Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

MFANYABIASHARA ALIYEFICHA MAFUTA YA KUPIKIA AKAMATWA RUVUMA

0
0
Katika hali isiyo ya kawaida mkuu wa mkoa wa Ruvuma CHRISTINA MNDEME amefanya ziara ya kushtukiza katika maghara ya kuhifadhia bidhaa ikiwemo mafuta ya kupikia na kukuta shehena ya mafuta hayo yakiwa yamefishwa katika maghara hayo, na kuagiza wamiliki wa bidhaa hiyo kukamatwa mara moja.

BALOZI WA IRELAND ASIFU MUHIMBILI KWA KUBORESHA HUDUMA

0
0
Balozi wa Ireland nchini Paul Sherlock leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la kuona maendeleo ya miradi mbalimbali  inayofadhiliwa na Serikali  ya Ireland.

Katika ziara hiyo Balozi Sherlock ameambatana na ujumbe wa watu saba wakiwemo wabunge watatu kutoka Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali nchini Ireland. Ujumbe huo umetembelea jengo la watoto katika wodi ya watoto wenye Saratani na jengo la wazazi namba moja wodi ya watoto wachanga .

Balozi huyo akipatiwa   maelezo  kuhusu watoto wenye Saratani Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tumaini la Maisha (TLM) Dkt. Trish Scanlan amesema TLM  wanashirikiana na MNH kuhakikisha wanaokoa  maisha ya watoto wenye saratani kwa kuwapatia matibabu  stahiki.

Akifafanua amesema ugonjwa wa Saratani  kwa watoto ambao unaongoza nchini ni Saratani ya damu, jicho , figo pamoja na saratani ya matezi.
  Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock akitambulisha ujumbe wa watu saba wakiwamo wabunge watatu wa Kamati ya Hesabu za Serikali ya Ireland kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru alipotembelea hospitali hiyo leo. Balozi huyo ameitembelea MNH leo ili kuona na kupatiwa maelezo ya miradi mbalimbali ya afya inayofadhiliwa na Serikali ya Ireland. Waliosimama nyuma ya Balozi huyo ni watumishi wa MNH wakiwamo wakurugenzi, wakuu wa idara na vitengo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na ujumbe wa watu hao leo.
  Mkuu wa Kitengo cha Saratani kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Rehema Laiti (kulia) akiwaeleza wabunge wa kamati hiyo jinsi wanavyowahudumia watoto wenye matatizo ya saratani waliolazwa kwenye hospitali hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tumaini la Maisha, Dkt. Trish Scanlan akieleza taasisi yake inavyotoa huduma ya tiba kwa watoto wenye saratani ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akiwa na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock katika hospitali hiyo.
 Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Paul Sherlock (kushoto) na ujumbe wake wakiwa picha ya pamoja na watendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

TENGA AZITAKA KLABU ZA LIGI KUU KUWEKEZA KWA VIJANA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Aliyekuwa Rais wa Zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) Leodegar Tenga amewataka uongozi wa klabu za Kandanda nchini   kuwekeza katika soka la Vijana ili kupunguza matumizi ya kununua wachezaji wa kigeni.

Akizungumza na Globu ya jamii Michuzi, Tenga amesema kuwa klabu hizo zinatakiwa zitambue umuhimu wa kuwekeza kwenye kuandaa wachezaji wa baadae ilo kuweza kupunguza ununuaji wa wachezaji ambao kwa muda mwingine huwezi kupata mchezaji yule unayemtaka na ukimpata atakua na gharama kubwa.

"Ukitaka mafanikio lazima utengeneze mchezaji, klabu zetu zikiwa na mfumo huo wa uwekezaji kwa soka la vijana zitapunguza gharama kubwa wanazozipata kwa kununua wachezaji ambao kwa muda mwingine utapata mchezaji ambaye hujawahi kumuona uwezo wake na ukimtaka wa kiwango cha juu basi gharama zitakuwa kubwa," amesema Tenga.

Amesema, mafanikio yanakuja taratibu ila klabu zinatakiwa kukubali kwa mwaka mmoja au miwili kutengeneza timu bora kwa kuwaandaa wachezaji wako mwenyewe.

Tenga alitoa ushauri huo kwa klabu hizo baada ya kuona timu za Vijana zikiweza kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali nchini ikiwemo Serengeti Boys kurejea nchini wakiwa na kombe la CECAFA Challenge kwa vijana wenye umri wa miaka 17.

"Tumeona vijana wakipambana na kwa bahati nzuri mimi nilikuwepo  Kule Burundi mashindano yalikofanyika, pamoja na changamoto za Mvua vijana waliweza kupambana na walicheza vizuri na kuibuka na ushindi huo ambao umeleta kombe nyumbani,"amesema Tenga.

" Baada ya miaka kadhaa  tutakuwa na timu nzuri ya taifa kwani tutakuwa na wachezaji wengi waliokulia katika misingi mizuri ya kimpira".

Mbali na kuwa Rais wa TFF ,Tenga alicheza mpira kwa mafanikio makubwa katika klabu ya Yanga miaka ya 80 sambamba na katibu mkuu wa Yanga wa sasa Charles Mkwasa.

Halmashauri Wilaya ya Longido yapewa siku 7 kuhakikisha imejibu hoja zote zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG)

0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Longido imepewa siku 7 kuhakikisha imejibu hoja zote zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) kwa mwaka fedha kuanzia 2015 hadi 2017.

Akitoa agizo hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amesema halmashauri kupata hati ya mashaka kwa hoja zinazojibika na zinazojirudia kila mwaka ni uzembe wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo.

“Watumishi bado wapo wachache wanaofanya kazi kwa mazoea bila ya kufuata sheria na taratibu za kiutumishi”.Ameuwagiza uongozi wa halmashauri ya Longido kutoa barua za onyo kwa watumishi wote waliotajwa kwenye taarifa ya mkaguzi wa nje ili iwe fundisho kwa watumishi wote umma.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega,amesema ifike wakati sasa viongozi kutoonea huruma mtumishi yoyote anaebainika ana makosa, kwani hoja nyingi katika halmashuri hiyo zimekuwa zikijirudiarudia kila mwaka.Amesema hatua madhubuti ni lazima sasa zichukuliwe ili kudhibiti tabia hii ya mazoea ya hoja kujirudiarudia kila mala.

Akisisitiza zaidi mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo amesema kazi ya viongozi ni kusimamia sheria na taratibu za kazi,hivyo ataendelea kusimamia sheria za utumishi wa umma katika halmshauri yake kwani mpaka sasa hali imeanza kubadilika kwa watumishi kuwa na nidhani.

Aidha, amesema halmshauri ipo tayari kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na mkuu wa mkoa na kuhakikisha halmashauri yake haitapata tena hati ya mashaka kwa miaka inayokuja.Gambo yupo katika ziara ya siku 3 wilayani Longido ambapo atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanywa katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Longido alipokuwa akuzungumzia hoja za CAG.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Daniel Chongolo akimchukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo baada ya kutoa maelekezo ya namna ya kujibu hoja za CAG.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, akisoma baadhi ya hoja zilizotolewa na mkaguzi wa nje (CAG) katika kikao chake na watumishi wa halmashauri ya Longido.

RC Wangabo aagiza DED kuchunguzwa

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuanzisha mchakato wa kinidhamu na uchunguzi mara moja dhidi ya Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wialaya ya Kalambo kutokana na utendaji kazi wake usioriddhisha..

Amesema kuwa mkurugenzi huyo amekuwa akichelewesha juhudi za serikali baada ya kushindwa kumaliza ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya cha Mwimbi kwa wakati na kuchelewa kuanza ujenzi wa kituo kipya cha afya cha Legeza mwendo hata baada ya kupatiwa Shilingi Bilioni 1.1 na serikali kwaajili ya vituo vyote viwili vilivyopo katika halmashauri hiyo.

“Huyu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo utendaji wake siridhwi nao hata kidogo katika mazingira ya sekta ya afya kwa ujumla wake, ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika kituo cha afya cha Mwimbi ulianza mwezi wa nane mwaka 2017 mpaka leo naongea hapa mwezi wa tano mwaka 2018 kituo cha afya kile bado hakijakamilika,” Alisema

Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wauguzi katika siku yao ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kimkoa katika kata ya Laela, Wilaya ya Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo .

JAFO AKEMEA WIZI WA VYUMA VYA MADARAJA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea wananchi wenye tabia mbaya ya kuiba vyuma vinavyo wekwa katika kingo za madaraja kwamba watakapobainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

 Jafo ametoa onyo hilo alipokuwa wilayani Nzega mkoani Tabora alipokwenda kukagua aneo la Nhombola panapotarajiwa kujengwa daraja kubwa katika mwaka wa fedha 2018/2019.

Daraja la Nhombola ni moja ya ahadi ya Rais John Magufuli ambapo katika mwaka wa fedha 2018/2019, Ofisi ya Rais TAMISEMI imetenga Sh.milioni 500 kupitia wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo.

Akikagua eneo hilo, Waziri Jafo amesema baadhi ya watu wana tabia ya wizi wa vyuma ambavyo wanakwenda kuviuza kama vyuma chakavu. Jafo amesisitiza kwamba Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hivyo wananchi wanapaswa kuilinda miundombinu hiyo kwani inapo haribiwa wao ndio wanaotaabika. 

Amemtaka kila mmoja awe mlinzi wa miundombinu inayogharamiwa na serikali yao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Tabora na wilaya ya Nzega wakikagua eneo ambalo miundombinu ya barabara itapitishwa.
 Viongozi wakikagua eneo litakapojengwa daraja la Nhombola 
Wananchi wakiwa upande wa pili wa mto katika eneo ambalo litajengwa daraja la Nhombola.

MADHIMISHO YA KIMONDO CHA MBOZI KUFANYIKA MWEZI JUNI MKOANI SONGWE

0
0
Na Hamza Temba-WMU-Songwe

Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na wadau wengine wa uhifadhi na maendeleo utafanya maadhimisho ya siku ya Kimondo cha Mbozi kwa mara ya kwanza katika historia kwenye Kijiji cha Ndolezi Kata ya Mlangali, wilayani Mbozi kuanzia Juni 28 hadi 30 mwaka huu .

Maadhimisho hayo yataenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Vimondo duniani ambayo yaliazimiwa kufanyika Juni 30 kila mwaka na kikao cha Umoja wa Mataifa cha tarehe 6 Desemba, 2016.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho pia kiliazimia tarehe hiyo kuwa siku ya kuelimisha umma kuhusu elimu ya anga na mafanikio ya tafiti mbalimbali yaliyopatikana kuhusu elimu hiyo, kutambua juhudi zilizofanyika, kuweka sheria za kimataifa na kutoa tahadhari juu ya athari zinazoweza kutokea endapo dunia itafanya uharibifu juu ya anga.

Taarifa hiyo imetolewa jana katika Kijiji cha Ndolezi wilayani Mbozi na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Herman Tesha wakati akiwasilisha taarifa ya maandalizi ya maadhimisho hayo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga ambaye alitembelea kituo hicho kwa ajili ya kukagua shughuli za maandalizi.

Amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutangaza Kimondo kama kivutio muhimu cha utalii mkoani Songwe pamoja na vivutio vingine vya mkoa huo kwa ujumla ili kutoa fursa ya uwekezaji kwenye sekta ya utalii mkoani humo. 

Amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na kongamano la uwekezaji na sayansi ya vimondo, maonesho ya malikale, maonesho ya kiutamaduni, mashindano ya riadha (Kimondo Marathon), mashindano ya netiboli na mpira wa miguu (Kimondo Ligi).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiangalia Kimondo cha Mbozi alipotembelea kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua mpaka wa eneo la kituo cha kimondo na vijiji jirani alipotembelea kituo hicho cha utalii  katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akikagua kituo cha taarifa cha Kimondo cha Mbozi alipotembelea kituo hicho cha utalii  katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimondo duniani yatakayofanyika Juni 28 hadi 30 mwaka huu. Kimondo cha Mbozi ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika na kinakadiriwa kuwa na tani 12 na mchanganyiko wa madini ya Chuma 90%, Nickel 8.69%, Copper 0.66%, Sulphur 0.01% na Phosphorus 0.11.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya watalii wa ndani waliotembelea kituo cha utalii cha kimondo katika kijiji cha Ndolezi, wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Nyuma yao ni jengo jipya la kituo cha taarifa ambalo ujenzi wake umekamilika.

JAFO AKEMEA WIZI WA VYUMA VYA MADARAJA

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amekemea wananchi wenye tabia mbaya ya kuiba vyuma vinavyo wekwa katika kingo za madaraja kwamba watakapobainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

 Jafo ametoa onyo hilo alipokuwa wilayani Nzega mkoani Tabora alipokwenda kukagua aneo la Nhombola panapotarajiwa kujengwa daraja kubwa katika mwaka wa fedha 2018/2019.

Daraja la Nhombola ni moja ya ahadi ya Rais John Magufuli ambapo katika mwaka wa fedha 2018/2019, Ofisi ya Rais TAMISEMI imetenga Sh.milioni 500 kupitia wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo.

Akikagua eneo hilo, Waziri Jafo amesema baadhi ya watu wana tabia ya wizi wa vyuma ambavyo wanakwenda kuviuza kama vyuma chakavu. Jafo amesisitiza kwamba Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hivyo wananchi wanapaswa kuilinda miundombinu hiyo kwani inapo haribiwa wao ndio wanaotaabika. 

Amemtaka kila mmoja awe mlinzi wa miundombinu inayogharamiwa na serikali yao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi wa mkoa wa Tabora na wilaya ya Nzega wakikagua eneo ambalo miundombinu ya barabara itapitishwa.
 Viongozi wakikagua eneo litakapojengwa daraja la Nhombola 
Wananchi wakiwa upande wa pili wa mto katika eneo ambalo litajengwa daraja la Nhombola.

MVUA YAKATA DARAJA LA TABATA KISIWANI

0
0
Na Mdau wa blog ya jamii
Japokuwa mvua zinaendelea kunyesha, zikiwa zinaweza kuleta madhara makubwa katika barabara mbali mbali jijini Dar es Salaam na nchini kwa Ujumla lakini zipo barabara zinaweza kuokolewa iwapo watendaji husika watafanya kazi zao kwa weledi na bila kusukumwa na mamlaka za juu.

Napenda kutolea mfano barabara ya kutoka Tabata Mwananchi karibu kabisa na ofisi za gazeti la Mwananchi kuelekea Tabata Kisiwani, barabara hiyo imekatwa na maji yaliyoshindwa kupita katika matundu ya Daraja ambayo yameziba hiyo yakaamua kutafuta njia mbadala ya kupitia.

Matundu hayo hayajaziba leo wala jana, yemeziba tangu mvua za awali, na mvua hizo zilikuwa zikisimama hata kwa wiki moja lakini hakuna jitihada zilizochukuliwa na wahusika kuzibua matundu hayo ili kuruhusu maji yapite na kutokuharibu tena barabara.

Unaweza kujiuliza, hivi kipindi mvua zinasimama mamlaka husika hazioni umuhimu wa kuzibua milango ya daraja hilo?, Je hawaoni mateso tunayoyapata wakazi wa Tabata Kisiwani? Je hawajui kuwa kukosekana kwa mawasiliano kati ya wakazi wa Tabata Kisiwani na sehemu zingine ni hatari kubwa hata kwa wagonjwa na akina mama wajawazito pale inapotokea dharura? Je wanataka hadi kiongozi wa juu ili awape maelekezo? na kama wanajua je wanataka kupata nini baada hiyo barabara kuharibika?

Mvua ya leo ndio imekata kabisa barabara nakufanya magari yashindwe kupita huku ile barabara ya kutokea upande wa Tabata Kimanga nayo haipitiki kwakuwa Makalavati yaliyowekwa yameliwa na maji hiasi cha magari kushindwa kupita, kwa ujumla hali si shwari kabisa.

Naziomba mamlaka zinazohusika pamoja na uongozi wa Tabata Kisiwani kuliona hili kama dharura, ili wakazi wa Tabata kisiwani na sisi tujione kama watanzania huru na wenye kustahili kuhudumiwa na watu wenye kupata malipo yanayotokana na kodi zetu, pia naiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuingilia kati suala hili ili kunusuru maisha ya wanatabata Kisiwani ili dharura itakapotokea tuweze kujitete kwa haraka.
 Muonekano wa Daraja la Tabara Mwananchi kuelekea Tabara Kisiwani lililovyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha baada ya maji kushindwa kupita kwenye matundu ya daraja hilo na kupita juu.
Muonekano wa Barabara ya kuelekea Tabata Kisiwani kutoka Tabata Mwananchi maji yakiwa yamejaa barabarani baada ya maji wengi kushidwa kupita katika matundu ya daraja lililopo katika barabara hiyo.

JAMII YAASWA KUJENGA MISINGI BORA YA MALEZI YA WATOTO –NKINGA

0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JAMII imeaswa kujenga misingi imara ya malezi ya  watoto ili wasiweze kuishi maisha ya mitaani na ambayo yanasababisha kokosa haki za kupata elimu pamoja na malezi mengine.

Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga wakati akizindua ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania, amesema kuwa sehemu salama ya kuishi watoto ni katika familia au jamii.

Amesema kuwa katika ripoti hiyo watoto wa kike wamekuwa wakionekana katika majira ya usiku wakijiuza huku watoto wakiume wanaonekana majira ya mchana na usiku.

Nkinga amesema kuwa serikali itafanyia kazi mapendekezo ya ripoti hiyo ili katika kuweza kuhakikisha watoto hao wanakwenda katika familia zao.

Amesema sababu zinazowafanya watoto kuishi na kufanya kazi mitaani  ni umasikini pamoja na ukatili wa kupindukia na kuamua baadhi ya watoto kutoroka katika familia zao na kuingia mitaani.

“Jamii iendelee  kuishi kwa amani na misingi bora katika malezi ya watoto katika kuhakikisha hawakimbilii mitaani kwa kuishi kwa kukosa chakula, elimu pamoja wengine kupoteza maisha kutokana na kupigwa “amesema Nkinga.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Railway Afrika, Peter Kent akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati ya shirika hilo katika masuala ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Mwakilishi Mkazi USAID Kizazi Kipya Project wa PACT Tanzania, Levina Kikoyo akizungumza jinsi ya utafiti waliofanya katika ripoti hiyo.
 Sehemu ya wadau mbalimbali wa masuala ya watoto waliohudguria katika uzinduzi wa ripoti ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akiwa na wawakilishi wa mashirika wakati wa uzinduzi ya Taifa ya Watoto wanaoishi na kufanya Kazi Mitaani nchini Tanzania uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Balozi Seif akutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya Kifalme ya Oman

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya  Kifalme ya Oman Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi alisema uwepo wa Jumla la Ajabu liliopo Forodhani Mji Mkongwe maarufu {Beit Al Ajaib}utaendelea kuwa utambulisho wa Zanzibar Kimataifa katika masuala ya Kihistoria na Utamaduni.

Alisema Jengo hilo Maarufu ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Dunia    tokea Karne ya 17 linastahiki kufanyiwa matengenezo makubwa ili kulirejeshea hadhi yake ya kawaida na Oman tayari imeshajitolea kugharamia matengenezo hayo.

Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi aliyeambatana na Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Bwana Hamud Al Has alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

Katibu Mkuu Salum alisema hatua ya Serikali ya Oman kujitolea gharama za Matengenezo ya Jumba hilo imekuja kutokana na Historia kubwa ya Uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Oman kwa Karne kadhaa zilizopita.

Alisema Historia ya pande hizo mbili zenye udugu wa Damu hasa katika masuala ya Utamaduni utaendelea kuwepo na kuimarishwa kwa faida ya Vizazi vya sasa na vile vitakavyokuja  hapo baadae.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya  Kifalme ya Oman Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi Kulia akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar. Katikati yao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed na Nyuma ya Balozi Seif ni Balozi Mdogo wa Oman aliyepo Zanzibar Bwana Hamud Al Has.
 Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi aliyenyanyua Mkono akielezea Mikakati ya Oman katika kuendeleza Uhusiano na Zanzibar wakati akizungumza na Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kutoka Kulia.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kwanza Kutoka Kulia akiishukuru Serikali ya Oman kwa misaada inayoendelea kutoa kwa Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Serikali ya  Kifalme ya Oman Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi aliyevaa Kilemba akifafanua jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao na Balozi Seif. Kushoto ya Bwana Salum Mohamed Al – Mahrooqi ni Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo na Kulia ya Balozi Seif ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 14/05/2018

WAZIRI UMMY AFUNGUA MDAHALO WA WABUNGE JIJINI DODOMA KUHUSU WAJIBU WA WAZAZI KATIKA MALEZI

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) azungumzia mafaniko na changamoto za ofisi yake

0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Profesa Mussa Juma Assad amesema ofisi yake imefanikiwa kutoa taarifa kwa wakati, kila inapofika Machi 30 ya kila mwaka licha ya kukabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti.
Profesa Assad ameeleza hayo leo jijini Dodoma kwenye mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ambao unalenga kupitisha bajeti ya mwaka na kujadili masuala ya kiutendaji ambayo yanawasilishwa na kuitishwa na wajumbe.
Akizungumza katika mkutano huo, CAG amesema ufinyu huo unaosababisha shughuli za kiofisi kutofanyika pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu ya dharula yanayoibuka nje ya ukomo wao wa bajeti.
“Baraza hii limekuwa na ufanisi mkubwa katika kusimamia majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye mkataba,”amesema Prof. Assad.
Amesema pamoja na mafanikio mbalimbali ambayo ofisi hiyo imeyapata, bado zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili na zinahitaji utatuzi wa kina.
Amezitaja changamoto nyingine kuwa ni kushindwa kukamilisha ujenzi kwa ajili ya Ofisi katika mikoa iliyolengwa kutokana na kutotolewa kwa fedha za maendeleo kama ilivyopangwa na kwa wakati.
Aidha amesema katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa Fedha 2017/18 hadi kufikia Machi, 2018 Ofisi ilishindwa kuwajengea uwezo watumishi kulingana na viwango vya kimataifa vya ukaguzi kutokana na ufinyu wa bajeti.
“Kuna changamoto ya mwenendo wa upatikanaji wa fedha za matumizi mengineyo na maendeleo kutoka mfumo mkuu wa serikali kutoendana na mahitaji halisi ya majukumu ya Taasisi hususani ukaguzi na mafunzo kwa watumishi,”amesema.
Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ,Utumishi, Dk.Laurean Ndumbaro ameitaka ofisi ya Taifa ya ukaguzi kutekeleza agizo la serikali kuhamishia shughuli zake mkoani Dodoma.
Dk. Ndumbaro amesema tayari viongozi mbalimbali wa serikali walishahamia, hivyo ni mategemeo yake kuwa Ofisi ya Taifa ya ukaguzi nayo pia ipo katika mkakati wa kuhamishia shughuli zake jijini Dodoma kama ambavyo taasisi nyingine zimefanya.


 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Asaad (kushoto) akiwa na  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro (kulia)wakifurahia jambo wakati aliokuwa kimsindikiza mara baada Katibu Mkuu huyo kufungua mkuatano mkuu  wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya CAG uliofanyika mjini Dodoma leo.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akizungumza wakati wa kufungua mkutano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) lililofanyika mjini Dodoma leo .
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya CAG.
 Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof Musa Asaad akitoa taarifa ya Ofisi yake wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya CAG lililofanyika leo jijini  Dodoma .
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dk.Laurean Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya CAG.
wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Ukaguzi

YANGA HAITAKAA KUISAHAU MICHEZO HII 7

0
0
Leo hii tumekusogezea Michezo 7 iliyochezwa na Timu ya Yanga katika michezo hiyo Yanga imetoa sale michezo miwili na kufungwa michezo mitano.

VOA Swahili: Duniani Leo Mei 14, 2018

KUMBUKUMBU ya Marehemu Mzee Stephano Mnyika

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA MEI 14, 2018

INVITATION TO ICT SHORT COURSES

DC SHINYANGA AFUNGUA WARSHA YA MASUALA YA JINSIA KWA WALIMU ILIYOANDALIWA NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

0
0
Warsha hiyo iliyoandaliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga kwa ufadhili wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga imefanyika leo Jumatatu Mei 14,2018 katika chuo hicho mjini Shinyanga kwa kukutanisha walimu 100.Warsha hiyo ni sehemu ya Mpango Maalumu uliobuniwa na Chuo hicho kwa ajili ya kujenga uwezo watumishi wa umma hasa walimu juu ya masuala ya jinsia.

Akifungua warsha hiyo,Matiro alisema mbinu stahiki za kupambana na ukatili wa kijinsia zitafanikiwa endapo dhana,aina,matokeo na sababu za ukatili zitaeleweka kuanzia ngazi ya msingi hususani shuleni ambapo watoto wanatumia muda mwingi wa maisha yao.“Niwapongeze sana kwa kuanzisha mpango huu wa kuwafikia walimu,warsha hii ni nyeti sana na huenda kuna walimu ambao walishawahi kushuhudia ama kutenda vitendo vya kibaguzi kwa watoto kwa kujua ama kutojua,kwa hali hii vitendo hivyo vina athari kubwa katika maendeleo ya kitaaluma kwa watoto”,alisema Matiro.

Aidha alisema ni jukumu la walimu na shule kuweka kanuni na taratibu ambazo zitatoa ulinzi na kusaidia jamii nzima ya shule kuishi kwa amani na kuzingatia usawa.“Niwaombe msiishie kwa walimu pekee kutoa elimu hii,bali wafikieni pia watumishi wote wa umma kwani nao kwa sehemu yao wana mchango mkubwa katika ujenzi wa jamii inayothamini usawa wa kijinsia”,aliongeza.
Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa warsha hiyo.Kushoto ni Mratibu wa Masuala ya Jinsia katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga,Getrude Pastory Massawe ambaye pia Afisa Masoko wa chuo hicho.Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo na kueleza kuwa kukosekana kwa usawa baina ya wasichana na na wavulana shuleni na katika jamii ni chanzo kikuu cha ukatili kitu kinachofanya ukatili kuwa suala la kijinsia.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kituo cha Shinyanga, Paschal Mheluka akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyokutanisha walimu 100 kutoka shule za msingi na sekondari zilizopo katika manispaa ya Shinyanga.
Mratibu wa Masuala ya Jinsia katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Shinyanga,Getrude Pastory Massawe ambaye pia Afisa Masoko wa chuo hicho akizungumza wakati wa warsha hiyo ambapo alisema wameamua kuanzisha mpango wa kutoa elimu ya masuala ya jinsia kwa walimu ili kuhakikisha walimu hao wanatoa elimu kwa wanafunzi wao kumaliza vitendo vya ukatili katika jamii.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.





Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images