Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WAZIRI MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) KUKAGUA UTENDAJI

$
0
0
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Profesa Makame Mbarawa (MB) leo tarehe 17 Aprili, 2018 amefanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.

Mhe. Profesa Mbarawa ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kwa lengo la kukagua utendaji na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Posta, katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta Luteni Kanali mstaafu Dr. Haruni Kondo.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alitaka kujionea matumizi ya mifumo ya kielektronik na namna ambavyo Shirika limejipanga kuitumia mifumo mbalimbali ili kusimamia utendaji kwa ukaribu. Mhe. Waziri Mbarawa alitembelea idara ya Fedha, Idara ya Barua na Logistiki, Idara ya Sheria, Idara ya Masoko na pia alikagua mifumo udhibiti wa gharama za mafuta na mwenendo wa magari ya Shirika yanayosafiri kati ya Dar es salaam na mikoani.

Katika ziara hiyo Mh. Waziri ameitaka menejimenti ya Shirika kusimamia utendaji kazi na kuzingatia weledi na matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akizungumza na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati alipofika kwenye Ofisi za shirika hilo, kukagua utendaji katika Idara mbalimbali za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia baadhi ya mikataba iliyoingiwa na shirika hilo. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta, Agnes Mtango. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe. 
Afisa Msimamizi wa Magari ya Shirika (Transport Officer), Mhandisi Lameck  Francis (kulia), akimweleza Waziri Profesa Mbarawa namna ya mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo, unavyofanyakazi.


TFF YASOGEZA MBELE MECHI YA SIMBA, LIPULI

$
0
0
Na Agness Francis,Blogu ya Jamii

MECHI ya wana Paluhengo Lipuli na vinara wa Ligi Simba uliotarajiwa kuchezwa  Ijumaa Aprili  20 mwaka huu katika Uwanja wa Samora Mjini Iringa imesogezwa mbele.

Mchezo huo wenye namba 202 wa Ligi Kuu ya Vodacom Lipuli dhidi ya  Simba SC  sasa hautachezwa kama tarehe ya mwanzo iliyopangwa na  (TFF).Umesogezwa  mbele kwa siku moja.

Bodi ya Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania (TFF) wameamua Mechi hiyo ichezwe Aprili 21,mwaka huu kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Samora mkoani  Iringa.

Ambapo Sababu za mabadiliko hayo ni wamiliki wa uwanja kuutumia Aprili 20, 2018 kwa shughuli nyingine za kijamii.

Ikiwa  kwa mujibu wa ratiba Mbeya City inasubiri kuvaana na  Yanga SC Aprili 22  mara baada ya kurejea.

Kikosi hicho ambacho kipo  nchini Ethiopia kuchuana na  Welaita Dicha Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mtanange huo utakaopigwa katika Dimba la Uwanja wa Sokoine uliopo Jijini Mbeya huku Mbeya city wakiwa wenyeji wa Yanga.

MVUA DAR YAKATA MAWASILIANO MIKOCHENI, DAWASCO YATOA RAI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MVUA zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam zimeendelea kuleta madhara katika maeneo ya Mikocheni barabara ya Chato mtaa wa Lukuledi  baada ya barabara hiyo kukatika na kujaa maji.

Akizungumza na Michuzi Blog, Kaimu Meneja uhusiano wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO) Everlasting  Lyaro ameeleza  maji hayo ni ya mvua na karavati  linalomwaga maji hayo ni yale yanayokusanywa maeneo  ya Mwenge, Mwananyamala na Mikocheni.

Aidha ameeleza walienda eneo la tukio  na kugundua tatizo hilo halikuwa lao bali ni watu  wa ujenzi wa barabara chini ya Manispaa na tayari suala hilo limekabidhiwa kwa makandarasi waliojenga barabara hiyo.

Pia ametoa rai kwa wananchi kwa kuwataka kuhifadhi miundombinu hasa mita zitakazosombwa na maji na watakaokumbwa na tatizo hilo watarekebishiwa mita hizo bure. Amewataka wananchi kutoa taarifa  kwa maeneo yatakayokosa huduma ili  washughulikie mara moja.

Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Abdul Rashid ameeleza  tukio hilo lilianza jana saa nane mchana baada ya magari kadhaa kupita ghafla barabara ilishuka na maji kuanza kumwagika hali iliyosababisha barabara kushindwa kupitika na ugumu wa biashara.

Hadi waandishi wetu  wanaondoka eneo la tukio sehemu ya barabara hiyo iliendelea kukatika.
 Muonekano wa   mtaa wa Lukuledi  barabara ya Chato baada ya kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam.
Mpita njia akijaribu kukwepa shimo lililopo katika barabara ya Chato, Mikocheni jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

WANAWAKE WAWILI MKOANI RUVUMA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUMILIKI MASHAMBA YA BHANGI

$
0
0
wanawamke wawili waliojulikana kwa majina ,TEOFRIDA NJAKO miaka 27 na INVOLATA KOMBA miaka 61 kabila lao ni wamatengo kutoka wilayani MBINGA,mkoani RUVUMA wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa Wanamiliki MAshamba ya bhangi hekali moja kwa kila mtuhuwa.

 Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma SACP GIMMIN MUSHY wakati akiongea na RUVUMATV. HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

RUVUMA TV: MTIA MIMBA, MTIWA MIMBA NA MTETEZI WA MIMBA WOTE NDANI

Hoja ya haja: Dawa ya adha ya mafuriko jijini Dar es salaam ni kuzibua njia ya maji bonde la msimbazi - Prof Tibaijuka

$
0
0

Anaandika Mama Prof. Anna Tibaijuka
Bila nidhamu ya kuheshimu Mipango miji mafuriko yatakuwa common feature ya jiji la DSM. Regrettably. Tatizo siyo mvua kubwa. Tatizo ni kuziba natural drainage system hivyo maji ya mvua kushindwa kwenda baharini.

Nilipokuwa Ardhi nilijitahidi sana kuokoa bonde la msimbazi kwa mujibu ya 1979 master plan. Call it the Nyerere Master plan. Sikufanikiwa. There was no political will for it. Bonde likaendelea kujengwa. Kwa hiyo maji hayana njia za kufika baharini. 
Mind you Bonde  la Msimbazi ndiyo njia pekee kwa maji yote yatokayo Pugu Hills Ukonga Airport  Tazara Tabata Kigogo magomeni Ilala kufika Jangwani grounds hadi salender bridge yanapoingia baharini. Pia maji kutoka ubungo Manzese Tandale magomeni Kagera  kinondoni hananasif Muhimbili  hadi jangwani njia ni hiyo tu moja.
Kwa upande wa chuo kikuu mto mbezi na mto mlalakuwa na mto Mdumbwi ( Kawe)  imejengwa na njia za maji kuifikia kuzibwa. 

You do not need to be an expert in urban planning to know that WATER FINDS ITS OWN LEVEL. ALSO TO KNOW THAT IN SOME YEARS HEAVY RAINS SHALL BE EXPERIENCED. ALL THESE THINGS ARE PREDICTABLE.

Mfano at Jangwani grounds tulisema lakini uharaka wa kukamilisha mradi wa DART uka overide any other consideration. Nilisikitika sana knowing it was a recipe for disaster lakini urban planning is a political activity. Without the support of political power, all knowledge and expertise go to waste. They cannot help much.
Nimeona nielezee hili kwa watu wanaotaka kujua kwa nini wataalam wametufikisha hapa. Sio wataalam. No interests. Na utamaduni wa kutoheshinu utaalam. Na wananchi kutaja quick solutions. 
Going forward lazima kurejea plan ya Mwalimu ya 1979. To salvage the Msimbazi Valley as THE CENTRAL CITY PARK. Waliojenga wawe resettled with compensation kama wanastahili. New developments in this valley ziwe arrested. 

Mama T in Dodoma Bungeni

IGP Simon Sirro atembelea kiwanda cha ushonaji cha jeshi la polisi jijini Dar es salaam

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wanaojifunza ushonaji katika kiwanda cha ushonaji kilichopo katika Bohari Kuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya ghafla kiwandani hapo ili kuona utendaji wao.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiangalia namana askari wa Jeshi hilo wakitekeleza majukumu yao kwa kushona sare za Jeshi hilo katika kiwanda cha ushonaji kilichopo katika Boharia Kuu ya Polisi jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya ghafla kiwandani hapo ili kuona utendaji wao. Picha na Jeshi la Polisi

Launch of the SADC Liaison Office in the Democratic Republic of Congo

$
0
0
The Executive Secretary of the Southern African Development Community (SADC), Dr. Stergomena Tax (right), introducing  officials of the SADC Liaison Office in the Democratic Republic of Congo (DRC), Mobhare Matinyi from Tanzania (second from left) and Ambassador Pedro Kissoka from Angola (left), to the ambassadors, representatives of the government of DRC,  political parties, religious organizations and civic societies and members of the press during the launching of the office. Second from right is SADC interpreter, Makunzi Kinguza. The ceremony was held on the night of April 16, 2018, at the Beatrice Hotel in Kinshasa. The office is expected to consult and engage stakeholders in the preparations towards holding elections in December 2018.
 Ambassadors, representatives of the government of DRC,  political parties, religious organizations and civic societies and members of the press during the launching of the office
From left are Tanzania's Ambassador to the DRC, Lieutenant General (rtd) Paul Ignace Mella; Chief of Staff in the Office of the President of DRC, Jean-Pierre Kambila Kankwende; SADC Executive Secretary, Dr. Stergomena Tax; Charge d'Affaires of the Angolan Embassy, Alberto Cabongo and the Zambian Ambassador, Friday Nyambe.

VOA Swahili: Duniani Leo 17th April 2018

Uzinduzi Wa Jarida La CHAUKIDU

TUNAKAGUA DENI LA WAGONJWA NJE-WAZIRI UMMY MWALIMU

WAKEREKETWA WA NDANDA TUSIKATE TAMAA TUSHIKAMANE,TUISAIDIE TIMU YETU ISISHUKE DARAJA

$
0
0
Wadau wa soka na wakeleketwa wa timu ya NDANDA SC wamewaomba wadau wa timu hiyo ndani ya mkoa wa Lindi , Mtwara na Tanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika kuisaidia timu hiyo kwa michango pamoja na uwajani pindi timu yao inapocheza. Wadau hao wamesema kufanya hivyo itayosaidia kuongeza hamasa kwa wachezaji sambamba nakuingiza mapato kwaajili ya uendeshaji wa timu yao.

RATIBA YA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA RC WA ARUSHA MHE. MRISHO GAMBO

WASHINDI WA 'MZUKA WA SOKA NA COKA' MOSHI NA MWANZA WAKABIDHIWA ZAWADI

$
0
0
Wateja wa vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola katika mikoa ya Kilimanjaro na Mwanza waliojishindia zawadi kupitia promosheni ya kampuni hiyo inayoendelea ya ‘Mzuka wa Soka na Coka’wamekabidhiwa zawadi zao.Promosheni hiyo inawezesha kujishindia luninga za kisasa, Pikipiki, fedha taslimu, soda za zawadi nyinginezo. Meneja Mkuu wa Masoko na Mauzo ya Kiwanda cha Bonite Bottlers ,Christopher Loiruk akikabidhi zawadi za pikipiki kwa washindi, Andrea Tarimo na Elizabeth Msangi, katika hafla iliyofanyika mjini Moshi.
Eric Masawe wa Sambarai Moshi akipokea kitita cha shilingi 100,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha wa Bonite Bottlers,Ramadhan Ananth.
Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouse shayo, akikabidhi zawadi za luninga kwa washindi
Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouse shayo,akikabidhi zawadi za luninga kwa washindi
Wakazi wa Mwanza, Ibrahim Martin na Nyamaili Werema wakiwa na luninga zao baada ya kukabidhiwa katika hafla iliyofanyika Mwanza.

THE 8TH INTERNATIONAL TÜBINGEN AFRICA FESTIVAL 2018 IN GERMANY NOW OFFICIALLY OPEN FOR REGISTRATION & PARTICIPATION.

$
0
0
 The one-year break is over, its now time to get back to business as usual and this time on a big note. The festival is now called GAIEXPO as it has included African Small and Medium enterprises worldwide. This sector shall promote the continent Africa not just as tourist but  business destination with endless opportunities in sectors such as Agriculture, Agri-business -food,Tourism, Arts and Culture etc. 
We are calling on all small businesses and enterprises, Africa and Diaspora Entrepreneurs, Traders, workshops givers, trainers, Artist, panelist... in Africa, Germany, Europe & USA to register and participate. GAIEXPO is an African market and meeting place open to countries, companys, Ngo´s with interest in sub-Sahara Africa to share contacts, information, network and do deals.  
We look forward to meeting you in Tübingen, Germany 2018 contact:



Susan Tatah Managing Director Germany-Africa International Festival (GAIEXPO)

Mzalishaji mbegu apata Tuzo ya Ujasiriamali ya Citi Foundation

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) na Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati) kwa pamoja wakikabidhi cheti kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yetu Microfinance, Attemius Millinga (kushoto) ambapo taasisi yake imekuwa na ubunifu mkubwa wa bidhaa zake sambamba na mifumo ya kutolea huduma na methodolojia wakati wa hafla fupi ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwanamke aliyefanya vyema kwenye ujasiriamali mdogo, Lucy Kiongosi akipozi baada ya kupokea cheti kilichoambatana na dola za Marekani 2000 wakati wa hafla ya tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika mwishoni wa wiki jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso.
 Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (katikati)  akikabidhi cheti kwa Mjasiriamali mdogo aliyefanya vyema mwenye umri wa miaka 18-25 tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation, Mopaya Madi (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia).
 Mshindi wa jumla wa tuzo za Ujasiriamali za Citi Foundation Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Beula Seed and Co & Sons, Zabron Mbwaga (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanzania Microfinance Association (TAMFI), Joel Mwakitalu (wa pili kushoto), Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa CITI Bank, Joseph Carasso (kulia) akikabidhi cheti kwa Ofisa mikopo Rose Chacha (kushoto) wakati wa hafla fupi za tuzo za ujasiriamali za Citi Foundation zilizofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni ni Mkurungenzi wa Fedha na Masoko wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Alexander Mwinamila.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 17.04.2018

RUVUMA TV: WAKULIMA WALIOTAPELIWA MILIONI 56 WAMEANZA KULIPWA PESA ZAO

$
0
0
Zaidi ya wakulima mia moja wa korosho katika Kijiji cha Namiungo Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma waliokuwa wametapeliwa Tani 15 za korosho zenye thamani ya Shilingi Milioni 56 na Kampuni ya ZUMA CARGO wameanza kulipwa fedha zao.

MICHUZI TV: BARABARA YA JANGWANI YAFUNGUKA RASMI

$
0
0

 Sehemu ya Magari pamoja na Watembea kwa miguu wakipita katika eneo la Jangwani, jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya kufunguliwa rasmi jioni ya leo. Eneo hilo lilifungwa kwa muda kutokana na kufurika maji yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha katika meneo mengi hapa nchini. 
 Mabasi ya Mwendo kasi yakipita katika njia yake baada ya kufunguliwa rasmi barabara ya Morogoro eneo la Jangwani, ambalo lilifungwa kwa muda kutokana na kufurika maji yatokanayo na mvua zinazoendelea kunyesha katika meneo mengi hapa nchini. 
 Sasa mabo yamerejea kama ilivyokuwa awali.
 Katapila likiendelea na zoezi la kusukuma maji ili kufanikisha kupatikana kwa njia.
 Mwendesha baiskeli akikatika eneo la Jangwani kwa mtindo wa miguu juu.

PICHA YA SIKU: MAFURIKO

$
0
0
Mmoja wa wakazi wa nyumba zilizokumbwa na Mafuriko eneo la Jangwani akiwa amelala kando ya nyumba aliyokuwa akiishi baada ya kujaa maji.

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images