Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO

$
0
0
TTCL PESA, Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, ambao ni watoaji wa huduma za fedha mtandao inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla kwamba, imefanya mabadiliko ya Jina na Nembo zinazoitambulisha Kampuni hiyo. 

TTCL PESA ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Julai 2017 ikiwa na lengo kuu la kuwapa Wananchi huduma za kiwango cha juu kabisa cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma fedha, kupokea fedha, kulipia huduma na kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia simu zao. 

Mabadiliko haya yanakuja miezi 9 baada ya TTCL PESA kuanza huduma zake kwa Mafanikio makubwa. Hatua hii ni kuridhia ushauri wa Wateja na wadau wetu waliopendekeza kufanyika mabadiliko ya jina na Nembo ili kuongeza mvuto wa huduma, kukidhi mahitaji ya Soko na urahisi wa kuitambua huduma hii miongoni mwa huduma zinazotolewa na Taasisi nyingine. 

Huduma za fedha Mtandao ni Sekta inayokua kwa kasi duniani kote. Hapa Nchini Tanzania, miamala inafanyika katika jamii kupitia njia hii na kusaidia sana katika kuokoa muda, kurahisisha manunuzi, kutoa ajira kwa Makundi mengi ya wananchi hasa Wanawake na Vijana, kuongeza Mapato ya Nchi kupitia tozo za kodi, kuongeza usalama wa fedha na kuepusha uwezekano wa vitendo vya kihalifu kama wizi na utapeli visiweze kutokea kwa urahisi. 

Kwa kutambua umuhimu wa Jina la huduma na Nembo kuwa ni nyenzo muhimu sana katika mikakati ya Biashara na hasa biashara yenye ushindani mkubwa kama hii ya Fedha Mtandao, TTCL Corporation inaamini kuwa, Jina na Nembo mpya zitakidhi mahitaji ya Wadau na Ushindani wa soko sambamba na kusaidia harakati za kuongeza kasi ya kusambaa kwa huduma za Fedha Mtandao zinazotolewa na Shirika letu kupitia Kampuni yake tanzu ya TTCL PESA. 

Tunaileta T-Pesa kuja kuwa muhimili mkuu wa miamala ya kifedha Tanzania. Tunamlenga kila mwananchi kufaidika na huduma za tpesa ambazo zimekuwa nafuu na salama zaidi. Uzinduzi wa nembo hii ni mwanzo wa mambo mazuri na makubwa yatakayoletwa na T-Pesa. Nia yetu ni kuwa sehemu ya kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa kuhakikisha tunatoa suluhisho la uhakika katika miamala ya kifedha hususani katika malipo ya huduma za umma and ukusanyaji wa malipo hayo. T-Pesa itashirikiana na taasisi zote za umma, mabenki na taasisi binafsi katika kufikia malengo haya na mwisho kutoa huduma bora nafuu na za uhakika kwa watanzania. 

Imetolewa na; 
Ofisi ya Uhusiano, 
TTCL Makao Makuu, 
Dar Es Salaam. 
3 Machi, 2018

TRA Yatakiwa Kutekeleza Majukumu Yake Kwa Kuzingatia Weledi

TAASISI YA MEN AT WORK YACHANGIA DAMU KUWASAIDIA WENYE UHITAJI

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha


TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Wanaume ya Men At Work imeendesha mchakato wa kuchangia damu kwa lengo la kutaka itumike kuwasaidia akina kinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi.Pia damu hiyo itawasaidia majuruhi wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru mkoani Arusha.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Maxwell  Stanslaus amesema leo mkoani hapa wameamua kuchangia damu  kama mchango wa wanaume kujitoa kwa ajili ya jamii na kuisaidia jamii kwani wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa kwa ujumla.Stanslaus amewataka wanaume wote nchini 
kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii .

"Kwa sasa  tumeamua kushirikiana na kitengo cha damu salama kuchangia damu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa damu katika benki ya damu,"amesema Stanslaus .Ameongeza taasisi hiyo ina kazi ya kuwahasisha wanaume wanawajibikaji na kushiriki katika nafasi za malezi  familia na jamii ili kujenga familia imara na hatimaye taifa imara.

Kwa upande wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson amesema kuwa anajisikia faraja kuchangia damu  ili kusaidia kuokoa maisha ya kinamama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.Kwa upande wa Melayeki  amesema kwake ni mara yake ya kwanza kutoa damu, hivyo amewatoa hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu.

Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work akichangia damu
 Wanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Rodgers Nelson   wakichangia damu katika viwanja vya Sheikjh Amri Abeid(picha na Woinde Shizza,Arusha )

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus  akizungumza na Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoendeshwa ma taasisi yake.


Serikali Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Viongozi Kutoa Chanjo Kuzuia Saratani Ya Mlango wa Kizazi

RAIS DKT MAGUFULI AHANI MSIBA WA MKUU WA MKOA MSTAAFU MAREHEMU MZEE ABBAS KANDORO MJINI IRINGA LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa pole kwa wafiwa walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitambulishwa kwa watoto wa marehemu walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiomba dua pamoja na wafiwa walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018. Picha na IKULU  

YANGA YAKWEA PIPA KUWAFUATA USM ALGER

$
0
0

Na Agness Francis,Blogu ya Jamii

KIKOSI cha Timu ya Yanga SC kimeondoka leo kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya kucheza na Timu ya  USM  Alger Nchini Algeria katika hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wawakishilishi hao wa Tanzania  ambao wanatarajia kucheza na USM Alger katika mchezo wao wa kwanza hatua ya makundi  kombe la shirikisho wanaondoka leo saa 11 jioni kupitia Dubai.

Yanga wamesafiri na wachezaji 20 pamoja na viongozi 8 wakiwepo na benchi la ufundi ambapo mtanange huo utachezwa nchini Algeria  Mei 6  mwaka huu  saa 4 Usiku.

Akizungumza leo katika Makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam, Msemaji wa kikosi hicho Dismas Ten amewataja baadhi ya wacheza ambao wapo katika msafara huo ni Rostand Youth,Ramadhani Kabwili,Gadiel Maiko,Obrey Chirwa,Pato Ngonyani,Kelvin Yondani,Ibrahim Ajibu. Dismas Ten amesema wachezaji hao ni wale ambao wapo katika programu ya mwalimu,

"Tunahitaji matokeo na maandalizi ya muhimu yameshafanyika ukizingatia tupo ugenini.Mchezo ni mgumu na kikosi cha USM Alger kipo vizuri, si timu ya kuibeza wapo kwenye michuano haya ya kimataifa kwa mudu mrefu,"amesema.

TANZIA:DAKTARI BINGWA WA USINGIZI KWA WATOTO NA WAGONJWA MAHUTUTI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) AFARIKI DUNIA

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi anasikitika kutangaza kifo cha Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa kilichotokea jana jioni tarehe 02/05/2018.

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na unatarajiwa kusafirishwa kesho tarehe 04/05/2018 kwenda katika kijiji cha Nzihi kilichopo  Iringa vijijini kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika tarehe 05/05/2018.

Heshima za mwisho zitatolewa kesho tarehe 4/5/2018 katika ukumbi wa kufundishia uliopo chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili kuanzia saa 2 asubuhi hadi  saa 3  na baadaye nyumbani kwa kaka wa Marehemu kuanzia saa 6 mchana.

Kwa namna ya kipekee Prof. Janabi anatoa  pole kwa familia ya Marehemu, Wafanyakazi  wote, ndugu,  jamaa, marafiki  pamoja na wote walioguswa na msiba huu.

Msiba uko nyumbani kwa kaka wa marehemu Ndugu Lumumba Mhewa mtaa wa Mivumoni Madale.
  
“Bwana Ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe”.
  
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
03/05/2018 

Wapangaji wa Muda Mrefu NHC Wapewe Fursa ya Kununua Nyumba - Kassim Majaliwa.

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim  Majaliwa ameiagiza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kukaa pamoja na chama cha wapangaji wa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ili kusikiliza changamoto zao pamoja na kutoa fursa kwa wapangaji wa muda mrefu kununua nyumba hizo.
Mhe. Majaliwa ametoa tamko hilo leo Bungeni, Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ilala Mhe. Azzan Mussa Zungu juu ya lini Serikali itakutana na wanachama na wamiliki wa nyumba za NHC ili kutoa fursa kwa wapangaji wa muda mrefu kuzinunua nyumba hizo badala ya kuwaondoa.
"Shirika la nyumba inayo sera inayotoa muongozo namna nyumba hizo zinavyotakiwa kutumika ikiwemo na maamuzi kwa wale wanaokaa kwa muda mrefu kwenye nyumba hizo inapofikia thamani ya nyumba kushuka iweze kurasimishwa rasmi ili kutoa fursa kwa wapangaji hao kuweza kuzinunua kwa kulipa kiwango kidogo kidogo," alisema Waziri Mkuu.
Aliendele kusema, asilimia kubwa ya wapangaji wa muda mrefu wa nyumba hizo ni wastaafu ambao hawana nyumba. Hivyo ameitaka NHC kuangalia jambo hilo na kuwapa fursa wapangaji hao kulipa kidogo kidogo kadiri ya uwezo wao.
Wakati huo huo Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutotumia lugha ya kuudhi au kutumia nguvu pindi wanapokusanya kodi kwa wafanyabiashara. Badala yake wawaelimisha wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kuwaeleza ni kwa kiasi gani kodi hiyo imefikia.
Amesema hayo, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Tunduma Mhe. Frank Mwakajoka kuhusu kauli ya Serikali juu ya usumbufu unaoletwa na TRA kwa wafanyabiashara wakati wa kukusanya kodi.
"Serikali imeunda chombo cha kusikiliza kero za wananchi ndani ya TRA lakini kama hawatasikilizwa wanauwezo wa kupeleka kero zao Wizara ya Fedha au kwa kiongozi yoyote mkubwa katika eneo lake kama vile Mkuu wa Mkoa au Wilaya," alisema Waziri Mkuu.
Aidha ameitaka Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuwa na mazungumzo na wafanyabiara. Pia tathmini ya kodi isiwe kiwango kikubwa kuliko mtaji wa mfanyabiashara.
Hata hivyo amesema hatua zitachukuliwa kwa yeyote ambaye hatatumia utaratibu mzuri wa kukusanya  kodi na amewataka wafanyabiashara kufanya biashara kwa amani. 
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akisisitiza kuhusu umuhimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu na kuepuka vitendo vyote vya kuwabugudhi wafanyabiashara wakati wa kutekleza jukumu la kukusanya kodi katika maeneo yote nchini wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu leo Bungeni  Jijijni Dodoma.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job  Ndugai akisisitiza jambo wakati akijibu miongozo ya wabunge  leo Bungeni  Jijini Dodoma  mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt.  Mwigulu  Nchemba akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 leo Bungeni Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wageni waliofika bungeni  wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi  Isack Kamwelwe akitoa maelezo kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kufikisha huduma za maji kwa wananchi kote nchini.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza kuhusu taratibu za matibabu hasa kuhusu kitendo cha baadhi ya viongozi kuonyesha mfano katika kutoa chanjo cha wasichana wenye umri wa miaka kuanzia 14 ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
Mbunge wa viti maalum (CCM) Mhe. Amina Mollel akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanajengewa mazingira rafiki yatakayowawezesha kushiriki katika ujenzi wa uchumi. 
( Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)


MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI DKT. MWAKYEMBE ALIPOHOTUBIA SIKU UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa kongamano la maadhimisho ya kilele cha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizindua mpango maalumu wa Kitaifa kuhusu Muelekeo wa Uhuru wa Kujieleza ulioandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika (MISA TANZANIA) wakati wa kilele cha kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo mjini Dodoma. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA TANZANIA) Bi. Salome Kitomari.
 Mwakilishi wa UNESCO nchini Bw. Jaco Du Toit (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe moja ya machapisho ya Jumuiya hiyo kuhusiana na Uhuru wa Vyombo vya Habari wakati wa kilele cha kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo mjini Dodoma.
 Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya hapa nchini Bw. Charles Stuart akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wakati wa kongamano la maadhimisho ya kilele cha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi. Edda Sanga akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wakati wa kongamano la maadhimisho ya kilele cha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo mjini Dodoma.
 Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Bw. Deodatus Balile akizungumza na wajumbe (hawapo pichani) wakati wa kongamano la maadhimisho ya kilele cha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa habari, viongozi wa taasisi na Mashrika ya Kimataifa yanayojihusisha na masuala ya habari hapa nchini wakati wa kongamano la maadhimisho ya kilele cha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo mjini Dodoma.

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA OFISI ZA UHAMIAJI LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Koplo, Yakobo kiwawa (kushoto) wakati akiingia katika Ofisi ya Uhamiaji leo Mjini Dodoma Kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole ili  kutengenezewa pasi/hati ya kusafiria.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha wageni walipotembelea Ofisi ya uhamiaji leo Mjini Dodoma kabla ya kuchukuliwa alama za vidole kwa ajili ya kutengenezewa pasi ya kusafiria.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akichukuliwa alama za vidole kwa ajili ya kutengenezewa pasi ya kusafiria leo katika Ofisi ya uhamiaji Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, Ndg. Edwin Mwasota (kulia) leo katika Ofisi za uhamiaji Mjini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

BASF yafungua ofisi mpya Tanzania

$
0
0
 BASF, ambayo ni kampuni ya kemikali inayoongoza duniani, imezindua ofisi zake mpya jijini Dar es salaam, Tanzania.

Ofisi hiyo ilizindliwa na Balozi wa Balozi wa Ujerumani Tanzania Detlef WaechterJijini Dar es Salaam huku akiipongeza BASF kwa hatua hiyo kubwa.

Makamu wa Rais wa BASF Afrika, Bw. Michael Gotsche alisema, “Ujio wetu nchini Tanzania utatuwezesha kuchangia katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na hali ya ushindani sokoni na wakati huo huo kutuwezesha kuwafikia.”

Alisema ofisi hiyo itatoa huduma za mauzo pamoja na msaada wa kiufundi kwa wateja wa BASF Tanzania.

Alisema BASF ilianza kufanya biashara katika bara la Afrika kama miaka 90 iliyopita ikielekeza nguvu zake kwenye sekta za viwanda zikiwemo ujenzi, nguo, magari, kilimo, plastiki na sekta ya afya.

Alisema Uzinduzi wa ofisi mpya Tanzania utapanua wigo wa BASF barani Afrika na utaongeza ushirikiano kati ya BASF na makampuni ya Kitanzania uliojaa ubinufu mkubwa na utakaolenga ukuaji endelevu.

Alisema miongoni mwa mikakati ya ukuaji wa kampuni ya BASF barani Afrika ni kuwekeza kwa kuwa na uwepo wa ndani na uzalishaji wa ndani wa nchi husika. BASF katika miaka ya hivi karibuni imefungua ofisi zake nchini Zambia, Ivory Coast and Kenya.

“Siku zote hapa BASF huwa tunafanya tathmini ya utendaji wa kiuchumi wa kampuni na kuchukua hatua stahiki zitakazo tuelekeza katika hatua husika zitakazotuwezesha kutanuwa wigo kuingia kwenye masoko mapya na kurahisisha upatakinaji wa bidhaa zetu kwa wateja wetu,” alisema Gotsche.

Kutokana na uzoefu wa kitaalamu na upana wa huduma na bidhaa wanazotoa kuanzia bidhaa za utendaji, plastiki, kemikali, mafuta na gesi pamoja na bidhaa za ulinzi wa mazao, BASF inalenga kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma na msaada wanaohitaji.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa BASF Tanzania, Bw. Mats Idvall, kipaumbele cha BASF ni kuvuka matarajio ya wateja wake. “Tanzania inawakilisha kitovu cha uchumi wa viwanda kwa biashara nyingi kutokana na mazingira yake mazuri ya kiuchumi yalio imara”, alisema. “Kuanzishwa kwa ofisi hizi mpya unadhihirisha ni kiasi gani BASF imejitolea kukuza biashara katika soko hili muhimu sana kimkakati”, aliongeza.
Balozi wa Ujerumani Tanzania Detlef Waechter akikata utepe kuzindua rasmi ofisi za BASF Tanzania katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa BASF Tanzania Mats Idvall, Makamu wa Rais BASF Afrika, Michael Gotsche na Malin Idvall ambaye ni mke wa Mkurugenzi wa BASF Tanzania.

Balozi wa Ujerumani Tanzania Detlef Waechter (kulia) akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa ofisi za BASF Tanzania Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kusoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BASF Tanzania Mats Idvall na  Makamu wa Rais BASF Afrika, Michael Gotsche.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA BARABARA NA KUFUNGUA KIWANDA CHA KUZALISHA CHAKULA CHA KUKU NA VIFARANGA

$
0
0


 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa sehemu mbalimbali baada ya kuzindua rasmi kiwanda cha kuzalisha vifaranga na chakula cha kuku cha Silverland kilichopo Ihemi nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Msenza alipowasili eneo la Ihema kuzindua barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga mkoani Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa na kulia kwa Rais ni Mama Janeth Magufuli.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongea  na Naibu Balozi wa Denmark nchini Mhe. Camilla Christensen wenye sherehe za uzinduzi wa barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga eneo la Ihema mkoani Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.  
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Balozi wa Denmark nchini Mhe. Camilla Christensen na viongozi wengine wakizindua barabara ya Iyovi-Iringa-Mafinga eneo la Ihema mkoani Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018

MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) ATOA TAARIFA YA UTENDAJI WA TPC KWA KIPINDI CHA MWAKA 2016/2017

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji ya shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017. Kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang'ombe, akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Meneja Rasilimali za Shirika wa TPC, Macrice Mbodo. 
Kaimu Meneja Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta, Mwanaisha Saidi (kulia), akijibu badhi ya maswali ya waandishi wa habari katika mkutano huo. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya watendaji wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari, wakati Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji ya shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, jijini Dar es Salaam leo.  
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, wakati akitoa taarifa ya utendaji wa Shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo, akitoa taarifa ya utendaji wa Shirika kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, jijini Dar es Salaam leo.  
Baadhi ya watendaji wa Shirika la Posta Tanzania, wakiwa katika mkutano huo na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

LAZIMA TUSIMAMIE NIDHAMU, HATA AKIKOSEA MWALIMU AMBAYE NI MKE WA KIGOGO ACHUKULIWE HATUA-KATIBU TUME YA UTUMISHI WA WALIMU

$
0
0
*Apiga marufuku mwanafunzi kuchapwa viboko shuleni, atoa mbinu za ufundishaji
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
KATIBU wa Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania Winfrida Rutahinfwa ametoa  maagizo kwa Walimu wakuu na Wakuu wa shule nchini kutoogopa kuwachukulia walimu ambao watabainika wanakiuka nidhamu ya utumishi hata kama walimu hao watakuwa ni wake wa viongozi wa ngazi za juu Serikali.

Pia amewaagiza walimu kubuni mbinu za kufundisha wanafunzi ili wafaulu kwenye masomo huku kwa walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam hasa wa Shule za Sekondari kujikita katika kufundisha wanafunzi ili wafaulu kwani kwa sasa shule za mkoa huo zinafanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani.

Rutahinfwa amesema hayo leo wakati anazungumza na walimu wakuu wa shule za msingi, Wakuu wa shule za sekondari, maofisa elimu na viongozi wa ngazi mbalimbali wa sekta ya elimu mkoa wa Dar es Salaam na hasa wa Manispaa ya Ilala jijini.

"Mwalimu mkuu wa shule ya msingi na mkuu wa shule sekondari ndiko mamkalaka ya nidhamu yanakoanzia kwa maana kwenye ngazi za shule,hivyo nitoe mwito walimu wakuu na wakuu wa shule chukueni hatua kwa walimu wanapokosea.

"Mwalimu hata akiwa mke wa kiongozi achukuliwe hatua pale anapokiuka nidhamu,anapokuwa kwenye majukumu yake ni mwalimu na akirudi nyumbani ndio atabaki kuwa mke wa kiongozi.

"Hivyo hakuna sababu ya kuogopa kuchukua haua kwasababu mwalimu aliyekosea ni mke wa mkubwa.Tufuate sheria na kanuni za utumishi wa umma na zile za Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania.Anayekosea aanywe, apewe karipio na akiendelea achukuliwe hatua zaidi,"amesema  Rutahinfwa .


Baadhi ya walimu walimi wakuu wa shule za msingi,wakuu wa shule za sekondari,waratibu wa elimu na maofisa elimu mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamesimama kumkaribisha Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Tanzania Winfrida Rutahinfwa.

UCHAGUZI MKUU YANGA WAOTA MBAWA, SASA KUFANYIKA JUNI 7, VIONGOZI WATOA SABABU

$
0
0
Na Agness Francis,Blogu ya Jamii.

UONGOZI na Kamati ya Maandalizi Klabu ya Yanga SC wamefanya mabadiliko kwa kusogeza mbele tarehe ya Mkutano Mkuu wao.

Mkutano Mkuu wa klabu hiyo ulikuwa ufanyike Mei 5 mwaka huu lakini sasa unatarajia kufanyika Juni 7 mwaka huu katika Bwalo la Polisi Oyestabey jijini Dar es Salaam kuanzia saa tatu asubuhi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Charles Boniphase Mkwasa amesema kamati imekaa na kujadiliana, hivyo wameona wasogeze mbele tarehe ya mkutano huo kwa sababu za kimsingi zilizojitokeza.

"Tuna mechi nyingi za Ligi zitakazokuwa zinaendelea  hapa katikati pamoja na hilo baadhi ya  viongozi watakuwa nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza katika hatua ya makundi katika Shirikisho Barani Afrika dhidi ya  USM Alger, "amesema Mkwasa.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Makundi ya WhatsApp ya Yanga Tanzania Bakili Makele amewataka wanachama wote wa klabu hiyo nchini kulipi kadi zao.
"Ni muhimu kwa kila mwanachama kulipia kadi yake ya uanachama iwe ya Benki au ya kawaida ili auhudhurie mkutano huo ili kila mmoja apate haki yake ya kuchangia  na hatimaye kuondoa changamoto zilizopo na tusonge mbele,”amesema Makele.


KIROBA CHA MAHINDI CHAGANDA KICHWANI KWA KIJANA ALIYEKIIBA MLANDIZI

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha 
 KIJANA Frank Joseph (25) ,mkazi wa Dar es salaam amezua gumzo huko  Mlandizi mjini Kibaha mkoa wa Pwani  baada ya kiroba cha mahindi cha kilo 20 alichoiba nje ya nyumba ya mama mmoja kumganda kichwani kwa zaidi ya saa nne leo  Mei 3, 2019  majira ya saa 12 asubuhi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa walizipata kutoka kwa mwenyekiti Ally Nyambwilo, na kwamba baada ya taarifa hizo walifika eneo la tukio na ambapo walifanikiwa kumuokoa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa hatarini kushambuliwa na wananchi. 
Kamanda Shanna alieleza kuwa askari polisi walimchukua mtuhumiwa ambaye aliwaonyesha alikochukua mzigo huo lakini mwenye nyumba hakuwepo muda huo, hivyo mtuhumiwa alipelekwa kituoni akiwa na mzigo kichwani wakati harakati za kumpata mmiliki zikiendelea. 
Aidha Kamanda Shanna alisema, mmiliki wa mzigo huo alipofika kituo cha polisi Mlandizi alionana na mtuhumiwa huyo na kumfungua zipu ya suruali na kuongea maeneo yake na baadae mtuhumiwa alipoambiwa ashushe mzigo ukitoka kichwani ukabanduka. 
Kamanda Sganna aliwaonya vijana kuacha kuvuna vitu ambavyo hawakupanda na badala yake wajishughulishe kupata mali kwa jasho lao. 
Frank Joseph alikiri kuiba mzigo huo ambao uligoma kushuka kichwani hadi mhusika alipofungua zipu ya suruali ndipo akapata wepesi kuushusha mzigo huo.
"Nilikua napita nikaona mzigo upo nje nikaubeba nilivyokua naushusha haukutoka kichwani na ulivyogoma kutoka nikaamua kurudi kwa mwenyewe lakini sikumkuta hadi nilipomuona kituo cha polisi alivyofungua zipu ya suruali yangu na kuongea maneno yake nikaweza kuushusha mzigo" alisema 
Mtuhumiwa huyo alisema alijitahidi kufanya kila aliloweza ili mzigo huo utoke kichwani ikiwa ni pamoja na kulala ili akinyanyuka ubaki chini lakini aliponyanyuka, alinyanyuka nao kichwani! 
Hivyo baada ya kuzunguka nao kwa muda mrefu na alipochoka alilazimika kujisalimisha polisi ili asije akauawa na raia wenye hasira watakapobaini kuwa ni mwizi. 
 Frank ambae alidai anafanya kazi ya kusukuma mkokoteni ambapo aliwashauri vijana kuacha tamaa na kufanya kazi zao kwa bidii na kwamba hawezi kurudia tena kuiba baada ya tukio hilo.
Mtuhumiwa  anaedaiwa  kuiba kiroba cha mahindi chenye kilo 20 huko Mlandizi Kibaha Mkoani Pwani Frank  Joseph akiwa kituo cha polisi cha Mlandizi mkoa wa Pwani alikofikishwa huku akiwa na mzigo uliomganda kichwani na ni hadi alipofika mwenye nao ndipo uliposhuka kichwani 
Kamanda wa polisi mkoani Pwani  ACP Jonathan Shanna (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha polisi Mlandizi kuhusiana na tukio la wizi ambapo kijana Frank Joseph (23) aliiba kiroba cha mahindi chenye kilo 20 huko Mlandizi Kibaha ambapo baada ya kuiba mzigo uliganda juu ya kichwa mwenye nao alipofika na kuushusha. 
Picha na Mwamvua Mwinyi

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 03.05.2018

VITAMBULISHO VYA TAIFA KUWEZESHA WANANCHI DODOMA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOJITOKEZA

$
0
0
Kati ya fursa muhimu kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma ni kusajiiwa Vitambulisho vya Taifa kama sehemu ya maandalizi msingi ya kunufaika na kazi zitakazopatikanam baada ya Mkoa huo kupandishwa hadhi na kuwa Jiji. Kati ya fursa muhimu ni pamoja na fusra za kibiashara, ubia katika uwekezaji n.k ambazo zote hizi zinamlenga mtanzania.
Hayo yamebainika wakati wa kutembelea na kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu unaoendelea katika maeneo mbali mbali ya mkoa huo ikiwemo wilaya ya Dodoma.
Akizungumzia maendeleo ya zoezi hilo Afisa Usajili Mkoa wa Dodoma Bw. Khalid Marisho amesema mpaka sasa mwitikio wa wananchi ni mkubwa kulinganisha na hapo mwanza kabla wananchi hawajatambua na kuona manufaa ya kuwa na Kitambulisho cha Taifa.
Wananchi wa Kata ya Zuzu Wilaya ya Dodoma wameonyesha kufurahishwa na mwenendo wa  zoezi hilo; baada ya kutambua manufaa makubwa yapatikanayo kwa mtu kuwa na Kitambulisho
Mzee Ngowolo ni mkazi wa Zuzu mwenye Umri wa miaka 65, ambaye amezungumza na kueleza kwanini amejitokeza kusajiliwai. “Ni haki yetu ya Msingi sisi kutambuliwa kama Watanzania, mbali na kutambulika kirahisi kitambulisho kitaturahisishia katika upatikanaji wa huduma za kijamii kwani taarifa zote za muhimu zinazohitajika zitakuwepo kwenye Kitambulisho hicho” alisema
Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa nchini inayoendelea na zoezi la Usajili na Utambuzi zoezi ambalo linategemewa malizika kufikia mwezi mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.
 Wananchi wakiwa katika foleni kuelekea kwenye chumba cha usajili uliohusisha uchukuaji wa alama za kibaiologia, saini ya kielektroniki pamoja na picha zoezi linaloendelea katika kata ya Zuzu wilaya ya Dodoma tangu kuanza kwake tarehe 29/04/2018.
 Afisa Mkaguzi msaidizi wa uhamiaji Bw. Aloyce luhombo akifanya mahojiano na wananchi waliofika katika moja ya vituo vya usajili Vitambulisho vya Taifa Kata ya Zuzu ili kubaini hadhi halisi ya uraia wao.
 Wananchi kutoka mitaa mbalimbali kata ya Zuzu wakiendelea na zoezi la ujazaji wa fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa katika kituo cha kutoa huduma ya Usajili na Utambuzi Kata ya Zuzu wilayani Dodoma
 Mtendaji wa kata ya Zuzu Bw. Mabrouk Seif – (aliyeinama kwenye meza), Maccelina Chuwa -Mtendaji wa Mtaa wa Zuzu pamoja na Silvana Malyampa – Mwenyekiti wa Mtaa wakiwahudumia wananchi wa Kata na mtaa wa Zuzu waliofika katika moja ya Vituo vya usajili wa Vitambulisho vya Taifa wilayani Dodoma.
Bi Rehema Ngole, mkazi wa mtaa wa Soweto Kata ya Zuzu, akiweka saini ya kielektroniki kwenye mashine inayotumika kufanya Usajili na kurekodi taarifa za mwombaji wa Kitambulisho cha Taifa.

Duniani Leo Mei 3, 2018

MJ RECORDS TANZANIA RELEASE FIRST TRACK FOR A WIDE WORLD EXPECTED SINGER NAMED “KELLAH”

$
0
0
MJ records music audio studio from EAST AFRICA - TANZANIA is about to shake the top music charts in AFRICA and WORLD WIDE once again by introducing the long time caged singer named KELLAH from its zoo with an exclusive massive song called “UKINIMISS” in April 23, 2018. In their own words the management of KELLAH said, “We have big faith that this song will reach far (Whole Africa and worldwide), and we have KELLAH to back up our words”.
Now with 2 years of spadework and refinement under MJ RECORDS AUDIO STUDIOS, Kellah is set to untether her first new single; Produced by Daxo Chali, “Ukinimiss” perfectly fuses a catchy tropical house, trap to a mid temple afro-pop. The captivating music video shot and directed in Tanga, Tanzania by leading cinematographer Frank Papushka. "Ukinimiss" song contains in its instrumentation "brassy horn bleats", warm island rhythms and an African beat.
Lyrically, "Ukinimiss" is a plea for bringing back the memories of lovers, with Kellah asking her lover to meet again to places where they shared secrets and memories.
This song will be available in all digital platforms. To get in touch with KELLAH and watching her video, see the following links:

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images