Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109594 articles
Browse latest View live

ngoma azipendazo ankal

0
0
Ngoma ya 'Mashemeji Wangapi' ya hayati Mbaraka Mwinshehe Mwaruka bado mbichi hadi hii leo..

Sony dolby surround music system zinauzwa

0
0
Ninauza music wa Sony dolby surround, ni used,ziko 3 na  ndio zimefika kutoka Germany,kama zilivyo kwenye picha,ina mlango wa glass kwa mbele,kwa watu watakaokuwa interested wanaweza kuwasiliana na mimi kwa email hii add gabrielbudo@outlook.com ama kwa simu 0768808819 Naitwa Budo



Ngoma Africa band watingisha International African Tubingen 2013,Ujerumani,Mabalozi wa kiafrika nchini humo waipongeza FFU

0
0
Si nyingine bali Ngoma Africa band aka FFU ilifanikiwa kuutetea ubingwa wake wa bendi bora na kujichukulia Tuzo ya kimataifa ya IDA kule mjini Tubingen,Ujerumani katika maonyesho ya kimataifa ya International African Festival Tubingen 2013.

Bendi hiyo maarufu kwa kuwatia kiwewe washabiki na mdunduko wake imevunja rekodi kwa kuwa na washabiki wa kimataifa kila pembe.

Katika maonyesho ya International African festival 2013,yaliyofanyika mjini Tubingen,ujerumani Ngoma Africa band imekubalika sio na washabiki tu bali pia mabalozi kutoka nchi mbali mbali za kiafrika nchini Ujerumani ! bendi Tusikose kuwasikiliza ffu at www.ngoma-africa.com
kamanda mkuu ras makunja mstari wa mbele.
Kikosi kazi Ngoma Africa band.
Mabalozi wa nchi za Togo,Senegal na Kongo DRC wakiwa jukwaani kuipongeza Ngoma Africa band mwenye kipaza sauti Kamanda Ras Makunja.

balozi wa DRC Excellence Madame Clémentine Shakembo Kamanga,akiipongeza Ngoma Africa,mabalozi wengine wa nchi za kiafrika,ujerumani wakishuudia.
ffu na mitutu yao.

Airtel yakabidhi zawadi kwa washindi wake wa wiki hii

0
0
Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Bw, jackson Mmbando (Kulia) akiwa na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki hii Bw, Rakesh Mawji huku akitoa pesa zake mara baada ya kutumiwa kupitia huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam leo.
Meneja wa Duka la Airtel Makao makuu Bi, Happy John (kulia) akiwa na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki hii Bw, Rakesh Mawji akihesabu pesa zake mara baada ya kuzitoa kupitia huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam leo.
Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Bw, jackson Mmbando (kushoto) akiwa na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki hii Bw, Steven Maguru huku akihesabu pesa zake mara baada ya kuzitoa kupitia huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam leo.
Kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel Bw jackson Mmbando akimpongeza mume wa mshindi wa wiki hii Bw, Hassan Abdalah mara baada ya mke wake (kati) Bi Mwajuma kukabidhiwa zawadi yake shilingi milioni moja na kuitoa kupitia huduma ya Airtel Money Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar es salaam leo.
Kati ni Mwalim steven Maguru akionyesha pesa yake kwa furaha kiasi cha shilingi laki moja aliyotoa kupitia Airtel money mara baaada ya kushinda milioni moja na kupokea yote kupitia Airtel Money. Kulia ni mshindi mwingine wa wiki hii Bw, Rakesh Mawji na kushoto ni meneja Uhusiano wa Airtel bw, jackson Mmbando mara baada ya kukutana na washindi hao makao makuu ya Airtel jijini dar es salaam leo

kijiwe cha ughaibuni

MABONDIA WATAKA KUZICHAPA KAVU KAVU KABLA YA MPAMBANO WAO

0
0
Rais wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwaamulizia mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto na Simba Watunduru baada ya kusaini mkata wa kupambana August 30 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam.
Mabondia Simba Watunduru kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakitunishiana misuli wakati wa kutangaza mpambano wao.Picha na SUPER D.

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Simba Watunduru wamekiuka miko ya mchezo wa masumbwi baada ya kutaka kuchapana makonde kavu kavu mbele ya Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' wakati wa utiaji saini mkataba wa makubaliano wa kupambana mchezo wa kirafiki August 30 katika ukumbi wa Diamondi Jubilee.

Akizungumzia tukio hilo rais huyo alisema sijawai kuona vitu kama hivi vya ajabu maana vijana wamekamiana mpaka kufikia hatua ya kutaka kuchapana kavu kavu nje ya ulingo tena mbele yangu,hata hivyo mzozo huo umekubaliana kumalizika siku ya mpambano wao ambapo atajulikana nani mbabe zaidi ya mwenzake.

Nae bondia Ibrahimu Class aliyeanzisha mzozo huo ameahidi kummaliza mapema mpinzani wake ambapo anatarajia kumchakaza raundi za awali na bondia Simba nae ameahidi kumchapa class kwa K,O.

"Kiukweli kabisa huyo ni kijana mdogo sana na mmemuaisha kwangu sasa siku hiyo mimi nita mpiga K,O mbaya sana najua kuwa kwa Tanzania hii mimi ndie naongoza kuwapiga wapinzani wangu kwa K,O pindi nikutanapo nao ulingoni" alisema Simba.

Mpambano huo unatarajiwa kuwa ni mkali sana na wenye mvuto wa kipekee utakaopigwa August 30 katika ukumbi wa Diamondi Jubilee,jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Lindi afungua warsha ya wadau wa Shirika la Mpingo

0
0
Mkuu wa mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila akifungua warsha ya wadau wa Shirika la Mpingo iliyofanyika katika ukumbi wa PEC(Kwa Sultan).Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Mpingo,Felician Kilahama na Mkurugenzi wa MCDI,Gasper Makala.
Mwenyekiti wa Bodi ya shirika la Mpingo,Felician Kilahama akiongea na wadau wa shirika hilo kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa wa lindi kufungua warsha hiyo,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa lindi,mkuu wa wilaya ya kilwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya kilwa ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa,Ally Mohamed Mtopa
Wajumbe wa bodi na wadau wa shirika la Mpingo wakiwa katika warsha hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Lindi akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa shirika la Mpingo waliohudhuria warsha ya wadau wa Shirika hilo iliyofanyika wilayani kilwa.

Na Abdulaziz Video,kilwa

Mkuu wa mkoa Lindi Ludovick Mwananzilah ameiomba serikali kupitia wizara ya nishati na madini kupunguza bei ya bidhaa na vifaa vinavyo tumia mafuta na gesi ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya kuni na mkaa.

Ombi hilo amelitolewa kwenye warsha shirikishi ya wadau wa shirika la kuhifadhi mipingo na maendeleo(MCDI) iliyoshirikisha wilaya za Kilwa, Nachingwea na Rufiji iliyofanyika kwenye ukumbi PEC wilayani Kilwa.

Mwanazilah alisema kuharibifu wa mazingira unatokana na kukatwa kwa miti kwa matumizi ya kuni na mkaa yamekuwa makubwa kutokana na kipato cha wananchi kuwa kidogo ambacho hakiwezi kukidhi kununua mafuta na gasi.

Alisema kutokana na hali hiyo ni vyema wizara kwa kushirikiana na wadau wengine wa mazingira kuhakikisha kuwa bei ya vifaa za gasi iliyoanza kuzalishwa wilayani Kilwa mkoani Lindi vinapunguzwa bei ili kuwafanya wananchi wengi wenye kipato kidogo wanaweza kumudu kupata gas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kupunguza matumizi ya mkaa na kuni kwa lengo la kuhifadhi mazingira.

“Ndugu wana warsha, leo hii tumepata fursa ya kukutana na kujadiliana juu ya suala zima la Utunzaji Misitu kiendelevu, Lengo la Warsha hii ni kujadili kwa kina na kukubaliana ni jinsi gani Shirika la MCDI liendelee kuziwezesha jamii katika kusimamia Misitu ya vijiji kwa uendelevu ili Misitu iendelee kuchangia katika kuboresha maisha ya wananchi wetu” alisema mkuu huyo wa mkoa.

Alisema ni jambo jema sana kwani Misitu yetu ipo hatarini kuangamia iwapo haitasimamiwa vizuri na kwa uendelevu. Misitu yetu inakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo kilimo cha kuhamahama na uchomaji moto Misitu.

Mkuu wa mkoa huyo alichukua nafsi hiyo washiriki wote tuzingatie Usimamizi Bora wa Mazingira na hususani Misitu ili isipotee na tuendelee kunufaika na manufaa yatokanayo na rasilimali za Misitu ikiwa ni pamoja na mbao, asali na uuzaji wa hewa ya ukaa. (Carbon).

WERUWERU GOLDEN JUBILLEE 1963 - 2013

0
0
WERUWERU FIFTY YEARS ANNIVERSARY STEERING COMMITTEE CALLINGALL ASSUMPTA/WERUWERUALUMNI TO PARTICIPATE IN THE PREPARATIONS AND CELEBRATIONSOFTHEGOLDENJUBILEEATWERUWERUSEPTMEBR21ST 2013.TO REGISTER AND PLEDGE PLEASE VISIT www.weruweru.mediart.co.tz.

IT’S TIME TO GIVE BACK TO YOURALMAMATER.PLEASE BE INFOMREDTHAT THE NEXTALUMNIMEETINGISSCHEDULEDFORAUGUST25TH2013AT3PM AT THECINECLUB.PLEASE OBSERVE TIME! LETS PLAY OUR PART IT CANBE DONE.

Kilimanjaro Premium Lager yawapa raha Simba SC

0
0
WADHAMINI wakuu wa klabu ya Simba, Bia ya Kilimanjaro, wanatarajia kufanya mambo makubwa zaidi kwa timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania, imefahamika.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati wa semina maalumu iliyoandaliwa na wadhamini hao kwa ajili ya wachezaji, viongozi na benchi la ufundi la Simba iliyofanyika katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini.

“Kila mwaka Kilimanjaro Premium Lager imekuwa ikiongeza thamani ya udhamini wake tangu tulipoanza mwaka 2008. Mwaka huu pia tutaleta kitu kingine kipya ambacho tutakitangaza wakati ukifika. Lengo ni kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika na udhamini huu,” alisema Kavishe. Kavishe aliongeza kuwa semina hiyo ilikuwa na lengo kuelezana masuala mbalimbali yanayohusiana na udhamini na jinsi ambavyo Simba SC na Kilimanjaro Premium Lager zinanufaika kutokana na udhamini huo na kuainisha maeneo ya kuboresha.

Kwa sasa, bia ya Kilimanjaro Premium Lager hutumia takribani Sh. Milioni 495 kwa ajili ya udhamini wake kwa klabu ya Simba kila mwaka, fedha ambazo hutumika kwa ajili ya ulipaji wa mishahara ya wachezaji, ukarabati wa majengo, kugharamia Mkutano Mkuu wa Wanachama, vifaa vya timu pamoja na tamasha Siku ya Simba.

Akizungumza katika mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are, alisema semina hiyo imewafumbua macho viongozi na wachezaji katika masuala mbalimbali na kwamba kuanzia msimu ujao, klabu itajitahidi kufanya vizuri zaidi katika eneo la mahusiano bora na wadhamini pamoja na wadau wa klabu ya Simba.

Kwa upande wa wachezaji, Ramadhani Chomboh (Redondo), alisema semina hiyo imekuja katika wakati mwafaka kwa vile katika soka la sasa, udhamini na hadhi na maslahi ya wachezaji ni mambo yanayokwenda sambamba.

Kilimanjaro Premium Lager imefanya semina hiyo kwa klabu ya Simba ili kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya mdhamini huyo na klabu na vile vile kuboresha. 

Viongozi wa klabu ya Simba pamoja na benchi la ufundi na wachezaji ambao wengi ni wapya pia walitumia fursa hiyo kuweza kukaa pamoja katika mazingira mwanana na tulivu kwenye hoteli hiyo ya kitalii huku wakishiriki michezo mbalimbali ya kujifurahisha ikiwemo mpira wa kikono, kuogelea na mingine kwa siku nzima. Wadhamini hao wamepanga kufanya semina nyingine kama hiyo kwa ajili ya mabingwa wa ligi kuu, Young Africans SC siku zijazo.

RAIS SHEIN WA ZANZIBAR AFUNGUA MKUTANO MKUU WA JUMUIYA YA MAHAKIMU NA MAJAJI AFRIKA MASHARIKI

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua Mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki,(EAMJA) ulioanza leo katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Jumuiya ya (ZAJOA) Zanzibar Jaji Abraham Mwampashi,akitoa hutuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki,(EAMJA) unaoendelea kwa siku tatu katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel,iliyopo nje ya Mji wa Unguja.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki,(EAMJA) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipokuwa akiufungua Mkutano huo wa siku tanu leo katika Ukumbi wa Hoteliya Zanzibar Beach Resort iliyopo nje ya Mji wa Unguja.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Mahakimu na Majaji wa Afrika Mashariki,(EAMJA) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipokuwa akiufungua Mkutano huo wa siku tanu leo katika Ukumbi wa Hoteliya Zanzibar Beach Resort iliyopo nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) pamoja na Majaji wa Nchi za Afrika Mshariki, wakisimama wakati wimbo wa Taifa wa Nchi hizo ukipigwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka kwa Nchi hizo,ambao utakchukua siku tatu katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Hotel,iliyopo nje ya Mji wa Unguja.

TAARIFA TOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO

CCM Mkoa wa Kagera kimetimua madiwani wake wanane

0
0
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera, leo kimewafukuza madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kupitia chama hicho na kufutwa nyadhifa zao za udiwani kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea



Waliofukuzwa ni:

  1. Richard Gaspar (Miembeni )

  2. Murungi Kichwabuta (Viti maalum)

  3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

  4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

  5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

  6. Robert Katunzi (Hamugembe)

  7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

  8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo)

MKUU WA MKOA WA RUKWA AWAPELEKA WATAALAM WA MAJENZI KUTOKA CHUO KIKUU CHA MUST KWA AJILI YA KUANDAA MICHORO YA MAJENZI YA UWEKEZAJI WA KITALII KATIKA ENEO LA MAPOROMOKO YA MTO KALAMBO

0
0
 Njia panda kuelekea Kalambo Falls. Maporomoko hayo yanayopatikana Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo ni pili kwa ukubwa barani afrika yakiwa na urefu wa mita 235.  Maporomoko hayo yapo mpakani na nchi jirani ya Zambia.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa baadhi ya maelekezo kwa wataalam hao wa majenzi kutoka MUST na wale wa ardhi kutoka Halamashauri ya Wilaya ya Kalambo juu ya mpango wa majenzi wa eneo hilo la kitalii hivi karibuni. Mpango huo ni pamoja na kujenga geti la kukusanyia ushuru, eneo la mahoteli, na huduma nyingine muhimu.
 Wataalamu wa majenzi kutoka chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), kushoto Omary Mwenunge na Mark Nassary wakiwa kazini kupata taswira ya maeneo hayo na kuyafanyia kazi ikiwa ni kuweka michoro ya huduma mbalimbali zitakazokuwa zinapatikana katika eneo hilo la kitalii Mkoani Rukwa.
 Wataalam hao wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya hivi karibuni walipotembelea eneo hilo. Nyuma yao ni Maporomoko ya Mto Kalambo yenye urefu wa mita 235.
 Wataalam hao kutoka MUST wakistaajabu maporomoko ya mto Kalambo.
Sehemu ya maangukio ya mto kalambo
Sehemu ya mapitio ya mto kalambo baada ya kupita kwenye maporomoko.
Picha ya maporomoko hayo ikionekana kwa urefu yakiwa na mita 235  (kutoka juu hadi chini)(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa "rukwareview.blogspot.com")

MASHINDANO YA MIJADALA YA SHULE ZA SEKONDARI MWANZA KUANZA SEPT. 2

0
0
Mkurugenzi wa Stopper Entertainment, Mukhsin Mambo,(katikati) akifafanua jambo kuhusiana na Mashindano ya Shule za Sekondari(Interschools Debate Compatations) katika Semina iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa JB. Bellemonte Hoteli, iliyopo jijini Mwanza. kulia Meneja Mipango, Aisha Eddy na Mratibu wa Mashindano Baraka Samson.
Mkurugenzi wa Stopper Entertainment, Mukhsin Mambo, akitoa mafunzo kwa walimu wa Shule za Sekondari za Mkoa wa Mwanza kuhusiana na Mashindano ya Shule za Sekondari(Interschools Debate Compatations), semina iliyofanyika katika ukumbi wa JB.Bellemonte Hoteli.

===============================
Mashindano ya Mijadala kwa shule za sekondari mkoani Mwanza (Interschools Debate Competition), yanatarajiwa kuanza septemba 02 mwaka huu.

Akizungumza katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala kutoka katika shule mbalimbali za sekondari mkoani Mwanza, mkurugenzi wa Stoppers Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, Bwana Mukhsin Mambo, amesema jumla ya shule 32 kutoka mkoani Mwanza, zitashiriki katika shindano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani humo na Tanzania kwa ujumla.

Mambo, amesema shindano hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika kujieleza mbele ya jamii.

Amesema nia na madhumuni ya shjindano hilo, mbali na kuondoka na kitita cha zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.

Miongoni mwa shule zitakazoshiriki shindano hilo ni pamojana Nsumba sekondari, Nganza Sekondari, Butimba sekondari, St. Joseph Girls Sekondari, Buswelu Sekondari, New Hellen Sekondari, Hill crest Sekondari, Bismark Sekondari.

Rais Kikwete akutana na Vijana walioacha kutumia madawa ya Kulevya Ikulu jijini Dar leo

0
0
Kijana Jimmy Changchuu alieachana na matumizi ya dawa za kulevya akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete picha aliyochora yeye na kijana mwenzake wakati vijana hao walimpomtembelea Rais Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Vijana hao wanalelewa katika kituo cha Pilli Missanah Foundation kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Vijana walioachana na Matumizi ya dawa za kulevya kutoka katika kituo cha Pilli Missanah Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia pembeni ya Rais ni Mwanzilish Kituo hicho Bi.Pilli Missanah na watatu kushoto ni mfadhili mkuu wa kituo hicho Bwana Zacharia Hans Poppe(picha na Freddy Maro).

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameiagiza Wizara  ya Afya kupitia kitengo cha magonjwa ya akili  pamoja na Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini kushirikiana na Kituo cha Ushauri Nasaha cha Pili Misana Foundation, ambacho kinawasaidia  waathirika wa  madawa ya kulevya ili kiweze kuwahudumia watu wengi zaidi hapa nchini.

Rais Kikwete amesema hayo leo Ikulu alipokutana na  vijana walioachana na matumizi ya dawa za kulevya ambao wamepata ushauri nasaha na usaidizi kutoka katika kituo cha Pili Misana kilichopo  Kigamboni jijini Dar es Salaam.“Jamii lazima ishiriki katika utatuzi wa jambo hili, ni tatizo kubwa na linamgusa kila mtu na inabidi wote tushiriki katika kulipiga vita” Mhe. Rais amesema na kumpongeza Bi. Pili Misana na 

Zacharia Hans Pope ambaye ndiye mfadhili wa kituo hicho ambacho  tayari vijana wapatao 203 wamepatiwa huduma ya ushauri nasaha na kuweza kuachana na madawa ya kulevya na kurudia katika shughuli zao za kimaendeleo.

Rais Kikwete amesema tatizo la madawa ya kulevya ni la muda mrefu lakini hapo awali lilikuwa halisikiki sana kwa sababu jitihada za kuzuia madawa hayo zilikua hazitangazwi wala kufuatiliwa sana.

“Sasa hivi juhudi mbalimbali za kupambana na madawa ya kulevya zinatangazwa na hivyo kusikika sana na pia taarifa nyingi zinazohusiana na madawa ya kulevya zinawekwa wazi kwa jamii” Mhe. Rais amesema, na kueleza kuwa taarifa nyingi zinawekwa wazi na kutangazwa ili kushirikisha jamii katika kupambana na tatizo hili.

Kiasi cha vijana 35 leo wamefika Ikulu ambapo wametoka katika nyanja mbalimbali za kitaaluma, elimu na kijamii na pia umri tofauti kutoka miaka 14 hadi miaka 53. Kituo hicho kinahudumia watu wenye jinsia tofauti wake kwa waume kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Rais Kikwete amesema Serikali inafanya jitihada kubwa sana za kuwasaidia vijana mbalimbali na bado itaendelea kutoa msaada huo, huku juhudi mbalimbali za kupambana na madawa hayo zikiendelea.

Naye mfadhili wa kituo hicho Bw. Zacharia Hans Pope ameitaka jamii kushiriki na kuwa karibu zaidi na vijana ili kuweza kusaidia katika mapambano ya madawa ya kulevya na athari zake nchini.

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwadishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu Dar-es-Salaam, Tanzania. 
13 August, 2013



MEYA WA ILALA AKABIDHI MSAADA WA TAA ZA THEATER HOSPITALI YA AMANA ZENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI SITA

0
0
20130812_122149_resized
Mstahiki Meya Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa hospitali ya Amana na wafanyakazi wake wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa taa za chumba cha upasuaji katika hospitali hiyo inayohudumia wakazi wa Manispaa ya Ilala yenye kadirio la wakazi 1,179,992sqkm ambapo pia Hospitali ya Amana hutoa huduma kwa wakazi wa Manispaa zingine na hata Mikoa ya Jirani.
20130812_122751_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi rasmi msaada wa taa hizo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk.Meshack Shimwela kwenye hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo.
20130812_122844_resized
20130812_123726_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa akiongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk.Meshack Shimwela (kulia) kuelekea kukagua chumba cha upasuaji katika hopspitali hiyo.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa kupitia wadau wake ametoa msaada wa taa hizo zenye thamani ya shilingi Millioni sita laki saba na tisini elfu 6,790,000/= ambapo msaada huu wa taa umefika kwa wakati muafaka utakaowawezesha madaktari kuwahudumia wagonjwa wengi na kupunguza msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ambao kwa hakika walilazimika kufanya pasuaji muda wa mchana peke yake hali ambayo ilisababisha msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo.

Kwa upande wa huduma ya upasuaji hospitali ya Amana inahudumia wagonjwa kati ya 20 mpaka 30 kwa siku kwa kutumia theater mbili ambazo ni main theater na maternity theater zenye vyumba vinne vya upasuaji (theater rooms). Kwa muda mrefu Hospitali hiyo ilikuwa inakabiliwa na tatizo la kuharibika kwa taa ya upasuaji (operating lamp) ambayo imepelekea kutumia vyumba vitatu vilivyopo theater kubwa (Main theater).

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHIWA KATIBA NA VIONGOZI WA SHIMUTA IKULU DAR LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Nyaraka za Katiba ya Shirikisho hilo, kutoka kwa Mwenyekiti wake, Khamis Mkanachi, wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salam, leo Agosti 13, 2013 kwa ajili ya mazungumzo. Katikati ni Naibu Katibu wa Makamu wa Rais Mohamed Khamis.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa Shirikisho, wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salam, leo Agosti 13, 2013 kwa ajili ya mazungumzo na kumkabidhi Katiba ya Shirikisho hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mlezi wa Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania, (SHIMUTA) Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirikisho hilo baada ya maongezi yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Picha na OMR

mazishi ya marehemu erasto msuya mfanyabiashara aliyepigwa risasi majiuzi jijini arusha

0
0

Heshima za mwisho kwa mwili wa Maremu Erasto Msuya.


 Nyumba ya milele ya marehemu Erasto Msuya ikiandaliwa.

Ni siku takribani sita zimepita tangu mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliyefahamika kwa jina la Erasto Msuya kupigwa risasi na kufariki dunia papo hapo katika eneo la Bomang'ombe karibu na njia panda ya KIA (Kilimanjaro International Airport), leo ni siku ya mazishi ya mfanyabiashara huyo ambaye alikua akiishi jijini Arusha maeneo ya kwa Iddi. Jana jumatatu utaratibu wa kuuaga mwili wa marehemu nyumbani kwake ulifanyika na leo Jumanne umepelekwa kuzikwa huko Mirerani katika kijiji cha Kairo.

wanted: chinese language courses

0
0
Dear Mr. Michuzi,
 
I am looking for a Chinese Language Centre in Dar es Salaam where  Chinese Language courses are  offered. Kindly advice if you or any mdau know or have heard of such place.
 
Thanks and Kind Regards,
M

Acid Attack on Two British Girls in Zanzibar: Statement by the British High Commissioner

0
0
The British High Commissioner, Dianna Melrose, commented today on the acid attack in Stone Town, Zanzibar on 7th August which left two British nationals injured. Speaking following the incident, she said:

“It was a shocking attack and our thoughts and sympathy go out to the young women and their families. We wish them a speedy recovery and will continue to do all we can to support them.

I would like to thank the Governments of Tanzania and Zanzibar for their public condemnation of the attack and their stated determination to leave no stone unturned in finding the perpetrators, and ensuring they are brought to justice. This will reassure British tourists planning to travel to the island.
Pending police investigations, it would be unwise to leap to conclusions about the motive for the attack or what it means for foreign visitors. Nevertheless, we have updated our Travel Advice to inform people of the attack and reiterate the need for caution”.

The British High Commission provided consular assistance to the girls and their families, including facilitating the victims’ flight from Zanzibar to Dar es Salaam, supporting them while in hospital in Dar Es Salaam and liaising with the insurance company over their medical evacuation.
Zanzibar remains a popular tourist destination and most visits are trouble free. 
British nationals are however encouraged to take care and to read our Travel Advice at: www.gov.uk/foreign-travel-advice/tanzania”

Viewing all 109594 articles
Browse latest View live




Latest Images