Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

DONGOBESH FC YANYAKUWA UBINGWA WA KURUGENZI CUP 2018 MBULU DHIDI YA REMA 1000 FC

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimkabidhi kombe kapteni wa timu ya Dongobesh FC ya Dongobesh Iddi Podoksi mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Rema 1000 FC ya Hayodm katika mchezo wa fainali Kombe la Kurugenzi Cup 2018 uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom mjini Haydom wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.
Kapteni wa timu ya Dongobesh FC ya Dongobesh Iddi Podoksi akinyanyua kombe juu mara baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Rema 1000 FC ya Haydom katika mchezo wa fainali Kombe la Kurugenzi Cup 2018 uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom
Wachezaji wa Dongobesh FC wakifurahia kombe lao mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Rema 1000 FC kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Haydom katika fainali ya Kurugenzi Cup 2018.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akizungumza na kumshukuru Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi kwa kushiriki kwake katika fainali za michuano hiyo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI MAVUNDE APONGEZA MIPANGO YA MJASARIAMALI KIJANA BI HADIJA JABIR KATIKA KUTENGENEZA NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa GBRI Co. Ltd Bi Hadija Jabiri kwa mafanikio makubwa aliyopata kupitia kilimo cha mbogamboga.

Aidha amempongeza kwa kuajiri takriban Wafanyakazi 236 sambamba na uanzishwaji wa mpango wa ushikirishwaji wakulima wadogo wadogo(out-growers) ambao wataiuzia Kampuni hiyo mazao mbalimbali ya mboga mboga ili aweze kufikia mahitaji ya soko la nje ambayo ni tani 26 kwa wiki za maharage machanga na njegere changa.

Mavunde ametoa pongezi hizo leo alipofanya ziara fupi kutembelea Mashamba hayo ya Mboga mboga yaliyopo Kijiji cha Kiwele, Halmashauri ya Iringa Vijijini yanayomilikiwa na Bi Hadija Jabiri kijana mdogo mwenye umri wa miaka 27.

Mavunde amesisitiza pia utekelezwaji wa agizo la Waziri Mkuu kwa Tawala za mikoa juu ya utengwaji wa maeneo mahsusi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi za Vijana ili Vijana wengi zaidi wapate fursa za maeneo ya kufanyia shughuli mbalimbali na pia kuitaka Mifuko ya Uwezeshwaji Wananchi Kiuchumi kusaidia jitihada hizi za Bi Hadija ili aweze kufikia mahitaji ya soko.

Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri Mavunde,Meneja wa PackHouse Bw.Ferdinand Sinkala amesema kwamba Kampuni yao ina soko kubwa la Maharage na Njegere changa katika nchi za Uingereza,Ireland na Sweden lakini changamoto kubwa inayowakabili ni upatikanaji wa ardhi ili kuwa na eneo kubwa zaidi waweze kulima na kukidhi mahitaji ya soko la nje.

Amesema kwa sasa wameamua kuwashirikisha wakulima wadogo wadogo kulima mazao hayo ili waweze kukidhi mahitaji ya soko la tani 26 kwa wiki,lakini pia ameiomba Serikali kuunga mkono jitihada za Vijana walioamua kushiriki katika Kilimo hasa kilimo cha mboga mboga kwa kuwawezesha ili waweze kufikia malengo yao.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akikagua shamba la mboga mboga.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akikabidhiwa mboga mboga.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiwasikiliza wataalam wa GBRI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi ,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akiwa ameshika maharage machanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa GBRI Co. Ltd Bi Hadija Jabiri 

UFALME WA UINGEREZA UMEINGILIWA?

$
0
0
Francis Daudi, Melukote Town!

Jana dunia ilisimama kupisha ndoa ya kifalme, Mwana Mfalme Henry Charles Albert David ‘Prince Harry’ mwenye miaka 33 alimuoa mwigizaji wa Marekani, Bi Meghan Markle mwenye miaka 36. Hii ndio kusema Meghan Markle ambaye alishaoana na Trevor Engelson kisha kutalikiwa mwaka 2013 anakuwa Duchess wa Sussex.

Wote wawili, yaani Prince Harry na Meghan Markle wanatoka katika familia za wazazi ambao wana historia ya kutalikiana! Lakini kikubwa zaidi ni kuwa haikutarajiwa Harry kuoa nje kabisa ya Ufalme wa Uingereza. Prince Harry kwa takribani miaka 7 iliyopita alikuwa akim‘DATE’ binti Chelsy Davy, mara kadhaa waligombana na kurudiana. Wakati Fulani mwaka 2011 ilitaarifiwa kuwa wameachana. Na sasa Prince Harry akaanza kuonekana Binti Cressida Bonas hadi mwaka 2014.

Kama utani vile, Prince Harry alimrudia Chelsy Davy ila wakati huu mwana mfalme alihakikisha taarifa hizi hazisambai tena mpaka lengo la ndoa litakapotimia. Maisha ya kujificha, huku wakisubiri kutangaza uchumba mwezi June, 2016 walivurugana tena.

Mwaka 2017 tetesi zikasambaa kuwa sasa mtoto wa Mfalme Prince Harry amekuwa na safari nyingi Marekani na huko kuna ‘Shemeji’ ambaye jina halikujulikana mpaka Harry alipoutobolea umma kuwa ana mchumba ambaye ni mwigizaji Meghan Markle. Ilikuwa habari mbaya na ya kushtua hasa kwa kuwa Meghan Markle anajulikana sana na kwenye jumba la ufalme ilionekana sasa wameingiliwa na ‘Mtalikiwa’.

Pamoja na mazonge hayo yote, Prince Harry aliwaalika Ma-Ex wake hapo jana! Wote walikuwepo Kanisani St. George’s Chapel. Mara kadhaa waandishi walijaribu kuwazunguka Chelsy Davy na Cressida Bonas. Haikuwezekana kwani ulinzi ulikuwa ni Mkali sana.
Kihistoria, Prince Charles ambaye ni baba wa Prince Harry aliwaalika Ex’s wake wakati wa Ndoa yake na Princess Diana iliyofanyika Julai 29, 1981. Kati ya hao ni Camilla, ambaye alikuja kuwa mke wa Prince Charles baada ya kutalikiana na Princess Diana mwaka 1985. Hii ndio kusema, Prince Charles alipata kuwa na Camilla kabla ya kumuoa Princess Diana. Ndoa ilipovunjika Prince Charles akamuoa Camilla ambaye ni mkewe mpaka leo. 
Inaelezwa kuwa historia inaweza kujirudia kwa Prince Harry na Chelsy Davy ambapo wamekuwa pamoja kwa muda mrefu Zaidi.

BALOZI WA CHINA ATETA NA DK MENGI, AAHIDI KUSAIDIA MABADILIKO

$
0
0
CHINA imetaka watanzania kutumia fursa ya kuwa na maji mengi na ardhi ya kutosha kufanya shughuli za kilimo na kuzalisha mazao mengi ambayo wanaweza kuyauza nchini humo na pia kuyatumia kama malighafi kwa viwanda vya ndani.

Taifa hilo kubwa kiuchumi duniani, limesema kwamba ufunguo wa maendeleo ya viwanda upo katika kilimo na biashara ya kilimo hivyo ipo haja kwa watanzania kufanya bidii katika kufanikisha kilimo.Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi, ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki.

Katika mazungumzo hayo Dk Mengi aligusia zaidi kuhusu China kuona haja ya kusaidia kuinua kilimo cha Tanzania kutokana na mabadiliko yanayofanywa Tanzania ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.Alisema uchumi huo utawezekana kwa kutumia rasilimali za kilimo kama malighafi na kilimo cha Tanzania kinahitaji sapoti kubwa ya kukifanya kuwa cha biashara.

Balozi wa China alikiri kwamba ipo haja ya kukibadili kilimo cha Tanzania ambacho kwa sasa ni cha kifamilia zaidi na kuwa cha biashara na kusema wapo tayari kushiriki katika ndoto za watanzania kwenda kwenye uchumi wa viwanda kwa kutegemea malighafi za kilimo.Hata hivyo alisema kwamba China inahitaji sana mazao ya kilimo kutoka Tanzania, kasoro ni kuwa uzalishaji bado ni mdogo sana.

Alitolea mfano wa kuwepo kwa kiwanda cha mafuta ya kula ya alizeti kwamba mbegu huwa hazitoshi na hivyo kiwanda hicho cha Wachina kulazimika kuagiza mbegu kutoka nje.Alisema kwa sasa kiwanda hicho kinatengeneza tani elfu 10 za mafuta wakati uwezo wa kiwanda ni tani laki moja kwa mwaka.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi akifafanua jambo kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke (kushoto) wakati wa mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke akisoma muonekano wa mbele wa kitabu kinachozungumzia maisha ya Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi ulioandikwa “I Can, I Must, I Will - The Spirit of Success” wakati wa mazungumzo yao kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mh. Wang Ke akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi zawadi ya kasha la majani ya chai (China Green Tea) kutoka nchini China mara baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kibiashara baina ya makampuni ya China na Tanzania ofisini kwa mwenyekiti huyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


IBADA YA KUMTAWAZA ASKOFU DKT. MAIMBO .W. MNDOLWA KUWA ASKOFU MKUU WA KANISA LA ANGLIKANA TANZANIA

WASAIDIZI WA MAKAMU WA RAIS WATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA RAHMAN DODOMA

$
0
0
Wasaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametoa futari kwa kituo cha watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Dodoma.

Kituo hicho chenye watoto 120 ambao kati ya hao 75 ni yatima ambapo hupatiwa Elimu ya Dini na Lugha.

Wasaidizi hao ambao waliwakilishwa na Kaimu Katibu wa Makamu wa Rais Bi. Maulidah Hassan na Msaidizi wa Masula ya Siasa Ndugu Nehemia Mandia kwa pamoja walisema imekuwa utamaduni wao kukutana, kuzungumza na kusaidia watoto yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na walemavu na wameahidi kuendelea kusaidia kila inapowezekana. 

Nae mwanzilishi wa Kituo hicho Bi. Rukia Hamisi ameshukuru kwa wasaidizi wa Mheshimiwa Makamu wa Rais kufika ofisini kwake na ameomba Mheshimiwa Makamu wa Rais akipata nafasi naye afike kituoni kwani watoto wanampenda sana pili alishukuru kwa futari.




MWANDISHI MATHIAS CANAL APEWA TUZO YA HESHIMA NA ASASI YA WAZALENDO NA MAENDELEO TANZANIA (AWAMATA)

$
0
0
Mwandishi wa habari na mchambuzi wa mambo mbalimbali nchini Tanzania Ndg Mathias Canal (Kushoto) akikabidhiwa tuzo ya cheti cha heshima kwa mchango wa utendaji katika jamii na Ndg Mohamed shabani ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya jinsia, wazee na watoto wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA).
Mwandishi wa habari na mchambuzi wa mambo mbalimbali nchini Tanzania Ndg Mathias Canal akionyesha cheti cha tuzo ya utambuzi wa utendaji wa kizalendo katika jamii alichokabidhiwa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA).

Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Mwandishi wa habari na mchambuzi wa mambo mbalimbali nchini Tanzania Ndg Mathias Canal amepewa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) ikiwa ni alama ya kutambua mchango wake na kazi za kizalendo na maendeleo anazozifanya nchini.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Ndg Mohamed shabani ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya jinsia, wazee na watoto wa asasi hiyo ya AMAWATA Taifa amesema Asasi hiyo imehamasika kutoa tuzo ya cheti cha heshima na pongezi kwa Mathias Canal kwa sababu ni mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi na kuhabarisha wananchi kuhusu mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kihabari jambo ambalo limekuwa ni chachu kwa vijana wengine nchini.

Alisema kuwa Mathias Canal ni moja ya waandishi wabunifu sana na kama mwandishi kijana amekuwa na maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla, ambapo amehamasisha vijana wengine kushirikiana nae katika mtandao wake wa Wazo Huru Blog na WazoHuru.Com chini ya kampuni yake ya habari inayotarajiwa kukamilisha usajili wake hivi karibuni.

“Tumekuwa tukimfatilia tangu akiwa Mhariri na mtangazaji wa redio Free Africa (RFA) na baadaye kuwa mwandishi wa kujitegemea ambapo amefanya kazi na viongozi mbalimbali wa dini, siasa, jamii na serikali kwa ujumla wake, kwa muda mrefu kama asasi tumeshawishika kumpa tuzo hii, kwa ufanyaji kazi ya kizalendo na maendeleo hasa anapoumiza kichwa kwa ajili ya kutengeneza ajira kwa vijana wenzake kupitia mtandao Wazo Huru Blog" Alikaririwa Mohamed

Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Kampuni ya Wazo Huru Media Group (C.E.O), Ndg Mathias Canal amemshukuru Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa Ndg Chief Mrindoko Babu Mwidadi sambamba na watendaji wote wa Asasi ya AWAMATA kwa kumpatia tuzo hiyo ya heshima kwani alidhani tuzo hiyo hutolewa kwa viongozi wa serikali pekee.

“Sikufikiria kama ningeweza kupata heshima hii katika umri wangu huu, kwani nimekuwa nikishuhudia viongozi mbalimbali wakipewa tuzo hii akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na hata Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kaka yangu Mhe Antony Mtaka, hivyo hii ni heshima kubwa sana kwangu, imenipa moyo wa kufanya kazi kwa bidii na weledi zaidi kwa manufaa ya Taifa langu” Alikaririwa Canal

Sambamba na hayo pia Canal alitoa wito kwa Vijana wenzake kutimiza wajibu wao, katika kusukuma gurudumu la Taifa mbele ikiwa ni pamoja na kujitokeza katika shughuli mbalimbali za kijamii sambamba na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) ni asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojishughulisha na uelimishaji wa uzalendo kwa Watanzania na kufundisha mbinu za kujitegemea ili kuondokana na umaskini pia inatoa tuzo kwa watu wanaofanya vizuri katika masuala mbalimbali ya kizalendo na kuwasaidia wananchi kutoka katika lindi la umasikini.

Naibu Waziri afanya ziara kiwanda cha HUACHENG kinachojihusisha na uchinjaji na usafirishaji wa nyama ya Punda

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola ametoa muda wa miezi sita kwa kiwanda cha HUACHENG kinachojihusisha na uchinjaji na usafirishaji wa nyama ya Punda Mkoni Dodoma kuondoa mabaki ya miundo mbinu ya vyuma na mbao ambavyo awali vilikua vikitumika katika uchinjaji wa ngo'mbe.

Mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika kiwanda hicho iliyolenga kufuatilia maagizo ya Serikali yaliyotolewa hapo awali, Waziri Lugola ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kutafuta wawekezaji ambao wanaweza kutumia miundo mbinu hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi. "Mvua itakaponyesha mahali hapa patakuwa na uchafuzi wa hewa, na kwetu sisi wana mazingira magofu kama haya ni uchafuzi wa mazingira, hivyo ndani ya miezi sita kama hamjapata ufumbuzi, ondoweni mabaki haya". Lugola alisisitiza.

Aidha, Kiwanda hicho kimetakiwa kufuata takwa la kisheria la kufanya Ukaguzi wa Mazingira kwakuwa awali kiwanda hicho kimekua kikifanya shughuli zake bila kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira. Waziri Lugola ameupa uongozi wa Kiwanda hicho muda wa miezi miwili kukamilisha takwa hilo kama lilivyoainishwa katika Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.

Katika ukaguzi huo Waziri Lugola amegundua pia kiwanda hicho hakina Mpango Endelevu kama Sheria inavyoelekeza, hivyo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limeagizwa kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo ndani ya miezi miwili.

Msemaji wa Kiwanda hicho Bw.Michael Gao amesema kuwa maagizo hayo yatatekelezwa kikamilifu na kwa muda uliotolewa. Kiwanda hicho huchinja punda ishiriki kila siku na wanasafirishwa kupelekwa katika Nchi za China na Vietnam.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola mwishoni mwa wiki ameendelea na ziara ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira. Pichani akipata maelezo kutoka kwa Afisa Afya wa Jiji Bw. Carle Lyimo mara baada ya kutembelea kiwanda cha kuchinja punda cha HUACHENG kinachomilikiwa na raia wa China.
Mganga wa Mifugo Bw. Merjoly Mariki Msimamizi wa viwanda vya nyama Kanda ya Kati akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Naibu Waziri Mhe. Kangi Lugola mara baada ya kukagua kiwanda cha kuchinja Punda eneo la Kizoto Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa taka.
Mabaki ya miundo mbinu ambayo awali ilikua ikitumika katika kuchinja ngombe katika kiwanda cha HUACHENG Jijini Dodma ikiwa imetelekezwa baada ya mwekezaji huyo kutoitumia tena na kujishughulisha na uchinjaji wa punda.
Sehemu ya punda wakisubiri kuchinjwa, imeelezwa kuwa nyama ya punda hao ina soko kubwa sana katika Nchi za China na Vietnam. Wastani wa punda ishiriki huchinjwa kila siku katika Kiwanda hicho.

KUMBUKUMBU

REHEMA FOUNDATION YAKABIDHI MRADI WA MAJI SHULE YA SEKONDARI ZOGOWALE

$
0
0
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Zogowale ,mjini Kibaha Mkoani Pwani ,wakishangilia kupata huduma ya maji shuleni hapo ,baada ya kujengewa kisima cha kupampu kilichogharimu zaidi ya sh.mil.11 ,(wa katikati)Mkurugenzi wa Rehema Foundation ,Mohammed Cesur.

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

CHANGAMOTO ya maji safi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa shule ya sekondari Zogowale, Mjini Kibaha mkoani Pwani, inabaki historia baada ya kujengewa kisima kirefu cha kupampu, kilichogharimu zaidi ya sh. mil 11, kwa msaada kutoka taasisi ya Rehema.

Licha ya hilo, shule hiyo bado inakabiliwa na kero kubwa ya ukosefu wa uzio hali inayotishia usalama kwa wanafunzi na walimu. Akizungumza wakati wa makabidhiano ya kisima hicho ,kaimu mkurugenzi wa Rehema Foundation ,Rafii Jongo ,alisema ujenzi wa kisima hicho umekamika kwa wiki mbili .

Alielezea ,taasisi hiyo inajihusisha na masuala ya kijamii na hadi sasa imeshasaidia kuchimba visima ndani ya jamii 185 Tanzania Bara na Visiwani ambapo kwa mkoa wa Pwani imechimba visima 50.# "Tunatoa pia misaada ya chakula na kugawa nyama ya ng'ombe kwa watu wasiojiweza nyakati za mfungo tatu ,Na kila mwaka tunachinja ng'ombe 1,000, tunapeleka watanzania kusoma masomo mbalimbali nchini Uturuki" alisema Jongo .

Nae Mkurugenzi wa taasisi hiyo ,Mohammed Cesur aliwataka wanafunzi watunze kisima hicho kwa ajili ya manufaa ya shule na jamii inayowazunguka. Aliwaasa wanafunzi wajitahidi kusoma ili kuinua taaluma zao . Cesur alisema, changamoto ya maji itakuwa imekwisha hivyo anaamini wanafunzi hao wataelekeza juhudi zao katika masomo .

Kwa upande wake ,mkuu wa shule ya sekondari ya Zogowale ,Tatu Mwambala alisema awali walikuwa wakitumia visima vilivyopo nje ya shule na katika mradi wa kijiji . Alisema maji yalikuwa si ya uhakika na sio salama ambako walipoteza muda kutafuta maji . Tatu alielezea ,ipo changamoto nyingine kubwa ya ukosefu wa uzio hali inayosababisha kushindwa kuwa na usalama wa kutosha.

"Tumeanza kujenga uzio kwa jitihada za wazazi na jamii ,tumekwama kifedha ,tunaomba wadau watusaidie kwa ari na mali kumalizia ujenzi huo ""Shule hii ina wanafunzi wa kike ambapo inatakiwa wawe kwenye usalama zaidi kuliko shule kuwa haina uzio"alisisitiza Tatu .

Mwanafunzi wa kidato cha tano shuleni hapo ,Shamim Shomvi alisema, walikuwa wakipata shida ya maji na kusababisha kutumia muda mwingi kwenda kutafuta huduma hiyo badala ya kujisomea. Alisema, walitumia maji ya visima vya chini ambayo hayakuwa salama, " wanafunzi wengine waliugua magonjwa ya matumbo kama typhoid". Shamim aliwashukuru Rehema Foundation, na kuwaomba wasisite kuwasaidia kutatua matatizo mengine yanayowakabili . Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Jennifer Omolo aliwasihi kuutunza mradi huo ili udumu katika kipindi kirefu.
Baadhi ya viongozi wa shule ya sekondari Zogowale ,serikali ya mtaa wa Zogowale na halmashauri ya Mji wa Kibaha wakiwa pamoja na mkurugenzi wa taasisi ya Rehema Foundation ,Mohammed Cesur ,wakifurahia uzinduzi wa mradi wa maji shuleni hapo ,baada ya kujengewa kisima cha kupampu kilichogharimu zaidi ya sh.mil.11.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Zogowale Tatu Mwambala, akishukuru baada ya kupokea mradi wa maji shuleni hapo uliojengwa kwa msaada wa taasisi ya Rehema Foundation. (Picha na Mwamvua Mwinyi).

DKT KALEMANI AZINDUA USAMBAZAJI WA GESI ASILIA MAJUMBANI

$
0
0
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Matiku Makori wakiwasha jiko lililofungwa gesi asilia tayari kwa matumizi ya nyumbani katika eneo la Mikocheni mtaa wa TPDC jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza katika uzinduzi wa usambazaji wa gesi asilia majumbani kwa mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara hafla iliyofanyika katika stesheni ndogo ya kupokea gesi hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Matiku Makori (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amezindua usambazaji wa gesi asilia kwa mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara na hivyo kutoa fursa kwa wanananchi wa mikoa hiyo kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 40 kutokana na gesi ya mitungi inayotumiwa majumbani.

Dkt. Medard Kalemani, amesema kuanza kwa matumizi ya gesi hiyo kutawasaidia wananchi wa mikoa hiyo na hususani wa jiji la Dar es Salaam, kupunguza gharama kwa asilimia 40, ikilinganishwa na gharama ya matumizi ya mitungi ya gesi inayotumiwa na wananchi wengi hivi sasa. 

Dkt Kalemani amesema usambazaji huo wa awamu ya kwanza unaofanywa kuanzia eneo la Ubungo mahali ambapo kituo cha gesi hiyo kutokea Mtwara, utaigharimu Serikali kiasi cha Sh Bilioni 4 zitakazotumika kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali kutoka eneo hilo hadi itakapopelekwa. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba akielezea hisitoria ya mradi huo na jinsi utakavyoweza wafaidisha wananchi watakafungiwa gesi hiyo asilia.

Ameyataja maeneo ambayo usambazaji wa gesi hiyo kwa awamu ya kwanza utafanyika kuwa ni pamoja maeneo yote ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Ubungo, Survey, Makongo juu, Sinza, Mikocheni, Mwenge, Tegeta hadi kiwanda cha Sao Hill. 

Pamoja na maeneo hayo, mengine ni pamoja na maeneo ambayo gesi kutoka Ubungo hadi Gereza la Keko itapita, Ubungo hadi Mbagala, pamoja na maeneo ya Kimara hadi Tabata, huku Waziri huyo akimuagiza Mkandarasi aliyepewa kazi ya usambazji wa gesi hiyo kukamilisha kazi hiyo ifikapo Septemba Mwaka huu. 

Aidha amesema awamu ya pili ya usambazaji huo inatarajiwa kuanza Julai mwaka huu huku akitajwa kuigharimu Serikali kiasi cha Sh Bilioni 11, ambapo usambazaji huo utafanywa katika maeneo ya Kigamboni pamoja na Mkuranga na kwingineko ndani ya Jiji la Dar es Salaam. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Matiku Makori akitoa shukrani zake za pekee kwa shirika la TPDC kuwanzisha mradi utakaowaletea wananchi matokeo chanya ikiwa ni pamoja na kupunguza uharibifu wa mazingira.

“Hatua hii inakwenda kumaliza suala la matumizi ya nishati ya mkaa ambapo inakadiriwa kuwa asilimia tisini (90%) ya wananchi wa Dar es Salaam wanaitumia na hivyo kuchangia uharibufu wa mazingira pamoja na misitu, imani yetu matumizi ya gesi asilia yatasaidia kuleta mageuzi makubwa ya nishati hapa nchini” amesema Dkt Kalemani. 

Pamoja na hayo amesema umeme unaozalishwa kupitia mitambo ya Kinyerezi 2, Kinyerezi 3 uliopo katika matengenezo pamoja na mtambo wa Somangafungu unaotarajiwa kuzalisha Megawati 330 kuanzia mwaka ujao, kwa pamoja itasaidia kuzalisha zaidi ya Megawati 2,780 za umeme. 

Amewataka wenye viwanda kukaa tayari kwa ajili ya kuunganishiwa nishati hiyo kwa Jiji la Dar es Salaam huku akimtaka mwekezaji wa kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara kuomba kuunganishiwa nishati hiyo ‘hata leo’ Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba, amesema maandalizi kwa ajili ya usambazaji wa gesi hiyo katika maeneo yote yaliyoainsihwa katika mpango wa awali umekamilika na kwamba kinachofuata sasa ni kuwaunganishia wananchi nishati hiyo. Alisema ukiacha uunganishaji wa gesi hiyo kwa wananchi, pia wataviunganishia viwanda viliwili vilivyopo eneo la Mikicheni, kikiwemo kiwanda cha Wazo pamoja na IPTL.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akipata maelezo jinsi mtambo unavyopokea gesi asilia na kuisambaza majumbani.

Taasisi ya Mo Dewji yatoa msaada kwa watoto wenye saratani

$
0
0
Taasisi ya Mo Dewji imetoa msaada kwa watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya saratani katika kituo cha Tumaini la Maisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Msaada ambao umetolewa ni unga wa ngano, khanga na sabuni za kuogea, kufua na kunawia mikono.

Akikabidhi msaada huo, Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul alisema taasisi yao itaendelea kuwa na utaratibu wa kutoa msaada katika kituo hicho ili kuwafariji watoto ambao wanapatiwa matibabu.

Alisema hiyo sehemu ya kwanza kutoa msaada kwani wamekuwa na utaratibu wa kusaidia jamii kutokana na uhitaji uliopo hivyo kwa kufanya hivyo wanaamini watakuwa wamegusa maisha ya Watanzania wengi.

Aidha, Paul amewataka watu wengine wenye uwezo kuweka utaratibu wa kusaidia watu wengine wenye uhitaji kama watoto waliopo katika kituo cha Tumaini la Maisha.
Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto ambao wanapatiwa matibabu katika kituo cha Tumaini la Maisha.
Kaimu Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Belinda Paul akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasimamizi wa kituo cha Tumaini la Maisha wakati walipokuwa wakikabidhi msaada katika kituo hicho.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (USDM) ambao wanalipiwa gharama za masomo na Taasisi ya Mo Dewji wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wanaopatiwa matibabu katika kituo cha Tumaini la Maisha.

RAIS DK. SHEIN AKUTANA NA BALOZI MPYA WA CANADA, CUBA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Balozi Mpya   wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Canada pia akiiwakilisha Tanzania nchini Cuba Mhe. Alphayo Kidata  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha (Picha na Ikulu).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  mgeni wake Balozi  Mpya wa    Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Canada pia akiiwakilisha Tanzania nchini Cuba Mhe. Alphayo Kidata  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na  mgeni wake Balozi   Mpya wa    Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Canada pia akiiwakilisha Tanzania nchini Cuba Mhe. Alphayo Kidata  baada ya mazungumzo yao alipofika kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na  mgeni  wake Balozi   Mpya wa    Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Canada pia akiiwakilisha Tanzania nchini Cuba Mhe. Alphayo Kidata  baada ya mazungumzo yao alipofika kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar leo.

LIVE BUNGENI: WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. DKT. HAMISI KIGWANGALLA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YAKE 2018/2019

SERIKALI HAITAJIUSISHA NA UPANGAJI WA ADA KWA SHULE BINAFSI-NAIBU WAZIRI WILLIAM OLE NASHA


SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU, MHE. JAJI WARIOBA OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA.

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Jaji. Joseph Sinde Warioba (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. 
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kushoto) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu. Mhe. Jaji. Joseph Sinde Warioba (kulia) alipowatembelea jana katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma. Katikati ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Jaji. Joseph Sinde Warioba (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Jijini Dodoma. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Jaji. Joseph Sinde Warioba (kulia) akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kushoto), wa pili kulia ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai na kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

MOZAMBIQUE AND GREAT LAKES AFRICA ENERGY SIGN MoU FOR POWER GENERATION

$
0
0
The Government of Mozambique has signed a Memorandum of Understanding (MoU) with Great Lakes Africa Energy (GLAE) to generate electric power using natural gas for domestic use at an estimated value of US $400million.

The agreement signed last Friday in Maputo, Mozambique with GLAE, a United Kingdom registered Pan African energy solutions provider, will involve the construction of a 250 megawatt gas fired electricity generating power plant.

As part of the agreement, GLAE will develop, finance, build, own and operate the power plant to be fed with natural gas supplies from Mozambique’s Rovuma Basin.The MoU agreement was signed by Mozambique’s Minister for Mineral Resources and Energy, Dr. Max Elias Tonela, and GLAE Director, Mr. Michael Kearns.

The agreement follows the result of Mozambique’s Rovuma Basin domestic gas tender, the results of which were announced in January 2017.Michael Kearns of GLAE said: “As part of the Mozambique Government’s intended use of natural gas for the development of domestic power projects, GLAE will develop, finance, build, own and operate a 250 megawatt (MW) gas-fired electric generating power plant, planned in Northern Mozambique.”

Mozambique, which has vast offshore gas resources, has decided to use some portion of the extracted gas for domestic power projects, with an aim of achieving a sustainable economic growth, including domestic energy production.

Speaking on behalf of the Government of Mozambique, Bruno Senguaio, Assistant to the Minister, said: “Mozambique has considerable renewable and conventional energy resources and is fast becoming a significant energy producer. Our Government’s chief priority is to ensure a secure and reliable energy supply for the people of Mozambique. This is why the project is so important. In GLAE we have found a reliable partner which will help us deliver this power plant.”

The power plant in Northern Mozambique is a key regional infrastructure project. It will accelerate the development and industrialization of several other industrial projects, which have been shelved due to the lack of a steady power supply. At 250MW, GLAE’s Northern Mozambique gas fired power plant will be one of the largest conventional sources of electricity in the country.
Mozambique Minister for Mineral Resources and Energy Dr. Max Elias Tonela (left) confers with Great Lakes Africa Energy (GLAE) Shareholder, Humphrey Kariuki (centre) and GLAE Director, Mr. Michael Kearns (right) at an MoU signing ceremony in Maputo, Mozambique. The Government of Mozambique has signed a Memorandum of Understanding (MoU) with Great Lakes Africa Energy (GLAE) to generate electric power using natural gas for domestic use at an estimated value of US $400million.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AZINDUA MRADI WA UUNGANISHWAJI WA UMEME WA GRIDI YA TAIFA KWA MIKOA WA LINDI NA MTWARA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewahakikishia watanzania wote kuwa Serikali itafikisha umeme kila kona na kila kijiji.

Waziri Mkuu aliyasema hayo mara baada ya kuzindua mradi wa uunganishwaji wa umeme wa Gridi ya Taika kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye hafla iliyofanyika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika mkoani Lindi leo Mei 21, 2018.

Hata hivyo aliwataka kuwa wavumilivu kwani mipango ya serikali ambahyo ni kuhakikisha umeme unafika sio tu maeneo ya mijini bali pia kwenye vijiji vyote vya Tanzania.“Kitendo kinachofanyika hapoa leo ni ushahjidi wa ahadi hiyo ya serikali na ninachowaomba Watanzania ni kuwa na subira kwani serikali inatekeleza ahadi ilizotoa kuhakikisha watanzania wanapata umem wa uhakika na wa bei nafuu.”

Akizungumzia uzinduzi huo ambao sasa umetoa sukuhisho la uhaba wa umeme kwenye mkoa huo wa Lindi Waziri Mkuu alitoa maagizo kwenye halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha maeneo yote nyeti ya huduma za kijamii yanafikishiwa umeme ikiwemo shule na hospitali.“Hatutarajii kuwa na eneo lenye shida ya umeme, hapa ni umeme masaa 24, na tafsiri ya serikali kuwa hapa ni umeme wa uhakika na wa kutosha ndio hii ambayo leo hii tumezindua.” Alisema.

Alisema sera ya serikali ni ya uchumi wa viwanda,na kwamba, wale watu wanaotaka kuwekeza viwanda vya Korosho, Salfa na vifaa mbalimbaki kwenye mkoa wa Lindi sasa ni wakati wao kwenda mkoani humo na kuwekeza kwani hivi sasa kuna umeme wa uhakika.Aidha Waziri Mkuu aliwaasa wananchi kuwa walizni wa miundombinu ya umeme, na kuwataka wanapoona vitendo vya watu wakihujumu mkiundombinu basi taarifa za kuwashughulikia watu hao ni vema zikatolewa kwa vyombo husika ili kuchukua hatua.

“Naomba vifaa vyote vinavyoletwa kwenye maeneo yenu, kwenye vijiji vyenu basi tuvilinde ili hatimaye tuweze kunufaika na uimarishwaji wa miundombinu ya umeme.” Aliasa Wazir Mkuu.Kupitia mpango w REA, yaani umeme vijijini Serikali imepunguza kutoka Shilingi 380,000/= hadi shilingi 27,000/= tu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa mradi wa uunganishwaji umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Mradi huo sasa umeondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika kwenye mikoa hiyo ya Kusini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,(katikati) na viongozi wengine wa serikali wakiwemo mawaziri akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kuunganishwa umeme wa Gridi ya Taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mahumbika Mkoani Lindi leo Mei 21, 2018. 
Waziri Mkuu Majaliwa akimpongeza Waziri Dkt. Kalemani.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (wapili kulia), akiwa na viongozi wengine, wakiimba wimbo wa taifa baada ya kufanya uzinduzi.
Waziri Mkuu Majaliwa, na viongozi wengine, akipatiwa maelezo ya ,mradi huo na mmoja wa wataalamu wa TANESCO, kwenye kituo cha Mahumbika.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiongoza kikao cha thelathini na tatu cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri-TAMISEMI Mhe.Josephat Kandege akijibu hoja mbalimbali za wabunge  wakati kikao cha thelathini na tatu cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt Hamisi Kigwangalla  akiteta jambo na Naibu wake Mhe.Japhet Hasunga wakati kikao cha thelathini na tatu cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Dkt Hamisi Kigwangalla akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt Suzan Kolimba  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge wakati kikao cha thelathini na tatu cha mkutano wa kumi na moja leo Jijini Dodoma.
 Viongozi waandamizi wa Wizara ya maliasili na Utalii wakiongozwa na Katibu mkuu Meja Jenerali  Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu Dkt.Aloyce Nzuki wakifatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma.

Picha na Daudi Manongi, MAELEZO,DODOMA.

SERIKALI YAHIMIZA HALMASHAURI KUBUNI MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUJIONGEZEA MAPATO

$
0
0
Serikali imeeleza kuwa Uchukuaji wa baadhi ya vyanzo vya mapato katika halmashauri ulifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti iliyoridhiwa na Bunge ya mwaka 2015 kifungu namba 58 ikiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa ukusanyaji na matumizi ya mapato hayo.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Suzana Mgonukulima, aliyependekeza itungwe sheria ya kuibana serikali ikiwa haitarejesha fedha zilizotokana na vyanzo vya mapato vilivyopo kwenye Miji, Halmashauri, Manispaa na Majiji zitakazokusanywa na kuwekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Bajeti, mgao wa fedha kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali utazingatia bajeti iliyoidhinishwa, upatikanaji na mtiririko wa fedha, utekelezaji mpango wa ununuzi na mpango wa kuajiri hivyo hakuna Fungu litakaloruhusiwa kufanya matumizi ya aina yoyote mpaka kuwe na fedha za kulipa matumizi husika.

“Usimamizi wa Mapato hayo kwa mujibu ya Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 Kifungu namba 58 unazingatia mapato kuingizwa kwenye Sheria ya Kuidhinisha Matumizi ya Fedha za Serikali, aliyepewa mamlaka ya kukusanya mapato ya Serikali atawajibika katika ukusanyaji wenye ufanisi, utunzaji wa hesabu, utoaji wa taarifa na kuzuia ufujaji wa mapato”, alisema Dkt. Kijaji. 

Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images