Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WAZIRI UMMY AZINDUA MASHINDANO YA BANDA CUP AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 16 ambazo zinashiriki michuano ya Banda Cup ikiwa ni mchango wake kusaidia mashindano hayo.

Makabidhiano hayo yalifanywa kwa timu 16 ambazo zinashiriki mashindano hayo wakati alipokwenda kuyafungua kwenye viwanja vya CCM mkwakwani mjini Tanga.Mashindano hayo yameanzishwa na Beki wa timu ya Baroka FC ya nchini Afrika kusini Abdi Banda akiwa na lengo la kusaidia kuinua vipaji vya soka na kuvikuza ili kuweza kuwa na hazina kubwa kwa siku zijazo.

Akizungumza juzi wakati akikabidhi vifaa hivyo ambazo ni Jezi seti mojamoja kwa kila timu shiriki,Waziri Ummy alisema mchezo wa mpira wa miguu unaweza kuwasaidia vijana iwapo watazingatia na kujituma.Alisema pamoja na hayo lakini anampongeza muandaaji wake kwa kuona namna ya kuyaanzisha ili kuwasaidia kukuza vipaji vya wachezaji wachanga ambao baadae wataweza kusaidia kwenye soka letu.

“Nimempongeza kwa moyo wake wa uzalendo na sio kwamba ana fedha nyingi sana lakini kile kidogo anachokipata ameona ashirikiana na watuwa Tanga hivyo nasi tutahakikisha tunashirikiana naye”Alisema.Hata hivyo Waziri huyo alisema licha ya kutoa vifaa hivyo lakini atatoa fedha kwa Mfungaji bora 100,000, mwamuzi bora 100,000, timu yenye nidhamu 200,000, mlinda mlango bora 100,000 huku mchezaji bora akitoka na 100,000.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Ummy,Mratibu waMashindano Ibrahimu Kidiwa alisema katika mashindano hayoyanashirikisha timu 16 ambapo mshindi wa kwanza atapata.sh.500,000,mshindi wa pili atapata 250,000,mshindi wa tatu atapatash.100,000 na mipira miwili (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha).

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akizungumza wakati akifungua mashindano ya Vijana ya Banda Cup kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani mjini Tanga ambapo pia alitoa vifaa vya michezo kwa timu zote 16 ambazo zinashiriki mashindano hayo.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Jezi mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Jezi mmoja wa viongozi wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoa na viongozi wa timu zinazoshiriki michuano ya Banda Cup mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo.


HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKALAMA SHIKAMANENI KUINUA WILAYA YENU-WAZIRI JAFO

$
0
0
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka wananchi wa wilaya ya Mkalama iliyopo mkoani Singida kushikamana ili kuinua wilaya yao kimaendeleo.


Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia umati wa wananchi wa wilayani hiyo katika shughuli za uzinduzi wa wiki ya elimu inayofanyika wilayani Mkalama.Jafo amebainisha kwamba wilaya ya Mkalama ilikuwa wilaya ya mwisho katika matokea ya darasa la saba ya mwaka 2017 hivyo wanapaswa kushikamana kuondoa aibu hiyo.



Katika mkutano huo, amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo kwa kazi kubwa anayofanya ambayo imesaidia kusukuma maendeleo wilayani humo kwa kushirikiana vyema na serikali na kufanikisha miradi ya afya, maji, pamoja na elimu. Aidha amesema kwasasa serikali inaboresha kituo kimoja cha afya na pia anefanikisha  mpango kabambe wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo imepangwa kujengwa katika bajeti ya 2018/2019.



Kadhalika, Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkalama kumwita mkandarasi aliyejenga jengo la halmashauri ambaye ni Kampuni ya Mzinga kurudi haraka ndani ya wiki ijayo ili arekebishe maeneo yenye dosari.Pamoja na hayo, Jafo amesisitiza watumishi wote kuwa waadilifu kwani Ofisi yake anayoiongoza haiwezi kuvumilia ufisadi, wizi, uzembe, na ubabaishaji kazini.


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo akisalimiana na viongozi na wananchi wa wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi akimtembeza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kwenye vikundi mbalimbali vya burudani.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi akimkaribisha Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kuzungumza katika uzinduzi wa wiki ya elimu.
Jengo la Halmashauri ya Mkalama ambalo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo ameagiza lifanyiwe marekebisho.
Baadhi ya vikundi vya burudani vikitumbuiza katika uzinduzi wa wiki ya elimu wilayani Mkalama

UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA MJI WA NANYAMBA MKOANI MTWARA WA SUASUA

$
0
0
Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri ya mji wa Nanyamba mkoani Mtwara Mhandisi MEDRAD MMOLE amesema kukosekana kwa vibarua kumepelekea kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo unaofanywa na kandarasi ya Suma JKT.

WATEJA KUWASILIANA BILA KIKOMO NA SUPER HALO YA HALOTEL

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii 

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imezindua kifurushi kisichokuwa na ukomo wa muda kitakacho wawezesha wateja wa mtandao huo kuwasiliana bila kikomo kupitia kifurushi kabambe cha Super Halo.

Wateja wa mtandao wa Halotel watakao jiunga na kifurushi hicho wataweza kupiga simu au kutumia intaneti hadi pale vifurushi vitakapokwisha muda wa matumizi.

Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika katika Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo Mhina Semwenda amesema kuwa, uzinduzi huo wa vifurushi vya Super Halo ni mapinduzi mengine makubwa katika sekta ya mawasiliano kwa kuondoa ukomo wa muda katika vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti.

Amesema kama kampuni wamedhamiria kuwafurahisha wateja Kwa huduma kabambe za mawasiliano bila ya kuwa na wasiwasi wa kuisha kwa muda wa matumizi ya mawasiliano. Pia ameeleza kuwa mteja wa Halotel anaweza kujiunga kwa kuanzia shilingi 500 na kupata dakika 17 za kupiga Halotel bila kikomo cha muda na kwa shilingi 500 na kwa 500 hiyo hiyo mteja anaweza kujiunga na kupata MB 110 za intaneti za kutumia bila kikomo. 

Ameeleza lengo kubwa la kifurushi hicho ni kumwezesha mteja kuona thamani ya pesa yake na kuweza kufurahia mawasiliano ya kupiga simu na kutumia MB za intaneti bila kikomo.
 Baadhi Wateja wa Mtandao wa Halotel  wakiangalia vifaa mbalimbali vinavyo vinavyouzwa na kampuni ya simu ya  Halotel mara baada ya uzinduzi huo.
 Afisa Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala  akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Milimani City jijini Dar es  Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda akizungumza katika uzinduzi wa kifurushi kisichokuwa na ukomo kilichopewa jina na Super halo katika ukumbi wa Mlimani City  jijini Dar as Salaam.

CAG AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA OFISI YAKE

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Profesa Mussa Juma Assad amesema ofisi yake imefanikiwa kutoa taarifa kwa wakati, kila inapofika Machi 30 ya kila mwaka licha ya kukabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti.

Profesa Assad ameeleza hayo leo jijini Dodoma kwenye mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ambao unalenga kupitisha bajeti ya mwaka na kujadili masuala ya kiutendaji ambayo yanawasilishwa na kuitishwa na wajumbe.

Akizungumza katika mkutano huo, CAG amesema ufinyu huo unaosababisha shughuli za kiofisi kutofanyika pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu ya dharula yanayoibuka nje ya ukomo wao wa bajeti.“Baraza hii limekuwa na ufanisi mkubwa katika kusimamia majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye mkataba,”amesema Prof. Assad

Amesema pamoja na mafanikio mbalimbali ambayo ofisi hiyo imeyapata, bado zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili na zinahitaji utatuzi wa kina.Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni kushindwa kukamilisha ujenzi kwa ajili ya Ofisi katika mikoa iliyolengwa kutokana na kutotolewa kwa fedha za maendeleo kama ilivyopangwa na kwa wakati.

Aidha amesema katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa Fedha 2017/18 hadi kufikia Machi, 2018 Ofisi ilishindwa kuwajengea uwezo watumishi kulingana na viwango vya kimataifa vya ukaguzi kutokana na ufinyu wa bajeti.“Kuna changamoto ya mwenendo wa upatikanaji wa fedha za matumizi mengineyo na maendeleo kutoka mfumo mkuu wa serikali kutoendana na mahitaji halisi ya majukumu ya Taasisi hususani ukaguzi na mafunzo kwa watumishi,”amesema.

Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ,Utumishi, Dk.Laurean Ndumbaro ameitaka ofisi ya Taifa ya ukaguzi kutekeleza agizo la serikali kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma.Dk. Ndumbaro amesema tayari viongozi mbalimbali wa serikali walishahamia, hivyo ni mategemeo yake kuwa Ofisi ya Taifa ya ukaguzi nayo pia ipo katika mkakati wa kuhamishia shughuli zake jijini Dodoma kama ambavyo taasisi nyingine zimefanya.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma  Asaad (kushoto) akiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro (kulia)wakifurahia jambo wakati aliokuwa kimsindikiza mara baada Katibu Mkuu huyo kufungua mkuatano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya CAG uliofanyika mjini Dodoma leo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akizungumza wakati wa kufungua mkutano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika mjini Dodoma leo .

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya CAG.
Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof Musa Asaad akitoa taarifa ya Ofisi yake wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya CAG lililofanyika leo jijini Dodoma .
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya CAG.

wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Ukaguzi

ULEGA APOKEA MIFUKO 200 YA SARUJI YA UJENZI WA ZAHATI MKURANGA

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amepokea mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya Sh.milioni tatu kutoka Shirika la Bima la Taifa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.

Akizungumza na Michuzi blog, Ulega ameeleza leo kuwa mifuko hiyo ya saruji itatumika itatumika katika ujenzi wa zahanati katika vijiji mbalimbali kama Kibamba, kazole, Yavayava na Mkanonge wilayani humo.

Ulega amesema kuwa kazi hiyo ni ya wote katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli na kuifikisha Tanzania mbele zaidi na kusisitiza ujenzi wa miundombinu hasa ya madarasa na zahanati unaendelea katika vijiji mbalimbali na hiyo ni katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za msingi.

Aidha Ulega amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo wa kusaidia Wilaya ya Mkuranga kwa ujenzi wa shule na zahanati.

Kwa upande wa Meneja Masoko wa Shirika la bima la taifa Elisante Maleko ameeleza utoaji wa mifuko hiyo ya saruji ni kutokana na uhusiano mzuri baina yao, hivyo wakaona faida wanayopata kutoka kwa wananchi hao ambao ni wateja wazuri ni kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya madarasa na zahanati katika vijiji mbalimbali vya Mkuranga.

Mkurugenzi wa Shirika hilo tawi la Ubungo Segeja Mabulla amemshukuru mbunge na mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwakutanisha na kutoa elimu ya kuwasaidia wananchi kuhusu masuala ya bima.Pia amewapongeza wakazi wa Wilaya hiyo kwa kuwa wateja wazuri wa bima za halmashauri na bima za maisha.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akipokea mifuko 200  saruji kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la bima la Taifa,Elisante Maleko yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya zahanati na madarasa leo mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akipokea kava la tairi la gari kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la bima Taifa,Elisante Maleko  leo mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na  Mbunge wa Mkuranga  Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Rais Magufuli ateua wenyeviti wawili wa Bodi.

Fanya haya kufanikisha mfungo wa Ramadhani

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani umekaribia ambapo Waislamu wote nchini na duniani wanatarajiwa kuanza kufunga. Mwezi huu muhimu kiimani huchukuliwa kama kipindi cha toba ambapo waumini hufunga kwa kujinyima kula, kufanya ibada pamoja na kufanya matendo mema na ya huruma katika kipindi chote cha mfungo. 

Ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa Ramadhani, Jumia Travel imekukusanyia mambo yafuatayo ya kufanya ndani ya kipindi hiki ili kukurahisishia kufanikishia mfungo wako. 

Kamilisha funga zako. Mafundisho yanawataka waumini wafunge kwa imani na kwa moyo wote ili kupata thawabu kutoka kwa Mungu, ikiwemo dhambi zao kusamehewa. Kuna faida kubwa za kufunga ambazo zinatarajiwa baada ya kuisha kwa mfungo. Kwa hiyo, endapo utafunga hakikisha unafunga kwa moyo wote na dhamira ya dhati moyoni ili uje ulipwe kwa matendo yako. 

Fanya matendo yatakayompendeza Mungu. Lengo kuu la Ramadhani ni kurudisha imani kwa mwenyezi Mungu kwa kuachana na anasa za dunia. Mfungo, kiasilia, utakusaidia kuyafanikisha hayo lakini utafanikiwa zaidi kwa kuyachunga matendo yako hususani yale yasiyompendeza muumba wako. Ni vema katika kipindi hiki kuwa unajikumbusha mara kwa mara kipindi chote cha mfungo, kwa kufanya hivyo utaogopa kutenda au kufikiria maovu. 

Soma Quran. Ramadhani ni mwezi wa Quran. Itakuwa haujaitendea haki na ni kazi bure kama hautokisoma kitabu hiki kitukufu. Hii hapa ni njia rahisi unayoweza kuifuata. Kwa kuwa utakuwa unafunga, maana yake utakuwa huru muda wa chakula cha mchana. Utumie muda huo kusoma. Kama hauna kitabu, mambo yamerahisishwa kupitia teknolojia siku hizi. Unaweza kupakua programu ya simu ya mkononi na kujisomea. Hii ni njia rahisi na inayowezekana ya kujisomea Quran. 

Chunga ulimi wako. Njia mojawapo rahisi inayoweza kuharibu funga yako ni kwa kujihusisha na umbeya na maongezi yasiyompendeza Mungu. Mwenyezi Mungu hamuhitaji mtu ambaye hataki kuachana na mienendo yake miovu katika kipindi cha mfungo. Hivyo basi, kwa mwaka huu, jitahidi kwa kadri uwezavyo kukaa mbali au kujiepusha na maongezi ambayo yatakupelekea kumkosea muumba wako. 

Toa msaada. Mtume Muhammad (SAW), alikuwa akijulikana kama mtu mwenye ukarimu wa hali ya juu, lakini kipindi cha mwezi wa Ramadhani ukarimu wake uliongezeka kupita kiwango. Ramadhani inakupatia fursa pekee ya kuongeza moyo wako wa kujitolea ili kujiongezea thawabu zaidi. Kwa kuongezea, utakuwa unafanya kama vile alivyofanya mtume wa Mungu. Kwa hiyo, hakikisha unawasaidia watu mbalimbali wasiojiweza na kuhitaji msaada katika kipindi hiki cha mfungo. 

Ramadhani ni kipindi muhimu cha kujitafakari kiimani, kujiimarisha na kujitoa kwa waumini wa dini ya Kiislamu. Jumia Travel ingependa kuwatakiwa Waislamu wote maandalizi ya mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuyazingatia mafundisho na yale yote yaliyoagizwa ili kumaliza salama.

Kamati ya Bunge ya Uganda Yamwagia Sifa Mradi wa DMDP

$
0
0
Kamati ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kutoka Nchini Uganda (PAC-LG) imemwagia sifa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam unaoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Tano za Mkoa wa Dar es salaam. 

Kamati hiyo yenye zaidi ya wajumbe kumi waliotemebelea Mradi wa DMDP unaotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wamesema ni mradi wa mfano na kuigwa na Nchi za Afrika Masshariki zinazopata mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia.

Akizungumza katika ziara hiyo ya mafunzo Mwenyekiti wa Kamati hiyo (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu amesema lengo la ziara yao ni kuona namna ambavyo miradi ya Uboreshaji Miundombinu inayotekelezwa kwa fedha za Mkopo toka Benki ya Dunia;

“Tunapenda kuona ubora wa miradi hiyo, taratibu za ulipaji fidia zilivyofuata, maelekezo ya mkopo wa fedha hizo yalivyozingatiwa na zaidi namna ambavyo fedha zilivyopokelewa, zinavyosimamiwa na wataalamu, zinavyotumika na zinafanyiwa ukaguzi na zaidi suala zima la thamani ya fedha”Value for Money” kuonekana katika miradi hiyo” alisema Mhe. Okumu.
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege (kushoto) akiwapokea wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Nchini Uganda waliotembela Wizara kuona ubora wa miradi ya Benki ya Dunia inavyotekelezwa. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu (kulia) akiwa na mjumbe wa Kamati hiyo toka Uganda wakifuatilia kikao na Naibu Waziri wa Tamisemi(hayupo pichani) Mhe. Joasephat Kandege. 
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege akifurahia jambo wakati wa kikao cha Mapokezi ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa. 
Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP 
Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP 

IN LOVING MEMORY OF R.BRIAN SALVA RWEYEMAMU

$
0
0
R.BRIAN SALVA RWEYEMAMU 
1987 - 2014
Today, 15 May, 2018, the family of Salva Rweyemamu and Isabella Kafumba Rweyemamu commemorates four years of the untimely departure of their beloved son, R. Brian Salva Rweyemamu. It is a day that has developed into a highly dreaded date of every calendar year. This day and date brings back to life the collective, immensely desperate agony of the difficult events of that morning of May 15, four years ago.

Brian, this day also brings back memories of your very courageous last struggle and fight to retain your life at Lugalo General Military Hospital, Dar es Salaam, surrounded by your parents, friends and family. You fought very hard to remain alive as you had always fought to succeed throughout your very short and cheerful life. These memories remain sadly vivid and difficult to bear even with the quick passage of time. It is a scene none of us would want to witness again in life.

As we sadly remember this day, the fourth anniversary of your eternal departure, R. Brian Salva Rweyemamu, we also continue to be firmly committed to you, our inspiration. You made us very happy during your short life and we remain sincerely thankful for that. As always, our thoughts and prayers continue to be with you.

You were not only our son, our father, our brother and our cousin but also our best friend. We also continue to thank God for your precious and memorable life that made us all so happy.

Your only child, your son, B. Calvin Brian Rweyemamu, continues to especially miss you dearly. His visits and prayers to your resting place at Kinondoni Cemetry are almost daily when he is on holidays in Dar es Salaam, from school. We continue to take very good care of him on your behalf and we are united as family to see him succeed in life. Indeed, he remains a wonderfully happy boy.

You will always be remembered by him, your son, by your sisters Brenda and Sonia, by your parents Salva and Bella and all the family and friends. RIP BRIAN.

Standard Chartered wazindua michuano ya kuwania tiketi ya kwenda kuiona Liverpool

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Benki ya Standard Chartered jana ilizindua awamu ya tatu  ya michuano ya soka ya kuwania kombe lake. Michuano hiyo ya kuwania kombe la Standard Chartered 2018 huchezwa kwa dakika 10 kila upande ukicheza kwa dakika 5. Michunao hiyo inasaka timu itakayoenda kushuhudia kipute kinachopigwa na timu ya Liverpoool. Hii ni mara ya tatu kwa michuano hiyo ya kusisimua kufanyika katika ardhi ya Tanzania kuanzia mwaka 2010.

The Standard Chartered Group ndio wadhamini wakubwa wa Liverpool Football Club kuanzia mwaka 2010 hadi  2018/2019. Kwa kushirikiana na klabu hiyo benki ya Standard huendesha mashindano ya soka ya dakika 10 katika masoko yake makubwa ya Bara la Asia, Afrika na Mashariki ya kati. 

Pia michuano hiyo inawezesha kuchangia katika kuendeleza soka. Ikiwa katika mwaka wake wa saba tangu kuanzishwa kwake katika masoko hayo, mashindano hayo yameendelea kuwa na nguvu zaidi kukiwa na washindi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia.

Kenya ilitwaa ushindi mwaka 2016, Korea kusini (2015), Vietnam (2014), Thailand (2013) na Singapore (2012). Michuano hiyo kwa kaiwada ina sehemu tatu kuanzia nchi wenyeji, kikanda na fainali zake hufanyika viwanda vya Anfield – Uingereza. Mwaka huu benki hiyo imebadili mfumo wa michuano na kwamba mshindi atapata tuzo na kwenda Anfield.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank nchini Tanzania, Bw. Sanjay Rughani, alisema kwamba mwaka huu kutakuwa tofauti na kwamba mshindi wa mashindano ya ndani yenye timu 32 atatwaa kombe na  kwenda kuangalia mtanange wa ligi kuu ya England.

Timu zitakazoshiriki ni pamoja na wateja wa benki hiyo na michuano hiyo itaanza Juni 23 mwaka huu. Mwaka jana mashindano hayo yalikuwa ya kikanda ambapo timu kutoka Tanzania, Kenya na Uganda zilichuana vikali na timu ya Tanzania ya Azania – Mikoani Traders  walishinda na kwenda kwenye fainali Anfield.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akitoa utambulisho kwa meza kuu wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia kwenda kushoto ni Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa Kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu, Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo, Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( wa pili kushoto) akizungumzia ziara ya nyota na nahodha wa zamani wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu akielezea kuhusu safari yao ya Anfield ambapo aliongeza na kusema amefurahishwa na msimu huu ambapo mashindano hayo hayashirikisha timu za nchi jirani wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo akizungumzia  ujio wa Hyypia ambapo alisema ni nafasi adhimu kwa timu yake kunolewa na nahodha huyo wakati wakijiandaa na mashindano ya mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana, katika mkutano na waandishi wa habari kwenye hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) ya uzinduzi wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kulia) akitoa salamu za TFF ambapo aliipongeza benki ya Standard Chartered nchini kwa kuinua soka la Tanzania kimataifa kupitia mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashinano hayo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba.
Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (wa kwanza kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( kushoto) wakizundua sanamu ya nyota na nahodha wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba ( wa kwanza kulia), Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu (wa pili kushoto) pamoja na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (wa tatu kulia).
Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (wa kwanza kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani ( kushoto), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (wa kwanza kulia), Kocha wa timu ya Azania ambao ni mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2017, Saleh Hafifu (wa pili kushoto) pamoja na Kocha wa Serengeti Boys (U17), Oscar Milambo (wa tatu kulia) wakipata picha ya ukumbusho baada ya kuzindua sanamu ya nyota na nahodha wa Liverpool, Sami Hyypia anayetarajiwa kutua nchini Juni 20 wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waandishi wa habari na wadau wa michezo waliohudhuria wa sherehe za uzinduzi wa awamu tatu wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HERI YA MAADHIMISHO YA MWAKA MMOJA WA SPORTPESA,BADO TUNAIKUMBUKA ZIARA YA EVERTON

$
0
0
Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa siku ya Jumatano ya Mei 9, imetimiza mwaka mmoja tangu ilipoanza uendeshaji wa shughuli zake za kibiashara nchini.SportPesa ambayo imeanzia nchini Kenya mwaka 2014, iliingia Tanzania kwa kishindo ikiwa imejidhatiti katika kusaidia kukuza sekta ya michezo ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii.Katika kutimiza azma yake, SportPesa ilianza kwa kutoa mchango wa Shilingi Milioni 50 kusaidia maandalizi ya timu ya Serengeti Boys iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya vijana ya AFCON iliyofanyika nchini Gabon mwaka jana.

Baada ya hapo SportPesa iliendelea kuiteka sekta ya michezo nchini kwa kuingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano na vilabu vikongwe vya Simba na Yanga pamoja na mkataba wa mwaka mmoja na Singida United.Udhamini huo ulishuhudia vilabu vya Simba, Yanga na Singida United vikishiriki michuano mipya ya SportPesa Super Cup ambayo ilikuwa na lengo na kumpata mshindi mmoja atakayechuana na klabu ya Everton.


Kwa takribani wiki moja (kuanzia Juni 5-11), uwanja wa Uhuru ulifurika mashabiki lukuki waliokuja kushuhudia ladha ya michuano hiyo ambayo pia vilabu vya Gor Mahia, AFC Leopards, Tusker na Nakuru All Stars kutoka Kenya sambamba na Jang’ómbe kutoka Zanzibar vikitoana jasho kuzisaka zaidi ya Shilingi Milioni 60.

Ziara ya Everton
Sote ni mashahidi jinsi SportPesa ilivyojitoa mhanga kuileta nchini klabu ya Everton ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya EPL kutembelea Tanzania na hivyo kuitangaza vyema nchi yetu kimataifa.Sahau kuhusu mashabiki waliofurika uwanja wa Taifa Julai 13 kumshuhudia Wayne Rooney akivaa uzi wa Everton kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, dhidi ya Gor Mahia, lakini sote ni mshahidi jinsi ziara ile ilivyoleta manufaa makubwa.
Tunakumbuka jinsi sekta ya utalii ilivyonufaika ambapo Balozi wa Everton, Leon Osman alipata fursa ya kutembelea Kreta maarufu ya Ngorongoro bila kusahau jinsi uwanja wetu wa taifa ulivyoweza kurekebishwa kwenye sehemu ya kuchezea na vyumba vya kubadilishia nguo ili kufikia viwango vya kimataifa kwa Everton kuweza kuutumia.Lakini pia hatuwezei kuzisahau semina za uongozi wa Soka zilizotolewa na wataalam wa Everton kwa viongozi wetu wa soka bila kusahau kliniki za soka za vijana na misaada mbalimbali ya kijamii waliyotoa kwa wale wenye uhitaji.

Bajaji 120 Achilia mbali sekta ya michezo, lakini SportPesa pia imefanya promosheni za aina yake zilizokuwa na lengo ka kuinua kipato cha mtanzania mmoja mmoja.Shinda na SportPesa” ilikuwa gumzo kwa zaidi ya siku 170 kuanzia Oktoba mwaka jana ambapo watanzania 120 waliweza kujishindia bajaji mpya aina ya TVS KING kila siku, kila wiki.Ama hakika familia 120 zina neno la shukrani kwa SportPesa kutokana na uwezeshaji ule ambao tumeshuhudia jinsi ulivyotoa ajira kwa vijana wa kitanzania.

Sio rahisi kuilezea SportPesa kwa Makala moja kwani mambo ambayo wamefanya kwa kipindi cha mwaka mmoja ni mengi na makubwa.Kwa niaba ya wapenda michezo wote nchini, tunapenda kuitakia kampuni ya SportPesa Heri ya maadhimisho ya mwaka mmoja na hakika hatutaweza kuisahau ziara ya Everton kwani ilimfumbua macho kila mmoja wetu na kuona kuwa kila jambo linawezekana kama tukiweka nia.

TUKIO LA CAREER DAY:CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI ,LAWAKUTANISHA WAHITIMU NA WAAJIRI

$
0
0
Na Dixon Busagaga,Moshi 

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU) ,Prof, Faustine Bee ameshauri kuanzishwa kwa ujasiliamali wa Kiushirika utakao saidia wahitimu wa vyuo vikuu nchini kujipatia kipato na kuongeza kasi ya ukuzaji wa Uchumi kabla ya kupata ajira ya kudumu.

Katika maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere uliopo chuoni hapo ,Prof Bee alitolea mfano, moja ya changamoto zilizopo kwa baadhi ya vyama vya ushirika kwa kukosa wataalamu wa kuweka vizuri hesabu ya vitabu vyao.

“Pamoja na juhudi hizi binafsi za kwenda kutengeneza ajira na kuanzisha ujasiliamali wa mtu mmoja mmoja ,ni vema sasa tuone namna ambavyo tutaanzisha ujasiliamali wa kiushirika kwa maana wahitimu wa chuo kikuu wanapo maliza waende kuanzisha vyama vya ushirka vya aina tofauti.”alisema Prof Bee.

“Kuna vyama vina shida ya uandishi wa hesabu wa vitabu vyao ,tupate ambao watakuwa wakifanya kazi hiyo na watakuwa wakijipatia pesa,lakini pia wapo wengine ambao wangeweza kuanzisha vyama vya ushirika vya aina tofauti ,vya fedha, vya mazao ,vya uvuvi, ili mradi viongeze kasi ya ukuzaji wa uchumi wetu na pia kutengeneza ajaira kwa atu wengine .aliongeza Prof ,Bee.

Maadhimisho ya siku hii yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere uliopo chuoni hapo yalitanguliwa na maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na kuuzwa na wanafunzo wa chuo hicho pamoja na uwasilishaji wa mada ambapo mgeni rasmi katika tukio hilo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akaikumbusha menejimenti ya chuo sehemu ya wajibu wa chuo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira (katikati) akiwa ameongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) Prof, Faustine Bee ( mwenye tai) alipowasili chuoni hapo kwa ajili ya tukio la Career Day ,tukio ambalo Mghwira alikuwa mgeni rasmi .
Baadhi ya Wanafunzi na wageni mbalimbali waliohudhuria tukio la Career Day lililofanyika katika ukumbi wa Mwl Nyerere ,Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa tukio la Career Day alipoalikwa kuwa mgeni rasmi ,tukio hilo limefanyika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) Prof,Faustine Bee akizungumza katika tukio hilo .
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala na Fedha wa Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MOCU) Prof Freddy Kilima akizungumza wakati wa tukio la Career Day .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Pro Faustine Bee wakifurahia kazi ya Sanaa ya uchoraji iliyofanywa na mwanafunzi wa Mwaka wa tatu wa Shahada ya Sheria katika chuo hicho ,Omega Lyimo .

Maandalizi ya ukarabati wa Beit El Ajaib yaiva

$
0
0
Na Salum Vuai, WHUMK
MAANDALIZI ya matengenezo ya jengo la Beit Al Ajaib lililoko Forodhani mjini Zanzibar yameanza kufuatia ziara ya ujumbe kutoka Wizara ya Urithi na Utamaduni ya serikali ya Oman.

Ujumbe huo unaoongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Salum Mohammed Mahruki, uliwasili nchini jana Mei 11, na leo ulitembelea jengo hilo kujionea hali halisi ya uchakavu uliosababisha lisite kutumika kama kivutio cha utalii kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Msafara wa timu hiyo pia umemjumuisha mshauri mwelekezi ambaye ni mtaalamu wa uhifadhi majengo Dk.  Enrico d’Errico, ambaye amekuja mahsusi kushauri njia bora ya kulitengeneza jengo hilo na mengine ya kihistoria nchini.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha watendaji wakuu wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Urithi na Utamaduni ya Oman Salum Mohammed Mahruki, aliomba jengo hilo lisafishwe haraka, wakati wataalamu wakifanya tathmini ya kina ili kujua ukubwa wa kazi hiyo.

“Kwa namna tulivyoliona jengo hili, ni lazima kazi ya kulitengeneza ianze haraka iwezekanavyo, vyenginevyo tutazidi kuchelewa kwani tayari muda mwingi umepotea tangu lilipopata hitilafu,” alisisitiza.

Alifahamisha kuwa, sura ya Mji Mkongwe wa Zanzibar inaongezewa haiba na kuwepo kwa jengo hilo, ambalo kila mtalii anayefika anastaajabishwa na kuvutiwa na utaalamu pamoja na malighafi zilizotumika kulisimamisha tangu mwaka 1883.
 OFISA Mkuu wa Idara ya Makumbusho Abdalla Magofu (aliyeshika mwamvuli), akitoa maelezo kwa ujumbe kutoka serikali ya Oman juu ya hali ya jengo la Ngome Kongwe lililoko Forodhani mjini Zanzibar. Kulia kwa ofisa huyo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Urithi na Utamaduni nchini Oman, Salum Mohammed Mahruki.
  MSHAURI Elekezi na mtaalamu wa uhifadhi majengo kutoka Wizara ya Urithi na Utamaduni nchini Oman Dk. Enrico d’Errico (kushoto), akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo Salum Mohammed Mahruki na wajumbe wengine, walipolitembelea jengo la Beit El Ajaib mjini Zanzibar, ambalo serikali ya Oman inakusudia kulifanyia matengenezo makubwa.
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe Zanzibar Issa Sariboko Makarani, Katibu Mkuu wa Urithi na Utamaduni wa Oman, watendaji wakuu wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakiliangalia kwa nje jengo la Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Unguja, walipofanya ziara kukagua majengo ya kihistoria yanayohitaji kufanyiwa matengenezo.


WADAU WA UTALII WAKUTANA KUJADILI MPANGO KABAMBE WA MIAKA KUMI KUENDELEZA HIFADHI YA TAIFA YA MAHALE MKOANI KIGOMA.

$
0
0

Na Editha Karlo wa blog ya Jamii,Kigoma

WATANZANIA wametakiwa kujenga tabia ya kutembelea hifadhi za Taifa mbalimbali zilizopo nchini ili kuweza kujionea urithi na vivutio adimu vilivyopo kwenye hifadhi hizo.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga aliyasema hayo leo wakati warsha ya siku moja ya wadau mbalimbali wa Mkoani Kigoma wa Hifadhi ya milima ya mahale kilichokuwa kinajadili mpango kabambe wa miaka kumi wa kuendeleza hifadhi ya Taifa ya mahale.

Alisema katika Mkoa wa kigoma tumepata bahati ya kuwa na hifadhi mbili za Taifa ambazo ni hifadhi ya Taifa ya milima ya Mahale na Hifadhi ya Taifa ya gombe hivyo lazima juhudi za kutangaza hifadhi hizo ziongezeke.

"Tunajua Hifadhi ya mahale inachangamoto ya usafiri wa kufika kule kwani ili kufika inakulazimu kusafiri kwa njia ya maji kwa muda mrefu kutumia boti za kawaida,tunaomba mtuwekee speed boti, ila TANAPA mnafanya kazi kubwa ya kuhakikisha watalii wanaweze kufika Mahale kwa njia ya barabara"alisema Maganga

Maganga alisema kuwa mtu mmoja anapotembelea hifadhi ni sawa na watu kumi wametembelea kwani akitoka huko anakuwa balozi wa wengine.Mkuu huyo wa Mkoa alisema pia kupitia sekta ya utalii lazima iendane na kauli mbiu ya serekali ya sasa ya Tanzania ya viwanda."Hawa watalii kutoka nchi mbalimbali wanaokuja kutembea vivutio vyetu pia huwa wanaangali wapi pa kuwekeza tutumie fursa hizo za kuwashawishi waje kuwekeza nchini"alisema

Naye Ahmed Mbugi meneja wa ujirani mwema wa hifadhi ya milima ya mahale kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la hifadhi la Taifa(TANAPA)Allan Kijazi amesema kuwa ili mpango huo uweze kufanikiwa wamekusanya maoni mbalimbali ya wadau kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoa na leo maoni hayo wanayawasilisha kwa wadau mbalimbali kupitia warsha hiyo.

Mbugi alisema kuwa wao kama shirika wanajitahidi mahitaji yote muhimu yanapatikana kwa wageni wanaoenda kutembelea hifadhi.Alisema Hifadhi ya milima ya mahale inachangamoto ya usafiri ambapo miundombinu ya barabara ya kwenda huko haikuwa rafiki hapo awali lakini sasa hivi toka barabara itengenezwe watalii wameongezeka kwenda mahale.

Alisema kupitia mpango huo kabambe wa kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale ambao umewashirikisha wadau wa ngazi zote baada ya miaka kumi hifadhi ya milima ya mahale ili kukabiliana na changamoto zinazoikumba hifadhi hiyo.
 Picha ya pamoja baina ya wadau mbalimbali wa utalii wa Mkoa wa Kigoma na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali mstaafu Emanuel Maganga muda mfupi baada ya kuzindua warsha ya kujadili mpango kabambe wa miaka 10 wa kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa utalii wa Mkoa wa kigoma inayojadili mpango kabambe wa miaka 10 ya  kuendekeza hifadhi ya Milima ya Mahale
 Meneja wa ujirani wa hifadhi ya milima ya Mahale, Ahmed Mbugi akielezea hifadhi ya milima ya mahale kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan Kijazi kwenye kikao cha wadau wa utalii wa kuendeleza hifadhi ya Mahale
 Wadau wa utalii wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika warsha ya siku moja ya kupitisha mipango kabambe ya miaka 10 ya kuendeleza hifadhi ya milima ya mahale

JAFO AKERWA NA GHARAMA KUBWA ZA UJENZI WA BWENI ENDASAK

$
0
0
.Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Seleman Jafo amesikitishwa na gharama kubwa iliyotumika katika ujenzi wa Bweni la wanafunzi katika Shule ya Sekondari Endasak.

Ameyasema hayo wakati akikagua bweni la shule ya Sekondari ya Endasak leo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara.Amesema hajaridhishwa na gharama kubwa iliyotumika ya shilingi milioni 175.6 ya ujenzi wa Bweni moja wakati katika maeneo mengine fedha hizo hutumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni mawili.

"Inasikitisha sana kuona dhamani ya jengo lililojengwa haliwndani na fedha Ilizotolewana Serikali" Anasema Jafo.Amewataka viongozi w halmashauri kusimamia miaradi ya maendeleo kwa weledi na umakini mkubwa ili iendane na dhamani ya fedha zinazotolewa na Serikali.

Wakati huohuo, Mkuu wa Shule ya Endasak Mwl. Gisera Msofe amemueleza Mhe.Jafo kuwa Ujenzi wa bweni la wanafunzi wa shule hiyo umegharimu shilingi bilioni 170.6@ na mradi huo unatekelezwa kwa njia ya" Force Account"

Aidha ameishukuru Serikali kwa utoaji wa elimu bila malipo na ujenzi wa bweni kwa kuwa wanafunzi wengi wanapata elimu bila kuchangia na kuongeza hamasa kwa wazazi kusomesha watoto.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) akizungumza katika ukaguzi wa bweni la shule ya Sekondari ya Endasak
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) akikagua bweni la shule ya Sekondari ya Endasak
Bweni la shule ya sekondari Endasak
Wanafunzi wa shule ya sekondari Endasak
 

MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akijibu miongozo  mbalimbali ya wabunge leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Mhandisi Isaac Kamwelwe wakati wa kikao cha ishirini na tisa cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Dk.Adelardus Kilangi wakati wa kikao cha ishirini na tisa cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Charles Tizeba  akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Dk.Adelardus Kilangi akiteta jambo na Mbunge wa Vunjo Mhe.James Mbatia wakati wa kikao cha ishirini na tisa cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
Picha zote na Daudi Manongi.MAELEZO-DODOMA.

MWAKILISHI WA JIMBO LA TUNGUU AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA CHUO KIKUU ZANZIBAR (ZU)

$
0
0
  MWAKILSHI wa Jimbo la Tunguu Simai Mohamed Said akisalimiana na Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu Zanzibar (ZU) Pr. Musta Roshash alipofika ofisini kwake Chuoni hapo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
 MWAKILSHI wa Jimbo la Tunguu Simai Mohamed Said akisaini kitabu cha Wageni baada ya kufanya ziara ya kutembelea Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU).
 MWAKILSHI wa Jimbo la Tunguu Simai Mohamed Said katikati akizungumza na Wakuu wa chuo hicho kushoto kweke ni Makamo Mkuu wa Chuo hicho Pr. Musta Roshash kulia ni Mkuu wa Utawala Ahmad Majid Ali.
 MWAKILSHI wa Jimbo la Tunguu Simai Mohamed Said akizungumza na baadhi ya  wanafunzi  wanaotoka Nje ya Nchi ya Tanzania alipofanya ziara ya kutembelea chuoni hapo.
  MWANAFUNZI kutoka Nchi ya Zambia Cristina akizungumzia changamoto na mafanikio mbalimbali zinazowakabili chuoni hapo.
 MWANAFUNZI kutoka Nchi ya Malawi Hassan akichangia baadhi ya changamoto wanazozipata na kumtaka Mwakilishi huyo kuwasaidia kuzitatua changamoto hizo.
 BAADHI ya Wanafunzi kutoka Nje ya Nchi yaTanzania wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu alipofanya ziara ya kutembelea Chuoni hapo.
MWAKILSHI wa Jimbo la Tunguu Simai Mohamed Said alievaa suti akipiga picha ya pamoja na wanfunzi wanaoteka Nje ya Nchi ya Tanzania (Picha na Abdalla Omar Maelezo - Zanzibar).

MUHIMBILI KUFUNGA MASHINE YA KUDHIBITI TAKA HATARISHI

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili inatarajia kufunga mashine ya kisasa ya utasishaji taka ambayo itapunguza uchomaji wa taka za plastiki ambazo zina madhara kwa binadamu Mashine hiyo yenye thamani ya Dola Laki moja imetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo (UNDP) hivyo Hospitali ya Taifa Muhimbili itakua hospitali ya kwanza ya Umma kuwa na mashine hiyo. 
 Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni kutoka UNDP ambao umekuja kwa lengo la kukagua utekelezwaji wa mradi wa mazingira , Mkuu wa Idara ya Mazingira MNH Muhandisi Veilla Matee amesema mashine hiyo itafungwa wiki hii na wiki ijayo itaanza kufanya kazi na kutoa fursa kwa kampuni mbalimbali kuja kununua malighafi ambayo hutumika kutengeneza vifaa vya plastiki. ‘’ Tumepokea mashine ya utasishaji kutoka UNDP na mara baada ya kufungwa mashine hiyo tutatoa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo watendaji wetu ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi, mbali na kupewa mashine hiyo ya kisasa pia UNDP wametupatia vitendea kazi mbalimbali vya kuhifadhi taka ambavyo vitatusaidia sana katika mradi huu ’’amefafanua Injinia Matee. 
Hospitalia ya Taifa Muhimbili kwa siku huzalisha taka hatarishi kilo 800 kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa inayowahudumia . Mradi huo wa mazingira unasimamiwa na Idara ya Mazingira kwa kushirikiana na Kitengo cha Uhakiki na Ubora Muhimbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru akizungumza na ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia  Maendeleo (UNDP) ambao umekuja kuangalia utekelezwaji wa mradi wa mazingira . UNDP wametoa msaada wa mashine ya kisasa ya utasishaji ambayo itasaidia kupunguza uchomaji wa taka za plastiki.

Taka 02: Mkuu wa Idara ya Mazingira Muhandisi Veilla Matee akiwasilisha mada  kuhusu uzalishaji wa taka Muhimbili kwa wadau mbalimbali wa mazingira ambao wameambatana  na ujumbe kutoka UNDP .

Mkuu wa Idara ya Mazingira Muhandisi Veilla Matee akiwasilisha mada  kuhusu uzalishaji wa taka Muhimbili kwa wadau mbalimbali wa mazingira  ambao wameambatana na ujumbe kutoka UNDP .
Wadau hao wakimsilikiza Muhandisi Matee  alipokua akifafanua jambo wakati wa tukio hilo.
Mshauri wa masuala ya Mazingira kutoka UNDP Zambia Bi. Winnie Musonda akiuliza swali mara baada ya kuwasilishwa kwa mada hiyo mapema leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA BANDARINI DAR ES SALAAM KUKAGUA MATANKI YA MAFUTA YA KULA

$
0
0
8
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Doto James, mwenye kofia ngumu ya njano ni Mkurugenzi wa kampuni ya uingizaji mafuta nchini TLS & VOT Bw. Claudio Ghirardi, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Olesante ole Gabriel anayefuatiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuchunguza mafuta ya Kula na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Profesa Joseph R. Buchweishaija.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa maelekezo na kuulia maswali alipowasili eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018, Nyuma yake ni Mkurugenzi wa kampuni ya uingizaji mafuta nchini TLS & VOT Bw. Claudio Ghirardi,
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitoa pongezi kwa Bw. Ben Usage Asubisye baada ya kumpandisha cheo kuwa kamishna kamili kutoka Kaimu Kamishna wa Forodha na Bidhaa za Ndani katika Mamlaka ya Mapato (TRA) alipotembelea  eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiondoka eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018.
8
 ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akinunua mapapai na ndizi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akigawa mapapai na ndizi kwa wananchi nje ya eneo lenye matanki ya kuhifadhia mafuta ya kula baada ya kushushwa melini alipofanya safari ya ghafla kukagua uingizwaji na ugawaji wa ulipiaji wa ushuru  bidhaa hiyo kwenye bandari ya Dar es salaam leo Mei 15, 2018.



Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images