Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

DIAMOND, NANDY WAJUTIA WALICHOWEKA MTANDAONI

$
0
0

*Waahidi kutofanya makosa tena, waomba vijana kuitumia mitandao vizuri


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WASANII wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva Nassib Abdul ' Diamond' na Faustina Charles 'Nandy' kila mmoja ameonekana kujutia kitendo cha kusambaza picha chafu mtandaoni ambazo ni kinyume na maadili ya Mtanzania huku akiwaomba vijana kutoitumia mitandao vibaya.

Diamond na Nandy kila mmoja kwa wakati wake walisambaza picha chafu mtandaoni hali iliyosababisha Serikali kushindwa kuvumilia na hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam liliamua kuwakamata na kisha kuwahoji kabla ya leo kuzungumza na waandishi wa habari wakiwa Mamakala ya Mawasiliano Tanzania(TCRA).

Kwa upande wa Diamond amesema anajua kitendo cha kusambaza video ambayo imekwaza wengi na kwamba tukio hilo sasa limemfundisha kuwa anatakiwa kuwa mtumiaji mzuri wa mtandao na si kuweka picha ambazo hazina maadili ya kitanzania na kuomba vijana wengine kuacha tabia ya aina hiyo.

"Nikiri binafsi ninao mashabiki wengi mtandaoni ambao wanafuatilia kila ninachokifanya na wakati mwingine wanaiga kutoka kwangu.Niwaombe waitumie mitandao ya kijamii vizuri kwani unaweza kufanya jambo kwenye mtandao ukadhani upo kama chumbani kumbe ni tofauti.Mtandao hakuna tofauti na kufanya jambo barabarani kwani kila mtu ataona.
"Kosa la kusambaza picha chafu mtandaoni limenifanya nijifunze mambo mengi tu na TCRA wametueleza madhara yake na kubwa zaidi sheria na kanuni ambazo ni mpya zinazoweza kumbana anayetumia mtandao vibaya,"amesema Diamond.

Amefafanua yeye na wasanii wengine wangi wanayo tabia ya kuamini wanaweza kufanya chochote hasa kinachohusu sanaa ya muziki kumbe haiko hivyo kwani pamoja na kufanya muziki bado Serikali nayo inawajibu wa kusimamia maadili yetu.Amesema anatambua juhudi ambazo zinafanywa na Serikali katika kuhakikisha wasanii wa Tanzania wanapiga hatua na kuwa na maendeleo yanayotokana na kazi yao lakini matendo ambayo baadhi ya wasanii wanafanya yanaweza kukatisha tamaa viongozi wanaopigania maslahi ya wasanii nchini.

"Kikubwa ni vijana kuacha kutumia mitandao vibaya na kwa wasanii lazima tuunge mkono jitihada za Serikali kwa kuwa mabalozi wa kukemea matendo mabaya yanayofanyika mtandaoni,"amesema.Kwa upande wa Nandy ameendelea kuomba radhi kwa kitendo cha picha zake za faragha kusambaa mtandaoni na kusisitiza haikuwa dhamira yake na hivyo anaomba msamaha kwa Watanzania wote na hasa mashabiki wake.

"Naomba radhi kwa kilichotokea na sikuwa na tafuta kiki kama baadhi ya watu wanavyodhani, ni tukio ambalo haikuwa dhamira yangu, hivyo naomba nisamehewe,"amesisitiza Nandy wakati anazungumza akiwa TCRA.

TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kusimamia usafiri wa anga kwa kuzingatia taratibu na kanuni za usafiri huo ili kuweka uwiano wa haki kwa waendeshaji na abiria wanaotumia usafiri huo.

Ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akizindua rasmi Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuwapongeza kwa kuamua kuweka mikakati ya kununua rada nne kwa kutumia fedha za ndani.

“Lazima msimamie kanuni na taratibu zilizopo, wajibu wenu ni kutoa haki kwa watumiaji na abiria kwa usawa, hatutaki kusikia mnakandamiza watumiaji wa usafiri na mkisimamia vizuri eneo hili mtafanya idadi ya watumiaji kuongezeka na makampuni kuendelea kuwekeza zaidi kwenye usafiri” amesisitiza Prof. Mbarawa.

Waziri Prof. Mbarawa amesema yeyote anaevunja taratibu zilizowekwa kwenye usafiri wa anga Mamlaka hiyo ichukue hatua stahiki kulingana na taratibu zilizopo ili usafiri huo uweze kuwa na nidhamu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari wakati akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka hiyo, mjini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Mamlaka hiyo, lililofanyika mjini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari nyaraka mbalimbali mara baada ya kulifungua mjini Dodoma. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) lililofanyika mjini Dodoma. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA VIONGOZI WA CHAMA CHA WANUNUZI WA PAMBA NCHINI,WAKUU WA MIKOA INAYOLIMA PAMBA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Chama Wanunuzi wa Zao la Pamba Tanzania pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma, Mara, Morogoro, Manyara, Mwanza, Singida, Simiyu, Shinyanga na Tabora, Ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma, Aprili 19, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO (IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII)

WASANII DIAMOND,NANDY WAKUTANA TCRA

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI MBADALA BENKI YA DUNIA, KANDA YA AFRIKA

$
0
0
Na. WFM- Washngton DC

Mikutano ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2018 imeanza rasmi mjini Washington D.C. Katika mikutano hiyo kutakuwa na Magavana, Mawaziri wa Fedha, Sekta Binafsi pamoja na Wanataaluma mbalimbali kuweza kujadili hali ya uchumi wa dunia pamoja na kupunguza umasikini.

Katika mikutano hiyo Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe, kuhusu maendeleo ya hali ya uchumi wa Tanzania huku akisisitiza kwamba ni wakati mzuri sasa wa kusemea hali ya uchumi wetu kwa nguvu zote.

Akiendelea kutoa ufafanuzi Dkt Mpango alieleza hatua ambazo Serikali imezifanya ili kuweka mazingira mazuri katika sekta binafsi, na kwamba Serikali imeandaa mpango kazi wa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika Taifa la Tanzania.

Pia Waziri Mpango alielezea miradi mikubwa ambayo nchi imeanza kuitekeleza, ikiwamo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa na Ujenzi wa Bwawa kubwa la kuzalisha Umeme wa Megawati 2100 la ‘Steigler’s Gorge’ katika Maporomoko ya Maji ya Mto Rufiji. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wakwanza kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe (hayumo pichani) kuhusu mpango kazi wa kuboresha uwekezaji Tanzania. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha Dkt. Yamungu Kayandabila.
Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe (kulia) akimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (hayumo pichani) wakati wa majadiliano ya namna ya kuendeleza miradi ya maendeleo nchini Tanzania, kushoto kwake ni Mshauri wa Mkurugenzi huyo Bw, Zarau Kibwe.
Picha ya pamoja ya wajumbe walioshiriki majadiliano ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe kuhusu uboreshaji wa sekta binafsi, miradi ya maendeleo, ukuaji wa uchumi pamoja na sekta ya ukuaji wa viwanda. Wanaopeana mikono kulia Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)kushoto Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Bw. Andrew Bvumbe. Kutoka kulia ni Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha Dkt. Yamungu Kayandabila, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles Kichere, wa pili kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga na wa pili kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji Mbadala Benki ya Dunia, kanda ya Afrika Bw, Zarau Kibwe.

MICHUZI TV: DIAMOND, NANDY WAOMBA RADHI KWA KUSAMBAZA VIDEO MITANDAONI

DK.SHEIN AKUTANA NA MAKAMU WA SHIRIKA LA NDEGE LA MISRI EGYPTAIR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Makamo wa Rais wa Shirika la Ndege la Misri EGYPTAIR Bw.Mohamed Alabbady alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Makamo wa Rais wa Shirika la Ndege la Misri EGYPTAIR Bw.Mohamed Alabbady (katikati) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Makamo wa Rais wa Shirika la Ndege la Misri EGYPTAIR Bw.Mohamed Alabbady alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao (hawapo pichani),
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akibadilishana mawazo na Makamo wa Rais wa Shirika la Ndege la Misri EGYPTAIR Bw.Mohamed Alabbady (kushoto) mara baada ya mazungumzo yao yalifanyifika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na Ujumbe aliofuatana nao (wa pili kulia) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Misri Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor na Kaimu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ofisi ya Zanzibar Bw.Mohamed Haji Hamza(wa pili kulia),

Picha na Ikulu

SERIKALI ITAHAKIKISHA INAULINDA, INADUMISHA NA KUUENZI MUUNGANO WETU

VOA Swahili: Duniani Leo 19th April 2018

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 19.04.2018

HARUSI YA ALIKIBA YATIKISA MOMBASA..

Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii, Yayapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda akiongea baada ya Airtel kuibuka kinara katika kutoa hudumia kupitia mitandao ya kijamii, akishuhudia Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Bi Bearice Singano Mallya.
------------------------------------
Airtel Tanzania imetajwa kuwa moja ya makampuni bora ambayo yanajibu vizuri maswali ya mashabiki na wateja wake katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2018.
Ripoti hii imetolewa na kampuni ya Socialbakers ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya kijamii. 
Kwa mujibu wa Socialbakers, tathmini ya robo hii ya mwaka ilifanyika kuanzia Januari 1, 2018 hadi Machi 31, 2018 na kuifanya Airtel Tanzania iibuke kidedea.
Kampuni hiyo ya Social bakers imekabidhi cheti kama ishara ya ushindi huu na kuonesha kuwa Airtel iliweza kujibu vizuri maswali ya mashabiki wake na wateja kupitia mtandao wa Face book kwa asilimia 98 na hivi kuyapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania. 
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda alisema wanajivunia kupata utambulizi huo na inaonesha jinsi gani wamekuwa wakijituma kuhakikisha wateja wao wanapata majibu ya maswali yao kwa wakati kupitia mitandao ya kijamii hususani Face book. 
“Tunayo faraja kuweza kutambuliwa kwa namna hii na sisi tunalo jukumu la kuendelea kuhakikisha wateja na mashabiki wetu wanapata majibu wanayohitaji kwa wakati na mitandao ya kijamii imeturahisishia kazi hii hususani kupitia Face book tumeweza kujibu maswali kwa haraka na kwa wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja,” alisema. 
Mitandao ya kijamii kama Face book inatakiwa kutangazwa zaidi ili itumike kwa wingi kwani itapunguza usumbufu wa wateja kusubiri majibu kwa muda mrefu kama ilivyokuwa hapo awali ambapo walilazimika kupiga simu Airtel. “Kwa kupitia mitandao ya kijamii majibu yanatolewa hapo hapo na hili ndilo limetufanya tutambuliwe kwani tumeweza kutumia njia hii kwa ufanisi mkubwa na tathmini ya Socialbakers imeonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu tulijibu maswali kwa asilimia 98 na hivi kuibuka kidedea,” aliongeza Ndunda
Kwa mujibu wa Socialbakers, utambulizi huu unatokana na namna kampuni imeweza kujibu maswali ya watu kwa muda wa mwezi mitatu. Ili utambuliwe, lazima kampuniipokee maswali 50 kutoka kwa mashabiki katika robo husika na maswali hayo yaweze kujibiwa kwa zaidi ya asilimia 65. 
Socialbakers ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya kijamii hususani Face book, Twitter, Google+, LinkedIn na YouTube ili kusaidia makampuni kujua mafanikio ya kampeni mbalimbali kupitia mitandao hii.  

BENKI YA CRDB KUPELEKA WATEJA WAKE 24 KUANGALIA WORLD CUP URUSI

UNESCO YAWANOA MAFUNDI MITAMBO WA REDIO ZA JAMII 25

$
0
0
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limeanza kutoa mafunzo ya siku saba kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Shirika hilo jijini Dar es salaam, mafunzo hayo yanagusa masuala yanayozunguka jamii namna ya kuyafanya kifanisi na kitaalamu ili kuweza kurusha matangazo yaliyomazuri kwa jamii ambayo yameanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka huu.

"Washiriki hawa wanatoka katika radio 25 za jamii zinazosaidiwa na shirika letu.Kubwa ni kuwapa mafundi mitambo hao elimu kuhusu namna ya kuifanya radio ya jamii kuwa bora wakati wa urushwaji wa matangazo kwa jamii husika,"imesema.

Imeongeza Unesco kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC) husaidia radio za jamii na mtandao wa radio za jamii (TADIO).

Ufadhili huo umelenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania hasa wale wa vijijini wanafanya uamuzi sahihi kuhusu maisha yao kwa kupata taarifa sahihi kutoka redioni.
Afisa Miradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Rose Ngunangwa akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za jamii 25 yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyoanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka huu.
Meneja wa Huduma za Ufundi kutoka TBC, Mhandisi Yusuph Afidhu akizungumza na washiriki kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za jamii zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.
Mkuu wa Studio Redio ya TBC, Mhandisi Omary Salum akitoa mada kuhusu namna ya studio inavyobidi kuwa ili kuweza kurusha matangazo kistadi wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa radio za jamii 25 yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Baadhi ya mafundi mitambo wa radio za jamii wakichangia mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25 yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaliyoanza Aprili 19 hadi Aprili 25 mwaka huu.
Baadhi ya mafundi mitambo wa radio za jamii wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo kwenye kituo cha TBC cha Tazara wakati mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa mafundi mitambo wa radio za jamii 25.

KUSOMA ZAIDI BODYA HAPA

Nawapongeza GeoPol Kutimiza Taratibu za Usajili Nchini- Waziri Dkt Mwakyembe

TANZANIA KUNADI VIVUTIO VYA UTALII DUNIANI KUPITIA TAMASHA LA URITHI WA UTAMADUNI WA MABARA NCHINI UFARANSA

$
0
0
Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 za bara la Afrika zitakazoshiriki katika tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ linalotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa katika mji wa ‘Cherbourg’ mwezi Julai mwaka huu.

Tanzania inashiriki tamasha hilo la kihistoria kwa mara ya kwanza ambapo itapata fursa ya kutangaza utamaduni wake na vivutio vya utalii vya mambo ya kale hivyo kuongeza idadi ya watalii na mapato.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha hilo Jijini Dar es Saalam jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, alisema tamasha hilo litatoa fursa pana kwa nchi kutangaza vivutio vyake ikiwemo vile vya Zamadamu.

“Kimsingi tamasha hilo linatarajiwa kutoa fursa kwa Tanzania kutangaza vivutio vyake na hivyo kuvutia watalii wengi kuja nchini, kila nchi itapewa banda lake la kuonyesha vivutio vyake , Tanzania naamini inakuwa na vivutio vingi vyenye kupendeza watalii kama vile Zinjathropus, Ngoma za makabila mbalimbali pamoja na nyimbo.

“Baada ya tamasha hilo, kutakuwa na ongezeko kubwa la watalii nchini na ninaamini hata zile nchi ambazo hazina rekodi nzuri ya kuja Tanzania kwa wingi  zilizopo Bara la Asia zitaanza kuja,’’. alisema Kigwangla.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ Jijini Dar es Saalam jana.
 Waziri Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
 Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asngya Bangu akiongoza zoezi la utambulisho.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UTT AMIS PLC YATOA ELIMU YA UWEKEZAJI WA PAMOJA KWA WASTAAFU WATARAJIWA WA WAKALA WA MISITU TANZANIA

$
0
0
Ofisa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS PLC, Bi. Martha Mashiku, akitoa elimu ya uwekezaji wa pamoja kwa wastaafu watarajiwa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika Ukumbi wa Mkutano wa Hoteli ya Kings Way mkoani Morogoro. (Na Mpiga Picha Wetu).
 Baadhi ya washiriki wakipata elimu juu ya Uwekezaji wa Pamoja kwa wastaafu watarajiwa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania.

WAGENI WAMIMINIKA BANDA LA TANZANIA WTM AFRIKA

$
0
0
Na: Geofrey Tengeneza-Capetown Afrika Kusini

Banda la Tanzania katika maonesho ya Kimataifa ya WTM Afrika yanayofanyika jijini Capetown Afrika Kusini limeendelea kutembelewa na watu wengi wanaotembelea maonesho haya kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali zinazohusu Tanzania na vivutio vyake vya utalii sambamba na kufanyamzungumzo ya kibiashara na wafanyabiashara katika sekta ya utalii kutoka Tanzania.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi umebaini kuwa watu wengi wanaotembelea banda la Tanzania wamekuwa wakivutiwa zaidi na yanayotolewa kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, pori la akiba la Selous n.k

Kwa upande wa wadau wa utalii kutoka sekta binafsi kutoka Tanzania wanaoshiriki maonesho haya wameelezea kuridhishwa kwao na namna wanavyoendelea kukutana na kuingia makubaliano na wafanyabiashara wenzao wa utalii wakubwa wa kimataifa.

“ Namshukuru Mungu maonesho ni mazuri na nimefanikiwa kukutana na wafanyabiashara ya utalii kutoka mataifa mbalimbali na kufanya makubaliano katika biashara yetu hii” anasema Bw. Naiman Meyassy Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Quest Horizonya jijini Arusha.

Mapema Naibu balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Bi Rosemary Jairo alitembelea banda la Tanzania na kuelezea kufurahishwa kwake namna ilivyojipanga na kushiriki vema katika onesho hili. “Nimefurahishwa sana na banda letu na namna mnavyoitangaza nchi yetu, napenda niwaponze sana Bodi ya Utalii kwa uratibu mzuri wa ushiriki wetu kama nchi” alisema naibu Balozi.

Katika onesho hili la WTM Afrika mwaka huu Tanzania inawakilishwa na makampuni 17 kutoka sekta binafi chini ya uratibu wa Bodi ya utalii Tanzania (TTB) wanaoshiriki katika banda la Tanzania wakati makampuni mengine zaidi ya 10 yanashiriki binafsi yakiwa na mabanda yao katika maonesho hayo. Mbali tna TTB taasisi nyingine zinazoshiriki maonesho hayo ni Shirika la Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na Kamisheni ya utalii Zanzibar.

Meneja Utafiti na Maendeleowa Bodi ya Utalii Tanzania, Ndugu Gladstone Mlay akitoamaelezo kwa wageni waliyotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya utalii “World Travel Market (WTM)” yanayofanyika nchini Afrika Kusini. 
Baadhi ya mawakala wa utalii wa Tanzania waliyoshirikikatika maonesho ya Utalii ya WTM Afrika 2018 wakiuza huduma za utalii wanazozitoa kwa wageni waliyotembelea Banda la Tanzania. 
Baadhi ya mawakala wa utalii wa Tanzania waliyoshirikikatika maonesho ya Utalii ya WTM Afrika 2018 wakiuza huduma za utalii wanazozitoa kwa wageni waliyotembelea Banda la Tanzania. 

WAFANYABIASHARA MKOANI SIMIYU WAUNGA MKONO SERIKALI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA MKOA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu wamekubali kuunga mkono Serikali katika Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mkoa wa Simiyu inayotarajiwa kuanza kujengwa mwezi Juni mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa na Wafanyabiashara hao katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa kilichofanyika  jana Mjini Bariadi, ambacho kilifanyika kwa lengo la kuzungumzia fursa za biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo, changamoto zinazowakabili na utatuzi wake.

Awali akifungua kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo imekusudia kuwa na shule kubwa itakayoweza kuchukua wanafunzi 1000 ambayo itakayopatikana kwa kujenga upya shule ya Sekondari Simiyu (Kidato cha kwanza hadi cha Nne), ambapo aliahidi kuwa ofisi yake itatoa fedha kiasi na akawaomba wafanyabiasha wazawa kuchangia Ujenzi wa shule hiyo kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa.

Amesema  pamoja na kujenga upya Shule ya Sekondari Simiyu, katika shule hiyo kutajengwa mabweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike ili wanafunzi wote wa kike wasome wakiwa wanafunzi wa bweni(boarding).

 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima Mhe. Njalu Silanga akizungumza katika kikao cha Wafanyabiashara wa Mkoa huo na Mkuu wa Mkoa huo katika Kikao kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika kikao chao na Mkuu huyo wa Mkoa kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images