Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

MALARIA YAPUNGUA MPAKA ASILIMIA 7. 3 NCHINI.

0
0
Na Ripota wetu Kasulu, Kigoma 

MAAMBUKIZI ya viashiria vya ugonjwa wa Malaria Nchini Tanzania yame pungua kwa Watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 na kufikia asilimia 7.3 kwa Mwaka 2017 hii ni kuzigatia harakati zinazo fanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mashirika ya Marekani (USAID) pamoja na shirika la WHO kuhakikisha wanautokomeza ugonjwa huo. 

Akizindua takwimu zilizo tolewa na Ofisi ya Takwimu ya Tanzania leo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu , alisema Siku ya leo kupitia maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa Kigoma, atazindua rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017. 

Kwa Mujibu wa Mkurugenzi mkuu ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Albina Chuwa alithibitisha Matokeo ya sasa ya utafiti huu, yanaonesha kuwa kiwango cha malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Tanzania kimeshuka kwa Zaidi ya nusu kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3. Hii ni kwa kutumia kipimo cha haraka cha utambuzi wa vimelea (mRDT). 

Waziri Ummy alisema utafiti huo unaonesha Mikoa yenye kiwango kikubwa cha watoto wenye malaria ni, Kigoma (asilimia 24.4), Geita (asilimia 17.3), Kagera (asilimia 15.4) na Tabora (asilimia 14.8) ambapo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Njombe, Songwe na Dodoma ina kiwango kidogo cha maambukizi chini ya asilimia moja. 

"Takwimu hizi, zinaonesha kupungua kwa kiwango cha malaria kwa kiasi kikubwa, na hii ni habari njema kwetu sote na inaonesha ni jinsi gani Serikali yenu ipo tayari kutoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa malaria inadhibitiwa na hatimae tuweze kuitokomezwa kabisa Ili kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa, tunapaswa kufanya kazi kwa pamoja katika kufikia malengo tuliyojiwekea ili jamii, hasa watoto chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wajawazito ambao ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa wa malaria waweze kuepukana na ugonjwa huu", alisema Waziri Mwalimu. Alisema Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, lakini bado kuna changamoto, ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo ya kutokomeza malaria nchini. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akionyesha rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako – kwanza kulia, Balozi wa Uswizi ha Tanzania Florence Tinguell na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid na Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni– kwanza kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid na na Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Takwimu Tanzania – NBS Albina Chuwa.


Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa Serikali na viongozi wa mashirika mbali mbali ya kimataifa, wakiwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu kushoto akipokea ramani ya Tanzania inayoonyesha maeneo yaliyopungua kwa malaria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Malaria Duniani Mkoani Kigoma,pichani kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.
Afisa Mradi JOHNS HOPKINS  VectorWorks  Jacqueline Madundo akitoa maelezo mafupi kuhusu mfumo unaosimia uwajibikaji katika maswala ya vyandarua nchini kwa Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa  kilele cha Maadhmisho ya Malaria yaliyofanyika leo katika wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DK.SHEIN AWASILI MKOANI DODOMA LEO

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge  mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mkoani humo, ambapo anatarajiwa kushiriki katika sherehe za maadhimishi ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanzania zitakazofanyika leo,katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)  akisalimiana na Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika mapokezi yake mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mkoani humo, ambapo anatarajiwa kushiriki katika sherehe za maadhimishi ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanzania zitakazofanyika leo,katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma (Picha na Ikulu.).  

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI MJINI DODOMA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, bungeni mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. 
 aziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Josephat Kandege, bungeni mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Musoma  Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye  (katikati) na Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 25, 2018. (Picha na  Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya El Shadai ya mjini Dodoma kwenye viwanja vya bunge, Aprili 25, 2018. Wapili kushoto ni mwalimu wa Shule hiyo, Vincent Kawilima.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. Kutoka kushoto ni Dkt, Raphael Chegeni wa Busega, Danstan Kitandula wa Mkinga, Venance Mwamomoto wa Kilolo, Mussa Sima wa Singida Mjini na Mbunge wa Kuteuliwa Abdallah Bulembo. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ELIMU MATUMIZI YA ARDHI INAYOTOLEWA NA PELUM TANZANIA IMESAIDIA PUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
OFISA Mradi wa mradi wa Ushirika wa wananchi katika kusimamia sekta ya kilimo, Anna Marwa amesema, kupitia elimu ya matumizi ya ardhi inayotolewa na Pelum Tanzania migogoro ya ardhi imepungua kwa asilimia 80.

Aidha amesema, kupungua kwa migogoro hiyo kumetokana na kuongezeka kwa uelewa kwa wananchi na kuwepo kwa mpango wa matumizi ya ardhi ambao umeanisha maeneo na matumizi yake huku mafunzo pia yakisaidia uelewa wa haki ya ardhi kupanda kwa asilimia 30.

Marwa ameyasema hao leo mjini Morogoro kwenye mdahalo wa haki za ardhi wilayani Mvomero ambapo mada kuu ni Usimamizi sahihi wa mpango wa matumizi ya ardhi na uundwaji wa vyombo vya utatuzi wa migogoro ya ardhi vimesaidiaje kupunguza migogoro ya ardhi kijijini.

Amesesema mbali na mafanikio hayo, wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali, ikiwemo kushindwa kuwafikia wananchi wengi zaidi kuwapimia vipande wa ardhi kwani katika kila kijiji walikuwa wakikaa siku nne tu na idadai ya watu ni wengi  na kushindwa kuwapimia wanakijiji wengi.

Pia uelewa wa haki ya ardhi bado haujafikia watu wengi na kuongeza kwenye mafunzo yao wamegundua suala la arddhi ni mtambuka na linahitaji ushirikishwaji wa Serikali, wadau na mashirika binafsi ili kukabiliana na changamoto za ardhi.

Akitoa maoni yake baada ya kupata mafunzo hayo, Mwenyekiti wa kijiji cha Melela wilayani humo amesema,  migogoro ya ardhi imepungua kwa kiwango kikubwa na kila eneo limetengwa kwa shughuli maalum, watu wametambua maeneeo wanayotakiwa kufanyia shughuli zao.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Melela, Amin Membe akielezea namna mafunzo ya Pelum juu  mpango wa matumizi ya ardhi katika kijiji hicho yalivyosaidia kupunguza migogoro ya ardhi  na kuwa sasa ardhi inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa sehemu husika.
 Afisa mradi wa  mradi wa ushirika wananchi katika kusimamia sekta ya Kilimo, Anna Marwa akielezea wanakijiji wa wilaya ya Mvomero, mafanikio na Changamoto za utekelezaji wa mradi wa mafunzo ya elimu juu ya shughuli za ardhi katika mdahalo wa haki za ardhi wilaya ya Morogoro uliomalizika leo Mjini Morogoro.
 Afisa Mtendaji wa Mela, Jotham Mbwambo akieleza wadau hawapo pichani namna walivyojifunza na kuweza kupunguza migogoro ya ardhi katika kijiji cha Meela na kwani kwa kipindi cha miezi sita kati ya migogoro 21 wamefanikiwa kutatua migogoro kumi na nane na kubakia mitatu tu.
 Mfalme Ole Kerei ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri ya kijiji cha Mela  akitoa maoni yake katika mdahalo  wa haki za ardhi wilaya ya Mvomero uliofanyikia Mjini Morogoro.
 Diwani wa kata ya Sungaji katika Halimashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro, Deogtratious Daniel  ambaye pia ni mgeni rasmi katika mdahalo wa haki za ardhi Wilaya ya Mvomero akizungumza na wadau mbali mbali wa ardhi wakati wa ufunguzi wa mdahalo huo uliofanyika leo Mjini Morogoro.
Daniel amemwakilisha Kaimu Mwenyekiti wa Halimashauri ya Morogoro katika mdahalo huo.
Wadau wa ardhi, wakulima na viongozi wa vijiji mbalimbali walioshiriki mdahalo wa haki za ardhi wilaya ya Mvomero wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo Mjini Morogoro.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

REX ENERGY YAWAANDAA VIJANA 100 KUTOKA DIT KABLA YA KUWAPA AJIRA

0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Rex Energy inayojuhusisha na utoaji wa huduma ya umeme wa jua Francis Kibhisa ameamua kutoa mafunzo ya vitendo kwa wahandisi 100 ambao wamehitimu Dar es Salaam Institute Technology(DIT)na baada ya hapo atawapa ajira huku akifafanua ipo haja ya kuhakikisha vijana wa kitanzania wanapata ajira.

 Kibhisa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema wameamua kuja na utaratibu wa kuwachukua wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini na kisha kuwapata elimu kwa vitendo kabla ya kuwapa ajira na wale ambao wataonekana wanamudu majukumu yao basi watapewa ajira.

Amesme wameanza na Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuchukua wahitimu hao 100 kutoka DIT na baada ya mafunzo hayo watawasambaza kwenye matawi yao yaliyopo Dar es Salaam na mikoani ambapo watakuwa kwenye majaribio kwa mwaka mmoja na baada ya hapo watapata ajira.

Amefafanua ndani ya muda huo watakuwa wanalipwa baadhi ya stahiki zao kama ambavyo wanapewa walioajiriwa ili wajikimu kimaisha wakati wanaendelea na majukumu yao.

"Sisi tumeanza na tutaendelea, kuna vijana wengi ambao wamehitimu vyuoni lakini hawana pakwenda, kwetu tumeamua kuwapa ajira vijana hao na kabla ya kufika kwenye ajira tumeamua kwanza tuwape elimu ya kile ambacho watakwenda kukifanyia kazi.

"Bahati nzuri kauli mbiu ya Serikali ni watu kufanya kazi na hivyo wameona wanayo nafasi ya kuhakikisha wanaunga mkono kauli mbiu hiyo kwa kuwaajiri vijana wa kitanzania nao wawe sehemu ya ujenzi wa maendeleo ya nchi yetu.

"Ushauri wangu wenye uwezo wa kuajiri ni vema wakafanya kila linalowezekana kuajiri vijana wa kitanzania.Tumeanza na wahandisi hao zaidi ya 100 ambapo tutawapa mafunzo kwa siku tatu na baada ya hapo watakwenda kwenye maeneo yao ya kazi,"amesema.

Ameongeza Rex Energy wamekuwa kwenye soko sasa kwa miaka 18 huku akielezea changamoto kubwa iliyopo ni kuingizwa kwa vifaa ambavyo havijakidhi ubora , hivyo ameomba waaoingiza vifaa hivyo hasa vinavyohusu masuala ya Sola wakazingatia ubora unaohitajika kimataifa.

Ametoa rai kwa vijana nchini wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na kueleza Mhandisi wa sasa atakombolewa kwa kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo.

Kuhusu mafunzo ambayo wanayaotoa kwa vijana hao kabla ya kuwapingia maeneo ya kufanyia kazi, Kibhisa amesema wanafundisha namna ya kuhudumia mteja, mhandis wa sasa atakombolewa kwa kufanya kazi kwa bidii.

Baadhi ya vijana wanaopatiwa mafunzo hayo na Rex Energy akiwamo Coletha Jackson na Nyaronga Nguka wamesema yameongeza maarifa zaidi ya yale ambayo wameyapata wakiwa DIT.

Pia wamewashauri vijana badala ya kukaa vijiweni kuchangamkia fursa kama ambayo wameipata wao baada ya kuona kwenye mtandao kuhusu taarifa ya Rex Energy waliomba na hatimaye wamepata.
Mkurugenzi Mtendaji wa Rexy Energy, Francis Kibhisa akizungumzia jijini Dar es Salaam leo kuhusu mafunzo wanayoyatoa kwa wahitimu 100 wa DIT ambao wamewachukua kwa lengo la kuwaajiri.
Baadhi ya vijana wakiendelea kuwepewa mafunzo kutoka kwa watalaam wa Rexy Energy jijini Dar es Salaam.

VOA Swahili: Duniani Leo 25th April 2018

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 24.04.2018

Ufunguzi rasmi wa maonesho ya kipekee ya bidhaa za viwanda vya Tanzania nchini Kenya

0
0

Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Mwangi Kiunjuri akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa wiki ya Tanzania nchini Kenya ambayo imeambatana na maonesho ya huduma, vivutio vya utalii na bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 28 Aprili 2018 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (KICC) Jijini Nairobi, Kenya.


Mhe. Waziri Kiunjuri akihutubia wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Wiki ya Tanzania nchini Kenya ambayo itaenda sambamba na Maonesho ya bidhaa za viwanda, Kongamano la biashara na Maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanzania. Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, Kenya tarehe 25 Aprili 2018.
Mhe. Wanjuri katika hotuba yake amesisitiza umuhimu wa kilimo cha kisasa ili kupata mazao yatakayokidhi vigezo vya ubora na kuingia katika ushindani wa biashara kimataifa utakaopelekea maendeleo ya uchumi hususan uchumi wa viwanda.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Wiki ya Tanzania nchini Kenya ambapo alieleza kuwa tukio hili ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya marais wa Tanzania na Kenya walipokutana katika Mkutano wa 19 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akiwakaribisha wageni waalikwa katika hafla ya ufunguzi rasmi wa wiki ya Tanzania nchini Kenya.
Katika ufunguzi huo Mhe. Chana alieleza  umuhimu wa maonesho hayo ni pamoja na kuzitangaza huduma na bidhaa za viwanda  vya Tanzania ili ziweze kupenyeza katika soko la Kenya. Maonesho hayo yametoa fursa kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania kukutana na kufanya mazungumzo ya biashara na wafanyabishara kutoka katika kampuni za Kenya.

Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Katibu wa kamati ya maandalizi ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya, Balozi Anisa Mbega  na mjumbe kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Francis Mossongo wakifuatilia hafla ya ufunguzi.

Sehemu ya wafanyabiashara kutoka Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa hafla hiyo. 
Sehemu nyingine ya wafanyabiashara wakifuatilia hafla ya ufunguzi huo.



Sehemu ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa  nchini Kenya wakifuatilia hafla ya ufunguzi.

Sehemu nyingine ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa  nchini Kenya wakifuatilia hafla ya ufunguzi.

Wajumbe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wakifuatilia hafla hiyo.
 =======================================================================
Wakati huo huo Mhe. Waziri Kiunjuri alitumia fursa hiyo kukabidhi vyeti kwa washiriki pamoja na kutembelea mabanda ya maonesho.

Mhe. Waziri Kiunjuri akikabidhi cheti cha ushiriki kwa mwakilishi wa kampuni ya Lake Group, Bw. Peter Sifa

Mhe. Waziri wa Kiunjuri akimkabidhi cheti cha ushiriki mwakilishi kutoka Kampuni ya vinywaji (Tanzania Distillers Ltd)
Mhe. Waziri Kiunjuri akikabidhi cheti cha ushiri kwa mmoja wa wafanyabiashara kutoka Zanzibar, Bw. Nassoro Omar wa Kampuni ya ZANOP.
Mhe. Kiunjuri akimkabidhi cheti mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maonesho na Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE),  Bw. Edwin Rutageruka.

Mhe. Waziri Kiunjuri akimkabidhi cheti Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na mwenyekiti mwenza wa kamati ya maandalizi ya Wiki ya Tanzania nchini Kenya, Bw. Godfrey Simbeye kwa kufanikisha zoezi la uratibu wa wiki hiyo.

Mhe. Waziri Kiunjuri akipokea maelezo kwa mmoja wa washiriki wa maonesho ya bidhaa kutoka Tanzania, Bw. Amir Esmail kutoka kampuni ya kahawa ya AMIMZA.

Kikoa cha Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) chafanyika jijini Dar es Salaam

0
0
Na Brighton James - JKCI,
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kuepuka vitendo vya rushwa  ili waweze kutoa huduma bora ya bila upendeleo ya matibabu kwa wagonjwa. Rai hiyo imetolewa leo na Asseri Mandari kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) makao makuu wakati akitoa mada ya rushwa sehemu ya kazi katika kikao chaWajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mandari alisema kuwa katika maeneo mengine ya Hospitali baadhi ya wagonjwa  wanashidwa au kuchelewa kupata huduma bora kutokana na mazingira ya rushwa kutawala.
“Ninawapongeza kwa huduma bora ya matibabu ya moyo mnayoyatoa kwa wananchi jambo la muhimu ni  kufanya kazi zenu  kwa kufuata maadili ya utumishi wa Umma, kuwaheshimu wateja wenu bila ya kuwabagua kutokana na hali zao za maisha, kutumia lugha nzuri kwa wateja na kutunza siri ya kazi zenu”, alisisitiza Mandari.
Aliendelea kusema kuwa  athari zinazotokana na  vitendo vya rushwa ni pamoja na kushuka kwa pato la taifa kutokana na kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa, kudumaza mipango ya maendeleo na kuchochea umaskini kwa mtu mmoja mmoja au zaidi.
Athari zingine ni  wananchi kukosa imani na Serikali iliyopo madarakani, kushuka kwa kiwango cha uwajibikaji kazini , kukwamisha utoaji wa haki na kuongezeka kwa maovu.
Akitoa mada kuhusu kazi na uendeshaji wa majukumu ya baraza Mkurugenzi Msaidizi wa Mabaraza kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu   Andrew Mwalwisi alisemabaraza haliwezi kuwepo kama chama cha wafanyakazi hakipo hivyo basi  wajumbe wahakikishe wanawahamasisha wafanyakazi ili wajiunge na chama hicho.
 Alisema wajumbe ni viongozi hivyo basi wanatakiwa kuwa na taarifa sahihi za maeneo yao ya kazi na kushiriki kikamilifu katika vikao vya baraza la Wafanyakazi kwa kutoa mapendekezo na ushauri wa kitu gani Menejimenti ifanye ili kuboresha utoaji wa huduma na maslahi ya wafanyakazi na siyo kufanya maamuzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza  Prof. Mohamed Janabi aliwashukuru wajumbe wa baraza hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha kuwa huduma bora ya matibabu ya magonjwa ya moyo inatolewa  kwa wananchi.
“Mimi pamoja na Menejimenti yangu tutahakikisha kuwa maoni yote yaliyotolewa katika kikao hiki tunayafanyia kazi ili kuboresha ufanisi wa kazi katika Taasisi yetu. Nanyi wajumbe muhakikishe kuwa yale yote yaliyofundishwa na kujadiliwa  katika kikao hiki mnaenda kuyafanyia kazi”,
“Boresheni utendaji wenu wa  kazi kwa kuhakikisha mnatoa  huduma bora kwa wakati ikiwemo kuwahudumia vizuri wagonjwa na wateja wetu wengine , kuwahi kufika kazini na kuwepo eneo la kazi muda wote wa kazi kwa kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa kazi  na kupunguza  malalamiko kutoka kwa wananchi”,  alisema Prof. Janabi.
Katika kikao hicho mada mbalimbali zilijadiliwa  ikiwa ni pamoja na rushwa sehemu ya kazi, uendeshaji wa majukumu ya Baraza na kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi kwa mwaka wa fedha 2017/18.
 Mwenyekiti wa  Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi akiongoza kikao cha baraza kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo Renatha Miiruko.
 Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza mada ya rushwa sehemu ya kazi iliyotolewa na Asseri  Mandari  kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) makao makuu wakati wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kwa mwaka 2017/18  wakati wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo kwa mwaka 2017/18  wakati wa kikao cha Baraza hilo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo kilichoganyika leo jijini Dar es Salaam. Mstari wa kwanza katikati ni Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi. Picha na JKCI

MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA MTUMISHI WA OFISI YA WAZIRI MKUU, AMTEMBELEA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO HOSPITALI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaleo (Jumatano, Aprili, 25, 2018) ameshiriki maziko ya aliyekuwa mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu marehemu Bw. Atufigwege Mwakasege yaliyofanyika katika makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma. 
Bw. Mwakasege ambaye alihamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 29, 2016 akitokea Ofisi ya Rais-TAMISEMI amefariki dunia Aprili 23 mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alikuwa amelazwa baada ya kuugua.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama amesema kifo hicho kimeiachia pengo kubwa  kwa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na familia. 
“Natumia fursa hii kutoa pole kwa wanafamilia hususan mjane na watoto. Marehemu ameacha pengo ndani ya familia, hivyo tumuombe Mwenyezi Mungu awape uwezo na nguvu ya kuweza kuhimili pengo hilo.” 
Marehemu Bw. Mwakasege ambaye alizaliwa Desemba 25, 1959 katika kitongoji cha Mwanjelwa mkoani Mbeya, ameacha mjane Bibi Judith Mwakasege pamoja na watoto wane ambao ni Henry, Joel, Eva na Kelvin Mwakasege. 
Maziko hayo pia yamehudhuriwa na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mama Mary Majaliwa, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola, Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi, Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wakati huo huo, WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Bw. Abbas Kandoro ambaye amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu.
Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatano, Aprili 25, 2018), Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta Bw. Kandoro na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye hospitali hiyo wakihudumiwa vizuri. 
Pia Waziri Mkuu amemjulia hali Mbunge wa Viti Malumu (CUF) Bi. Shamsiha Azizi Mtambo ambaye amelazwa katika ya Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU)kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma akipatiwa matibabu. 
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba madaktari wataendelea kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku.
Kwa upande wake, Bw. Kandoro alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia hali, pia aliwashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali hiyokwa huduma nzuri wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakitoa heshima za mwisho kwa mfanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Atufigegwe Mwakasege, nyumbani kwa marehemu eneo la Kikuyu mjini Dodoma Aprili 25, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  wakiweka shada la  maua kwenye kaburi la mtumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Atufigegwe Mwakasege katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kikuyu mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro ambaye amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma kwa matibabu leo  Aprili 25, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


WANANCHI WAJITOLEA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA PANGANI MJINI KIBAHA

0
0
 Wakazi mbalimbali kutoka mitaa ya kata ya Pangani, Kibaha Mjini wakionekana pichani kujitolea katika nguvu kazi kujenga shule ya sekondari ya Pangani 
Msaidizi wa mbunge wa jimbo la Mjini Kibaha ,Method Mselewa (aliyeshika tofali) akiwaunga mkono wakazi wa kata ya Pangani ,katika zoezi la kujitolea kujenga shule ya sekondari. Picha na Mwamvua Mwinyi.

RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA AKUNWA NA KASI YA RAIS MAGUFULI

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB,  DKT. AKINUMWI  ADESINA, ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuahidi kuwa benki yake itawekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1 nukta 5 kwenye sekta mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili ijayo. 
Dkt. Adesina ameyasema hayo alipowasili kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.
"Tunajivunia uhusiano wetu wa muda mrefu na Tanzania ambayo ni mnufaika anayeongoza miongoni mwa nchi za kiafrika kupata ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu kutoka benki yetu ambapo tangu mwaka 1971, Benki imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.6" alisema Dkt. Adesina
Alisema kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.
"Katika miundombinu ya barabara peke yake, Benki yangu imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.1 na kwamba uwekezaji huo utasaidia kuboresha usafirishaji wa bidhaa na abiria hivyo kuchochea ukuaji na uendelezaji wa uchumi wa viwanda" alisema Dkt. Adesina.
Dkt. Adesina ameutaja mradi mwingine mkubwa wa kusafirisha umeme wenye msogo wa kilovolti 400 wenye njia yenye urefu wa kilometa 670 katika Ukanda wa Kusini na Kusini Magharibi mwa Tanzania, unaohusisha pia ujenzi wa vituo vya kupozea umeme katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga, wenye thamani ya dola milioni 220.
"Miradi hii pamoja na ile wa umeme wa kutumia joto ardhi pamoja na maji inayotarajiwa kupatiwa fedha na Benki hiyo, itasaidia sana mkakati wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, ambaye ammwagia sifa kwa utendaji kazi wake mahili, wa kujenga uchumi wa viwanda kwa kuwa na umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu" aliongeza Dkt. Adesina.
Alisema Tanzania imepiga hatua katika viwango vya wananchi kupata huduma ya umeme ambapo awali ilikuwa asilimia 18 lakini hivi sasa kiwango hicho kimepanda hadi kufikia asilimia 38 na kwamba lengo la benki hiyo ni kutaka kiwango hicho kifikie asilimia 82 katika miaka michache ijayo.
Alisema ili kufikia hatua hiyo Benki yake ina mpango wa kuboresha Shirika la Ugavi wa Umeme nchini-TANESCO ili liongeze uzalishaji wa umeme wenye gharama nafuu, kuongeza ufanisi na kutengeneza faida ili kuchochea maendeleo ya viwanda.
Aidha, Rais huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, ameeleza kuwa benki yake inasiadia kuendeleza kilimo nchini kupitia Mpango wa Kukuza Kilimo katika Ukanda Kusini mwa Tanzania-SAGCOT, kwa kukuza masoko na uongezaji thamani ya mazao ya wakulima yanayozalishwa kupitia mradi huo.
Akizungumzia miradi ya kikanda, Dkt. Adesina alisema kuwa benki yake imewekeza katika miradi ya nishati ya umeme na miundombinu ya barabara ili kuunganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi na Kenya ili kurahisisha biashara na kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme katika nchi hizo.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameeleza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni mshirika mkubwa wa Maendeleo wa Tanzania kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika nyanja mbalimbali.
Alisema kuwa AfDB, licha ya kusaidia kwa kiasi kikubwa kufadhili miradi ya ujenzi wa barabara, nishati na mingine mingi na mfuko mkuu wa Serikali, mwaja jana ilitoa pia mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 50 kwa ajili ya kukuza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB, zinazotumika kukopesha wakulima.
Dkt. Mpango amesema kuwa Rais huyo akiwa hapa nchini atatembelea mradi wa kituo cha kupooza umeme cha Zuzu kilichoko mkoani Dodoma na ataungana na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua barabara ya Dodoma-Babati hadi Arusha, iliyofadhiliwa na Benki hiyo na washirika wake.
 Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (katikati) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, wakiingia kwenye jengo la watu mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya Rais huyo kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mjini Dodoma
 MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akizungumza jambo wakati Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) wakigonga "tano" wakati wa mazungumzo yao wakati rais huyo alipowasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.
2921
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.

BALOZI DKT. ABDALLAH SALEH POSSI AKUTANA NA WAFANYABISHARA WA POLAND WENYE NIA YA KUWEKEZA TANZANIA JIJINI WARSAW

0
0
Mnamo April  24, 2018  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi, alikutana na wadau mbalimbali wa uwekezaji katika mkutano wa kibiashara ulioandaliwa na jumuia ya biashara ya Poland jijini Warsaw. Mkutano huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya safari ya kibiashara inayotarajiwa kufanyika mwezi juni mwaka huu. Safari hiyo itahusisha wafanyabiashara kutoka Poland wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania. 

Balozi aliwahimiza wafanyabiashara kutoka Poland kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali, haswa zinazotegemea mali ghafi kutoka nchini, na zenye uwezo wa kutengeneza ajira kwa wananchi wengi, na hivyo kupunguza utegemezi wa uagizaji bidhaa kutoka nje. Sekta hizo ni kama vile madawa, nguo, kilimo na chakula (hussusan uzalishaji wa sukari na mafuta ya kula). Pia balozi aliwahimiza wawekezaji hao kuangalia fursa katima sekta nyingine, haswa nishati mbadala na utalii.

Wahudhuriaji walionyesha kurishishwa na muelekeo wa uchumi wa Tanzania. Licha ya baadhi ya watoa mada kuainisha changamoto mbalimbali, mkutano huu ulitoa taswira ya kujengeka ushawishi miongoni mwa wafanyabiashara wa Poland kuhusiana na uwekezaji Afrika, haswa Tanzania.
Mada mbalimbali ziliwasilishwa na: Balozi Jerzy Drożdż, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kimataifa kutoka kutoka taasisi ya biashara ya Poland (Polish Chamber of Commerce); Bw. Eugeniusz Rzewuski, Kaimu Balozi wa zamani wa Poland nchini Tanzania; Balozi. Jan Wieliński, Balozi Mstaafu wa Poland katika nchi kadhaa za Afrika; Bw. Robert Zduńczyk, Rais wa Taasisi ya Uchumi Poland-East Africa; Bi, Agata Świtalska-Krych, Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo wa Wielkopolski, mfuko unaosaidia biashara ndogo na za kati, na maendeleo mijini; Bw. Konrad Pawlik, Makamu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Poland; Bi. Katarzyna Kwiecień, Mkurugenzi wa National Support Center for Agriculture; Bw. Wojciech Rząsiecki, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Serikali (Government Export Credits) Wizara ya Mambo ya Nje ya Poland; Bw. Łukasz Porażyński, kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Ujasiriamali na Teknolojia ya Poland; Bw. Piotr Maciaszek, mkurugenzi wa Export Credit Insurance Corporation Joint Stock Company (KUKE); Bw. Arkadiusz Zabłoński, Mkurugenzi wa Idara ya Kusaidia Biashara ya Mauzo ya Nje (Department of Export Support, BGK).
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi, akiongea na wadau mbalimbali wa uwekezaji katika mkutano wa kibiashara ulioandaliwa na jumuia ya biashara ya Poland jijini Warsaw ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya safari ya kibiashara inayotarajiwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu. Safari hiyo itahusisha wafanyabiashara kutoka Poland wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania. Kulia kwake ni kiongozi wa Diaspora ya Watanzania nchini Poland Bw. Julius Zellah ambaye taasisi yake inafanya kazi kwa karibu na wafanyabiashara wa Poland.
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi, akibadilishana mawazo  na wadau mbalimbali wa uwekezaji pembeni ya mkutano wa kibiashara ulioandaliwa na jumuia ya biashara ya Poland jijini Warsaw.
 Wadau mbalimbali wa uwekezaji wa nchi ya Poland wakiwa kwenye mkutano wa kibiashara ulioandaliwa na jumuia ya biashara ya Poland jijini Warsaw uliohudhuriwa na  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi
  Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, ambaye pia anaiwakilisha Tanzania nchini Poland, Dr. Abdallah Saleh Possi akiwa na Kiongozi wa Diaspora ya Watanzania nchini Poland Bw. Julius Zellah pamoja na viongozi wa wafanyabiashara kutoka Poland wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania. 
Balozi Jerzy Drożdż, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kimataifa kutoka kutoka taasisi ya biashara ya Poland (Polish Chamber of Commerce) akitoa mada kwenye mkutano huo.

TANZANIA FREIGHT FORWARDERS ASSOCIATION EXTRA-ORDINARY MEETING APRIL 28, 2018 AT KARIMJEE HALL IN DAR ES SALAAM

UNESCO yafunga mafuzo ya Mafundi Mitambo wa Radio za jamii 25

0
0
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu UNESCO inavyoshiriki moja kwa moja kwenye jamii hasa kuzisadia Radio za kijamii ili kufanya kazi zake kifanisi wakati wa kufunga mafuzo ya mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar yaliyofanyika kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mafunzo haya ya siku saba yameratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC, Joseph Kambanga akizungumza namna TBC ilivyojitolea kuzisaidia Radio za kijamii ili kuimarisha upatikanaji wa habari na hata kuimarisha mitambo ya urushwaji wa matangazo kwenye jamii haraka wakati kufunga mafuzo ya mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar yaliyofanyika kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Rose Mwalongo akisisitiza umoja wa mafundi mitambo waliopata mafunzo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Fundi Mitambo wa Redio Jamii Orkonerei FM, Baraka David Ole Maika akitoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) pamoja na Shirika la utangazaji la Tanzania(TBC) kwa kuweza kutoa mafunzo kwa mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 yalifanyika kwa Siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Rose Mwalongo(wa kwanza kushoto) pamoja na walimu waliotoa mada mbalimbali katika mafunzo kwa mafundi mitambo wakiwa kwenye mkutano wa kufunga mafunzo hayo.

Baadhi ya mafundi mitambo wa radio za kijamii 25 wakifuatilia mada wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu ambao ni mafundi mitambo kutoka radio za kijamii 25 mara baada ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku saba.


QATAR AIRWAYS YATEMBEZA WAANDISHI MJINI DOHA.

0
0
Qatar Airways yapeleka waandishi kutoka vituo mbalimbali vya habari na utangazaji  vya Africa kwa ajili ya matembezi mjini Doha. Katika matembezi hayo wanahabari walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali kama Makumbusho ya Sanaa ya kiislamu (museum of Islamic art) haya ni makumbusho yaliyopo katika mji mkuu wa Qatar, Doha. Pia walitembelea Kijiji cha kitamaduni cha Katara, Katara ni kijiji kitamaduni huko Doha, Qatar. 

Iko katika pwani ya mashariki kati ya West Bay na Lulu ambayo Ilifunguliwa mnamo Oktoba 2010. Walitembelea The Grand Mosque, Msikiti wa Kitaifa Qatar. Huu ni mojawapo ya misikiti mikubwa ya kihistoria nchini Qatar, Msikiti huu uko katika wilaya ya Jubailat Doha. Wanahabari hao pia walipata nafasi ya kutembelea maeneo kama Souq waqif, Falcon souq, na Gold souq ambapo waliweza kujionea vitu vingi kama mapambo na vito vya thamani vilivyotengenezwa kwa dhahabu na madini ya aina mbalimbali.

Katika ziara yao mjini Doha waandishi wa habari walitembelea Qatar foundation, Al Shaqab sehemu ambayo hutumika kuwapa mafunzo farasi katika jamii za kiarabu, the Pearl na Khalifa International Stadium; ambayo inajulikana kama Uwanja wa Taifa, ni uwanja unaotumika kwa shughuli mbalimbali huko Qatar ambao pia ni kama sehemu ya eneo la Doha Sports City, ambalo linajumuisha Aspire Academy, Kituo cha Hamad Aquatic, na Aspire Tower park. Uwanja ulipewa jina hilo baada ya Khalifa bin Hamad Al Thani, ambaye zamani alikuwa kiongozi wa dini ya kiislamu (Emir) nchini Qatar. Mbali na maeneo hayo wanahabari walitembelea Regency sealine camp, Desert Safari, pia kituo cha utangazaji cha Al Jazeera.

Qatar Airways ina Zaidi ya miaka 20 katika kutoa huduma za anga, Ni shirika la ndege ambalo limejishindia tuzo mbalimbali ambapo kwa mwaka 2017 Qatar airways ilipata tuzo nyingi Zaidi ya tano na mwaka huu  imeshinda tuzo mbalimbali zikiwemo Crystal cabin award, Skytrax world airport award 2018, 2018 TripAdvisor travelers’ choice awards na Apex passenger choice award 2018. Qatar Airways imeshinda tuzo za Skytrax airline of the year mara nne (4) mfululizo katika miaka ya 2011, 2012, 2015 na 2017.

                                       “QATAR AIRWAYS, GOING PLACES TOGETHER.” 
    
 Wanahabari kutoka Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja walipokwenda kutembelea Makumbusho ya sanaa ya kiislamu mjini Doha.
 Waandishi na wadau wa habari wakiwa wamepumzika baada ya kuwasili Hamad International Airport mjini Doha, Qatar.  
Waandishi na wadau wa habari kutoka nchi mbalimbali za Africa i.e Tanzania, Uganda wakiwa katika picha ya pamoja walipokuwa Doha.

RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA AKUNWA NA KASI YA RAIS MAGUFULI

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, DKT. AKINUMWI ADESINA, ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuahidi kuwa benki yake itawekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1 nukta 5 kwenye sekta mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili ijayo,

Dkt. Adesina ameyasema hayo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.

“Tunajivunia uhusiano wetu wa muda mrefu na Tanzania ambayo ni mnufaika anayeongoza miongoni mwa nchi za kiafrika kupata ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu kutoka benki yetu ambapo tangu mwaka 1971, Benki imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.6” alisema Dkt. Adesina

Alisema kuwa miradi inayoendelea hivi sasa nchini Tanzania kupitia ufadhili wa Benki yake imefikia thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 2 ambapo uwekezaji mkubwa uko katika sekta za nishati ya umeme, usafiri, miundombinu ya barabara, kilimo, maji na usafi wa mazingira, kusaidia Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na uendelezaji wa rasilimali watu.

“Katika miundombinu ya barabara peke yake, Benki yangu imewekeza zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.1 na kwamba uwekezaji huo utasaidia kuboresha usafirishaji wa bidhaa na abiria hivyo kuchochea ukuaji na uendelezaji wa uchumi wa viwanda” alisema Dkt. Adesina.

Dkt. Adesina ameutaja mradi mwingine mkubwa wa kusafirisha umeme wenye msogo wa kilovolti 400 wenye njia yenye urefu wa kilometa 670 katika Ukanda wa Kusini na Kusini Magharibi mwa Tanzania, unaohusisha pia ujenzi wa vituo vya kupozea umeme katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Shinyanga, wenye thamani ya dola milioni 220.

“Miradi hii pamoja na ile wa umeme wa kutumia joto ardhi pamoja na maji inayotarajiwa kupatiwa fedha na Benki hiyo, itasaidia sana mkakati wa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, ambaye ammwagia sifa kwa utendaji kazi wake mahili, wa kujenga uchumi wa viwanda kwa kuwa na umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu” aliongeza Dkt. Adesina.
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akizungumza jambo wakati Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) akisisitiza jambo alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kupokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango. 
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kulia) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) wakigonga “tano” wakati wa mazungumzo yao wakati rais huyo alipowasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma.


Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika -AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) wakiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo pia anatarajiwa kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mjini Dodoma. 

WAKALA WA VIPIMO YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA WA PAMBA

0
0
Wakala wa Vipimo (WMA) Tabora inaendelea na zoezi la kutoa elimu kwa Wakulima wa pamba kuhusu Mizani sahihi zinazotakiwa kutumika wakati wa msimu wa ununuzi wa pamba, elimu hii ya vipimo ni ya muhimu kwa Wakulima wakiwa katika maandalizi ya kuelekea katika msimu wa ununuzi wa pamba . 

Mpaka sasa Wakala wa Vipimo (WMA) Tabora imetoa elimu kwa Wakulima wa pamba katika wilaya mbili (2) ambazo ni Nzega na Igunga, na takribani kata 20 zimefikiwa na kupata elimu hiyo ambapo zoezi bado linaendelea. 

Wakulima wa pamba wameipokea kwa furaha elimu ya utambuzi wa mizani sahihi iliyo hakikiwa na wakala wa vipimo, kwani itawasaidia kuwabaini kwa urahisi wale wanaotumia mizani ambazo hazija hakikiwa wakiwa na lengo la kutaka kuwaibia pamba yao. 

Pia, elimu ya utambuzi wa mizani sahihi zilizohakikiwa na WMA itawasaidia Wakulima kuuza pamba safi, kwani apo awali walikuwa wanajihusisha na uchafuzi wa pamba kwa kuweka michanga, kokoto, mafuta ya kenge pamoja na maji ili waweze kuongeza uzito katika pamba pindi waendapo kuiuza.

Wakala wa Vipimo inatoa wito kwa wadau wote wa zao la pamba kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa aina yeyote haswa uchakachuaji wa mizani wakati wa ununuzi wa pamba, kwani kwa yeyote atakaye kamatwa kwa makosa hayo atashitakiwa kwa mujibu wa sheria ya vipimo sura na. 340.


Pia, WMA ina namba maalumu kwa ajili ya wananchi kupiga na kupata msaada pindi wakutanapo na changamoto za kivipimo, namba hiyo ni 0800 110097 namba hii ni bure kabisa.
 Wakulima wa pamba mkoa wa Tabora wakioneshwa sehemu ya kuweka lakili (seal) na kubandika stika ya WMA mara baada ya mizani kuhakikiwa.

 Wakulima wa pamba mkoa wa Tabora wakielekezwa na afisa vipimo namna ya kutambua mizani ya saa (salter) iliyo hakikiwa na wakala wa vipimo.

Afisa Vipimo akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mizani iliyo hakikiwa kwa wakulima wa pamba katika Wilaya ya Igunga kijiji cha mwabakina kata ya mbutu mkoani Tabora.

SEHEMU YA PILI YA HISTORIA YA VITA YA MAJI MAJI

0
0
Waanzilishi wa mwanzo wa Vita ya Maji Maji walikuwa ni Machifu na mganga wa jadi kutoka jamii za Wangindo na wamatumbi na baadaye vuguvugu hilo lilienea kama moto kwenya jamii nyingi ikijumuisha jamii za Wamatumbi,Wamwera,Wangindo,Wangoni,wapogoro,Wandendeule,Wabena,Wasangu na nyingine nyingi. Kwa undani wa Historia hii ya Vita ya Maji Maji tizama sehemu ya pili ya Historia ya Vita hivyo.
KAMA ULIPITWA NA SEHEMU YA KWANZA YA HISTORIA YA VITA YA MAJI MAJI HII HAPA CHINI.

Basata kutoa tuzo kwa wanafunzi wa Sekondari hapa nchini

0
0
Na Agness Francis,Blogu ya Jamii

BARAZA  la sanaa Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua kukuza na kuendesha sekta ya sanaa   kutoa tuzo kwa wanafunzi wa kidato cha 4 kwa shule 5 za Sekondari waliofanya vizuri masoma ya sanaa  hapa nchini.

Shule hizo zitakazo husika  katika kupewa tuzo hizo ni Mbeya Sekondari wanafunzi 2,Dodoma Sekondari 1,Edmund-Recesinon Sekondari Arusha 1,Mvuha Sekondari Morogoro 1 pamoja na Murungwa sekondari Kagera 2.

Baraza hilo limeamua kufufua  programu  endelevu ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi  wa shule za sekondari waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha 4 kwa mujibu wa sheria namba 23 mwaka 1984.

Ambapo safari hii watatoa kwa wanafunzi waliomaliza mwaka 2016 na kufaulu katika masomo ya sanaa za ufundi,maonyesho na muziki. 

Aidha amezungumza na wandishi wa habari  katika ofisi zake basata Jijini Dar Es Salaam mkurugenzi wa masoko na ukuzaji sanaa Basata Vivian Shalua  amesema kuwa utoaji wa tuzo hizo itachochea wanafunzi wengi kusoma masomo hayo katika kazi za sanaa na kuwasaidia kuongeza ufaulu wao darasani hasa ukizingatia sanaa ni nyenzo katika kumuandaa mtoto kielimu na kimaadili.

"Sanaa ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi ambao wameweza kijipa kipato na umaarufu kupitia fani hizi za Sanaa,hata hivyo masomo haya yamekuwa hayapatiwi kipaumbele kama yalivyo masomo mengine katika shule za msingi na sekondari"amesema Mama Shalua.

Mama shalua ametoa wito kwa kuwaalika  wadau wote wa sanaa  hapa nchini kufika kushuhudia utoaji wa tuzo hizo ambazo kauli mbiu yake (sanaa ni kazi ,nchi yangu kwanza).

Tuzo hizo zitatolewa Aprili 28 mwaka huu saa 4 asubui katika ukumbi wa Basata Sharifushamba Ilala Jijini Dar Es Salaam.
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images