Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA MKUU WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM)

0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta (katikati) alieongozana na Dkt. Kadida Mashaushi (kulia) tarehe 17 Aprili, 2018 Ofisini kwake Mjini Dodoma. 
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akikabidiwa zawadi kutoka kwa Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Tadeo Satta (katikati) alieongozana na Dkt. Kadida Mashaushi (kulia) tarehe 17 Aprili, 2018 Ofisini kwake Mjini Dodoma. 

MASAUNI AWATAKA WANANCHI KUWEKA FEDHA BENKI, AZIOMBA TAASISI ZA KIFEDHA ZA KIISLAMU AFRIKA KUONGEZA KASI KUWEKEZA NCHINI

0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Taasisi za Fedha za Kiislamu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka Watanzania kuweka Fedha zao katika Benki za Kiislamu zilizopo nchini ambazo hazina riba ili ziwasaidie katika mafanikio mbalimbali. Pia Masauni aliipongeza Taasisi hiyo kwa kuwekeza nchini. Kulia ni Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, na katikati ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Kibesse. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi za Fedha za Kiislamu Afrika, Muhammad Mughal alipokua anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake kwa Taasisi yake. Hayo alizungumza katika Mkutano wa Tano wa Taasisi hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka Watanzania kuweka Fedha zao katika Benki za Kiislamu zilizopo nchini ambazo hazina riba ili ziwasaidie kupata mafanikio zaidi. Wapili kulia ni Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, na watatu kulia ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Kibesse. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Taasisi za Fedha za Kiislamu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka Watanzania kuweka Fedha zao katika Benki za Kiislamu zilizopo nchini ambazo hazina riba ili ziwasaidie katika mafanikio mbalimbali. Pia Masauni aliipongeza Taasisi hiyo kwa kuwekeza nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimpa zawadi Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo Saqware. Kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Kibesse, kulia ni Balozi wa Nigeria, nchini, Dk. Sahab Isa Ga, na wapili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi za Fedha za Kiislamu Afrika, Muhammad Mughal. Mkutano wa Tano wa Taasisi hiyo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam, ambapo Masauni alikua mgeni rasmi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kutoka kulia mstari wa mbele), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi za Fedha za Kiislamu Afrika pamoja na washiriki wa Mkutano wa Tano wa Taasisi hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Masauni ambaye alikua mgeni rasmi katika mkutano huo, aliwataka Watanzania kuweka Fedha zao katika Benki za Kiislamu zilizopo nchini ambazo hazina riba ili ziwasaidie kupata mafanikio zaidi. Pia Masauni aliipongeza Taasisi hiyo kwa kuwekeza nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MKE WA RAIS WA ZAMANI WA MAREKANI AFARIKI DUNIA

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

BARBARA Bush mke wa Rais wa 41 wa Marekani George Herbert Bush na mama wa George W. Bush Rais wa 43 wa Marekani amefariki dunia jana April 17 akiwa na miaka 92, ofisi ya ya George H. W yathibitisha.

Bi Barbara alikuwa mhimili wa siasa kwa mumewe aliye na miaka 93 sasa pamoja na mwanaye George W.Bush aliyehudumu kama Rais wa Marekani kwa miaka minne kuanzia mwaka 2000, chanzo cha kifo chake kinaelezwa ni maradhi yaliyosababishwa na umri hali iliyompelekea kudhoofu.

Bi Barbara alizaliwa Manhattam na kuhitimu masomo yake  Ashley Hall huko Carolina Kusini, alikutana na George Herbert Bush akiwa na miaka 16 na kufanikiwa kupata watoto sita wakiwamo George W. Bush Rais wa 43 wa Marekani na Jeb Bush Gavana wa 43 wa Florida.  mwezi januari mwaka huu walitimiza miaka 73 ya ndoa

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA WATANZANIA NA WAINGEREZA JIJINI LONDON

0
0
Picha na Habari za Freddy Macha
 Ulikuwa mkutano mfupi uliokusudia kutoa shukrani kwa wafadhili na Watanzania London wanaosaidia nyumbani. Fadhila hupitia Jumuiya ya Waingereza na Watanzania  (BTS) na kitengo chake cha TDT = shirika la Mfuko wa Maendeleo Tanzania.  BTS ilianzishwa mwaka 1975, na mlezi wake sasa hivi ni Rais mstaafu Ali Mwinyi.
BTS ilimkaribisha Makamu wa Rais Mheshimiwa Suluhu Samia, aliyekuja London wiki hii kudhuruia mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Madola.

Kawaida viongozi hutegemewa  hotuba ndefu zenye maelezo yanayochosha masikio.

Mhe Suluhu alitua chuo kikuu cha lugha za Afrika na Mashariki ya Kati (SOAS)  akasalimiana na kupeana mikono na wananchi wa pande zote mbili. Hiyo tu ilitosha kuonesha imani yake kwa wananchi wachapa kazi wa pande hizi mbili.

 Makamu wa Rais Mhe Suluhu Samia akizungumza na Dk Mohammed Hamza, kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Uingereza

Balozi wa Tanzania nchini  Uingereza, Dk Asha Rose Migiro akiwa na Kaimu Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe Marc Thayre

 Mwenyekiti wa Jumuiya Ya Uingereza na Tanzania (BTS)  Dk Andrew Coulson aliyefungua na kufunga kikao cha Brunei Gallery, SOAS.

Baadhi ya Watanzania waliohudhuria katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kiondo Wilkins, Dk Alex Paurine, Simon Mzuwanda na Joe Warioba 

TAMASHA LA AMKA KIJANA, TUIJENGE IRINGA YETU LAFANA MJINI IRINGA

0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akimtambulisha mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza (mwenye ushungi) huku mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Steve Nyerere akifuatilia kwa karibu wakati wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa Mwembetogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. 
Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza, Msanii wa Bongo Movies, Steve Nyerere ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu akizungumza machache na wakazi wa Iringa juu ya kutunza Amani, Upendo na Mshikamano wetu katika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwatambulisha wasanii wa Bongo Movie waliofika katika Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu lililofanyika uwanja wa MwembeTogwa, Iringa mwishoni mwa wiki iliyopita. 
Wasanii wa Bongo movies wakipata picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mhe. Richard Kasesela na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza na viongozi wengine wa Mkoa mara baada ya kumalizika kwa Tamasha la Amka Kijana, Tuijenge Iringa Yetu.







Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda

0
0
Na Mwandishi Wetu, Dar
BENKI ya Azania imeahidi kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafanikiwa kwa kuwezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa kutimiza malengo yao katika .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azania Bank, Charles Itembe alisema benki yao imeendelea kutengeneza faida kutokana na kujihusisha kwa kiasi kikubwa kutimiza matakwa ya wateja wao.

“Tunatambua umuhimu wa malighafi katika uchumi wa viwanda, ndiyo mana tuna utaratibu maalumu wa mikopo kwa ajili ya wakulima kwa sababu bidhaa zinahitaji malighafi ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na wakulima,” alisema Itembe.

Amesema  katika ripoti yabenki hiyo ya mwaka 2017 wamepata matokeo mazuri ingawa baadhi ya benki zilipata misukosuko katika uwekezaji.  Pia amebainisha wamepata faida ya Sh bilioni 1.8 kinyume na hasara waliyoipata mwaka mmoja uliopita.

Katika kuonyesha benki hiyo ipo kwa ajili ya kuinua wajasiriamali Itembe amesema mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kiasi kikubwa ndio wanaoiendesha kwa kuwa na uwekezaji wa zaidi ya asilimia 90 hali inayoonyesha inamilikiwa na wananchi.

“Kuna ongezeko la mapato halisi ya faida ya Sh milioni 25,056 kwa mwaka 2017 kutoka ongezeko la faida la Sh milioni 22,100 iliyorikodiwa kwa mwaka 2016. Amana zimeongezeka kwa asilimia 14.8 kutoka Sh bilioni 236,380 zilizoainishwa Disemba 2016 hadi Sh bilioni 271.3 Disemba 2017,” alisema Bw. Itembe.

Aliweka wazi kuwa mafanikio hayo katika biashara yametokana na kuwa karibu na wateja wao lakini pia mipango na mikakati waliyojiwekea katika uendeshaji shughuli za kibenki ikiwemo kuhakikisha benki hiyo inakuwa kituo kinachotoa huduma zote za kifedha.

“Hii ni benki inayomilikiwa kwa zaidi ya asilimi 90 na mifuko ya hifdhi ya jamii maana yake inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi ambao wanatoa michango katika benki hizo.  Katika kudhihirisha hilo mifuko hii imetoa  ongezeko la uwekezaji wa asilimia 91.1 kwa kiasicha Sh bilioni 57,881 December, 2017; kutoka Sh bilioni 30,058 Disemba mwaka 2016,” alisema Bw. Itembe.

Akitoa historia fupi ya benki hiyo, Bwana Itembe aliema: “Azania Bank ilianzishwa mwaka 1995 wakati Tanzania ilipoamua kwa na mfumo huria wa benki, ikiwa na wawekezaji 47  ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo hadi sasa inamiliki asilimia 98 ya hisa zote ikiongozwa na NSSF inayomiliki asilimia 35.8, Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB)  asilimia 1.5 na wawekezaji  wengine asilimia 0.93.”

Ofisa Mtendaji Mkuu huyo wa Azania Bank amesisitiza kuwa ikiwa mtu ataweka fedha zake katika benkihiyo atakuwa amegeneza afya ya mafao yake ya baadaye kwa sababu mifuko ya jamii ina hisa nyingi na kuweka wazi kuwa wanataka kuwa kitovu cha huduma za fedha nchini.

Sekta ya fedha nchini imekumbwa na changamoto ya kuwa na mitaji midogo na kutengeneza hasara kutokana na masuala mbalimbali yatokanayo na mazingira ya biashara, lakini benki ya Azania imedhamiria kujikita katika kusaidia wananchi ambapo inadai ndio wanaoiendesha kupitia mifuko ya jamii.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azania Bank, Charles Itembe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu benki yao ilivyoendelea kutengeneza faida kutokana na kujikita zaidi kwenye sekta ya viwanda kwa kuwezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa kutimiza malengo.

CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi

0
0
Benki ya CRDB leo imetangaza kuanza rasmi kwa kampeni ijulikanayo kama “Furahia kandanda murua nchini Urusi” #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiaji wa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Urusi, kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo Bi. Tully Esther Mwambapa, alisema kuwa Benki ya CRDB imeanzisha kampeni kwa kushirikiana na kampuni ya Visa International ili kutoa fursa kwa wateja wake kwenda kushuhudia fainali hizo, ambazo huvutia hisia za watu wengi dunuani kote.

“Wateja wetu wenye TemboCardVisa, TemboCardVisa-Electron, TemboCard Visa-Gold, TemboCardVisa- Platinum na TemboCardVisa-Infinite, wakati wa kampeni hii watatakiwa kulipia bidhaa au huduma wanazonunua kwa kutumia TemboCardVisa zao kupitia mashine za malipo (POS) zilizopo sehemu mbalimbali kama kwenye migahawa, maduka, mahospitali, vituo vya mafuta na kwingineko, ili waweze kujishindia zawadi hii kubwa” alisema.

Bi.Mwambapa aliendelea kusema kuwa “iii mteja aweze kushinda, anatakiwa kufanya miamala mingi zaidi kila wiki na kadri mteja anavyolipia zaidi kwa kutumia TemboCardVisa yake, ndivyo anavyojiongezea nafasi kubwa zaidi ya kushinda.

Washindi wa wawili watakaokuwa wamefanya miamala mingi zaidi kila wiki watajishindia safari ya kwenda Urusi ambayo itagharamiwa kila kitu na Benki ya CRDB, ambapo jumla ya tiketi 24 zitatolewa” alisema Bi. Tully Mwambapa.

Bi.Mwambapa aliendelea kusema kuwa pamoja na washindi wawili wa kwanza kujishindia safari hiyo, Benki pia kila wiki itatangaza washindi wengine 10 kupitia vyombo mbalimbali vya habari ambao watajishindia zawadi kemkem ikiwemo luninga zitakazokuwa zimeunganishwa na kulipiwa kinga’muzi cha DSTV, jezi za timu za mataifa mbalimbali, mipira, kofia, fulana na na zawadi zingine nyingi.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akionyesha vipeperushi vya kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu. 
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitangaza kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu. 

RUVU SHOOTING WAAHIDI KUMPAPASA KILA ATAKAYEKUJA MBELE YAO

0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii

BAADA ya ushindi mfululizo wa kikosi cha Ruvu Shooting na kuanza kujikita katika nafasi za juu, Msemaji wa klabu hiyo Masau Bwire ameweka wazi huo ni mwanzo tu kwani wamejipanga kuhakikisha wanawapapasa wale wote watakaokuja mbele yao.

Katika mchezo wa Ijumaa dhidi ya Azam,Ruvu Shooting iliweza kutoka na ushindi wa goli 2-0 na kwenye mchezo wa pili uliofanyika juzi wakiwa ugenini wakipambana na Ndanda waliibuka na ushindi wa goli 3-1.

Masau amesema mchezo wao dhidi ya Ndanda waliweza kufanya 'come back' na namna walivyorudi wakiwa nyuma kwa bao moja na kusawazisha kisha kushinda mchezo wa juzi.

Katika mchezo huo uliopigwa Nangwanda Sijaona, Ndanda ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kupata bao la mapema kabla ya Ruvu kuanza kusawazisha kisha kupata matokeo.Akizungumzia mchezo huo, Masau amesema kuwa waliweza kuupiga mpira mwingi wa kiulayaulaya huku akiitaja Yanga nayo ijiandae kupapaswa pale watakapokutana.

"Tumeupiga wa kiulaya, sisi mwendo wetu ni wa kupapasa tu, hakuna kumhurumia mtu maana tumezidi kuonyesha kuwa sisi ni bora. Tunawaomba na Yanga wajiandae maana tutakutana nao hivi karibuni" amesema.

Ruvu Shooting ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda FC na kuzidi kupambania tano bora katika msimamo wa ligi.Kwa sasa Ruvu Shooting wana alama 32 wakiwa katika nafasi ya saba wakipishana alama moja na Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya sita na alama 33.

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA WANAWAKE WA COMMONWELTH MJINI LONDON

0
0
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano jana jioni alikuwa ni miongoni mwa Jopo lililojadili kuhusu sera za kumwinua mwanamke kiuchumi wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wanawake linalofanyika kama sehemu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea hapa London.

Kwenye jopo hilo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliungana na Mhe. Dkt. Joseph Muscat, Waziri Mkuu wa Malta na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ya wanawake.
 

NI MARUFUKU KURUKA NYUMBA WAKATI WA KUWAUNGANISHIA UMEME WA REA WANANCHI- DKT KALEMANI

0
0
-Wekeni hata kwenye nyumba za nyasi
Na  Tiganya Vincent
SERIKALI imesema ni marufuku kwa Wakandarasi na Wataalamu kuruka nyumba wakati wa uunganishaji wa umeme kwa wananchi kupitia  Mradi kabambe wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatuunatekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Urambo na Kaliua na Waziri wa  Dkt. Medard Kalemani wakati alipokuwa akigaua utekelezaji wa zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo hayo.

Alisema ni marufuku kuruka nyumba hata kama ni nyasi kama mwananchi anataka umeme na amelipa shilingi 27,000 za kuunganishiwa umeme.

Kalemani alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha umeme unafika katika vijiji na vitongoji vyote na kwa wananchi wote bila kubagua.

“Nawaagiza Wakandarasi na Wataalamu wote hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba kwa sababu ya kuwa imeezekwa kwa nyasi…umeme ni nyumba kwa nyuma , kaya kwa kaya.., hata kama mtu hajakamisha nyumba yake kama kuna mti karibu na nyumba yake wekeeni hata hapo ili iwe rahisi kuingiza umeme atakapokuwa amekamisha nyumba yake” alisisitiza Waziri huyo.

 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta na viongozi wengine wakikata utepe wa uzinduzi wa uwashaji wa umeme wa REA katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele jana.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akibonyesha kitufe kuwasha umeme katika Kijiji cha Jionee Mwenyewe Kata ya Songambele baada ya kukamilika kwa mradi wa uwekaji wa miundombinu katika eneo hilo.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) na Mbunge wa Urambo Magreth Sitta(kushoto) na wananchi wa kiijiji cha Jionee Mwenyewe kata ya Songambele wakishangilia mara baada ya uzinduzi wa uwashaji wa umeme katika eneo hilo jana. 
 Waziri wa Nishati Medard Kalemani akimpongeza Diwani wa Kata ya Vumilia kupitia ACT Wazalendo Kassim Shushu (kushoto) baada ya kumkabidhi eneo la shamba lake linalokadiriwa kuwa ekari moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kupozea umeme. Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

0
0
KUZIONA SIMBA SIMBA NA YANGA ELFU 7

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara(VPL) msimu wa 2017/2018 kati ya Simba na Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika mchezo huo namba 178 utakaofanyika saa 10 jioni Kiingilio cha chini kitakuwa shilingi Elfu Saba (7,000) wakati kiingilio cha juu kitakuwa shilingi Elfu Thelathini.

Jukwaa la VIP A itakuwa shilingi Elfu Thelathini (30,000),VIP B na C shilingi Elfu Ishirini (20,000) na Upande wa Mzunguko kwenye viti vya rangi ya Chungwa,Bluu na Kijani itakuwa shilingi Elfu Saba (7,000)

Tiketi tayari zimeanza kupatikana kuanzia sasa kupitia Selcom


FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM(ASFC) KUPIGWA JUNI 2,2018 SHEIKH AMRI ABEID

Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) inatarajia kuchezwa Juni 2,2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha.

Katika mashindano ya ASFC mwaka huu kumefanyika maboresho ya kuongeza zawadi ambapo awali mshindi wa pili alikuwa hapati zawadi na katika msimu huu wa mashindano hayo mshindi wa pili atajikusanyia kiasi cha shilingi Milioni Kumi huku bingwa akibeba kitita cha shilingi Milioni Hamsini.

Zawadi nyingine zitakazotolewa ni pamoja na Mchezaji bora wa mashindano atakayezawadiwa shilingi milioni Moja,Kipa Bora atapata shilingi Milioni Moja huku mfungaji Bora pia akipata shilingi Milioni Moja wakati mchezaji Bora wa mchezo wa fainali akijizolea shilingi Laki Tano.


TFF YAVITAKA VILABU KUFUATA UTARATIBU,YASISITIZA HAITASITA KUVIKATA FEDHA KWA KUKIUKA MIKATABA.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) linavitaka vilabu vyote kuwa makini na mikataba wanayoingia na Wachezaji pamoja na makocha wao.

TFF haitasita kuzikata fedha klabu zote zitakazokuwa na madeni yanayodaiwa iwe kwa kukiuka mikataba yao na wachezaji,makocha au kwa namna nyingine yoyote.

Kumekuwa na klabu zinalalamika kinyume na utaratibu tunazitahadharisha kufuata utaratibu unaofahamika kinyume cha hapo hatutasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayekiuka utaratibu.

TFF inaendelea kusisitiza kwa klabu kutoa malalimiko yao kwa njia za kikanuni ili kuepuka hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi yao kama Ibara ya 50 ya katiba ya TFF inavyozungumza pamoja na Kanuni za Maadili.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

Ikulu yaiadhibu RAS Iringa kwa kuwachapa magoli 49-8

0
0
Na Bahati Mollel-TAA, Iringa
TIMU ya Ofisi ya Rais Ikulu imewachapa bila huruma wenyeji RAS Iringa kwa kuwafunga magoli 49-8 katika mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) mkoani Iringa.
Ikulu inayofundishwa na kocha mzoefu Mary Protas ambapo wafungaji wake Fatuma Machenga aliibeba timu yake kwa kufunga magoli 48 huku Irene Elias alifunga bao moja pekee. Magoli ya RAS Iringa yamefungwa na Warda Sapal na Zitaamanzia Kididi kila mmoja manne.  
Katika mchezo wa soka timu ya RAS Iringa ilifungwa na Tumbaku ya Morogoro kwa magoli 3-0 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja w Samora.
Washindi walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Ramadhani Shegodo aliyefunga dakika ya tisa baada ya kupata pasi kutoka kwa Mohamed Mtawal; huku bao la pili lilipatikana dakika ya 29 kwa shuti  kali la Ushindi Nzogela.
Bao la tatu lilifungwa na Salum Idd katika dakika 52 baada ya kupiga krosi murua iliyomshinda kipa Mashaka Peter aliyejikuta akiusindikiza mpira langoni mwake.
Hatahivyo, Tumbaku itabidi wajilaumu kwa kukosa magoli mengi ya wazi, ikiwemo dakika ya 20 mshambuliaji wake Issa Simbaliana kukosa penalti  iliyotolewa na mwamuzi Steven Makuka baada ya Nzogele kuchezewa rafu na Dickson Kiboye wa RAS Iringa, lakini kwa kupaisha mpira juu ya goli.
 Mfungaji Fatuma Machenga (GS) wa Ikulu akifunga mbele ya mlinzi wa RAS Iringa (GK), Maria Mwita katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) Iringa. Ikulu wameshinda magoli 49-8.
 Mlinzi wa pembeni Ester Turuka (WA) wa RAS Iringa akirusha mpira kwa mfungaji wao Warda Sapal (GS) huku mlinzi Lilian Sylidion (GD) wa Ikulu akijitahidi kuzuia katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Chuo Kikuu cha Katoliki (RUCO) Iringa. Ikulu wameshinda magoli 49-8. 
  Mchezaji  Sharifa Hamis (kulia) akifanya mazoezi ya kucheza bao na Ambakisye Mwasunga (kushoto) wakifanya mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Mei Mosi kwa upande wa michezo ya jadi inayofanyika kwenye uwanja wa Somora mkoani Iringa. Katikati ni mchezaji wa mchezo wa draft Bw. Omar Said akiangalia. 
 Beki Nestory Tweve (3) wa timu ya Tumbaku ya Morogoro akitafuta njia ya kuwapita Francis Singa na Abdul Kawamba (wenye jezi nyeusi) wa RAS Iringa, katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Mei Mosi uliofanyika jana kwenye uwanja wa Samora. Tumbaku walishinda magoli 3-0. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA CHUO IFM

0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (MB) akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM),  Prof. Tadeo Satta pamoja na Uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)(haupo pichani) ofisini kwake mjini Dodoma leo Jumatano  Aprili 18, 2018.

KIKOSI KAMILI CHA YANGA DHIDI YA WELAYTA DICHA

0
0
KIKOSI cha Yanga kinashuka leo dimbani katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika wakiwa ugenini dhidi ya timu ya Welayta Dicha kutoka Ethiopia.

Yanga inayoshuka dimbani wakiwa na ushindi wa goli 2-0 walioupata wakiwa nyumbani katika mchezo uliochezwa April 7 mwaka huu.

Katika mchezo wa Kwanza Yanga waliweza kucheza bila nyota wake watatu wakitumikia adhabu ya kuwa kadi mbili za njano ambao wamejumuishwa kwenye kikosi cha kwanza cha leo.

Yanga wakiwa chini ya Kocha msaidizi Noel Mwandila na Shadrack Nsajigwa kitashuka dimban katika uwanja wa Hawasa kutafuta ushindi wa aina yoyote, sare au kutokufungwa goli zaidi ya moja.

Matokeo hayo yanambeba Yanga na wataweza kuingia katika hatua ya Makundi ya kombe la Shirikisho ambapo wataweza kujinyakulia kitita cha mamilioni.

Youthe Rostand
Hassan Ramadhan 
Haji Mwinyi
Abdallah Shaibu 'Ninja'
Kelvin Yondani

Pappy Tshitshimbi
Thabani Kamusoko
Raphael Daud
Pius Buswita

Obrey Chirwa
Yusuf Mhilu

MPRU YAPATA MTENDAJI MPYA

0
0
Na John Mapepele, Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina amemteua John David Komakoma kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu nchini (MPRU) baada ya kumsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa awali Dkt. Milali Machumu kutokana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kubaini dosari katika usimamizi wa Kitengo hicho.

Pia Waziri Mpina amevunja Bodi ya Wadhamini ya MPRU iliyokuwa chini ya Uenyekiti wa Profesa John Machiwa ambayo ilikuwa na Wajumbe nane.Mpina alisema ameamua kuvunja bodi na kumsimamisha Mtendaji huyo kwa mamlaka aliyonayo kulingana na Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Na 29 ya mwaka 1994.

Aidha Mpina amemwagiza Katibu Mkuu wa Uvuvi kuunda Kamati ya kuchunguza utendaji wa kazi wa Mtendaji wa awali.Akizungumza mara baada ya uteuzi huo Komakoma ambaye ni mtaalam wa Bailojia ya Baharini amesema atahakikisha kuwa maeneo yote ya bahari yaliyotengwa yanahifadhiwa kikamilifu ili kuleta Mchango mkubwa katika taifa letu.

“Nina imani kwamba maeneo haya ni muhimu sana kwa uhifadhi wa raslimali za bahari na utalii endelevu hivyo hatuna budi kuyasimamia kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo” alisisitiza Komakoma.Kitengo cha Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu kiliundwa na sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu  Mwaka 1994 ambapo baadhi ya majukumu yake makuu yameanishwa katika sehemu ya VI kifungu cha 10 ambayo ni pamoja na kulinda na kuhifadhi maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa bioanuai pamoja na mifumo ya ikolojia ya baharini na mwambao wa pwani.

Kuhamasisha wananchi kutumia kwa busara raslimali ambazo hazitumiki kabisa au hazitumiki kikamilifu kwa sasa, kusimamia maeneo ya bahari na mwambao wa pwani ili kuwezesha matumizi endelevu ya raslimali na ukarabati wa maeneo yaliyoharibiwa.Kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi wanashirikishwa katika nyanja zote za upangaji,uendelezaji na usimamizi wa raslimali.

Hadi sasa kuna Hifadhi za Bahari tatu na Maeneo Tengefu 15 hapa nchini katika mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Mtwara.Kabla ya uteuzi huu Komakoma alikuwa akikaimu nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Uvuvi katika Kitengo cha Udhibiti Ubora, Usalama, Viwango na Masoko ya Mazao ya Uvuvi katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Ndogo ya Kutathmini Utendaji wa Sekta ya Uvuvi katika Ziwa Victoria baada ya kukabidhi taarifa hiyo mjini Dodoma hivi karibuni.Waliokaa kuanzia kushoto Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Bonaventure Baya Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi, Dk Yohana Budeba, aliyesimama kuanzia kushoto John Komakoma Kaimu Meneja wa MPRU.


SHIRIKA LA KIMATAIFA LA WATER MISSION TANZANIA LAFANIKISHA MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA KIJIJI CHA KASANDA- KIGOMA

0
0
Kiongozi wa mbio za mwenge,Charles Kabeho akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Kasanda iliofadhiliwa na Water Mission Tanzania.
 Shamrashamra za uzinduzi wa mradi
Kiongozi wa mbio za mwenge, Charles Kabeho, akiongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Kasanda,(kushoto) ni Mkurugenzi wa Kanda wa shirika la kimataifa la Water Mission, Will Furlong Shirika la kimataifa la Water Mission Tanzania lafanikisha mradi wa maji safi na salama katika Kijiji cha Kasanda Wakazi wa kata ya Kasanda, wilayani Kakonko mkoani Kigoma, jana,wameanza kupata maji safi na salama kutokana na kuzinduliwa kwa mradi mpya wa maji chini ya ufadhili wa Shirika la kimataifa la Water Mission Tanzania. 

Mradi huu utanufaisha zaidi ya kaya 729 zinazoishi maeneo hayo. Miradi ya Kakonko na Kasanda, ni miongoni mwa miradi zaidi ya 20 ya kuwapatia wananchi maji safi na salama ambayo imetekelezwa na shirika la Water Mission Tanzania tangu mwaka 2014. Miradi ya Kasanda na Kakonko ni tofauti na ile iliyotekelezwa maeneo mengine kwa kuwa iko katika maeneo yaliyopo karibu na kambi ya wakimbizi ya Mtendeli. 

 Mkurugenzi wa Kanda wa shirika la kimataifa la Water Mission, Will Furlong alisema “Water Mission Tanzania, kupitia ufadhili wa taasisi ya Poul Due Jensen Foundation ambayo zaidi inajulikana kama, Grundfos Foundation, imewezesha ufanikishaji miradi 8 ya maji safi na salama kwa jamii mbalimbali nchini. 

Mradi mwingine wa Zeze mkoani Kigoma nao tayari umezinduliwa mwezi huu. Mashirika ya Water Mission Tanzania na Grundfos Foundation, yanashirikiana kuhakikisha huduma za maji safi na salama zinafikia jamii zenye changamoto katika kanda ya Afrika Mashariki”. 

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huu mkubwa wa maji ulioambatana na sherehe za mbio za Mwenge katika kata hiyo,Kiongozi wa mbio za mwenge,Charles Kabeho,alisema kuwa kuzinduliwa kwa mradi huo ni jambo la kihistoria kwa wakazi wa eneo hilo ambalo kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kupata maji safi na salama.

 “Kwa niaba ya serikali napenda kutoa shukrani kwa wadau wa maendeleo wanaounga mkono jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazokabili jamii kama ambavyo hawa wenzetu wa Water Mission Tanzania ,wamekuwa mstari wa mbele kufanikisha miradi ya maji sehemu mbalimbali hapa nchini”alisema Kabeho. 

Alisema kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa muda mrefu ilisababisha akina mama kutembea mwendo mrefu kutafuta maji sambamba na wananchi wengi kuathirika kwa kupata magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia maji yasio salama kwa matumizi ya binadamu. Kabeho,alitoa wito kwa wakazi wote wa eneo hilo kujiona ni sehemu ya mradi huu na kuhakikisha wanatunza miundo mbinu ya mradi wakati wote sambamba na kutoa ushirikiano kwa wataalamu wanaofanya ushauri wa uendeshaji mradi. 

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MKUTANO WA JUKWAA LA WANAWAKE

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan, jana jioni alikuwa ni miongoni mwa Jopo lililojadili kuhusu sera za kumwinua mwanamke kiuchumi wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wanawake linalofanyika kama sehemu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea hapa London.

Kwenye jopo hilo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliungana na Mhe. Dkt. Joseph Muscat, Waziri Mkuu wa Malta na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ya wanawake.

Makamu wa Rais aliweza kuelezea hatua mbalimbali ambazo serikali kali imechukua ili kumwinua mwanamke kiuchumi ikiwa pamoja na kuwapatia haki ya kumiliki ardhi, kuboresha elimu kwa mtoto wa kike, kuwapa nafasi za uongozi na pia Serikali ipo kwenye hatua za kuhakikisha  mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake.

Makamu wa Rais yupo jijini London kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano wa Jukwaa la Wanawake ikiwa Sehemu ya mkutano wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini London, Uingereza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Waziri Mkuu wa Malta Mhe. Dkt. Joseph Muscat  mara baada ya mkutano wa Jukwaa la Wanawake kumalizika  jijini London, Uingereza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

HUDUMA ZA MAJI ZAIMARIKA,TEKNOLOJIA KUONDOA MATUMIZI YA MKAA

CCM WAAMUA KUMJIBU ZITTO KUHUSU TRIL 1.5/- ,WAMTAKA AACHE TABIA YA KUPOTOSHA UMMA

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole kimesema Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe(ACT-Wazalendo) ni mpotoshaji mkubwa na vyombo vya kisheria vinastahili kumchukulia hatua.

Kimesema Ziito kupotosha kuwa kuna fedha Sh.Trilioni 1.5 za Serikali zimeibiwa si kweli na kwamba wameipitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) hakuna fedha ambayo imepota au kuibiwa na kiasi ambacho kimetajwa kwenye ripoti cha makusanyo na matumizi kipo sahihi .

"Tumepitia kwa usahihi taarifa ya CAG na kujiridhisha hakuna fedha iliyobwa kama Zitto anavyopotosha na kutaka kuaaminisha umma.Huu ni upotoshaji mkubwa na lazima tuukemee maana unaleta sintofahamu kwenye jamii."Zitto siku hizi amekuwa na tabia ya uongo.Nimetoa tafsiri yangu na kuelezea ukweli kuhusu fedha hizo anazodai kuwa hazipo.CCM hatuwezi kukaa kimya wakati kuna muongo mmoja anafanya kazi ya kupotosha na kuaminisha umma kitu ambacho si cha kweli,"amsema Polepole.

Amefafanua taarifa ya CAG kuwekwa wazi ni msimamo wa Serikali na hawana tatizo na kuongeza kwa bahati mbaya kuna utamaduni wa baadhi ya watu kila jambo la Serikali hata liwe nzuri wao lazima walififishwe Pia amekiri Serikali ya CCM imeanza kuchukua hatua kwa kuwawajibisha waliosababisha ufujaji wa fedha za umma na mtindo huo uendelee na mtu akibainika mkosaji achukuliwe hatua .

"Mkaguzi amefanya ukaguzi na kubaini kuna maeneo yanaviashiria vya ubadhirifu hatua zimechukuliwa.Uongozi wa awamu ya tano unajinasibu kwa uongozi bora ambao umejikita kwenye kufanya kazi na haupo tayari kuona ubadhirifu unafumbiwa macho uwe ndani ya Serikali, kwa taasisi za umma au binafsi na hata kwenye vyama vya siasa"amesema.

Amesema ni utaratibu mzuri na ndio maana yote ambayo CAG ameona wamekubaliana yafanyiwe kazi na kusisitiza wanafahamu Zitto amelelewa vibaya huko nyuma lakini anatakiwa kufahamu sasa ni Serikali ya Awamu ya Tano na CCM ni mpya haipo tayari kuwavumilia wapotoshaji.

"Zitto amekuwa na tabia ya uongo uongo sana, siku za nyuma alianza kuongopa kuhusu njaa wakati njaa hakuna na anaongopa kuhusu ripoti ya CAG.Vyombo vya kisheria vimchukulie hatua maana kuongopa ndani ya nchi yetu ni kosa,"amesisitiza.

RAIS DKT MAGUFULI ATOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA MRISHO GAMBO

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe Marehemu Rehema Paul Mumbuli ambaye pia ni mama  wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  leo Aprili 18, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpa pole  Muu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kumfariji kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18, 2018.
 Mama janeth Magufuli akimpa pole  Muu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kumfariji kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18, 2018.
 Mama Janeth Magufuli akimpa pole Mzee Mashaka Gumbo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kuwafariji  leo Aprili 18, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga waombolezaji baada ya kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18, 2018. Picha na IKULU
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images