Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

KCB BENKI YATOA MSAADA WA MAASHINE YA ULTRASOUND YA TSH MILIONI 14 ARUSHA

$
0
0
 Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha,Bi.Juvita Lubuva(kulia)akisalimiana na maofisa wa ofisi ya Meya wa jiji la Arusha walipofika katika Kituo cha Afya cha Ngarenaro kwa ajili ya kukabidhiwa  msaada wa  mashine ya Ultrasound yenye thamani ya Tsh Milioni 14  iliyotolewa na benki hiyo  kwa Kituo  hicho cha Afya.
 Mwakilishi wa Meya wa jiji la Arusha Bw.Michael Kivuyo(kushoto)akipokea msaada wa  mashine ya Ultrasound yenye thamani ya Tsh Milioni 14  kwa niaba ya Kituo cha Afya cha Ngarenaro,kutoka kwa Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha,Bi.Juvita Lubuva(kulia)
Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha,Bi.Juvita Lubuva(kulia)akimsikiliza jambo Mwakilishi wa Meya wa jiji la Arusha Bw.Michael Kivuyo(kushoto)pindi alipomkabidhi msaada wa  mashine ya Ultrasound yenye thamani ya Tsh Milioni 14 iliyotolewa na benki hiyo  kwa Kituo cha Afya cha Ngarenaro.

//michuzi2.rssing.com/chan-7007653/article4542-live.html

SWAHILI RADIO KUANZA KURUSHA MATANGAZO HEWANI HIVI KARIBUNI KUTOKEA JIJINI WASHINGTON D.C. USA

$
0
0
  Alex akifurahia baada ya mitambo kuonyesha mafanikio katika majaribio

 Wakurugenzi wa Swahili Radio Bwana Alex na DMK wakiendesha kipindi cha majaribio hewani

SWAHILI RADIO
Ni Radio iliyoanzishwa Jijini Washington DC USA na Kampuni ya "MMK MEDIA GROUP LLC " ambao wanamiliki Swahili Radio On Line,Swahili TV on Line,Swahilitv Blog, Swahili Magazine USA-AFRICA,na The Bridge Show ndani ya DCTV.
Radio hii pamoja na TV ziko kwenye majaribio kwa sasa na zitaanza kuwa hewani kwa watu wote kusikiliza na kuangalia punde muda wa majaribio utakapo malizika.Watanzania hao watatu wote kwa pamoja wanayofuraha kubwa kwa jinsi ambavyo majaribio ya kazi hizi yanavyoendelea na kwa kingereza wanasema THEY CAN'T WAIT TO BRING TO YOU WHAT YOU HAVE BEEN WAITING FOR.

"PROGRAMS ZA RADIO KWA KUANZIA"

*KIPINDI CHA BURUDANI NA MICHEZO DUNIANI*
*MAPENZI NA MAISHA*
*MAISHA UGHAIBUNI*
*HABARI ZA DUNIA*
*THE WEEKEND SPECIAL*

KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA SWAHILITV.BLOGSPOT.COM








michuano ya kombe la kagasheki yaingia fainali uwanja wa kaitaba, bukoba

$
0
0
Picha na Habari na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya BILELE FC  imelazimika kupigana kufa na kupona ili waweze kutinga hatua ya fainali katika michuano ya Kombe la Kagasheki ikicheza dakika 90 na timu ya Kitendaguro fc bila ya kufungana. Baada ya kuongezwa 30 Bilele FC imeweza kuifunga timu hiyo maarufu kwa jina la Makhirikhiri yeye maskani yake Kitendaguro - Kibeta. 
Bao la pekee la timu ya Bilele limefungwa dakika kipindi cha kwanza cha dakika 120 na mchezaji Ndomondo, huku wakicheza pungufu baada ya mwenzao kupewa kadi nyekundu katika kipindi cha pili cha dakika 90. 
Ushindi huu unawasogeza Bilele hatua ya Fainali wakimsubiri mshindi wa kesho kati ya timu ya Kashai Fc na timu Rwamishenye Fc mtanange utakaochezwa kesho Jumatano saa 10.00 jioni hapo hapo uwanja wa Kaitaba.

Timu zikisalimiana muda mfupi kabla ya mtanange kuanza

Timu zikisalimiana muda mfupi kabla ya mtanange kuanza hapa kwenye Uwanja wa Kaitaba
Picha ya pamoja Waamuzi wa mtanange huu na manahodha wa timu 

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya Barry White ya 'Can't Get Enough Of Your Love Baby' ni njema

CHADEMA chaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba nchini kote

$
0
0


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kuanzia jana kinaanza rasmi kuendesha Mabaraza ya Katiba, ambapo wananchi wote watashirikishwa kujadili na kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya, kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo;

1. Mikutano ya hadhara, itakayoanza leo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiongozwa na     timu mbili za viongozi wakuu, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibroad Slaa. 
    
    Mikutano hiyo itafanyika nchi nzima. Ratiba ya mikutano yote, itatolewa kwa umma,     kupitia vyombo vya habari (mainstream & social media).

2. Kutuma ujumbe mfupi kwa simu. Mwananchi anaweza kutuma maoni yake ya Katiba     Mpya kupitia simu ya mkononi, kwenye NAMBA HII YA SIMU; 0789 24 82 24.


4. Mitandao ya kijamii, mf; Jamii Forums, facebooks, twitter, group emails, k.m mabadiliko, 
    wanabidii n.k, utaratibu wake utatolewa kwa umma, kupitia vyombo vya habari, ikiwa ni 
     pamoja na kuwekwa hapa, namna ambavyo Watanzania wote watashiriki kutoa maoni 
     yao kwa njia hii.

Tumaini Makene
CHADEMA Senior Information(Press) Officer
0752 691569/ 0688 595831

Vijana kutoka Ujerumani wafurahia ushirikiano na Serikali ya Tanzania.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana kutoka Taasisi ya MitoSt ya Hamburg Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia ushitikiano wao wa kubadilishana rasilimali watu na kujitolea kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth Coalition (TYC) walipotembelea Wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo wageni hapo wamekuja na ujumbe mahususi wa furaha kwa wote.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana  wanaojitolea kutoka Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia mpango wao wa kubadilishana rasilimali watu kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth Coalition jana jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizarani hapo.
 Afisa Mipango wa MitOst  Mete Odabasi akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kwa niaba ya Wizara ya Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo kufuatia ushirikiano waliopewa katika ziara yao hapa nchini.
 Mmoja wa wanachama wa Tanzania Youth Coalition (TYC) ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bibi Neema Kassala (kushoto) akichangia mada walipokutana na Mkurugenzi wa  Maendeleo yaVijana walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam kufuatia kuwa wenyeji wa wageni kutoka Taasisi ya MitoSt ya jijini Hamburg Ujerumani waliopo nchini.
 Mmoja wa wakilishi kutoka Taasisi ya MitOst yenye makao yake jijini Hamburg Ujerumani Bibi Lusinja Czesnik (wa pili kutoka kushoto) akichangia mada jana walipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana leo jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya vijana hapa nchini.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya kitamaduni kutoka kwa Afisa Mipango wa taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani Mete Odabasi walipokutana na Mkurugenzi huyo  Jana jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya vijana hapa nchini.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza namna Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo  jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana na wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza nama Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Frank Shija wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

JENGO LINAPANGISHWA MAENEO YA KINONDONI JIJINI DAR

$
0
0
Jengo la SSTL Group linalofaa kwa matumizi ya Kiofisi na lenye urefu wa Ghorofa tatu lililopo Maeneo ya Kinondoni Kanisani kama ukitokea Biafra,linapangishwa kwa bei nzuri sana.

kwa mawasiliano
+255 22 2761186
+255 22 2761019

Email: sstl@sstl.co.tz
Muonekano wa Jengo hilo kwa Upande wa mbele.
Muonekano wa Jengo hilo kwa upande wa ubavuni.
Muonekano wa ndani upande wa chini.
Jenereta la kisasa kabisa.
Ngazi za kwenda juu na chini.
Moja ya sehemu za Ofisi ndani ya jengo hilo.
Sehemu ya Mapokezi.

warsha ya kuboresha mahusiano mema ya utendaji unaozingatia misingi ya sheria mahali pa kazi yafunguliwa mkoani morogoro

$
0
0
Afisa Rasilimali watu kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Sarah Zayumba, (aliyesimama), akisisitiza jambo wakati akifungua warsha inayolenga kuboresha mahusiano mema sanjari utendaji unaozingatia misingi ya sheria mahali pa kazi. Warsha hiyo inayojumuisha wajumbe wa Tuico kupitia TBL nchini imefanyika mkoani Morogoro jana.
Afisa Rasilimali watu kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Sarah Zayumba, wa pili kushoto, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Tuico Taifa kabla ya kufungua rasmi warsha ya siku mbili ya wajumbe wa Tuico kupitia TBL nchini iliyofanyika mkoani Morogoro jana. Warsha hiyo pamoja na mambo mengine, imelenga kuboresha mahusiano mema sanjari na utendaji unaozingatia misingi ya sheria mahali pa kazi.
Wajumbe wa Tuico kupitia Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), na baadhi ya viongozi wa TUICO Makao Makuu, wakiwa katika picha ya pamoja mkoani Morogoro jana, muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha iliyojadili pamoja na mambo mengine, maboresho, mahusiano mema sanjari na utendaji unaozingatia misingi ya sheria mahali pa kazi.

TANROAD YAPANIA KUONDOA KERO YA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI MWANZA

$
0
0
Meneja wa TANROAD mkoa wa Mwanza Mhandisi Leonard Kadashi akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujenzi unaoendelea wa moja ya madaraja na hapa ilikuwa ni katika eneo la daraja la Mabatini jijini Mwanza, ambalo linajengwa sambamba na utanuzi wa barabara njia tatu kuondoa kadhia ya msongamano.
  
WAKALA wa Barabara Mkoa wa Mwanza(TANROAD) hatimaye imeanza utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete na serikali kwa kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya Lami ya Usagara hadi Kisesa yenye urefu wa kilomita 17.8 ili kupunguza msongamano wa magari makubwa na madogo kuingia Jijini Mwanza.


Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mwanza Mhandisi Leonarld Kadashi alisema serikali baada ya kupata fedha ilitangaza kazi na kupatikana Mkandarasi aliyeshinda ambaye ni Kampuni ya kizalendo ya Nyanza Road Works Ltd ya Jijini Mwanza ambapo kwa sasa Mkandarasi huyo yupo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa barabara hiyo ya Usagara-Kisesa ya kiwango cha lami.
 “Kazi imeanza tangu mwezi Julai mwaka huu na inaendelea kwa kasi na tayari Mkandarasi aliyopo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa barabara hiyo  anaendelea na kazi ya kusafisha barabara ambapo kilomita 5 tayari na ujenzi wa madaraja sanjari na ujenzi wa nyumba za kambi ya Mhandisi mushauri na msimamizi na wafanyakazi wake kisha kuendelea na ujenzi wa kuweka lami”alisema

Mama Lishe wa Kichini na Swala zima la Usafi

$
0
0
Heshima yako Ankal.

Naomba kushea na Wadau swala hili la hali ya mama lishe wa uchina kuhusiana na suala la Usafi.Hapa kwetu Tanzania mama lishe wengi hawazingatii suala la usafi wa Mazingira wanayofanyia kazi.Matokeo yake watu wengi kutopendelea kula/kununua chakula chao.

Hali ni Tofauti China,watu wengi wanakula kwa Mama Lishe kwa sababu mazingira ya maandalizi ya chakula chao ni mazuri.Binafsi walikuwa wananishangaa ninapopata chakula hotelini kwamba ni gharama sana.Yaani Lunch time mtu anabeba familia yake anaenda kupata msosi kwa Mama lishe.Wachina wako busy sana kiasi kwamba hata muda wa kupika wengine hawana!Hapo ni jijini Guangzhou.

Hii ni changamoto kwa mama lishe wa kibongo ambao wametapakaa kila kona.Ni ajira inawaingizia kipato.

Wasukuma Maguta wapo lakini ni wasafi sana,wa kwetu ni wachafu hawaheshimu kazi zao.Niliangalia mambo mengi nikawa najaribu kulinganisha na nyumbani Tanzania.

Wenzetu wako mbali sana.

Na Mdau

Kamati ya Mbio za Uhuru Marathon yatangazwa rasmi leo

$
0
0
 Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella Mukangara akitangaza majina ya wanakamati aliowateuwa kuratibu mbio za uhuru mwaka huu nchini,Dkt Mukangara amewataja wajumbe hao kuwa ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq  (Mwenyekiti) na  Wajumbe wengine katika kamati hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa. Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
 Mratibu wa mbio za uhuru nchini Innocent Melleck akizungumza na waandishi wa habari juu ya mipango mbalimbali ya mbio za uhuru nchini ,Kulia ni Waziri wa habari,Vijana,utamaduni na michezo Dr Fenella Mukangara ambapo waziri amewateuwa wajumbe kumi watakaoratibu mbio hizo mwaka huu.
Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali nchini wakiwa katika chumba cha mikutano cha wizara ya habari tayari kumsikiliza Mheshimiwa waziri atangaze kamati hiyo.
==========   ========   =========

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara jana alitangaza wajumbe watakaosimamia mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Dk. Fenella alisema wajumbe wa kamati hiyo itakayokuwa na watu 10 itakuwa na jukumu la kuhakikisha mbio hizo zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kamati hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq huku ikiwa na wajumbe wengine kutoka katika sekta mbalimbali nchini.
Wajumbe wengine katika kamati hiyo iliyoundwa na waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sofia Mjema, Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda na Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa.
Wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals, Innocent Melleck, Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), Gabriel Nderumaki, George Kavishe kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mhariri Mtendaji wa Uhuru, Jossiah Mfungo na Habib Gunze WA Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.
Waziri Fenella alisema mbio hizo zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne kukiwa na mbio ndefu za kilomita 42, mbio za kati kilomita 21, mbio za kujifurahisha kilomita 5 na mbio fupi ambazo ni maalumu kwa viongozi zikiwa za kilomita 3.
“Mbio hizi zina lengo kuu la kuimarisha umoja, upendo, mshikamano na amani kwa Taifa letu. Tunategemea Watanzania wengi, ikiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, wanafunzi wa ngazi mbalimbalio na wananchi kwa ujumla wataungana na kushiriki mbio hizi,” alisema.
Naye Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema wazo kubwa la kuanzisha mbio hizo ilikuwa ni kutaka kuwakumbusha Watanzania kuuenzi umoja, amani, mshikamano ulipo pamoja na uhuru wetu.
Mratibu huyo alisema, mpaka sasa wanariadha zaidi ya 300 kutoka nje ya Tanzania wameomba kushiriki mbio hizo za aina yake hapa nchini.
“Sisi kama vijana tukaona kuna haja ya kufanya kitu cha kuwakumbusha Watanzania wenzetu kwani tunatakiwa kudumisha urithi wa amani, mshikamano na uhuru wetu tulioachiwa na mababu zetu,” alisema.
Melleck alisema mbali na mbio hizo kufanyika siku hiyo, pia kutakuwa na tamasha kubwa la burudani litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam ikiwa ni mkesha wa kusubiri siku ya Uhuru.
Mbali na hayo Waziri Fenella naye alizitaka taasisi mbalimbali kuhakikisha wanazidhamini mbio hizo kwani zina manufaa kiubwa kwa taifa.

Rais Kikwete afanya Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Adam H. Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam jana, Jumanne, Agosti 13, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi unaanzia Juni 8, mwaka huu, 2013.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mayingu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF.

Bwana Mayingu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

14 Agosti, 2013

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa akagua kazi ya Ujenzi wa Mkuza wa bomba la Gesi katika wilaya ya kilwa Mkoani Lindi

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abadalah Ulega akipata maelezo ya ujenzi wa Mkuza wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam toka kwa Eng Ahmeid Chinemba,Mratibu wa Mradi Mkoa wa Lindi alipokagua kazi zinavyoendelea.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abdalah Ulega akisikiliza maelezo toka kwa Mratibu wa mradi huo,Eng Ahmeid Chinemba alipokuwa akikagua kazi zinavyoendelea za kuandaa njia ya litakapopita Bomba la gesi kuanzia vijiji vya somanga hadi Kiranjeranje wilayani Kilwa.
Kambi ya Njia nne wilayani Kilwa ni Moja kati ya kambi za Wachina Watakaoanza kutandaza bomba la kusafirisha Gesi kati ya Songosongo,Mtwara kuelekea Dar Zikiwa katika hatua ya umaliziaji wa majengo ya kuishi wafanyakazi..Kambi kama hii ipo katika kijiji cha Nangurukuru na Kitomanga wilayani Lindi.

Na Abdulaziz Video,Kilwa

Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi,Abdallah Ulega amefanya ziara ya siku moja kukagua maendeleo ya Ujenzi wa njia ya bomba la gesi(Mkuza)kazi ambayo imeanza kati ya Songosongo,Mtwara Dar na kutarajiwa kazi zote kukamilika ndani ya Miezi 18.

Ulega alitembelea kati ya kijiji cha Somanga na Kiranjeranje kukagua kazi inavyoendelea na changamoto za na kuzungumza na wananchi na kuwataka waitumie vyema fursa hiyo katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa Ushirikiano kwa wawekezaji ili wanufaike na huduma za kimaendeleo katika wilaya yetu.

“Ndg zangu wana kilwa hizi fursa mzitumie kwa kusomesha watoto wenu ili wanufaike na ajira za gesi hii,Hata hivyo nasikitika kwa kuwa nimeambiwa na hawa wachina kuwa mmeanza kuwaibia jamani tutafika mlikuwa kwa amani na hawa wageni mnapata ajira za muda mnalipwa sasa angalieni tumewaletea askari nyie wenyewe mnaona raha?Serikali imejipanga na kusimamia mnanufaika na miradi hii…alimalizia Ulega alipokuwa akisalimiana na wananchi wa njia nne wilayani Kilwa.

Kwa Upande wake mratibu wa Mradi huo wa Mkuza Mkoa wa Lindi,Eng Ahmeid Chinemba akitoa maelezo ya kazi hizo kwa Mkuu wa wilaya huyo,Alibainisha kuwa kazi hiyo ambayo Itagharimu Jumla ya Dola Bilion 1.2 inatekelezwa na kampuni ya mabomba ya petrol ya China imeanza kwa kuandaa mkuza kati ya Songosongo Nyamwage kuelekea Dar es salaam na Somanga Nangurukuru Mtwara.

Chinemba pia alieleza kuwa sambamba na ukamilishaji wa mkuza huo pia tayari kambi kuu 3 za za malazi na ofisi kwa wafanyakazi wa kazi hizo zipo katika hatua ya mwisho katika Vijiji vya Njianne,Nangurukuru na Kitomanga ambapo pia mabomba ya kazi yakiwa yanapokelewa katika kambi ya Kiranjeranje.

Kufuatia Uwepo wa Gesi asilia ya Songosongo wilayani Kilwa na kusafirishwa kwenda Dar tayari inauzwa kwa zaidi ya Viwanda 30,huku jamii ya wakazi kijiji cha Songosongo wakinufaika na utumiaji wa nishati ya umeme bila malipo huku Halmashauri ya wilaya Kilwa ikikusanya kodi ya Huduma pamoja kusaidia huduma mbalimbali za kijamii

Zaidi ya Milioni 37/- zatolewa na Airtel Tanzania kwa washindi wa 'Airtel Yatosha'

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akimkabidhi  Bw. Godbless Kweka kitita cha shilingi milioni moja aliyojishindia katika droo ya promosheni  ya Airtel Yatosha wiki hii. Wanaoshudia (kutoka wapili kushoto) ni washindi wengine wa milioni moja Bw. Rashid Hamis, Bi. Magret Kalengea na Bw. Hamis Athumani  Esia. Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi kuu ya Airtel Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akimkabidhi  Bi. Magret Kaengea (kulia) shilingi milioni moja aliyojishindia katika droo ya promosheni ya Airtel Yatosha wiki hii.
----------------------------------------------
Airtel kupitia promosheni yake kabambe ya Airtel Yatosha shinda nyumba 3 tayari imeshakabidhi jumla ya shilingi milioni 37/- taslim kwa wateja wake nchini.
Airtel leo ikiwa katika muendelezo huo wa kutoa zawadi imewazawadia washindi saba wa wiki hii kiasi cha shilingi milioni saba ambapo wateja 7 kila mmoja aliondoka na kitita chake cha shilingi milioni moja kufuatia droo iliyochezeshwa makao makuu ya airtel siku ya Jumatatu ya wiki hii.

Mmoja wa washindi walioibuka na kitita cha shilingi milioni moja ni Bw. Rashidi Hamis ambaye ni fundi wa magari aliyeeleza wazi kuwa hakutegemea kabisa kupata kiasi hicho cha fedha katika msimu huu na anamshukuru Mungu kwa Airtel kumchagua kama mmoja wa washindi hao.
“Nawashukuru sana Airtel, kwa pesa hii nitaitumia kwa ajili ya shughuli zangu binafsi za kimaendeleo na nategemea itaniendeleza kiuchumi kwa kuweza kuimarisha maisha yangu,” alisema.
Washindi wengine wa milioni moja ni pamoja na John Joseph kutoka Karatu, Gideon Rwegosora kutoka Tanga, Omari Abeid kutoka Shinyanga, Hamis Esia kutoka Dar es salaam, Godbless Kweka kutoka Mtwara na Magreth Kalengea kutoka Dar es salaam.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Airtel Bw. Jackson Mmbando alisema leo tunayofuraha kupata washindi wa promosheni ya Airtel yatosha na kuwakabithi zawadi zao. Washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini  na kujishindia kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kwa kutumia huduma za Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi vyetu mbalimbali.
Wateja wa Airtel wanaweza kujishindia milioni moja kila siku kwa kupiga *149*99#, chagua 2, chagua kifurushi chochote cha siku, wiki au mwezi kitakacho kufaa. Kumbuka vifurushi hivi pia vitakuingiza moja
kwa moja kwenye droo ya Airtel Yatosha Mpaka sasa Airtel imetoa shilingi milioni 37 kwa washindi 37 na 
inaendelea na promosheni hiyo ambayo inadumu kwa siku 90.
Sambamba na hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni jijini Dar es Salaam bado zinashindaniwa kupitia promosheni ya Airtel yatosha baada ya moja kuchukuliwa na mshindi wa kwanza Bw. Silvanus Juma mkazi wa Iringa.

Bwana Johan Hosselaer wa E-Exchange ya Ubelgiji akutana na Balozi Dr. Diodorus Kamala leo

$
0
0
Bwana John Hosselaer mtaalam mshauri wa masuala ya mipango na mikakati ya maendeleo wa taasisi ya E-Exhange ya Ubelgiji akiwasilisha kwa Dr. Diodorus Buberwa Kamala Balozi wa Tanzania Ubelgiji na Jumuiya ya Ulaya taarifa ya ziara yake ya kikazi aliyofanya Tanzania. Taarifa hiyo inabainisha mikakati mbalimbali inayoweza kusaidia kuinua kipato cha wakulima kwa wastani wa shilingi za Kitanzania 2400 kwa siku. Utafiti huo umefanyika Wilaya ya Missenyi, kata Kanyigo.

warsha ya misingi ya sheria mahali pa kazi kwa Wajumbe wa Tuico kupitia TBL

$
0
0
 Afisa Rasilimali watu kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Sarah Zayumba, (aliyesimama), akisisitiza jambo wakati akifungua warsha inayolenga kuboresha mahusiano mema sanjari utendaji unaozingatia misingi ya sheria mahali pa kazi. Warsha hiyo inayojumuisha wajumbe wa Tuico kupitia TBL nchini imefanyika  mkoani Morogoro jana.
 Afisa Rasilimali watu kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Sarah Zayumba, wa pili kushoto, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Tuico Taifa kabla ya kufungua rasmi warsha ya siku mbili ya wajumbe wa Tuico kupitia TBL nchini iliyofanyika mkoani Morogoro jana. Warsha hiyo  pamoja na mambo mengine, imelenga kuboresha mahusiano mema sanjari na utendaji unaozingatia misingi ya sheria mahali pa kazi.
 
Wajumbe wa Tuico kupitia Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), na baadhi ya viongozi wa TUICO Makao Makuu, wakiwa katika picha ya pamoja mkoani Morogoro jana, muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha iliyojadili pamoja na mambo mengine, maboresho, mahusiano mema sanjari  na utendaji unaozingatia misingi ya sheria mahali pa kazi. 

Rwanda MPs discuss evictions of Rwandans from Tanzania

$
0
0
photo
About 4,000 Rwandans have been received in Kirehe district after being evicted from the Kagera region in the north-western part of Tanzania since last week. The New Times/Timothy Kisambira.
The East African Community (EAC), should use appropriate channels to sort problems affecting citizens of any partner state, outgoing Speaker of Parliament Rose Mukantabana told lawmakers yesterday.

She was briefing MPs about last Thursday’s meeting of the Parliament’s Bureau, where matters concerning the eviction of Rwandans from Tanzania were discussed. 

The Bureau, made up of the Speaker, president of the Senate and heads of House committees, comforted the returnees, rallied for their support and lauded government for the effort put in facilitating the affected people.

The MPs met yesterday for an extraordinary session convened to pass two Bills – one on genocide ideology and another establishing the general statutes for public service.

Mukantabana said: “The final outcome of our discussions was the appreciation that within the East African Community, if a problem arose, it can be discussed at a diplomatic level, and a solution worked out in a mutual manner.”

The Speaker stressed that it was important information she had to share with MPs though it was not time for debate on the matter.  About 4,000 Rwandans have been received in Kirehe District after being evicted from the Kagera region in the north-western part of Tanzania since last week.

Global Football Tournament 2013 ( Show The Red Card to Racism)

$
0
0
Dear sir/madam,

Tampere Africans Sports (TAS) ry would like to warmly invite you to attend fourth 
Global football tournament 2013 on Sunday 18.8.2013 and Sunday 1.9.2013 at Pyynikki stadium.

Global football tournament is an annual event organised by and for
foreigners living in and around Tampere. The tournament’s main goal is to
encourage interaction between and amongst immigrant groups.

TAS ry is a registered association that aims to organise and encourage
immigrants towards sports and other activities.

HOTUBA YA JK KATIKA MAJUMUISHO YA ZIARA YAKE YA SIKU SITA MKOA WA KAGERA JULAI 2013

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images