Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

DAWA ZAVUSHWA KUPITIA MTO WENYE MAMBA MKOANI RUVUMA

$
0
0

Na Dotto Mwaibale, Ruvuma

WANANCHI wanaoishi katika Vijiji vya Mkenda na Mitomoni vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wamesema changamoto kubwa waliyonayo ni mazingira magumu ya miundo mbinu ambayo inasababisha ugumu wa ufikishaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutoka Bohari ya Dawa (MSD).

Wakazi hao wamesema kuwa, mazingira ya kufikisha dawa kwenye vijiji hivyo hutegemea zaidi usafiri wa kuvuka mto Ruvuma ambapo hulazimika kutumia boti,ambapo hata hivyo maisha yao yanakuwa na mashaka ndani ya mtumbwi hiyo ambayo iko wazi kutokana na mto huo kuwa na mamba wengi.

"Changamoto yetu kubwa ni usafishaji wa dawa kuja hapa kijijini kutokana na kutegemea zaidi mto huu ambao una mamba wengi, hata mwaka huu mwanzoni mtumbwi huu mnaouona ulipinduka na watu wakiwapo wauza mitumba waliuawa na mamba; lakini tunashukuru Bohari ya Dawa (MSD) kwani wao wanaweza kutuletea dawa kwa wakati" alisema Mwenyekiti wa kamati ya Afya wa kijiji cha Mitomoni Omar Hassan.

Alisema ili kuondoa changamoto hiyo, wanaiomba serikali kuhakikisha inaboresha miundombinu ya barabara, ili dawa hizo zisafirishwe kwa njia ya barabara badala ya kutegemea mto huo. Alisema yeye na kamati yake wamekuwa wakipokea dawa mara nne kwa mwaka kutoka MSD na kuzihakiki kwa ajili ya matumizi.

"Pamoja na changamoto ya miundombinu lakini tumekuwa tukihakikisha dawa zinazoletwa na MSD zinafika kituoni na kutumika ipasavyo,"alisema.Alisema kutoka Songea mjini hadi Kijiji cha Mitomoni, Songea vijijini, katika kituo hicho cha afya ni km 135 na MSD imekuwa ikihakikisha dawa hizo zinafika.
Wakazi wa vijiji vilivyopo kandokando ya mto Ruvuma wilayani Nyasa mkoani Ruvuma na wafanyakazi wa Bobari ya Dawa (MSD), wakisaidia kushusha maboksi yenye dawa na kuyaingiza kwenye mtumbwi baada ya kupelekewa na MSD Kanda ya Iringa leo na baadae kuyapeleka katika Zahanati ya Kijiji cha Mitomoni.
Maboksi ya dawa yakiingizwa kwenye mtumbwi.
Wakazi wa Kijiji cha Mitomoni wakisubiri mtumbwi ili kuwavusha upande wa pili wa mto Ruvuma.
Dawa zikipelekwa Zahanati ya Mitomoni.


WIZARA YA AFYA YAWAONYA WANAOTOA HUDUMA ZA KIMAABARA BILA VIBALI

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jami, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka watoa huduma za kimaabara kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa na vibali, kwani kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo , Mkurugenzi Msaidizi Huduma ya uchunguzi na magonjwa Dk. Charles Massambu amesisitiza sheria itachukua mkondo wake kwa wale wanaohudumia wananchi shughuli za kimaabara lakini hawana vibali au kusajiliwa.

"Hakuna mtoa huduma atakaetoa huduma za maabara bila kusajiliwa.Tukibaini tutamchukulia hatua kali za kisheria," amesema Dkt. Massambu.

Aidha Massambu ameeleza baraza linatambua uwezo na utaalamu katika kuelimisha jamii ya watanzania kuhusu majukumu katika kuwahudumia.Pia kutokana na changamoto za majibu ya vipimo kutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine , Wizara imechukua hatua ya uhakiki wa ubora wa vipimo.

"Tanzania kuna maabara 33 ambazo ni nyota moja mpaka nne,nyingine nane zilizo na hadhi ya kimataifa ambapo vipimo vyake huwa ni sawa na vya nchi nyingine za nje.
 Mkurugenzi msaidizi wa huduma za uchunguzi wa Magonjwa Dkt Charles G Massambu akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam akiwataka watoa huduma ya maabara wasio na vibali kutoka baraza la wataalamu la maabara  kujisajili au kuacha kufanya kazi hiyo.
 Msajili wa Baraza la wataalamu wa maabara akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam akielezea kuhusu umuhimu wa kusajili huduma hizo.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CHAMA CHA MAPINDUZI KUENDELEZA UHUSIANO NA MSHIKAMANO WAKE KWA VYAMA RAFIKI

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akimkabidhi Rais wa Chama Cha Ukumbozi wa Afrika Kusini (ANC) Rais wa Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa barua maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli, Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg, jana. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu Mkuu wa ANC Ace Magashule Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Rais wa ANC Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Makao Makuu ya ANC Jijini Johanesburg, jana. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Gaudentia Kabaka. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa ANC Gwede Mantashe, Makao Makuu ya ANC Jijini Johanesburg. 
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa ANC, Makao Makuu ya ANC jijini Johanesburg. Katika ziara hiyo ambao Kinana ameambatana na Wenyeviti wa Jumuiya za Chama cha Mapinduzi, ikiwa na lengo la kuendeleza uhusiano na mshikamano uliopo baina ya Vyama hivyo. 

UN WATOA ELIMU YA MALENGO YA DUNIA KWA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa (UN) kwa kushirikiana na Shirika la Seed Trust wameanzisha timu ya vijana 20 wenye ulemavu wa aina mbalimbali kutoka vyuo sita vya elimu ya juu nchini.

Lengo la timu hiyo ni kufanya ushawishi na utetezi kwa wanafunzi wenye ulemavu ili kuwajengea uwezo wa kusaidia maendeleo endelevu ya kidunia.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari inaelezea kupitia mafunzo hayo ambayo yameshirikisha wanavyuo walemavu kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini yanatoa nafasi ya kundi la watu wenye ulemavu kushirikishwa katika utekelezaji wa mwaka wa pili wa elimu ya malengo endelevu ya dunia yanayosema hakuna binadamu yeyote atakaye achwa nyuma.

Pia katika mafunzo hayo Umoja wa Mataifa umetoa machapisho maalum takribani 1000 yaliyoandikwa kwa lugha ya alama yatakayowezesha watu wenye ulemavu wa macho kusoma na kuelewa mipango ya maendeleo endelevu ya kidunia.

Hivyo katika kutekeleza malengo hayo vijana hao watafundishwa pamoja na kuzunguka kuhamasisha malengo hayo kwa walemavu wengine katika vipaumbele mbalimbali ikiwemo elimu na afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
 Mkuu wa mawasiliano kutoka Umoja wa Mataifa Hoyce Temu akiongea na waandishi wa habari na kufafanua baadhi ya mambo  baada ya kikao cha mafunzo kwa vijana  20 wenye ulemavu uliofanyika mkoani  Morogoro.
 Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Seed Trust Magreth Nkanga, ambaye pia ni mbunge mstaafu aliyekuwa akiwakilisha kundi la walemavu akishukuru un kwa kutoa machapisho maalum takribani 1000 yaliyoandikwa kwa lugha ya alama, yakihusu mkakati ya elimu ya malengo endelevu ya dunia.
 Kijana mwenye ulemavu wa macho Godbless Muro, mwanafunzi wa Shahada ya sayansi ya siasa na utawala, Chuo kikuu cha Dodoma akisoma moja ya chapisho iliyoandikwa kwa maandishi ya nundunundu yenye ujumbe wa maendeleo endelevu ya kidunia.
 Vijana mbalimbali wenye ulemavu sambamba na waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini wakati wakikao cha utoaji elimu ya malengo endelevu ya dunia kilichofanyika mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa bodi ya shirika la Seed Trust kushoto Steven Mashishanga akimkabidhi katibu tawala msaidizi, mkoa wa Morogoro Ernest Mkongo moja ya chapisho maalumu kwa watu wenye ulemavu la mpango wa elimu ya maeneleo ya dunia, katikati Mkuu wa mawasiliano kutoka Umoja wa Mataifa Hoyce Temu.

Mtanzania Ateuliwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Mazingira

$
0
0

Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Antonio Guterres ametangaza uteuzi wa Bi.Joyce Msuya kutoka Tanzania kuwa naibu katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia program ya mazingira yenye makao makuu yake Nairobi nchini Kenya.


Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa mataifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo tarehe 22 Mei, Bi Msuya anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Bw.Ibrahim Thiaw wa Mauritania aliyemaliza muda wake ambaye katibu Mkuu wa umoja wa mataifa amemuelezea kuwa na utumishi uliotukuka katika kipindi chake cha uongozi.


Bi.Joyce Msuya amekua akifanya kazi kama mshauri wa makamu wa rais wa benki ya dunia anayeshughulikia nchi za Asia Mashariki pamoja na ukanda wa Pasifiki tangu mwaka 2017, makao makuu ya benki ya Dunia Washington D.C Marekani.


Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi.Msuya atatumia muzoefu wake wa miaka 20 katika benki ya Dunia, pamoja na uzoefu wake katika masuala ya maendeleo ya kimataifa katika kazi yake mpya na anaimani kuwa ataleta mabadiliko makubwa katika umoja wa mataifa.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo Bi.Msuya amewahi kufanya kazi kama mwakilishi maalum wa benki ya Dunia na mkuu wa kundi la benki ya dunia nchini Korea ya kusini,pamoja na mratibu wa taasisi ya benki ya dunia katika Asia Mashariki na ukanda wa Pasifiki ofisi iliyoko China, na ameahi kuwa na nafasi mbalimbali za juu katika benki ya dunia na washirika wake.


Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa Bi.Joyce Msuya ana Shahada ya uzamili ya Maikrobailojia na kinga kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada pamoja na shahada ya Baiokemia kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde,Scotland.


Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira ni mpango wa kidunia wa mazingira unaolenga kutoa mwelekeo katika uongozi na usimamizi wa mazingira, na kuwashauri wadau na nchi wanachama kwa ujumla njia sahihi za kutunza na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira inafanya kazi na serikali,mashirika na asasi za kimataifa duniani kote. 

Riadha Tanzania wampongeza Mkurugenzi mpya MultiChoice

$
0
0
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limempongeza Mkurugenzi wa MultiChoice Tanzania, Maharage Chande kwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa MultiChoice Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Mei 20 mwaka huu, Kampuni ya MultiChoice Africa Limited, ilithibitisha uteuzi wa Wakurugenzi wawili, ambako Mtanzania Maharage Chande ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, anakuwa Mkurugenzi mpya wa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Uteuzi huo uliotangazwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa, Brand de Villiers, unabainisha kuwa Maharage anachukua nafasi ya Stephen Isaboke aliyekuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki ambaye sasa anakuwa Mkuu wa Mamlaka (Group Executive Head of Regulatory). Uteuzi ambao unaanza Juni Mosi mwaka huu.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa, Brand de Villiers, amesema uteuzi wa Maharage umezingatia uwezo na upeo wake mkubwa aliyouonyesha katika kipindi alipoiongoza MultiChoice Tanzania tangu alipojiunga nayo Juni 2016.

Rais wa RT, Anthony Mtaka, amesema familia ya Riadha Tanzania imepokea kwa furaha uteuzi huo wa Maharage, hasa ukizingatia katika uongozi wake, MultiChoice Tanzania kupitia DStv, imekuwa mshirika mkubwa katika kuchangia maendeleo ya mchezo wa Riadha hapa nchini.

“Sisi kama Riadha Tanzania, tumepokea kwa faraja kubwa kupanda kwa cheo kwa Mtanzania mwenzetu Maharage Chande, hakika tutamkumbuka kwa mengi katika kusapoti maendeleo ya Riadha hapa nchini….Tunamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya na bila shaka mapenzi yake katika mchezo wa Riadha atayaendeleza,” alisema Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

TANZANIA YAPIGIWA MFANO MATUMIZI BORA YA FEDHA ZA MAENDELEO ZA BENKI YA AfDB

$
0
0
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeitaja Tanzania kuwa moja ya nchi za Afrika zenye matumizi bora ya fedha zinazofadhiliwa na Benki hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya barabara na nishati.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayesimamia nchi 7 za Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro wakati  wa kikao  cha Magavana wa nchi za Afrika kwenye Mkutano wa  mwaka wa Benki ya AfDB unaoendelea Mjini Busan, Jamhuri ya Korea ya Kusini.

Dkt. Nyamajeje alisema kuwa changamoto nyingi zinazotokea katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa nchi  za Afrika zinatokana na  ukosefu wa  wataalamu wa fani mbalimbali, jambo linalosababisha miradi mingi  kutomalizika kwa wakati  hata hivyo Benki ya AfDB inaendelea kuangalia ni jinsi gani inaweza kusaidia kutatua matatizo hayo na kuleta maendeleo chanya kwa nchi za Afrika.

Akizungumza katika Mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Khamis Shaaban, alisema kuwa Serikali ya Tanzania imesawasilisha barua kwa uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ili iweze kusaidia katika ujenzi wa  Uwanja wa ndege ya Msalato Jijini Dodoma na Uwanja wa ndege wa Zanzibar,  aidha miradi hiyo ikiridhiwa na kutekelezwa  itakua kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi wa Viwanda nchini Tanzania.

Tanzania ni wadau wakubwa  katika Benki ya AfDB hivyo inanufaika na mikopo nafuu inayotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa Barabara  za kiwango cha Lami hususani mkoa wa Tabora na pia miradi ya  Nishati  ya umeme na maji maeneo mbalimbali nchini.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban(kushoto) akizungumza kwenye mkutano wa Magavana kutoka nchi za Afrika  kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini wakati wa Mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mjini Busan- Korea Kusini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (katikati) akiwa na baadhi ya Magavana wa nchi za Afrika, kushoto kwake ni  Gavana wa Kenya Mhe. Henry Kiplagat Rotich na kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB,  Dkt. Nyamajeje Weggoro baada ya kumaliza majadiliano yanayaozihusu nchi wanazoziwakilisha, Mjini Busan- Korea Kusini.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango-Korea)

FORMER BOT GOVERNOR WINS INTERNATIONAL ACCOLADE

$
0
0
Former Bank of Tanzania Governor Prof. Benno Ndulu is the winner of the 2018 African Bankers Central Bank Governor of the Year Award in recognition of his contribution to financial inclusion and increased access to banking services in Tanzania. This is the third such recognition for him. He also received such awards in 2009 and 2015.

Prof. Ndulu was honoured this evening at the ongoing annual meetings of the African Development Bank (AfDB) in Busan, South Korea. The Executive Director of the AfDB for the East Africa region, Dr. Namajeje Weggoro, received the award on behalf of the former Governor.

The award is being granted to me and through me the BoTI requested and organisers agreed that Dr. Namajeje Weggoro, the Executive Director at the AfDB for East Africa Constituency to receive this award on my behalf. I had not known then about BoT Deputy Governor Julian Banzi Raphael participation at the AfDB annual meetings, otherwise he could have on behalf, he said in a telephone interview in Dar es Salaam.

According to African Banker Group Publisher and Managing Director, Mr. Omar Ben Yedder, the magazines awards committee chose Prof. Ndulu from amongst his peers to be the winner of the African Banker Central Bank Governor of the Year Award.

Prof. Ndulu has been honoured in recognition of his considerable achievements during his term as Governor, most notably in championing financial inclusion and overseeing increased access to banking services for over 70 per cent of Tanzanias population.

 In this respect, you are a pioneer, both in Africa and globally. You have also been a frontrunner in terms of regulation and maintaining cautious oversight of the banking sector as a whole, as well as encouraging probity and best practice in the industry, he said in an invitation letter to the award winning ceremony.

The awards giving ceremony brought together key banking industry players and top government officials from Africa and around the world to honour the achievements of institutions and individuals who have contributed immensely to the reform, modernization and expansion of the continents banking and financial sector, whilst driving Africas sustained economic growth.

It is the third time Prof. Ndulu, is being recognized as the Best Central Bank Governor in Africa. The first time was in 2009, when he was awarded by Emerging Markets magazine during the Annual Meetings of the World Bank and International Monetary Fund in Istanbul, Turkey. 

Prof. Ndulu also won the 2015 Best Central Bank Governor in Africa award by the Africa Investor magazine. The award, which was in recognition of Prof. Ndulus competence and contribution in attracting investment and developing a hospitable environment for investment in Tanzania, was presented to him on the fringes of the United Nations General Assembly in New York, United States. 

Prof. Ndulu completed his 10-year tenure as Bank of Tanzania Governor in January 2018.

INTRODUCING New Hit Sebene " HAPA KAZI TU" by Ngoma Africa Band based in Germany

MKUTANO WA WADAU KATI YA SERIKALI, WAAJIRI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KUHUSU MASWALA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KUFANYIKA JIJINI MBEYA, MEI 26, 2018

Ilala Yaahidi Kudumishia Miradi ya Dar – Urban

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imeahidi kuendeleza na kudumisha miradi iliyoachwa na shirika la Plan International katika maeneo ya Buguruni na Vingunguti.

Ahadi hiyo imetolewa leo jijini humo na Katibu Tawala wa Halmashauri hiyo, Edward Mpogolo alipokuwa akifunga programu ijulikanayo kama Dar – Urban iliyoanzishwa na shirika hilo ambayo imedumu katika maeneo hayo kwa miaka 26.

Mpogolo amesema kuwa shirika hilo limefanya kazi nzuri tangu kuanzishwa kwa program hiyo kwani imeleta mapinduzi makubwa katika kuimarisha huduma muhimu kwa wananchi kwa kuboresha sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, afya na ujenzi wa miundo mbinu.

“Toka mwaka 1992 wamekuwa na sisi wakitusaidia kutuboreshea huduma mbalimbali na katika kipindi chote hicho wameweza kutujengea shule mbili za msingi, kutujengea kituo cha Afya cha Buguruni, kuwaelimisha na kuwainua vijana hivyo tunawaahidi kuisimamia na kuidumisha miradi yote waliotuachia”, alisema Mpogolo.

Mpogolo amefafanua kuwa baada ya shirika hilo kujenga shule mbili za msingi za Vingunguti na Buguruni Moto Mpya mnamo mwaka 2016 ufaulu uliongezeka kutoka asilimia 49 mpaka asilimia 98 pia tangu walipojenga kituo cha afya mnamo mwaka 2002 wagonjwa walikuwa 40 mpaka 50 kwa siku lakini kwa sasa kituo kinapokea wagonjwa kati ya 500 mpaka 600.

Vile vile katika kuelimisha vijana, Mpogolo amesema kuwa shirika hilo linajitahidi kuendana na Sera ya Serikali nchini ya kuwasaidia vijana ambapo wameweza kuelimisha vijana zaidi ya 2,000 na vijana hao wametumika kuwaelimisha wenzao zaidi ya 29,000 walioweza kujianzishia shughuli zao binafsi kwa ajili ya kujikimu. 

Saba Wafariki kwa kipindupindu Rukwa

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule amethibitisha kufariki kwa wagonjwa saba wa kipindupindu katika Wilaya ya Sumbawanga huku wagonjwa wengine 44 wakibaki wodini kuendelea kupatiwa matibabu na wagonjwa 115 wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

Amesema kuwa ugonjwa huo umelipuka tarehe 6 Mei, 2018 katika Kijiji cha Mayenje, kata ya Milepa katika bonde la ziwa Rukwa na kusambaa katika meneo mengine ya Wilaya na hatimae kupatikana kwa wagonjwa wawili katika hospitali ya rufaa ya mkoa.

“Sasa hivi katika bonde la ziwa Rukwa kuna shughuli za uvunaji wa mpunga na hivyo watu wengi hutokea huku juu kwenda bondeni kutafuta vibarua vya kuvuna mpunga kwenye maeneo hayo yaliyoathirika na kipindupindu, maji yanayotumika huko ni machafu kutoka katika madimbi na mito nawaomba viongozi wa dini watoe tahadhari kwa waumini hasa katika maeneo yale yalioathirika zaidi,” Alisema.

Alisema hayo alipopewa nafasi ya kutoa taarifa hiyo ya ugonjwa wa kipindupindu na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo wakati wa Mkutano uliowakutanisha wadau wa afya Mkoani hapa kwaajili ya kuzungumzia tahadhari ya ugonjwa wa Ebola uliopo katika nchi ya jirani ya Kongo.

Kwa upande wake Mh. Wangabo alisema kuwa elimu ya tahadhari itatolewa kwa wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara ya wakuu wa wilaya, madiwani pamoja na wakurugenzi ili ifikie hatua ya kusema “kipindupindu sasa basi”.

TAASISI YA HUMANITY ACTION FOR CHILDREN FOUNDATION YATOA VIFAA KWA WALEMAVU

$
0
0
 Mwanzilishi wa Taasisi ya Humanity Action For Children Foundation, Rahma Mohamed Abdallah akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa kwa makundi ya watu wenye ulemavu kwa mkoa wa Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya  Humanity Action For Children Foundation, Rashid Mchujuko akizungumza mara baada ya kukabidhi Vifaa kwa makundi ya watu wenye ulemavu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Mjumbe wa Bodi wa Taasisi ya  Humanity Action For Children Foundation, Haji Janguo akikabidhi Magongo ya kutembelea kwa watu wenye ulemavu wa viungo  wa mkoa wa Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Sabrina Semsimba  huku wajumbe wengine wakishuhudia 

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AWATEMBELEA WANANCHI JAMII YA WAHADZABE NA WATATOGA HUKO ESHKESH WILAYANI MBULU MKOA WA MANYARA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa jamii za Wahdzabe Watatoga na Wasukuma wakati alipotembelea Kata ya Eshkesh kijiji cha Dumanga Yaeda Chini wilayani Mbulu mkoa wa Manyara wakati alipozitembelea jamii hizo ili kuzungumza nao kuhusu maisha yao pamoja na uhifazi wa tamaduni na mila zao ambao unaweza kuwa Kivutio cha Utalii pia lakini pia kujua mahitaji yao ya muhimu katika maisha ya jamii hizo.(PICHA NA JOHN BUKUKU FULLSHANGWE-MBULU)
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa jamii za Wahdzabe Watatoga na Wasukuma wakati alipotembelea Kata ya Eshkesh kijiji cha Dumanga kutoka kulia ni Gesso Bajuta diwani wa kata ya Endamilay wilayani Mbulu., Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduzi Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Beleko na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga.
Wananchi wa Eshkesh Jamii ya Watatoga wakiwa katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akizungumza katika mkutano huo.

WAZIRI JAFO ALIVALIA NJUGA SUALA LA WATU WENYE ULEMAVU WAWEZE KUPATA FURSA ZA AJIRA PAMOJA NA KUPATIWA MATIBABU BURE

$
0
0
Na Victor  Masangu, Kisarawe
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa  (TAMISEMI)  Selemean Jafo amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya jamii kuwabagua na kuwanyanyasa  makundi ya watu  wenye ulemavu na  badala yake wabadilike na kuwashirikisha kikamilifu katika shughuli zote  za kimaendeleo sambamba na kuwapatia  fursa za ajira katika sekta mbali mbali  ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na kuondokana na wimbi la umasikini.

Jafo ametoa kauli hiyo  wakati wa sherehe za ugawaji wa vifaaa saidizi  kwa watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali wanaotoka katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wadau wa wengine wa maendeleo.

 Katika hatua nyingine  Waziri Jafo alimuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha anawakatia walemavu wote bima ya afya ili waweze kutibiwa bure ili   kuondokana na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata, na kuongeza kuwa atatoa kipaumbele cha kwanza kwa watu  wenye umelamvu katika fursa za ajira zilizotangazwa na serikali.
 WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa  (TAMISEMI)  Selemean Jafo (kushoto) akimkabidhi fimbo maalumu kwa ajili ya kutembelea mmoja wa watu wenye ulemavu wa macho, kulia katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa saidizi vikiwemo baiskeli za miguu mitatu zipatazo 40, viti  vya mwendo 15 pamoja na fimbo 100.
  WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa  (TAMISEMI)  Selemean Jafo  (aliyevaa suti nyeusi) akimkabidhi fimbo maalumu kwa ajili ya kutembelea mmoja wa watu wenye ulemavu wa macho,kulia katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa saidizi vikiwemo baiskeli za miguu mitatu zipatazo 40,viti  vya mwendo 15 pamoja na fimbo 100.
  Mwenyekiti wa Shirikisho la wa wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Ummy Ndariananga akitoa taarifa kwa mgeni rasmi kuhusina na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali.
  Mkuu wa Wilaya ya  Kisarawe Happiness Seneda akizngumza na walemavu na baadhi ya wananchi ambao walifika katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiuzungumza katika halfa ya ugawaji wa vifaa hivyo kwa watu wenye ulemavu katika  halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.(Picha Na Victor  Masangu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Mhe.Roberto Mengoni wakati alipotembelewa ofisini kwake Bungeni Dodoma Mei 22, 2018.
 Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Mhe.Roberto Mengoni akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na Balozi wa Italia Nchini, Mhe.Roberto Mengoni alipomtembelea Jijini Dodoma Mei 22, 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama na Balozi wa Italia Nchini Mhe.Roberto Mengoni wakiendelea na mazungumzo wakati Balozi huyo alipomtembelea Bungeni Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA)

Article 18

$
0
0
maonyesho haya yatajulikama kama Dodoma Expo. yatafanyika tarehe 23 & 24 kwenye viwanja vya Jamhuri Dodoma. Tunawakaribisha sana kushiriki kuonyesha bidhaa zenu, kwa pamoja tunakutanisha wajenzi wote na tujenge makao makuu

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Tulia Ackson akitambulisha wageni wa jukwaa la Spika wakati wa kikao cha thelathini na tano cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
Rais wa Umoja wa Vijana wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe.Mboni Mhita akitoa shukurani mbele ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania toka achaguliwe kuongoza umoja huo ivi karibuni nchini Afrika ya kusini ambapo atatumikia kwa muda wa miaka mitatu.
Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge na Mbunge wa Shinyanga Mjini Mhe.Stephen Maselle akitoa shukurani mbele ya Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania toka achaguliwe kuongoza Bunge hilo  ivi karibuni nchini Afrika ya kusini. 
Wanafunzi wa Sekondari ya Huruma ya Jijini Dodoma(kushoto) na Wanachuo wa Chuo cha Diplomasia(kulia) wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Augustine Mahiga akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt.Augustine Mahiga na Naibu wake Mhe.Dkt.Suzan Kolimba wakipitia hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kabla ya kuwasilisha leo Jijini Dodoma.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.fatma Toufiq(CCM) akiuliza swali kutaka  kujua  mpango wa Serikali kudhibiti hali ya wanafunzi kupewa ujauzito na  waendesha bodaboda leo Jijini Dodoma.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO, DODOMA.

MUME AUAWA NA MKE KWA KUTAKA APIKIWE.

$
0
0
JOSEPH MPANGALA-MTWARA.      

Mtu mmoja aliyejulikana kwa Jina la Ahamad Salum mkazi wa Kata ya Namiyonga Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara ameuawa na Mke wake Sofia Swaleh  Kwa Kuchomwa Kisu Kifuani kutokana na Majibizano ya Kupika Chakula Kingine.

Uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa kabla ya Mauaji hayo kulitokea Ugomvi baina ya Marehem na Mkewe ambapo Marehem alipikiwa Chakula na baada ya Kula Hakushiba hivyo akashinikiza Mke wake kumuandalia Chakula kingine Ndipo Ugomvi ukaibuka,na Ndipo Mke wa Marehemu Sofia Swalehe akachukua Kisu na Kumchoma eneo la Kifuani na kupelekea Ahamad Salum kufariki dunia kutokana na kupoteza Damu Nyingi.

Akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara DCP Lucas Mkondya amesema Watu wawili wanashikiliwa na Polisi Mmoja ni Jirani, Mussa Bakari ambaye aliingia ndani ya Nyumba baada ya kusikia Ugomvi ukiendelea na akashirikiana na Mke wa Marehem Sofia Swalehe kuua.

Aidha Kamanda Mkondya amewataka wananchi kutumia Viongozi wa Kiserikali na Kidini kuweza kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili katika Jamii.

'Nitoe rai kwa wananchii Magomvi hayana tija wajaribu kukaa na Kususuluhisha sio mnakaa na kugombana kwa kitu Kidogo mpaka mnapoteza Maisha kwa kitu Kidogo kama Chakula"

WAZIRI MKUU MAJALIWA AAGANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA, ALPHAYO KIDATA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Alphayo Kidata ambaye alikwenda  kwenye Makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay  jijini Dar es salaam kuaga, Mei 23, 2018.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Alphayo Kidata ambaye alikwenda kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kuaga, Mei 23, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Canada, Balozi Alphayo Kidata baada ya mazungumzo yao kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Mei 23, 2018.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images