Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live

HESLB KUANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO MWEZI UJAO

$
0
0
 
  • Yawakumbusha waombaji kuandaa nyaraka muhimu
  • Mwongozo wa kina kutolewa mwanzoni mwa Mei, 2018

Jumanne, Aprili 17, 2018

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu wananchi kuwa inatarajia kuanza kupokea maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi ujao (Mei, 2018) baada ya kukamilishwa kwa maboresho makubwa ya mfumo wa uombaji kwa njia ya mtandao.

Maboresho ya mfumo wa maombi
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru (pichani) amesema katika taarifa yake leo (Jumanne, Aprili 17, 2018) kuwa maombi yote yatapokelewa kwa njia ya mtandao (www.olas.heslb.go.tz) ambao umefanyiwa maboresho na Kituo cha Kompyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UCC-UDSM).

Aidha, Bw. Badru amesema dirisha hilo la litafunguliwa sambamba na kutangazwa kwa mwongozo wa kina utakaotoa utaratibu wa kuwasilisha maombi, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi, sifa na vigezo vitakavyotumika katika kuchambua na kutoa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba, 2018.

“Tunawasihi wale wote wanaotarajia kuomba mkopo wa elimu ya juu kusoma kwa makini mwongozo tutakaoutoa kwa vyombo vya habari na tovuti mwanzoni mwa mwezi Mei, 2018 na kuuzingatia,” amesema Bw. Badru.

Bw. Badru amefafanua kuwa wito wa Bodi ya Mikopo umetolewa kutokana na uzoefu wa miaka iliyopita ambapo waombaji wa mikopo waliwasilisha maombi yao bila kuzingatia mwongozo uliotolewa na kusababisha baadhi ya wanafunzi kukosa mikopo.

“Mwaka jana, kwa mfano, zaidi ya waombaji 10,027 kati ya waombaji zaidi ya 61,000 hawakuambatisha nyaraka muhimu kama vyeti vya kuzaliwa au hata vile vya vifo vilivyothibitishwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kama tulivyoelekeza,” amesema.


WASANII PELEKENI NYIMBO ZENU BASATA KWA AJILI YA UHAKIKI ILI ZIPANGIWE MADARAJA

JAJI MKUU AFUNGUA KIKAO CHA WADAU KUJADILI KAZI YA ULINGANISHO WA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA –LUSHOTO (IJA)

$
0
0
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akifungua Kikao cha Wadau Kujadili kazi ya ulinganisho wa chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) na Vyuo vingine vya Mafunzo endelevu. Kikao hicho kati ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama na Wadau wa Vyuo vingine vinavyotoa mafunzo endelevu kimelenga katika kujadili uzoefu na nafasi ya ushirikiano wa karibu baina ya Chuo hicho na Vyuo vingine vya Umma vinavyotoa mafunzo endelevu kwa Watumishi wa umma na Wadau mbalimbali katika Sekta ya Sheria, kikao hicho kilifanyika Aprili 16 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwl. Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu, Mhe. John Mrosso akiongea jambo na Wadau walioshiriki katika kikao hicho, katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali.
 Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, alipokuwa akielezea kuhusu Chuo hicho.
 Wajumbe wa Kikao walioshiriki ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora,Chuo cha Kodi n.k, Washiriki wakifuatilia kwa makini, katika kikao hicho Chuo cha Uongozi wa Mahakama kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania wamechukua maoni yote yaliyotolewa na Wadau hao na wameahidi kuyafanyia kazi katika kuboresha Mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho kwa manufaa ya Watumishi wa Mahakama na Wananchi kwa ujumla.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kikao walioshiriki ni Wawakilishi kutoka Chuo cha Dar es Salaam, Chuo cha Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora,Chuo cha Kodi n.k, aliyeketi nyuma wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila.
Picha ya pamoja ya ushiriki: aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji Mstaafu, Mhe. John Mrosso, wa pili kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Shaaban Lila, wa kwanza kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali na wa kwanza kushoto ni Mhe. Jaji Dkt. Paul Kihwelo, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA).
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)

DRFA KUENDESHA KOZI YA WAAMUZI VIJANA (U-20)

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii

CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)  kimetangaza kozi ya siku tano 5 ya waamuzi wa soka iliyoandaliwa mmahsusi kwa ajili ya vijana wenye umri chini ya miaka 20.

Akizungumza leo Ofisa Habari wa DRFA Karim Boimanda amesema  kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) na Chama cha waamuzi itawahusu zaidi vijana waliochini ya umri wa miaka 20.

Amesema kozi hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa programu ya maendeleo ya soka la vijana (Youth Development Program) ambayo ilianza kwa kozi ya ukocha wa soka la vijana iliyomalizika mwanzoni mwa Machi.

Ametaja ada ya ushiriki wa kozi hiyo inayotarajiwa kuanza Aprili 30 mwaka huu ni Sh.25000 huku msisitizo wakati wa usajili ukitarajiwa kuwekwa kwenye suala la umri.

Kozi hiyo itafanyika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume jijini Dar es Salaam na malipo yote yanatakiwa kufanyika kupitia benki ya Akiba Commercial (ACB) kwenye akaunti namba  10100548227 (DSM REGIONAL FOOTBALL ASSOCIATION) kisha kuwasilisha 'deposit slip' kwenye ofisi za DRFA kwa ajili ya kukabidhiwa risiti.

MPANGO WA ELIMU AFRIKA KULETWA TANZANIA NA PIZZA HUT

$
0
0
Mpango wa Pizza Hut wa Elimu wa Afrika Kuletwa Tanzania


Chapa kubwa ya Pizza duniani yabadili boksi zake kuwa boksi nyenkundu za kujisomea kama mradi wake wa kuhamasisha watoto kusoma duniani

KAMPENI mpya inayosafiri ya Pizza Hut Afrika inayohamasisha kusoma kwa watoto imefika jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inayoenda kwa jina la ‘Kipande cha Afrika (Slice of Africa)’ inaongozwa na Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport na timu yake ambayo wanasafiri katika miji 14 na nchi 12 barani Afrika kufuatia mchoro wenye umbo la kipande kikubwa cha chakula aina ya pizza.

“Badala ya kusambaza pizza tunasambaza viboksi vya rangi nyekundu (Red Reading Boxes) tukishirikiana na shirika lisilo la kiserikali ‘READ Educational Trust’, katika kutafuta njia za kivumbuzi za kuendeleza elimu kwa ajili ya watoto katika kila nchi,” alisema Davenport. 

“Kutokana tafiti zinazosema kwamba zaidi ya watoto milioni 280 barani Afrika hawajui kusoma, kampeni hii ni muhimu sana. Elimu na kujisomea ni fursa kubwa katika kuleta maendeleo na tumelenga kutumia ukuaji wa migahawa yetu barani Afrika ili kuleta mabadiliko katika jamii tunazotumikia.”

Katika safari yao timu hiyo ya ‘Slice of Africa’ ikiwa na wafanya biashara wa kampuni hiyo ya Pizza Hut watazindua kampeni ya kujitolea kwa wateja katika kila nchi ili kukusanya fedha zitakazojumuishwa na za kampuni hiyo ili kuweza kusambaza maboksi mengi zaidi.
Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport (kushoto) akiwa na watoto kutoka Shule ya Msingi ya Nzinga wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha watoto kusoma na kuandika wa Kiafrika ambapo walipewa boksi nyenkundu zenye vifaa mbalimbali vya kusoma na kuandika. Kampeni hii ni mradi wa kijamii wa kampuni hiyo ulioanzishwa mwaka 2016. Mradi huu uliundwa ili kuhamasisha elimu kupitia utoaji wa rasilimali na kushirikisha wateja ili kuleta mabadiliko katika jamii.
Meneja Mkuu wa Pizza Hut Afrika Ewan Davenport (kushoto) akionyesha vifaa ambavyo vitakuwa kwenye mradi wao mpya uitwao "Red Reading Boxes" kwa ajili ya kuhamasisha watoto kusoma na kuadika. Kampeni hii ni mradi wa kijamii wa kampuni hiyo ulioanzishwa mwaka 2016. Mradi huu uliundwa ili kuhamasisha elimu kupitia utoaji wa rasilimali na kushirikisha wateja ili kuleta mabadiliko katika jamii.


Benki ya CRDB kushiriki Tanzania Day nchini Marekani

RAIS DK.SHEIN AKUTANA NA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR (NEC)

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Mhe. Jecha Salim Jecha alipokuwa akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano mara walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na wajumbe wake.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akipokea Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa kipindi cha miaka mitano (ZEC) kutoka kwa Jecha Salim Jecha alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Wajumbe wa Tume yake leo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakiongozwa na Mwenyekiti  Jecha Salim Jecha mara baada ya kukabidhi  Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya  Tume hiyo leo kwa kipindi cha miaka mitano walipofika Ikulu Mjini Zanzibar. 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (katikati)   akiwa katika picha ya pamoja  na Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakiongozwa na Mwenyekiti Jecha Salim Jecha (wa tatu kushoto) mara baada ya kukabidhi  Taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya  Tume hiyo  leo kwa kipindi cha miaka mitano walipofika Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha na Ikulu)

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA PRINCE WILLIAM JIJINI LONDON

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Prince William katika jumba la Kifalme la Buckingham Palace.

Makamu wa Rais alimweleza Prince William kuwa Tanzania inatambua mchango wake katika kuzuia ujangili wa wanyama pori na Serikali ya Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbali mbali ya kupambana na kuzuia ujangili ingawa bado hatujawa na tekinolojia yenye uwezo wa wa kutambua na kuona wanyama wote lakini tumeendelea kuimarisha ulinzi wa wanyama pori.

Kwa upande wake Prince Williams alimuahidi Makamu wa Rais kusaidia katika kuboresha ulinzi wa wanyama pori kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu na pia Prince William amemualika Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano unaohusu masuala ya Wanyapori unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu jijini London.

Makamu wa Rais Mhe. Samia yupo nchini Uingereza kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi za jumuiya ya Madola.​ 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Prince Williams leo katika Jumba la Kifalme la Buckingham Palace ikiwa sehemu ya ratiba zake jijini London ambapo anamuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya za Madola. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimbidhi picha ya kuchorwa Prince Williams leo katika Jumba la Kifalme la Buckingham Palace kama zawadi na ishara ya kutambua mchango wa Prince William katika kupambana na ujangili, Makamu wa Rais yupo jijini London kumuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali za Jumuiya za Madola. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)




YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJNI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  Job  Ndugai akisisitiza jambo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Mhe. January  Makamba akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof.  Palamagamba  Kabudi akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mapema leo Bungeni mjini Dodoma. 
 Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mery Mwanjelwa akisisitiza kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa wakulima wa Korosho wanapata malipo  yao kwa wakati mara baada yakuuza  zao hilo.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mapema leo Bungeni mjini Dodoma
  Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akisisitiza jambo Bungeni mapema leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.
  Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo.  (Picha zote na Frank Mvungi-  MAELEZO, Dodoma)

UHARIBIFU WA MAZINGIRA ULIVYOCHANGIA KUONGEZA MAFURIKO KATIKA BONDE LA MTO MSIMBAZI

$
0
0

Mmoja wa Wakazi wa Dar es Salaam ambaye alikuwa akivuna chupa za maji taka zilizojaa katika Daraja la Mto Msimbazi ambapo imeonesha kuwa uharibifu wa Mazingira na utupaji  taka hovyo umekithiri katika bonde la mto Msimbazi kumechangia kuziba kwa mifereji mingi inayopitisha maji kwenda baharini.
Vijana wa jiji la Dar es Salaam wakiokota machupa katika bonde la mto Msimbazi mara baada ya machupa hayo kuletwa na maji ya mvua yaliyofurika kuja na takatka hizo
Sehemu ya takataka zilizojaa katikati ya Barabara ya Morogoro ambazo zimeletwa na maji ya mvua yaliyotapishwa kutoka mto Msimbazi.
Mmoja wa wa kazi wa Jiji akiwa amejitwika mzigo wake katika bonde la jangwani mara baada ya kuokot katika bonde la mto Msimbazi
Bibi wa makamo akiwa amejibanza katika kituo cha mabasi ya yaendayo haraka mala baada ya makazi yake kusombwa na maji katika eneo la Jangwani.

Muendesha baiskeli ya Magurudumu matatu akijaribu kiunua baiskeli mara baada ya kuteleza katikati ya barabra ya Morogoro ambapo tope limetanda mara baada ya tope kutapika kwenye mwendokasi

MAMBOSASA AELEZEA NAMNA ALIVYOMKAMATA DIAMOND KABLA YA KUMUACHIA KWA DHAMANA

$
0
0

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ameeleza  namna ambavyo wamemkamata na kumhoji msanii maarufu Nassib Abdul a.k.a Diamond  na kisha kumuachia kwa dhamana.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na Michuzi blog,Kamanda Mambosasa amesema alimakata Diamond jana kati ya saa 11 na saa 12 jioni na kisha walimhoji kutokana na kusambaza picha za utupu katika mtandao.

"Polisi tumemshikilia Diamond na kisha tukamhoji kwa kusambaza picha za utupu mtandaoni,"amesema Mambosasa na kuongeza kuwa hilo ni kosa la kimtandao hivyo sheria itachukua mkondo wake.

Alipoulizwa kama Diamond bado anashikiliwa Polisi au laa, Mambosasa amejibu baada ya kumhoji walimuachia kwa dhamana wakati upelelezi ukiendelea."Upelelezi ukikamilika tutaendelea na hatua nyingine za kisheria,"amesisitiza.

Tigo yamwaga zawadi washindi 84 promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus jijini Dar es Salaam leo

$
0
0


Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya kukabidhi simu janja aina ya Tecno R6 kwa washindi 52 kutoka Dar es Salaam wa wiki hii katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Tatu Shomari Kandi (kati) mjasirialimali n amkaazi wa Tabata jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Mariam Yatela Omari (kati), mhudumu wa saluni katika eneo la Kisarawe, Dar es Salaam baada ya kuibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Boni Japhet Sanga (kati) mjasirialimali n amkaazi wa Tabata jijini Dar es Salaam baada ya kuibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni ya Tigo Nyaka Nyaka Bonus jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtaalam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA IRAN

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza mgeni wake Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian (wa pili kulia), ugeni kutoka Bunge la Iran ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.  Kulia ni Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang na Afisa kutoka ubalozi wa Iran nchini Tanzania Ndg. Maisara Ally (wa pili kushoto)
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na mgeni wake Mwenyekiti wa kamati ya urafiki baina ya Bunge la Tanzania na Iran, Mhe. Dkt. Ardeshir Noorian (wa pili kulia), Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang (kulia) na Afisa kutoka ubalozi wa Iran nchini Tanzania Ndg. Maisara Ally (wa pili kushoto) walipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

DC MATIRO AONGOZA MKUTANO WADAU WA CHANJO SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI MKOA WA SHINYANGA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro amefungua na kuongoza mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga uliolenga kujadili namna ya kufanikisha zoezi la chanjo hiyo kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 mkoani humo. 

Mkutano huo umefanyika leo Jumanne Aprili 17,2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.

Akifungua mkutano huo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga alisema Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa chanjo imeanzisha chanjo mpya ya kuwakinga na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14.

Matiro alisema saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza nchini Tanzania kwa kusababisha vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti ambazo zote zinasababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akina mama vitokanavyo na saratani hivyo kunahitajika juhudi na ushirikiano zaidi kupunguza vifo hivyo.

“Lengo la kuanzisha chanjo hii ni kukinga mabinti kutokana na madhara makubwa yanayoweza kuwapata ambayo husababisha vifo vingi kwa wanawake,na walengwa wa chanjo hii mwaka huu ni wasichana wote wanaotimiza miaka 14 ambapo katika mkoa wa Shinyanga wasichana wasiopungua 29,479 watachanjwa”,aliongeza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga 
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dkt. Rashid Mfaume akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga. 
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Shinyanga.

UAMUZI KESI MBOWE, WENZAKE KUPELEKWA MAHAKAMA KUU AU LAA KUJULIKANA MEI 15

$
0
0

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

UAMUZI wa kesi inayowakabili viongozi 9 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ya kufanya maandamano/mkusanyiko usio halali unatarajiwa kutolewa Mei 15 mwaka huu kama iende Mahakama Kuu au laa.

Hatua hiyo inatokana na mvutano wa hoja za kisheria zilizotolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kisha kujibiwa leo na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Hata hivyo majibu yake Wakili Nchimbi ameiomba Mahakama hiyo kutupilia mbali hoja za utetezi zilizotolewa na Kibatala kwa madai zitasababisha ucheleweshaji wa shauri hilo.Nchimbi amefafanua kwa kudai mazingira ya mwenendo wa kesi hiyo toka ilipoanza hadi leo hakuna swali lolote la msingi lililoibuliwa na upande wa utetezi ambalo linajikita na uvunjifu ama ukiukwaji wa haki ya kikatiba.


SERIKALI YAELEZA UTEKELEZAJI HOJA ZA CAG SEKTA ZA AFYA NA ELIMU

$
0
0
Ahadi hiyo imetolewa mjini hapa leo na Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia walipozungumza na waandishi wa habari kueleza utekelezaji wa hoja za CAG katika sekta zao.

  Waziri Ummy: Tunakagua Deni la Wagonjwa Nje

Akieleza utekelezaji wa hoja mbalimbali katika sekta ya Afya, Waziri Ummy ameeleza kuwa Wizara ya Afya, baada ya kupata taarifa ya CAG kuhusu kuongezeka kwa deni la matibabu ya wagonjwa wanaopata rufaa nje ya nchi, imeamua kufanya uchunguzi wa kina wa kitabibu na kihasibu kujua usahihi wa deni hili ili kuchukua hatua madhubuti.

Aidha, amesisitiza kuwa Wizara imekubaliana na ushauri wa CAG wa kuhakikisha Serikali inaendelea kuboresha utoaji wa huduma za kibingwa hapa hapa nchini nchini ili kupunguza gharama. Waziri Ummy ameeleza hatua mbalimbali zilizochukulia kutekeleza agizo hilo ikiwemo kuanza kutolewa hapa nchini huduma za upasuaji wa moyo, upandikizaji wa figo, uwekaji wa vifaa vya usikivu na matibabu ya magonjwa ya mifupa na mishipa ya fahamu.

Kwa upande wa huduma za kibingwa katika maradhi ya saratani, Waziri Ummy alisema tatizo kubwa lililopo sasa ni huduma za kiwango cha juu cha kupima ugonjwa huo ambazo hazipatikani sehemu nyingi za Afrika. Hata hivyo alisema katika mwaka mmoja ujao Tanzania itamaliza tatizo hilo kwani Serikali imetenga Shilingi bilioni 14.5 mwaka ujao wa fedha kununua mashine ya kupima saratani (PET-CT-SCAN) 
.
Kuhusu uingizwaji wa bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 1.94 kwa kutumia vibali vya kughushi, Waziri Ummy amesema wameshachukua hatua za haraka kupitia Bodi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwabaini wote waliohusika na tayari baadhi wameshakabidhiwa kwenye vyombo vya dola huku TFDA ikichukua hatua za kujiunga na mfumo wa TRA ili kutambua nyaraka zisizo halali.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akijibu hoja zilizotolewa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za  Serikali (CAG)kwa mwaka wa fedha unaoishia june 2017. Mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,  Prof. Joyce Ndalichako akitioa maelezo kuhusu kuhusu mafanikio ya Wizara hiyo hasa katika ukusanyaji wa mikopo iliyoiva kwa wanafunzi wa elimu ya juu wakati akijibu  hoja zilizotolewa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za  Serikali (CAG)kwa mwaka wa fedha unaoishia June 2017. Mapema leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kabla yakuwakaribisha Mawaziri kushiriki katika mkutano na Waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu hoja mbalimbali zinazogusa Wizara zao katika ropoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia June 2017.
Serikali imesisitiza kuwa hakuna hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika sekta zote na hususani sekta za Afya na Elimu ambayo haitatekelezwa ili kuhakikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafikiwa ipasavyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMPUNI 30 KUTOKA UFARANSA KUJADILI UWEKEZAJI NCHINI TANZANIA .

MAONYESHO VIVUTIO VYA UTALII YAAANZA BEIJING NCHINI CHINA

$
0
0
Na Ripota Wetu, China
MAONESHO ya vivutio vya utalii (China Outboard Travel & Tourism Market – COTTM) kwa mwaka 2018 yameanza leo jijini Beijing China, na kuhusisha  mataifa zaidi ya 150. Tanzania imewakilishwa na Bodi ya Utalii kwa kushirikiana na  Kamisheni ya Utalii Zanzibar wakiambatana na baadhi ya kampuni ya kitalii hapa nchini.

Akizungumza kwa niaba ya  Bodi ya Utalii nchini, Irene  Mville ambaye pia ni Ofisa Utalii habari ameeleza lengo la maonesho hayo ni kutangaza utalii, ambapo Tanzania  inatumia  fursa hiyo kutangaza vivutio vinavyopatikana nchini.  Ameitaja China kama  soko jipya wanalopatikana watalii.

"Kwa kadri uchumi wa China unavyozidi kukua ndivyo idadi ya watalii kutoka China itazidi kuongezeka.  Mwaka 2016 Wachina milioni 120 walikwenda nje ya nchi kutalii na kutumia dola za Kimarekani Bilioni 1.2.

"Hivi sasa nyumbani Tanzania tunaendelea kupokea watalii kutoka China. Idadi ya watalii waliokwenda mwaka 2016 ni 37,000. Ukilinganisha na milioni 120 hiyo idadi ni ndogo sana,"amesema Irene

Aidha,amepongeza ushirikiano mkubwa na hatua kadhaa ambazo zimekuwa zikichukuliwa na ubalozi wa Tanzania nchini China ikiwa ni pamoja na uwepo wa maonesho na makongamano ya kitalii  na kutumia mitandao ya kijamii ya China  kutangaza vivutio vya utalii nchi yetu.
Afisa  Habari - Utalii (Bodi ya Utalii Tanzania) Bi.Irene F.Mville (Kushoto) akizungumza na baadhi ya Wateja waliojitokeza kwa nia ya Utayari wa Kupata taarifa juu ya Vivutio vya Utalii nchini  Tanzania kwenye maonyesho ya vivutio vya utalii yaliyofanyika jijini Beijing nchini China.
 Afisa Mipango kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bw.Hassan Ameir Vuai (Katikati) akitoa huduma kwa moja ya wateja waliotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho ya vivutio vya utalii yaliyofanyika jijini Beijing nchini China.
 Afisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Eugen S. Malley (kulia) akifafanua jambo mara baada ya kutembelewa na wadau wa Utalii katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya vivutio vya utalii yaliyofanyika jijini Beijing nchini China.
Mkurugenzi wa Hango Trade Company  ambaye pia ni Mtanzania anayesoma nchini China  Bi.Angelina Makoye akitafsiri lugha ya kingereza kwenda kichina wakati akielezea fursa za  Utalii  zilizopo nchini Tanzania kwenye maonyesho ya vivutio vya utalii yaliyofanyika jijini Beijing nchini China.
Umati mkubwa ukiwa umefurika katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya vivutio vya utalii yaliyofanyika jijini Beijing nchini China.
Moja ya Kampuni inayojishughulisha na Shughuli za Utalii hapa nchini, wakimhudumia mteja aliyetembelea Kampuni hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Prof. Ndalichako Atoa Maagizo kwa Watendaji kufuatia ripoti ya CAG, aainisha mageuzi Bodi ya Mikopo

MAVUNDE AMWAGA NEEMA KWA WAJISIRIAMALI DODOMA,AWATAKA WACHANGAMKIE FURSA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe.Anthony Peter Mavunde ameahidi kuwapatia vikundi vya wajasiriamali mafunzo ya UJASIRIAMALI na kuviwezesha vikundi katika kata zote 41 zilizopo Jimbo la Dodoma Mjini.

Mavunde ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Cavillam wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyowashirikisha zaidi ya wajasiriamali 2000 kutoka viunga mbalimbali vya Manispaa ya Dodoma,ambapo mafunzo hayo sasa yataanza kutolewa kwa kila kata  ili kuhakikisha idadi kubwa zaidi ya wajasiriamali inafikiwa na kupata mafunzo haya yenye lengo la kumuandaa mjasiriamali wa Dodoma kupata ujuzi wa utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.

Aidha Mavunde amewataka wajasiriamali hao kutumia fursa za ujio wa shughuli za Serikali Mjini Dodoma kama sehemu ya kukuza uchumi wao na kujiletea maendeleo binafsi.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo hayo,Mkurugenzi wa Taasisi ya MJASIRIAMALI KWANZA , Dk.Mujungu amemshukuru Mbunge Mavunde kwa udhamini wa mafunzo hayo na pia kumpongeza kwa kugawa mashine ndogo ndogo zenye thamani ya Tsh 55,000,000 kwa Vikundi vya Wajasiriamali katika kata 31 za Manispaa ya Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akifungua Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyowashirikisha zaidi ya wajasiriamali 2000 kutoa viunga mbalimbali vya Manispaa ya Dodoma.
 Baadhi ya wajasiriamali walioshiriki mafunzo.
 Baadhi ya wajasiriamali walioshiriki mafunzo.
 Wajasiriamali walioshiriki.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na mmoja wa washiriki wa semina.
Viewing all 109984 articles
Browse latest View live




Latest Images