Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

TCCIA YAZINDUA HUDUMA YA TYM

$
0
0
Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu (katikati) akizundua huduma mpya ya TMY leo, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda ​akifwatiwa na Patrick Emmunel Meneja Maendeleo ya Viwanda TCCIA, wa Mwisho kulia ni Helen Mangare Afisa Uhusiano Eag akifatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula. 

CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kimezindua huduma ya ‘TCCIA Youth Membership’ (TYM) ambayo ni uanachama wa vijana kwenye chama hicho.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa Rais wa TCCIA, Octo Mshiu alisema mpango huo umekuja kufuatia chama hicho kutambua umuhimu wa Vijana na Wanawake ambapo kupitia mkutano wake mkuu wa mwaka ilipitisha mabadiliko ya katiba yake ambapo iliweza kuingiza uwakilishi wa wanawake na vijana kwenye TCCIA.Mshiu alisema Kutokana na kutambua umuhimu huo TCCIA kwa kushirikiana na washauri wake wa Biashara na Masoko tumeweza kuanzisha huduma hii muhimu ya Wanachama Vijana.
Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu (katikati) akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa TYM, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula.

“ Wote tunatambua kwamba ajira ni changamoto kubwa Duniani na Tanzania pia, hivyo kuwajenga na kuwaandaa vijana kujiajiri na kuboresha uelewa wao wa biashara ni jambo la muhimu sana, “alisema Mshiu.Aliongeza kuwa ili kujenga Taifa lenye tija, mafanikio na uwezo wa kutumia fursa zilizopo ndani ya Tanzania, kanda ya Afrika Mashariki, Afrika na Dunia ni kuwa na vijana waliondaliwa vyema kwenye ujasiriamali huku ujuzi likiwa ni jambo la msingi.

Tunaamini kwa dhati kabisa kuwapa fursa Vijana ya kuwa wanachama wa TCCIA sio tu itawaongezea upeo wa kujua biashara bali pia kuwapa fursa ya kujifunza kutoka kwa wanachama waandaminizi wanaomiliki biashara na viwanda, ’’alisema..

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Gotfrid Muganda alisema TCCIA imedhamiria kuwa muhimili wa kusaidia akinamama na Vijana kufikia malengo yao ya kuwa wafanyabiashara wabobezi, kwani moja ya malengo ya kuanzishwa kwa TCCIA ni kukuza biashara.Kwa upande wa Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa Masoko na Biashara wa TCCIA, Imani Kajula alisema lengo moja wapo kuu la TCCIA ni kujenga vizazi nyenye uwezo wa kufanya biashara, hivyo TYM ni huduma maalum ya kuvutia na kuongeza uwezo wa vijana sio tu kuwa wajasiriamali wazuri bali pia kuona Zaidi fursa na kuzitumia..Kajula alisema TYM itaendelea kufungua matawi kwenye vyuo, mikoa na maeneo mbalimbali Nchini ambapo wiki hii inatarajia kuzinduliwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na baada ya hapo vyuo vingine vitafuata.
Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula. akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo mbele ya waandishi wa Habari kulia kwake ni Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu

Alisema TYM itawapa fursa vijana kujifunza kutoka kwa wanachama wazoefu, kubadilishana mawazo, kupata fursa ya mafunzo na pia mijadala ya biashara, kilimo na viwanda.

Maamuzi ya Kamati ya Saa 72 kwa matukio mbalimbali ya mechi za Ligi Kuu

$
0
0
Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita ilipitia taarifa na matukio mbalimbali na kufanya uamuzi ufuatao;

Mechi namba 171 (Njombe Mji 0 vs Simba 2). Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikina katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 3, 2018 kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, ikiwemo pia mshabiki mmoja wa timu hiyo kuingia uwanjani na kuchukua taulo la kipa wa Njombe Mji lililokuwa golini. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 165 (Mtibwa Sugar 0 vs Simba 1). Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho ya mechi hiyo iliyofanyika Aprili 9, 2018 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kitendo hicho cha washabiki wa Simba iliyokuwa ikicheza ugenini ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, wakati adhabu dhidi yao imezingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 177 (Singida United 0 vs Mtibwa Sugar 3). Mchezaji Tafadzwa Kutinyu wa Singida United amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kufanya vitendo vyenye kuonyesha imani za ushirikina katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 6, 2018 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Katika mchezo huo, Kutinyu alichukua taulo la kipa wa Mtibwa Sugar na kulirusha jukwaani kwa washabiki wa Singida United ambao waliondoka nalo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 37(7) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.

Mechi namba 184 (Mbao 0 vs Lipuli 0). Klabu ya Mbao imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mshabiki wake kuingia uwanjani na kuchukua glovu za akiba za kipa wa Lipuli zilizowekwa golini na kukimbia nazo, kitendo kinachoonyesha imani za kishirikina.

Adhabu dhidi ya Mbao katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 6, 2018 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.

Mechi namba 185 (Yanga 1 vs Singida United 1). Klabu ya Singida United imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 11, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kitendo hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi ya klabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Vilevile Bodi ya Ligi imepeleka malalamiko kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) dhidi ya Meneja wa Singida United, Ibrahim Mohamed kwa kuongoza vurugu za timu yake kulazimisha kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.

Mechi namba 191 (Simba 3 vs Mbeya City 1). Klabu ya Simba imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika sita katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 12, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kitendo cha Simba ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo wakati adhabu dhidi yao imekijita katika Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mechi namba 194 (Azam 0 vs Njombe Mji 1). Kocha wa Azam, Aristica Cioba amesimamishwa hadi suala lake la kumtukuna Mwamuzi baada ya mechi kumalizika litakaposikilishwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Uamuzi wa kumsimamisha umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.

Kabla ya kumtukana Mwamuzi, Kocha huyo aliondolewa kwenye benchi (ordered off) kwa kupinga maamuzi kwa maneno na vitendo katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 15, 2018 katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mechi namba 200 (Simba 2 vs Tanzania Prisons). Klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuwakilishwa na maofisa watatu badala ya wane kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 16, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kitendo chao ni ukiukaji wa Kanuni ya 14(2a) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA 

SALAMU ZA HERI YA MIAKA 54 YA MUUNGANO, KUTOKA OFISI YA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI NCHINI

KONCEPT Yawajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana Kibiti

$
0
0
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele akitoa nasaha kwa wanafunzi wa shule ya wavulana Kibiti Boys .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii. 
Wanafunzi wa kidato cha sita wapatao 451 wa shule ya wavulana Kibiti Boys iliyopo wilaya ya kibiti Mkoani wakisikiliza kwa makini nasaha zilizokuwa zikitolewa na Mkurungezi wa KONCEPT Krantz Mwantepele alipotembelea shule hii mapema wiki katika kuwajengea uwezo katika maandalizi yao ya mitihani ya mwisho na pia kuwapa dondoo za mafanikio katika maisha kwa ujumla. 
Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kwa Mkurungezi wa KONCEPT Krantz Mwantepele Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii. 
Wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana Kibiti wakionesha kuwa wamehamasika na nasaha zilizotolewa na Mkurungezi mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele .Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii. 
Mkuu wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys Dismas Njawa akifafanua jambo kabla ya kufunga kongamano hilo lililoendeshwa na Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT Krantz Mwantepele . Kongamano lililokutanisha wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya wavulana ya Kibiti Boys wapatao 451 ambapo walipata nafasi ya kujengewa uwezo wa kujiamini na nasaha za maisha ya mafanikio kwa ujumla.Kongamano hilo lilifanyika shuleni hapo wilayani Kibiti mkoani Pwani mapema wiki hii.

MSAMAHA WA RAIS KWA WAFUNGWA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 26 APRILI, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWAONGOZA MAELFU YA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 54 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZILIZOFANYIKA MKOANI DODOMA

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati akipigiwa wimbo wa Taifa kabla ya kwenda kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya Majeshi ya Tanzania katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshma katika maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika jukwa kuu kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Wananchi, Magereza na Polisi vikipita kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Kikosi cha Makomando wa (JWTZ) kikipita na kutoa heshma mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Mmoja wa Makomando wa JWTZ akitoa Heshma kwa kupiga Saluti wakati akipita mbele ya Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (haonekani pichani )katika ya maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

TCCIA YAZINDUA HUDUMA YA TYM

$
0
0

Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu (katikati) akizundua huduma mpya ya TMY leo, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda ​akifwatiwa na Patrick Emmunel Meneja Maendeleo ya Viwanda TCCIA, wa Mwisho kulia ni Helen Mangare Afisa Uhusiano Eag akifatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula.

CHAMA cha Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) kimezindua huduma ya ‘TCCIA Youth Membership’ (TYM) ambayo ni uanachama wa vijana kwenye chama hicho.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Makamu wa Rais wa TCCIA, Octo Mshiu alisema mpango huo umekuja kufuatia chama hicho kutambua umuhimu wa Vijana na Wanawake ambapo kupitia mkutano wake mkuu wa mwaka ilipitisha mabadiliko ya katiba yake ambapo iliweza kuingiza uwakilishi wa wanawake na vijana kwenye TCCIA.Mshiu alisema Kutokana na kutambua umuhimu huo TCCIA kwa kushirikiana na washauri wake wa Biashara na Masoko tumeweza kuanzisha huduma hii muhimu ya Wanachama Vijana.
Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu (katikati) akiongea na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa TYM, kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda na Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula.

“ Wote tunatambua kwamba ajira ni changamoto kubwa Duniani na Tanzania pia, hivyo kuwajenga na kuwaandaa vijana kujiajiri na kuboresha uelewa wao wa biashara ni jambo la muhimu sana, “alisema Mshiu.Aliongeza kuwa ili kujenga Taifa lenye tija, mafanikio na uwezo wa kutumia fursa zilizopo ndani ya Tanzania, kanda ya Afrika Mashariki, Afrika na Dunia ni kuwa na vijana waliondaliwa vyema kwenye ujasiriamali huku ujuzi likiwa ni jambo la msingi.

Tunaamini kwa dhati kabisa kuwapa fursa Vijana ya kuwa wanachama wa TCCIA sio tu itawaongezea upeo wa kujua biashara bali pia kuwapa fursa ya kujifunza kutoka kwa wanachama waandaminizi wanaomiliki biashara na viwanda, ’’alisema..

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA, Gotfrid Muganda alisema TCCIA imedhamiria kuwa muhimili wa kusaidia akinamama na Vijana kufikia malengo yao ya kuwa wafanyabiashara wabobezi, kwani moja ya malengo ya kuanzishwa kwa TCCIA ni kukuza biashara.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa EAG Group ambao ni washauri wa Masoko na Biashara wa TCCIA, Imani Kajula alisema lengo moja wapo kuu la TCCIA ni kujenga vizazi nyenye uwezo wa kufanya biashara, hivyo TYM ni huduma maalum ya kuvutia na kuongeza uwezo wa vijana sio tu kuwa wajasiriamali wazuri bali pia kuona Zaidi fursa na kuzitumia..Kajula alisema TYM itaendelea kufungua matawi kwenye vyuo, mikoa na maeneo mbalimbali Nchini ambapo wiki hii inatarajia kuzinduliwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na baada ya hapo vyuo vingine vitafuata.
Mkurugenzi Mtendaji wa Eag Group Imani Kajula. akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo mbele ya waandishi wa Habari kulia kwake ni Makamu wa Rais TCCIA Octavian Mshiu.Alisema TYM itawapa fursa vijana kujifunza kutoka kwa wanachama wazoefu, kubadilishana mawazo, kupata fursa ya mafunzo na pia mijadala ya biashara, kilimo na viwanda.

WALIOKUBWA NA MAFURIKO DAR WAKUMBUKWA KWA MISAADA YA CHAKULA, MALAZI

$
0
0
Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

MKOA wa Dar ea Salaam umeadhimisha miaka 54 ya Muungano kwa kutoa misaada ya chakula na malazi kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni.

Akizungunza leo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema misaada iliyotolewa ni pamoja na magodoro, chandarua, nashuka, mito, sukari, unga,mchele pamoja na mafuta ya kupika.

Makonda amesema misaada hiyo itagawanywa kwa familia zaidi ya 600 zilizoathiriwa na mafuriko lengo likiwa ni kusaidia familia hizo ambazo zimekuwa zikiishi kwa tabu baada ya mvua kuharibu vyakula na mali.

Aidha amezishukuru taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center kwa kuamua kutumia maadhimisho ya muungano kugusa maisha ya familia zilizokuwa zikiishi kwa tabu.

Pia amesema kuwa Mkoa umeandaa mkakati wa kukabiliana na mafuriko ya mara kwa mara ambapo hivi karibuni atahitisha mkutano na wananchi wote waishio mabondeni ili kuangalia namna bora kutatua suala hilo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa taasisi ya Miraj Islamic Center Abdullah Mrus na Mwenyekiti wa taasisi ya Abdullah Aid Arif Ally Abdurahman wamesema wameamua kutumia siku ya muungano kuzikumbuka na kusaidia familia ambazo zimekumbwa na mafuriko na sasa zinaishi kwa tabu.

Aidha wamempongeza Rais Dr. John Magufuli kwa kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (kushoto) akipokea msaada wa chakula na malazi kwa familia zilizoathiriwa na mafuriko kutoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya Miraj Islamic Center,Abdullah Mrus na Mwenyekiti wa taasisi ya Abdullah Aid Arif Ally Abdurahman leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza leo katika hafla ya kupokea msaada.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwashukuru viongozi wa taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center kwa kuamua kutumia maadhimisho ya muungano kugusa maisha ya familia zilizokuwa zikiishi kwa tabu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi za Abdullah Aid na Miraji Islamic Center leo.

MZEE MAJUTO KUPELEKWA NCHINI INDIA KWA MATIBABU

$
0
0
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto anatarajia kupelekwa nchini India kwa matibabu kutokana na tatizo linalomkabili. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutoka kumsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona mzee Majuto amekuwa akihangaika mara kwa mara kutafuta matibabu.

 "Tumeona mzee wetu anahangaika na matibabu ya mara kwa mara ambayo hayakamiliki sasa tumekuja na wazo la kumpeleka nchini India ili akatibiwe tatizo lake liishe na huu ndiyo wakati mwafaka wa watu tujitoe si mpaka mtu ashindwe kuongea tuanze michango," alisema nyerere. "Jamani ifike wakati tujitoe kumsaidia mtu akiwa yupo hai na tusisubiri afariki ndiyo tuanze kuchanga, wakati ni sasa akiwa anaumwa tunamchangia anapatiwa matibabu na anaendelea na maisha," amesema Nyerere.

 Tunamshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuunga mkono kusaidia mwenzetu, pia Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taiga (NEC) Salim Asas ambaye yeye amesema atatusaidia kwa hali na mali na ameanza kutupa tiketi 2 za ndege. Tunataka mwenzetu akatibiwe maradhi yake yaishe aendelee na majukumu yake ya kujenga nchi na familia yake kwa ujumla. 

Nyerere amewaomba wadau mbali mbali akiwemo Azam, DSTV na wengine wote wenye mapenzi mema kumsaidia mzee Majuto ili apone na aendelee na shughuli. Kwa Upande wa Mzee Majuto amewashukuru watu wote ambao wamekuwa wakijitokeza kumsalimia na waendelee kumuombea ili apone. "Sina cha kuwapa zaidi ni kuwaombea muendelee na moyo mlionao, mimi sina pingamizi kwenda kutibiwa nchini India, nipo tayari kamilisheni mipango yote mje kunichukua," amesema. Ujumbe wa Steve Nyerere uliambatana na msanii mwenzake Aunty Ezekiel pia wakiwemo na waandishi wa habari wa mitandao ya jamii.
Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akimsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' akiongea machache mara baada ya kumtembelea Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam. Mzee Majuto akitoa shukrani zake mara baada ya kutembelewa na kuonyeshwa mwanga wa matibabu zaidi nchini India.
Msanii Aunty Ezekiel akimsalimia Mzee Majuto.

AIRTEL NA VETA WAUNGANA KUTOA MAFUNZO KUPITIA SIMU YA MKONONI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

KATIKA kuadhimisha Siku ya kimataifa ya mtoto wa kike kampuni ya simu ya Airtel Tanzania sambamba na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi(VETA), wamekuja na mbinu mpya ya kutoa mafunzo kupitia simu ya mkononi.

Akizungumza na Michuzi blog Meneja mradi wa Airtel Jane Matinde ameeleza leo jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na VETA wameamua kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kupitia apllication ya Vsomo inayopatika playstore bure kabisa ambayo baada ya kusoma ukifaulu kwa asilimia 40 atachaguliwa katika VETA iliyokaribu kuweza kuendelea na masomo.

Aidha ameeleza zaidi ya kozi 11 zinapatikana, hivyo vijana wanatakiwa kupakuwa application hiyo ili kujifunza kozi mbalimbali kama vile umeme wa majumbani na malipo ya kozi hizi ni shilingi laki moja na ishirini pekee.Kwa upande wa Meneja mradi wa Vsomo kutoka VETA Charles Mapuli ameeleza hadi sasa waliopakua application hiyo wapo zaidi ya 3500, waliosajiliwa 10,800 na waliosoma na kufanya mitihani wapo 120.

Pia masomo hayo ni ya muda mfupi kwa miaka miwili hadi mitatu na itawasaidia vijana wengi kufikia malengo yao na kufikia azma ya serikali ya kujenga Tanzania ya viwanda.

Meneja mradi wa Airtel Jane Matinde akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es salaam kuhusiana na fursa ya Vsomo ambaye inatoa fursa ya kusoma masomo ya ufundi kupitia simu ya mkononi.
Katibu mkuu Wizara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu akisikiliza maelezk kutoka kwa Meneja mradi wa Airtel Jane Matinde kuhusiana na kusoma kupitia simu ya mkononi maarufu kama VSOMO.
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza meneja wa Vsomo,Charles Mapuli kutoka VETA katika maonesho ya siku ya kitaifa ya mtoto wa kike na Tehama leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii.

AfDB YARIIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA NISHATI YA UMEME INAYOFADHILIWA NA BENKI HIYO NCHINI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,  Dkt. Akinumwi  Adesina, amesema Benki hiyo imeridhishwa na utekelzaji wa miradi ya nishati hapa nchini kwani inachochea mageuzi katika maisha ya wananchi .
 Akizungumza mara baada ya kuwasili Mkoani Dodoma na kutembelea  kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mkoani Dodoma, amesema kuwa  benki hiyo inatambua na kupongeza juhudi za  Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.
Dkt. Adesina ameeleza kuwa ujenzi wa kituo hicho cha kupoza umeme ni mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano ya kuondoa changamoto ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa wananchi wake na umelenga pia kupunguza tatizo la upatikanaji wa umeme katika nchi jirani zinazopakana na Tanzania ikiwemo Burundi na Kenya.
Alisema kuwa katika kuhakikisha mpango huo wa kupeleka umeme huo na kuunganisha na nchi jirani, Benki yake imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 75 kufanikisha mradi huo wenye thamani ya zaidi ya dola milioni 220.
"Umeme ni jambo muhimu sana katika maendeleo ni sawa na damu katika mwili wa binadamu, ukiwa na damu mwilini unakuwa na hai kama huna unakufa! kwa hiyo uchumi bila umeme wa uhakika hauwezi kushamiri" alisisitiza Dkt. Adesina
Aliahidi kuwa Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza maendeleo ambapo hivi sasa Benki yake iko katika mazungumzo na Serikali ili mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 165 uweze kupatikana kwa ajili ya kujenga mradi wa nishati ya umeme katika ukanda wa Kaskazini Magharibi mwa nchi.
"Vile vile tutawasilisha kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Benki yetu ili kiasi cha dola za Marekani milioni 45 kinachoombwa na Serikali kwa ajili ya kujenga mradi wa umeme unaotokana na joto ardhi uweze kupatikana ili kuboresha na kuwa na umeme wa uhakika nchini kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya viwanda nchini" alisema Dkt. Adesina
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha zuzu mkoani humo .
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdori Mpango ( Mb) akimuongoza Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma ambapo alitembelea na kukagua mradi wa kituo cha kupoza umeme cha zuzu mkoani humo.
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina akisisisitiza jinsi Benki hiyo inavyoridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa nishati hali itakayochochea maendeleo.
Mhandisi Mkuu wa Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, Mkoani Dodoma Bw. Joseph Mongi akitoa maelezo kuhusu namna kituo hicho kinavyofanya kazi wakati wa ziara ya Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina katika kituo hicho.
Sehemu ya Miundombinu ya kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma kama inavyoonekana.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu, wakimuongoza Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kukagua miundombinu ya Kituo cha kupoza umeme cha Zuzu, mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango).


AfDB PRESIDENT DR.AKINWUMI ADESINA COMMENDS PRESIDENT MAGUFULI PERFORMANCE

DKT. MWAKYEMBE:TASNIA YA MAVAZI NA MITINDO INACHANGIA KATIKA KUKUZA UTALII NCHINI 2

MICHUZI TV: Rais wa Benki ya maendeleo Afrika aelezea mpango wake wa kuibadili Dodoma

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA AfDB MJINI DODOMA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kuwasili mjini Dodoma kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina ambaye aliambatana na ujumbe wake mkoani Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika mjini Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiapongezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi  Adesina ambaye alihudhuria maadhimisho ya Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU

SHEREHE YA MCHAPALO YA KUSHEREHEKEA MIAKA 54 YA MUUNGANO YAFANA WASHINGTON, DC

$
0
0
Balozi Mhe. Wilson Masilingi akisoma hotuba yake.aliyelezea mambo mbalimbali ikiwemo kuitangaza Tanzania katika maswala ya utalii ikiwemo uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Marekani. Katika hotuba hiyo Mhe. Balozi Wilson Masilingi aliongelea jinsi ya nchi ya Tanzania ilivyokua na amani na salama kwa watalii kwenda Tanzania kwenda kujionea vivutio mbalimbali na katika kuimarisha utalii, Serikali ya awamu ya tano chini ya Rasi Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amenunu ndege sita za usafiri zikiwemo tatu ambazo zimeshaanza kufanya kazi na zinginge tatu zitawasili ifikapo mwezi wa June mwaka huu ikiwemo ndege kubwaya Dreamline. Katika sherehe hiyo video ya vivutio mbalimbali zikiwemo mbuga zetu za hifadhi ya taifa zilikua zikionyeshwa.
 Bwn Eric Stromayer mwakilishi kutoka Deperttment of State (Duputy AssistantSecretary Bereau of Africa Affairs ) akisoma hotuba yake na kuelezea uhusiano wa Marekani na Tanzania tangia zaiara ya baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere alivyotembelea Marekani mwaka 1963 enzi hizo ikiongozwa na Rais John Kennedy.
Mshereheshaji Julia Nyerere akisisitiza jamabo na utaratibu wa kitu gani kinafuata
Mapokezi wakihakikisha kila mgeni anapokelewa vizuri na kwa ukarimu kwenye mchapalo wa kusherehekea sikukuu ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika siku ya Alhamisi April 26, 2018, Washington, DC katika hotel ya Fairmont Washington na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchi Marekani. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production chini ya udhamini wa Kilimanjaro Studio.
Kulia ni Balozi wa Tanzania nchiniMarekani Mhe. Wilson Masilingi akifuatiwa na mkewe Marystela Masilingi wakiwa pamoja nae Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Mutta na mkewe wakijiandaa kupokea wageni waalikwa kwenye mchapalo wa kusherehekea sikukuu ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika siku ya Alhamisi April 26, 2018, Washington, DC katika hotel ya Fairmont Washington na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchi Marekani.
Wageni wakiwasili huku wakisalimiana na Mhe. Balozi Wilson Masilingi, mkewe Marystela Masilingi,Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Muta na mkewe.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi, Mkewe Marystela Masilingi, Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Brigedia Jenerali Adolph Mutta na mkewe wakipiga picha ya kumbukumbu na wageni waalikwa waliokuwa wakiingia ukumbini..
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi na mkewe Marystela Masilingi wakiwa na mgeni wao. Bwn Eric Stromayer mwakilishi kutoka Deperttment of State (Duputy AssistantSecretary Bereau of Africa Affairs ambaye ndiye aliyekua mgeni rasmi wakiwa wamesimama kwa nyimbo za Taifa Tanzania na Marekani.

Puma Energy Tanzania yajivunia ufanisi wa huduma ya mafuta iliyotoa kwa ndege kubwa ya Emirates

$
0
0
AMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania imejivunia ufanisi wa huduma ya mafuta iliyotoa kwa ndege kubwa aina ya Airbus 380 inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Emirates iliyotua kwa dharura Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Meneja Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza alisema hatua hiyo ni sehemu ya uthibitisho kuwa Tanzania kupitia kampuni ya Puma Energy ina uwezo wa kutosha kutoa huduma ya nishati hiyo hata kwa ndege kubwa zaidi duniani.

“Uwezo wa kutoa huduma ya nishati ya mafuta kwa ndege kubwa kama hizi tena kwa ufanisi ni moja ya kivutio muhimu kwa mashirika mengine makubwa kuweza kuleta ndege zao hapa nchini hasa kipindi hiki ambapo Serikali imejipanga kuleta mageuzi katika sekta ya anga hivyo Puma Energy Tanzania tunajivunia kuwa sehemu ya kuwezesha mageuzi hayo,’’ alisema.

Akizungumzia zoezi hilo lililofanyika mapema siku ya Jumatano kabla ndege hiyo haijaondoka hapa nchini kuelekea Mauritius, Meneja wa Kituo cha Mafuta cha kampuni hiyo kilichopo JNIA, Mohammed Ngayahika alisema lilifanyika kwa kasi na ufanisi mkubwa likihusisha jumla ya lita 98,709 za nishati hiyo.

“Kwa hapa nchini Puma Energy ndio yenye uwezo pekee wa kujaza mafuta kwenye ndege kubwa kutokana na uwekezaji mkubwa iliyoufanya kwenye vifaa vya kisasa vyenye uwezo wa ‘kupump’ mafuta kwa kasi kubwa kama tulivyofanya kwenye zoezi hili ambapo tulisukuma mafuta kwa kasi ya lita 2,800 kwa kila dakika moja na hivyo kufanya zoezi hili kuwa rahisi sana tena kwa ufanisi mkubwa na kwa kuzingatia taratibu zote za kiusalama,’’ alisema.

Naye, Emmanuel Ngowi kutoka kampuni hiyo ambae ndiye aliyeendesha zoezi hilo alisema baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Shirika la Ndege la Emirates lilionyesha kuridhishwa kwake na ubora wa huduma hiyo hatua ambayo muhimu katika muendelezo wa biashara. “Kwa muda mrefu Puma Energy tumejenga sifa nzuri katika utoaji wa huduma zetu kutokana na ufanisi wetu, rekodi nzuri katika masuala ya usalama pamoja na bei yenye ushindani,’’. aliongeza

Ndege hiyo iliyopaswa kutua nchini Mauritius , ilitua kwa dharura uwanjani hapo majira ya saa 7:15 mchana ikiwa na abiria 475 kufuatia hali mbaya ya hewa kwenye uwanja ilipotakiwa kutua nchini humo.
 Mtoa huduma ya Mafuta ya ndege wa kampuni ya Puma Energy katika Kituo cha Mafuta cha kampuni hiyo kilichopoUwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam BwEmmanuel Ngowi akisimamia ujazaji wa mafuta kwenye ndege kubwa aina ya Airbus 380 inayomilikiwa na Shirika la Ndege la Emirates iliyotua kwa dharura kwenye uwanja huo hivi karibuni.
 Zoezi la ujazaji mafuta likendelea…!

 Kisha taratibu zote za manunuzi zilifuatwa!

DC WA BUHIGWE AWAPONGEZA VIJANA KIGOMA KWA KUUENZI MUUNGANO

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma ,

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti amewapongeza Vijana wa Kigoma kwa kitendo walichokifanya cha kuuenzi Muungano wa Tanzania, kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Bodaboda bila kujali itikadi za Vyama vyao.

Pongezi hizo alizitoa jana Mara baada ya Mchezo huo uliofanyika katika Viwanja vya Kawawa Manispaa ya Kigoma ujiji, wakati akitoa zawadi kwa washindi, ambapo vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM waliibuka washindi kwa penati tano kwa nne dhidi ya timu ya Vijana wa Bodaboda na kuwapatia kila timu mbuzi mmoja na mchele kilo 20 kwa ajili ya kudumisha na kuuenzi Muungano.

Brigedia Gaguti alisema Vijana hao wameonesha Mfano mzuri wa kuigwa na wameienzi falsafa ya Muungano kwa kitendo walichokifanya na kuwataka Vijana hao kuendelea kudumisha umoja na mshikamano hata katika maendeleo ili kuhakikisha Mkoa wa Kigoma unasonga mbele,kufanya kazi kwa bidii pamoja na Kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Nitoe pongezi kwa Vijana wa kigoma kwa Viongozi wa UVCCM na Boda boda kwa hili mlilolifanya la kudumisha Muungano na kuuenzi na kuudumisha , lakini kubwa zaidi mmetoa funzo kwa mchezo huu mlioufanyam, hili ni funzo hata kwa vijana wengine na Watanzania wote mnatakiwa kuishi kwa ushirikiano sio kwa michezo tu hata katika Mambo mengine ya maendeleo ili kuendeleza umoja, mshikamano na uzalendo kama Watanzania bila kujali itikadi za Vyama vyetu", alisema Mkuu huyo.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Kigoma Silvia Sigura alisema Wao kama Viongozi wa Vijana walibuni mchezo huo katika sikuku ya Muungano,lengo likiwa ni kuwaunganisha Vijana wa Mkoa wa kigoma kuwa wamoja na kuendeleza ushirikiano katika kuuinua Mkoa wa Kigoma.

Alisema Michezo ni Afya,ni jambo linaloweza kuwaunganisha Vijana kwa umoja na kuendelea kushirikiana katika Mambo mbali mbali,na Kuwaomba Vijana kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri  ili kudumisha amani na mshikamano wa Taifa la Watanzania bila kuangalia Vyama vyao na kuendeleza umoja na mshikamano katika kazi na mambo mbali mbali ya Kijamii.

Nao baadhi ya Vijana wa boda boda walioshiriki katika Mchezo huo January Exavery alisema wanaushukuru sana uongozi wa UVCCM mkoa wa Kigoma kwa Kuandaa mchezo huo wa kirafiki na kuomba ushirikiano huo waliouanzisha uendelee na kuwaasa vijana wengine waachane na ushabiki wa Vyama vya siasa kwa kufanya mambo yasiyo na msingi na wafanye kazi.

Alisema Rais anafanya kazi kibwa kuhakikisha Wananchi wanapata hiduma bora na maendeleo na kuwaasa Vijana kiwa Wakati huu ni wakati wa kufanya kazi kwa kushirikiana na sio wakati wa kukaa vijiweni na kuzungumzia siasa zisizo na Maendeleo na Wafanye kazi kwa bidii ilikuondokana na Umasikini.
MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Brigedia Jenerali Marko Gaguti akizungumza wakati akiwapongeza Vijana wa Kigoma kwa kuandaa mchezo wa kirafiki baina ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi na Bodaboda bila kujali itikadi za Vyama vyao kwa dhana ya kuuenzi Muungano wa Tanzania, .

JAJI MKUU AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI MITI KATIKA KIWANJA CHA MAHAKAMA-DODOMA

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa upandaji miti, kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, kushoto ni Mhe. Ferdinand Wambali,Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akipanda mti wake.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipanda mti.
Watumishi na Wadau mbalimbali nao walishiriki katika zoezi la kupanda miti.
 

SIMBA VS YANGA KUMEKUCHA APRIL 29, MSIKIE HAJI MANARA...

Viewing all 110016 articles
Browse latest View live




Latest Images