Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

WAZIRI UMMY AZINDUA TAWI LA CCM KATA YA USAGARA APOKEA WANACHAMA 50 PAPO HAPO

$
0
0
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni  Mbunge wa Viti Malumu (CCM) mkoa wa Tanga akimkabidhi kadi ya CCM moja ya wanachama wapya waliojiungana chama hicho wakati alipokwenda kufungua tawi la CCM Kata ya Usagara leo ambapo jumla ya wanachama wapya 50 walipokelewa kulia ni Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini (CCM) Joseph Msukuma
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Malumu (CCM) mkoa wa Tanga akifungua tawi la CCM Kata ya Usagara leo ambapo pia alipokea wanachama wapya 50 walipokelewa kushoto ni Mbungewa Jimbo la Geita Vijijini (CCM) Joseph Msukuma kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Hamisi Mkoba
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazeena Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Malumu (CCM) mkoa wa Tanga akipandisha bendara ya Tawi la CCM Kata ya Usagara Jijini Tanga alipokwenda kufungua tawi la CCM kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Hamisi Mkoba na kulia ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Makorora kulia ni Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini (CCM) Joseph Msukuma
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazeena Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Malumu (CCM) mkoa wa Tanga akifungua tawi hilo


ZUHURA MAGANGA ATWAA KWA KISHINDO NAFASI YA UWENYIKITI TAPSEA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga (katikati) akishangilia sambamba na wanachama wenzake wa TAPSEA baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguli wao uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.  Mwenyekiti huyo amepewa ridhaa hiyo ya kukiongoza chama hicho kwa mara nyingine tena baada ya muda wake wa awali kumalizika, ambapo alimshinda mpinzani wake, Habiba Mhina kwa zaidi ya asilimia 90.
Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), wakishangilia ushindi wa Mwenyekiti wao baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa Chama chao kwa mujibu wa Katiba yao.
Uongozi Mpya wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania chini ya Mwenyekiti wake, Zuhura Maganga (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Mkutano wao Mkuu, uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu Zanzibar (SUZA), Tunguu, Zanzibar.

WATAALAMU WA NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO

$
0
0
Wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamefanya ziara katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni vilivyopo mkoani Morogoro. 

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa, kampuni ya State Grid iliyopewa kazi hiyo katika mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwasha umeme katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni tarehe 16 Mei, 2018.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (katikati) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika kijiji cha Mandera kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika ziara hiyo. Kulia ni Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Yusuph Msembele.
Moja ya transfoma zilizofungwa na kampuni ya State Grid katika kijiji cha Mandera kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Meneja Mwandamizi wa TANESCO- Kanda ya Kati, Mhandisi Atanasius Nangali ( wa pili kulia) akifafanua jambo katika ziara hiyo.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (kushoto) akimsikiliza mwananchi wa kijiji cha Kibaoni kilichopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Joseph Mkude (kulia) katika ziara hiyo.

Shindano la utunzi wa hadithi la Andika Challenge lazinduliwa

$
0
0
Na Mwandishi wetu
TAASISI ya Dr Ntuyabaliwe imezindua shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni wenye lengo la kuibua vipaji vya watoto katika kubuni na kutunga hadithi.

Shindano hilo linatarajiwa katika siku za usoni kufika Tanzania nzima.

Uzinduzi huo umefanywa katika shule ya msingi Kinondoni wilayani Kinondoni.

Akizindua shindano hilo Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya alisema shindano hilo ni muhimu kwa nchi hii hasa katika kukuza uwezo wa kusoma na kuandika na kuibua vipaji vya wanafunzi katika kukuza lugha ya Kiswahili na ubunifu.

Alisema kwamba serikali inafurahishwa na jinsi taasisi hiyo inavyofanywa ya kuibua vipaji vya watoto na kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuangalia usomaji wa vitabu na shindano la andika challenge.

Alisema anajua kwamba Taasisi hiyo ilianza na maktaba katika shule za msingi na kuhamasisha usomaji wa vitabu na sasa wanakuja na shindano hilo litakalosambaa nchi nzima.

Alisema andika challenge ni muhimu kwa watoto.

“Tunaamini kuwa tunaenda kukuza vipaji vya watoto…katika kutunga hadithi kwa kuongoza watoto katika kuhakikisha kwamba uchaguzi wa mada zinakuwa na maana zikizingatia fani na maudhui, moja ya tanzu au kipera cha simulizi “ alisema.
 Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga akizungumza machache na kuitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura, Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi pamoja na Afisa Elimu kata ya Mwananyamala, Joshua Biswalo wakiwa meza kuu.
 Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu wa shule ya msingi Kinondoni wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi pamoja na  Mtendaji wa Kata ya Mwananyamala, Mickidadi Ngatumbura (kushoto).
 Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya akitoa mkono wa pongezi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi wakati wa hafla ya uzinduzi wa shindano la Andika Challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza kuhusu vigezo vya kushiriki na zawadi kwa tano bora kwa wanafunzi wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni watakaoshiriki shindano la Andika Challengekatika hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba ya shule ya msingi Kinondoni mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi Brian Jackson wa darasa la saba shule ya msingi Kinondoni akitoa neno loa shukrani kwa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe kwa kuzindua shindano hilo la andika challenge wakati hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwanafunzi Blessing Elianoki wa darasa la sita.
 Mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi wakizundua shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waandishi wa habari na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni waliohudhuria uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Kinondoni waliowakilisha wenzao katika hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni iliyofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Kinondoni mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe, Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Esther Kaaya, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kinondoni, Bw Emmanuel Ntenga pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliowakilisha wenzao katika hafla fupi ya uzinduzi wa shindano la andika challenge kwa watoto wa shule za msingi manispaa ya Kinondoni uliofanyika kwenye ukumbi wa maktaba shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wanawake wajipumzisha Kunduchi, wasema wanastahili kupumzika

$
0
0
WANAWAKE wamama wanastahili kupewa nafasi na jamii kupata muda wa kupumzika na kufurahia maisha kutokana na wao kuwa wafanyakazi wa mwaka mzima.

Kauli hiyo imetolewa na mwandazi wa siku ya wamama iiliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Magdalena Gisse, mama wa mtoto mmoja, mfanyakazi wa RDF alisema kwamba aliamua kuandaa siku ya wamama kutokana na ukweli kuwa mwanamke hana muda wa kupumzika na kutuliza akili yake katika maisha yake yote.

Aidha alisema sherehe hizo pia zilitumika kuwakusanya wanawake na kuwaunga na wenzao kwa lengo la kuelezana majukumu yao ya kuhakikisha wanalea watoto.

Alisema watu wazima wote wamefikia kiwango hicho kutokana na wamama zao kujitolea maisha yote kwa ajili yao na kusema pamoja na kustahili kupumzika pia wanahitaji kuheshimiwa kutokana na wajibu wao.

Alisema katika sherehe hizo waliwaalika wamama pekee kwa kuwa walitaka wapumzike bila kufikiria katika kipindi kifupi kile kuhusu watoto wao na waume zao.

Baba anaweza kurejea nyumbani akapita baa na kupumzika lakini mwanamke hawezi anakimbilia nyumbani kwa ajili ya kuangalia watoto wao kama wamekula na pia baba akirejea naye apate nafasi yake.
 Mwandazi wa siku ya wamama (mother’s day eve party), Magdalena Gisse akizungumza kuhusu umuhimu wa siku hiyo kwa wamama iliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Mfanyabiashara Latifa Kabange akielezea umuhimu wa wamama kuwa na muda wa kupumzika na kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujasiriamali wakati wa siku ya wamama iliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa upishi wa Hoteli ya Kunduchi Beach & Resort, mama Shilpa Suchak akizungumza kuhusiana na siku ya wamama duniani ambapo huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Mei wakati wa usiku maalum wa siku hiyo uliofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
 Sehemu ya wamama waliojumuika pamoja kusherehekea siku ya wamama (mother’s day eve party) iliyofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki
 Baadhi ya wamama walioshiriki katika picha ya kumbukumbu wakati wa sherehe za awali kuelekea maadhimisho ya siku hiyo ya wamama (mother’s day eve party) zilizofanyika katika hoteli ya Kunduchi Beach & Resort Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SIMIYU YAWAHAKIKISHIA WADAU UPATIKANAJI WA MIUNDOMBINU MUHIMU UWANJA WA NANENANE

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkoa wa Simiyu umewahakikishia wadau wote wa Nanenane mwaka 2018 upatikanaji wa miundombinu muhimu hususani miundombinu ya maji, umeme na barabara katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo eneo la Nyakabindi Mjini Bariadi, ambapo Mkoa huo utakuwa mwenyeji wa Maonesho hayo Kitaifa mwaka 2018.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini alipokutana na Kamati ya Maadalizi ya Maonesho Nanenane kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambao walitembelea uwanja huo na kupewa eneo ambalo litatumika na wizara hiyo kuonesha shughuli zake.

Sagini amesema viongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na viongozi wa Taasisi nyingine za Serikali wameshafanya mazungumzo na kuweka mipango ya namna kila Taasisi itakavyoshiriki katika kuhakikisha miondombinu ya maji, umeme na barabara inawekwa vizuri ili kufanikisha Maonesho hayo

“Tumeshazungumza na TANESCO na wako tayari kuteremsha Transifoma kwenye eneo lile ili tupate umeme, tumezungumza na Mamlaka za Maji ili tupate fedha za kuchimba kisima kirefu cha maji ya kutosheleza wadau wetu na kuhusu barabara tumezungumza na TANROADS na TARURA, tunatarajia wiki mbili zijazo mambo yatakuwa tofauti pale” alisema Sagini.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara ya mifugo na Uvuvi kutembelea Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini Bariadi Mkoani humo.
 Bi. Merry Yongolo Mratibu wa Maonesho ya Nanenane Wizara ya Mifugo na Uvuvi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara hiyo kutembelea Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
 Baadhi ya watalaam wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT)  wakiendelea na kusafisha eneo lao kwa kutumia greda katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi,  Mjini Bariadi Mkoani Simiyu, ikiwa ni maandalizi ya Maonesho hayo yatakayofanyika Kitaifa mkoani humo.
 Dkt. Khamis Mkuli kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya ziara ya wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Nanenane wa Wizara hiyo katika Uwanja wa Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziwa Mashariki uliopo Nyakabindi, Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akiwaonesha baadhi ya viongozi na wataalam kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga eneo la Uwanja wa Maonesho ya Nanenane  Kanda ya Ziawa Mashariki uliopo Nyakabindi Mjini Bariadi Mkoani humo, wakati wa ziara yao walioifanya hivi karibuni mara baada ya kufanya kikao cha pamoja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DR. SHEIN AZINDUA TAWI LA CCM FUONI MICHENZANI

$
0
0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein  akifungua pazia kuashiria kulifungua Tawi jipya la CCM Fuoni Michenzani hafla iliyofanyika katika Wilaya ya Dimani Kichama,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Sadala (Mabodi).
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na  Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Wananchama wa CCM Tawi la  Fuoni Michenzani  mara baada ya kulifungua rasmi  Tawi jipya la CCM Fuoni Michenzani (kushoto) Mwenyekiti wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani Nd,Amina  Idarusi  na (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Sadala (Mabodi). (Picha na Ikulu)
 Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi na Wananchama wa CCM Tawi la  Fuoni Michenzani wakimsikiliza   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza nao mara baada ya kulifungua  Tawi jipya la CCM Fuoni Michenzani.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Tawi la CCM Fuoni Michenzani Nd,Amina Idarusi   alipofika kulifungua Tawi hilo,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Sadala (Mabodi).

WATAALAM NISHATI, REA, TANESCO WAKAGUA MIRADI YA REA MOROGORO

$
0
0
Wataalam kutoka  Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wamefanya  ziara katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni vilivyopo mkoani Morogoro. Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kukagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) Katika ziara hiyo ilielezwa kuwa, kampuni ya State Grid iliyopewa kazi hiyo katika mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwasha umeme katika vijiji vya Mandera, Mtego wa Simba na Kibaoni tarehe 16 Mei, 2018.
 Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (katikati) akielezea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya umeme katika kijiji cha Mandera kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika ziara hiyo. Kulia ni Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Yusuph Msembele.
 Moja ya transfoma zilizofungwa na kampuni ya State Grid katika kijiji cha Mandera   kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
 Meneja Mwandamizi wa TANESCO- Kanda ya Kati, Mhandisi Atanasius Nangali ( wa pili kulia) akifafanua jambo katika ziara hiyo.
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy (kushoto) akimsikiliza  mwananchi wa kijiji cha Kibaoni kilichopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Joseph Mkude (kulia) katika ziara hiyo.

WAZIRI JANUARI AZUNGUMZIA SOMO LA MUUNGANO BUNGENI, AAHIDI KUWASILIANA NA WIZARA YA ELIMU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingra Januari Makamba amesema watawasiliana na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kuangalia namna ya kupandisha hadhi Muungano kupitia mtaala wa somo la uraia ambalo linafundishwa shuleni.

Januari Makamba amesema hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo moja ya swali liliuliza kuna mkakati gani wa kuwa na mtaala wa somo la Munungano ambalo litajikita kuelezea kwa kina historia ya Muungano uliopo kati ya Tanzania Bara na Visiwani.
Hivyo Jauari ameliambia Bunge kuwa kwa sasa shuleni kuna mtalaa wa somo la uraia ambalo ndani yake wanafunzi wanafundishwa historia inayohusu muungano wetu lakini amesikia ushauri ulitolewa na wataufanyia kazi.

"Ni ushauri mzuri ambao umetolewa na mbunge kuhusu umuhimu wa somo la Muungano.Tumepokea ushauri huo na niwahakikishie wabunge tutaufanyia kazi kwa kuzungumza na Wizara ya Elimu na kisha tuone namna ya kufanya.Ni kweli historia ya muungano ikifundishwa shuleni itasaidia kuongeza uelewa,"amesema.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingra Alphaxad Kangi Lugola amesema hakuna kero za muungano bali kuna changamoto za Muunga na kuwaomba wabunge kuanzia sasa wawe wanasema changamoto.

Lugola ametoa kauli hiyo wakati anajibu maswali ya wabunge ambapo kila mmoja aliyepata nafasi alikuwa akiuliza swali kwa kuanza na kutaja kero za Muungano.Hivyo wakati anajibu maswali hayo Naibu Waziri huyo aliamua kufafanua kuwa ni vema wabunge wakafahamu hakuna kero bali kunachangamoto za Muungano.

MAHAKAMA KUU YAMTOA LULU GEREZANI, YAMRUDISHA NJE

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetoa amri ya muigizaji Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela sasa atumikie adhabu hiyo kwa kifungo cha nje.

Hivyo kuanzia sasa Lulu amebadilishiwa adhabu na anatumia kifungo hicho akiwa uraiani na tayari Jeshi la Magereza limethibitisha kupokea amri hiyo ya Mahakama Kuu.

Akizungumza kwa njia ya simu na Michuzi Blog iliyotakaka kupata ukweli wa taarifa hizo, Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini amethibitisha ukweli wa taaarifa za Lulu kubadilishiwa kifungo hicho na kusisitiza hiyo imetokana na amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania.

"Ni kweli ndugu zetu wa Michuzi Blog, Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri hiyo na hivyo Lulu atatumia adhabu ya kifungo cha nje badala ya kukaa jela.Taarifa rasmi kuhusu Lulu tutaitoa kwa vyombo vya habari hapo baadae kwani tunaendelea kuiandaa lakini kwa kifupi,"amesisitiza Mboje.

Akifafanua zaidi Naibu Kamishna wa Magereza Augustino Mboje ni kwamba ielewe bado ni mfungwa wao na angeendelea kukaa jela hadi Novemba 12 mwaka huu ili kifungo chake kimepunguzwa kwa msamaha wa Rais. "Rais amempunguzia moja ya sita ya adhabu ya kifungo chake kwani ilikuwa atoke Machi 12 mwaka 2019."
Kwa mujibu wa Jeshi la Magereza ni kwamba hivyo Lulu atatumikia adhabu yake kwa kupangiwa kazi za kufanya za kijamii katika moja ya wilaya nchini na haijafahamika atapangiwa wilaya gani kutekeleza adhabu yake hiyo.

Kwa kukumbusha tuLulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kutiwa hatiani kwa kuua bila kukusudia msanii mwenzake Stiven Kanumba(marehemu).Kanumba alifariki saa nane usiku, mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake yake na Lulu ambaye inaaminika walikuwa na uhisiano wa kimapenzi. Hivyo kitendo cha Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa amri ya kubadilishiwa adhabu Lulu ya kutumia kifungo chake nnje kinatoa fursa kwake kupata auheni ya adhabu hiyo.

JESHI LA MAGEREZA LAFAFANUNA KUHUSU KUBADILISHIWA KIFUNGO CHA NJE MFUNGWA NAMBA 1086/2017 ELIZABETH MICHAEL 'LULU'

WANANCHI WA KIJIJI CHA MKASALE WILAYANI TUNDURU WAMSHUKURU RAIS.

$
0
0
Wananchi wa kijiji cha MKASALE katika TARAFA YA NAMASAKATA wilayani TUNDURU mkoani RUVUMA wameishuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwajengea kituo cha afya ambacho kitaweza kuhudumia wakazi zaidi 43,195 . 

Ambapo serikali imeleta milioni 400 huku mkuu wa mkoa wa Ruvuma CHRISTINA MNDME akiahidi kuleta wataalamu wenye sifa pamoja na vifaa tiba HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

mabingwa wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 Simba SC watembelea Bungeni Jijini Dodoma leo

$
0
0
 Sehemu ya wachezaji wa timu ya Simba Sports Club wakifuatilia mjadala wa kipindi cha maswali na majibu wakati mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 walipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
 Viongozi wa timu ya Simba Sports Club wakifuatilia mjadala wa kipindi cha maswali na majibu wakati mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 walipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Tulia Ackson, Baadhi ya Naibu Mawaziri na Wabunge wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya Simba Sports Club wakati mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 walipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso wakiwa katika picha ya pamoja na mshambuliaji wa timu ya Simba Sports Club Bw. Emmanuel Okwi (kushoto) wakati  mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzaniana Bara 2018 walipotembelea Bungeni leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
Picha zote na Octavian Kimario wa WHUSM

MIAKA 70 YA NAKBA YA WANANCHI WA PALESTINA

$
0
0
Taifa letu la Palestina  linaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya Nakba (janga), likiendeleza mapambano kabambe ya kurudisha haki zake thabiti za kizalendo, kuondoa athari na matokeo yake ambayo bado yapo katika nyanja zote za maisha ya taifa letu. Hiyo ni tangu utekaji wa ardhi yote ya Palestina ya kihistoria hadi kuwatoa nusu ya wananchi wa Palestina nje ya nchi yao.



 Kwa yakini mapambano ya kitaifa kwa ajili ya ukombozi yatathibitisha malengo yake hata kama ni kwa muda mrefu, licha ya uadui wa utekaji na uhalifu wake unaoendelea, na licha ya uungaji mkono wa Marekani uliopitiliza chini ya Rais wake Donald Trump kwa  taifa tekaji la Israel, hasa uamuzi wake wa kusikitisha wa kuizingatia Jeruselemu kuwa ni mji mkuu wa taifa tekaji na kuhamishia ubalozi wa Marekani mjini Jerusalemu, jambo linalokiuka  sheria ya kimataifa na maazimio yake, pia ni jambo linaloifanya Marekani kuunga mkono utekaji na uadui dhidi ya wananchi wa Palestina na suala lake la kizalendo.


Kama ilivyo kila mwaka tarehe 15 Mei, wananchi wetu popote pale walipo kwa nguvu za kizalendo na taasisi zake huikumbuka kumbukumbu hii yenye kuumiza kwa shughuli na harakati mbali mbali. Lakini mwaka huu unashuhudia mabadiliko makubwa na muhimu katika kuutukuza mnasaba huu, kwani inaenda sambamba na safari kubwa ya kurejea iliyoanza tangu wiki kadha kwenye mipaka ya kihistoria ya Palestina pamoja na ukanda wa Gaza.
 Makumi ya watu wamekufa mashahidi na maelfu wamejeruhiwa. Kilele chake kitakuwa tarehe 14 -15 Mei, hii kwa kuthibitisha wananchi wetu wameshikamana na malengo na haki zake za kizalendo na mbele kabisa haki yake ya kurudi vijijini kwao na mali zao; na haki ya kusimamisha taifa lake huru lenye heshima kamili katika mji wake mkuu Jeruselemu, pamoja na kuondolewa kuzingira kuovu katika ukanda wa Gaza.

Ukweli msimamo wa Marekani na hatua iliyoichukua mnamo Januari mwaka huu, wa kupunguza msaada wake kwa UNRWA kwa kiasi cha dola za kimarekani millioni 65 toka kile kiasi inachokitoa kwa UNRWA. Uamuzi huu kwa taifa letu umepelekea hofu kwa suala la wakimbizi kwa kujaribu kulifuta na kuliweka hatarini kwa masilahi ya msimamo mkali wa serikali ya Israel ambao unajitahidi kwa nguvu zote kulitokomeza suala la wakimbizi ambalo ndio kiini cha suala la Palestina. Hiyo ni kukausha vyanzo vya misaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia na kuwahudumia wakimbizi wa Palestina (UNRWA), hadi kufikia kuliondoa kikamilifu.


Katika kumbukmbu ya 70 ya Nakba (janga) ya Palestina,majukumu yetu wote yanaongezeka kuhusiana na suala letu la haki,katika ulazima wakupambana na kukabiliana na maelezo ya kizayuni na kiizraeli kuhusu Nakba lililowakumba Wananchi wa Palestina, ambalo limepelekea kuhamishwa maelfu ya wapalestina, hasa kile kilichojumuishwa na “Mpango wa Dalet” uliopitishwa na Shirika la Kizayuni mwanzoni mwa mwaka 1948 na kuachiwa utekelezaji wake Haganah (kikundi cha mauaji na utesaji) kwa muongozo wa uwazi,kama vile kuua,kuhofisha,kuzingira miji na vijiji vya palestina,kuchoma nyumba na mali,kuzika mabomu katika vifusi ili kuwazuia wenyeji kurejea Kartika nyumba zao.

Vikundi vya hagana na jumuiya zingine za kizayuni kufuatia mpango huo zimetekeleza mauaji 28,huku mauaji mabaya zaidi katika hayo ni yale ya mjini Deir Yassin mnamo tarehe 9 April 1948. Hii ni pamoja na kuvunjwa na kuteketezwa miji na vijiji 531,kuhamishwa wapalestina laki nane (8) waliofanywa kuwa ni wakimbizi katika nchi yao, ni sawa waliokuwa katika ardhi ya mwaka 48,Ukingo wa Magharibi au Ukanda wa Gaza.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TANZANIA YATINGA FAINALI MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA LA WATOTO

$
0
0
Mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa kike yameendelea tena leo mjini Moscow nchini Urusi katika uwanja wa klabu ya Lokomotive, ambapo michezo ya nusu fainali ilichezwa wakati Tanzania ikipambana na Uingereza.

Timu ya Tanzania imefanikiwa kutinga hatua ya fainali kwa kishindo baada ya kuibamiza na kuisambaratisha bila ya huruma timu ya Uingereza kwa magoli 2-1, yaliyowekwa wavuni na mlinzi Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari. 

Magoli ya mechi zote yalifungwa kipindi cha pili huku Tanzania walionekana wakiumiliki mchezo kwa asilimia kubwa sana na watoto wa  kitanzania walionyesha umahiri mkubwa sana mbele ya Mheshimiwa Balozi wetu na wa Tanzania nchini Urusi na pia maafisa wa Ubalozi wetu walihudhuria kutazama mechi hio. 

John Wroe ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Street Child United lililoshiriki kuandaa mashindano hayo alimpokea Mheshimiwa balozi na ujumbe wake na kisha baada ya mechi alimpa pongezi sana kwa ushindi uliopata Tanzania leo dhidi ya Uingereza. 
Timu ya Tanzania imefika fainali tena ikiwa imeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu chini ya mlinda mlango mahiri Sifaeli Geofrey na pia Tanzania inaelekea kutetea taji lake fainali kwani ndio mabingwa wa kombe hili tangu yalipofanyika mashindano haya mwaka 2014 nchini Brazil. 

Tanzania itacheza fainali na Brazil hapo kesho kutwa ambapo Brazil waliibwaga timu ya Ufilipino katika nusu fainali kwa goli 1-0. Tuendelee kuiombea Tanzania ibebe tena kombe na tuendelee kuitangaza Tanzania Kimataifa zaidi. Mungu Ibariki Tanzania. 


YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.January Makamba akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge kuhusu changamoto za Muungano wakati wa kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt.Hussein Mwinyi akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.
Picha zote na Daudi Manongi,
 Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Dkt.Florens Turuka  na Naibu Katibu Mkuu Bi.Immaculate Ngwale pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo wakati wa kikao cha ishirini na nane cha mkutano wa 11 leo Jijini Dodoma.
 Majenerali wastaafu wa Jeshi la Wananchi watanzania(JWTZ)  wakifuatilia kipindi cha maswali  na majibu leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Wachezaji wa Timu ya Simba ambao pia ni mabingwa wa ligi kuu Bara kwa  mwaka 2017/18 wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
 Viongozi wa Timu ya Simba  wakifuatilia shughuli mbalimbali za Bunge leo Jijini Dodoma kwa mualiko maalumu wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai.
MAELEZO DODOMA

Mradi wa Maji Kimbiji na Mpera Kuwanufaisha Wananchi

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Mradi wa maji wa Kimbiji na Mpera kuanza kuwanufaisha Wananchi baada ya kukamilika kwa awamu ya pili ambayo itahusu ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji ambapo utaanza kutekelezwa katika  bajeti ya mwaka 2018/2019.
Akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Mhe. Lucy Simon Magereli aliyeta kujua ni lini mradi huo utakamilika ili kuondoa adha kwa wananchi wa Kigamboni ambao wengi wao wanatumia visima vifupi ambavyo si salama, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa   Aweso amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaondoa adha ya upatikanaji wa maji kwa Wananchi wa maeneo mbalimbali ikiwemo Kigamboni.
“Serikali imeanza kutekeleza miradi mbalimbali minne (4) ya uboreshaji wa huduma ya maji kwa mpango wa muda mfupi kwa wakazi wa Kigamboni,” alisema  Mhe.  Aweso
Akifafanua Mhe. Aweso  amesema kuwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa mtandao wa mabomba, kusambaza maji ya kutoka Ruvu chini kupitia bomba linalovuka bahari eneo la Kurasini kwenda Kigamboni ili kusambaza maji maeneo ya Tipper, Chuo cha Mwalimu Nyerere na Kigamboni Ferry kuelekea Mji Mwema.
Ameitaja miradi mingine kuwa ni  ujenzi wa miundo mbinu ya kusambaza maji kutoka visima vya Vijibweni kuelekea maeneo ya ofisi mpya ya Manispaa ya Kigamboni na kuendeleza kisima cha mita 600 cha Kisarawe  ili kufikisha maji Kibada na maeneo ya Viwanda (Light Industry Zone) la Kimbiji.
Akizungumzia  mikakati ya Serikali kumaliza ujenzi wa miundo mbinu ya Maji katika Kata za Igowole, Nyololo, Mninga, Mtambula, Nyigo na Idunda, Mhe. Aweso amesema kuwa Kata za Igowele, Nyololo, Mninga, Mtambula na Idunda zina jumla ya vijiji 23 vyenye wakazi takribani elfu 69,119.
Mhe. Aweso amesema kuwa, katika mwaka wa fedha 2017/2018, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetenga Shilingi Bilioni 2.67 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji vijijini zikiwemo kata hizo ambapo hadi sasa usanifu wa kina umekamilika na uandaaji  wa makabrasha ya zabuni unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2018.
Kazi hizo zinatekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Iringa (IRUWASA)  kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na Sekretarieti ya Mkoa wa Iringa.
Aidha amesema, Ujenzi wa miundo mbinu ya miradi hiyo ya maji unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.25 kwa ajili ya miradi ya maji vijijini katika halmashauri ya Wilaya ya Mufindi zikiwemo Kata za Igowole, Nyololo, Mninga, Mtambula, Nyigo na Idunda.

Tanzania Yaanza Maandalizi Ya Kuridhia Mkataba wa Kupambana na Silaha za Baolojia na Sumu

$
0
0
Na Frank Mvungi- MAELEZO

Serikali Kuridhia mkataba wa kupambana na silaha za  baolojia na sumu mara baada ya taratibu kukamilika kufikia mwezi Septemba 2018 ambapo  waraka wa mapendekezo ya kuridhia mkataba huo umeshaandaliwa.
Akijibu swali  la mbunge wa viti maalum Mhe. Jasson Rweikiza aliyetaka kujua, kwa nini Tanzania haijajiunga na mkataba wa kupambana na silaha za sumu  (Biological Weapons Convention), Waziri  wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa waraka wa mapendekezo ya kuridhia mkataba huo ukishapitia ngazi husika utawasilishwa  Bungeni kwa ajili ya kuridhiwa.
“Tanzania ilisaini mkataba wa kupambana na silaha za baolojia na sumu tarehe 1 Agosti, 1972 lakini mpaka sasa haijaridhia mkataba huo, kutoridhiwa kwa mkataba huo kulitokana na kutoonekana athari zake za moja kwa moja kwa wakati huo ambapo matumizi salama ya mkataba ikiwemo utafiti wa magonjwa ya binadamu, wanyama na mimea yameendelea kufanyika nje ya mkataba huo,” alisema Dkt. Mwinyi.
Dkt. Mwinyi amesema, changamoto zinazotokana na matishio mbalimbali ikiwemo ugaidi, zimesababisha hitaji la kuridhiwa kwa mkataba huo na kutekelezwa kwa vitendo baada ya kutungiwa sheria.
Aliongeza kuwa Serikali inafahamu madhara yaliyopo hivi sasa ya kutoridhiwa kwa mkataba huo ikiwemo Tanzania kuwa katika kundi dogo la nchi ambazo hazijaridhia mkataba huo kama vile Haiti, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Misri, Somalia na Syria ambapo Tanzania kuwepo katika kundi hilo hakutoi taswira nzuri kwa jamii ya Kimataifa.
 Aliongeza kuwa kutoridhiwa kwa mkataba huo  ni pamoja na kuwanyima fursa wataalamu wetu kupata mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika kujenga uwezo wa kukabiliana na athari za mashambulizi ya silaha za sumu na kibaolojia na pia kunanyima fursa kwa wataalamu na viongozi wa kitanzania kushiriki kwenye uongozi wa taasisi mbalimbali za kimataifa zinazosimamia sheria za silaha za kibaolojia na sumu.
Athari nyingine ni kukosesha Serikali kutoa haki za msingi kupitia mahakama kwa makosa mbalimbali yanayoweza kufanywa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tanzania ilisaini mkataba wa kupambana na silaha za baolojia na sumu tarehe 1 Agosti, 1972  ambapo kwa sasa hatua za kuridhia mkataba huo zimeanza kuchukuliwa na Serikali kutokana na mahitaji ya sasa.

Tanzania Health Summit yachangia Milion Moja ya UpasuajI wa mtoto

$
0
0
 Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wa    Tanzania Health Summit wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa mfano wa  hundi ya shilingi milioni moja fedha ambazo zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mbaruku Kabwe aliyelazwa JKCI  kwa ajili ya matibabu. Kushoto ni mama wa mtoto Asha Omary mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
 Rais wa  Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi hundi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mbaruku Kabwe aliyelazwa katika Taasisi hiyo kwa ajili ya matibabu. Kila mwaka  Tanzania Health Summit wanaandaa mashindano ya Heart Marathon lengo likiwa  ni kusaidia watoto wanaosumbuliwa na  magonjwa yasiyoambukiza ukiwemo ugonjwa wa moyo.
Picha na JKCI

HALMASHAURI ZATAKIWA KUJIBU HOJA ZA UKAGUZI KWA WAKATI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo amewaagiza wakurugenzi wote nchini kujibu hoja za wakaguzi kwa wakati ili kupunguza hati Chafu na Mashaka kwa Halmashauri.


Ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na Kamati ya ulinzi na Usalama na Manejimeti ya Mkoa wa shinyanga leo wakati akiwa katika ziara ya kutembelea miradi yamaendeleo Mkoani hapo.



Amesema Wakurugenzi wanawajibu wa kuhakikisha hoja zote zinazotolewa na wakaguzi zinafanyiwa kazi mapema kwa kutoa majibu stahiki na wakati."Kumekuwepo na changamoto kubwa kwa baadhi ya Halmashauri  kutotoa majibu ya hoja za wakaguzi zinapotolewana kusababisha kupata hati chafu na zenye mashaka" Amesema



Mhe.Jafo amesema katika hoja za CAG mwaka huu imeonekana kuwa vitabu 379 havijaonekana, hivyo ameziagiza Halmashauri zote nchini kutumia mifumo ya Tehama ili kupunguza ubadhilifu wa mali ya umma na kupunguza  mianya ya wizi wa fedha za serikali.



Kuhusu usimamizi wa  fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya Miradi ya maendeleo Mhe.Jafo amewaagiza Wakurugenzi kusimamia fedha hizo kea weledi ili miradi hiyo iendane na dhamani ya fedha zilizotolewa nakukamilika kwa wakati.



Amewataka kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo, rasilimali fedha na rasilimali watu ili kuleta maendeleo kwa jamii.



Wakati huo huo, Waziri Jafo amewataka viongozi wote wa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanasimamia suala zima la mauaji ya vikongwe kwa imani za kushirikina kwa kuwa linarudisha nyuma maendeleo na kutoa sura mbaya kwa jamii.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab akizungumza katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama.
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images