwenye masuala ya umiliki wa ardhi na hivyo kumpa nafasi zaidi kisheria kupata, kumiliki, kutumia na kugawa ardhi kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwa wanaume. 

Kuwepo kwa mabadiliko haya chanya kwa baadhi ya jamii imetokana na kusambaa kwa elimu ambayo imekuwa ikitolewa na Shirika la PELUM Tanzania kupitia mradi wa Ushiriki wa wananchi katika kusimamia sekta ya kilimo unaofadhiliwa na watu wa marekani. 

Angolile Rayson ambaye ni Afisa Mradi amesema vijiji vyote 30 vya mradi ambavyo 27 kati yake toka wilaya sita za Morogoro, Mvomero, Kilolo, Mufundi, Bahi na Kongwa vimefanyiwa mpango wa matumizi ya ardhi, wananachi wake walikuwa wakiendeleza mila na tamaduni potofu za kuona kuwa mwanamke si sehemu ya familia hivyo hapaswi kumiliki ardhi kwani ataolewa na kwenda kuendeleza ukoo mwingine. 

Lakini baada ya kufanya mafunzo kwenye vijiji hivyo juu ya haki za mwanamke kumiliki ardhi, jamii imebadilika na sasa mwanamke si tu amekuwa akimilikishwa ardhi peke yake bali pia ana maamuzi nayo kisheria kuitumia kwa shughuli zozote za kiuchumi, kukodisha na hata akiamua kuiuza. 

“Tunashukuru baada ya kutoa elimu juu ya haki za mwanamke kumiliki ardhi wakati wa kutekeleza mpango wa matumizi ya ardhi, wanaume wengi wamewapa wenza wao maeneo wamiliki kwa majina yao wenyewe na wengine wamemiliki umiliki wa pamoja yaani mke na mume na zaidi ya yote hata watoto wa kike kwenye baadhi ya familia wamepewa maeneo na wazazi wao wamiliki. Shirika kupitia Hamlashauri za wilaya husika tumewapimia maeneo yao na kwa sasa wanasubiri hatimiliki za kimila ili wawe na umiliki halali jambo ambalo sisi kama Shirika tumeona ni sehemu kubwa ya mafanikio.” Alifafanua Angolile 
Wananchi wa Kijiji cha Mawala, Wilaya ya Kilolo Iringa, wakisaidia kutekeleza baadhi ya shughuli za mpango wa matumzi ya ardhi ya kijiji chao.
Bahati Mwinyimvua mwananchi toka kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero Morogoro. Akichangia hoja kuhusiana na umiliki wa ardhi kwa wanawake
Ng’eng’enu Mambega katibu wa kamati ya maamuzi kijiji cha Mela, wilaya ya Mvomero Morogoro akibainisha jinsi elimu ya umiliki wa ardhi kwa wanawake ulivyosaidia kuwabadili kifikra na kuwapa wenza wao maeneo wayamiliki. 


Angolile Rayson Afisa mradi toka Shirika la PELUM Tanzania akichangia mada kuhusiana na mpango wa matumzi ya ardhi.

Wataalamu toka Halmashauri sita wapatiwa mafunzo ya mfumo rahisi wa upimaji ardhi.

0
0
Wataalamu 16 toka Halmashauri za Wilaya ya Morogoro, Mvomero, Bahi, Kongwa, Kilolo na Mufindi walio chini ya Idara ya Ardhi, maliasili na mazingira wamejengewa uwezo juu ya utumiaji wa mfumo mpya na rahisi wa upimaji ardhi unaofahamika kwa jina la MAST (Mobile Application for secure tenure).

Akiongea Mkoani Iringa wakati wa ufunguzi wa ziara hiyo ya mafunzo iliyoandaliwa na Shirika la PELUM Tanzania, Donati Senzia Mratibu wa PELUM alisema lengo hasa la ziara hiyo ni kuwapatia elimu wataalamu hao na kuona ni jinsi gani wataweza kuutumia mfumo huo kwenye Halmashauri zao kupitia miradi ya upimaji ardhi ambayo watakuwa nayo. 

Akifafanua jinsi mfumo huo unavyofanya kazi, Mustapha Issa ambaye ni Mkurugenzi msimamizi wa shughuli za miradi USAID LTA-Iringa, alisema kuwa mfumo huu ulitengenezwa kwa ajili ya uhakiki wa maslahi na upimaji wa vipande vya ardhi ambao hutumia simu za kisasa. 

Alisema mbali na kuwa mfumo huu kutoa ajira kwa vijana wengi kama wapimaji wasaidizi baada ya kupatiwa mafunzo jinsi ya kuutumia lakini pia mfumo huu ni rahisi na hautumii muda mwingi kuanzia kwenye zoezi la upimaji, uchukuaji taarifa, utunzaji taarifa hadi kufikia hatua ya kutoa hatimiliki. 

Halikadhalika mchoro unajichora wenyewe moja kwa moja wakati wa upimaji kipande, upigaji wa picha hufanyika na kuhifadhiwa kwenye mfumo mara tu baada ya mpimaji kujiridhisha na taarifa ya mteja wake na wakati huohuo taariza zote za mmiliki wa kipande husika zinachukuliwa na kuhifadhiwa na mfumo kwa ajili ya kukamilisha zoezi la utoaji wa hatimiliki. 
Mustapha Issa  Mkurugenzi msimamizi wa shughuli za miradi USAID LTA-Iringa, akielezea jinsi mfumo wa MAST unaotumia simu za kisasa  unavyofanya kazi wakati wa upimaji wa vipande vya ardhi.
   Sadoth Kyaruzi Afisa Mpango miji na vijiji halmashauri ya Mvomero, Morogoro akichangia jambo wakati wa mafunzo ya MAST.
 Timu ya wataalamu toka Halmashauri za wilaya sita, Morogoro, Mvomero, Kilolo, Mufindi, Bahi na Kongwa. Wawakilishi toka masharika wanachama (INADES na UMADEP) pamoja na maafisa mradi wa PELUM Tanzania wakipewa maelezo na mmoja wa vijana waliopewa mafunzo juu ya utumiaji wa mfumo wa MAST.
 Timu ikichukua alama za shamba la mwananchi (wakiongozwa na mmiliki wa shamba) ili kuweza kupata mchoro kamili na ukubwa wa shamba husika.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: Benki ya CRDB yapunguza riba hadi 16% na kuongeza muda wa kulipa mkopo ...

KIJANA WA MALI ALIYEMWOKOA MTOTO AKUTANA NA RAIS WA UFARANSA, APATA DONGE NONO

0
0
 Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KIJANA raia wa nchini Mali, Mamoudou Gassam (22) ambaye Jumamosi iliyopita amefanya kitendo cha kishujaa cha kumuokoa mtoto mdogo aliyetaka kudondoka kutoka jengo la ghorofa ya nne, amekutana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kupatiwa zawadi nono.

Mamoudou amekutana na Rais Macron mapema leo kwenye Ikulu ya Elysee Palace kwa ajili ya kufanya mazungumzo pamoja na kupongezwa kwa msaada alioutoa.


Rais Macron amempatia cheti cha Uraia wa Ufaransa kijana huyo ambaye alihamia nchini hapo kwa njia zisizokuwa za kihalali takribani miezi miwili iliyopita kwa ajili ya kutafuta maisha. Lakini pia Rais Macron amempatia kazi Mamoudou katika jeshi la zima moto la Ufaransa.


Kupitia mtandao wa Twitter Rais Macron ameweka picha akiwa Ikulu na kijana Mamoudou na kuandika, “With Mr. GASSAMA who saved Saturday the life of a child climbing 4 floors with bare hands. I announced to him that in recognition of this heroic act he would be regularized as soon as possible, and that the brigade of the firemen of Paris was ready to receive it.”



Kijana huyo ameeleza kuwa alikuwa akipita tu mtaani ndipo alipoona umati wa watu umekusanyika mbele ya jengo.

"Nilijitolea kwa sababu alikuwa ni mtoto," gazeti la Le Parisien lilimnukuu akisema . "Nilikwea jengo... Namshukuru Mungu nilimuokoa." Mamoudou

Wahudumu wa kampuni ya zima moto jijini Paris walifika eneo la tukio na kupata tayari mtoto ameokolewa.

"Kwa bahati nzuri kulikuwa na mtu mwenye nguvu za mwili na mwenye ujasiri wa kwenda na kumchukua mtoto," waokozi wa zima moto walilieleza  shirika la habari la AFP.

Maofisa wa eneo hilo walionukuliwa na vyombo vya habari vya Ufaransa wakieleza kuwa wazazi wa mtoto huyo hawakuwa nyumbani wakati akiokolewa.

aidha baba yake amekuwa akihojiwa na polisi kwa  kushukiwa kumuacha mwanae bila mtu wa kumuangalia, zimeeleza taarifa za mahakama.

RAIS NA MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AONGONZA MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
  Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakishangilia baada ya kuwaita  Ndg. Mizengo Pinda na Ndg. Makongoro Nyerere waingie ukumbini baada ya kukubaliwa kuwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
 Wajumbe wakishangilia baada ya  Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli kuwaita  Ndg. Mizengo Pinda na Ndg. Makongoro Nyerere waingie ukumbini baada ya kukubaliwa kuwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
 ais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli   akiongoza  Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Katika ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Jumatatu Mei 28, 2018
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein akipendekeza majina ya wanachama wa CCM kutoka visiwani wataopigiwa kura kuwa wajumbe Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukumbi wa Kikwete leo Jumatatu Mei 28, 2018 
Picha na IKULU.

BREAKING NEWZZZZ: CCM YARIDHIA KINANA KUSTAAFU U-KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO LEO

0
0

*Asema anatambua juhudi zake na mchango wake, 
pia ametambua umri wake
*Kinana ashukuru kukubaliwa na Rais, aeleza 
Mangulla alivyojitoa mhanga
ugumu wanaupata

Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Rais Dk.John Magufuli amesema ametafakari kwa kina na kuamua kuridhia kung'atuka kwa Katibu Mkuu  wa Chama hicho Abdulrhaman Kinana lakini hadi atakapomaliza muda wake ndipo atapumzika.

Dk.Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na Wajumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa kwenye kikao kilichofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema anatambua juhudi kubwa ambazo zimefanywa na Katibu MKuu wao.

"Ni zaidi ya mara mbili Katibu Mkuu wetu ameomba kumpuzika lakini nikawa namkatalia na hata alipokuwa anaanzisha hoja hiyo kisiri siri mimi nilikuwa naanzisha pointi nyingine.

"Lakini nieleze tu natambua juhudi kubwa ambazo amefanya.Lakini pia nikatambua kuna makatibu wakuu wengi wamekitumikia chama chetu na wengi tu maana walikuwepo hata kabla mimi kuanza shule ya msingi.

"Natambua umri alionao Katibu Mkuu wetu.Hivyo  nilimuita mzee Shein(Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) nikamueleza akaniambia mruhusu akapumzike,nikamuita mzee Mkapa naye mkubalie.Hivyo nimekubalia acha akampumzike,"amesema.

Pia amesema jana alimuita Katibu Mkuu Kinana na wakazungumza akimini huenda atabadili mawazo yake lakini bado akabaki na mawazo."Hivyo nimemkubalia akapimzike lakini atapumzika baada ya kumaliza muda wake,"amefafanua Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Magufuli.

KINANA ASHUKURU KUKUBALIWA KUPUMZIKA

Wakati huo huo Katibu Mkuu Kinana  amesema kuna wakati wa kufanya kazi na wakati wa kupumzika na anaelewa ugumu ambao CCM wanaupata wa kutomkubalia.

"Naangalia nyuso zenu zinaonesha namna ambavyo hampo tayari kunikubalia lakini Mwenyekiti wetu amesema tumewahi kuwa na makatibu wakuu wengi na kweli tumekuwa na makatibu wakuu saba kabla yangu. Hivyo nakushukuru Mwenyekiti kwa kunikubalia, nashukuru Makamu Mwenyekiti  kwa kunikubalia na  nashukuru mzee Mangula kwa kunikubalia.

"Nakumbua kuna siku Mwenyekiti alikuja pale Lumumba na uliamua kujitoa mhanga kwani alipokuuliza kuhusu kupumzika ulimwambia anikubalie.Mwenyekiti kama alikukasirikia hivi lakini nashukuru sana maana ulinisaidia na ulijitoa mhanga,"amesema Kinana.


Amesema amekitumikia Chama hicho kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 30 lakini kwa kipind cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2013 alijitolea sana ndani ya CCM lakini hatimaye anashukuru kwa kukubaliwa kwa ombi lake na Mwenyekiti wao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akisoma barua ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia) ya kumuomba kujiuzuru nafasi hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia)  akisema machache ya kushukuru baada ya  barua yake ya  kuomba kujiuzuru nafasi hiyo kukubaliwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli  na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018

 Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia)  akisema machache ya kushukuru baada ya  kuwasilisha barua yake ya  kuomba kujiuzuru nafasi hiyo kukubaliwa mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli  na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli,  baada ya kumkubalia, akimshukuru na kumwombea kila la heri Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana (kulia)  baada ya kusoma barua yake ya  kuomba kujiuzuru nafasi hiyo mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) iliyokutana ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam leo Mei 28, 2018.

OFISA UTUMISHI TRA AIELEZEA MAHAKAMA KUWA MALI ALIZOJAZA MSHTAKIWA NI ZA FAMILIA NA ZINA UMILIKI WA NUSU KWA NUSU

0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

OFISA Utumishi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Evans Emil (53) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mali ambazo alijaza mshtakiwa Jenifa Mushi kwenye fomu za rasirimali na madeni ni za familia ambapo amedai mali nyingi zilizojazwa kwenye fomu hizo, zina umiliki wa nusu kwa nusu mshtakiwa na mkewe na watoto wao.

Evans ambaye ni shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka amedai hayo wakati akitoa ushahidi katika kesi inayomkabili, Aisa Msaidizi wa Forodha Wa  (TRA), Jennifer Mushi ya  kukutwa akimiliki magari 19 mali ambayo hailingani na kipato chake,

Akitoa ushahidi wake leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Shaidi huyo alidai, yeye aliajiliwa TRA mwaka 1996 akiwa na majukumu ya kushughulikia ajira, kusimamia nidhamu, maslahi ya wafanyakazi, utawala na majukumu mengine atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

Alidai taratibu moja wapo kwa mtu ambaye atakuwa ameajiriwa na kuthibitishwa pamoja na mambo mengine anatakiwa kujaza fomu ya tamko ya rasilimari na madeni  ambazo anatakiwa kuijaza kila mwaka wa kalenda na isizidi ndani ya miezi mitatu.

Alidai,  fomu hizo ujazwa chini ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma na kanuni ya utumishi ya TRA pale mtumishi anapoajiriwa na kuripoti kazini.

Amedai, lengo kubwa la kujaza fomu hiyo ni kujua mali na madeni ya mfanyakazi na kufahamu uadilifu wa mtumishi, kutokana na mazingira ya kazi ya TRA ikiwa ni kudhibiti vitendo vya rushwa na kujilimbikizia mali.

VIDEO: HUU NDIO MSINGI NA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA TAIFA - DKT ABBASI

TPA TANGA YAJIVUNIA KASI YA UTOAJI HUDUMA

0
0
MENEJA wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama amesema wanajivunia kuboreshwa huduma zao kwa kiwango kikubwa ikiwemo uandaaji wa nyaraka kwa kasi na usalama wa kutosha kwa wateja na hivyo kutumia muda mfupi kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja.

Salama aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea maonyesho ya kimataifa ya sita ya biashara ambapo alisema kutokana na hali hiyo hakuna sehemu ambayo mteja anaweza kupita akikwama bila wao kujua mara kila hatua wanazokuwa wakipitia wanatambua mara moja.

Alisema kuwa sehemu ambazo mteja anaingia kwenye bandari hiyo anapata taarifa moja kwa moja hiyo ikiwa wanakumbana na vikwazo vya namna yoyote zikijitokeza inawawia rahisi kuweza kuona na kuvishughulia kwa muda mfupi ili kuweza kuondoa usumbufu ambazo unaweza kuwakabili wafanyabiashara.

“Kwa kweli huduma za bandari ya Tanga tumeziboresha kwa kiasi kikubwa kutokana na kasi ya uandaaji wa nyaraka lakini hata usalama wa kutosha kwa wateja ambao wamekuwa wakiitumia hali iliyofanya kutumia muda mfupi kutokana na taasisi zinazohusika kuwepo sehemu moja hivyo kuwawia rahisi kuweza kufanya shughuli zao kwa wakati mmoja “Alisema.
 MENEJA wa Bandari ya Tanga (TPA) Percival Salama kulia akimueleza Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Charles Mwijage  mipango ya bandari hiyo na namna walivyoboresha huduma zao kwa wafanyabiashara wanayoitumia
 Waziri wa Viwanda, Biashara  na Uwekezaji Charles Mwijage akisalimia na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga alipokwenda kufungua maonyesho ya sita ya biashara ya kimataifa

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kushoto akisisitiza jambo kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya kufungua maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DKT ABBASI: HUU NDIO MSINGI NA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA TAIFA.

MOJA YA HOTUBA YA ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA CCM KATIKA MKUTANO WA HADHARA MJINI TABORA

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images