Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

WILAYA GAIRO YAANZA KILIMO CHA MAZAO YA PAMBA, KOROSHO NA KAHAWA

$
0
0

Utekelezaji wa mazao ya kimkakati hasa Pamba msimu wa 2017/2018 kama ilivyoelekezwa na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim watekelezwa kwa vitendo wilayani Gairo. 
 
Hayo yameelekezwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven alipotembelea Wilaya ya Gairo mwanzoni mwa wili iliyopita ili kuhamasisha kilimo cha Pamba ambapo ekari moja ya pamba unapata shilingi milioni 1.4. Alidha Dkt. Kebwe alirudi wilayani Gairo kukagua utekelezaji wa maagizo yake ikiwemo kutembelea mashamba darasa ya viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya Mhe. Siriel Mchembe, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rahel Nyangasi na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Agnes Mkandya. 
 
Mhe. Mchembe alimpa taarifa Mkuu wa Mkoa kuhusu kilimo cha pamba ambapo hekta 181 zimelimwa, pembejeo zimepokelewa ikiwemo mbegu za pamba kilo 3,996 viuadudu mililita 120 na mabomba 10. Mbali na Pamba wilaya ya Gairo wameweza kulima zao la Korosho ekari 2,618 jumla ya miche 70,800 pamoja na zao la kahawa idadi ya miche 800 na mbegu gramu 3,000.
 
 Pamba, Korosho na Kahawa ni mazao ya kimkakati na ya kibiashara hapa wilayani Gairo ambapo mazao hayo yatawainua na wananchi kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati kama ambavyo sera za awamu ya tano za Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza. Mwisho wananchi wa Gairo walimshukuru sana Mkuu wa Mkoa, Dkt. Kebwe Steven kwa kazi kubwa anayofanya kuhamasisha Kilimo cha mazao ya kimkakati Wilaya ya Gairo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akikagua shamba darasa la Mhe. Mchembe Mkuu wa Wilaya Gairo. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akiongea na wananchi Kijiji cha Kisitwi Gairo. 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kebwe Steven akikagua kiwanda cha mvinyo itokanayo na ndizi. Kiwanda hicho ni kati ya viwanda vipya 6 vilivyoanzishwa mwaka 2018.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Gairo Mhe. Rahel Nyangasi akiwa kwenye shamba darasa lake la zao la Pamba. 

Harmonize Ft Diamond Platnumz - Kwangwaru ( Official Video )

Mafundi Sanifu Barabara Wafundwa Kuhusu Mazingira

$
0
0
Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Julius Chambo akifafanua jambo kwenye hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi wa barabara kwa mafundi sanifu yanayofanyika mkoani Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi wa barabara wakifuatilia hotuba ya ufungaji wa mafunzo hayo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Julius Chambo.
Mhitimu wa mafunzo ya tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi wa barabara akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Julius Chambo mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Mwakilishi wa wahitimu wa mafunzo ya tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi wa barabara, Bw. Seth Rengia akiwasilisha maoni ya wahitimu wa mafunzo hayo kwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Julius Chambo (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya tathmini na usimamizi wa athari za mazingira katika miradi ya ujenzi wa barabara yanayofanyika mkoani Morogoro.

MAKONDA AWATAHADHARISHA WALIOTELEKEZA WATOTO, AWAONYA WATAKAOKAIDI WITO WAKE KUKIONA

$
0
0
MKUU  wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewatahadharisha wanaume wanaodhani wanaweza kukaidi wito wa kufika ofisini kwake baada ya kulalamikiwa kutelekeza watoto ambapo amewatumia salamu kwa kuwaambia wasimjaribu wala kupima mamlaka aliyonayo.

Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano ya kipindi cha tathimini ya mchakato wa kudai haki za watoto waliotelekezwa ambapo amesema tangu Jumatatu zaidi ya 17,000 walifika ofisini kwake na Kati ya hao 4,400 wamesikilizwa. 

Aidha Makonda amesema kinachomfariji ni kuona idadi kubwa ya kinababa wanaofika ofisini kwake wanakubali kumlea mtoto ambapo hadi sasa familia 295 zimekubali kuhudumia mtoto na familia 29 zimepima DNA.* 

Hata hivyo  Makonda amesema baada ya zoezi hilo ataunda tume ya kuangalia changamoto zilizopo katika sheria ya matunzo ya mtoto* kisha kuifikisha kwa waziri husika kwaajili ya kufikishwa Bungeni kwaajili kufanyiwa marekebisho. 

Pamoja na hayo Makonda amesema hatoyumbishwa na baadhi ya watu wasiojua uchungu wanaopata kinamama kwa kubeza zoezi hilo kwakuwa yeye ametambua Mateso waliyokuwa wakipata kinamama waliotelekezwa. 

Makonda amesema ikitokea mwanamke aliefika ofisini kwake na kumshitaki mwanaume aliezaanae kisha uchunguzi ukafanyika na kubaini udanganyifu mwanaume anayo haki ya kufungua kesi ya kudhalilishwa na afisa ustawi wa jamii wa mkoa atalazimika kuwa shahidi mahakamani. 

WATU WENYE DHAMBI WANAPENDA GIZA NDIO MAANA UKIWASHA NURU WANAIBUKA KUPINGA.

AZAM WAIOMBA TFF WASOGEZA MBELE MECHI YAO DHIDI YA NJOMBE MJI

$
0
0
Na Agness Fracis,Blogu ya Jamii

UONGOZI wa Azam FC umeomba mchezo wao dhidi ya Njombe Mji usogezwa mbele kutokana na muda mchache waliopumzika baada ya kumalizana na Ruvu Shoting ya Mlandizi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa Azam Jaffary Maganga amesema wameomba mchezo kusogezwa mbele ili kupata nafasi ya kujiandaa ikiwa ni jana wametoka ugenini kucheza na timu ya Ruvu shooting.

"Tumeandika barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania( TFF) kuomba mchezo dhidi ya Njombe Mji ya mkoani Njombe usogezwe mbele badala ya kuchezwa kesho ikiwa sheria za FIFA zinasema inatakiwa kupumzika saa 72 na si 48,"amesema.

Mchezo huo uliotarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la Azam Complex Chamazi.Ambapo kikosi hicho cha Azam kimerejea jana hiyo hiyo kutoka Mlandizi kuendelea kujifua na mazaoezi kukabilia na Njombe Mji katika mchezo wao ujao.

"Tumerejea jana usiku kutoka Uwanja wa Mabatini Mlandizi tulipomaliza tu mechi na kikosi kipo mazoezini kujiandaa nadhani nnajua Njombe Mji ni timu nzuri pia"amesema Jaffary Maganga.

Azam FC walikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ruvu Shoting na kuendelea kubaki nasafi ya 3 wakiwa na alama 45,huku vinara Simba wakiendelea kujikita Kileleni kwa alama 52 na Mabingwa watetezi Yanga wao wakishikilia nafasi ya pili kwa pointi 47,katika msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

KWA TAARIFA HII YA HALI YA HEWA CHUKUA TAHADHARI

AFRIKA ZINDUKA BAGAMOYO PLAYERS YATIKISA KIGODA CHA NYERERE

$
0
0
Na Sophia Mtakasimba (TaSUBa).

Mchezo wa kuigiza wa jukwaani unaofahamika kwa jina la Afrika zinduka, umetikisa tamasha la kumi la kigoda cha Mwalimu Nyerere lililoendelea  katika ukumbi wa Nkuruma wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.


Mchezo huo uliobeba ujumbe wa namna  Bara la Afrika linavyoteseka na umasikini mkubwa ile hali  lina utajiri mkubwa wa mali asili , ardhi na madini umetungwa , umeongozwa na kuchezwa na Kikundi cha “Bagamoyo Players” cha Taasisi ya Sanaa na utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ili kuchagiza ujumbe wa tamasha la mwaka huu uliosema “wimbi la uporaji wa rasilimali Afrika wanyonge wanajikwamuaje”


Akizungumza katika siku ya pili ya Tamasha hilo Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama , amesema kuwa igizo hilo limeakisi namna halisi ya maisha ya sasa ya muafrika hivyo ni wakati wa kuzinduka.


“Wenzetu wa TaSUBa wametuambia Afrika Zinduka ,sasa huu ndio wakati wetu wa kuzinduka na kuona namna Afrika inaweza kunufaika na rasilimali zake.” Alisema bi Mlama


Tamasha la kigoda cha kitaaluma cha Mwl,nyerere  ambalo kwa mwaka huu limetimiza miaka kumi toka kuanzishwa kwake limefanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 11-13 Aprili  ambapo mada mbalimbali kuhusu masuala ya kijamii zimejadiliwa .
 Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.
 Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.
Wasanii wa kikundi cha Bagamoyo Players cha TaSUBa wakionesha igizo la Afrika Zinduka katika tamasha la kumi la kigoda cha mwalimu Nyerere.
washiriki wa tamasha wakifuatilia igizo la Afrika Zinduka

MWALIMU MKUU SEKONDARI ASHUSHWA CHEO KWA UTORO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEME amemshusha cheo mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Magazine EDMUNDI KATUMBI iliyoko wilayani Namtumbo kwa kosa la utoro huku walimu watano wa shule hiyo kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Rais Magufuli afanya uteuzi Majaji wa Mahakama Kuu 10, Naibu AG, Naibu DPP, Wakili Mkuu wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali

SHEREHE ZA WAFANYAKAZI ZA MEI MOSI KITAIFA KUFANYI MJINI IRINGA

$
0
0
Na Francis Godwin
SHIRIKISHO   la  vyama huru    vya  wafanyakazi Tanzania  (TUCTA) ambao  ni  waandaaji  wa  sherehe  za  wafanyakazi kitaifa  (MEI  MOSI) wamempongeza  Rais  Dkt  John Magufuli kwa  kukubali  mwaliko  wao  wa  kuwa  mgeni  rasmi katika sherehe  za  Mei  Mosi  ambazo mwaka huu zitakazofanyika  kitaifa  mkoani Iringa.
Rais wa shirikisho  la  vyama huru    vya  wafanyakazi Tanzania  (TUCTA)  Tumaini  Vyamhokya alisema  leo  kuwa  katika  sherehe  hizo  za  wafanyakazi duniani kwa  Tanzania  zitafanyika  katika  mkoa  wa  Iringa kwenye  uwanja  wa  Samora  na  kuwa tayari  Rais Dkt  Magufuli  amekubali  kuwa  mgeni  rasmi.  Hivyo  aliwataka  wafanyakazi   kujitokeza  kwa  wingi  kushiriki sherehe  hizo  na  kuwa  kupitia sherehe  hizo  watapata fursa ya  kujua  mikakati ya  serikali  dhidi ya wafanyakazi  nchini japo  hadi  sasa  wanapongeza  hatua  iliyofikiwa na  serikali ya  kuwarejesha  kazini  wafanyakazi  waliokuwa  wamesimamishwa kazi  kutokana na elimu  yao ya  darasa la  saba.
Rais   huyo  alisema  kuwa  TUCTA  imefanya  jitihada  kubwa  za  kukutana na  serikali  kuwapigania  wafanyakazi hao  walioondolewa kazini   kutokana na  elimu   yao na  serikali  imesikiliza  na  imewarejesha  kazini. Alisema  kuwa  serikali  imeendelea  kufanya  jitihada  kubwa  kuongeza ajira  pamoja na  kusikiliza  kero  mbali mbali  za  wafanyakazi na  kuzipatia  majibu. Akielezea  juu ya maandalizi ya  sherehe  za mei  mosi  mkoani  Iringa  alisema  kwa  sehemu  kubwa   maandalizi yanakwenda  vizuri na  wamepata  ratibu ya  kuzunguka  wilaya  zote za  mkoa  wa Iringa kutoa elimu  pamoja na kututana na  wafanyakazi ili  kujua  changamoto  zao. 
 " TUCTA  inapenda  kuishukuru  serikali  ya  mkoa  wa Iringa kwa  kukubali  kupokea maadhimisho  haya  ya  Mei mosi 2018 TUCTA kwa  kushirikiana  na  serikali ya  mkoa wa  Iringa chini ya  mkuu wa  mkoa Amina Masenza pamoja na waziri  wa  nchi ofisi ya  waziri  mkuu  sera ,bunge  ,kazi ,vijana , ajira   na  watu  wenye  ulemavu Jenista Mhagama tumefanya maandalizi ya  kutosha"
Alisema  kabla ya  Mei  mosi  mambo  yakayofanyika  Iringa ni  pamoja na makongamano mawili ya  kimkoa na  moja la kitaifa  na kuwakongamano la kwanza  litafanyika April 23 katika  wilaya ya  Mufindi ambapo mgeni rasmi  atakuwa mkuu wa  wilaya ya Mufindi  Jamhuri  Wiliam wakati  kongamano la  pili  litafanyika  wilaya ya  Kilolo  April 25  na  mgeni  rasmi  ni mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah  huku April 27 litafanyika  kongamano la  kitaifa litakalohusu Tanzania ya  uchumi wa  viwanda kwenye  ukumbi wa  Kichangani ambalo  viongozi mbali mbali  wa  kitaifa  watashiriki. 

Aidha  alisema  kutakuwa na  michezo  ya  Mei  mosi ya fani mbali mbali itakayoanza April 16 hadi  April 30 katika uwanja wa  Samora kuwa  kwa  ajili ya  kuwafanya  wafanyabiashara na  wajasilia mali  kutumia  fursa ya  mei  mosi  Iringa maonyesho  ya  bidhaa mbali  mbali yatafanyika .
Rais  wa  shirikisho  la  vyama huru    vya  wafanyakazi Tanzania  (TUCTA) Tumaini  Vyamhokya kulia  akiwa na  wajumbe  wenzake kwenye kikao hicho cha maandalizi mjini Iringa.




 Rais  wa  shirikisho  la  vyama huru    vya  wafanyakazi Tanzania  (TUCTA) Tumaini  Vyamhokya katikati akiongoza  kuimba  wimbo wa  wafanyakazi  wakati wa  kikao  na  waandishi wa habari mkoa  wa  Iringa kuelezea maandalizi ya  Mei  Mosi  kitaifa  yatakayofanyika  mkoani Iringa
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela kulia  akiwapongeza  viongozi wa  shirikisho  la  vyama  vya  wafanyakazi
Wajumbe  wa TUCTA  wakiimba  wimbo  wa  wafanyakazi  leo
Wimbo   wa  kuwaunganisha  wafanyakazi

Introducing "Kwangwaru" (Official Music Video) by Harmonize Ft Diamond Platnumz

Tamko la Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania tawi la Mwanza

$
0
0

Makamu Mwenyekiti wa chama cha madereva  Said Yusuph Kipande akisoma tamko hilo Jumamosi Aprili 15, 2018 mbele ya wanahabari kwenye kikao cha madereva wa serikali tawi la Mwanza.



Introducing "Bora Nife" (Official video) by Aslay Ft. Bahati

Makamu wa Rais kumwakilisha Rais Magufuli Mkutano wa Wakuu wa Serikali Jumuiya ya Madola (CHOGM) London

$
0
0
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameondoka nchini jana kwenda London, Uingereza kushiriki kwenye Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 16 hadi 20 Aprili, mwaka huu akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Mkutano huo ambao Kaulimbiu yake ni “Kuelekea Mustakabali wa Pamoja” utafanyika chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa Theresa May na utafunguliwa na Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza.
Majadiliano ya Mkutano wa CHOGM 2018 yatajikita kwenye maeneo manne makuu ya kipaumbele ambayo yatajadili namna Jumuiya ya Madola inaweza kufikia mustakabali wenye ustawi zaidi; mustakabali endelevu zaidi; mustakabali wenye haki zaidi; na mustakabali wenye usawa zaidi.
Mijadala katika maeneo hayo ya kipaumbele itahusisha masuala mbalimbali ikiwemo, kukuza zaidi biashara na uwekezaji baina ya nchi za Jumuiya ya Madola kwa manufaa ya nchi wanachama na Jumuiya nzima; kukuza na kuendeleza misingi ya demokrasia; ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu pamoja na masuala ya uhalifu wa kimataifa kama vile ugaidi, uhalifu wa kimtandao na usafirishaji wa binadamu.
Jumuiya ya Madola ilianzishwa mwaka 1949 kupitia Tamko la London ambalo lilikuwa ni matokeo ya Mkutano wa Mawaziri Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Madola.  Jumuiya ya Madola ina wanachama 53 ambapo kati ya hizo, nchi 19 ni za Afrika, 7 ni kutoka Asia, 13 ni kutoka nchi za Carribean na Mabara ya Amerika, 11 ni kutoka eneo la Pacific na nchi 3 ni kutoka Ulaya.
Ujumbe wa Makamu wa Rais unajumuisha Mheshimiwa Dkt. Balozi Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais na ujumbe wake wanatarajia kurejea nchini Aprili 22, mwaka huu.
Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
15/4/2018

WAKALA WA UFUNDI NA UMEME WATUMIKA KUTENGENISHA MWILI WA MKURUGENZI KONGWA BAADA YA KUKANDAMIZWA NA ROLI AJALINI

$
0
0
*Mwili wahifadhiwa Hospitali ya Rufaa Dodoma,DC Kongwa azungumzia mazingira ya ajali

Na Ripota, Dodoma

INASIKITISHA na inaumiza sana!Hii ndio kauli unayoweza kuielezea kutokana na kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Izengo Ngussa.

Kifo cha Ngussa kimetokana na ajali ya gari yake kugongana na lori la mafuta eneo la Mbande Makaravati wilayani humo mkoani Dodoma.

Kutokana na gari yake kuharibika vibaya na kulaliwa na roli imesababisha mwili kubebwa na kipande cha gari lake kwa ajili ya kwenda kutolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), kwani uling'ang'ania kwenye bodi.Tukio la ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Ngussa limetokea usiku wa leo.Alikuwa kwenye gari ndogo akitokea Dodoma Mjini.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia Michuzi blog kuwa gari ya Mkurugenzi yenye namba T 619 DMA baada ajali hiyo gari yake ilikandamizwa na roli la mafuta.Hali hiyo ilisababisha mwili wake kuungana na bodi la gari lake na kushindwa kutolewa katika eneo la tukio.Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kimedai tangu jana asubuhi shughuli za utoaji mwili huo zilianza.Hata hivyo hazikufanikiwa kwani mwili wake ulikuwa umeng’ang’ania katika bodi ya gari.
"Saa 8 mchana kipande cha gari kilichukuliwa na gari la jeshi na kisha kupelekwa Temesa Dodoma ili bodi la gari litanuliwe na kuutoa mwili," kimedai chanzo hicho.Kwa sasa mwili umehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Rufaa Dodoma, baada ya Temesa kufanikiwa kuutoa mwili kwenye gari saa 10 ya jioni.

 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi amezungumzia kutokea kwa ajali hiyo na kuthibitisha kifo cha Mkurugenzi huyo.Amefafanu ajali imetokea  usiku na taarifa zikaanza kuzagaa alfajiri na kwamba alikuwa anatokea njia ya Dodoma mjini kuelekea Kongwa.

"Kutokana na mazingira ya ajali tulipata  wakati mgumu tulipokuwa tunautoa mwili kwenye gari take," ameongeza.Ameelezea kazi iliyofanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) na Kikosi cha Zimamoto ambao wameshiriki kikamilifu katika ukoaji. Ndejembi amefafanua  taarifa rasmi itatolewa na Jeshi la Polisi ambalo linaendelea kufanya uchunguzi.
Akimzungumzia Mkurugenzi Ngussa, amesema wamempoteza mtumishi mwadilifu na aliyekuwa anaipenda kazi na kwamba amefanya naye kwa miaka miwili."Amesaidia  wilaya kupata hati safi katika ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG)," amesema.

Kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma Dk.Caroline Damian amethibitisha kupokea na kuuhifadhi mwili wa Mkurugenzi huyo."Mwili wake umeumia sana katika maeneo ya kichwani.Amevunjika mkono na mguu mmoja wa kushoto," amesema.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, White Zuberi amesema Wilaya hiyo imepata pigo kutokana na kifo cha Mkurugenzi huyo  aliyekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo.


Naibu Waziri Maliasili na Utalii Hasunga atembelea pori la akiba Mkungunero

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata alipokuwa akitoa maelekezo kwa Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la la akiba la Mkungunero alipofanya ziara katika pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Maafisa hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (hayupo pichani) wakati akitoa maelekezo ya namna bora ya usimamizi wa hifadhi za wanyamapori alipofanya ziara katika pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (wa pili kulia) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata alipokuwa akimfafanulia jambo wakati wa kikao na Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa. Wakwanza kulia kwake ni Meneja wa pori la akiba la Mkungunero Bw. Emmanuel M. Birasso na Meneja wa pori la akiba la Swaga Swaga Bw. Alfred Choya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi – Usimamizi wa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata wakati wa kikao na Maafisa Hifadhi wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (katikati) akitizama sehemu ya ng’ombe waliokamatwa na Maafisa wa wanyamapori wa pori la akiba la Mkungunero kwa kuingia katika hifadhi hiyo wakati alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na mamlaka ya hifadhi ya pori la Mkungunero jana Wilayani Kondoa, ambapo zaidi ya ng’ombe 250 wanashikiliwa. Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi – Usimamiziwa Rasilimali za Wanyamapori wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. David Kanyata na kulia kwake ni Kaimu Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kondoa Bw. Juma Solomon Nyamwakirya.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (katikati) akimsikiliza Diwani wa Kata ya Bumbuta Bw. Bashiru Mtoro (kulia) alipofanya ziara katika hifadhi ya pori la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa jana. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kulia) akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa Bi. Hija Suru (kushoto) alipofanya ziara katika hifadhi ya pori la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Makota.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kulia) akimsikiliza Meneja wa pori la akiba la Mkungunero Bw. Emmanuel M. Birasso (kushoto) alipofanya ziara katika hifadhi ya pori la Mkungunero lililoko Wilayani Kondoa jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akimsikiliza Bw. Yohana Bilo ambaye ng’ombe wake wanashikiliwa na Maafisa Hifadhi wa pori la Mkungunero kwa kuingia katika pori hilo alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Japhet Ngailonga Hasunga (kushoto) akitoa maelekezo kwa wafugaji wa vijiji vinavyozunguka pori la akiba la Mkungunero alipofanya ziara ya kutatua migogoro kati ya wafugaji na hifadhi ya pori hilo jana Wilayani Kondoa.

PICHA ZOTE NA: OCTAVIAN KIMARIO- MAELEZO.

VIONGOZI KIVULE,DAR WAUNGANISHA NGUVU KUWASAKA VIBAKA DARAJANI

$
0
0
Na Richard Mwaikenda, Kivule, Dar


Viongozi wa Kata ya Kivule, Ukonga Dar, wameunganisha nguvu kuwasaka vibaka wanaowapora watu wanaopita wakati wa usiku katika Daraja linalojengwa MTO Kizinga.



Uamuzi huo umefanywa baada hivi karibuni Majira ya SAA 5 usiku ambapo mtu mmoja aliyekuwa akivuka katika Daraja la muda kuporwa na vibaka Simu na vitu vingine.



Tukio hili aliliripoti kituo kidogo cha POLISI cha Kitunda, na kwa viongozi wa Kata ya Kivule, akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kivule, Amos Angaya na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim.



Mwandishi wa Habari hii alishuhudia viongozi hao wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi, Kijana Jaffari aliyekamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika uporaji huo akishirikiana na wenzie.Viongozi hao walimnasa 'Kibaka' huyo kwa ushirikiano Mkubwa na waendesha bodaboda pamoja na wafanyabiashara ndogondogo wanaoendesha shughuli zao darajani hapo.



Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.Walimnasa Jaffari baada ya kutumia mbinu ya kuwatishia wanaoendesha shughuli zao darajani hapo kwamba wasipowataja vibaka basi wote watafukuzwa eneo hilo.



Kwa umoja wao, viongozi hao waliapa kutokomeza vitendo vya uovu vilivyoanza kuota mizizi katika eneo hilo la Daraja ambalo limekata mawasiliano ya usafiri Kati ya Kivule Mwembeni na Silari baada Daraja bovu kuvunjwa na kuanza kujenga jipya.Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kerezange, Ismail Ibrahim, Ujenzi wa Daraja hilo unatarajiwa kukamilika Mei, Mwaka huu.



Hivi sasa daladala kutoka Banana zinaishia upande wa Mwembeni na zinazotoka Frem kumi zinaishia Silari. Magari mengine yanapitia Daraja la Bombambili.
 Daraja la Kivule likiendelea kujengwa katika Mto Kizinga eneo la Sirali,Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakipita kwenye daraja la muda baada lile la awali kubomolewa kupisha ujenzi wa daraja hilo jipya ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi ujao. 

VERTIV YAJA NA VIFAA VYA KISASA KUKABILIANA NA MAJANGA YA UMEME

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

KAMPUNI ya Vertiv imefanya maboresho ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) vinavyotumika katika ujenzi, viwandani na maofisini kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati yao wamiliki wa viwanda na kampuni mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki.

Akizungumza jana Dar es Salaam, katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Rais wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John Wyk alisema kuwa wamefanya maboresho ya bidhaa zao ili kusaidia wateja wao kujua endapo vifaa vyao vimepata hitilafu au la.

Amesema bidhaa wanazozizalisha ni pamoja na vifaa vya kudhibiti nguvu ya umeme, Ac zinazotumika kwenye viwanda, UPS na ambazo zimewekewa uwezo wa kutoa taarifa kwa mtumiaji kama kifaa anachotumia kimeshindwa kufanya kazi kwa sababu gani.

‘’Tumefanya maboresho kwa bidhaa zetu ambapo wenye vituo vya data kama vile kampuni za simu, ofisi za serikali na kampuni binafsi watapata taarifa kuonesha kuwa kama UPS au AC za viwandani hazifanyi kazi kwa sababu ya umeme mdogo au kuna tatizo lingine ambalo linapaswa kufanyiwa marekebisho,’’ amefafanua Wyk.

Amesisitiza kuwa wanaendelea kuboresha bidhaa hizo ambazo zinatumika katika nchi za Jumuiya ya Afika Mashariki (EAC) na Ulaya kwa kuwa wanaamini ukuaji wa teknolojia unasaidia katika kuleta maendeleo chanya kwa kila nchi.

Naye mshirika wa kibiashara na Mtaalamu wa masula ya mawasiliano, Mihayo Wilmore amesema kuwa uboreshaji wa vifaa hivyo utasaidia maeneo mengi ikiwemo hospitalini na maofisini ambako matumizi makubwa ya teknolojia hufanyika.

Amesema kuwa watu wanaotumia mitambo mbalimbali katika shughuli zao, ni muhimu kujua ni muda gani vifaa vyao vimeweza kuzimika kwa sababu ya kuisha kwa umeme, hutupata ujumbe mfupi wa maandishi kuelezea tatizo lililotokea.

‘’Ni muhimu kwa hospitali kujua UPS wanayotumia inaweza kuzimika kwa muda gani na sababu gani zinazosababisha jenereta kuzimika hii itasaidia kurahisisha utoaji wa huduma haraka. Pia wameonesha uwezo wa kutengeneza vituo vya data katika simu au kompyuta ili kutoa taarifa kwa haraka kwa wateja wao,’’ ameeleza Wilmore.
Rais wa Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, John Wyk akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake katika soko la Tanzania Chini ya usambazaji wa kampuni ya Elcom Solution 
Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano kutoka Vertiv Kanda za Kusini mwa Afrika, Johan Terblanche akizungumza wakati wa Warsha ya kutambulisha bidhaa za kampuni yake juu ya umuhimu wa UPS kutoka Vertiv katika Data Centre. 
Mkurugenzi wa huduma wa Vertiv Mashariki ya Kati , Pascal Bodin akieleza namna kampuni hiyo ilivyoweza kunufaisha Viwanda vya ukanda huo.
Mshirika wa kibiashara wa Elcom Solution ambao wamewakaribisha Vertiv nchini, Mihayo Wilmore akieleza Waandishi wa Habari umuhimu wa mitambo ya Vertiv katika sekta ya Afya nchini.
Wakurugenzi wa EL- COM Solutions , Deen Nathwani, Jimy Apson na Amin Valji wakizungumza jambo wakati wa Warsha wa kutambuslisha bidhaa za Vertiv nchini.
Wafanyakazi wa Vertiv wakiwa katika picha ya pamoja na Washirika wao El-com Solution na washirika wengine kutoka nchini Kenya mara baada ya kumaliza warsha ya kutambulisha bidhaa zao Tanzania

Puma Energy kuchangamkia fursa ukuaji wa sekta ya anga.

$
0
0
KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy Tanzania imepanga kutumia vyema mageuzi yanayoendelea katika sekta ya anga nchini kwa kuboresha zaidi huduma zake ili ziandane na kasi ya ukuaji wa sekta hiyo.

Kwa mujibu wa Meneja Idara ya Mafuta ya Ndege wa kampuni hiyo, Raymond Tungaraza, kwasasa kampuni hiyo inaandaa mikakati itayoiwezesha kujitanua ili kunufaika zaidi na ongezeko la idadi ya ndege za kitaifa na kimataifa linalotarajiwa kufuatia mageuzi hayo.

“Tunachokifanya Puma Energy ni kuhakikisha tunakwenda sambamba na mabadiliko yanayoendelea katika sekta ya anga’’ alisema Tungaraza katika mahojiano yake na waandishi wa habari hivi karibuni katika Mkutano wa wadau wa sekta ya anga barani Afrika ulioandaliwa na Umoja Wa Mashirika ya Ndege barani Afrika (AFRAA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Ndege nchini (ATCl) uliofanyika visiwani Zanzibar hivi karibuni.

Alitolea mfano wa maboresho yaliyofanywa na kampuni hiyo katika mfumo wake wa huduma ya mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ili kuwezesha kampuni hiyo kukidhi mahitaji ya usambazaji wa nishati hiyo ambayo yanayotarajiwa kuongezeka mara tu baada ya kukamilika kwa upanuzi unaoendelea wa jengo la tatu la abiria (Terminal three).

Alisema lengo la kampuni hiyo katika sekta ya anga ni kutoa huduma ya mafuta kwa bei ya ushindani kwa wateja wake huku pia ikizingatia kutoa huduma hizo kwa kukidhi mahitaji ya viwango usalama na ubora wa kimataifa.

"Linapokuja suala la usambazi wa mafuta ya ndege huwa tunajitahidi sana kuhakikisha tunawapa urahisi zaidi wateja wetu kwa kuhakikisha tunaratibu kila kitu sisi kuanzia uagizaji, utunzaji, uhifadhi na usafiri hadi kwenye vituo vyetu vilivyopo kwenye viwanja vya ndege kwa kutumia rasilimali watu wenye weledi zaidi katika suala hilo,’’ .

“Ni wazi tumejenga sifa nzuri katika utoaji wa huduma zetu kutokana na ufanisi wetu, rekodi nzuri katika masuala ya usalama pamoja na bei yenye ushindani,’’ alitaja.

WAZIRI MWAKYEMBE: TATUENI KERO ZA WADAU KWA HARAKA NA UFANISI

$
0
0

Na Anitha Jonas – WHUSM,Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wamehimizwa kutumia muda wao wa kazi kuwahudumia wananchi kwa kujibu hoja na kutatua kero zao kwa haraka na ufanisi.

Hayo yamesemwa leo Mkoani Dodoma na Waziri Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe alipokuwa akifungua kikao cha 13 cha Baraza la Wafanyakazi cha Wizara hiyo, ambacho hufanyika mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za watumishi.

“Ni wajibu wa kila mtumishi kuzingatia maadili na weledi katika kuhakikisha utumishi wa umma unaheshimika na kuwajibika kwa wananchi ambao ndio wadau wakubwa wa kazi zetu” amesema Dkt. Mwakyembe. Aidha Dkt. Mwakyembe ameziagiza mamlaka zinazosimamia nidhamu katika Wizara hiyo kutosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wasiotimiza wajibu wao ili kuimarisha utendaji wa kazi.

“Serikali ya awamu ya tano ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha taratibu za kiutendaji zinafuatwa na kuzingatiwa” amesema Dkt. Mwakyembe. Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi alimshukuru mgeni rasmi kwa kuwafungulia kikao hicho ambacho kipo kwa mujibu wa sheria, na kuwasisitiza watumishi kuyafanyia kazi yale yote waliyoelezwa.

“Nawaomba watumishi kuzingatia na kutekeleza wajibu wenu katika majukumu yenu ya kila siku,kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizoainishwa katika mikataba ya ajira” amesema Bibi.Susan.

Naye Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bw.Makoye Alex Nkenyenge alimshukuru mgeni rasmi kwa niaba ya wajumbe wote na kuhaidi kuyafanyia kazi yale yote aliyoyaeleza katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku. 
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisoma risala wakati wa ufunguzi wa kikao cha 13 cha  Baraza la Wafanyakazi lililofanyika katika Ukumbi wa Waziri Mkuu leo Mkoani Dodoma.

 Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Makoye Alex Nkenyenge akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi (Hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa kikao cha13 cha  Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika leo Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi za Waziri Mkuu
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mfuko wa kufarijiana Bw. Mussa Varisanga akiwasilisha taarifa kuhusu mfuko huo wakati wa kikao cha 13 cha Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ,kilichofanyika leo Mkoani Dodoma.

 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakisikiliza uwasilishwaji wa mada na taarifa mbalimbali wkatika kikao cha 13 cha Baraza hilo.

 Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakisikiliza uwasilishwaji wa mada na taarifa mbalimbali katika kikao cha 13 cha Baraza hilo.

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images