Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA VODACOM KUWAWEKA PAMOJA WATEJA WAKE KUPITIA HUDUMA YA IFLIX

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Vodacom imeamua kuwaweka pamoja wateja wake zaidi ya milioni 12 kupitia huduma ya Iflix.

Ambapo Vodacom imeingia mkataba na kampuni ya Iflix inayotoa huduma ya burudani katika nchi zinazoendelea ambapo huduma hiyo inawapa wateja wanaotumia mtandao wa Vodacom kuangalia vipindi bora duniani,sinema na vingine vingi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kuingia makubaliano hayo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara Hashim Hendi amesema kampuni yao imedhamiria kuingiza Tanzania katika huduma ya kidigitali hasa kwa wateja wao.

Aidha Hendi amebainisha hata wasanii na waandaaji wa filamu watapata fursa ya kuuza kazi zao katika kampuni hiyo ambapo italeta kipato katika tasnia hiyo inayofanya vema hapa nyumbani na nchi za Afrika Mashariki kwa ujumla.

"Ikiwa imeshasaini zaidi ya kampuni 240 ya usambazaji duniani,Iflix inawapa watazamaji wake chaguo kubwa la vipindi vya Tv vinavyosifika pamoja na sinema zinazopendwa na mashabiki kitaifa ikiambatana na sinema kubwa za Bollywood kama vile Love Shagun,Sharafat Gayi tel lene na nyingine nyingi,"amesema Hendi.

Kwa upande wa Muandaaji wa filamu nchini Rita Paulsen amesema wanayofuraha kwa Iflix kuwatambua waandaaji wa filamu Tanzania na kuongeza hatua hiyo itasaidia kwenda na wakati.

Wakati Muanzilishi wa Iflix Britt amesema anayo furaha ya kuingia ubia na Vodacom kufikisha huduma hiyo nchini Tanzania.

"Tumedhamiria kuwapatia chaguo kubwa kabisa la vipindi vya burudani kwa uhitaji wa matakwa yao wenyewe waweze kutazama au kupakua kwenye kifaa chochote atakachopenda mteja"amesema Britt.

Ili mteja kupata huduma hiyo anatakiwa kupakua App ya Iflix bila malipo,na vifurushi maalum mteja ata bonyeza *149*01# kisha kuchagua intanenti halafu kifurushi ikifuatiwa na Iflix,kifurushi cha siku kwa Sh.1,000,cha wiki 6,500 na cha mwezi 18,000.
 Mkurugenzi kitengo cha biashara Vodacom, Hashim Hendi akizungumza katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam mara baada ya makubaliano hayo kuhusu huduma hiyo ya Iflx inavyoweza kutoa burudani kwa wateja wao.
Mkurugenzi mkuu Inflix Britt akizungumza katika ofisi za makao makuu ya  Vodacom Jijini Dar es salaam namna na jinsi huduma hiyo katika utendaji wake wa kazi kuonyesha filamu mbalimbali pamoja na vipindi vingine vingi hapa duniani
Mwandaaji wa Filamu nchini Rita Poulsen akitoa shukrani kwa Iflix kwa kuweza kuwatambua waandaji wa Filamu Tanzani na kufikisha huduma hiyo katika ofisi za Vodacom Jijini Dar es salaam.

RC MAKONDA AZINDUA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO CHANIKA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
RAIS wa Shirika la Misaada la Korea Kusini (KOICA), Lee Mi Kyung amezindua Hospital ya Mama na Mtoto Chanika iliyojengwa kwa jitihada  za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliyetafuta wafadhili hao.

Ujenzi wa hospital hiyo ya kisasa umegharimu zaidi Sh.billion 9.8 ambapo ndani kuna vyumba vya kisasa vya upasuaji, vyumba vya madaktari, maabara, chumba cha mionzi, wodi ya wazazi,wodi ya watoto njiti na chumba cha operesheni (Theater).

Pia vyumba vya kujifungulia, chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), vyoo vya kisasa pamoja na nyumba za familia 28 za madaktari ambapo ndani ya nyumba hizo kuna huduma zote za muhimu.

RC Makonda amesema aliamua kutafuta wafadhili wa kujenga hospital hiyo baada ya kuona kilio cha kinamama waliokuwa wakipoteza maisha na watoto baada ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya. 

Aidha RC Makonda amemuomba Rais wa KOICA kumjengea hospital nyingine mbili kwenye Wilaya mpya za Ubungo na Kigamboni ili kusaidia maboresho ya huduma za afya. 

Pamoja na hayo Makonda ameshukuru Serikali ya Korea Kusini kwa ufadhili wa hospital hiyo yenye hadhi ya kimataifa.

Kwa upande wa Rais wa KOICA Lee Mi Kyung amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo huku akipongeza Tanzania kwa kudumisha amani tofauti na Mataifa mengine. 

Uzinduzi wa hospitali hiyo umeenda sambamba na uzinduzi wa magari mawili ya kisasa ya kubeba wagonjwa (ambulance).
  Rais wa KOICA bi. Lee kwakushilikiana na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa hospitali ya Mama na Mtoto Chanika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii)
 Rais wa KOICA, Lee Kyung akimkabidhi funguo ya gari la kubeba wagonjwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  jijini Dar es  Salaam.
 Muonekana wa gari la wagonjwa lililokabidhiwa  na Rais wa KOICA 
Rais wa KOICA bi. Lee kyung akisalimiana na baadhi wagonjwa katika hospitali hiyo mara baada ya kuizindua.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Rais wa KOICA bi. Lee Kyung wakiwaaga wananchi walihudhuria uzinduzi wa hospitali hiyo

UFUNGUZI SHEREHE ZA MAONESHO WIKI YA UTAFITI WA SAYANSI YA BAHARI WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Mgeni Rasmi Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Aida Juma akitoa hotuba ya ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa  Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari Chuo Kikuu Dar es salaam Zanzibar Dk. Matern S.P.Mtolera akitoa hotuba ya Makaribisho kwa Mgeni rasmi  katika Ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa  Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Kitengo cha Uratibu wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Aida Juma kushoto akipatiwa maelezo kuhusiana na utafiti wa mwani na Mtafiti wa Mwani Dk. Flower Ezekiel Msuya katika ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika Ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Baadhi ya wanafunzi wa Sayansi  waliohudhuria katika Ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa  Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari Chuo Kikuu Dar es salaam Zanzibar, Dk. Matern S.P. Mtolera akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Sherehe za Nne za Maonesho ya Wiki ya Utafiti wa  Sayansi ya Bahari iliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Bahari Dar es Salaam Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja. Picha Na Yussuf Simai/Maelezo Zanzibar.



SERIKALI YASISITIZA HAKUNA UPOTEVU WA SHILINGI TRILIONI 1.5

$
0
0
Serikali leo imelithibitishia Bunge na umma kwa ujumla kuwa kufuatia maneno ya baadhi ya watu yaliyosheheni upotofu, siasa na yenye nia ya kuchafua taswira ya nchi kwamba kuna Shilingi trilioni 1.5 zimepotea, ukweli ni kwamba hakuna upotevu huo na mchanganuo wa matumizi uko wazi. 

Akitoa taarifa hiyo ya kina Bungeni leo, huku akiainisha mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesisitiza kuwa chini ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, fedha za umma ziko salama na wanaojaribu kufanya ufujaji hatua kali zinachukuliwa. Taarifa kamili yenye aya 12 ni kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 49 ya Kanuni za Bunge Toleo la Januari 2016, naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu Kauli ya Serikali juu ya madai ya kutoonekana kwa matumizi ya shilingi trilioni 1.51 kwenye matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2012/13 hadi 2016/17, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ilikuwa kwenye kipindi cha mpito cha miaka mitano ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kuandaa hesabu za Serikali kwa kutumia mfumo wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma (International Public-Sector Accounting Standards – IPSAS Accrual). 

Katika kipindi hicho, Serikali iliendelea kukusanya taarifa mbalimbali kwa kutumia mfumo huu ili kutuwezesha kutambua kikamilifu hesabu za mali, madeni pamoja na mapato yanayotokana na kodi. “IPSAS Accrual” ni mfumo wa kiuhasibu ambapo mapato yanatambuliwa baada ya muamala husika kukamilika na sio wakati fedha taslimu inapopokelewa; na matumizi yanatambuliwa wakati muamala wa matumizi umekamilika na sio wakati fedha inalipwa. Mfumo huu ni mzuri na una faida nyingi ikiwa ni pamoja na miamala ya Mapato na Matumizi kutambuliwa wakati husika na siyo wakati wa fedha taslimu inapopokelewa au kulipwa. 


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa ya Serikali kuhusu hoja ya kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali shilingi trilioni 1.51 leo Bungeni mjini Dodoma. 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa kila kipande cha ardhi hapa nchini kinapimwa ili kuchochea maendeleo wakati wa kipindi  cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. 

Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kagera Mhe. Oliver Semuguruka akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kuhusu maboresho yanayopaswa kufanywa katika sekta ya afya ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi katika Mkoa wa Kagera na katika hosipitali zote za umma. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akisisitiza kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi kuendelea kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao kote nchini leo Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akijibu miongozo ya wabunge mapema leo Bungeni mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Sehemu ya wageni waliofika Bungeni kwa ziara ya mafunzo wakifutilia kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. 

WIZARA YAAMSHA ARI YA WANANCHI KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0
Wizara ya Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kuendelea na kampeni ya kuamsha ari ya Wananchi kushiriki katika Miradi ya Maendeleo na katika kipindi cha Julai 2017 hadi Machi 2018, Wizara imefanya uhamasishaji katika Mikoa 11 ya Iringa, Dodoma, Mwanza, Pwani, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Kagera na Shinyanga.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2017/2018 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Bungeni Mjini Dodoma.

Waziri Ummy ameeleza kuwa uhamasishaji huu umewezesha ujenzi wa majengo ya Kituo cha Afya Mondo, Wilaya ya Misungwi (Mwanza); ujenzi wa bwawa la maji Maghangu Mpwapwa (Dodoma); ujenzi wa Zahanati Ufyambe (Iringa); ujenzi wa shule ya sekondari na kituo cha afya – Uvinza (Kigoma); ujenzi wa shule ya sekondari na kituo cha afya – Mpanda (Katavi); ujenzi wa kituo cha afya –  Sumbawanga (Rukwa); ujenzi wa kituo cha afya – Mbozi (Songwe); ujenzi wa shule ya sekondari – Manispaa ya Mbeya (Mbeya).

Pia amesema kuwa Kampeni hii ya Kuamsha Ari ya Wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo imesaidia  kuchangia fedha na vifaa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Makazi ya wazee (Kagera); kuzindua Kituo cha Mkono kwa Mkono (One Stop Centre) cha wahanga wa ukatili wa kijinsia na ukatili wa watoto Wilaya ya Kahama (Shinyanga) na ujenzi wa madarasa mawili katika Kijiji cha Chambasi, Kisarawe (Pwani).

Aidha Mhe. Ummy Mwalimu ameongeza kuwa Wizara imeendelea kushirikiana na Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kutekelza miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa Huduma kwa jamii na kwa kipindi cha kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Machi, 2018, jumla ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali192 yalisajiliwa.

Mhe.Ummy Mwalimu alisema pia imeongeza Ustawi wa watoto wazee na jamii nchini kwa kushirikiana na wadau imeendelea kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017/18 – 2021/22). Katika mwaka 2017/18, Kazi zilizofanyika chini ya mpango huu ni kutoa elimu kuhusu athari za mila na desturi zenye madhara kwa jamii ikiwemo ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni kwa makundi mbalimbali katika jamii.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge waliochangia Hotuba wameipongeza Wizara kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa huduma kwa wananchi.

Naye Mwanyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Mandeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba ameiomba Wizara kuajiri Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini ili kuondokana na upungufu uliopo kwani Maafisa hawa ni watu muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Zanzibar Mhe. Najma Giga amesema kuwa Wizara inatakiwa kukaa na wadau ili kupata namna bora ya kutokomeza tatizo la ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwani limekuwa ni tatizo linalosumbua katika sehemu nyingi hapa nchini.

“Naomba suala hili la Ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto tuondokane nalo maana tatizo hilo linalowakumba na kuwasababishia ukatili mkubwa watoto na wanawake wenzetu” alisisitiza Mhe. Najma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasilisha Utekelezaji wa Bajeti ya kwa Mwakawa fedha  2017/2018 na makadirio ya mapato na matumizi kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 Bungeni Mjini Dodoma.

Waziri Ummy Mwalimu kuzindua maadhimisho siku ya Malaria Duniani ,Kasulu mkoani Kigoma

$
0
0
Tanzania inatarajia kuungana na nchi zingine duniani kwenye kuadhimisha siku ya Malaria Duniani ambayo ufanyika April 25 kila mwaka.

Maadhimisho hayo ya kitaifa yatafanyika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma huku Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii akitarajiwa kuzindua ripoti ya hali ya Malaria nchini.

Akiongea jijini Dar es Salaam leo, Waziri Nyoni ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi kutoka VectorWorks alisema kutakuwa na shamra shamra mbali mbali kuanzia tarehe 22 April kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho hayo.

VectorWorks ni mradi wa miaka mitano wa kupamba na malaria hapa nchini umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na John Hopkins Center for Communications.

‘Sisi kazi yetu ni kuhakikisha hali ya ugonjwa wa malaria inapungua. Kwa sababu hiyo, tumekuwa na zoezi endelevu la kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa kila kaya hapa nchini. Vile vile, tunatumia vituo vya afya kuwafikia walengwa wakuu ambao ni akinamama waoenda kliniki na watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja, alisema Nyoni.

Akina mama wanaonza kliniki ni lazima wapatiwe chandarua chenye dawa ya muda mrefu bure. Hii njia bora ya kujikinga na mbu waenezao malaria. Vile vile tunafanya kazi kwa kushirikiani na Serikali kupitia Wizara ya Afya kitengo cha kupamba na Malaria nchini ambao wamekuwa wakipuliza dawa yenye viatilifu kwenye maeneo yenye masalia ya mbu. 

Tumepiga hatua kubwa kupunguza malaria hapa Tanzania kwa hivyo natoa wito wangu kwa kila Mtanzania kuhakikisha analala kwenye chandarua kwenye dawa ya muda mrefu, aliongeza Nyoni.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni mimi natokomeza malaria, wewe je?

Wasanii Nchini Waaswa Kuenzi Busara za Wazee

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Wasanii wa filamu nchi washauri kuheshimu na kutahmini mawazo na busara za wazee pindi wanapopata wasaa wa kukutana nao.

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo alipokaribishwa kutoa neno wakati wa tukio fupi la Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherryl ‘‘Monalisa” kutoa shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania.

Fissoo alisema kuwa imekuwa ni desturi kwa baadhi ya vijana kuchukulia ushauri au mawazo yanayotolewa na wazee au watu wa makamu kuwa umepitwa na wakati hivyo hautakuwa na manufaa kwao.

“Nikuombe mwanangu Monalisa nenda ukawe balozi mwema, waanbie wenzako waenzi na kuheshimu busara za wazee, naamini kwa kufanya hivyo mtayaona mafanikio ya kazi zenu,”

Aidha mama Fissoo ameongeza kuwa Monalisa amekuwa msanii wa mfano wa kuigwa hasa katika nyanja ya maadili kitu ambacho wasanii wengi wanapaswa kuzingatia .
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bi. Joyce Fissoo akizungumza alipokuwa ameambatana na Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa kwa ajili ya kutoa shukrani kwa wajumbe wa kamati ya tamasha la muziki na sanaa za maonesho jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea nchini na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika. 
Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa kamati ya tamasha la muziki na sanaa za maonesho jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika.  Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania, Faza Lusozi Paul na kulia ni mama mzazi wa Monalisa, Bibi. Suzan Lewis.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania, Faza Lusozi Paul akizungumza jambo mara baada ya Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa (wapili kulia) kutoa neno la shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika. Wakwanza kulia ni mama mzai wa Monalisa, Bibi. Suzan Lewis.
Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za dansi nchini, Mzee King Kikii akitoa nasaha kwa Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa (hayupo pichani) mara baada ya msanii huyo kutoa neno la shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Shukrani hizo zimetokana na wajumbe hao kumpa maneno ya kheri na busara msanii huyo hatimaye kurejea na ushindi wa nafasi Msanii Bora wa Kike Afrika. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (KBF), Bi. Joyce Fissoo.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bibi. Joyce Fissoo (waliokaa kushoto) na Msanii wa Bongo Movie Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa(wanne kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Tamasha la Muziki na Sanaa za Maonesho Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UONGOZI WA IFM WAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO MKUU WA MKOA WA DODOMA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akifanya mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),  Prof.Tadeo Satta(kulia) ofisini kwake Dodoma katikati ni Dkt. Kadida Masha

BALOZI SEIF AKUTANA NA UONGOZI WA TAASISI YA FAWE

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Taasisi za Kiraia katika kuona malengo na dhamira zilizojipangia katika kuwahudumia Wananchi zinafanikiwa vyema.

Alisema Taasisi nyingi za Kiraia zilizoanzishwa Nchini zimeonyesha mwanga wa matumaini katika kusaidia huduma za Kijamii hasa kwenye Sekta na miradi ya Elimu jambo ambalo Serikali inastahiki kujivunia na kuendelea kuzipa ushirikiano huo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Uongozi wa Taasisi ya Kiraia ya kumjengea uwezo wa Kielimu Mtoto wa Kike na Mwanamke ya Forum for African women Educationalist {FAWE} hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema kundi kubwa la Wanawake hivi sasa tayari limeshaamka katika kufukuzia maendeleo hasa katika masuala ya Kielimu kupitia Taasisi za Kiraia jambo ambalo limewapa nafasi ya kushiriki katika makundi mbali mbali ya maamuzi katika maeneo yao.

“ Kazi kubwa iliyofanywa na FAWE imewezesha kutoa msukumo kwa kundi kubwa la wanawake kuamka katika kufukuzia maendeleo”. Alisema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Alieleza kwamba Historia inaonyesha wazi jinsi gani Mwanamke alivyokuwa akikosa fursa kwa Karne nyingi zilizopita kutokana na mfumo dume uliokuwa ukitumika kuwanyima haki zao hasa katika fursa za Uongozi na Maamuzi ya msingi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akizungumza na Uongozi wa Taasisi ya Kiraia ya kumjengea uwezo wa Kielimu Mtoto wa Kike na Mwanamke ya Forum for African women Educationalist {FAWE} hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mratibu wa FAWE Bibi Hinda Abdullah Ajmin na wa kwanza kutoka Kulia ni Mshika Fedha wa FAWE Bibi Sabra Issa Mohammed.
Mratibu wa Fawe Bibi Hinda Abdullah Ajmin Kushoto akimfafanulia Balozi Seif Miradi mbali mbali iliyoanzishwa na Taasisi hiyo ambayo tayari imeshamsaidia Mtoto wa Kike kujikomboa Kielimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alizungumza na Viongozi wa Dini pamoja na wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto kujadiliana Wimbi la vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia na kuangalia Mikakati ya kupambana na janga hilo. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAFURIKO JANGWANI KUPATIWA UFUMBUZI

$
0
0
Na. WFM- Washington D.C
Benki ya Dunia (WB) imekubali kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na athari za mafuriko zinazosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha kila mwaka katika Jiji la Dar es Salaam na kuleta madhara makubwa hususan katika eneo la Jangwani jijini humo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wakati akizungumza na ujumbe wa Benki ya Dunia ulioongozwa na Mkurugenzi wa Benki hiyo kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird, katika mikutano ya kipupwe inayoendelea mjini Washngton DC.

Dkt. Mpango amesema kuwa Benki ya Dunia imekubali kusaidia kukabiliana na mafuriko katika bonde la mto Msimbazi hasa katika eneo la  kutoka Magomeni Mapipa kwenda Faya  na tayari Benki hiyo imeanza  zoezi la kutafiti eneo la Jangwani ili kuweza kuangalia namna nzuri ya kugharamia uboreshaji wa  mifereji katika bonde la mto Msimbazi ili kumaliza kero hiyo kwa wananchi wa Dar es Salaam.

“Tumewaeleza Benki ya Dunia  changamoto hii ambayo imekuwa inajirudia kila mara na kusababisha upotevu wa maisha ya watu, kusababisha kufungwa kwa barabara , watu kushindwa kwenda kazini na wanafunzi kushindwa kwenda shule, hivyo wameonesha nia ya kumaliza kero hii kwa wananchi “ Alisema Dkt. Mpango.

Amesema kuwa baada ya timu ya Benki ya Dunia kumaliza kufanya kazi yao kwa kushirikiana na Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, Serikali inaamini njia ya kudumu itapatikana na kuondokana na tatizo hilo la mafuriko ya mara kwa mara katika eneo la Jangwani
 Baadhi ya Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wakiwa kwenye majadiliano ya pamoja ambapo walizungumzia vipaumbele vinne, ikiwemo kuendeleza sekta ya viwanda pamoja na kukuza umoja wa kikanda katika sekta ya fedha na uwekezaji, mjini Washington DC Marekani.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akisikiliza majadiliano katika mkutano wa SADC, ambapo alishauri katika utaratibu wa uandaaji wa bajeti ni vyema Mawaziri wa Fedha wakashirikishwa. Kushoto kwake ni Gavava wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, mjini Washington DC Marekani.
 Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini majadiliano kati yake na Benki ya Dunia ya namna yakumaliza tatizo la mafuriko eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Bw. Khamis Mussa Omar na wa kwanza kulia kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na wa pili kulia kwake ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere mjini, Washington DC Marekani.
Ujumbe wa Benki ya Dunia ukiongozwa na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Somalia, Burundi na Malawi Bi. Bella Bird. (upande wa kulia mwenye scarf shingoni) wakijadiliana na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) namna ya kutatua changamoto za mafuriko eneo la Jangwani, mjini Washington DC  Marekani.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

BENKI YA KILIMO TANZANIA KUFUNGUA OFISI ZA KIKANDA KWA AWAMU

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inatekeleza Mpango wa Miaka Mitano (2017- 2021), wa kusogeza huduma karibu na wateja kwa kuanzisha ofisi za Kikanda katika Kanda ya Kaskazini, Kusini, Kati, Ziwa, Nyanda za Juu Kusini na Zanzibar kwa awamu. 

Hayo yameelezwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu maswali ya msingi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Jacqueline Msongozi (CCM), aliyetaka kujua lini Serikali itapeleka Benki ya Kilimo katika Mkoa wa Ruvuma ili wananchi waweze kukopeshwa.

Aidha, Mhe. Msongozi alitaka kufahamu utayari wa Serikali kupunguza riba ya mikopo wanayokopeshwa Wakulima katika Benki hiyo.

Akijibu maswali hayo, Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa hadi kufikia Juni 30, 2018 Ofisi ya Kanda ya Kati, Dodoma, itakuwa imefunguliwa ambayo pia itakuwa ni Makao Mkauu ya Benki hiyo.

“Baada ya ufunguzi wa ofisi ya Kanda ya Kati kukamilika Benki Itafanya uchambuzi wa fursa zilizopo Kikanda na hivyo kuchukua hatua na taratibu za kufungua ofisi nyingine kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa Benki hiyo inatoa mikopo kwa kutumia mfumo wa makundi, kundi la kwanza wakulima wadogo wadogo kwa riba ya asilimia 8- 12, kundi la pili la miradi mikubwa ya kilimo kwa asilimia 12 – 16 kwa mwaka na kundi la mwisho ni mikopo ya ushirika ambapo riba yake inaendana na hali ya soko la matumizi ya mkopo.

Kuhusu kupunguza riba kwa wakopaji, Dkt. Kijaji alibainisha kuwa majadiliano ya kiwango cha riba yanaweza kufanyika kulingana na historia ya mkopaji.

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI HOJA YA CAG KUHUSU TRILIONI 1.5

HATUA NANE BORA LIGI KUU WANAWAKE KUENDELEA WIKIENDI HII

$
0
0
Agness francis,Blogu ya jamii

LIGI ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite inatarajia kuendelea wikiendi hii katika hatua ya nane bora huku wadhamini wa ligi hiyo wamekabidhi jezi rasmi kwa timi hizo kwa lengo la kuhakikisha wanafanya vizuri ndani ya nje.

Ratiba ya ligi hiyo inaonesha Aprili 21 zitachezwa mechi  tatu na mchezo mmoja utachezwa Jumapili ya Aprili 22 mwaka huu .Pia siku hiyo hiyo katika Uwanja wa Karume Evergreen watakuwa nyumbani dhidi ya Alliance.

Wakati kwenye uwanja wa Mbweni JKT Quenns watakuwa wenyeji wa Simba Queens na Kigoma Sisters ikiwa katika dimba la Tanganyika wakiavaana na Baobab.

Pia mechi nyingine itakuwa kati ya Panama na Mlandizi Queens  itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Samora Iringa.

Akizungumza leo, Meneja Masoko wa Serengeti Anitha Msangi amesema wanaami kuidhamini Ligi Kuu ya Wanawake kwao inadhihirisha namna ambavyo wanachangia kuleta  mafanikio katika mpira wa Wanawake nchini.

"Mashabiki wanayo nafasi kubwa katika maendeleo ya mpira wa Wanawake na niwaombe wajitokeze kuunga mkono Ligi Kuu ya Wanawake" amesema Msangi.

Hata hivyo ligi hiyo ilikuwa imesimama ili kupisha maandalazi ya timu ya Taifa ya Wanawake iliyokuwa na mchezo wa kufuzu fainali za Afrika kwa Wanawake dhidi ya Zambia.

MADAKTARI BINGWA WABAINI WAGONJWA ZAIDI YA 460 WA MOYO SONGWE

$
0
0
Wagonjwa 467 wenye matatizo ya moyo wamebainishwa na kupatiwa huduma ya ushauri na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa waliotoa huduma kwenye kambi maalumu ya siku 4 katika hospitali ya Vwawa-Mbozi Mkoani Songwe.

Timu ya Madaktari Bingwa na wauguzi 5 wameeleza kuwa wagonjwa 18 kati ya hao waliowahudumia wamepewa rufaa ya kufika hospitali za Rufaa kwa ajili ya matibabu Zaidi.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo George Lyego Longopa Kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema wameanza matibabu siku ya Jumanne na kila Daktari amekuwa akiona zaidi ya wagonjwa 60 kutokana na hamasa ya wagonjwa waliojitokeza kupata matibabu ya magonjwa ya moyo.

 “Tumeona wagonjwa wengi na tumeamini kuwa Songwe tatizo la Magonjwa ya moyo bado ni kubwa, wagonjwa wengi wamekutwa na matatizo ya shinikizo la damu, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri pamoja na matatizo ya mishipa ya damu kuziba”, amesema Dkt Longopa.

Afisa Muuguzi Kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Flora Kasembe ameeleza kuwa mtindo wa maisha ya wananchi wa Songwe unaweza kuwa ni chanzo cha magonjwa ya moyo hasa kutokana na uwepo vyakula vingi lakini wananchi hawali mlo kamili.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo George Lyego Longopa Kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete akichukua maelezo ya mgonjwa wa moyo katika hospitali ya Vwawa-Mbozi.
 Afisa Muuguzi Kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Flora Kasembe akimpima shiniko la damu mwandishi wa habari Manuel Kaminyoge katika hospitali ya Vwawa-Mbozi,
 Baadhi ya wagonjwa wakisoma kipeperushi kinachoeleza masuala ya lishe wakati wakisubiri kupata huduma ya madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika hospitali ya Vwawa-Mbozi.

MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA CHOGM 2018

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) ambapo anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mkutano huo ambao Kaulimbiu yake ni “Kuelekea Mustakabali wa Pamoja” unafanyika chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa Theresa May na umefunguliwa na Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza.
Majadiliano ya Mkutano wa CHOGM 2018 yatajikita kwenye maeneo manne makuu ya kipaumbele ambayo yatajadili namna Jumuiya ya Madola inaweza kufikia mustakabali wenye ustawi zaidi; mustakabali endelevu zaidi; mustakabali wenye haki zaidi; na mustakabali wenye usawa zaidi.
Mijadala katika maeneo hayo ya kipaumbele itahusisha masuala mbalimbali ikiwemo, kukuza zaidi biashara na uwekezaji baina ya nchi za Jumuiya ya Madola kwa manufaa ya nchi wanachama na Jumuiya nzima; kukuza na kuendeleza misingi ya demokrasia; ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu pamoja na masuala ya uhalifu wa kimataifa kama vile ugaidi, uhalifu wa kimtandao na usafirishaji wa binadamu. 
Jumuiya ya Madola ilianzishwa mwaka 1949 kupitia Tamko la London ambalo lilikuwa ni matokeo ya Mkutano wa Mawaziri Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola.  Jumuiya ya Madola ina wanachama 53 ambapo kati ya hizo, nchi 19 ni za Afrika, 7 ni kutoka Asia, 13 ni kutoka nchi za Carribean na Mabara ya Amerika, 11 ni kutoka eneo la Pacific na nchi 3 ni kutoka Ulaya. 
Makamu wa Rais pia alishahudhuria mikutano mbali mbali inayoambatana na mkutano huo ukiwemo mkutano wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi pamoja na Mkutano wa Kutokomeza Malaria kabisa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikizungumza kwenye Mkutano wa  Lacanster ambapo Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola wamekutana jijini London, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi mbalimbali wakifuatilia mada kwenye Mkutano wa  Lacanster ambapo Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola wamekutana jijini London, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bi. Theresa May muda mfupi kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano Lacanster ambapo Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola Wanakutana jijini London kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland. Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland muda mfupi kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa Mkutano Lacanster ambapo Wakuu wa Nchi na Serikali za Nchi za Jumuiya ya Madola Wanakutana jijini London kushoto ni Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Theresa May. Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 


RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI KUTOKA UMOJA NA AFRIKA (AU) NA MISRI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa Amani na Usalama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Balozi Smail Chergui Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Kamishna wa Amani na Usalama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Balozi Smail Chergui Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kamishna wa Amani na Usalama wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Balozi Smail Chergui Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Misri ambaye kwasasa ni Mshauri wa Rais wa Misri Injinia Ibrahim Mahlab kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Misri ambaye kwasasa ni Mshauri wa Rais wa Misri Injinia Ibrahim Mahlab kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu wa Misri ambaye kwasasa ni Mshauri wa Rais wa Misri Injinia Ibrahim Mahlab Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Misri ambaye kwasasa ni Mshauri wa Rais wa Misri Injinia Ibrahim Mahlab mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

KIWANDA CHA MAFUTA CHA MURZAH CHATEKETEA KWA MOTO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Sehemu ya Kiwanda cha  Mafuta cha MURZAH kikiteketea kwa moto huku baadhi ya ya Magari ya Askari wa kikosi cha Zima Moto wakijitahidi kuzima moto huo ambao mpaka sasa chanzo chake hakijajulikana.
  Sehemu ya Kiwanda Cha  Mafuta cha MURZAH kikiteketea kwa moto huku baadhi ya ya Magari ya Askari wa kikosi cha Zima Moto wakijitahidi kuzima moto huo ambao mpaka sasa chanzo chake hakijajulikana.
 Askari wa Jeshi la Zima Moto wakijaribu kuudhibiti moto ambao ulikuwa unarukia upande wa pili wa Kiwanda cha Africariers  mara bada sehemu ya Kiwanda cha Mafuta cha Murzah kuteketea kwa moto
Askari wa Zima Moto na baadhi ya wakurugenzi wa Kiwanda Cha Murzah wakiw akatika harakati za kuzima moto huo.--

SIDO YAKABIDHI VYETI VYA KUTAMBUA VIWANDA VIDOGO NA VYA KATI 300 DAR

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIRIKA la kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo(SIDO),limetoa vyeti vya kutambua viwanda vidogo vidogo na vya kati kwa wamiliki na wajasiriamali zaidi ya 300 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tukio la utoaji vyeti hivyo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo aliekabidhi vyeti vya kuwatambua wamiliki na wajasiriamali wa viwanda hivyo ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ambaye alipaswa kuwa mgeni rasmi.

Kabla ya kutolewa kwa vyeti hivyo vya kuvitambua viwanda hivyo vidogo na vya kati kwa Mkoa wa Dar es Salaam imelezwa kuna wajasiriamali 600 na kati yao ndio hao wamepewa vyeti ili kutambua viwanda vyao na mchango wao katika jitihada za kuleta maendeleo kuelekea Serikali ya viwanda nchini.

Akizungumza kwenye tukio hilo lililohudhuria na mamia ya wajasiriamali wa mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Lyaniva amesema SIDO wamefanya tukio la kihistoria kwa kutambua mchango wa wamiliki wa viwanda hivyo na kuongeza Serikali kwa upande wake itazifanyia kazi changamoto za wajasiriamali hao.

"Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye mgeni rasmi kwenye tukio hili na mimi nimemwakilisha kutokana na majukumu aliyonayo, amenituma nifikishe salamu zake kwenu.Kwanza anatoa pongezi na shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa SIDO kwa kuendelea na majukumu yao ya kuwasimamia wajasiriamali wadogo na wakati ili watimize malengo yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lyaniva (mwenye sharti la mikono mirefu),akikata utepe katika mfao wa cheti ikiwa ni kuashiria kuanza kwa tukio la utoaji vyeti vya kutambua viwanda vidog vidogo 300 jijini.Vyeti hivyo vimetolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo(SIDO).
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akisoma maelezo yaliyokuwa kwenye mfano wa cheti ambacho kimeandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo(SIDO) kwa ajili ya kuwakabidhi wamiliki na wajasiriamali ambao wanamiliki viwanda vidogo na vya kati jijini Dar es Salaa.Tukio hilo limefanyika leo.
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikabidhi cheti kilichotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo(SIDO) kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSPF Adam Mayingu(wa kwanza kushoto) kwa niaba ya Mfuko huo leo jijini Dar es Salaam. Pia SIDO imetoa vyeti hivyo kwa wamiliki na wajasiriamali wa viwanda wapatao 300 kati ya wajasiriamali 600 wa mkoa huo wanataotambuliwa na shirika hilo.
Baadhi ya wamiliki na wajasiriamali wa viwanda vidog na vya kati wakiwa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lyaniva kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda wakati wa utoaji vyeti vya kutambua viwandao vidogo na vya kati 300 katika mkoa huo ambavyo vimetolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo(SIDO) leo jijini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania, Bi. Wang Ke, ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa China nchini Tanzania, Bi. Wang Ke, ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembembo, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 20, 2018, kutoka kushoto ni Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa, wa kwanza kulia ni Mbunge wa Mtama, Nape Mnauye na wapili kulia ni Mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hilaly. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Munira Mustafa Khatib, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 20, 2018, kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Eng. Ramo Makani, kwenye jengo la Utawala Bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2018.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NEWZ ALERT AGNESS MASOGANGE AFARIKI DUNIA

$
0
0

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

HATUNAYE TENA!Hiyo ndio kauli unayowez kuielezea baada ya 
kuwepo kwa taarifa za kufariki dunia kwa video queen hot zaidi 
nchini na muigizaji wa filamu Agnes Gerald maarufu Masogange.

Ni ngumu kuamini kama Masogange amefariki dunia lakini huo 
ndio ukweli.Najua itakuchua dakika kadhaa kutafakari kifo cha 
binti huyo mwenye urembo wake na aliyejaaliwa kuwa na mvuto 
kwa mwenye kuona.

Taarifa kuhusu kifo cha Masogange zinaeleza amefariki dunia leo 
Aprili 20 , mwaka huu katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo 
Mwenge Dar es Salaam.Masogange amefariki dunia akiwa bado 
binti mwenye umri mdogo tu hasa kwa kuzingatia amezaliwa 
mwaka 1989.

Hata hivyo haijafahamika sababu za kifo chake zaidi ya kuelezwa tu amefariki baada ya kuugua muda mfupi na kukimbizwa hospitalini hapo ingawa wapo wanaosema kifo chake kimesababishwa na shinikizo la damu.

Aidha Michuzi Blog imeshuhudia Mwili wa Marehemu Agness Masogange ukiondolewa kituo cha Afya cha Dkt Ngoma  na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jioni hii.

Kifo chake ni pigo kwa Watanzaia walio wengi na hasa mashabiki 
wa muziki wa kizazi kipya kwani pamoja na kufanya shughuli zake 
binafsi lakini alipata umaarufu zaidi baada ya kuanza kutumiwa na 
wasanii maarufu katika nyimbo zao.

Ni hivi karibuni tu Masogange alitikisa vyombo vya habari nchini 
baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhukumu kwenda 
jela  miaka miwili au kulipa faini ya Sh.milioni 1.5 baada ya kutiwa 
hatiani kwa makosa mawili la kutumia dawa za kulevya aina ya 
heroine na pili kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

Hata hivyo Masogange katika kipindi chote cha kesi hiyo ya dawa 
za kulevya hakuwahi kukanusha na baada ya kutolewa hukumu 
alilipa faini ya Sh.milioni 1.5 na akatangaza kuwa a furaha ya aina 
yake kwani alikuwa anabanwa na hata alipotaka kusafiri ilikuwa 
lazima apate kibali.

Hatimaye pamoja na Watanzania kumpenda zaidi Muumba wa 
Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo amemuita .Bwana ametoa na 
Bwana ametwaa.Kwake tutarejea.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images