Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600 MKOANI GEITA

0
0
Na Veronica Kazimoto, Geita.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesajili jumla ya wafanyabiashara wapya 600 katika kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyofanyika mkoani Geita ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Menenja wa TRA mkoani hapa James Jilala ameishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa kufika mkoani Geita hususani katika maeneo ambayo hakuna ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na kufanikiwa kusajili wafanyabiashara wengi ndani ya wiki moja.

“Nianze kwa kuishukuru Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa hatua ambayo mmeifanya ya kufika katika Mkoa wetu wa Geita hasa maeneo ambayo hatuna ofisi ya TRA na kufanikiwa kusajili wafanyabiashara wengi kwa muda mfupi kitu ambacho kimekuwa historia kwetu,” alisema Jilala.

Jilala alisema kuwa, baadhi ya wafanyabiashara walishindwa kusajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa wakati, kwasababu walitakiwa kusafiri zaidi ya kilomita 100 kwenda Geita mjini kwa ajili ya kupata huduma hiyo. Hivyo, zoezi hili limewarahisishia wafayabiashara kusajiliwa na kupatiwa TIN.

Naye Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Gabriel Mwangosi alisema kuwa , pamoja na usajili wa wafanyabiashara hao, shughuli mbalimbali zimefanyika katika kampeni hiyo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kupitia semina na kuwatembelea katika sehemu zao za biashara.

“Katika zoezi hili tumefanya shughuli nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuwatembelea wafanyabiashara mahali wanapofanyia biashara zao, tumesajili wafanyabiashara wapya na tumetoa semina mbalimbali ambazo tunaamini kabisa zitakuwa zimebadilisha mtizamo, utendaji na mwenendo mzima wa ulipaji kodi katika Mkoa huu wa Geita,” alieleza Mwangosi.

Kampeni ya huduma na elimu kwa mlipakodi ni moja ya mikakati ambayo Mamlaka ya Mapato Tanzania imejiwekea katika kuhakikisha kuwa inasajili wafanyabiashara 1,000,000 katika mwaka huu wa Fedha wa 2017/18.
Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwasajili wafanyabiashara wapya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi, kusajili wafanyabiashara wapya, pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Afisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Lameck Ndida akitoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi kwa wafanyabiashara wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki ikiwa na lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kodi, kusajili wafanyabiashara wapya, pamoja na kusikiliza malalamiko, changamoto na maoni kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita James Jilala (kulia) akijadiliana jambo na Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Gabriel Mwangosi wakati wa kampeni maalum ya utoaji huduma na elimu kwa mlipakodi iliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Geita. Katikati ni Afisa wa Kodi Mwandamizi wa TRA Makao Makuu Maternus Mallya.

Libeneke pekee la ufugaji nchini laja na app mpya

0
0
Daktari wa Mifugo na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Dkt. Augustino Chengula, amekuja na app yake  ya UFUGAJI inayopatikana google play store. App hii ni ya tovuti ya ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali pamoja upampanaji wa magonjwa. Tovuti yake ni ufugaji.co.tz. Hii ni tovuti pekee nchini iliyoshheeni elimu muhimu sana ya ufugaji. 
Link ya App play store ni hii hapa

Huduma ya ‘Total wash’ yazinduliwa Dar

0
0
Total ambayo ni moja ya makampuni ya mafuta yanayoongoza nchini, imezindua huduma mpya na maalumu ya kuosha magari ijulikanayo kama “Total Wash” ambayo kwa sasa inapatikana katika vituo vya Africana, East Oysterbay na Port Access Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mauzo wa Total Tanzania, Nikesh Mehta alisema huduma hiyo mpya ina lengo la kuboresha huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwani wateja wataoshewa magari yao kwa haraka zaidi kwa kupitia utaalamu wa ‘jet wash.

“Tunalo lengo pia la kuhakikisha kuwa huduma zote zinapatikana katika kituo kimoja hasa kwa wateja wa Total ambao hawana muda mrefu wa kusubiri tutahakikisha wanapata huduma iliyo bora baada ya kujaza mafuta na kupata huduma nyingine za kiufundi tunazotoa,” alisema.

Alisema huduma hiyo imepokewa vizuri na wateja katika vituo vya Africana, East Oysterbay na Port Access.

“Kuna sehemu nyingi za kuosha magari lakini huduma hii ni ya kipekee kutokana na utaalamu na teknolojia inayotumika ambayo itahakikisha wateja wa Total wanapata huduma iliyo bora na ya viwango vya juu,” alisema na kuwataka wateja wengi zaidi wajaribu huduma hiyo.

Alisema kwa wateja wanaohitaji kutumia huduma hiyo, wanatakiwa kununua sarafu maalumu (token) katika maduka ya Total (Café Bonjour) yanayopatikana katika vituo vyao na kila sarafu itakuwa na kipimo cha muda kulingana na huduma inayotolewa..

Bw. Mehta alisema wana mpango wa kuanzisha huduma hiyo katika vituo zaidi nchini katika siku za hivi karibuni.

Total ina vituo 90 nchi nzima na inajivunia kwa kuuza mafuta na vilainishi vyenye ubora wa hali ya juu kama vile Total Quartz, Total Rubia na Special 4T lakini pia inajivunia kutoa huduma zinazoaminika na kukubalika kote.
Mmoja wa wahudumu wa Total akiosha moja ya magari kwa kutumia teknolojia mpya ya 'jet wash'.

TASAF YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUJADILI UTEKELEZAJI MPANGO KUNUSURU KAYA MASKINI-PSSN.

0
0
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF- na wadau wa Maendeleo wameanza mkutano jijini Dar es salaam kupitia pamoja na mambo mengine utekelezaji wa Shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ------PSSN- unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF. 

Pamoja na Mkutano huo ulioanza leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam , wadau hao wa Maendeleo,maafisa wa serikali na wenyeji TASAF watatembelea mkoa wa Kagera,Shinyanga,Manyara,Unguja,Pemba na Tanga ambako watakutana na viongozi wa serikali na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kujionea namna Mpango huo unavyoendelea kuchangia uboreshwaji wa Kaya za Walengwa. 

Utaratibu wa serikali kupitia TASAF kukutana na Wadau wa Maendeleo hufanyika kila baada ya miezi sita kwa lengo la kutathimini utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ulioanza kutekelezwa mwaka 2012 Tanzania Bara, Unguja na Pemba. 

Hadi sasa takribani Kaya za Wanufaika Milioni Moja na Laki Moja zimeandikishwa kwenye Mpango ambapo licha ya kupata ruzuku inayotolewa kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili, walengwa hao wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli za kujiongezea kipato kupitia utaratibu wa Ajira ya Muda, Mpango wa kuweka akiba na kukopeshana kupitia vikundi kama njia mojawapo ya kujiimarisha kiuchumi. 

Aidha Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unatekelezwa kupitia Kaya Maskini ambazo zilibainishwa na wananchi wenyewe kwenye maeneo yao kwa sasa unatekelezwa katika asilimia 70 ya vijiji nchini kote wakati jitihada za kutafuta fedha ili kukamilisha asilimia 30 ya vijiji viliyosalia zinaendelea. 

Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa kwenye mkutano huo zinaonyesha kuwapo kwa mafanikio makubwa kwa walengwa ambao wengi wao wameanza kujiwekea rasilimali ambapo mifano ya uboresha makazi,kupata uwezo wa kuhudumia kaya zao,elimu na afya zimebainishwa kupatikana kwa kaya za walengwa . 

Zifuatazo ni picha za wadau wa Maendeleo na maafisa wa serikali na TASAF wakiwa kwenye Mkutano wao ulioanza leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF, Amadeus Kamagenge(aliyesisima) akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Maendeleo na Serikali ulioanza leo mjini Dar es salaam . 

Kiongozi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Mohamed Muderis (aliyesimama) akitoa maelezo kwenye Mkutano wa Wadau wa Maendeleo,Serikali na TASAF unaojadili maendeleo ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.


Baadhi ya Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa TASAFna Serikali wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Baadhi ya Wadau wa Maendeleo,Maafisa wa TASAFna Serikali wakiwa kwenye Mkutano wa kujadili Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 

MPINA AWATAKA WAWEKEZAJI VIWANDA VYA PUNDA KUONGEZA BEI

0
0
Na John Mapepele, Dodoma 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewataka wawekezaji wa viwanda vya kuchinja Punda nchini kupandisha bei ya kununua wanyama hao badala ya shilingi laki mbili ya sasa kwa punda mmoja ili kudhibiti utoroshaji wa mifugo nje ya nchi ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya mifugo elfu kumi inatoroshwa mipakani kwa siku kwenda nje ya nchi inakonunuliwa kwa bei ya juu. 

Akizungumza leo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika Kiwanda cha Punda cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma alichokifungua hivi karibuni, Waziri Mpina alisema bei hiyo haiendani na gharama halisi ya ufugaji wa Punda hali inayowafanya wafugaji kuwatorosha mifugo na kulikosesha taifa mapato makubwa. 

Alisema ili punda aweze kufikia hatua ya kuchinjwa inachukua kiasi cha miaka miwili ambapo gharama zake za ufugaji zinakuwa juu ukilinganisha na bei ya shilingi laki mbili anayouzwa kwa wenye viwanda vya punda nchini.

Aidha alisema kumekuwa na utoroshaji mkubwa wa mifugo wanaokadiriwa kufikia takribani 1,614,035 kwa mwaka unaofanyika kwenye mipaka ya nchi yetu ambapo takribani shilingi bilioni 32.28 zinapotea kama ushuru na takribani shilingi bilioni 24.21 zinapotea kutokana na kodi ya mapato ambayo ingelipwa kwa nyama ambayo ingeuzwa hapo nchini. 

Aidha Mpina ameunda tume ya wataalam kutoka Wizarani kwa ajili ya kuja kufanya tathmini kama kiwanda hicho kimetimiza masharti yote yaliyotolewa na Serikali baada ya kukifungua Februari mosi mwaka huu ambapo alisema ikibainika kuwa kiwanda hakijakidhi masharti yaliyotolewa na Serikali kitachukuliwa hatua kali zaidi za kisheria ikiwa ni pamoja na kukifungia kufanya kazi zake. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani) akikagua kiwanda cha kuchinja Punda cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma alichokifungua hivi karibuni leo. (Picha na Jumanne Mnyau) 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani) akipokea maelezo ya usindikaji wa nyama Punda kutoka kwa mfanyakazi wa wa kiwanda cha kuchinja Punda cha Hua Cheng Limited Elizabeth Peter.(Picha na Jumanne Mnyau) 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina(mwenye miwani) akitembezwa katika kiwanda cha kuchinja Punda cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma alichokifungua hivi karibuni na Meneja Mkuu wa kiwanda hicho bwana Xun Long Go .(Picha na Jumanne Mnyau) 

UMOJA WAFANYABIASHARA UJERUMANI WATUA NCHINI KUFUNGUA OFISI YA URATIBU WAWEKEZAJI

MVUA YAUA WATU NANE DAR , MAKONDA ATOA TAHADHARI

0
0

*Ashauri wanafunzi wasiende shule kwa siku mbili, waliokuwa majumbani nao wakae huko huko

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MVUA zinazoendelea kunyesha katika Jiji la Dar es Salaam imesababisha vifo vya watu nane katika Jiji hilo huku miundimbinu ya barabara nayo ikiharibiwa.

Akizungumza kuhusu athari za mvua ambazo zinaendelea kunyesha jijini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema taarifa ambazo anazo ni kwamba kuna watu 8 wamekufa kutokana na mvua hizo.Amefafanua taarifa rasmi itatolewa kwani kinachoendelea sasa ameagiza kata zote kufanya tathimini ya athari za mvua hizo.

Ameongeza vifo hivyo vimetokana na mafuriko katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ameeleza ipo haja ya wakazi wa Jiji hilo kuhakikisha wanakuwa makini katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.

"Mvua hizi zimesababisha maafa ambako taarifa ambazo ninazo kuna watu 8 wamefariki dunia kwasababu ya hizi mvua.Tutatoa taarifa rasmi baadae.Pia mvua zimesababisha kuharibika kwa miundombinu na barabara nyingi kutopitika,"amesema Makonda wakati anazungumzia athari za mvua akiwa eneo la Jangwani jijini Dar es Salam ambako eneo hilo maji yamejaa.

Pia Makonda amesema athari za mvua hizo zingeweza kuwa kubwa zaidi iwapo watu wangetoka majumbani kwao, na hivyo ameshauri ni vema Walimu wakuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakatoa ruhusa kwa siku mbili ili wanafunzi wasiende shule ili kuepuka maafa kwani baadhi ya magari yamekuwa yakitumbukia mtoni.

"Nito rai kwa walimu wakuu na hasa kwa Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam kuwapa taarifa walimu wa shule zote kuwa kwa siku mbili hizi yaani Jumanne na Jumatano wanafunzi wasiende shuleni.

"Hii itasaidia kupunguza maafa ambayo yanaweza kutokea kwa kuruhusu watoto waende shule huku tukijiua miundombini yetu haiko salama.Kwa wale ambao wako mabodeni nishauri waondoke huko kwani wanaweza kupata athari zaidi na kwamba hakuna sababu ya kupanda juu ya paa la nyumba kulinda bati,"amefafanua Makonda.

Makonda ameitumia siku ya leo kufanya ziara ya kuzunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambako ameshuhudia namna ambavyo mvua hiyo imeleta madhara katika maeneo mbalimbali ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha hawajengi kwenye njia za maji na kubwa zaidi kutunza mazingira.

SERIKALI KULINDA THAMANI YA SHILINGI KWA KUONGEZA THAMANI YA BIDHAA ZA NDANI

0
0
Na: WFM

Serikali imeeleza kuwa inalinda thamani ya Shilingi kwa kudhibiti mfumuko wa bei ya huduma na bidhaa, kuhamasisha usafirishaji na uuzaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani nje ya nchi kupitia program ya “Export Credit Guarantee Scheme” na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima ya fedha za Kigeni.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Devotha Mathew Minja aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kulinda thamani ya Shilingi kwa kuwa wapo wamiliki wa majengo ambao wanapangisha majengo kwa kutumia fedha za kigeni kama vile Dola ya Kimarekani badala ya fedha ya Kitanzania hivyo kusababisha kuendelea kuporomoka kwa thamani ya shilingi.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa matumizi ya fedha za kigeni sambamba na Shilingi ya Tanzania hapa nchini yanasimamiwa na Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Kigeni ya mwaka 1992 (The Foreign Exchange Act, 1992), Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya Mwaka 2006 na Tamko la Serikali la mwaka 2007 kuhusu matumizi ya fedha za kigeni kulipia bidhaa na huduma katika soko la ndani.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa mwezi Desemba 2017, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), alitoa tamko kwa umma kuwa kuanzia Januari Mosi, 2018 bei zote hapa nchini zitangazwe kwa Shilingi ya Tanzania zikijumuisha kodi ya nyumba za kuishi na ofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, bei ya vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.

“Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni, ambapo zinajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, visa kwa wageni na gharama za viwanja vya ndege na hoteli, hata hivyo wageni hao wanapaswa kutambuliwa kwa vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa Kampuni”. Alieleza Dkt. Kijaji.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji


MATUKIO KATIKA PICHA WAZIRI MKUU MJINI DODOMA LEO APRIL 16,2018

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Mkwawa Iringa .katika Viwanja vya Bunge Dodoma leo April 16/2018 kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mbunge wa Viti Maalumu Rita Kabati
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana mawazo na Mbunge wa Kuteuliwa Mama Salma Kikwete. katika Viwanja vya Bunge Dodoma leo April 16/2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimia na Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Khadija Shabani. katikati mwenye Miwani wakiwa pamoja na Mjasilia mali , Warda Obathan. katika Viwanja vya Bunge Dodoma leo April 16/2018.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana mawazo na Mbunge wa Viti Maalumu Upendo Peneza. katika Viwanja vya Bunge Dodoma leo April 16/2018. .PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

MAKAMU AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA KIMATAIFA JIJINI LONDON

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amkutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza  Mhe. Penny Mordaunt .
Makamu wa Rais ambaye amewasili nchini Uingereza leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Katika mkutano wake na Waziri huyo wa Uingereza Makamu wa Rais alielezea hatua kubwa iliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Elimu mara baada ya kuamua Elimu iwe bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
Pia Makamu wa Rais alishukuru mradi wa DFID unatekelezwa mkani Simiyu na kuomba mradi huo uongezewe maeneo ili uweze kuwanufanisha watoto wengi wa kike.
Makamu wa Rais pia alizungumzia namna Majukwaa ya Kuwawezesha wanawake kiuchumi yanavyofanya kazi huku taratibu mbali mbali zinafanyika ili mabenki yaweze toa mikopo kwa riba nafuu.
Mwisho Makamu wa Rais alizungumzia jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kuboresha Mazingira ya kufanya Biashara nchini.
Naye Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada wanazofanya katika kuboresha huduma za kijamii, alisema nchi yake ipo tayari kusaidia katika masuala ya makusanyo ya kodi, kuboresha uwezo wa walimu kwa kuwapatia mafunzo mbali mbali.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt jijini London. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt(kushoto) jijini London. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahige jijini London. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akipokelewa na  Balozi wa Tanzania Nchi Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro alipowasili jijini London.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mbele ya Balozi wa Tanzania Nchi Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro jijini London. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

KARIBU KWENYE UZINDUZI WA JARIDA LA CHAUKIDU DULLES AIRPORT, VIRGINIA

BALOZI SEIF AKUTANA NA UJUMBE WA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI MISRI

0
0
Zanzibar inaweza kuimarika zaidi kiuchumi, Maendeleo na Ustawi wa Jamii endapo uwekezaji katika Sekta ya Utalii, ujenzi wa Miji Mipya ya Nyumba za Makaazi ya Wananchi wa kawaida, Uvuvi, pamoja na Mifugo itajengewa miundombinu imara katika utekelezaji wake.

Hayo yamejiri kufuatia Kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Wawekezaji Wanane kutoka Nchini Misri ukiongozwa na Bwana Amgad Hassoun ulipozungumza na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ukiongoza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Vuga Mjini Zanzibar.

Mmoja wa Viongozi wa Ujumbe huo kutoka Misri Profesa Hossam El – Borombaly alisema zipo Taasisi na Makampuni ya Uwekezaji Nchini Misri yenye uwezo wa kuwekeza katika Sekta za Uvuvi, Miji Mipya, Mifugo na Miradi ya Utalii lakini kinachohitajika ni namna ya kuitekeleza kupitia Mikopo ya Benki zilizojitolea kusimamia Miradi hiyo.

Profesa Hossam alisema ujenzi wa Miji ya Kisasa ambayo Misri imeshakuwa na uzoefu mkubwa inaweza kustawisha Wananchi wa Kipato cha chini kwa kupata Makaazi bora sambamba na upatikanaji wa Ofisi zenye hadhi inayokubalika Kimataifa.

Alieleza kwamba mradi huo unazingatia hali halisi ya Kimazingira hasa ikitiliwa maanani mfumo wa misimu ya hali ya hewa kama ule wa masika wakati mwengine huambatana na mvua kubwa zinazosababisha mafuriko na kuleta Maafa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akizungumza na Ujumbe wa Viongozi Wanane wa Taasisi za Uwekezaji kutoka Nchini Misri hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi Wanane wa Taasisi za Uwekezaji kutoka Nchini Misri Bwana Amgad Hassoun wa Pili kutoka Kulia akimueleza Balozi Seif maeneo ambayo Kampuni za Misri zinaweza kuwekeza Miradi yao Visiwani Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA BRAZIL

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (katikati) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu (hayupo pichani) walipokutana kwa Majadiliano ya Kisiasa yaliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Aprili, 2018. Majadiliano hayo yalifanyika wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili ya Mhe. Balozi Fernando hapa nchini. Pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu namna ya kuboresha mashirikiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili hususan katika eneo la biashara na uwekezaji. 

Pia Naibu Mawaziri hao walijadili namna ya kutekeleza kikamilifu Mradi wa Pamba kwenye eneo la Ziwa Victoria na matokeo ya kusainiwa kwa mkataba wa msamaha wa deni la Tanzania kwa Brazil pia lilijadiliwa. Aidha, Brazil wameahidi kushirikiana na Tanzania kwenye sekta ya afya hususan katika kupambana na maradhi ya Selimundu (Sircle-cell) na kwa upande wa Zanzibar watashirikiana katika afya ya mama na mtoto hususan kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wachanga. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil, Mhe. Balozi Fernando Jose Marroni de Abreu (katikati) nae akizungumza wakati wa majadiliano ya kisiasa kati yake na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (hayupo pichani). Wengine kwenye picha ni Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Alfonso Iglesias Puente (kushoto) na Mkuu wa Idara inayoshughulikia masuala ya Kaskazini na Mashariki mwa Afrika kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Brazil, Bw. Paulo Cypriano. 
Mhe. Dkt. Susan Kolimba akimsikiliza kwa makini Mhe. Fernando de Abreu (hayupo pichani), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Brazil wakati wa Majadiliano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Brazil. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) 
Mhe. Dkt. Kolimba na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo hayo 
Mhe. Fernando de Abreu na Ujumbe wake wakifuatilia mazungumzo
Mhe. Dtk. Kolimba kwa pamoja na Mhe. Balozi Fernando wakishuhudia uwekwaji saini wa Hati ya Makubaliano kuhusu kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Kisiasa kati ya Tanzania na Brazil uliokuwa ukisainiwa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Mhe. Dkt. Emmanuel Nchimbi na Balozi wa Brazil nchini, Mhe. Carlos Alfonso Iglesias Puente. 
Mhe. Balozi Nchimbi na Mhe. Balozi Puente wakibadilishana Hati hiyo mara baada ya kusaini huku Naibu Mawaziri wakishuhudia 

Dkt Mwakyembe aeleza misingi ya kisheria Mawaziri kueleza Utekelezaji

MICHUZI TV: JANGWANI YAFURIKA, BARABARA YAFUNGWA KWA MUDA

0
0
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika eneo la Jangwani jijini Dar es salaam, baada ya Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi hapa nchini, hali iliyofanya Mto Msimbazi kufurika maji na kupelekea sehemu ya eneo hilo katika barabara ya Morogoro kufungwa kwa muda. hali hiyo pia ilisababisha kituo cha mabasi yaeneondayo haraka (UDA RT) kufungwa na mabasi yote kusitisha safari zake za kuelekea maeneo ya katikati ya mji. Kwa mujimu wa Mamlaka ya hali ya hewa nchini, hali hii ya mvua inatazamiwa kuendelea hadi hapo Aprili 19, 2018, hivyo Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhali ya mvua hiyo ambayo inaweza kuleta madhara.
 Maji yakiwa yameenea kisa sehemu ya eneo la Jangwani.
 Mmoja wa wakazi wa maeneo ya jirani na Jangwani akisaka chochote kwenye maji hayo, bila kujali usalama wake.
 Nyumba zilizo kando ya eneo la Jangwani zikionekana kujaa maji.
 Eneo la Jangwani linavyoonekana kutokea upande wa Mapipa, Magomeni.
 Maji ni mengi sana.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAMLAKA VIWANJA VYA NDEGE WATAKIWA KUTAFUTA MBINU MBADALA KUJIENDESHA

0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amelitaka Baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwa na mbinu mbadala ili kuiwezesha mamlaka hiyo kujiendesha  pasipo kutegemea bajeti kutoka Serikali Kuu.

Pia amelitaka baraza hilo kujithamini kwanini viwanja vilivyopo hapa nchini havipo miongoni mwa viwanja 10 bora  Afrika na kuwataka  waandae  mkakati wa kuiwezesha viwanja hivyo kuingia katika ushindani wa kimataifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya  kuzindua  baraza la sita la wafanyakazi wa TAA, Prof.Mbarawa, aliyekuwa mgeni rasmi amesema haiwezekani viwanja vya ndege vilivyopo hapa nchini vikose uwezo binafsi wa kujiendesha wakati kuna fursa nyingi za kuipatia mamlaka hiyo mapato.

“Lazima mjiulize kwanini hadi leo kununua gari ndani ya uwanja wa ndege mnasubiri fedha kutoka Serikali kuu wakati katika viwanja hivi kuna sehemu mmepangisha watu fedha zinaenda wapi"

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA Richard Mayongela amesema  mpaka sasa wamenunua magari sita kutoka kwenye mfuko wa TAA ili kuongeza ufanisi katika kazi za kila siku.

Amesema wamefanikiwa kupata fedha ya kujenga ukuta kwenye kiwanja cha ndege cha Mwanza ili kuzuia wananchi kupita kwenye uwanja huo.

"Leo tunazindua baraza la sita la wafanyakazi wa TAA ili kuongeza ufanisi kwenye viwanja vyetu vyote hapa nchini na asiyefanya kazi kwa ufanisi atawajibika,"amesema Mayongela.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza jambo alipokuwa anafungua mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela akizungumza mafaniko waliyoyapata pamoja na kuelezea changamoto wanazozipata wakati wa mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa baraza anayemaliza muda wake na pia ni Kaimu  Meneja rasilimali watu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) akizungumza jambo wakati wa mkutano wa sita wa mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa  alipokuwa anafungua mkutano  wa baraza kuu la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) mara baada kuzindua mkutano huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA BIL 12.97/-KIGOMA

0
0
Editha Karlo,Blog ya jamii Kigoma

MKUU wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga ameupokea Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2018 leo kutoka kwa Mkuu wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu katika kijiji cha Nyamtukuza Eilayani Kakonko ambapo mwenye huo utatembela miradi 50 yenye thamani ya Sh.bilioni 12.97.

Mwenge huo utakimbizwa katika halmashauri zote nane za Mkoa wa Kigoma na kati ya miradi hiyo miradi 24 itazinduliwa, miradi 11 itafunguliwa, miradi 11 itawekewa mawe ya msingi na miradi 2 itakaguliwa. 

Pia miradi 2 itakuwa ya uwezesho wa vikundi vya wajasiriamali vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Mwenge wa mwaka huu umebeba ujumbe wa kauli mbiu"Elimu ni ufungo wa maisha wekeza sasa kwa maedeleo ya Taifa letu".

Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu kitaifa ni Charles Kabeho(Dar es salaam)akishirikiana na Issa Abasi(Kusini Pemba)Agusta Safari(Geita)Ipyana Mlilo(Tanga)Dominick Njunwa(Kigoma)na Riziki Hassa(kusini Unguja).

Aprili 24 mwaka huu Mwenge huo utahitimisha mbio zake mkoani humo na kukabidhiwa mkoani Tabora kwa ajili ya kuendelea na mbio zake.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akisoma taarifa ya Mkoa ya miradi ya mwenge kwa kiongozi mwenge 2018 Charles Kabeho.
Mkuu wa Mkoa wa kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akimkabidhi mwenge wa uhuru 2018 Mkuu wa Wilaya ya Kakonko kanali Hosea Ndagalu kwa ajili ya kuukimbiza katika Wilaya yake.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA MIUNDOMBINU ILALA

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisaidiwa kuvuka kwenye daraja la muda alipokuwa akikagua leo daraja la Mto Msimbazi linalounganisha Ulongoni B na Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ambalo ni moja ya madaraja yaliyobomoka kutokana athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha. Mjema alifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua katika wilaya hiyo. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA, KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkuu wa Wilaya Mjema, akizungumza na wakazi wa Ulongoni baada ya kuwafuata upande wa pili kwa kutumia daraja hilo hatari.

 Mjema akiondoka baada ya kukagua daraja hilo la Ulongoni B.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema (kulia) akishauriana na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi wa Manisapaa ya wilaya hiyo, Msongela Palela alipofika kukagua daraja la Banguo Pugu Mnadani eneo ambalo mto umeacha kupita darajani na kumega eneo la barabara hali iliyosababisha kukata mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.
 Wakiangalia jinsi mto Msimbazi ulivyoacha mkondo wake wa kawaida na kumega ardhi maeneo ya makazi ya watu pamoja na kuharibu barabara.
 Baadhi ya nyumba eneo la Bangua ambazo zimo hatarini kubomolewa na mafuriko.

CAG ametuonesha njia-Dkt Tizeba

RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amefanya ziara ya kuwatembelea na kuwapa pole wahanga wa mafuriko na kuwataka wananchi waishio maeneo ya mabondeni kuhama ili kuokoa maisha yao. RC Makonda amesema kuwa hadi sasa zaidi ya watu 7 wamepoteza maisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo ambapo amesema njia pekee iliyobaki ni wananchi kuchukuwa tahadhari.
Kufuatia mwendelezo wa mvua hizo RC Makonda ameziomba mamlaka husika kusimamisha masomo kwa muda wa siku mbili ili kuwaepusha wanafunzi kukumbwa na Maafa. Aidha RC Makonda amesema serikali inaendelea na ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya na mvua ikiwemo madaraja, Barabara,shule pamoja na kuzibua mitaro.
Akiwa Mtaa wa Mfaume Kata ya upanga RC Makonda ameshuhudia jengo la gorofa kumi likiwa limepata hitilafu ya kutitia ambapo ameagiza mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina na kuwasihi wakazi wa jengo hilo pamoja na majirani kutafuta sehemu ya kujisitiri kwa wakati huu kwa mustakabali wa usalama wao. 
Pamoja na hayo RC Makonda amewahimiza wananchi kufuatilia tahadhari zinazotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa nchini pamoja na vyombo vya habari.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live


Latest Images