Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

MANISPAA YA UBUNGO YAINGIA MKATABA NA BENKI YA CRDB KUTOA MIKOPO YA VIJANA NA WANAWAKE

$
0
0
 Meya wa Manispaa ya Ubungo,Boniface Jacob akizungumza kabla ya kutiliana Saini Mkataba na Benki ya CRDB Juu ya Mikopo ya kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
 Meya wa Manispaa ya Ubungo,Boniface Jacob akitia saini Mkataba wa makubaliano wa kushirikiana na benki ya CRDB Kutoa Mikopo  kwa  kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
 Mkurugenzi  wa Halamashauri ya Manispaa ya Ubungo, John Kayombo akizungumza kabla ya kumkaribisha mwakilishi wa benki ya CRDB Kuelezea walivyojipanga kutoa mikopo kwa kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
 Muwakilishi wa Benki ya CRDB, Philip Stephene akizungumza kuhusu benki yake itakavyotoa mikopo kwa kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
 Sehemu ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Wakishuhudia tukioa la utiaji saini baina ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na CRDB  kwa kina Mama na Vijana wa Halmashauri ya Ubungo .
Sehemu ya Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakifutilia tukio hilo la utiaji saini na benki ya CRDB

WANAJESHI JWTZ WATUNUKIWA NISHANI ZA UMOJA WA MATAIFA SUDAN

$
0
0
​Na Luteni Selemani Semunyu
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Kikosi cha 11 wametakiwa kujivunia mafanikio yaliyopatikana kufuatia  utumishi wao uliotukuka kwa kipindi cha Mwaka Mmoja waliokuwa wakishiriki Ulinzi wa amani Jimboni Darfur nchini Sudan na kutunukiwa Nishani ya umoja wa Mataifa.

Hayo yalibainishwa na mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID   jimboni Darfur Luteni Jenerali Leonard Ngondi wakati wa sherehe za kuwatunuku Nishani Askari wa JWTZ  katika sherrehe zilizofanyika Khor Abeche na kuhudhuruliwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serkali ya Sudan.

“ Kutunukiwa nishani ni jambo la Kujivunia kwa kuwa zimetolewa kwa sababu Askari wamefanya kazi Nzuri amabayo inapaswa kupongezwa hasa kutokana na Doria zilizofanyika ikiwemo katika safu za Milima ya jaber ambayo inakaliwa na Waasi” Alisema Luteni Jenerali Ngondi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Operesheni ya Jaber Mara  Lameck Kawiche alitoa wito kwa Wanajeshi wa Tanzania kuendeleza utayari  wao ili kuhakikisha  wanalinda heshima ya jeshi hilo kwa kufanya kazi kwa Weledi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama ilivyotokea Nchini Kongo.

“ Najivunia Utimamu wa jeshi la Tanzania tuna kila sababu kumpongeza Rais na Amiri Jeshi kwa kuridhia Majeshi ya tanznia Kushiki Operesheni za Umoja wa Mataifa sambamba na Mkuu wa Majeshi kya Ulinzi kwa mafunzo kwa Wanajeshi Wake” Alisema  Kawiche.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi UNAMID Jimboni Darfur Sudan, Luteni Jenerali  Leonard Ngondi ( wa Tatu  kushoto) akiwasili katika Uwanja wa ndege wa Khor Abeche katika sherehe za uvishaji nishani  walinda Amani kutoka Tanzania  Hivi karibuni wa nne Kushoto ni kamanda wa kikosi cha Tanzania Kanali Wiliam Sandy .(Picha na Luteni Selemani Semunyu.
Kamanda Kikosi cha Tanzania  TANZBATT 11 Jimboni Darfur nchini Sudan, Kanali William Sandy kulia akivishwa nishani na  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi UNAMID. Luteni Jenerali  Leonard Ngondi katika sherehe za uvishaji nishani  walinda Amani kutoka Tanzania  Hivi karibuni.(Picha na Luteni Selemani Semunyu)
Mnadhimu Mkuu wa mpango wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID akivisha nishani walinda Amani kutoka Tannzaia katika sherehe za uvishaji nishani walinda Amani kutoka Tanzania hivi karibuni katika eneo la Khor Abeche(Picha na Luteni Selemani Semunyu).


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA 

Muhimbili Yapandikiza Figo Wagonjwa Wanne

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kupandikizia figo wagonjwa wa nne ikiwa ni mara ya pili kutoa matibabu hayo ya ubingwa wa juu nchini.

Upasuaji huo umefanywa na wataalam wa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalam kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India na umekua na mafanikio makubwa kwani wagonjwa wote hali zao zinaendelea vizuri . 

Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Museru amesema  Novemba mwaka jana Muhimbili iliweka historia kwa kufanya upasuaji  mkubwa na wa kwanza nchini kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano za kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Akifafanua amesema upasuaji huo wa figo ukifanyika nchini unagharimu Shilingi Milioni 21 na endapo mgonjwa akipelekwa nchini India matibabu yake yanagharimu Shilingi Milioni 80 hadi Shilingi milioni 100.

“Shughuli hii inatuonyesha kwamba hospitali sasa inaweza kupandikiza figo na lengo letu ni kuhakikisha huduma hii inakua endelevu ili kuokoa fedha za serikali kupeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi na pia kuwafikia Watanzania wengi ambao wanahitaji kupandikizwa figo,’’amesema Profesa Museru.

Amesema Hospitali ya Muhimbili itaendelea na shughuli hiyo na kwamba kila mwezi itapandikiza figo kwa wagonjwa watano hivyo kwa mwaka itafanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 60.
 Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya BLK ya India wakimpandikiza figo mgonjwa baada ya ndugu yake kutoa figo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo na Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Isaack Mlatie na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo na Upasuaji wa Hospitali ya BLK, Dkt. Ankur Arya. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo na Upasuaji wa Hospitali ya BLK India, Dkt. H. S. Bhatyal wakiendelea na upandikizaji figo kwa mgonjwa.
 Wataalamu wakiaandaa figo baada ya kuitoa kwa mchangiaji kabla ya kuipandikiza kwa mgonjwa.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo na Upasuaji wa Hospitali ya BLK India, Dkt. H. S. Bhatyal (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wengine baada ya kutoa figo kwa mchangiaji.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

STAND UNITED YATAKA FEDHA ZAKE ZILIZOKATWA NA TFF, YATISHIA KUJITOA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uongozi wa Stand United umetishia kujitoa katika mashindano ya Azam Sports HD Federation Cup baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kuwakata mapato yao.

Hatua hiyo ya TFF imekuja baada ya kuwa na malalamiko kutoka kwa wachezaji mbalimbali wa timu za ligi kudai pesa zao za usajili au malimbikizo ya mishahara.

Akielezea hatua hiyo moja ya kiongozi wa Stand United 'chama la wana' amesema kuwa kama hawatalipwa pesa za mashindano ya FA watachukua uamuzi wa kujitoa kwani Tff imekata pesa  na  kuwalipa wachezaji wanaowadai bila kuwashirikisha.

Hata hivyo kwa upande wa Shirikisho la soka TFF wao wamesisitiza kuwa utaratibu huo wa kuzikata fedha utaendelea kwa wale wote ambao wamekiuka mikataba yao na wachezaji au makocha.

TFF haitasita kuzikata fedha klabu zote zitakazokuwa na madeni yanayodaiwa iwe kwa kukiuka mikataba yao na wachezaji,makocha au kwa namna nyingine yoyote.

Kumekuwa na klabu zinalalamika kinyume na utaratibu tunazitahadharisha kufuata utaratibu unaofahamika kinyume cha hapo hatutasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayekiuka utaratibu.

TFF inaendelea kusisitiza kwa klabu kutoa malalimiko yao kwa njia za kikanuni ili kuepuka hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi yao kama Ibara ya 50 ya katiba ya TFF inavyozungumza pamoja na Kanuni za Maadili.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapteni mstaafu George Mkuchika akisisitiza kuhusu sheria inayotumika kutoa likizo kwa watumishi katika sekta ya umma na binafsi pale wanapojifungua.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kuboresha makazi ya Askari Polisi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Paramagamba Kabudi akizungumza jambo kwa Waziri wa Madini ,Mhe. Anjella Kairuki wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.
 Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo.
Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya wabunge katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma wakati wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)

Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kikula umeanzia tarehe 17 Aprili, 2018.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mhe. Rais Magufuli amewateua Makamishna wa Tume ya Madini kama ifuatavyo:
  1. Bw. Doto James – Katibu Mkuu, Fedha na Mipango.
  2. Bi. Dorothy Mwanyika – Katibu Mkuu, Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
  3. Dkt. Florens Turuka – Katibu Mkuu, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  4. Mhandisi Musa Iyombe – Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  5. Bw. Haroun Athuman Kinega – Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini (FEMATA).
  6. Dkt. Evaristo Emmanuel Longopa – Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  7. Prof. Abdulkarim Hamis Mruma – Mkurugenzi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafutaji Madini Tanzania (GST).
  8. Dkt. Athanas Simon Macheyeki – Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI).
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Uteuzi wa Balozi Mstaafu Njoolay umeanza tarehe 17 Aprili, 2018.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili, 2018


MWANDISHI WA HABARI PASCAL MAYALA AFIKISHWA MBELE YA KAMATI YA MAADILI YA BUNGE

$
0
0
Mwandishi wa kujitegemea, Ndg. Pascal Mayala (kushoto) akihojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge mjini Dodoma kwa kuandika habari yenye maudhui ya kudharau Bunge kwenye safu yake ya gazeti la Rai Mwema.

PROF. TIBAIJUKA’S IRRESPONSIBLE REACTION TO THE CURRENT DAR-ES-SALAM FLOOD MENACE.

$
0
0
BY MOHAMED MATOPE
Yesterday, I read an article from a social media site written by former Minister of land and urban development, Mama Professor  Tibaijuka. After going through the article, I was dismayed, to say the least, with her attempt to erase the history of the role she played in exacerbating the flood problem currently affecting hundred thousands of people in the country. “Without discipline and respect of the urban development plan, floods are going to be an ongoing menace”, wrote Dr. Tibaijuka. She continues by saying, “When I was a minister of land, I worked so hard to prevent Msimbazi valley from flooding by abiding to the Nyerere Master Plan. However, there was no political will for it.” The unanswered question on her part is: who was lacking the political courage to reinforce the Nyerere Master plan during her tenure as Minister?
To make the puzzle even more complicated, we know that she said that she was a Minister in charge of oversee the city survey, and development. The last time I checked, the Minister was the chief executive officer of the ministry, making her, the only political appointee in the ministry. So it appears, as Tupac Shakur said, the darker the flesh , the deeper the root. We can't deny that Msimbazi valley housing is a long-standing city construction disaster and that it's unfair to blame her alone for it.  The failure, however, to acknowledge that she was a part of the problem is irresponsible.
The US President Nixon used to say “the buck stops right here with me.” With this concept, he was able to accept and absorb the blame for all the wrong actions and decisions of his government. This is what is lacking in our African leaders, today. They are only willing to take credit when good things happen under their watch and quickly distance themselves from their unfavorable decisions. In short, they don’t want to own-up to their mistakes or take responsibilities when they fail to fulfill their duties. History has taught us that if we don’t learn from our mistakes, we are bound to repeat them.

In this case, Dr. Tibaijuka has either chosen to deny her load of responsibility that has directly contributed to the current ongoing flood calamity or is entirely insensitive and  blatantly void of empathy to the hundreds of thousands of people in Dar-es-salaam currently displaced or living under the water. It is utterly disgusting and purely insulting to tell these people that their problem will never be solved, and yet she was in charge of fixing it. She couldn’t/wouldn’t do it and no one will. It's undeniable that she is well informed on the matter. Reading her article, there is no doubt that she knows the root cause of the problem well enough. She mentions every area of the city, where the water is coming from and how it floods the city. However, she offers little to no details on how to mitigate it.
It would have been wiser for her to start writing her article by apologizing and saying…. “I'm terribly sorry to all the people affected by the floods; I feel your pain, more so, I let you down. When I was in the position of authority, I fell short in pursuing  measures that could potentially reduce or eliminate the cause of today’s flood problem. My ministry failed to implement the plan that was made to curb the problem, and for that, I would like to offer my sincere heartfelt apologies. Nevertheless, from my experience, here is my advice to the current Minister on how to go about implement a solution for this problem.
Sometimes, the best way forward, starts with acknowledgement of the issue and the factors that led you down the path you are on. A great leader is not defined by their appearances, power or words but rather by the actions they take - something Dr Tibaijuka has clearly shown a great lack of in this case.

ILI UWE MWALIMU MKUU LAZIMA SHULE YAKO IFAHURISHWE KUANZIA ASILIMIA 60 HADI 90

$
0
0
Katibu tawala mkoa wa Ruvuma HASSAN BENDEYEKO amesema ili mwalimu katika shule husika ateuliwe mkuwa mwalimu mkuu ni lazima awe amefaurisha wanafunzi kwa asilimia 60 hadi 90 hii itasaidi kwa mkoa wa Ruvuma katika kukabiliana na uporomokaji wa elimu kwa kipindi cha mwaka 2017 baada ya mkoa huo kufanya vibaya katika matokeo ya kidato cha nne. HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Aprili 18, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

THE NGOMA AFRICA BAND BASED IN GERMANY: MOST INFLUENTIAL BAND OF ALL TIME

$
0
0

    THE NGOMA AFRICA BAND  The Golden Voice of East Africa Soulful Vocals,hypnotic guitars and driving Rhythm of BONGO DANCE ready to Thrill fans at major festivals in Germany






It's the first African band to use is music as cross culture bridge from  East Africa to the World! Ngoma Africa Band wich has been named The Golden Voice of East Africa is a fast-growing band with a huge fans base worldwide.Its's the first African band to use is music as cross culture bridge from Tanzania in East Africa to the World. Ngoma Africa Band, a Tanzanian band base in Germany,founded in the year 1993 by Ebrahim Makunja also known as Kamanda Ras Makunja,named several time is the best band in many festivals. This is beacuse of the way the band presents itself Live on stage.It penetrates the souls of the fans and automatically the audience became crazy!,especially when the band applies the EXTRA ORDINARY "Bongo Dansi" or "MZIKI WA DANSI" wich simple means danceable music from Tanzania.

The Fans found rhythm unique,you only can hear this beat when the Ngoma Africa band plays.Because of this reputitation of sends fans crazy with the beats and rhythm.
Ngoma Africa band have numbers of talented musician's including mult- talented soloist Chris-B aka  ,other are Matondo Benda aka Mo Benda, Glory Mundeke,
,Aj Nbongo,Jessy Ouyah,Flora Williams,Jonathan Souza "Jojo" and others
The spirit of the Ngoma Africa Band unites with the sprits and souls of the fans and other audience. 
The Ngoma Africa Band have released the album "Mama Kimwaga"(sugar Mum),also numbers of Hit sigles CD,like Apache wacha Pombe(Stop over Drinking alcohol),Anti-Corruption Squard,Single CD "Jakaya Kikwete 2010".,and CD "Bongo Tambarare" 2013 including song "Uhuru wa Habari" (freedom of the Press),Single CD La Mgambo (2015) , Mapenzi ya Pesa (2016)and "Awamu Ya Tano Uwanjani(2018)

Most of the songs are written in various east African languages.But majority in SWAHILI or KISWAHILI the spoken language in Tanzania and its neighbouring east African countries. 
The Ngoma Africa Band bellong to the fans!Musician are just the servant'sIt's the first African band to use is music as cross culture bridge from Tanzania in East Africa to the World!
Listen songs at www.ngoma-africa.com and be connected at contact@ngoma-africa.com


WANAFUNZI WA TANZANIA VINARA UANDISHI WA INSHA EAC NA SADC.

$
0
0
Wanafunzi wa shule za Sekondari hapa nchini wameibuka washindi wa Tuzo za uandishi wa Insha zinazotolewa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ( SADC).
Akiongea mbele ya Wazazi na Walimu wa Wanafunzi waliopata ushindi wa insha hizo kwa  mwaka 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Wazara ya Elimu Dkt. Ave Maria Semakafu amesema washindi wa Tuzo hizo wametoa taswira tofauti na dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa elimu ya Tanzania si bora katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za kusini mwa Afrika.
Akifafanua Dkt. Semakafu amesema kuwa mashindano hayo ni kielelezo kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutoa elimu bora na wanafunzi walioshinda tuzo za uandishi bora wa insha wameonyesha kwa vitendo mafanikio ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta ya elimu.
‘’Matokeo ya Insha hizi pia yanaonesha picha tofauti na mawazo yaliyojengeka katika jamii kuwa shule binafsi ni bora kuliko shule za Serikali kwani baadhi ya wanafunzi kutoka shule za serikali wamejitokeza na kufanya vizuri katika mashindano ya uandishi wa insha.’’ Alisisitiza Dkt. Semakafu.
Mwanafunzi bora wa mashindano ya insha hizi kwa Jumuiya ya EAC ni Michael Msafiri  kutoka shule ya Sekondari Kibaha ya Mkoani Pwani.
Kwa upande wake Kaimu mratibu wa mashindano ya insha kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini mwa Afrika (SADC) Bw. Salum Salum amesema kuwa ushiriki wa wanafunzi katika uandishi wa insha umepanua maarifa ya wanafunzi walioshiriki katika shindano hilo.
“Maarifa ya wanafunzi yameongezeka hasa kuhusu mipango ya Jumuiya hizi na katika mchakato mzima wa mtangamano ndani ya Jumiya hizo na baina ya Jumuiya na Jumuiya” Alisisitiza Salum
Akifafanua amesema kuwa anawapongeza viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Mafunzo ya Amali Zanzibar na Baraza la Mitihani Tanzania kwa kusaidia kufanikisha mashindano hayo.
Pia alitoa wito kwa wakuu wa shule kuwasaidia wanafunzi kufuata taratibu zote za uandishi wa Insha kwa ufanisi ili kupanua wigo wa wanafunzi kushiriki katika mashindano hayo.
Hafla ya kuwatunuku tuzo washindi wa uandishi wa Insha hizo imefanyika leo mjini Dodoma ikihusisha Insha za Jumuiya ya Afrika Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bi. Ave Maria Semakafu akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako  wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya Insha kwa washindi wa kitaifa kwa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), hafla hiyo  imefanyika leo mjini Dodoma .

 Mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Kagemuya  ya Mkoani Kagera Bw. Arnold Matungwa akipokea zawadi kama mmoja wa washindi wa insha hiyo wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi  hao leo mjini Dodoma.
Mshindi wa jumla wa insha kwa wa nafunzi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki Bw.   Michael Msafiri kutoka shule ya Sekondari Kibaha ya Mkoani Pwani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bi Ave Maria Semakafu  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa insha kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), hafla hiyo imefanyika leo mjini Dodoma.
Picha zote na WEST

Timu ya Tanzania kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Australia yarejea mikono mitupu

$
0
0
 Kiongozi wa Msafara wa wachezaji waliyokwenda katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Australia ambaye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo akizungumza na kwa waandishi wa habari (hawapo picha)kuhusu hali ya mashindano pamoja na suala la mchezaji mmoja kutoroka kambini  mara baada ya kuwasili nchini leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wa Jijini Dar es Salaam.

 Bondia Selemani Kidunda (wa kwanza) akiwasilini leo jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea nchini Australia ambapo alikwenda kwa ajili ya Mashindano ya Jumuiya ya Madola  nyuma yake ni Bondia mwenzie Haruna Swanga.
 Mwanariadha wakike Bi.Sara Ramadhani akiwa amewasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini Australia ambapo alikwenda katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola na ameshika nafasi ya tisa katika mbio za Kilometa 42.
Kapteni wa Timu ya wachezaji waliyokwenda nchini Australia katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola Bw.Masoud Mtalaso (kulia) akirejesha bendera aliyokabidhiwa wakati wanakwenda katika mashindano kwa Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Alex Nkenyenge (kushoto) mara baada ya kurejea nchini leo jijini Dar es Salaam. Na Anitha Jonas – WHUSM

KATIBU MKUU MSTAAFU HAZINA RAMADHAN MUSSA KHIJJAH AZIKWA DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, ameongoza waombolezaji na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo kumzika Katibu Mkuu Mstaafu na Mlipaji Mkuu wakati wa Serikali ya Awamu ya  Nne, Marehemu Ramadhani Mussa Khijjah (pichani) , aliyefariki jana alfajiri nyumbani kwake Jet Lumo, Wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 65.
Marehemu Khijjah amezikwa katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, saa 10 jioni, na maziko yake yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, na dini, halkadhalika na baadhi ya Makatibu Wakuu Wastaafu.
Akielezea wasifu wa marehemu Khijjah, katika risala iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa ununuzi wa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Iddi Lemmah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James ameelezea masikitiko yake kufuatia kifo hicho na kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Marehemu Ramadhani Mussa Khijjah aliajiriwa na Wizara ya Fedha tarehe 06 Aprili, 1976 kwa cheo cha Mtakwimu Daraja la III na akapandishwa cheo Mnamo tarehe 01 Agosti, 1979 kuwa Mtakwimu Daraja la II, na tarehe 01 Aprili, 1981 alibadilishwa Kada kuwa Mchumi Daraja la II.
"Kutokana na utendaji wake mzuri wa kazi pamoja na uadilifu aliendelea kupandishwa cheo kuwa Mchumi Mwandamizi Daraja la I na tarehe 1 Februari, 1988 alipandishwa cheo kuwa Mchumi Mwandamizi Daraja la III. Wizara iliendelea kumpandisha vyeo ambapo tarehe 01 Agosti, 1991 alipandishwa cheo kuwa Mchumi Mwandamizi Daraja la II" ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo
Mnamo tarehe 26 Januari, 1993 aliteuliwa kuwa Kamishna wa Sera na Utafiti, cheo ambacho aliendelea kukitumikia hadi alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo ya Fedha tarehe 28 Novemba, 2002.
Tarehe 23 Novemba, 2008 aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali nafasi ambayo aliitumikia hadi alipostaafu kwenye Utumishi wa Umma mnamo tarehe 11 Juni, 2013.
Marehemu Ramadhani Mussa Khijjah alikuwa mchapakazi mwadilifu katika utumishi wake na hii imedhihirisha wazi ambapo mnamo tarehe 09 Desemba, 2012 katika Maadhimisho ya Sherehe ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mheshimiwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alimtunuku nishani ya Utumishi mrefu na maadili mema katika Utumishi wa Umma.
"Kwa masikitiko makubwa Viongozi na Wafanyakazi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango tunaungana na familia ya marehemu katika maombolezo ya msiba huu mkubwa na tunaahidi kuenzi hazina aliyotuachia" alieleza Bw. Iddi Lemmah.
Imetolewa na: 
Benny Mwaipaja
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

IGP akabidhiwa ripoti ya uchunguzi wa kuwekwa mawe na mchanga katika korosho

$
0
0
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akishuhudia Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akimkabidhi IGP Simon Sirro  ripoti ya uchunguzi wa kuwekwa mawe na mchanga katika korosho ghafi iliyosafirishwa kwenda Vietnam mjini Dodoma leo  Aprili 18.2018. Picha na Ofisi ya Waziri mkuu.


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akktana na Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB)

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Robert Bundala, nje ya jengo la utawala bungeni mjini Dodoma  leo Aprili 18, 2018. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Kilolo Mhe. Venance Mwamotona na watatu kulia ni Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wasiyoona Tanzania(TLB), Jonas Lubago. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Wadau wa dawa na vifaa tiba nchini watakiwa kuchangamkia fursa

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Josephat Kandege amewataka wauzaji, waagizaji, wasambazaji na wadau wote wa dawa pamoja na Vifaa Tiba Nchini kuchangamkia fursa inayotolewa na Serikali ya kuwa Mshitiri mteule ‘Prime Vendor’ kusaidia katika utoaji wa dawa katika Mikoa yote Tanzania.

Kandege ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Wadau wa dawa  ‘Vendors Forum’ kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na wadau wa Afya ‘HPSS’ chenye lengo la kuweka uelewa wa pamoja kuhusu uanzishwaji na utekelezaji wa mfumo wa Mshitiri.


Amesema “mfumo huu utatumika kupata mahitaji ya bidhaa za Afya pale ambapo vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma vitakosa au kupata kiwango pungufu toka Bohari Kuu ya Dawa na pia utasaidia kupunguza kero za Afya ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya”.


Sasa basi ninyi kama wazabuni muhimu katika sekta hii ya Afya wenye Uzalendo na nia njema na Nchi ya Tanzania mnatakiwa kujitokeza katika mchakato wa kumpata Mshitiri (Prime Vendor) wa kila Mkoa ambaye atakidhi vigezo kwa mujibu wa taratibu manunuzi alisema Mhe. Kandege.


Wakati huo huo Naibu Waziri Kandege aliwafahamisha wadau wa dawa kuwa Serikali imagatua mipango na bajeti kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya na inapeleka Fedha moja kwa moja kwenye akaunti za benki zilizofunguliwa katika kila kituo hii itasaidia katika kufanya manunuzi ya dawa hizo na kurahisha mchakato wa malipo.


“Hivyo niwahakikishie kuwa utaratibu wa malipo utakua ni rahisi na wa haraka zaidi kwa kuwa Hospital, Vituo vya Afya na Zahanati husika zitahusika kuagiza dawa kwa Mshitiri pale mahitaji ya dawa hizo zitakapokosekana kutoka MSD” alisema Mhe. Kandege.


Alimalizia kwa kuwataka Wadau wote wa Dawa kutumia kikao hiki kuelewa kwa undani kuhusu utaratibu huu na kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa kumpata Mshitiri Mteule kwani zoezi hili litaendeshwa kwa uwazi na kwa usindani mkubwa.


Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe amesema hivi sasa wako katika uwekezaji Mkubwa katika Sekta ya Afya kwa kuzingatia kuwa Bajeti ya Dawa imeongezwa kutoka Bil 31 kwa mwaka 2015/16 hadi kufikia Bil 269 kwa mwaka 2017/18 hivyo ongezeko hili la bajeti linatakiwa kwenda sambamba na uhakika wa upatikanaji wa dawa na zenye ubora chini ya usimamizi makini wa wataalamu wa Afya.


Dr. Ntuli alisema mpango huu utaleta manufaa kwa wananchi wote ambao watakua chini ya mpango wa Tele kwa Tele na wale wanaopata huduma kupitia mfuko wa Bima ya Afya iliyoboreshwa; Tunataka kila mmoja apate dawa anayoihitaji kwa wakati.


Naye Mfamasia toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard alisema mfumo wa Mshitiri Mteule umeanzishwa kwa sababu ya changamoto zilizoonekana awali za kutumia mzabuni kama vile taratibu za manunuzi kuchukua muda mrefu na gharama za manunuzi kuwa kubwa na zinazotofautiana kati ya Halmashauri moja na nyingine ndani ya Mkoa mmoja.


Changamoto zingine alizozibainisha ni kubadilika kwa bei mara kwa mara kila manunuzi yanapofanyika, kutokuwa na uhakika wa ubora wa bidhaa kutokana na kuhifadhiwa na kusafirishwa katika mazingira mbayo si salama na zaidi baadhi ya wazabuni na watumishi kutokuwa waaminifu.


Matumizi ya mfumo huu umeelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Sera ya Afya ya Taifa ya mwaka 2007, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya na Sera ya Mashirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.

Kikao hiki cha wadau wa dawa ‘Vendor Forum’ kimefanyika kwa mara ya kwanza na kimehusisha wadau kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
 Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele) akifungua kikao cha wadau wa Afya ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika Ukumbi wa Dodoma Hotel.
  Mkurugenzi wa Afya Ofisi ya Rais Tamisemi Dr. Ntuli Kapologwe akitoa maelezo ya awali kabla hajamkaribisha mgeni rasmi kufungua kikao cha wadau wa Afya Vendor Forum.
 Mfamasia Mwandamizi  toka Ofisi ya Rais Tamisemi Regina Richard akielezea malengo la kikao cha Wadau wa Dawa ‘Vendor Forum’ kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel mapema leo.
  Wataalam toka Idara ya Afya Ofisi ya Rais-TAMISEMI pamoja na wadau wa Dawa wakiwa katika kikao maalum cha wadau wa dawa.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege(mbele katikati) katika picha ya pamoja na baadhi ya wataalamu na wadau wa dawa.


WANAFUNZI WA KIKE VAENI MAGAUNI MANNE KWA MPANGILIO ILI MFIKISHE NDOTO ZENU - RC RUVUMA

$
0
0
Wanafunzi wakike mkoani Ruvuma wametakiwa kuzingatia masomo yao ipaswavyo kwa kufuata utaratibu wa kuvaa magauni manne ili aweze kufanikisha malengo ya ndoto zao. Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma CHRISTINA MNDEME wakati wa tathimini ya elimu mkoa ambapo mwanafunzi wa kike anatakiwa kuvaa sare ya shule toka darasa la kwanza hadi chuo kikuu HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

NEWS ALERT: Rais Magufuli amteua Prof. Idris Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini

$
0
0
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425



OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

Ikulu, Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Idris Suleiman Kikula kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kikula umeanzia tarehe 17 Aprili, 2018.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Mhe. Rais Magufuli amewateua Makamishna wa Tume ya Madini kama ifuatavyo:
  1. Bw. Doto James – Katibu Mkuu, Fedha na Mipango.
  2. Bi. Dorothy Mwanyika – Katibu Mkuu, Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
  3. Dkt. Florens Turuka – Katibu Mkuu, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  4. Mhandisi Musa Iyombe – Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
  5. Bw. Haroun Athuman Kinega – Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji wa Madini (FEMATA).
  6. Dkt. Evaristo Emmanuel Longopa – Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
  7. Prof. Abdulkarim Hamis Mruma – Mkurugenzi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafutaji Madini Tanzania (GST).
  8. Dkt. Athanas Simon Macheyeki – Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI).
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Uteuzi wa Balozi Mstaafu Njoolay umeanza tarehe 17 Aprili, 2018.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

18 Aprili, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AJULIA HALI WAGONJWA WALIOLAZWA KATIKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara Dkt. Juma Ngasongwa walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam kuwajulia hali wagonjwa leo Aprili 18, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Celestine Bulima walipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam kuwajulia hali wagonjwa leo Aprili 18, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakipata maelezo toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam Profesa Mohamed Janabi walipotembelea taasisi hiyo kuwajulia hali wagonjwa leo Aprili 18, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli nakiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam Profesa Mohamed Janabi walipotembelea taasisi hiyo kuwajulia hali wagonjwa leo Aprili 18, 2018 .Picha na IKULU

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images