Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Wateja 84 wa Tigo wajinyakulia simu janja za TECNO R6

$
0
0

Huku ukiwa imebakia wiki tatu tu kabla ya kufika kikomo cha promosheni kabambe ya Nyaka Nyaka bonus inayoendeshwa na kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania, kampuni hiyo imewahamasisha wateja wake kuchamgamkia zawadi za bure za simu janja 268 zenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 zinazopatikana kupitia promosheni hiyo. 

Katika promosheni hiyo ya Nyaka Nyaka Bonus itakayofikia tamati katika wiki ya pili ya mwezi Mei, Tigo inatoa jumla ya simu janja 84 kila wiki kwa wateja wanaonunua bando za intaneti kuanzia TSH 1,000 kupitia Tigo namba *147*00#.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi za simu janja kwa washindi 47 kutoka Dar es Salaam kati ya washindi 84 waliopatikana nchi nzima katika promosheni hiyo wiki hii, Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael alisema kuwa  pamoja na fursa ya kujishindia simu hizo janja, wateja wote wanaonunua bando za intaneti kupitia *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa ajili ya matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter. 

‘Kupitia promosheni hii Tigo inalenga kuongeza idadi ya wateja wenye uwezo wa kufurahia huduma bora zaidi za kidigitali zinazopatikana kupitia mtandao wenye kasi ya juu zaidi na ulioenea zaidi nchini wa Tigo 4G. Hivyo tunawahamasisha wateja wetu wasibaki nyuma katika fursa  hii ya kipekee ya kunyakua simu hizi janja zenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6,’ Woinde alisema.

Naye Wilson Chusa ambaye ni mchungaji wa kanisa la Penuel katika eneo la Mtoni Kijichi, Dar es Salaam alielezea furaha yake kwa kushinda simu hiyo ambayo alisema itamsaidia kuwasiliana na washirika wa kanisa lake kwa urahisi zaidi. 

Promosheni ya Nyaka Nyaka bonus ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora ya kidigitali kupitia mtandao Tigo 4G ulioenea katika miji 22 nchini. 
 Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi simu kwa washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu 812 kwa washindi kutoka sehemu mbali mbali za nchi waliotumia namba *147*00# kununua bando za intaneti kutoka Tigo, huku kukiwa na simu 268 ambazo bado zinashindaniwa. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.
Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi simu kwa washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu 812 kwa washindi kutoka sehemu mbali mbali za nchi waliotumia namba *147*00# kununua bando za intaneti kutoka Tigo, huku kukiwa na simu 268 ambazo bado zinashindaniwa. Kushoto ni  Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael

TUNAAMINI WAAMUZI WATENDA HAKI MECHI YETU DHIDI YA YANGA-HAJJI MANARA

$
0
0
Uongozi wa klabu ya Simba umesema unaamini kabisa waamuzi wa mechi yao dhidi ya Yanga Jumapili, watatenda haki.


Klabu hiyo kupitia kwa Afisa habari wao, Haji Manara amesema hawatawalalamikia waamuzi kabla lakini wanaamini kikubwa ni haki na zaidi waamuzi wengi ni vijana na wanajua maana ya mchezo wa haki.



“Waamuzi watakaocheza tunaamini watafuata sheria 17 za soka kwa ajili ya kufanya haki itendeke,” alisema.

Manara amesema kuwa mpaka sasa kikosi chao hakina majeruhi hata mmoja kikosini kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao, Yanga utakaopigwa kwenye dimba la Jumapili Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Simba wakiwa vinara wa ligi hiyo kwa pointi 59 kutokana na mechi 25, watakuwa wenyeji wa mchezo huo dhidi ya Yanga waliopo nafasi ya pili na pointi 48, huku wakiwa wameshuka dimbani mara 23.

Simba inashuka dimbani Jumapili kuivaa Yanga katika mechi ambayo kama watashinda, basi watakuwa wamejihakikishia kubeba ubingwa kwa asilimia 95.

Manara amesema kwamba maandalizi yanaendelea vizuri baada ya kikosi cha timu hiyo kurejea wakitokea Morogoro walipoweka kambi ya siku tatu.

Amesema taarifa kutoka benchi la ufundi kwamba kikosi hicho kinaendelea vizuri na tayari kwa ajili ya mchezo huo kwa kuhakikisha wanapata pointi ili kujiweka katika mazingira mazuri ya mbio za ubingwa.

“Hadi leo hakuna majeruhi na timu inaendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Boko na kikubwa tunawaomba waamuzi kuzitendea haki kanuni na sheria za soka, waepuke kuingia na matokeo yao mfukoni,"alisema Manara.

Manara amesema anaiheshimu Yanga haswa kuelekea katika pambano hilo la watani wa jadi, hivyo huenda wasipate ushindi ila wanaenda kutafuta pointi muhimu katika mchezo huo.

“Tuna imani ya timu yetu inaweza kuchukuwa ubingwa, lakini sio kama tutashinda mechi zote, mashabiki watambue kwamba kuna mechi tutapoteza, lakini kikubwa wachezaji wanapambana kuhakikisha tunafikia malengo yaliyokuwepo tangu awali,” amesema Manara.


CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
TAASISI ya Childbirth Survival International (CSI) imetoa wa vifaa vya akina mama wajawazito ambavyo hutumika wakati wa kujifunga katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Lengo la msaada huo ni muendelezo wa CSI wa kuendelea na jitihada zao za kufanikisha uzazi salama nchini huku moja ya jukumu lao kubwa ni kuhakikisha vifo kwa mama mjazito na mtoto mchanga vinapungua au kwisha kabisa.

Akizungumza leo baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mmoja wa Waanzilishi na Mkurugenzi Mkazi nchini Tanzania Stella Mpanda amesema wamekuwa na utaratibu wa kusaidia na kutoa vifaa vya kujifungulia katika hospitali mbalimbali na sasa wameona ni vema wakatoa msadaa huo Hospitali ya Mnazimmoja.

"Tumeamua kusaidia vifaa hivi kwani nia yetu ni kuona mama mjazito na mtoto mchanga wanakuwa salama.Vifaa ambavyo tumekabidhi leo vitarahisisha mkunga kuwa na uhakika wa vifaa na hatimaye mama mjazito kujifungua salama.

"Ni vifaa ambavyo vimetimia kwani ndani yake kuna kila kitu kikiwemo kifaa cha Peguine Pum ambayo husaidia kumsafisha mtoto mara tu baada ya kuzaliwa kwani huondoa uchafu ambao huenda ameuvuta.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda(wa kwanza kulia) akikabidhi msaada wa vifaa vya akina mama wajawazito kwa Dk. Fillo Hyera (wa tatu kushoto) ambavyo hutumika wakati wa kujifunga katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda(wa kwanza kulia) akimkabidhi Mama Mjamzito. Yusta Prospa moja ya kifaa tiba ambacho hutumika wakati wa kujifungulia katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Dk. Fillo Hyera(kulia) akitoa shukrani kwa  uongozi wa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI) mara baada ya kukabidhi vifaa tiba vya wakina mama wajawazito.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

AZAM vs MTIBWA, SASA KUPIGWA SAA 10 JIONI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MCHEZO kati ya Klabu ya Azam FC na Mtibwa Sugar uliotarajiwa kuchezwa saa 8 mchana umefanyiwa mabadiliko ya muda, ambapo sasa utafanyika Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro, kesho Jumamosi saa 10.00 jioni.

Awali mchezo huo ulikuwa ufanyike saa 8.00 mchana, lakini Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeamua kuusogeza hadi jioni kutokana na ratiba ya wadhamini wa matangazo ya televisheni Azam TV kutobana muda huo.

Tayari kikosi cha Azam FC kimewasili mkoani Morogoro tokea jana saa 12 jioni kikiwa tayari kuvaana na Wakatamiwa hao, ambapo jioni ya leo kitafanya mazoezi ya mwisho kujiweka sawa na mchezo huo.

Timu hizo zimekuwa na upinzani mkali mara zote zinapokutana, katika rekodi zimecheza mechi 19 za ligi, Azam FC ikiwa imeshinda mara tisa, Mtibwa Sugar mara mbili huku mechi nane zikiisha kwa sare, ambapo hivi sasa inasubiriwa kuona namna matokeo yatakavyokuwa katika mechi yao ya 20 ya ligi.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye ligi ilikuwa ni Novemba 27 mwaka jana, zikitoka sare ya bao 1-1, Azam FC ikitangulia kufunga kupitia kwa winga Enock Atta kabla ya Kelvin Sabato kuisawazishia Mtibwa Sugar kwa mkwaju wa moja kwa moja wa adhabu ndogo.

Azam FC itamkosa Kocha Mkuu wake, Aristica Cioaba, ambaye amesimamishwa na Kamati ya Saa 72, kufuatia kuondolewa kwenye benchi na mwamuzi Jonesia Rukyaa, katika mchezo uliopita dhidi ya Njombe Mji ulioisha kwa suluhu.

Nahodha Msaidizi, Agrey Moris, atarejea tena kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kutocheza mchezo mmoja kufuatia kadi nyekundu iliyotokana na kadi mbili za njano aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ulioisha kwa Azam FC kupoteza kwa mabao 2-0.

Kikosi cha Azam FC kimejipanga kufanya vizuri katika mchezo huo na kuondoa rekodi mbaya ya kutoshinda katika mechi tatu zilizopita, ikipata suluhu mbili dhidi ya Mbeya City na Njombe Mji na kufungwa mmoja.

Hadi sasa kwenye msimamo wa ligi inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 huku wapinzani wao Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya sita kwa pointi 33

KAMISHNA WA OPERESHENI WA JESHI LA ZIMAMOTO AKABIDHI CHETI CHA SHUKRANI

$
0
0
 Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy J. Mwakatage (kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani “certificate of appreciation” Meneja Mkuu wa Dar es Salaam Yacht Club (DYC) Bw. Brian Fernandes (kushoto)  kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Dar es Salaam Yacht Club Masaki Jijini Dar es Salaam mapema leo hii.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy J. Mwakatage (kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani “certificate of appreciation” nahodha wa Tanzania Sea Rescue (TSR) Bw. Ally Saleh Kitobe aliyeiwakilisha kampuni yake  kwenye hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Dar es Salaam Yacht Club Masaki Jijini Dar es Salaam mapema leo hii.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy J. Mwakatage (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni zilizopewa vyeti vya shukrani “Certificate of appreciation” kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Brian Fernandes (wa tatu kushoto) kutoka Dar es salaam Yacht Club (DYC), Ally Saleh Kitobe (wa pili kushoto) kutoka Tanzania Sea Rescue na Issa Lwamba (wa pili kulia) kutoka Dar es Salaam Independent School (DIS). Makabidhiano yaliyofanyika mapema leo hii katika viwanja vya Dar es Salaam Yacht Club Masaki Jijini Dar es Salaam.

KAIMU BALOZI WA ZIMBABWE NCHINI AZUNGUMZA NA WABUNGE WA BUNGE LA TANZANIA WANAOWAKILISHA BUNGE LA AFRIKA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
 Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
 Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
 Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, walioongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge hao, Mhe. Asha Juma (katikati) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulie na kulia ni Mbunge wa Momba, Mhe. David Silinde
Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akiagana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

DKT. MWAKYEMBE AKUTANA NA WADAU WA SEKTA ZA WIZARA YA HABARI BUNGENI LEO

$
0
0
 Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Habari mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.
 Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Utamaduni mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.
 Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Sanaa na Mitindo mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.
 Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Muziki mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.

SERIKALI YAIPELEKA SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KWA WADAU KUPATA MAONI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu- Arusha
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kufanya mabadiliko katika Sera zake mbalimbali ili kuweza kuendana na wakati na kuwezesha kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoa huduma kwa watanzania.

Katika kulifanikisha hilo Wizara imeamua kuipeleka Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 kwa wadau ili iweze kutolewa maoni na baadae kufanyiwa marekebisho kuiwezesha kuendana na wakati.

Akifungua kikao kazi cha wadau wa Mashirika Yasiyo ya kiserikali kuijadili Sera ya Taifa ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Jijini Arusha, Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bibi Sihaba Nkinga amesema  kuwa  maoni ya wadau ni muhimu sana  katika mchakato wa maboresho wa Sera hiyo.

Bibi. Sihaba Nkinga ameleza kuwa Serikali imeamua kuwashirikisha wadau hao kwani kwa asilimia kubwa ndio watekelezaji wa Sera hiyo katika majukumu yao ya kila siku.

Ameongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa kazi zinazofanywa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini na zoezi hili la kuiboresha Sera hiyo litaleta mageuzi makubwa katika Sekta.
  Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akifungua kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
 Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Marcel Katemba akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali  ya kisera wakati wa ufunguzi wa  kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau wa NGOs kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Nicholous Zakaria  akieleza kuhusu umuhimu wa Baraza katika kuratibu utendaji kazi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini wakati wa ufunguzi wa  kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
  Baadhi ya wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini mara baada ya kufungua kikao kazi kilichofanyika Jijini Arusha kilichowakutanisha wadau hao kujadili maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali watatu kulia waliokaa  ni Mkurugenzi na Masajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NDEGE KUBWA YA ABIRIA YA EMIRATE KUTUA NCHINI YAIPANDISHA TANZANIA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA YA USAFIRI WA ANGA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) imesema kuwa kutua kwa Ndege kubwa ya ‘gorofa’ A380 ya Fly Emirates imedhihirisha kuwa uwanja  wa Kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius K Nyerere  na vyombo vyake kuwa madhubuti katika usafiri wa anga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Hamza Johari amesema  kuwa ndege hiyo licha kupata udhuru wa kushindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mauritius kumeipa heshima nchi katika kuwa na viwango katika utaoaji huduma ya usafiri wa anga.

Amesema kuwa Rubani wa ndege A380 ya Fly Emirates alifanya busara ya kuamua  baada ya kuona hali ya hewa ya Mauritius kutokuwa nzuri na  kuamua kutua kwenye Uwanja wetu wa kimataifa wa Mwalimu Julius  K Nyerere  na kuamini kuwa atatua bila wasiwasi.

Johari amesema kufuatia kutua kwa ndege hiyo kubwa  nchi imeweza kupata mapato katika huduma mbalimbali za kijamii kutokana na abiria waliokuwa katika ndege hiyo zaidi ya watu 500 ambao wote walilala katika hoteli zilizopo nchini.

Amesema kuwa ndege hiyo kubwa ya abiria duniani ndio mara ya kwanza kutua katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu  Julius K. Nyerere hivyo inaonyesha kujizatiti katika utoaji katika utoaji wa huduma ya usafiri wa anga.

Ndege hiyo imetua Aprili 24 katika uwanja wa Ndege Mwalimu Julius Nyerere ikitokea Dubai ambaye ilishindwa kutua mara tatu katika uwanja wa Mauritius na kuja kutua Tanzania

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kuwa wamekuwa na asilimia  64 kutoka 37 kwa viwango vilivyowekwa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) hivyo tuzo yake itatolewa na Rais wa shirika hilo kwa kumkabidhi Rais Dk.John Pombe Magufuli na mawasilino yanafanyika yanafanyika ujio wa Rais wa ICAO.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kutua kwa ndege kubwa ya ya Emirate abiria duniani ya A380 ya Ghorofa iliyotua katika uwanja wa Ndege wa Mwalumu Julius Nyerere , jijini Dar es Salaam

DKT. KOLIMBA AKUTANA NA MSHINDI WA MISS UNIVERSITY AFRICA 2017

$
0
0
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (kulia) akifafanua jambo kwa Miss World University Africa 2017, Queen Elizabeth Makune wakati alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dodoma. Miss Makune ameshinda taji la Miss World University Afrika lililoshirikisha mataifa 53 ya Afrika nchini Korea Desemba 2017.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba (kulia) na Miss World University Africa 2017 Bi. Queen Elizabeth Makune wakifurahia jambo alipomtembelewa ofisini kwake na Bi. Makune leo Jijini Dodoma. Miss Makune ameshinda taji la Miss World University Afrika lililoshirikisha mataifa 53 ya Afrika nchini Korea Desemba 2017.
 Miss World University Africa 2017 , Queen Elizabeth Makune (kushoto) akimueleza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba (kulia) jinsi mashindano yalivyo fanyika alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dodoma. Miss. Makune ameshinda taji la Miss World University Afrika lililoshirikisha mataifa 53 ya Afrika nchini Korea Desemba 2017.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA DODOMA-BABATI ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina, Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami, Kondoa mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli , Spika wa Bunge Job Ndugai, Wabunge pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono na kuwanyanyua juu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  mara baada ya wote kwa pamoja kukata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Chemba Juma Nkamia mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliojipanga kando kando ya barabara ya Dodoma-Babati mara baada ya kuifungua barabara hiyo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251
  Kikundi cha kwaya cha JKT Makutupora kikitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 zilizofanyika Kondoa mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili Kondoa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambaye alihudhuria  katika sherehe hizo za ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma-PICHA NA IKULU

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MOROGORO WASHIKA KASI

$
0
0
Afisa Msajili Mkoa wa Morogoro Ndg. Sererya Wambura (kulia\0 akiwa pamoja na Afisa Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta wa NIDA Ndg. Rajabu Kabeya wakipitia ripoti za Usajili na Utambuzi wa watu za mkoa wa Morogoro.
Ndg. Thabit Salum Likanyaga Mwenyekiti Serikali ya Mtaa wa Kilongo, Kata ya Mkundi akigawa fomu kwa wananchi wa mtaa wake kwa ajili ya zoezi la uchukuaji alama za kibaiolojia linaloendelea kwenye mtaa huo.
Wananchi Kata ya Kihonda Kaskazini, Mtaa wa Yespa wakiwa kwenye harakati za kujaza fomu na wengine wakiwa katika hatia ya kupigwa picha, kuweka saini ya kielektroniki na kuchukuliwa alama za vidole.
Maafisa Wasajili Wasaidizi Ndg. Alice Makarara aliyeketi na Ndg, Aziza Makoa wakitoa huduma kwa wateja waliofika ofisi ya wilaya ya NIDA ya Usajili Morogoro kuchukua vitambulisho vyao. Aliyeketi meza ya pembeni yao ni Ndg. Lucy Alphonce. Afisa Msajili Msaidizi wa NIDA akichakata taarifa za waombaji Vitambulisho vya Taifa Morogoro. 

POLISI YAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KUKUTWA NA SILAHA

$
0
0
JOSEPH MPANGALA -  MTWARA
Polisi Mkoa wa Mtwara Linawashikilia watu wawili Kwa kukutwa na Silaya aina ya Gobore na Shortgun pamoja na maganda ya Risasi 66 Bila ya Kibali cha Umiliki ambazo zilikuwa zikitumia katika matukio mbalimbali ya uwindaji Haram wa wanyama.
Mmoja wa watuhumiwa ni Yohana Maiko Mkazi wa kijiji cha  Lukula mwenye umri wa mika 33 ambaye amekutwa na Bunduki aina ya Shortgun na Mtuhumiwa wa  pili Severine Mtei kitere  mwenye umri wa miaka28 ambaye amekutwa na silaha aina ya Gobore na katika uchunguzi wa polisi Mtuhumiwa huyo amebainika kuwa ni Fundi wa kutengeza silaha hizo na Kuwauzia Watu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amesema watuhumiwa woote wanaendelea na kuhojiwa na jeshi la Polisi ili kuweza kujirisha kuwa mtuhumiwa wa pili severine Mtei amepata wapi maganda 66 anayotumia kwa kutengenezea   Risasi.
“Tunaedelea kumhoji kwanza tujue maganda ya hizi risasi aliyapata wapi na naNi alimuuzia na yameua wanyama wangapi mpaka sasa”

Wakati huo huo watu 12 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kutwa na madawa ya kuvya aina ya bangi kilo20 na gram182 ambap mkondya ameomba ushirikiano kutoka kwa wenyeviti wa mtaa pamoja na Watendaji

NEWZ ALERT:MTOTO WA MIEZI TISA AFA AJALINI BAADA YA BASI LA POLISI, NOAH KUGONGANA USO KWA USO MOROGORO

$
0
0

*Dereva wa Noah naye afariki, askari JWTZ, Polisi wajeruhiwa

Na Ripota Wetu,Morogoro 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitha kufariki dunia kwa watu wawili akiwamo mtoto wa miezi tisa Amina Hassan baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha gari ndogo aina ya noah pamoja na basi la Jeshi la Polisi.

Akizungumza kwa njia ya simu na Michuzi Blog jioni hii kuhusu ajali hiyo Kamanda Matei amesema imetokea saa saba mchana eneo la Mikese Maseyu mkoani humo, ambapo Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini kugongana uso kwa uso na basi hilo ambalo lilikuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam.

Amefafanua mbali ya kufa kwa mtoto huyo dereva wa Noah hiyo iliyopata ajali ambaye amemtaja kwa jina la Zimbao Cornel huku akielezea kujeruhiwa kwa askari Polisi wanne na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) nao wanne na wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

Alipoulizwa kuhusu idadi ya watu waliokuwa kwenye Noah amesema bado haijathibitika walikuwa wangapi lakini wanaendelea kufuatilia na kisha watatoa taarifa kamili.

Kuhusu hali za majeruhi Kamanda Matei amesema wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea kuimarika, hivyo kikubwa ni kuwaombea ili wapone haraka na kurejea kwenye ujenzi wa nchi.

Kabla ya kuthibitishwa na kamanda kuhusu ajali hiyo, Ripota Wetu ameshuhudia gari hiyo ya Noah ikiwa imeharibika vibaya na baada ya ajali kutokea waliopoteza maisha na majeruhi walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Kwa upande wa Muuguzi wa zamu kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoani Edwine Damas amekiri kupokea mwili wa mtoto huyo na majeruhi na wanaendelea kuwapatia matibabu.
 Pichani ni  gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini ikiwa imegongana uso kwa uso na basi la jeshi la polisi lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam eneo la Mikese Maseyu mkoani Morogoro.
Pichani ni  Baadhi ya Askari wa JWTZ na Jeshi la Polisi wakishiriki kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali ya gari aina ya Noah iliyokuwa ikitokea Kizuka Ngerengere kuelekea Morogoro Mjini ikiwa imegongana uso kwa uso na basi la jeshi la polisi lililokuwa likitokea mkoani Dodoma kuelekea Dar es Salaam eneo la Mikese Maseyu mkoani Morogoro.
 Baadhi ya Askari wa JWTZ wakitoa msaada kwa majeruhi mara baada ya ajali hiyo kutokea

AZAM vs MTIBWA, SASA KUPIGWA SAA 10 JIONI.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


MCHEZO kati ya Klabu ya Azam FC na Mtibwa Sugar uliotarajiwa kuchezwa saa 8 mchana umefanyiwa mabadiliko ya muda, ambapo sasa utafanyika Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro, kesho Jumamosi saa 10.00 jioni.

Awali mchezo huo ulikuwa ufanyike saa 8.00 mchana, lakini Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeamua kuusogeza hadi jioni kutokana na ratiba ya wadhamini wa matangazo ya televisheni Azam TV kutobana muda huo.

Tayari kikosi cha Azam FC kimewasili mkoani Morogoro tokea jana saa 12 jioni kikiwa tayari kuvaana na Wakatamiwa hao, ambapo jioni ya leo kitafanya mazoezi ya mwisho kujiweka sawa na mchezo huo.

Timu hizo zimekuwa na upinzani mkali mara zote zinapokutana, katika rekodi zimecheza mechi 19 za ligi, Azam FC ikiwa imeshinda mara tisa, Mtibwa Sugar mara mbili huku mechi nane zikiisha kwa sare, ambapo hivi sasa inasubiriwa kuona namna matokeo yatakavyokuwa katika mechi yao ya 20 ya ligi.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana kwenye ligi ilikuwa ni Novemba 27 mwaka jana, zikitoka sare ya bao 1-1, Azam FC ikitangulia kufunga kupitia kwa winga Enock Atta kabla ya Kelvin Sabato kuisawazishia Mtibwa Sugar kwa mkwaju wa moja kwa moja wa adhabu ndogo.

Azam FC itamkosa Kocha Mkuu wake, Aristica Cioaba, ambaye amesimamishwa na Kamati ya Saa 72, kufuatia kuondolewa kwenye benchi na mwamuzi Jonesia Rukyaa, katika mchezo uliopita dhidi ya Njombe Mji ulioisha kwa suluhu.

Nahodha Msaidizi, Agrey Moris, atarejea tena kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kutocheza mchezo mmoja kufuatia kadi nyekundu iliyotokana na kadi mbili za njano aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ulioisha kwa Azam FC kupoteza kwa mabao 2-0.

Kikosi cha Azam FC kimejipanga kufanya vizuri katika mchezo huo na kuondoa rekodi mbaya ya kutoshinda katika mechi tatu zilizopita, ikipata suluhu mbili dhidi ya Mbeya City na Njombe Mji na kufungwa mmoja.

Hadi sasa kwenye msimamo wa ligi inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46 huku wapinzani wao Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya sita kwa pointi 33

Uvutaji Wa Sigara Na Unywaji Wa Pombe Uliokithiri Husababisha Magonjwa Ya Mishipa Ya Damu Ya Moyo

$
0
0
Brighton James – JKCI.

Watanzania wameshauriwa kufanya mazoezi, kula vyakula bora, kuepuka uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe uliokithiri kwa kufanya hivyo watajiepusha na magonjwa ya mishipa ya damu ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yanaouwa watu wengi Duniani.

Ushauri huo umetolewa leo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani Mazen Albaghded wakati akiongea na waandishi wa habari katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Dkt. Albaghded alisema kuwa ulaji wa vyakula vyenye mafuta na bila kufanya mazoezi ambayo yangesaidia kuyeyusha mafuta hayo kunaweza kusababisha kupata kirahisi ugonjwa wa mishipa ya damu ya moyo. Wagonjwa wa kisukari na wenye shinikizo la juu la damu nao wanaweza kupata ugonjwa huo kirahisi.

“Mishipa ya damu inapozungukwa na mafuta baadaye huweza kuziba na hivyo damu kushindwa kwenda katika misuli ya moyo (myocardium) na kusababisha mtu kupata shambulio la moyo”, alisema.Akizungumzia kuhusu kambi hiyo ya matibabu ya siku nne Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Tulizo Shemu alisema wagonjwa wanaotibiwa ni wale wanaohitaji matibabu ya kibingwa yenye uhitaji wa uchunguzi yakinifu.

Dkt. Shemu alisema kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa njia ya kutoboa tundu dogo kwa mgonjwa wanaangalia kama mishipa ya moyo imeziba na ikiwa imeziba wanaizibua kwa kumuwekea mgonjwa kifaa maalum kinachojulikana kwa jina la “stent” ambacho kinasaidia mshipa wa damu usizibe tena.

Katika kambi hiyo ambayo ilienda sambamba na mafunzo ya kubadilishana ujuzi wa kazi jumla ya wagonjwa 23 wamefanyiwa vipimo na matibabu ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimzibua mgonjwa mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 23 wamezibuliwa mishipa ya damu pamoja na kufanyiwa uchunguzi.
Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani wakimzibua mgonjwa mishipa ya damu ya moyo ambayo imeziba kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa kutumia tundu dogo inayofanyika katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 23 wamezibuliwa mishipa ya damu pamoja na kufanyiwa uchunguzi.Picha na Brighton James – JKCI

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote.

Pia amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 27, 2018) wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma.

“Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo.”

Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zinazochochea  maendeleo.

Akijibu ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali  itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Ofisini kwake jijini Dodoma, Aprili 27, 2018. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Maimuna Tarishi na kushoto kwake ni  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John  Shibuda
PMO_0845
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Shibuda, katika kakao kati yake na kamati hiyo, ofisini kwake jijini Dodoma, Aprili 27, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WALIOFANYA UBADHIRIFU WA BILION 1.5 WASAKWE NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA- RAISI MAGUFULI

$
0
0

Na Mahmoud Ahmad Dodoma

RAIS John Mguguli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinawachukulia hatua kali watu wote waliohusika katika kufanya ubadhilifu wa zaidi y ash bilioni 1.5 ya mradi wa maji wa Ntomoko.

Agizo hilo alilitoa jana wakati wa ufunguza wa barabara ya Dodoma Manyara yenye urefu wa kilometa 251 iliyozinduliwa katika eneo la Bicha wilayani kondoa mkoani hapa ambayo itaongeza fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi wa mikoa hiyo miwili.

Akiwahutubia wananchi wa Kondoa na Manyara,muda mfupi baada ya kupatiwa taarifa ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Bilinithi Mahenge, kuelezea kuwa kuna ubadhirifu wa zaidi ya sh.bilioni moja na nusu zilizopotea katika mradi wa maji wa ntomoko na kuwakosesha huduma ya maji wananchi wa wilaya ya Kondoa na Chemba.

Mradi huo wa kutandika mabomba ya kusambazia maji kuwafikia wananchi ambapo waliopewa dhamana hiyo badala ya kutandika mabomba ambayo yanauwezo mkubwa wa kufikisha maji wao wakaweka mabomba madogo ambayo hayana uwezo .“Kama ni kuchomoka basi wachomoke wale wote waliofanya ubadhirifu wa mradi huu kwani wanawapa shida wananchi wanyonge ambao walikuwa wapate huduma ya maji tokea mwaka 1980” alisisitiza Rais

Aidha kwa upande mwingine Rais Magufuli akawataka viongozi wa wilaya hiyo kuacha migogoro ya wao kwa wao na kuwa migogoro inachangia kushindwa kuwapelekea wananchi huduma za maendeleo kwa wakati na yeye hakuwatuma kwenda kuibua migogoro hiyo. Kwa upande wake Rais wa Benki ya maendeleo ya Afrika Akinwim Adesina aiahidi neema kwa Jiji jipya la Dodoma na serikali kwa Ujumla kwamba atatoa ushirikiano kuahakikisha serikali na jiji hilo wanapata fedha za miradi.

Amesema kuwa Bara bara hiyo itafungua milango ya kiuchumi kwa lango la Kaskazini mwa Afrika na kusini ambapo hiyo itakuwa fursa pana kwa wananchi wa mataifa nane barani humo ambayo barabara hiyo inapita kutoka Cape town hadi Cairo nchini Misri

Nae waziri wa Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa amesema kuwa barabara hiyo yenye urefu wa km.251 imejengwa kwa jumla ya tsh.bilon 378.4 kati ya hizo fedha za ndani blion107.6 na zilizobakia zimechangiwa na wafadhili Benki ya maendeleo ya Afrika(AFDB) na shirika la maendeleo la Japani(JICA).

KAIMU BALOZI WA ZIMBABWE NCHINI, TAVENYIKA AZUNGUMZA NA WABUNGE WA BUNGE LA TANZANIA WANAOWAKILISHA BUNGE AFRIKA LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Matin Tavenyika (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma. Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma. 


Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, walioongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge hao, Mhe. Asha Juma (katikati) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulie na kulia ni Mbunge wa Momba, Mhe. David Silinde


Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akiagana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma. 
Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, walioongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge hao, Mhe. Asha Juma (wa pili kulia) walipokutana leo katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE

Habari za Umoja wa Mataifa leo Aprili 27, 2018

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images