Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

TUWAKUMBUKE NAKUWASHUKURU MASHUJAA WETU WANGALI HAI - GRACA MACHEL

$
0
0
Na Leah Mushi( Afrika Kusini)

“Embu jiulize ni namna gani shujaa wa taifa angejisikia pale ambapo amekaa mbele ya watu wa rika tofauti jinsia tofauti wenye mirengo tofauti ya kisiasa wote wakimsifia na kumshukuru kwa werevu wake wakulipigania taifa?”

Maneno ya Mama Graca Machel mwanaharakati wa masuala ya wanawake na watoto wa Afrika akiongea mbele ya umati wa watu kutoka maeneo mbalimbali duniani waliofika kutoa salamu za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Winnie Mandela aliyefariki tarehe 2 Aprili 2018 nchini afrika kusini.

Winnie Madikizela-Mandela (81) alikuwa mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo hali iliyopelekea kufungwa mara kadhaa mbali na kuendelea kupokea vitisho lakini aliendea kuwa mwanaharakati mpaka mauti yaliyomfika. 

Winnie Mandela ambaye kwa wengi anafahamika kama mama wa taifa la Afika Kusini pia alikuwa mke wa Nelson Mandela  kwa miaka 38 toka mwaka 1958 mpaka walipoachana mwaka 1996 na kufanikiwa kupata watoto wawili.

Akiongea katika Msiba huo mama Graca Machel ambaye amekuwa akimuita Marehemu Winnie Mandela “dada mkubwa” amesema ni wakati sasa wa kuwaita mashujaa wa taifa na kuwashukuru wangali wakiwa hai kwakuwa hakuna ajuae kama wanasikia na kuona vile wanavyosifiwa wakati wa Misiba yao.

Pia amekemea tabia ya jamii kuwananga na kuwasema watoto wa wapigania uhuru kwakuwa wengi wao wamekosa miongozi na malezi bora ya wazazi kwakuwa wazazi wao walikuwa na ujasiri wa kuacha familia zao na kupigania taifa hivyo si sawa kuwasema na kuwanyooshea vidole badala yake waoneshe upendo zaidi kwao katika kile kilichofanywa na wazazi wao.

Kuhusu rambirambi na ahadi zinazotolewa misibani Mama Graca amewataka wananchi na wanasiasa kuacha maneno ya hadaa kwakuwa mengi yanayoahidiwa hayatekelezwi.

Akitolea mfano wa ahadi zilizotolewa wakati wa wa msiba wa Nelson Mandela miaka mitano iliyopita amesema “ kwasasa ukiangalia Afrika kusini mambo yamekuwa mabaya zaidi ya kipindi Mandela yuhai na hii inaonesha kiasi gani watu hawaishi ahadi zao walizoahidi na ndio jambo hata leo watu wengi wameahidi kuendeleza harakati za Winnie Mandela lakini nani anajua kama zitatekelezwa?”

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Ian Ferrao concludes term as Vodacom Tanzania Managing Director

$
0
0
 Vodacom Tanzania PLC (Vodacom) has today announced that Ian Ferrao, the Company’s Managing Director will be stepping down in June 2018. Ferrao has reached the end of his 3-year tenure at Vodacom and has opted not to renew his contract and instead move on to pursue other interests. Speaking in Dar es Salaam today, Vodacom’s Board Chairman Mr. Ali Mufuruki expressed his views on the Executive’s anticipated departure applauding him on his achievements since joining the Company in 2015.
“The Board is thankful for Ian’s years of service and his fantastic leadership. Ian exits the Company having steered us through significant milestones, leaving a progressive legacy in the Tanzanian market,” said Mufuruki.
Mr Mufuruki added that during his tenure Mr. Ferrao led the Company through a turnaround strategy that improved operations and spearheaded revenue and profitability growth back into the business.



“Ian has been a tremendous asset to Vodacom Tanzania. We are grateful for his strong leadership over the 3 years which was grounded by a resilient and sustainable 3-year turnaround strategy and a vision which transformed how Vodacom does business today. He leaves behind a strong leadership team which is committed to the Company’s success,” said the Company Chairman. Under his wings, the Company became the first and only Telecom Company to list 25% of its stake equivalent to TZS 476,000,085,000 on the Dar es Salaam Stock Exchange with over 40,000 local retail shareholders – many first time buyers- participating in the IPO. The first AGM was held with more than 1,500 shareholders in attendance and since its listing in July 2017, Vodacom has paid dividend of TZS 28.5 billion to its new shareholders as promised in its prospectus. 


The dividend policy called for a minimum of 50% of declared profit to be paid as dividends while Vodacom paid 60% of that profit. Additionally, Vodacom has recorded strong financial results in the past three years with modest revenue growth. Vodacom has expanded its market leadership position in terms of customer numbers and revenue market share and leads the industry on customer satisfaction indices such as Net Promoter Score (NPS) with a +12 pts gap to the next competitor.
Prior to joining Vodacom Tanzania, Ferrao was the Managing Director of Vodacom Lesotho.
“We wish him and his family the very best. I look forward to welcoming the new CEO and I am confident that working with Vodacom Tanzania’s executive leadership team, the Company will enjoy continued success in the future” concluded Mufuruki.
On his part Ferrao said, “It has been an enormous privilege to lead Vodacom Tanzania during an important period of transformation and growth. I am proud to have worked with remarkable colleagues who are extremely committed to leading Tanzania into the digital age and change lives through technology. Vodacom is today focused on driving profitable growth with emphasis on quality and innovation to maximize shareholder value. I wish the Company continued success for the future.”
Ms. Sylvia Mulinge will succeed Ferrao as the Managing Director of Vodacom Tanzania PLC. She joins the Company from Safaricom in Kenya where she currently serves as the Director for Consumer Business having joined the company in 2006. Ferrao remains fully committed to ensuring a smooth transition is achieved as he prepares to hand over the reins by August 31, 2018. Ms. Mulinge starts her new role as Vodacom Tanzania Managing Director on June 1st 2018.

MKOPO WA DOLA MILIONI 65 WA KAGERA SUGAR WAWEKEZWA NCHINI

$
0
0

Na Benny Mwaipaja

Serikali imeeleza kuwa kiasi chote cha dola za Marekani milioni 65 zilizokopwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera kutoka Benki ya CRDB kwa udhamini wa Serikali mwaka 2004 kimewekezwa nchini na hakijapelekwa kuwekeza katika nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda hicho kukopa kiasi hicho cha fedha ambacho kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa uwekezaji uliofanywa katika Kiwanda cha Kagera ni wa takribani dola za Marekani milioni 250 hivyo haiwezekani mwekezaji kukopa dola milioni 65 na kuzipeleka Congo ili hali kiwango cha uwekezaji nchini ni kikubwa.

“Mwekezaji wa Kiwanda hicho ni wa ndani na amejitahidi kuajiri watanzania wengi hivyo Serikali ipo katika mchakato wa kukiwezesha kiwe cha mfano ili kiendelee kuleta matokeo chanya kwa watanzania”, alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali la msingi la Mbunge huyo, alitaka kujua kiwango cha hisa ambacho Serikali inamiliki katika kiwanda cha Sukari cha Kagera na kiasi cha fedha kilichokopwa na kulipwa na mwekezaji huyo kupitia udhamini huo wa Serikali.

Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa sasa haimiliki hisa zozote katika kiwanda hicho na kuongeza kuwa hisa zake katika kiwanda hicho ziliuzwa mwaka 2001 baada ya kukibinafsisha kiwanda hicho kwa Kampuni ya Kagera Saw Mills Limit.Aidha Dkt. Kijaji alifafanua kuwa mwekezaji wa Kiwanda hicho alikopa kiasi cha dola za Maerekani milioni 65 kwa kutumia udhamini wa Serikali mwaka 2004, ikiwa ni udhamini (guarantee) wa kipindi cha miaka 12.

Alisema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho mimerejesha zaidi ya dola za Marekani milioni 56.88, sawa na asilimia 87.5 ya mkopo wote, na kwamba marejesho ya mkopo uliobaki wa Dola milioni 8.12 yatafikia ukomo wake mwezi Julai, 2019.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akijibu swali la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Bungeni Mjini Dodoma, aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Kagera, kukopa kiasi cha dola milioni 65 za Marekani ambacho amedai kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.

Washindi Zaidi wa Nyaka Nyaka Bonus Wazawadiwa

$
0
0
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Yusra Ali Ramadhani (kulia) aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 83 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.

Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania imewazawadia wateja wake 84 simu janja aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.

‘Katika promosheni hii murwa, Tigo inatoa bure jumla ya simu janja 12 kila siku. Pamoja na haya, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter,’

‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo, ambapo kufikia sasa tumewazawadia wateja 756 simu hizi janja zenye uwezo wa 4G’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo.

Kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 24 nchini,’ alisema.

Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa asilimia 45% tu ya Watanzania ndiyo waliofikiwa na huduma za kimtandao, huku asilimia 84% ya wale waliofikiwa wakitumia simu zao za mkononi kama njia kuu ya kupata huduma hizo za mtandao. Ubunifu huu wa Tigo utahakikisha kuwa idadi ya watumiaji wa huduma za mtandao inaongezeka nchini.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 kwa Hamisi Mohammed Yusuph (kulia) aliyeibuka kama mojawapo ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu za kisasa 756 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia *147*00# tangu kuanza kwa promosheni hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Shisael (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi 84 wa wiki hii katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu za kisasa 756 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia *147*00# tangu kuanza kwa promosheni hiyo.  

A Letter to Comrade Martin Thembisile (Chris) Hani

$
0
0
Comrade Chris,
To an ordinary mortal it would seem odd that I should communicate with you, us being worlds apart. To a Christian, such as I am, and to you, born a Catholic, being a committed member of the South African Communist Party (SACP), notwithstanding, the belief in and notion of life in the world after comes naturally. 

Furthermore, very African as both of us are, we firmly believe in the presence in our midst, of the souls of the departed, residing in, among other places, the hills and mountains, the valleys, the pristine forests and woods, and in our homes, among other beauties mother nature has endowed mother Africa. I therefore have no hesitation whatsoever in undertaking this mission of communicating with you Comrade Hani, coming as it does, on the 25th anniversary of your departure.

The chilly southern hemispherical autumn Easter Saturday of 10th of April, 1993, was the longest day in the final struggle for the freedom of South Africa, and for the emancipation of the black person in Africa and the world over.

 For as you lay in blood, murdered by the fatal shots fired by one infamous polish immigrant by the name of Janusz Walus, momentarily South Africa came to a standstill, the calmness before the impending storm, as the rest of Africa tuned in to SABC, BBC, VOA, local channels, grapevines, or whatever means, hoping, against hope, that it would be, what we now refer to as fake news. Sadly, you had departed, and the final struggle for South Africa would never be the same without your presence. Janusz, as it turned out, was not acting alone. 

It was not an act of a madman, mad as the act was. For, an accomplice, a hard core racist by the name of Clive Derby-Lewis, would be apprehended in no time. As you are aware by now Clive was in the National Party and later on a Member of Parliament from the Conservative Party. Both Janusz and Clive would, after a charged trial, be sentenced to rendezvous with a hangman, an appointment they did not keep, luck having been on their part due to the scrapping of the death penalty by the then new era, with sentences being commuted to life imprisonment. Paroled due to ill health, the unrepentant Derby-Lewis would subsequently pass on, on 3 November 2016. 

Interviewed a few days before his encounter with death Clive stressed that you were “a hardcore communist determined at all costs to lay the country to waste…” Even as he approached his death-bed he was of the belief that you were radical, uncontrollable, and enemy number one of the white people. As for Janusz, the unrepentant murderer had the audacity to request for parole. Successful first, the parole was later overturned by the Supreme Court. His South African citizenship has been revoked and an order has been made for him to be deported back to his native Poland upon serving the reminder of his sentence.

SERIKALI YAPONGEZA UTENDAJI WA TANESCO

$
0
0
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu.

Na Veronica Simba - Ngara

Serikali imelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutokana na utendaji kazi wake mzuri katika kuwapatia watanzania kote nchini huduma ya nishati ya umeme. Pongezi hizo zilitolewa hivi karibuni, Aprili 8 mwaka huu, na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati wa hafla ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara.

“Nalipongeza Shirika letu la TANESCO. Kwakweli Shirika hili limebadilika sana kiutendaji, hasa katika Menejimenti na wafanyakazi. Wanafanya kazi kwa kujituma. Baadhi ya watu walizoea kulibeza Shirika hili lakini wanajitahidi sana kwa sasa,” alisema Waziri. Waziri alisema kuwa kazi ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati ni kulisimamia Shirika hilo ili liendelee kufanya kazi nzuri kwa manufaa ya wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu.

Akizungumzia Mradi huo wa kuiunganisha Ngara na umeme wa Gridi ya Taifa, Waziri Kalemani alisema kuwa ni wa manufaa makubwa kwani utapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji na hivyo kuliongezea shirika uwezo zaidi wa kuwahudumia wananchi. “Kwa kutumia mafuta, Uniti moja ilikuwa inawagharimu TANESCO shilingi 578 wakati huu wa Gridi utawagharimu shilingi 154 tu kwa Uniti,” alifafanua.

Waziri aliwataka watendaji wa TANESCO kuhakikisha wanawahudumia wana-Ngara na watanzania wote kwa ubora zaidi kutokana na uwepo wa umeme wa Gridi ya Taifa katika maeneo mengi zaidi na kuondokana na ule wa mafuta ambao una changamoto kadhaa.

Aidha, Dkt. Kalemani alibainisha kuwa, sambamba na zoezi la kuhakikisha Tanzania nzima inaunganishwa na umeme wa Gridi ya Taifa, pia Serikali inaendelea kupeleka umeme vijijini kupitia miradi inayotekelezwa kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Alisema kuwa, kufikia mwaka 2020, hakuna kijiji kitakachobaki bila kuwa na umeme.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze akiwasilisha taarifa ya Mkoa wake kwa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, wakati wa hafla ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu.

Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa dhamira yake ya dhati katika kuhakikisha inawaondolea watanzania kero na changamoto mbalimbali ikiwemo ya umeme.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka pamoja na kumuunga mkono Waziri kwa kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano; aliipongeza Wizara ya Nishati inayoongozwa na Dkt Kalemani ambayo alisema ndiyo msimamizi mkubwa wa shughuli zinazotekelezwa na shirika hilo. Alisema kuwa, kwa kuiunga Ngara na umeme wa Gridi ya Taifa, kiasi kikubwa cha fedha kitaokolewa. “Kwa harakaharaka, tutaweza kuokoa takribani shilingi bilioni mbili kwa mwaka baada ya kuzima mitambo hii ya mafuta.”

Aliongeza kusema kuwa TANESCO itaendelea kuzima vituo vya mafuta sehemu mbalimbali nchini ambapo itasaidia kupunguza gharama za kufua umeme kwa kutumia mafuta. Awali, akiwasilisha taarifa ya TANESCO kwa Mkoa wa Kagera, Meneja wake, Mhandisi Francis Maze alisema kuwa kabla ya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, Wilaya ya Ngara ilikuwa ikitumia umeme wa mafuta ambapo mahitaji ya juu kwa Wilaya hiyo ni megawati 1.38.
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leyla Muhaji akifurahia ngoma pamoja na kikundi cha burudani kilichokuwa kikitumbuiza wakati wa hafla ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu.

Mkutano wa Kimataifa wa Nane wa Wiki ya Kijani

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (Mb.) akihutubia kwenye Mkutano wa Nane wa Wiki ya Kijani, unaowakutanisha wadau mbalimbali wanao simamia na kutengeneza vifaa na miundombinu mbalimbali ya Tehama. Mkutano huo unatarajia kuangalia namna mbalimbali za kupambana na matumizi ya Tehama yanayochafua mazingira; umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Serikalini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akiwemo Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Dkt. Sira Ubwa (Mb.), Katibu Mkuu (Mawasiliano) Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi, Mkurugenzi wa ITU (International Telecomunication Union), Dkt. Chaesub Lee, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Kilaba. Mkutono huo unafanyika katika Hoteli ya Sea Clif Mangapwani, Zanzibar kuanzia tarehe 9-12, Aprili 2018. 
Waziri wa Ujenzi, Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa, akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo visiwani Zanzibar na kuelezea faida ya mkutano kufanyikia Unguja. Alisema kwa mazingira ya sasa, changamoto iliyopo mbele yetu ni kushirikiana kwa pamoja ili kuziepusha nchi zetu na uharibifu utokanao na matumizi ya vifaa chakavu vya kielektroniki. Mhe. Dkt. Sira alitumia fursa hiyo kuwapongeza kwa mjadala muhimu utakaoendelea wa utunzaji wa mazingira na kuwasihi wasiache kutembelea vivutio vya asilia vilivyopo visiwani humo. 
Mkurugenzi wa International Telecommunication Union (ITU) Dkt. Lee akizungumza kuhusu mjadala na maazimio ya mkutano huo muhimu wa kimataifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Wiki ya Kijani. 


Muhimbili Yapokea Msaada wa Vifaa Tiba

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa tiba kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wenye thamani ya shilingi milioni kumi.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bi. Nuru Mhando amesema mamlaka hiyo inatambua na kuthamini dhamira na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikisha huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wote hivyo imeamua kuunga mkono juhudi hizo kwa kutoa msaada wa viti vya kubebea wagonjwa  na vipima joto vya kisasa .

‘’Kwa kutambua hilo mamlaka imeona ni vyema iunge mkono juhudi hizi katika wiki hii ambayo tupo kwenye shamrashamra za kuadhimisha miaka kumi na tatu tangu TPA ianzishwe, Aprili 15 ,2005, Mamlaka imeona ni vyema kusheherekea kumbukumbu hizi kwa kutoa mchango huu ili kusaidia wagonjwa katika jengo la watoto.

‘’Tunaamini msaada huu utasaidia kuhudumia watoto wengi kwa wakati mmoja na hivyo kutatua changamoto ya ukosefu wa vifaa hivi ambavyo  mnakabiliana navyo,’’amesema Kaimu Mkurugezi huyo wa TPA.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za uuguzi  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),  Agness Mtawa ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, amesema  msaada huo utaongeza kasi ya utoaji huduma kwa watoto. Amefafanua kwamba jengo la watoto lina vitanda takribani 300 hivyo mahitaji ya viti vya kubebea wagonjwa pamoja na mahitaji mengine ni makubwa.

“Tunawashukuru TPA kwa msaada huu mliotupatia , mmeongeza kasi ya utoaji huduma niwahakikishie kwamba msaada huu utatumika kama ambavyo imekusudiwa,’’amesema Mkurugenzi Mtawa. Ametoa rai kwa wadau wengine kujitokeza kuchangia huduma za afya na kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma hizo.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Agness Mtawa (kulia) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akipokea msaada wa viti 20 vya kubebea wagonjwa kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bi. Nuru Mhando wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Nuru Mhando (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Agness Mtawa (kulia) wakiwasukuma watoto wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Nuru Mhando (wa tano kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Agness Mtawa wa Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja.

WAISLAMU DHEHEBU LA SHIA ITHNA ASHERI IMAMIA MWANZA WASHIRIKI IBADA KANISANI

$
0
0
Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee ambaye pia ni Mwenyekiti wa The Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya Ziwa akisisitiza jambo katika ibada iliyofanyika katika Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Bwiru jijini Mwana, mwenyekiti huyo na waumini baadhi ya dini ya Kiislamu waliakwa kushiriki kwenye ibada hiyo ambayo imeandika historia mpya baina ya Waislamu na Wakristo kuwa wote ni wamoja na wanamuabudu Mungu mmoja.Kutoka kushoto wa pili ni Kaimu Katibu Mkuu wa kanisa hilo Philipo Majuja.

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WAISLAMU wa madhehebu ya Shia Ithna Asheri Imamia wamesema kitendo cha Wakristo wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) cha kuwaalika kushiriki Ibada kanisani kimefungua ukurasa mpya kwa waumini wa madhehebu hayo nchini.

Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) Tawi la Tanzania Alhaji Sibtain Meghjee ametoa kauli hiyo juzi katika Ibada iliyofanyika katika Kanisa la AICT Bwiru jijini Mwanza ambapo alikabidhi fimbo 11 kwa walemavu wa macho,vitabu vya Kuran na kalenda kwa waumini wa kanisa hilo.

"Mambo mengi yaliyopo kwenye Biblia na Kuran asilimia 90 yanafanana na kinachotakiwa kwa waumini wa dini zote za Kikristo na Kiislamu ni kuvumiliana kutokana na imani zao na hivyo ushirikiano huo utadumisha amani na utulivu kwenye jamii bila kubaguana kwa kutofautiana kiimani,"amesema.
Sheikh wa Bilal Muslim Mission of Tanzania Sheikh Hashim Ramadhan akitoa neno kwa waumini wa kanisa la AICT Bwiru wakati wa ibada iliyowashirikisha pia waumini wa dini ya Kiislamu akisema wote ni watoto wa baba na mama mmoja na wanamwabudu Mungu mmoja na hakuna sababu ya kuchukiana bali kupendana.

Meghjee ambaye pia ni Mwenyekiti wa The Bilal Muslim Mission of Tanzania Kanda ya Ziwa amesema wapo baadhi ya watu wenye nia mbaya wamekuwa wakieneza propaganda chafu dhidi ya Uislamu wakiwahusisha na mambo mabaya kwenye jamii na kuipongeza serikali kwa kuanzisha kamati ya amani Mkoa wa Mwanza na kuufanya kuwa wa jamii moja bila kubaguana.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MAKAMU WA RAIS AZINDUA CHANJO YA KUKINGA SARATANI YA KIZAZI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu (katikati), Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu pamoja na wadau wengine wa Afya wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tuoaji wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine) uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem, jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshikilia chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine) wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem, wengine pichani ni mabinti waliokuwa wa kwanza kupatiwa chanjo hiyo wakati wa uzinduzi, kushoto ni Neema Felix (14) mkazi wa Mbagala na mwingine ni Hadija Bakari (14) mkazi wa Kigamboni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Binti mwenye umri wa miaka 14 anayefahamiaka kwa jina Hadija Bakari mkazi wa Kigamboni akichomwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine) wakati wa uzinduzi wa chanjo hiyo kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mabinti wa kwanza kupata chanjo ya ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi (HPV Vaccine), aliyesimama kushoto ni Hadija Bakari (14) mkazi wa Kigamboni na kulia ni Neema Felix (14) mkazi wa Mbagala.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MZEE MWINYI, KIKWETE WAONGOZA MAMIA YA WAKAZI DAR KUAGA MWILI WA MTOPA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

VIONGOZI wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali wakiongozwa na Rais mstaafu Mzee Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete wameongoza mamia ya wakazi wa Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Marehemu Mzee Ally Mtopa (76) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mzee Mtopa amefariki dunia jana asubuhi ya  Aprili 9 mwaka huu kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa ratiba ya maziko ya mzee Mtopa anatarajiwa kuzikwa kesho mkoani  Kijijini kwake Nanjilinji wilayani Kilwa mkoani Lindi ambako leo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walijitokeza kumuaga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Mwili wa mzee huyo ulianza kuagwa saa mbili asubuhi na kuendelea hadi mchana hospitalini hapo.
Kabla ya kuaga mwili huo viongozi kadhaa akiwamo Mzee Mwinyi, mzee Kikwete pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrhman Kinana walishiriki kwenye ibada iliyofanyika katika msikiti uliopo katika Hospitali hiyo ya Muhimbili.

Mbali ya viongozi hao walikuwepo viongozi wengine kadhaa ambapo kila mmoja aliyepata nafasi ya kumzungumzia Mtopa wamesema kifo chake ni pengo kwa CCM kwani alikuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha chama hicho kinasonga mbele.

Baada ya kuagwa kwa mwili huo safari ya kuusafirisha mwili huo ilieneza kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Lindi.
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete,  Rais Mstaafu, Alhaj Dk. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Ally Mohamed Mtopa leo katika Mskiti wa Mhimbili , jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka.
Rais wa Awamu ya Pili, Alhaj Dk.Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa mtoto wa marehemu wa wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Lindi, Ally Mohamed Mtopa mara baada ya kuaga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Waombolezaji wakiwa katika viunga vya hospitali ta Taifa Muhimbili baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Marehemu Mzee Ally Mtopa. 

NGORONGORO HEROES TUNACHOHITAJI NI USHINDI TU - NINJE

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii

KOCHA Mkuu wa Ngorongoro Heroes Ammy Conrad Ninje amesema wao hawataangalia ni waamuzi gani watakaochezesha mchezo huo ingawa Shirikisho la soka barani Afrika limetoa orodha ya waamuzi watakaotumika katika mchezo huo kutoka Congo Brazaville.

Kumeibuka na mjadala wa kwanini Mwamuzi wa Congo Brazzaville Fitial Charel Just Kokolo ameteuliwa kuchezesha pambano hilo, hata hivyo Ninje amesema hawatakuwa na wasiwasi kwani wanaamini haki itatendeka na kumpata mshindi kihalili.

"Sisi tunachohitaji ni fair unajua hatuwezi kupangua na pia lipo nje ya uwezo wetu, ila tunawahitaji wachezeshe kwa haki, atakayeshinda basi apate nafasi ya kusonga mbele, ukiangalia sisi na Congo DR tupo karibu kama ilivyokuwa kwa Congo Brazzaville lakini wao wapo karibu zaidi .Mimi nawatayarisha vijana wangu tukacheze mpira vizuri tujaribu kutumia nafasi zetu.

"Tusiangalie refarii, sisi wenyewe tujipange kwenda kuwa washindani na kuangalia ni mbinu gani tutazitumia ili tupate ushindi," ameeleza Ninje.

Kwa kukumbusha Ngorongoro Heroes watakuwa na kibarua kizito April 22 mwaka huu katika Uwanja wa Stade Des Martyrs uliopo katika jimbo la Kinshasa ambapo watalazimika kupata ushindi wa aina yoyote ama sare ya mabao ili kusonga mbele na kukutana na Mali.

Waamuzi wa mchezo huo wa marudiano wote wanatoka Congo Brazzaville .Muamuzi wa kati atakuwa Fitial Kokolo, waamuzi wasaidizi ni Beaudrel Ntsele Roul na Tritton Franck Audiard Diawa.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya 0-0 Kabwili alionesha kiwango bora kwa kuokoa hatari nyingi ambazo zilielekezwa langoni.

Hata hivyo katika michezo miwili ya kirafiki kati ya Msumbiji na Morocco kipa Aboutnalib Mshery alionesha kiwango kizuri pia.

Katika hatua nyingine kocha Ninje amesema kambi inaendelea vizuri na wamekuwa na mazoezi mazuri kwani sasa wamekuwa wakifanya mazoezi mara mbili kwa siku, wakijaribu kutatuta tatizo la ufungaji ambalo limejionesha katika michezo mitatu hadi hivi, huku ukizingatia kuwa wanahitaji kufunga bao katika mchezo wa marudiano.

TRA YAKUSANYA TRILIONI 11.78/- NDANI YA MIEZI TISA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA) imesema katika kipindi cha miezi 9 ya mwaka wa fedha 2017/2018 kuanzia Julai 2017 hadi Machi mwaka huu wamekusanya Sh.Trilioni 11.78.

Akizungumza Dar es Salaam leo ,Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Richard Kayombo amesema makusanyo hayo yameongezeka ikilinganishwa na Sh.Trilioni 10.86 zilizokusanywa kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha was 2016/17.Kiasi hicho in sawa na ukuaji wa asilimia 8.46.

"Katika Machi mwaka 2018 pekee TRA imekusanya jumla ya Sh.Trilioni 1.54 ikilinganishwa na makusanyo ya Machi mwaka 2017 ambapo ilikusanywa Sh.Trilioni 1.34 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 14.49," amesema Kayombo.

Amefafanua kufanikiwa Katika makusanyo hayo yametokana na walipa kodi ,viongozi wa ngazi zote na wananchi pamoja na kampeni kadhaa tunazofanya ikiwamo ya usajili wa walipa kodi nchi nzima.

Pia TRA inaendelea kuwakumbusha walipa kodi kulipa kodi kwa wakati ,kusikiliza malalamiko pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kulipa madeni ya nyuma.

Amefafanua kipindi hiki wanaendelea na usajili wa walipakodi wapya wakiwemo wamachinga ambapo kwa wiki hii wapo mkoa wa Geita.

"Tunawakarabisha wafanyabiashara wa mkoa wa Geita kujitokeza kusajiliwa na kupata namba ya utambulisho ya mlipakodi (TIN) na pia kutoa kero zao kwa maofisa wa mamlaka ili wasikilizwe na kuhudumiwa.

"Pia nachukua fursa hii kuwakumbusha wananchi Aprili hadi Juni ni robo ya mwisho ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa hiyo walipe kodi ya majengo ambayo kwa sasa unaweza kulipa kwa njia ya mtandao kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga *152*00# na kufuata maelekezo,"amesema Kayombo.

Amesema wanaendelea kutoa elimu ili kila anayestahili alipe kodi kwa hiari na kwa wakati na mwenye malalamiko yoyote ya makadirio amuone meneja wa eneo husika na vilelezo vyote.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu akiongoza kikao cha bunge mjini Dodoma Aprili 10, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Bungeni mjini Dodoma Aprili 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2018/2019 bungeni mjini Dodoma , Aprili10, 2018.
Waziri, wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwayembe akteta na Naibu wake, Juliana Shonza, bungeni mjini Dodoma Aprili10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa Alex (kushoto) na Antony Mavunde wakiteta bungeni mjini Dodoma, Aprili 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa Alex akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma Aprili 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde wakishangilia bungeni mjini Dodoma Aprili 10, 2018 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MPINA AFUFUA KIWANDA CHA NYAMA SHINGANYA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametoa siku saba kwa wawekezaji wa kiwanda cha nyama Shinyanga cha Kampuni ya Triple S Beef Limited na Agri Vision kuwasilisha hati zote za umiliki hati ya eneo la kiwanda na eneo la kuhifadhia mifugo baadha ya kushindwa kukiendeleza kwa miaka 11.

Akizungumza katika kiwanda hicho leo Mpina amuagiza Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji Jones Mwalemba kutoka Hazina kuhakikisha kwamba ifikapo Juni 30 mwaka huu kiwanda hicho kiwe kimempata mwekezaji ambaye ataanza kazi mara moja ya uchinjaji ili kutoa ajira na kuliingizia taifa mapato.

Aidha amemuagiza Msajili wa Hazina kuanza uhakiki wa mali zote za kiwanda hicho baada ya kubainika wizi uliokithiri katika kiwanda hicho. 

Pia Mpina ameamuru mmliki wa Kampuni inayolinda kiwanda hicho kukamatwa mara moja na kufikishwa katika mikono ya sheria kwa ajili ya kujibu mashitaka wa wizi wa mali za kiwanda hicho ambapo amemtaka Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuanzia sasa kiwanda hicho kilindwe na vyombo vya Serikali badala ya makampuni binafsi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akiangalia moja ya sehemu ya jengo la Kiwanda cha nyama cha Shinyanga iliyoharibiwa na kutolewa mabomba ambapo pia vitasa vya mlango vimetolewa alipofanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda hicho leo. (Picha na John Mapepele)Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina(Mwenye Miwani) akioneshwa eneo la kiwanda cha nyama Shinyanga na Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Jones Mwalemba(aliyenyoosha mkono) Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Asimwe Lovince kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Wilaya a shinyanga wa CCM. (Picha na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga ( Mwenye Miwani) Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakari Mkadamu akivunja kufuli la mlango mkuu wa kuingilia katika kiwanda cha nyama Shinyanga mara baada ya waziri Mpina kufanya ziara ya kushitukiza katika kiwanda hicho. (Picha na John Mapepele)Na John Mapepele, Shinyanga 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC ATOA ONYO KWA WATUMISHI WA SERIKALI WATAKAOSHINDWA KUSHIRIKI MICHANGO YA MAENDELEO

$
0
0
Na Shushu Joel, Busega.

MKUU wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera ametoa onyo kali kwa watumishi wa serikali watakaoshindwa kutoa michango ya maendeleo kwenye sehemu wanazoishi kwa kisingizio cha utumishi wa serikali.

Akitoa agizo hilo kwenye baraza la madiwani mkuu huyo wa wilaya aliwataka madiwani wote kwenda kuwasambazia watumishi wote wa serikali walio katika kata zao kushiriki kikamilifu michango yote ya kijamii ili kuhakikisha wanafanikisha malengo waliyojiwekea kwenye kijiji au kitongoji hicho.

Alisema kuwa kumekuwa na tabia za kutokushiriki kwa watumishi wa serikali kwenye shughuli za maendeleo mahali ambapo wanaishi kwa kisingizio cha kuwa ni mwajiriwa wa serikali hivyo awezi kuchangia michango ya aina yeyote ile katika jamii kwa madai kuwa serikali inawakata fedha za michango hiyo.

Aliongeza kuwa watumishi wanatakiwa kutambua kuwa nao ni wanajamii kama walivyo wengine hivyo wanatakiwa kutoa kila aina ya mchango unaokuwepo katika jamii wanazokaa kwa lengo la kusaidia maendeleo yanayopangwa na jamii ili kufanikisha kile wanachokihitaji kifanyike kwa maendeleo ya yote hivyo mnatakiwa kuchanga kama wanavyofanya wengine.

“Kwa mtumishi ambaye atakiuka agizo la uchangiaji wa maendeleo katika wilaya yangu basi jera inamuhita kwa kugoma kuchangia”

Kwa upande wake diwani wa kata ya Imalamate Richard Magoti amempongeza mkuu wa wilaya hiyo kwa kutoa tamko hilo kwani ilikuwa ni changamoto iliyokuwa ikiwasumbua juu ya majibu waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa watumishi wa umma katika suala la michango ya maendeleo.

Aliongeza kuwa katika kata yake changamoto hizo zilikuwa zinajitokeza lakini kulingana na uelewa wa baadhi ya watumishi walikuwa wakishiriki katika zoezi la uchangaji wa fedha katika kufanikisha miradi ya maendeleo inayokuwa na ubunifu kutoka kwa wananchi ili iweze kuwasaidia kwenye vijiji vyao.

Aidha Magoti amemtaka mkuu huyo wa wilaya kulisimamia kikamilifu jambo hilo kwani watumishi wengi wa serikali wamekuwa sio miongoni mwa jamii kutokana na kutokushiriki kikamilifu katika ufanikishaji wa miradi katika jamii.
MKUU wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwera (aliyesimama) akizungumza kwenye baraza la madiwani mkuu lililofanyika wilayani hapo.

"BQ CONTRACTOR" YANYAKUA TUZO YA UBORA YA KIMATAIFA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Injinia John Bura (wa pili kutoka Kulia) akiwa amenyanyua Tuzo ya Ubora ya Kimataifa (ISO 9001:2015) Baada ya Kampuni yake kukidhi viwango vya Kimataifa, baada ya kukabidhiwa na Mkaguzi wa Ubora wa Mifumo ya Kimataifa  (AQC Midle East FZE), Alfred Lihasi (kushoto), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julias Nyerere, jijini Dar es salaam leo. Mengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Contractors Association of Tanzania, Injinia Lawrence Mwakyambiki.
Mwenyekiti wa Contractors Association of Tanzania, Injinia Lawrence Mwakyambiki (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Injinia John Bura, Tuzo ya Ubora ya Kimataifa (ISO 9001:2015) kwa niaba ya Mkaguzi wa Ubora wa Mifumo ya Kimataifa (AQC Midle East FZE), Alfred Lihasi (kushoto). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori
Mkaguzi wa Ubora wa Mifumo ya Kimataifa (AQC Midle East FZE), Alfred Lihasi akiwasilisha mada katika mkutano wa Wakandarasi, uliofanyika
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julias Nyerere, jijini Dar es salaam leo
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Injinia John Bura wa pili kutoka Kulia akieleza manufaa ya Tuzo hiyo ya Ubora wa Kimataifa baada ya Kukabidhiwa. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori Kushoto ni Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Hilu Bura na Katikati ni Mtaalam wa Mawasiliano na Msaidizi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya BQ Injinia Lorenco Simon.

TAARIFA YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KWA UMMA-KUFUATIA TUKIO LA MOTO KWENYE UKUMBI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linapenda kutoa taarifa kwa umma kufuatia tukio la moto kwenye ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotokea mnamo tarehe 09 Aprili, 2018 majira ya saa 1:28 usiku mkoani Dodoma.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa moto huo ulisababishwa na shoti iliyotokana na Power bank iliyokuwa inatumiwa kuchaji simu. Shoti hiyo ilisababisha kuungua kwa simu, Power bank, sehemu ya meza na kapeti kitendo kilicholeta moshi mkubwa na taharuki miongoni mwa Wabunge. Ukiachilia mbali taharuki kwa Waheshimiwa Wabunge hakuna madhara kwa binadamu yaliyotokana na moto huo.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa rai kwa Watanzania wote kuchukua tahadhari kubwa hasa wanapokua wanatumia vifaa vya kieletroniki ambavyo kwa sasa vipo katika matumizi hadi katika ngazi ya familia. Moto huzuka tu endapo kitapatikana chakula cha moto, joto la kutosha na hewa ya oksijeni (fuel, heat and oxygen).

Sambamba na hayo Kamishna Jenerali anahimiza uzingatiaji wa kinga na tahadhari ya moto katika maeneo yote. Wamiliki wa maeneo ya umma, binafsi na biashara wanapaswa kufunga vizimia moto kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lipo imara na litaendelea kuwaelimisha Watanzania kuzingatia kinga na tahadhari ya moto ili kuhakikisha maisha na mali vinakuwa salama. Imetolewa na;

CGF. Thobias Andengenye
Kamishna Jenerali
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
10 Aprili, 2018

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND KUZURU NCHINI

$
0
0
ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA POLAND NCHINI 11-13 APRILI 2018

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Poland, Mhe. Prof. Jacek Craputowicz atafanya ziara ya kikazi nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 hadi 13 Aprili 2018. Katika ziara hiyo, Prof. Craputowicz pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) Jijini Dar Es Salaam tarehe 12 Aprili 2018. Viongozi hao watajadili namna ya kuboresha mahusiano na mashirikiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Poland, hususan katika eneo la uwekezaji na biashara. 

Poland ni moja ya nchi zinazounga mkono Sera ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020. Katika kuunga mkono Sera hiyo, Serikali ya Poland imetoa mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 110 kwa Serikali ya Tanzania. 

Kati ya fedha hizo, Dola za Marekani milioni 55 zimetumika kujenga kiwanda cha kuunganisha matrekta Wilayani Kibaha, Mkoani Pwani ambacho kimeshaanza kazi na Dola za Marekani milioni 55 ni kwa ajili ya kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ya kilimo katika mikoa minane ya Rukwa, Katavi, Manyara, Ruvuma, Dodoma, Shinyanga, Njombe na Songwe.

Prof. Craputowicz na mwenyeji wake watashiriki hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa ofisi ya Ubalozi wa nchi hiyo zilizopo nyumba namba 15, mtaa wa Mtwara, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 12 Aprili 2018. Poland ilifungua upya Ubalozi wake nchini mwaka 2017 baada ya kuufunga mwaka 2008 na kabla ya hapo nchi hiyo ilikuwa inawakilishwa kutokea Nairobi, Kenya. 

Baada ya ufunguzi viongozi hao watafanya mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi hizo saa tano asubuhi. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dar es Salaam
10 Aprili, 2018

WAFANYAKAZI TPA WATUMIA MAADHIMISHO YAO KWA KUCHANGIA DAMU KUSAIDIA WENYE UHITAJI

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), wameshiriki kuchangia damu kwa lengo la kusaidia wenye uhitaji wa damu nchini ili kunusuru maisha yao.

Tukio hilo la wafanyakazi hao kuchangia damu limefanyika leo kwenye moja ya viwanja vyao vilivyopo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza wakati wa uchangiaji damu katika Maadhimisho ya 13 tangu  kuanzishwa TPA, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari (Dowuta), Mashaka Karume amesema maadhimisho hayo ni daraja la kuwakutanisha wao na jamii kwa kutoa msaada sehemu mbalimbali likiwemo hilo la kuchangia damu.

Karume amesema maadhimisho ya hayo ni sehemu ya kukutana na menejimenti nje ya kufanya kazi  lakini tunashirikiana katika masuala ya kijamii.

"Maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya bandari kama wafanyakazi tunaona mafanikio ambayo ni pamoja na mamlaka kushiriki kutoa msaada pamoja na hili la uchangiaji damu,"amesema Karume
 Wafanyakazi wa TPA wakijiandaa katika uchangiaji damu katika viwanja vya bandari ikiwa ni maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafayakazi wa Bandari, Mashaka Karume akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uchangiaji damu katika maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafayakazi wa Bandari, Mashaka Karume akiwa katika picha pamoja na wafanyakazi wa mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images