Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA ASKOFU MKUU MTEULE WA KANISA LA ANGLIKANA NCHINI, IKULU JIJINI DAR

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu Mkuu Mteule wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Maimbo Mndolwa kabla ya kwenda kusimikwa rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa hilo mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Askofu Mkuu Mteule wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Maimbo Mndolwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Askofu Mkuu mteule wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Maimbo Mndolwa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Maimbo Mndolwa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Askofu Mkuu Mteule wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Maimbo Mndolwa aliyeambatana na mke wake Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda Dodoma kusimikwa rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Saba wa Kanisa hilo nchini. PICHA NA IKULU

Mapato Yatokanayo na Utalii Yaongezeka kwa Asilimia 5.6

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 2,131.57 kwa mwaka 2016 hadi kufikia Dola za Marekani 2,250.3 kwa mwaka 2017 ikiwa ni sawa na asilimia 5.6.
Hayo yameelezwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa MaliAsili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019.
"Idadi ya watalii walioingia nchini imeongezeka kutoka watalii  1,284,279 kwa mwaka 2016 hadi kufikia watalii 1,327,143 kwa mwaka 2017, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.3. Watalii kutoka Marekani wameongoza katika kuitembelea Tanzania wakifuatiwa na nchi za Uingereza, India, Uholanzi na Uswisi," amesema Dkt. Kigwangalla.
Ameendelea kusema, mafanikio hayo yanatokana na ujenzi wa miundombinu ya barabara, kuongezeka kwa kasi ya kuboresha na kutangaza vivutio vya utalii, kuimarishwa kwa mifumo ya ukusanyaji madhuhuli na kudhibiti matukio ya ujangili na matumizi yasiyo endelevu ya maliasili na malikale.
Vile amesema, katika juhudi za kutangaza utalii, Wizara imeendelea kutekeleza mikakati mabalimbali ikiwemo kuandaa utambulisho wa Tanzania Kimataifa (Destination Branding). Lengo ikiwa ni kuitambulisha Tanzania kama kituo mahsusi cha utalii Duniani.
Aidha, Wizara hiyo inashirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuanzisha chaneli maalum katika Televisheni ya Taifa (TBC 1) kwa ajili ya kutangaza utalii ambapo kwa sasa Wizara inaendelea na maandalizi ya kuanzisha studio ya kutangaza utalii kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Pia amesema, Wizara imeanza kutengeneza mfumo mmoja funganishi wa TEHAMA unaoitwa "MNRT Portal" kwa kutoa leseni na vibali, ukusanyaji wa takwimu na mapato kutoka vyanzo mbalimbali vya sekta ya Maliasili na Utalii.
"Mfumo huo utaunganishwa na mfumo wa Serikali wa malipo ya kielektroniki na kuhuishwa na mifumo mingine ya Serikali kama vile Uhamiaji, NIDA, TIRA, BRELA, TRA na NBS. Mfumo huo utaiwezesha Wizara kufuatilia watalii wa nje na wa ndani, kukusanya na kuchambua takwimu za sekta ya maliasili na utalii kwa wakati, kuimarishsa utoaji wa huduma kwa wateja na kufanikisha ukusanyaji udhibiti wa mapato," amesema Dkt. Kigwangalla.
Mfumo huo ambao utatumiwa na Wizara, Taasisi na wadau mbalimbali unatarajia kuanza kutumika rasmi mwaka ujao wa fedha.
Wakati huohuo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Nape Nnauye ameipongeza Serikali kwa kuboresha miundombinu ya utalii hususan barabara, huduma za maji na umeme ambavyo vimeendelea kuvutia watalii wengi kutembelea vivutio vya utalii na kuongeza idadi ya watalii hapa nchini.


 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMPUNI 380 KUONESHA BIDHAA ZAO KATIKA MAONESHO MAKUBWA YA KIMAITAFA UTALII YA KARIBU KILIFAIR MJINI MOSHI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilifair Ltd ,Tom Kunkler akizungumza mbele ya waandishi kuhusu tukio la Maonesho ya Kimatifa ya Utalii ya KAribu Kilifair yanayotaraji kufanyika mjini Moshi ,June 1 hadi 3 mwaka huu. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .

MAKAMPUNI 380 yanayojishughulisha na Utalii yanataraji kushiriki Maonesho ya Kimataifa ya Karibu Kilifair huku kampuni ya Kilifair Ltd inayoratibu maonesho hayo ikitangaza kuandaa safari za kifamilia zitakazoshirikisha watu kutoka nchi mbalimbali Duniani kujionea vuvitio vya utalii kwa lengo la kuvitangaza kimataifa.

Maonesho ya kimataifa ya Utalii yaliyopewa jina la Karibu Kilifair yanafanyika kwa mwaka wan ne sasa yakiwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Utalii wa Tanzania na nje ya nchi ,kwa lengo la kutangaza bidhaa mbalimbali za Utalii ikiwemo vivutio mbalimbali.

Kwa mara ya kwanza Kampuni ya Kilimanjaro SIR inayojishughulisha na ukoaji wa wageni waliopata matatizo katika maeneo yenye miinuko kama Mlima Kilimanjaro na Meru inataraji kushiriki katika maonesho hayo huku Shirika la ndege la Ethiopian Airlines likitangaza kutumia maonesho hayo kutangaza vivutio vya Utalii kwa wageni watakaosafiri na ndege wa shirika hilo.

Maonesho ya Karibu Kilifair yanayoratibiwa na Kampuni ya Kilifair Ltd awali yalijukiana kama Kilifair yakidhaminiwa na Kampuni mbalimbali za ndani na nje ya nchi .
 Viongozi wa Kampuni ya uokoaji ya Kilimanjaro SIR wakifuatilia maelezo juu ya manesho hayo yaliyokuwa yakitolewa kwa wanahabari. 
 Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Kilifair inayoratibu maonesho ya Karibu Kilifair ,Dominic Shoo akizungumzia tukio hilo kubwa la Kitalii. 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Uokoaji ya Kilimanjaro SIR ,Ivan Brown akizungumza wakati wa kikao na wanahabri kuhusu tukio hilo. 
 Meneja Mauzo wa Shirika la Ndege la Ethiopian Airlines ,Fitsimt Dejene ambao ni miongoni mwa wadhamini wa Maonesho ya Kimataifa ya Karibu Kilifair yanayotaraji kufanyika mjini Moshi. 

VIJANA WATAKIWA KUSIMAMA KIIMANI ILI WAFANIKIWE

$
0
0

 Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma akizungumza wakati wa Kongamano la tatu la Panda katika Chuo Kikuu Cha Tumaini Jijini Dar es Salaam ambapo Taasisi ya Her Initiative iliandaa kongamano hilo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Na Humphrey shao, Globu ya Jamii

Wito umetolewa kwa Vijana kutanguliza ibada kwanza katika shughuli zao za ujasilimali ili waweze kupata mafanikio ya kweli katika maisha .

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa elimu ya juu wanaojihusisha na masuala ya ujasiriamali chini ya Taasisi ya Her Initiative.

“ni Vizuri kongamno hili limefanyika katika mwezi huu mtukufu kwani Vijana wengi mnaingia katika biashara na kumsahau Mungu hali inayosababisha kuyumba kimaisha” amesema Vuma.

Ametaja kuwa suala la Imaan lina nafasi kubwa katika maisha ya Vijana kwani itasaidia kupunguza baadhi ya anasa ambazo zinapelekea kula mtaji wako wa baishara.
 
Amesema tatizo tulilonalo vijana wengi wetu hatujui umuhimu wa kujiwekea akiba kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe lakini ni wepesi kuweka bando hata la 30,000 ili mradi usikosekane facebook wala WhatsApp.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Juma Jux akizungumza na Vijana wa Chuo Kikuu katika Tamasha la Panda TUDARCO.
Muanzilishi wa Kampuni ya Mon Finance, Monica Joseph akieleza umuhimu wa kutunza akiba kwa Vijana ili waweze kufikia mafanikio.
Mtangazaji wa Radio , Meena Ally akiongoza mjadala wakati wa kongamano la Panda.
Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma akikabidhi cheti kwa mmoja wa Washiriki wa Mafunzo ya ujasiliamali.
Sehemu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu waliofika katika kongamano la Panda lililofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini

RAIS DKT. MAGUFULI AWAPONGEZA WABUNGE STEPHEN MASELE (MAKAMU WA RAIS BUNGE LA AFRIKA) PAMOJA NA MBONI MHITA (RAIS WA CAUCUS YA VIJANA YA BUNGE LA AFRIKA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM)

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wabunge, wa kwanza kushoto Stephen Masele ambaye amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika aliyeambatana na Mbunge mwingine Mboni Mhita (kulia) ambaye pia  amechaguliwa kuwa Rais wa Caucus ya vijana ya Bunge la Afrika katika uchaguzi uliofanyika Afrika ya Kusini wiki iliyopita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kuwapongeza wabunge hao wa Tanzania waliochaguliwa kushika nafasi za juu katika Bunge la Afrika.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge Mboni Mhita kwa  kuchaguliwa kuwa Rais wa Caucus ya vijana ya Bunge la Afrika katika uchaguzi uliofanyika Afrika ya Kusini wiki iliyopita. 
Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika Stephen Masele akizungumza na Wanahari Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Caucus ya vijana ya Bunge la Afrika Mboni Mhita PICHA NA IKULU

NEC YATEUA DIWANI WA VITI MAALUM KUPITIA CUF

NEWZ ALERT:WATENDAJI WATATU KITUO CHA UWEKEZAJI NCHINI WAFARIKI DUNIA

$
0
0

*Ni baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kugongana na Scania

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WATENDAJI watatu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC)  wakiwamo Wakurugenzi wawili na Meneja mmoja wamefariki dunia baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kupata ajali ya kugongana uso kwa uso na Scania katika Kijiji cha Msoga Chalinze mkoani Pwani.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Warioba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha vifo hivyo ambapo amesema  Zacharia Kingu na Martin Masalu ambaye ni Meneja wa Utafiti walifariki papo hapo wakati Said Amir alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitali kwa matibabu.

Amefafanua ajali hiyo imehusisha magari mawili ambayo ni gari namba STK 923 aina Toyota Landcruiser mali ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji iliyokuwa ikiendeshwa na Priscus Peter(23) mkazi wa Dar es Salaam kugongana na scania namba T 620AQV/ T 407DBY.

"Mei 21 mwaka huu saa 15:30 maeneo ya Msoga-Chalinze katika barabara ya Msoga/Msolwa Wilaya ya kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani, gari hizo ziligongana na kusababisha vifo na majeruhi,"amefafanua Kamanda Warioba.

Ameongeza majeruhi katika ajali hiyo ni Godfrey Kilolo(45) na dereva Priscus Peter ambao walipelekwa Hospitali ya Msoga kwa matibabu na tayari wameruhusiwa na miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani.

Eneo la ajali hiyo kwa mujibu wa taarifa limekaguliwa na na  ASP. Solla-Occid(W) akisaidiwa na INSP.MS Mkojera - DTO (W) Chkojera pamoja na F7704 PC Hamza ambaye ndiye mpelelezi wa tukio hilo.Hata hivyo juhudi za zinafanyika kumpata dereva wa Scania kwa mahojiano zaidi kwani alikimbia baada ya ajali kutokea.

Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha  ajali ni uzembe  wa dereva wa gari namba STK 5923 T ambaye alihama kutoka upande wake na kwenda kugongana na Scania hiyo.
Pichani ni  gari namba STK 5923 aina Toyota Landcruiser mali ya Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji iliyokuwa ikiendeshwa na Priscus Peter(23) mkazi wa Dar es Salaam kugongana na scania namba T 620AQV/ T 407DBY na kupelekea vifo na majeruhi. 

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akitolea ufafanuzi kuhusu hitaji la magari katika vituo vya polisi  leo Jijini Dodoma.
 Wabunge wa Viti Maalum Mhe.Munira Mustafa Khatib na Mhe.Halima Abdallah Bulembo wakifurahia jambo wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso akieleza mipango mbalimbali ya wizara yake katika kutatua changamoto za miradi ya maji wakati wa kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Mbunge wa Lupa Mhe.Victor Mwambalaswa akiuliza swali wakati wa kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt.Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.William Ole Nasha wakati wa  kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Augustine Mahiga akizungumza jambo na  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Mhe.Japhet Hasunga  wakati wa  kikao cha thelathini na nne cha Mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.


JENERALI MABEYO AANZA ZIARA RASMI NCHINI CHINA KWA LENGO LA KUDUMISHA USHIRIKIANO WA KIJESHI

$
0
0
Na Ripota Wetu, Blogu ya jamii
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo ameanza ziara rasmi nchini China yenye madhumuni ya kudumisha ushirikiano wa kijeshi kati ya Tanzania na China.

Taarifa kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa Jenerali Mabeyo ameanza ziara Mei mwaka huu na hiyo inatokana na mwaliko wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China.Akiwa huko atafanya mazungumzo rasmi na Mkuu wa Majeshi wa China Jenerali LI Zuocheng. Aidha, atakutana na Waziri wa Ulinzi wa China Jenerali WEI Fenghe kesho.

"Baada ya kuwasili nchini China Mei 20 Mei mwaka huu, Jenerali Venance Mabeyo alitembelea Ubalozi wa Tanzania nchini China ulioko mjini Beijing, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Maofisa wa Ubalozi wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Katika Mazungumzo hayo Balozi Kairuki amemueleza Jenerali Mabeyo, hali ilivyo nchini China kwa sasa katika nyanja mbalimbali zinazogusa uchumi, jamii za watu wa China na siasa, na nafasi ya nchi ya China kimataifa kwa sasa.

Aidha, Balozi Kairuki amefafanua hali ya maendeleo ya ushirikiano wa Tanzania na China kisekta na ujumla wake, pamoja na utekelezaji wake.

Kwa upande wake Jenerali Mabeyo, licha ya kueleza madhumuni ya ziara yake hiyo, pia alizungumzia hali ya sekta yake, na nafasi ya ushiriki wake kwenye utekelezaji wa majukumu ya Ulinzi na Usalama nchini.

Katika ziara hiyo, Jenerali Venance Mabeyo ameambatana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika kikao cha mazungumzo na  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa Kairuki, pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Ubalozi wa Tanzania nchini China.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo(kulia) akimkabidhi zawadi  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki(kushoto) alipotembelea ubalozi wa Tanzania nchini China.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki (Kulia).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja  na  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki, Maofisa waandamizi kutoka  Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Maofisa wa Ubalozi.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na  Maofisa waandamizi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini China, Maofisa wa Ubalozi pamoja na uwakilishi wa Watanzania wanaosoma nchini China.

IGP SIRRO AKUTANA NA BALOZI UFARANSA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier (katikati), alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, ambapo balozi huyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwenye masuala mbalimbali ya kiusalama. Picha na Jeshi la Polisi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume (Kulia), aliyeongozana na wajumbe wake wawili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam kwa lengo la Kujitambulisha na pia kujadiliana masuala mbalimbali ya kisheria. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume (Kulia), wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam kwa lengo la kujitambulisha tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Chama hicho na pia kujadiliana masuala mbalimbali ya kisheria. Picha na Jeshi la Polisi.

SERIKALI YAWATAKA WADAU WA NGOs KUENDELEA KUTEKELEZA SERA ZILIZO CHINI YA IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII

$
0
0
Na Mwandishi wetu Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeawataka wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuendelea kutekeleza Sera mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi na Msajili wa NGOs Bw. Marcel Katemba Jijini Dodoma wakati wa  Kikao kati ya Serikali na Wadau hao kinachokaa kwa siku moja kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi zao na kutekeleza Sera zilizo chini Idara kuu Maendeleo Jamii.

Ameongeza kuwa katika kutekeleza Sera mbalimbali Serikali inashirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanafanya kazi kubwa nchini katika kuleta maendelo ya jamii na Taifa katika sekta mbalimbali nchini.

“Wadau wa NGOs mnafanya kazi nzuri na kubwa katika kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa letu” alisisitiza Bw.Katemba.

Kwa upande wake Mwakilishi Kutoka Shirika la World Vision Tanzania Bi. Janeth Edson akitoa mrejesho wa makubaliano kati ya Serikali na NGOs kwa upande wa NGOs amesema kuwa wao kama wadau wataendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Sera mbalimbali na kuwaasa wadau kuendelea kuunganisha nguvu na Serikali katika kusogeza mbele gurudumu la maendeleo.
  Mkurugenzi na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau  Mashirika yasiyo ya Kiserikali  yanayotekeleza Sera zilizo chini ya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi Tausi Mwilima (kulia) akieleza yatokanayo na kikao kilichopita kati ya Serikali na wadau wa NGOs wanaotekeleza Sera mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii  Jijini Dodoma.
 Mwakilishi kutoka Shirika la World Vision Tanzania Bi Janeth Edson akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa hati ya makubaliano ya utekelezaji wa Sera mbalimbali baina ya Serikali na NGOs kwa upande wa NGOs katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao kati ya Serikali na wadau wa NGOs Jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAANDISHI WAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TFDA KATIKA KUHAMASISHA MATUMIZI SAHIHI YA BIDHAA

$
0
0
Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imeendesha kikao kazi cha wahariri na waandishi wa habari wa mikoa ya Shinyanga na Mwanza kwa ajili ya kuhamasisha kazi na majukumu ya TFDA na kujadiliana kwa pamoja mikakati ya Mamlaka ya kupambana na bidhaa duni na bandia katika soko na namna bora ya kushirikisha wananchi katika udhibiti na hatimaye kuhakikisha kuwa wanatumia bidhaa bora, salama na fanisi ili kumlinda mwananchi. 

Kikao kazi hicho kimefanyika Jumatatu Mei 21, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa TFDA Kanda ya Ziwa uliopo Buzuruga jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho cha siku moja Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi.Agnes Sitta Kijo, alisema kikao hicho kinahusu uhamasishaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura 219.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu alisema kuwa, TFDA itaendelea kufuatilia, kuondoa na kuteketeza bidhaa ambazo hazikidhi vigezo vya ubora, usalama na ufanisi ili kuepusha bidhaa duni na bandia  kutumika ambapo amewahimiza Wahariri na Waandishi kufikisha elimu watakayoipata kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akifungua kikao kazi kati ya TFDA, wahariri na waandishi wa vyombo vya habari wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa TFDA Kanda ya Ziwa, Mwanza tarehe 21 Mei, 2018.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bi Agnes Sitta Kijo akitoa maelezo ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kati ya TFDA, Wahariri na Waandishi wa vyombo vya habari wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa TFDA Kanda ya Ziwa, Mwanza tarehe 21 Mei, 2018. Kikao kazi hiki kilihusu uhamasishaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura Na.219.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa akieleza wajibu wa waandishi na wahariri wa habari katika kuleta ufanisi wa utekelezaji wa Sheria ya Chakula Dawa na Vipodozi Sura Na. 219.

Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza wa TFDA, Bw. Adam Fimbo akifafanua jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi nchini kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga (hawapo pichani).
Mkurugenzi wa Uendelezaji Huduma wa TFDA, Bw. Chrispin Severe, akieleza jambo wakati akiwasilisha mada kuhusu Dira Dhima na majukumu ya TFDA kwa wahariri na waandishi wa vyombo vya habari wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga. 
Mada kuhusu utambuzi wa dawa bandia na duni ikitolewa wakati wa kikao kazi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MSHAMBULIAJI AZAM AKIRI MAJERAHA YA NYONGA YAMEPUNGUZA KASI ALIYONAYO MSIMU ULIOPITA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

MSHAMBULIAJI wa Azam Shaaban Idd, amekiri kuwa nje ya dimba kwa takribani miezi saba akiuguza majeraha ya nyonga kulimwaribia kuendeleza kasi aliyokuwa nayo msimu uliopita.

Shaaban aliweza kuiongoza Azam FC kuichapa Tanzania Prisons mabao 4-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) akifunga hat-trick na jingine likitupiwa wavuni na kiungo Frank Domayo.

Mara baada ya Shaaban kukosa raundi ya kwanza ya ligi kutokana na majeraha aliyopata mwishoni mwa msimu uliopita, hivi sasa amerejea vema kabisa baada ya hat-trick hiyo kumfanya akikishe mabao nane kwenye ligi msimu huu, huku akiandika rekodi ya kufunga mabao sita ndani ya mechi nne zilizopita.

Mabao hayo nane yamemfanya kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita alipopandishwa timu kubwa akitokea Azam B, na kufunga mabao sita kwenye msimu wake wa kwanza wa ligi.

Akizungumzia mchezo uliopita, Shaaban alisema ilimlazimu kuvuta subira ili kurejea kwenye ubora wake na anamshukuru Mwenyezi Mungu hivi sasa ameanza kufanya vizuri huku akiahidi makubwa zaidi msimu ujao.

TANZIA

SPIKA JOB NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA NABII MWINGIRA NA WANAFUNZI KUTOKA CHUO KIKUU CHA MICHIGAN LEO OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha St. John kilichopo Jijini Dodoma, Prof. Emmanuel Mbennah (katikati) na mmoja ya Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Michigan kilichopo nchini Marekani walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha St. John kilichopo Jijini Dodoma, Prof. Emmanuel Mbennah (katikati) na mmoja ya Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Michigan kilichopo nchini Marekani walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Michigan kilichopo Mjini Michigan, nchini Marekani walipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat Mwingira (katikati) alipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. Kulia ni Mke wake wa Nabii, Ndg. Eliakunda Josephat Mwingira.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati)akimsikiliza Mhe. Anna Lupembe (aliesimama) akizungumza wakati walipotembelewa na ugeni ulioongozwa na Mtumishi wa Mungu Mtume na Nabii Josephat leo Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

TBF YATANGAZA TAREHE YA KUANZA MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

SHIRIKISHO la Mpira Kikapu Tanzania(TBF) imetangaza rasmi tarehe ya mashindano ya kikapu ya FIBA Zone V U18 (Wanawake na Wanaume ) kuwa yanatarajiwa kuanza June 17 hadi 22 2018 hapa Jijini Dar Es Salaam, Tanzania. 

Rais wa TBF Pharess Magesa amesema matarajio yao ni kuwa mmoja kati viongozi wetu wakuu wa nchi ndyie atakuwa mgeni rasmi wa mashindano hayo na yatarushwa mubashara (live) siku zote za mashindano na vituo vyote vikubwa vya TV na Radio ambavyo wametuma maombi.

Magesa amesema gharama za maandalizi ya timu zetu mbili za Taifa  na gharama za kuandaa mashindano haya ni kubwa, na tayari kuna wadau wameshajitokeza kutoa ahadi na wengine wameshasaidia. 

"Hadi sasa hivi TBF ina upungufu wa takribani Sh.milioni 100, kati ya hizo Sh.milioni 60 ni za kuandaa mashindano na Sh.milioni 40 ni za kuweka timu zetu 2 za wanawake na wanaume kambini na kununua vifaa vya michezo zikiwemo Jersey za kucheza na za mazoezi, truck suits, viatu, socks, mipira na madawa,"amesema Magesa. 

"Pia, tuna mahitaji mengi ili kufanikisha matengenezo ya uwanja wa ndani wa Taifa (indoor) ukiacha kuvuja paa na kukatika kwa umeme ambako kutadhibitiwa na msaada ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,"amesema.

UBA YAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE, YAAHIDI HUDUMA BORA ZA KIBENKI NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
UONGOZI wa United Bank for Africa(UBA) umesema umejipanga kuendelea kutoa huduma bora za kifedha kwa Watanzania huku ukifafanua kukua kwa teknolojia kumeifanya benki yao kutoa huduma zake kwa njia ya mtandao na kuwafikia wateja wengi zaidi.

Pia umeeleza mikakati yao katika kuhakikisha wanashiriki kuleta maendeleo nchini na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano.Pia umewahimiza wananchi umuhimu wa kuwa na Kitambulisho cha Taifa kwani vinarahisisha kwa wanaohitahi kufungua akaunti benki.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na uongozi wa UBA wakati wanazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusu mafanikio, malengo na mikakati yao katika utoaji wa huduma za kibenki nchini. Pia UBA umekutana na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM).

Mtendaji Mkuu wa UBA nchini Tanzania Chris Byaruhanga ,amesema tangu kuanzishwa kwa benki hiyo miaka 75 iliyopita nchini Nigeria na kufungua matawi katika nchini mbalimbali ikiwemo Tanzania wamepata mafanikio makubwa na benki hiyo imekuwa chachu ya maendeleo katika Bara la Afrika.

Amefafanua kwa Tanzania UBA imeendelea kujiimarisha katika kutoa huduma bora za kibenki na imekuwa mstari wa mbele kuchangia shughuli za kimaendeleo na kubwa zaidi uwepo wa benki hiyo umesaidia kutoa ajira kwa Watanzania.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Brendansia Kileo (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumzia mipango mbalimbali ya UBA. Wengine ni Mkuu wa Mahusiano ya ndani na nje wa UBA Nasir Ramon(kushoto) na Mtendaji Mkuu wa UBA nchini Tanzania Chris Byaruhanga(katikati).
Mtendaji Mkuu wa UBA nchini Tanzania Chris Byaruhanga (katikati) akizungumzia mafanikio ya benki hiyo kwa waandishi wa habari nchini.Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Brendansia Kileo na Mkuu wa Mahusiano ya ndani na nje wa UBA Nasir Ramon(kushoto)
Mkuu wa Mahusiano ya ndani na nje wa UBA Nasir Ramon (kushoto)akizungumzia mchango wa benki hiyo katika kuchangia maendeleo ya nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.Kati kati ni Mtendaji Mkuu wa UBA nchini Tanzania Chris Byaruhanga na kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Brendansia Kileo
Mmoja ya maofisa wa UBA akielezea ubora wa kadi ya benki hiyo kwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) leo jijini Dar es Salaam

WANAFUNZI WA CHUO KUKUU ZANZIBAR WAPEWA SOMO JUU YA UMUHIMU WA EAC

$
0
0
Mabalozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga pamoja na Suzane William Mollel wamekutana na Wafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar kilichopo Tunguu, Ujunga visiwani Zanzibar, kwa lengo la kutoa mafunzo na kuwahamasisha Wanafunzi wa vyuo vikuu (Vijana) nchini kote, kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuuimarisha katika Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, katika Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu hizo, Mei 21, 2018. Jumla ya Wanafunzi 410 walihudhulia Warsha hiyo.
Mwakilishi wa Chuo Kikuu Zanzibar, Saleh Mohammed akizungumza machache wakati akifungua warsha ya siku moja ya mafunzo na kuwahamasisha Wanafunzi wa vyuo vikuu (Vijana) nchini kote, kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuuimarisha katika Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, katika Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu hizo, Mei 21, 2018.
Muwakilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Kiongozi wa Mabalozi vijana EAC, Barbara Kaboha akizungumza wakati ufunguzi wa warsha ya siku moja ya mafunzo na kuwahamasisha Wanafunzi wa vyuo vikuu (Vijana) nchini kote, kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuuimarisha katika Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, katika Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu hizo, Mei 21, 2018.
Naibu balozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar, na kuwahamasisha kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuuimarisha katika Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, katika Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu hizo, Mei 21, 2018.
Balozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga (aliyesimama) akitoa mafunzo kwa baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar.

NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AKUTANA NA WANANCHI WALIOPISHA UJENZI KIWANJA CHA NDEGE CHA MSALATO, DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akizungumza na wananchi wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji (hawapo pichani), kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma mjini, Mhe. Anthony Mavunde akifafanua jambo kwa wananchi wa Kata ya Miyuji, Makutupora, Msalato na Nzuguni waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
Wananchi wa Kata ya Miyuji, Makutupora, Msalato na Nzuguni wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa (hayupo pichani), kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa, akisalimiana na wazee wa mtaa wa Mpamaa, Kata ya Miyuji mara baada ya kuzungumza nao kuhusu mpango wa Serikali wa kulipa fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, mkoani Dodoma.

LIVE BUNGENI: WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, DKT. KIGWANGALLA AKIWASILISHA MAJUMUISHO YA BAJETI YA WIZARA YAKE 2018/2019

Viewing all 110088 articles
Browse latest View live




Latest Images