Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109981 articles
Browse latest View live

Watanzania wahimizwa kujenga utamadunI wa kujisomea vitabu

$
0
0
Watanzania wamehimizwa kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu kwa ajiri ya kuibua fursa mbalimbali za kimaendeleo na kuacha tabia ya  kutumia vitabu kama sehemu salama ya kuhifadhia fedha ,  kama ilivyo kwa baadhi ya watu maeneo ya vijijin na mjini  huku waandishi wa vitabu wakitakiwa kuendelea kuandika vitabu kwa lengo la kujenga Taifa lenye wasomi.


Hayo yamesemwa na mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Prof, Ganka Nyamusogoro wakati wa uzinduzi wa siku ya kusoma vitabu duniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro, ambapo amesema  jamii nyingi za kitanzania zimejenga tabia ya kutosoma vitabu kama njia ya kuibua fursa  na kuongeza maarifa baadala yake wanatumia  vitabu kama sehemu ya kuhifadhia fedha  jambo ambalo ni kinyume na na malengo ya waandishi wa vitabu.
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa siku ya kusoma vitabu Duniani katika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
 Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  prof,Ganka Nyamusogoro akikagua moja ya vitabu vilivyooneshwa na chuo cha mzumbe wakati wa maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu Duniani,ambapo chuo cha mzumbe kimetoa nafasi kwa watu mbalimbali kusoma vitabu katika eneo hilo ambalo lipo maalumu kwa siku tatu chuoni hapo kuadhimisha siku hiyo ya kusoma vitabu.
 Wanafunzi wa chuo kikuu cha mzumbe  mkoani Morogoro na shule ya sekondari Mzumbe wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi  katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani ambaye pia ni makamu mkuu wa chuo hicho Prof, Ganka Nyamusongoro hayupo pichani.
 Diwani wa kata ya Mzumbe mkoani Morogoro Recho Kungi wa kwanza kushoto  akisisitizia wanafunzi  juu ya umuhimu wa kusoma vitabu katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani yaliyo fanyika chuo kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.
  Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe  Prof,Ganka Nyamusogoro ambaye pia ni Mgeni rasimi katika maadhimisho ya siku ya kusoma vitabu duniani chuo kikuu Mzumbe  Mkoani Morogoro  akisoma vitabu vya tafiti vilivyofanywa na wanazuoni wa chuo kikuu cha mzumbe mara baada ya kuzindua hafla hiyo.


CCM DAR YASHAURI WALIOZIBA NJIA ZA MAJI WAONDOLEWE, YATOA POLE KWA WALIOPOTEZA NDUGU KWASABABU YA MVUA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Dar es Salaam kimetoa pole kwa familia ambazo zimepoteza ndugu zao kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha huku kikitoa ushauri kwa Serikali kuwaondoa waliojenga kwenye njia za maji kwa lengo la kupunguza maafa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Cylivia Katekamba amewaambia leo waandishi wa habari kuwa chama hicho kinatoa pole kwa wote ambao wamefikwa na maafa na kuomba wenye uwezo wa kusaidia walioathrika na mvua hizo kujitokeza kusaidia.

" Mkoa wa Dar es Salaam umekumbwa na mafuriko na kusababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha.CCM mkoa tunatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kutokana na kuondokewa na ndugu zetu kutokana na mvua.

"Tunafahamu matatizo ya mafuriko yametokea kwetu na hata maeneo mengine duniani nayo wakati mwingine hukumbwa na mafuriko.Kubwa ni kuendelea kushikamana na kusaidia kwenye kipindi hiki.CCM tunatoa pole,"amesema Katekamba.

Pia ametoa mwito kwa walio maeneo hatarishi ni vema wakaondoka maeneo hayo na kufafanua kutokana kuzibwa kwa mitaro na njia za maji imesababisha hata maeneo ambayo huwa hayapati mafuriko safari hii maji yamejaa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Cylivia Katekamba(wa kwanza kushoto) akizungumza ma waandishi wa habari leo jijini wakati anatoa pole kwa waliokumbwa na mafuriko na familia ambazo zimepoteza wapendwa wao kwasababu ya mvua zinazonyesha.

Waziri Makamba aainisha Mikakati Kukabiliana na Taka za Kielektroniki kutekeleza Taarifa ya CAG

50 TECHNICIANS FROM 25 COMMUNITY RADIOS TO BE TRAINED ON PROFICIENCY

$
0
0
The UNESCO Dar es Salaam Office will conduct a 7-days capacity building training on Technical and Equipment Maintenance Proficiency for 50 technicians from 25 community radios in Tanzania Mainland and Zanzibar.

The training, slated for April 19-25, 2018, will take place in Dar es Salaam under the technical support from engineers from the Tanzania Broadcasting Corporation (TBC).

The objective of the training is to build capacity of local radios technicians on technical and equipment maintenance proficiency. Specifically, the training will focus on broadcasting hardware and software thus maintain performance and durability of radio equipment.

The training will contribute to strengthening of local radios and thus ensure their sustainability. Activities to be covered during the training include theory in broadcasting and transmission practical as well as physical mentorship program to seven CRs (Mpanda, Nuru, Mtegani, Micheweni, Tumbatu, Mazingira and Orkonerei).

The capacity building training builds upon the experience from similar training conducted in 2016, whereby feedback from the field indicated that the knowledge gained improved technicians’ skills and status of transmission and broadcasting equipment for each of the community radios. With online troubleshooting of technical equipment through a network of technicians created via WhatsApp and Google accounts, community radios were able to be on-air immediately after identifying a technical problem. This mechanism has helped to reduce costs of onsite repair and troubleshooting within the community radios.

UNESCO with the financial assistance from the Swiss Development Corporation (SDC) supports community radios and the Community Media Network (Tanzania Development Information Organization- TADIO).

Community radios in attendance under the SDC support with their regions in brackets are Nuru FM (Iringa), Pambazuko FM (Morogoro), Fadhila FM (Mtwara) Jamii Mtukwao FM (Mtwara), Loliondo FM (Arusha), Baloha FM (Shinyanga), Kahama FM (Shinyanga) Ileje FM (Songwe) and Tripple A FM (Arusha). In the list are Storm FM (Geita) and Sengerema FM (Mwanza), Kwizera FM (Kagera), Dodoma FM (Dodoma) and Kitulo FM (Njombe). Others are Uvinza (Kigoma), Mpanda (Katavi), Pangani (Tanga), Boma (Kilimanjaro), Mazingira (Mara), Mtegani FM (Unguja South,) Mkoani FM (Pemba South), Micheweni FM (Pemba North) Tumbatu FM (Unguja North), Ruangwa FM (Lindi) respectively.

The training covers 77.4% of all regions in the United Republic of Tanzania.

TAARIFA YA FURSA ZA UFADHILI WA MASOMO

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Simu:255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

               20 KIVUKONI FRONT,
                          P.O. BOX 9000,
                 11466 DAR ES SALAAM,  
                                   Tanzania.


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za mafunzo ya muda mrefu kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Pan African (PAU).
Mafunzo hayo ambayo yapo kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu yatatolewa katika kozi mbalimbali zikiwemo Baiolojia, Hesabu, Uhandisi, Sayansi ya Afya, Usimamizi wa Mazingira, Sayansi ya Michezo, Mifugo, Uongozi na Mtangamano, Lugha, Ukalimani wa Mikutano na Ufasiri, Uhandisi wa Maji na Nishati.  
Kwa waombaji wa Shahada ya Uzamili wanatakiwa kuwa na  miaka isiyozidi 30 kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 35 kwa waombaji wanawake. Aidha, kwa waombaji wa Shahada ya Uzamivu wasiwe na miaka zaidi ya 35 kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 40 kwa waombaji wanawake.
Maombi ya mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao (online) kupitia anuani ya barua pepe ya pau-au.net. Mwisho wa kutuma maombi ya fursa hizi ni tarehe 20 Aprili, 2018. Maelezo ya ziada kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia pau.scholarships@africa-union.org au www.pau-au.net. Mratibu wa Mafunzo haya ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 18.04.2018

BONGOMAKINI: Smart Phone kwa Kiswahili ni nini..??

ANKO ZUMO: 'NATAMANI KUFANYA KAZI NA EBITOKE'


HUDUMA ZA MAJI ZAIMARIKA, TEKNOLOJIA KUONDOA MATUMIZI YA MKAA

$
0
0
Upatikanaji wa maji mijini na vijijini umeimarika kutoka chini ya 50% ya awali kutokana na umakini katika ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji safi nchini. Aidha, ili kukabiliana na mazingira Serikali imeanza mchakato wa kutumia mifumo ya kisayansi ili kuondoa matumizi ya mkaa majumbani.

Hatua hizo zimebainishwa na Mhe. Isack Kamwelwe, Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira) walipokuwa wakieleza utekelezaji wa hoja za CAG katika sekta zao.

Akizungumzia hoja kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji nchini, Waziri Kamwelwe amesisitiza kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, ufuatiliaji na kuzibwa mianya ya ubadhirifu vimeleta mafanikio makubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji mijini na vijijini.

“Sisi kwa upande wetu CAG anatuonesha njia ili tufanye vizuri zaidi. Hadi kufikia Desemba, 2017, upatikanaji wa maji mijini umepanda hadi kufikia asilimia 78. Kwa upande wa vijijini, hadi kufikia Machi 2018, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imejenga vituo vya kuchotea maji 123,888 vyenye uwezo wa kuhudumia takribani watu milioni 30 sawa na asilimia 68.8,” alisema.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu hoja mbalimbali zilizobainishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  katika Wizara yake mapema mjini Dodoma  wakati wa mkutano na waandishi wa habari ( hawapo pichani).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January   Makamba akijibu hoja mbalimnbali zilizobainishwa katika ripoti  ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  katika Ofisi hiyo mapema mjini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa Mawaziri wote kukutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali zilizobainishwa katika  ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  katika Wizara zao mapema mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa  Aweso  mapema mjini Dodoma wakati wa mkutano  na waandishi wa habari uliowashirikisha  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January  Makamba. (Picha zote  na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)


 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Astashahada, Stashahada Msizipe Kisogo: Waziri Jafo

$
0
0
Na Atley Kuni OR TAMISEMI
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuanza kwa kozi za ngazi ya Shahada katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kisiwe kigezo cha kuondosha kozi za Astashahada na Stashahada katika chuo hicho.
Waziri Jafo alikuwa akizundua rasmi Bustani ya  Magufuli katika chuo hicho ambapo Bustani hiyo itatumika kuishi na kuenzi mchango wa kiongozi huyo wa Nchi kwasasa ambao ni uzalendo, kujituma pamoja na uadilifu katika kuwatumikia wananchi.
“Nimesikia maombi yenu yakutaka Kuanzishwa kwa kozi za Ngazi ya Shahada kusudi mtu anapo hitimu masomo yake ya ngazi za awali aweze kuendelea, naomba niwambie, tutajitahidi lifanikiwe, lakini angalizo langu kwenu, tutakapo anzisha Degree isiwe sababu yakusitisha kozi zinazoendelea kwa sasa, ikiwepo Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) ya kozi mnazo endelea nazo” amesema Jafo.
Waziri Jafo amesema, vyuo vingi vilipo anzisha ngazi ya Shahada na kusahau wataalam wa kada za kati vilichochea kukosekana kwa wataalam wakutosha katika ngazi ya kati hususan mafundi mchundo ambao walikuwa wakizalishwa katika vyuo hivyo.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo amewahakikishia Wakurufunzi hao wa chuo cha Hombolo uhakika wa kuajiriwa na Serikali kwa wale watakao fikia vigezo vinavyo hitajika katika nafasi mbali mbali ambazo serikali itatangaza.
 Waziri wa Nchi OR TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo (Mb), akizungumza  wakati wa uzunduzi wa mnara wa kuenzi uzalendo wa Mhe. Rais wa awamu ya tano wa Tanzania katika chuo cha Hombolo.




Baadhi ya watendaji wa Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo wakati wa zoezi la uzinduzi wa mnara wa fikra za kizalendo za Mhe. Rais Magufu
 Kikundi cha Ngoma za asili cha Swala kitoa borudani wakati wa  wa uzunduzi wa mnara wa kuenzi uzalendo wa Mhe. Rais wa awamu ya tano wa Tanzania, kikundi hicho kinachopatikana katika Kijiji cha Nkoyo, Hombolo ambacho ni maarufu katika mkoa wa Dodoma hususani kudumisha utamaduni wa mtanzania.
Mwonekano wa Mnara wa Magufuli Square, Sehemu iliyojengwa mahususi kwa ajili ya kuenzi uzalendo wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa vitendo
 Bodi ya Chuo cha Hombolo iliyo maliza muda wake wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mnara wa fikra za kizalendo za Mhe. Rais Magufuli.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WADAU WA DAWA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege amewataka wauzaji, waagizaji, wasambazaji na wadau wote wa dawa pamoja na Vifaa Tiba Nchini kuchangamkia fursa inayotolewa na Serikali ya kuwa Mshitiri mteule ‘Prime Vendor’ kusaidia katika utoaji wa dawa katika Mikoa yote Tanzania. 
Kandege ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Wadau wa dawa  ‘Vendors Forum’ kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na wadau wa Afya ‘HPSS’ chenye lengo la kuweka uelewa wa pamoja kuhusu uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri.
Amesema “mfumo huu utatumika kupata mahitaji ya bidhaa za Afya pale ambapo vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma vitakosa au kupata kiwango pungufu toka Bohari Kuu ya Dawa na pia utasaidia kupunguza kero za Afya ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya”.
Sasa basi ninyi kama wazabuni muhimu katika sekta hii ya Afya wenye Uzalendo na nia njema na Nchi ya Tanzania mnatakiwa kujitokeza katika mchakato wa kumpata Mshitiri (Prime Vendor) wa kila Mkoa ambaye atakidhi vigezo kwa mujibu wa taratibu manunuzi alisema Mhe. Kandege.
Wakati huo huo Naibu Waziri Kandege aliwafahamisha wadau wa dawa kuwa Serikali imagatua mipango na bajeti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya na inapeleka Fedha moja kwa moja kwenye akaunti za benki zilizofunguliwa katika kila kituo hii itasaidia katika kufanya manunuzi ya dawa hizo na kurahisha mchakato wa malipo. 
“Hivyo niwahakikishie kuwa utaratibu wa malipo utakua ni rahisi na wa haraka zaidi kwa kuwa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati husika zitahusika kuagiza dawa kwa Mshitiri pale mahitaji ya dawa hizo zitakapokosekana kutoka MSD” alisema Mhe. Kandege.
Alimalizia kwa kuwataka Wadau wote wa Dawa kutumia kikao hiki kuelewa kwa undani kuhusu utaratibu huu na kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kumpata Mshitiri Mteule kwani zoezi hili litaendeshwa kwa uwazi na kwa usindani mkubwa.

  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege(mbele) akifungua kikao cha wadau wa Afya ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika Ukumbi wa Dodoma Hotel.
Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi, Dr. Ntuli Kapologwe akitoa maelezo ya awali kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha wadau wa Afya Vendor Forum.
 Mfamasia Mwandamizi  toka Ofisi ya Rais Tamisemi, Regina Richard akielezea malengo la kikao cha Wadau wa Dawa ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel mapema.
  Wataalam toka Idara ya Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau wa Dawa wakiwa katika kikao maalum cha wadau wa dawa.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege(mbele katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu na wadau wa dawa.

Makomandoo wa Tanzania wafanya yao Darfur, watunukiwa nishani

UJANGILI NCHINI WAPUNGUA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 - DK. KIGWANGALLA

$
0
0

Na Hamza Temba-Dodoma

Serikali imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ujangili hapa nchini kwa zaidi ya asilimia 50.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.Dk. Kigwangalla alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita hakuna mauaji mapya ya wanyamapori yaliyoripotiwa na kwamba nyara zinazokamatwa hivi sasa ikiwemo meno ya tembo na ngozi za wanyamapori ni masalia ya zamani.

Amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kudhibiti vitendo vya ujangili ikiwemo doria za mara kwa mara za kiitelijensia ambazo zimekuwa zikishirikisha vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na raia wema. 

Alisema Serikali itaendelea kudhibiti vitendo hivyo kwa kuimarisha ulinzi katika maeneo ya hifadhi nchini ikiwa ni pamoja na kuanzisha jeshi maalum la usimamizi wa Misitu na Wanyamapori, Sheria ya wanyamapori na za taasisi za uhifadhi zimeanza kufanyiwa marekebisho kuwezesha mabadiliko hayo.

Katika hatua nyingine Dk. Kigwangalla amemueleza balozi Cooke kuwa, Serikali kupitia Wizara yake inaendelea kuimarisha  vivutio vya utalii hapa nchini kwa kupanua jeografia ya maeneo ya utalii sambamba na kuongeza vivutio ili kuongeza idadi ya watalii na mapato.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na msafara wa balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

ALI KIBA AFUNGA NDOA YA KIFAHARI MJINI MOMBASA NCHINI KENYA,KURUSHWA LIVE JIONI YA LEO

$
0
0
 
Mwanamuziki mahiri wa Bongofleva nchini Ali Kiba, leo amefunga ndoa na Binti wa Kimombasa ajulikanae kwa jina la Bi.Amina Khalef,ndoa hiyo imefungwa katika msikiti wa Ummu Kulthum uliopo mjini Mombasa nchini Kenya,ambapo hafla hiyo imehudhuriwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo mashuhuri .Aidha taarifa zinaeleza kuwa Harusi hiyo itakayokuwa ya aina yake itarushwa LIVE  na kituo cha televisheni ya AZAM jioni ya leo.
Mwanamuziki mahiri wa Bongofleva nchini  Ali Kiba akizungumza na 'mpambe' wake leo wakati akifunga ndoa na Binti wa Kimombasa ajulikanae kwa jina la Bi.Amina Khalef,ndoa hiyo imefungwa katika msikiti wa Ummu Kulthum uliopo mjini Mombasa nchini Kenya.

 Alikiba akifurahia jambo na marafiki zake mara baada kufunga ndoa 
 Ali Kiba akifurahia jambo akiwa na ndugu,jamaa na marafiki zake waliomsindikiza kwenye kuchukua 'jiko' mapema leo asubuhi huko mjini Mombasa. 
Msanii alikiba na Wapambe wake wakielekea kufunga ndoa.

Waziri Kamwelwe aainisha mikakati ya Serikali utekelezaji miradi mikubwa ya Maji


RAIA WA KIGENI WATAKIWA KUACHA KUINGILIA ZOEZI LA UANDIKISHWAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA

$
0
0
Editha Karlo,Kasulu.

MWENGE wa Uhuru 2018 unaondelea na mbio zake katika Mkoa wa Kigoma umewataka raia wa kigeni kuacha kuingiliza zoezi la uandikishwaji wa vitambulisho vya Taifa  linaloendelea sasa Mkoani humo, kwakuwa zoezi hilo ni haki ya Watanzania.

Mmoja wa wakimbiza mwenge Kitaifa   Dominik Njunwa  aliyasema hayo wakati akitoa ujumbe wa Mwenge, Katika Kijiji cha Shunga  Wilayani Kasulu wakati wa ufunguzi wa bwalo la kulia chakula katika Shule ya Sekondari Muyovozi, ambapo aliwaomba Watanzania waishio jirani na Nchi ya Burundi kuwafichua wale wote wasio Raia wa Tanzania  watakao jitokeza kujiandikisha katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa.

Njunwa alisema hairuhusiwi Raia yeyote asie Mtanzania kujiandikisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vya Taifa, kwakuwa vitambulisho hivyo vinatolewa kwa Watanzania pekee na ni kosa kubwa kwa Raia wa Nchi nyingine kupata kitambulisho hicho .

 Kaimu Mkuu  wa Wilaya  ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala aliwataka viongozi wa Vijiji na mitaa kuacha kuhujumu zoezi hilo la kuandukisha vitambulisho vya Taifa  kwa kuwaingiza watu wasio Watanzania iliwaweze kupata vitambulisho kwa atakae bainika anafanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo wa Wilaya  aliwataka wananchi kuwafichua wale wote wanaowahofia kuwa sio Raia wanaojitokeza kujiandikisha kwa ajili ya Kupata vitambulisho vya Taifa na kuwaripoti kwa vyombo husika ili kuweza kuchukuliwa hatua za Kisheria na waondolewe katika zoezi hilo.

Kanali Ndagala alisema zoezi hilo ni kwa Watanzania tu wanapopatiwa vitambulisho,Raia wasio wa Tanzania ni kosa na inaweza kuleta shida katika Taifa la Tanzania na Kuwaonya kuwa makini ili kuendeleza hali ya usalama hasa Kwa Mikoa iliyopo karibu na Nchi jirani za Burundi na Congo.

" Kuanzia Mwakani  Mtanzania akiwa na kitambulisho cha Taifa  anauwezo wa Kupata hati ya kusafiria wanapopata watu wasio Raia wakipata hati zetu za kusafiria inatupa shida sana na wanatumia kwa kufanya uhalifu jambo ambalo sio zuri katika Taifa letu marufuku kabisa kwa raia asie Mtanzania kuchukua Kitambulisho cha utaifa ", alisema Ndagala.

Mwenge wa Uhuru Wilayani Kasulu umekagua na Kuzindua Miradi 13 yenye thamani ya zaidi ya bilioni tano  miradi hiyo ni ya Maji, Afya na Maji na sambamba na Miradi hiyo Mwenge huo umezindua Kituo cha Afya Katika Kijiji cha Shunga kilicho jengwa na Kanisa la Agrikana  Dayosisi ya Westeni Tanganyika.
 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2018 Charles Kabeho akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa Wakazi wa kijiji cha Nyamidaho Wilayani Kasulu baada ya mwenge kuzindua mradi huo wa maji
Kiongozi wa mbio za mwenge 2018 Charles Kabeho akifungua Club ya wapinga rushwa katika sekondari ya Titye Wilayani Kasulu

WAGONJWA 19,371 WATIBIWA KATIKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUTOKA JANUARI HADI MACHI 2018.

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miezi mitatu ya Januari hadi Machi 2018 imeona jumla ya wagonjwa 19,371 wenye matatizo mbalimbali ya moyo kati ya hao wagonjwa wa nje ni 18,481 na waliolazwa ni 890.

Wagonjwa 105 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua kati ya hao watu wazima 53 na watoto 52. Kati ya wagonjwa 105 waliofanyiwa upasuaji 66 walifanyiwa na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo watoto wakiwa ni 35 na watu wazima 31.

Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa wagonjwa 231 kati ya hao watoto ni 20 na wakubwa 211. Kati ya wagonjwa 231 waliotibiwa wagonjwa watu wazima 211 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu wa ndani.

Kwa kipindi cha miezi mitatu tumekuwa na jumla ya kambi za matibabu nane (8) ambapo tulifanya matibabu kwa kushirikiana na washirika wetu kutoka nchi za Ujerumani, Israel, Australia , Marekani, India na Falme za Kiarabu. Katika kambi hizo jumla ya wagonjwa 39 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 17 na watu wazima 22. Wagonjwa 72 walifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya hao watoto 20 na watu wazima 52.

Tumefanya upasuaji wa kuunganisha mishipa ya damu (AVF- Arterio Venous Fistula) kwa ajili ya kusafishia damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo (Hemodialysis) 36.

Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi tunaowapokea mioyo yao kutokuwa katika hali nzuri hivyo basi tunawaomba wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara hii itawasaidia kujuwa kama wana matatizo ya moyo au la na kama wanamatatizo wataweza kupata tiba kwa wakati.

Wazazi na walezi tunawaomba wasisahau kupima afya za watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya kumfikisha Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulika mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Kwa wamama wajawazito wafanye uchunguzi (Fetal Echocardiography) wa kuangalia kama mtoto aliyeko tumboni anamatatizo ya moyo.

Aidha kwa upande wa gharama za matibabu Taasisi yetu imeyagawa katika makundi manne (4) tuna wagonjwa wanaotibiwa kwa bima mbalimbali ambazo tumeingia makataba nazo. Wagonjwa wanaolipia gharama zote wenyewe, wagonjwa wanaochangia kidogo huku gharama zingine zikilipwa na Serikali. Kundi la mwisho ni wagonjwa ambao hawalipii kabisa gharama za matibabu ikiwa watakidhi vigezo vyote vya kutokulipa.

Huduma zetu za matibabu ya moyo zinatolewa kwa watanzania wote wa Bara na Visiwani. Ifahamike kwamba fedha za matibabu zinazolipwa na wagonjwa zinatumika kununua vifaa tiba vya moyo kama mlango wa moyo (Valve), betri ya moyo (Pacemaker) na vinginevyo.

Kutokana na matibabu ya moyo kuwa ya gharama kubwa tunaendelea kuwasisitiza wananchi wajiunge na mifuko ya bima za afya ambayo itawasaidia kulipa gharama za matibabu pindi watakapohitaji kutibiwa. Pia itasaidia Hospitali yetu kuendelea kujiendesha yenyewe kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
19/04/2018

WANAFUNZI 346 WA KIDATO CHA KWANZA WILAYANI KAKONKO KUANZA MASOMO MWISHONI MWA APRILI

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma 

WANAFUNZI 346 wa kidato cha kwanza katika Wilaya Kakonko mkoani Kigoma ambao walikuwa hawajaanza masomo kutokana na shule walizopangiwa kuwa na uhaba wa madarasa wanatarajia kuanza masomo mwishoni mwa Aprili mwaka huu.

Hatua hiyo inatokana na jitihada za Serikali wilayani humo kuhakikisha wanafunzi waliofaulu na kutakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza wanakwenda shuleni.

Akizungumza hivi karibuni Ofisa elimu kwa Shule za Sekondari wilaani hapa Christopha Bukombe amesema miongoni mwa wanafunzi 1,714 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza walishindwa kuripoti ni 346 waliopangiwa katika shule ya Kanyonza, Muhange na Gwanumpu.
Bukombe ametoa takwimu hizo baada ya kupokea msaada wa mifuko ya saruji na mabati 60 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa vyumba vya madarasa vitano na baada ya mwezi huu kuisha wanafunzi watajiunga kutokana na changamoto kutatuliwa.

Amesema katika shule ya Kanyonza kuna wanafunzi 78, Muhange 97 na Gwanumpu 171 ambapo kutokana na upungufu huo walianza kuhamasisha wananchi kuchangia na Serikali imetoa Sh.milioni 8 katika shule mbili za Kanyonza na Gwanumpu na Sh.milioni 4 kwa shule ya Muhange.

Mchango huo wa umetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa lengo la kutatua changamoto hiyo na wanafunzi wataanza masomo kwani walichokuwa wanasubiri fedha kutoka Serikalini.Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amekabidhi saruji na mabati hayo kwa lengo la kuunga mkono jitihada za wananchi ambazo wamezionesha.

Amewapongeza watendaji wa kijiji, madiwani na wenyeviti wa vijiji kwa jitihada zao kubwa katika kufanikisha ujenzi wa madarasa ili wanafunzi wapate elimu.Amesema Serikali inatamani kuona kila mtoto anapata elimu na ni jukumu la wazazi kujitoa ili kutatua baadhi ya changamoto zinazo jitokeza, kwani Serikali haiwezi kufanya kila kitu.
"Niwaombe wananchi mnapoambiwa elimu bila malipo si kwamba hata kujitolea kwenye ujenzi mshindwe, watoto ni wa kwenu lazima mnapoona Serikali haijakamilisha jambo fulani mfanye wenyewe suala hili ni letu sote.

"Lazima wanafunzi wote wapate elimu ni haki yao hakuna urithi mwingine tutakao waachia watoto wetu zaidi ya elimu lazima mtambue kuna michango mingine Wananchi wanatakiwa kuchangia kuhakikisha changamoto hizi zinakwisha,"amesema Kanali Ndagala.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Gwanumpu, Toy Butono amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutoa msaada huo na kuwaomba wananchi kuendelea kuchangia.

NDITIYE: SHULE ZA SEKONDARI KIBONDO ZAONGOZA UFAULU KITAIFA

$
0
0
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb) wakati akipokea mbio za mwenge wa Uhuru ulipowasili Wilaya ya Kibondo kwenye jimbo lake la Muhambwe ukitokea Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma. Amesema kuwa Wilaya ya Kibondo imeongoza kwa ufaulu wa shule za sekondari kwa miaka miwili mfululizo ya masomo mwaka 2016 na 2017 ambapo kidato cha pili wameshika nafasi ya nane kitaifa na kidato cha nne wameshika nafasi ya tisa kitaifa na kuzibwaga sekondari nyingine zilizopo kwenye jumla ya Wilaya 187 nchini.

Nditiye amefafanua kuwa shule hizo zimezawadiwa kiasi cha shilingi milioni 680 na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mpango wa Elimu kwa Matokeo (E4P) ambao umeleta chachu, ari na ushindani kwenye kiwango cha ufaulu kwenye shule mbalimbali nchini. Amefafanua kuwa fedha hizo zimetumika kugharamia upatikanaji wa miundombinu mbalimbali kwenye shule ya sekondari ya Malagarasi na ya Wasichana ya Kibondo.

Ameongeza kuwa ushindi huo umeleta chachu na mwamko zaidi kwa wanafunzi, walimu, wazazi, walezi na wadau wa elimu kwenye Wilaya hiyo ambapo wamejipanga kuchangia ujenzi wa miundombinu mbali mbali kwenye shule za Wilaya hiyo ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi ambapo imeendana na kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu isemayo, “Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa kwenye Elimu kwa Maendeleo ya Taifa”.

Mhandisi Nditiye amesema kuwa Wilaya ya Kibondo inaunga mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muunano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli za kutoa elimu bure nchini kote kwa shule za msingi na sekondari ambapo wazazi hawalipi ada yeyote hivyo inawawezesha kushirikiana kuendeleza miundombinu ya shule na mahitaji ya huduma nyingine ili wanafunzi waweze kujisomea na hivyo kuongeza ufaulu wao.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb) akipokea Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili kwenye jimbo lake la Muhambwe Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akishiriki uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Mabamba kilichopo kwenye jimbo lake la Muhambwe wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru za kitaifa uliofanyiwa na kiongozi wa kitaifa wa mbio hizo Bwana Charles Kabeho (wa tatu kushoto) kwenye kata ya Mabamba wilayani Kibondo, Kigoma
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Mheshimiwa Loyce Bura (kulia) akipokea mbio za Mwenge wa Uhuru wa Taifa kwenye kijiji cha Mkubwa kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Kibondo na Kakonko
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akigawa chandarua kwa wanawake wenye watoto baada ya uzinduzi wa kituo cha Afya cha Mabamba kilichopo kwenye jimbo lake la Muhambwe wilayani Kibondo, Kigoma wakati wa mbio za Mwenge wa uhuru za kitaifa
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, Mbunge wa jimbo la Muhambwe wilayani Kibondo, Kigoma akipiga ngoma kuburudisha wapiga kura wake wakati wa kupokea mbio za Mwenge wa Uhuru za kitaifa uliowasili kwenye Wilaya hiyo
Shule za sekondari za Wilaya ya Kibondo zaongoza kwa ufaulu wa elimu katika ngazi ya kitaifa kwa miaka miwili mfululizo na kushika nafasi kati ya shule kumi bora za kitaifa na kuzishinda wilaya nyingine zote nchini

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

ELIMU KWA WAKULIMA WA PAMBA KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA YAPAMBA MOTO ILI KUCHOCHEA TANZANIA YA VIWANDA

$
0
0
Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) chini ya usimamizi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeendelea kutoa elimu  kwa wakulima  pamoja na kuhakiki mizani itakayotumika kununulia zao la Pamba ikiwa ni maandalizi ya msimu wa ununuzi wa Pamba kwa mwaka huu (2018).  Zoezi hili la utoaji elimu na uhakiki wa mizani itakayotumika kununulia Pamba  linaendelea  katika Mikoa ya Shinyanga, Geita, Simiyu, Mwanza, Tabora, Mara pamoja  na Kagera kwa kushirikiana na Ofisi ya Wakala wa Vipimo Makao Makuu.

Dhumuni kuu  la utoaji elimu  kwa wakulima wa zao la Pamba  Kanda  ya Ziwa  ni kuwawezesha  wakulima  kutambua mizani iliyosahihi   (inayoruhusiwa kwa biashara)  na ile iliyochezewa (isiyoruhusiwa kwa biashara)  ili waweze kujilinda wenyewe pindi maafisa vipimo wanapokuwa hawapo katika vituo vya kuuzia Pamba yao na pia ni kuwawezesha wakulima kupata  faida ya thamani kamili ya jasho lao.  
 Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoani Mwanza, Hemed Kipengere akitoa elimu kwa wakulima wa Pamba Wilayani Magu kuhusiana na mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kupima Pamba kwenye mizani ili Wakulima waweze kupata faida ya jasho lao la kulima Pamba.

Akizungumza na  Meneja Sehemu ya Elimu, Habari na Mawasiliano Bi. Irene John,  alisema katika maandalizi ya msimu mpya wa ununuzi wa Pamba Mwanza wanategemea kutoa elimu kwa Wilaya tano (5), Simiyu  Wilaya tano (5), Shinyanga Wilaya tatu (3), Geita wilaya sita (6), Tabora   Wilaya tatu (3) , Kagera Wilaya mbili (2) pamoja na Mara Wilaya tano (5). Hivyo, kwa mwaka huu jumla ya Wilaya 28 zimelima Pamba na zote zitapatiwa elimu  inayohusu matumizi ya vipimo sahihi  na faida zinazopatikana kwa mkulima kwa kuuza mazao yake kupitia mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo.

Mwaka huu tofauti kidogo na mwaka jana maana Serikali imefufua Vyama vya Ushirika ambapo ununuzi wote wa Pamba utafanywa na Vyama vya Msingi  ambayo vinasimamiwa na wakulima wenyewe badala ya kuuza Pamba yao kupitia Mawakala kama ilivyokuwa imezoeleka miaka ya nyuma.  Mkulima wa Pamba atanufaika zaidi  kwa kuuza mazao yake kupitia vyama vya msingi sababu mazao yote  yatakayopatikana  kutoka kwenye Pamba yaani mbegu pamoja na nyuzi  mkulima atahusika kupata faida ya uuzaji wa mazao hayo tofauti na mwanzo faida kama hii ilikuwa haipatikani kwake isipokuwa kwa mfanyabiashara tu.
 Afisa wa Wakala wa Vipimo mkoani Mara wakionesha mizani sahihi na ile isiyo sahihi ili wakulima waweze kujilinda wenyewe pindi maafisa wanapokuwa hawapo.

Pia kuuza Pamba kupitia vyama vya msingi itapunguza ulaghai kwenye mizani sababu wasimamizi na watumiaji wa Mizani watakuwa ni  wakulima wenyewe wa Pamba wala siyo mawakala.
 Irene  alisema Sheria ya Vipimo Sura 340 inawataka Wakala wa Vipimo  kuhakiki na kupiga chapa vipimo vyote vinavyotumika katika biashara ikiwa ni pamoja na  kuweka   sticker kwa kipimo kitakachokuwa tayari kimehakikiwa na kukutwa kikiwa sahihi  ili iwe rahisi kwa wakulima kuona na kutambua mizani iliyokaguliwa na kuruhusiwa kwa biashara kwa mwaka husika.

Bi. Irene ameongezea kuwa Wakala wa Vipimo itaendelea kufanya ukaguzi wa kushtukiza  na wakawaida wakati wowote  baada ya msimu wa ununuzi wa Pamba kuanza ili panapokuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu uonevu katika mizani yaweze kutatuliwa kwa haraka.
 Bi. Irene John  aliwasihi wakulima wanaolalamikiwa kuweka maji, kokoto pamoja na mchanga kwenye Pamba kwa ajili ya kuongeza uzito waache tabia hiyo mara moja  ili kuleta biashara ya haki.
 Lengo kuu la Wakala wa Vipimo ni kumlinda mlaji ili apate faida na thamani ya kile alichozalisha  na siyo kupunjwa  na wafanyabiashara  wajanjawajanja.  Irene  alisisitiza kuwa kwa wale watakaobainika kuchezea mizani  kwa ajili ya kuwaibia wakulima  adhabu imeboreshwa kuanzia mwaka juzi ( Nov. 2016) hivyo, faini  itaanzia  laki moja  badala ya elfu kumi kama ilivyokuwa imezoeleka kufikia  hadi milioni ishirini endapo mkosaji atakubali kosa.  Kesi ikifikishwa mahakamani na mlalamikiwa akakutwa kweli alikosa kulingana na ushahidi utakaokuwa umetolewa mshitakiwa atatozwa faini kuanzia laki tatu hadi milioni hamsini au kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Viewing all 109981 articles
Browse latest View live




Latest Images