Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA SPIKA WA EALA, BALOZI MDOGO WA MAREKANI NCHINI TANZANIA.

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson (kulia) pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Dkt. Inmi Patterson (kulia) pale ugeni kutoka ubalozi huo ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akikabidhiwa zawadi ya kitabu kutoka kwa Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Martin Ngoga (kushoto) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Ikiwa ni maandalizi kabla ya kuanza kamati za Bunge hilo leo, ikifuatiwa na vikao vitakavyoanza tarehe 17 Aprili, 2018 mpaka tarehe 26 Aprili, 2018 Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (kulia) akizungumza na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Martin Ngoga (kushoto) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Ikiwa ni maandalizi ya kamati za Bunge hilo linaloanza leo, ikifuatiwa na vikao vitakavyoanza tarehe 17 Aprili, 2018 mpaka Tarehe 26 Aprili, 2018 vitakavyofanyika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na bendera ya Bunge hilo walioongozwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Martin Ngoga (watatu kushoto) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Ikiwa ni maandalizi ya kamati za Bunge hilo linaloanza leo tarehe 10 Machi, 2018, ikifuatiwa na vikao vitakavyoanza tarehe 17 Aprili, 2018 mpaka Tarehe 26 Aprili, 2018 vitakavyofanyika Mjini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)


NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUCHEZWA APRILI 20 NA 21

$
0
0
Hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) inatarajia kuchezwa Aprili 20 na Aprili 21,2018.

Nusu fainali ya Kwanza itachezwa Ijumaa Aprili 20,2018 ikiwakutanisha Stand United ya Shinyanga watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage,Shinyanga saa 10 jioni.

Singida United ya Singida watawakaribisha JKT Tanzania ya Dar es Salaam kwenye nusu fainali ya pili itakayochezwa Uwanja wa namfua Jumamosi Aprili 21,2018 saa 10 jioni.

Washindi kwenye nusu fainali hizo watacheza mchezo wa fainali May 31,2018.

JIJI LA DAR LAKABIDHIWA MPANGO WA KUONDOA MSONGAMANO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

SHIRIKA la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kupitia timu yake ya wataalam wa miundombini wamekabidhi mpango mkakati wa miundombinu ya usafiri kwa lengo la kuondoa msongamano wa magari kwenye Jiji la Dar es Salaam.

Mpango mkakati huo umekabidhiwa leo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana unahusisha ujenzi wa miundombinu ya usafiri ya aina mbalimbali huku ukitoa mapendekezo ya kujengwa ofisi na masoko pembezoni mwa Jiji hilo ili kupunguza msongamano hasa kwa kuzigatia ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na idadi ya watu milioni 10.

Akizungumza leo baada ya kukabidhiwa mpango huo kutoka kwa JICA, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Liana ameahidi kuwa mpango huo utafanyiwa kazi ili kupunguza msongamano unatokana na ufinyu wa miundombinu ya usafiri.

"Timu ya wataala wa JICA  wamefanya utafiti wao na kuja na mpango huu wa miundombinu ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam na kutoa mapendekezo ya mpangilio mzuri wa miundombinu hiyo ili kuhakikisha msongamano unapungua.

"Jiji tunahusika zaidi na mpango huu ambao tumekabidhiwa leo na JICA kwa maana ndio wenye Jiji la Dar es Salaam.Hata hivyo ni mpango ambao utatumia na wadau wote wanaohusika na miundombinu ikiwemo Wizara,"amesema.

Amefafanua mpango huo unazugumzia miundombinu ya usafiri ya aina mbalimbali ikiwemo ya barabara na reli na lengo ni kuhakikisha msongamano unapungua kwani unachangia kukwamisha shughuli za uchumi wa Jiji la Dar es Salaam kutokana na muda mwingi kutumika barabarani.
Ameongeza kuwa "Mpango huo unaenda hadi mwaka 2030 na lazima uheshimiwe na kutekelezwa kama ambavyo mapendekezo yake yanavyotaka".

Pia amesema mpango huo unaonesha namna ambavyo miundombinu katika Jiji la Dar es Salaam inatakiwa iwe na kubwa zaidi wameshauri kuwepo na masoko na ofisi pembezoni mwa Jiji ambazo  zitasaidia wakazi wake kutokuwa na ulazima wa kuinga kati ya mji kwa wingi kufuata mahitaji.

"Ni mpango ambao tumeahidi kuufanyia kazi , unazungumzia namna ambavyo miundombinu ya reli kwa ajili ya usafiri wa treni iweje na iwe kwenye maeneo gani.Ofisi za pembezoni mwa miji nazo ziwe wapi pamoja na mambo mengine mengi yenye lengo la kupunguza msongamano.Mpango huo unaonesha kutakuwa na barabara za juu,"amesisitiza.

Alipoulizwa nafasi ya JICA katika kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango huo , Liana amesema JICA ndio wawezeshaji na washauri kuhusu mradi huo ingawa nao  wameshiriki.

UBUNIFU: MAKEKE AJA NA VAZI LA UNGO LINALOTAMBULIKA KWA JINA LA "LUPAHERO"

$
0
0
 LUPAHERO
Baada ya uzoefu mkubwa katika matumizi ya mapishi jikoni, ungo umejizolea umaarufu mkubwa baada ya kuingizwa rasmi katika tasnia yasm sanaa na hususani katika ubunifu wa mavazi na kupewa jina la LUPAHERO na Jocktan Makeke.

Maanaya LUPAHERO

Ubunifu huu wa mavazi umepewa jina la LUPAHERO ambalo ni mchanganyiko wa majina mawili ambayo ni LUPAPIKE, neno la kinyakyusa lenye maana ya ungo na neno la pilini LUHELO, ambalo ni neno la kihehe lenye maana ya ungo.

Muunganiko wa maneno haya mawili yamelenga kuleta dhana ya ushujaa kutokana na ladha ya mavazi hayo kuwa na dhima hiyo, huku neno Luhelo likitamkwa herufi zamwisho kama Hero, herufi L ikibadilishwa kuwa R ilikupata neno hero la kingereza lenyemaana ya shujaa na kukamilisha maana halisi ya ubunifu huo kuwashujaa wa ungo.  

Jinsi wazo lilivyopatikana.

Katika maandalizi yaonyesho la kwanza kufanywa chini ya MAKEKE INTERNATIONAL lililofahamika kama I AM MAKEKE ndipo wazo hili la lupahero lilipozaliwa. Kwamujibuwa MAKEKE INTERNATIONAL ilimchukua muda mrefu kupata wazo la kufanya katika onyesho hilo licha ya kua na bidhaa nyingi za kubuni nguo mbalimbali ofisini kwake.

Baada ya kuwaza kwa muda mrefu ndani ya ofisi, alitoka nje na kurudi baada ya kutuliza akilila na wakati akirudi aliuona ungo kupitia dirisha uliokua umetundikwa ukutani kama pambo la ofisia mbapo aliamua kuuchukua na kukaa nao huku kichwa kikiendelea kuwaza na kuwazua ni wazo gani ataonyesha kwenye onesho lililokua mbeleyake.
Baada ya kuwaza kwa masaa kadhaa wazo lilimjia na kutaka kutoboa ungo aliokua nao  kwakiasi cha kuweza kuvaa shingoni ambapo alifanya hivyo na kupata ladha ya mapambo ya shingoni ya kimasaii la katika mwonekano wa ungo na ndipo alipoanza kufikiria mikato mingine ambayo   ungo unaweza kuingia na kudhihirisha ubunifu wa ungo kama vazi.

Baada ya kupata yote hayo Makeke alichukua daftari na kuanza kuchora kila alichokua amekiwaza kwa ufanisi zaidi kufanyia kazi kwa muda aliokua nao hali iliyofanya ubunifu wa ungo kutumika kwamara ya kwanza katikatamasha la I AM MAKEKE mpaka hivisasa.

Mikato ya Lupahero

MAKEKE INTERNATIONAL 
imelenga zaidi kujenga dhana ya ushujaa na asili ya kiafrika ili kujenga mazingira ya kuweza kujiamini na kujua kuwa wewe ni bora zaidi kutoka na jinsi ulivyo kama mwafrika na shujaa akiwa katika kila jambo.
Follow us on Facebook  @makeke international Instagram@makekeinternational  
blog makekeinternational.blogspot.com

DK MAGUFULI KUZINDUA RASMI TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE (JMKF) KESHO IKULU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

RAIS Dk. John Magufuli kesho anatarajia kuzindua rasmi  Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete inayofahamika kwa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika Ukumbi wa Mikutno wa Jakaya Kikwete ulioko Ikulu, Dar Es Salaam. 

Rais mstaafu Kikwete ndiye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya JMKF na uzinduzi huo rasmi utahusisha maofisa waandamizi wa Serikali, mabalozi wanaoziwakisha nchi zao Tanzania na hasa mabalozi wa Afrika ambako Taasisi hiyo inalenga kufanya kazi mbali ya Tanzania, wakuu wa taasisi mbali mbali za kimataifa, wadau wa Taasisi ya JMKF, wakuu wa asasi zisizokuwa za kiserikali (NGO’s) na wakuu wa taasisi za kijamii wakiwemo viongozi wa dini.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam na Pioneer Communications Limited kwa niaba ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)imesema uzinduzi huo  utafuatiwa na chakula cha jioni ambacho Rais Magufuli atawaandaliwa wageni watakaohudhuria sherehe hiyo ya uzinduzi, akiwemo Rais Kikwete mwenyewe na mkewa Mama Salma Kikwete.

"Taasisi ya JMKF iliyosajiliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka Februari, 2017, ilianza kazi Machi, mwaka jana wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya Wadhamini ya Kimataifa ya Taasisi hiyo ilipofanya kikao chake kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt mjini Dar Es Salaam,"imesema taarifa hiyo.

Imeongeza taasisi hiyo inayolenga kufanya kazi na kuelekeza nguvu zake katika maeneo matano, itaanzia na maeneo matatu ambayo ni Afya ya Mama na Mtoto, Maendeleo ya Vijana na Uwezeshaji wa Wakulima Wadogo katika maeneo ya vijijini na mashambani katika jitihada zao za kujinasua katika umasikini ama kupunguza athari na madhara ya hali ya umasikini.

"Mheshimiwa Kikwete anasaidiwa katika uendeshaji wa Taasisi hiyo na Bodi ya Wadhamini yenye sura ya Kimataifa ambayo wajumbe wake wanatoka nchi za Tanzania, Marekani, Afrika Kusini, Ureno na Malaysia.Wadhamini hao ni Balozi Ombeni Sefue aliyepata kuwa Katibu Mkuu Kiongozi na Balozi wa Tanzania katika  Canada na Marekani.

"Pia Profesa Rwekaza Mukandala aliyekuwa Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kwa miaka mingi, Profesa William Mahalu wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustine mjini Mwanza na Balozi Mwanaidi Sinare Majar ambaye amepata kuwa Balozi wa Tanzania katika Uingereza na Marekani,"imefafanua.

Wengine ni Mfanyabiashara maarufu Abubakar Saidi Bakhressa, Balozi Charles R. Stith aliyepata kuwa Balozi wa Marekani katika Tanzania, Msomi na Mtumishi wa Umoja wa Mataifa Bwana Carlos Lopez, Waziri mwandamizi katika Serikali ya Malaysia, Dato Sri Idris Jala na  Mtaalamu wa Masuala ya Fedha kimataifa Genevive Sangudi, Mtanzania mwenye makazi yake Afrika Kusini na Marekani.

Kutokana na kikao hicho cha kwanza cha Bodi ya Udhamini Machi mwaka jana, wataalamu mbali mbali pamoja na washauri wa kila aina, wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa JMKF,  Omari Issa wamekuwa katika matayarisho makubwa ya kuandaa nyaraka mbali mbali za msingi za kuongoza dira na dhima ya Taasisi hiyo kwa ajili ya uzinduzi rasmi na kwamba shughuli hiyo ya Ikulu itatangazwa moja kwa moja kwenye Televisheni ya Taifa ya TBC na vyombo vingine. 

TECNO CAMON X NA X PRO ZATAMBULISHWA RASMI

$
0
0

 Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING ambayo ni kampuni mama ya TECNO, Andy VAN  (Katikati)akizungumza na wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Tecno ambayo ni Tecno CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3.
Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING ambayo ni kampuni mama ya TECNO, Andy VAN (Wapili kutoka kushoto) wakionesha simu aina ya Tecno  CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3 mara baada ya kuzindua simu hiyo.
KAMPUNI ya simu za mkononi inayofanya vizuri barani Afrika inaendelea kutanua soko lake baada ya kuzindua simu mpya TECNO CAMON X yenye 20MP SELFIE,mfumo mpya wa Android 8.1 Oreo na Hios ya 3.3, ikiwa ni muendelezo wa toleo la ‘TECNO CAMON’ iliyozinduliwa nchini NIGERIA (LAGOSI), Tarehe 5/4/2018.

Katika uzinduzi huo TECNO imejihakikishia uzalishaji na usambazaji wa simu zenye technolojia na ubora zaidi katika masoko zaidi ya 40 hasa katika nchi za Afrika. Kampuni ya simu ya TECNO hivi karibuni imeweza kuingia mkataba na moja kati ya kampuni bora katika upande wa mitandao (GOOGLE) iliyozindua mfumo mpya ya uendeshaji wa simu za mkononi Android 8.0Oreo (Go edition), utakaotumika katika matoleo yote ya TECNO kwa ndani ya mwaka 2018.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi Makamu wa Rais wa TRANSSION HOLDING Sambayo ni kampuni mama ya TECNO, Bwana Andy VAN amesema, “TECNO haizalishi simu kwa kuzingatia maoni ya wafanyakazi wetu tu, ila kampuni inazingatia zaidi ushauri na maoni ya watumiaji ili kuwapatia kilichobora zaidi ukilinganisha na zilizopita”.

In Loving Memory

CONSUMER EXPO 2018


MICHUANO YA COPA COCA-COLA UMISSETA YAPOKELEWA KWA SHANGWE MKOANI TANGA

$
0
0
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio ya uzinduzi.
Na Mwandishi Wetu. Mashindano ya shule za sekondari ya Copa Umisseta yanayoendelea ngazi ya mikoa, yamezinduliwa mkoani Tanga, katika uwanja wa Mkwakwani na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali , wadau wa michezo na mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella. 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye alimwakilisha Waziri wa TAMISEMI, aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kutoa udhamini wa mashindano ya ngazi za chini na aliipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kudhamini mashindano haya na kuahidi kuwa serikali itafanya kila jitihada kuunga mkono jitihada za kufufua michezo ya mashuleni ili kuhakikisha inashirikisha wanafunzi wengi. 
“Serikali itahakikisha inajenga miundombinu ya michezo sambamba na kuhakikisha walimu wanapatiwa mafunzo ya taaluma ya michezo,pia tutahakikisha ratiba za vipindi vya michezo mashuleni zinafuatwa badala ya kutumia muda wa vipindi hivyo kufundisha masomo mengine”Alisema Shigella. 
Kwa upande wake Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini, , Sialouise Shayo,alisema kampuni ya Coca-Cola kupitia udhamini wake inahakikisha wanafunzi wanaoshiriki mashindano haya wanapatiwa vifaa vya michezo. “Kampuni ya Coca-Cola imekuwa ikidhamini mashindano haya ya Copa Umisseta kwa kipindi cha miaka mitatu sasa,lengo letu kubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo kuanzia ngazi ya chini,tunaamini kuwa michezo mbali na kujenga afya pia ina fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi”alisema Shayo. 
Kampuni ya Coca-Cola inatarajia kutoa vifaa vya michezo kwa shule za sekondari 4,000 kutoka mikoa mbalmbali nchini. 
Uzinduzi wa mashindano haya mkoani Tanga ni wa pili kufanyika baada ya kuzinduliwa mkoani Dodoma na unatarajiwa kufanyika katika mikoa mingine sita nchini kabla ya kufanyika katika ngazi ya Taifa mwezi Juni mwaka huu koani Tanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akipokea zawadi ya mpira kutoka kwa Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini, Sialouise Shayo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akipiga danadana katika uzinduzi huo
 Wanafunzi wakipokea vifaa vya michezo. Wanafunzi wakichuana katika mchezo wa soka siku ya uzinduzi.

BBC News Africa appoints Larry Madowo as Business Editor

$
0
0

Larry Madowo joins the BBC from Wednesday 11th April, leading its new Business Unit. The appointment is part of the BBC World Service’s continuing expansion in TV and Digital Video content for audiences in Africa, including new business programmes. 
Larry is a well-known Kenyan journalist and has previously hosted his own radio show, written a weekly newspaper column and fronted many popular TV programmes.  Larry has a vast experience in broadcasting, having worked with various well established local and international media organisations, and has made many appearances previously on the BBC. He is also a pioneering digital journalist on the continent with an impressive following of over 3 million on social media.
Larrry Madowo, says: “I'm thrilled to be joining the BBC and look forward to amplifying stories about entrepreneurship, ingenuity and innovation that I've witnessed as I have travelled all over Africa. I grew up admiring the quality of journalism the BBC produces around the world and it is an honour to be a part of a bold new team that will tell authentic African stories for audiences across multiple platforms.”
 Solomon Mugera, Regional Editor for BBC News Africa says “Larry is a fantastic addition to our new team and will be key in leading our new focus on business news and how it affects the lives of ordinary Africans. Our new language services and content will ensure we reach new audiences with our bold, innovative and relevant news.”

WAZIRI MKUU AKEMEA UPOTOSHAJI KUHUSU MUUNGANO, aonya sukari isiwe sababu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waulinde Muungano baina ya Tanzania Bara na Zanzibar na akawaonya wasitumie Bunge hilo kuupotosha. 
Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Aprili 10, 2018) Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019.

Waziri Mkuu amesema mjadala ulioibuka jana kuhusu suala la Muungano haukuwa na afya na kwamba hatarajii kuona hali hiyo ikijirudia tena Bungeni kuhusiana na suala la Muungano. 
“Mjadala wa jana sijaupenda kabisa na wala haukuwa na afya, ulikuwa ni malumbano baina waheshimiwa wabunge wawili. Hatuzuii Mhe. Mbunge kuuliza jambo ili apate ufafanuzi lakini pia haturuhusu mtu na mtu watumie Bunge kupotosha ukweli wa mambo,” alisisitiza. 
Waziri Mkuu amelieleza Bunge kwamba kuna maboresho ambayo yanafanywa hivi sasa na Serikali za pande zote mbili lakini akatumia fursa hiyo kulihakikishia Bunge kwamba majadiliano bado yanaendelea kwenye vikao halali vya SMT na SMZ ambavyo vinaongozwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Akitoa ufafanuzi kuhusu chanzo cha malumbano hayo, Waziri Mkuu alisema kiini cha malumbano hayo ni suala la uagizaji sukari kutoka nje ya nchi ili kufidia upungufu wa sukari uliopo nchini (gap sugar). Alisema katika kutimiza azma hiyo, Serikali haiangalii kama muagizaji ametoka Tanzania Bara au Tanzania Zanzibar.
Akitoa mfano, Waziri Mkuu alisema katika mwaka 2016, upungufu uliojitokeza ulikuwa tani 140,000 lakini waagizaji waliopewa vibali walikuwa wawili kutoka Zanzibar, watatu kutoka Bara na kiwanda cha sukari cha Mahonda kilipewa kibali cha kuagiza tani 390. 
“Katika mwaka 2017, gap sugar ilikuwa tani 140,000 na waliopewa vibali walikuwa ni wawili kutoka Zanzibar na wawili kutoka Bara, lakini kwa mwaka huu (2018) gap sugar ni tani 135,000. 
Tofauti na miaka ya nyuma, safari hii tumewapa vibali wenye viwanda ndiyo waagize sukari kutoka nje. Kwa hiyo, jambo hili la sukari lisivuruge Muungano wetu,” alisisitiza. 
Waziri Mkuu alisema nia ya Serikali ni kuzalisha sukari ya kutosha hapa nchini ili nchi ijitegemee na kawataka Mawaziri wa Biashara wa Zanzibar na Tanzania wawe makini ili sukari inayoagizwa nje isije kufurika soko la ndani kwa sababu gharama za uzalishaji sukari ya ndani ni kubwa.

Maafisa wa Sekretarieti ya maadili watembelea Klabu ya Maadili wa Shule ya Msingi Chang’ombe Dodoma

$
0
0
 Mwenyekiti wa Klabu ya Maadili wa Shule ya Msingi Chang’ombe iliyoko Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Ndg. Yohana Sambila akifanya utambulisho kwa Maafisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Ofisi ya Kanda ya Kati Dodoma waliofika shuleni hapo kufuatilia maendeleo ya Klabu hiyo.
 Mjumbe wa Klabu ya Maadili Shule ya Msingi chang’ombe iliyoko Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Ndg. Paskali Lazaro akitoa neno la shukrani kwa Maafisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ofisi ya Kanda ya Kati Dodoma walitembelea Klabu hiyo kwa lengo kujua maendeleo yake.
 Katibu Msiaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ofisi ya Kanda ya Kati Dodoma, Bw. Cathlex Makawia akikabidhi vitendea kazi vya kujifunzia mambo ya maadili kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Maadili wa Shule ya Msingi Chang’ombe Ndg. Yohana Sambila wakati alipotembelea Klabu hiyo kwa lengokujua maendeleo yake. Aliyesimama pembeni ya Yohana ni  Katibu wa Klabu hiyo Ndg. Witness Msigwa.
Mwalimu wa Usawa wa Jinsia wa Shule ya Msingi Chang’ombe, Bibi. Salome Konki akichangia mada katika kikao kilichowakutanisha Wananchama wa Klabu ya Maadili shuleni hapo na Maafisa kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma waliotembelea Klabu hiyo kwa lengo kujua maendeleo yake.
Katibu Msiaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Ofisi ya Kanda ya Kati Dodoma, Bw. Cathlex Makawia(aliyekaa katikati) katika picha ya pamoja na Wananchama wa Klabu ya Maadili Shule ya Msingi Chang’ome pamoja na Walimu wao mara baada ya kumaliza kikao kilichokuwa na lengo la kujua maendeleo ya Klabu hiyo. Kutoka kushoto ni Bw. Dotto Mwatengule – Mwalimu Mlezi, Bibi Magreth Kisanga – Mwalimu Mkuu na kutoka Kulia ni Bibi. Salome Konki – Mwalimu wa Usawa wa Jinsia akifuatiwa Ndg. Yohana Sambila – Mwenyekiti wa Klabu ya Maadili.

UJENZI WA UKUTA MERERANI WAOKOA MAMILIONI - MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kukamilika kwa ujenzi wa ukuta kuzunguka mgodi wa Mirerani kutasaidia kuongeza mapato ya Serikali ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya wizi na utoroshaji wa madini yaTanzanite. 
Ametoa kauli hiyo Jumanne, Aprili 10, 2018 Bungeni mjini Dodoma kwenye mkutano wa 11 wa Bunge, wakati akihitimisha mjadala wa mapitio ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa mwaka 2017/2018 na mwelekeo wa kazi za Serikali kwa mwaka 2018/2019. 
Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa ujenzi wa ukuta huo uliozinduliwa Aprili 6, mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kutasaidia pia kudhibiti ulanguzi na biashara ya magendo pamoja na kuimarisha usalama kwenye mgodi, kwa wafanyakazi na wafanyabiashara wa Tanzanite. 
“Kukamilika kwa ujenzi huo pia kutasaidia kuongeza mapato ambapo katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018, Serikali imekusanya takriban shilingi milioni 714 ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi milioni 147.1 kwa mwaka mzima wa 2017,” alisema. 
Waziri Mkuu alisema kabla ya ujenzi huo, inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya madini ya Tanzanite yaliyokuwa yanazalishwa kila mwaka, yalitoroshwa kwa njia za panya na Serikali yetu haikuambulia chochote. “Hii ni kutokana na kukosekana udhibiti wa kutosha wa madini ya tanzanite kuanzia kwenye uzalishaji hadi kwa wauzaji,” alisema. 
Alisema mbali na kuwepo kwa eneo la wachimbaji ndani ya ukuta wa Mererani, pia kutajengwa maduka yaTanzanite na viwanda vya kuongeza thamani, hususan vya ukataji, uchongaji na ung’arishaji. Vilevile, kutakuwa na maeneo ya burudani ambayo yatastawisha zaidi biashara ya Tanzanite na kuwavuta watalii wengi kwenda kutembelea eneo hilo.

BONGO MOVIE KUIBUA VIPAJI VIPYA NA KUHUBIRI AMANI, UPENDO NA UZALENDO TANZANIA

TASAF YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI MKOANI SIMIYU

$
0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Awamu ya tatu umeendelea kunufaisha wananchi  wakiwemo wakazi wa kijiji cha  Nkoma wilaya ya Itilima  na  Nyakabindi    wilaya ya  Bariadi  mkoaniSimiyu.

 Hayo yamebainishwa na baadhi ya Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini katika Kijiji cha Nkoma wilayani Itilima, Mtaa wa Nyakabindi na Mtaa wa Old Maswa wilayani Bariadi wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Mmoja wa wanufaika wa Mpango huo, Bibi. Rebecca Masunga kutoka Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi, amesema TASAF imemsaidia kutoka katika umaskini sasa anapata kipato kinachomwezesha kujikimu, kwa kuwa amelima ekari tatu za pamba, ekari moja ya mahindi, ana ng’ombe 14 na mbuzi wanne na amenunua plau kwa ajili ya kulimia.  

“Nilikuwa maskini wa kutupwa , nilipoingia TASAF na kuanza kupokea zile elfu 36 nilikopa fedha nikalima nyanya ekari moja nikauza, nilipata shilingi laki sita nikanunua ng’ombe watatu wakakua;  baadaye nikawauza nikapata milioni moja na laki tano nilinunua ng’ombe 14 ndiyo hao mnaowaona tunawachunga sasa” alisema Rebecca Masunga

“Tuna kikundi chetu ambacho tunaweka fedha zetu baadaye tunagawana, tukisha gawana tunaenda kuzalisha, tunalima nyanya, kabeji, pamba halafu tunauza; mpango wangu wa baadaye niwe na mtaji mkubwa na nijenge nyumba bora ” alisisitiza Bibi.Masunga.
 
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa  wa Simiyu wakikagua shamba la pamba la mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga (mwenye kitambaa cheupe kichwani) wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
PICHA B
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa  wa Simiyu wakiangalia mifugo ya mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
PICHA C
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akimpongeza mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Rebecca Masunga wa Mtaa wa Nyakabindi wilayani Bariadi kwa kununua jembe la kukokotwa na ng’ombe (plau) kwa ajili ya kulimia, wakati wa Ziara ya Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa  wa Simiyu kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.
PICHA D
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa  wa Simiyu walipotembelea na kuona nyumba ya mnufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Maskini(TASAF), Bibi . Stella Masamaki  wa Mtaa wa Old Maswa wilayani Bariadi, wakati wa Ziara ya Kamati hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo.


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

KICHUYA KUMKABIDHI MSHINDI WA BAJAJI MAFINGA

$
0
0
Mkazi wa Iringa, Mafinga Ndugu Mathias Edward (25) ambaye pia ni mshindi wa bajaji kupitia promosheni inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa wakishirikiana na kampuni ya mtandao wa simu na wadhamini ya ligikuu Tanzania Vodacom wamemkabidhi bajaji hiyo mnano tarehe tisa mwezi huu. 

Alizungumza wakati wa makabidhiano yaliyoongozwa na mchezaji wa klabuya Simba Siza KichuyaNdugu Mathias alisema “Niliunganishwa na mjomba wangu ambaye makazi yake hasa ni mkoani Dodoma yeye ni mchezaji mzuri kwahiyo alinishawishi ili na mimi niweze kujiunga nakucheza. 
 
Kupitia bajaji hii itanisaidia kubadili maisha yangu na kuanza rasmi kujitegemea kimaisha nikiwa kama kijana nayekaribia umri wa miaka 28. Nikiwa kama kijana msomi mwenye stashahada ya ukutubi nilihangaika sana kutafuta ajira na mwisho ya siku nikaamua kujiingiza kwenye maswala ya kilimo ili kuinuaki patochangu. 
 
Nilikuwa nachezana SportPesa kwanjiaya USSD ambayo napiga*150*87#, urahisi ambao upo kwenye SportPesa na ndio unaotofautisha na kampuni nyingine za michezo ya kubashirini kwamba viwango vya kampuni nyingine za kubashirini vya juu sana lakini kwa kampuni kama SportPesa viwango vyao ni vizuri, rahisi sana kushindana kila kitu kiko wazi. 
 
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya bajaji mchezaji mahiri watimu ya Simba Shiza Ramadhani Kichuya alisema “Kwanza kabisa napenda kukupongeze kwa zawadi hii uliyoishinda kwa kupitia ubunifu wako mwenyewe, ninaimani kuna watu wengi ambao wanatamani siku moja washinde kama wewe ulivyobahatika na inakubidi uwe mfano kwao kwa kuwaelekeza ili nao waweze kubahatika” “Mimi nikiwa kama mchezaji wa timu kubwa inayoshiriki ligi kuu Taanza rasmi kuchezana SportPesa iliniwezekuibuka mshindi siku moja” alimaliza Kichuya

BUSTANI YA KISASA MANISPAA YA SONGEA KUNZA KUTUMIKA MWEZI MEI MWAKA HU

$
0
0
MRADI wa bustani ya kisasa ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma umekamilika ,unatarajia kuanza kufanyakazi mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza na Ruvuma TV Afisa habari wa Manispaa Albano Midelo, amesema Mkandarasi tayari amekabidhi mradi huo kwa Manispaa. Bustani hiyo itakuwa na sehemuya Mgahawa,Maegesho ya Magari,kituo cha Utalii,sehemunya michezo ya watoto na huduma za choo, Kwa undani wa habari hii tizama video yake.

WATAKAO KAMATWA KWA KUJIHUSISHA BIASHARA YA MAGENDO HAWATABAKI SALAMA

$
0
0
SERIKALI mkoani Tanga imesema kuwa haitakuwa na simile na wananchi watakaokamatwa kujihusisha na kuingiza bidhaa za magendo kupitia bandari bubu kwani wanachangia kuikosesha mapato serikali. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo.

Alisema kuwa kumekuwepo na wimbi kubwa la wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia bandari bubu kupitishia bidhaa za magendo ambazo sio salama kwa matumizi ya binadamu. “Katika hili hatutakiwa na msamaha wala kumuonea mtu haya tukikukamata chombo tutakitaifisha pamoja na mali zake huku muhusika atachukuliwa hatua kali za kisheri nilazima wananchi wajifunzi kuona umuhimu wa kutumia bandari rasmi”alisema DC Mwilapwa. 

Aidha aliitaka Mamlaka ya usimamizi wa bandari Mkoani Tanga kuhakikisha utendaji kazi wao unaendana na kasi ya maboresho ya bandari hiyo unaofanywa na serikali kwa sasa. Awali Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama alisema kuwa maboresho ya vifaa na vitendea kazi katika bandari hiyo yameweza kusaidia kuongeza ufanisi wa kuhudumia shehena za mizigo kutoka siku kumi hadi nne. 

Alisema kuwa kuhudumia shehena za mizigo katika kipindi kifupi kumesaidia kupunguza gharama kwa wateja wanaohudumiwa na bandari hiyo . “Licha ya kuhudumia mizigo kwa awamu mbili lakini uwepo wa vifaa umesaidia kuboresha uwezo wa bandari yetu ya kuhudumia mizigo kwa ufanisi zaidi”alibainisha Mkuu huyo.

Sherehe hizo zinakwenda sambamba na kauli mbiu Bandari za TPA ni chachu ya uchumi Viwanda na Ustawi nchini Tanzania (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za wiki ya bandari pamoja na maadhimishi miaka 13 ya Mamlaka hiyo kulia Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akifuatilia matukio mbalimbali kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia ni Afisa Mtekelezaji Mkuu wa Bandari ya Tanga Donald Ngaire.

"TUJIEPUSHE KUMSINGIZIA MUNGU AJALI TUNASABABISHA WENYEWE"-RC RUVUMA

$
0
0
mkuu wa mkoa wa RUVUMA CHRISTINA MNDEMA amewataka wamiliki wa vyombo vya moto kuacha tabia ya kutoa lawama badala yake wasimamie sheria za barabarani kwani ajali nyingi zinatokea ni uzembe wa madereva wao. Amebainisha hayo wakati akizungumza na wamiliki wa vyombo hivyo huku mamlaka inayosimamia barabara TARURA NA TANROAD kuhakikisha barabara zinaboreshwa ili kupunguza ajali zinazoonyesha kusababishwa na miundombinu.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images