Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

TPDC najitihada za kulihakikishia Taifa gesi ya kutosha

0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) akiwammiliki wa leseni za vitalu vya gesi na mafuta nchini kwa kushirikiana na mkandarasi, kampuni ya Dodsal wanaendelea kufanya utafiti (ukusanyaji wa takwimu za mitetemo “2D seismic data” utafiti unahusisha eneo lenye urefu wa takribani km 1287) zaidi wa gesiasilia katika Kitalu cha Ruvu kilichopo Mkoa wa Pwani na baadhi ya maeneo ya Dar es salaam kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gesi asilia au mafuta ya kutosha itakayojenga uchum iimara wa viwanda.

Akielezea umuhimu wa utafiti huo, Simon Kimario ambaye ni Mjiofizikia kutoka TPDC amesema kuwa lengo kuu la utafiti huo nimuendelezo wa utafiti wa mafuta na gesi unaofanywa na mwekezaji Dodsal Hydrocarbons akishirikiana na TPDC katika kitalu cha Ruvu ilikuwezesha kugundua gesi asilia nyingi zaidi na pengine mafuta ilikuhakikisha Taifa linakuwa na chanzo imara cha nishati ambacho kitalisaidia taifa katika kujenga uchumi wa viwanda.
Ramani inayoonyesha kitalu cha utafiti cha Ruvu

“Tayari hatua kadhaa zimeishafanyika kama vile; uandaaji wa ramani ya kiutafiti ambayo kazi yake nikuonyesha eneo la kitalu na maeneo muhimu ya kufanyia utafiti, ambapo kunapelekea kwenye hatua nyingine ya kwenda kwenye eneo halisi na kubaini mistaria ambayo taarifa za mitetemo zitachukuliwa, hatua ambayo itanguliwa na zoezi la kupata vibali na kuelimisha wananchi kuhusu namna zoezi zima na ushirikishwaji wa wananchi utakavyofanyika.”

Akiogelea hatua zinazoendelea sasa hivi ndugu kimario anaeleza kuwa shughuli zinazoendelea katika maeneo tofauti tofauti kwa sasa ni pamoja na usafishaji njia au mistari, kuchimba mashimo ya kina kifupi mita 7, 10 au 15 kutegemea na jiolojia ya eneo kwa ajili ya kuweka baruti (vyanzo vya mitetemo ) pamoja na kuweka mitambo maalum ya kuchukulia taarifa za mitetemo(seismic data).
Mtambo wa kuchoronga mashimo ya kuwekea baruti ukiwa kazini. Mtambo huu huchimba mashimo yenye urefu tofauti kati ya mita 7 hadi 15, kwaajili ya kufukia baruti ambazo zinapolipuliwa ndipo taarifa za miamba chini hupatikana baadae kuchakatwa na kutafsiriwa kitaalam ilikujua sehemu ya kuchimba kisima cha utafiti.

Aidha anaeleza kuwa, “Yapo maeneo mengine ambayo yamefikia kwenye hatua ya kubainisha maeneo maalum yatakayowekewa baruti pamoja na vifaa vya kunakili au kunasa taarifa za mitetemo, yapo maeneo ambayo tayari zoezi hili limeshafanyika na tayari hatua ya kulipua baruti na kunakili taarifa za mitetemo limekwishaanza kufanyika”.

Simon amethibitisha kuwa hadi sasa takribani mashimo yaliyopo kwenye misatri yenye urefu wa km 311 yameishasimikwa au kujazwa na baruti na mistari ya kijiofizikia yenye urefu wa Kilomita 116.9 kati ya 1287 imeshachukuliwa taarifa za kijiofizikia na kuendelea kufanyiwa uchambuzi wa awali.
Mmoja wa wataalam wa milipuko akipima urefu wa shimo kama limekidhi mahitaji ya kitaalam kabla ya kusimika/kujaza baruti ndani ya shimo.

Aidha akiongolea suala la vibali na fidia kwa wananchi ambao mazao yao yameathirika na yatakayoathirika na zoezi la uchukuaji wa taarifa za mitetemo, Mohamed Ally ambaye ni Msimamzi wa Vibali kutoka kampuni ya Envision Consulting Ltd ameeleza kuwa kumekuwa na ushirikiano mkubwa sana kutoka TPDC haswa panapohitajika vibali kutoka katika mamlaka mbalimbali za serikali na hivyo kumefanya kazi yao kuwa rahisi na yenye mafanikio.

Akiongolea suala la fidia, Mohamed anabainisha kuwa “pamoja na kuwa na mtathamini wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kushirikiana na viongozi kutoka ofisi za Kata, Wilaya, Mikoa pamoja Mthamini Mkuu wa wa Serikali na hivyo kufanya zoezi zima la uthamini na ulipaji fidia kufanyika kwa mafanikio makubwa na kupunguza migogoro na wananchi”.
Moja ya baruti zinazofukiwa chini ikiwa kwenye maandalizi ya kufukiwa kwenye shimo maalum kwa ajili ya kulipuliwa.

Pamoja na utafiti unaofanyika katika kitalu cha Ruvu, TPDC linaendelea na maandalizi ya utafiti katika maeneo mbalimbali nchini kama vile vitalu vya; Eyasi-Wemberi, Songo Songo Magharibi, Mnazi Bay kaskazini pamona na Vitalu vya 41B/41C.
Moja ya kitafaa maalumu (AVO) ya kunakili taarifa za mitetemo za kijiofizikia kikiwa kimesimikwa ardhini tayari kusubiri mitego ya baruti kulipuliwa ili kupata taarifa za mitetemo. Mtambo huu hutumika ili kupata taarifa za mitetemo zenye taswira ya pande mbili “2D”.

TASWIRA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza Mkutano wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mbunge wa kuleuliwa, Salma Kikwete, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo, akizungumza na Waziri wa Madini, Angela Kairuki, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 9, 2018.

RAIS DK.SHEIN APOKEA UJUMBE KAMPUNI YA KUSHAN ASIA AROMACOOPERATION YA NCHINI CHINA

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya “KUSHAN ASIA AROMA COOPERATION LIMITED” kutoka China Bw.Zhou Junxue akiwa na Ujumbe wa Viongozi aliofuatana nao leo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya “KUSHAN ASIA AROMA COOPERATION LIMITED” kutoka China Bw.Zhou Junxue (katikati) walipokuwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni hiyo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kampuni ya “KUSHAN ASIA AROMA COOPERATION LIMITED” kutoka China Bw.Zhou Junxue (kushoto) walipokuwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni hiyo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo (katikati) Bw.Guang William-Meneja Mauzo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Kampuni ya “KUSHAN ASIA AROMA COOPERATION LIMITED” kutoka China Bw.Zhou Junxue (kushoto) walipokuwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Kampuni hiyo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo (katikati) Bw.Guang William-Meneja Mauzo,Picha na Ikulu

MKOPO WA DOLA MILIONI 65 WA KAGERA SUGAR WAWEKEZWA NCHINI

0
0

Na Benny Mwaipaja

Serikali imeeleza kuwa kiasi chote cha dola za Marekani milioni 65 zilizokopwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera kutoka Benki ya CRDB kwa udhamini wa Serikali mwaka 2004 kimewekezwa nchini na hakijapelekwa kuwekeza katika nchi ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda hicho kukopa kiasi hicho cha fedha ambacho kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa uwekezaji uliofanywa katika Kiwanda cha Kagera ni wa takribani dola za Marekani milioni 250 hivyo haiwezekani mwekezaji kukopa dola milioni 65 na kuzipeleka Congo ili hali kiwango cha uwekezaji nchini ni kikubwa.

“Mwekezaji wa Kiwanda hicho ni wa ndani na amejitahidi kuajiri watanzania wengi hivyo Serikali ipo katika mchakato wa kukiwezesha kiwe cha mfano ili kiendelee kuleta matokeo chanya kwa watanzania”, alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali la msingi la Mbunge huyo, alitaka kujua kiwango cha hisa ambacho Serikali inamiliki katika kiwanda cha Sukari cha Kagera na kiasi cha fedha kilichokopwa na kulipwa na mwekezaji huyo kupitia udhamini huo wa Serikali.

Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali kwa sasa haimiliki hisa zozote katika kiwanda hicho na kuongeza kuwa hisa zake katika kiwanda hicho ziliuzwa mwaka 2001 baada ya kukibinafsisha kiwanda hicho kwa Kampuni ya Kagera Saw Mills Limit.Aidha Dkt. Kijaji alifafanua kuwa mwekezaji wa Kiwanda hicho alikopa kiasi cha dola za Maerekani milioni 65 kwa kutumia udhamini wa Serikali mwaka 2004, ikiwa ni udhamini (guarantee) wa kipindi cha miaka 12.

Alisema kuwa mpaka sasa kiwanda hicho mimerejesha zaidi ya dola za Marekani milioni 56.88, sawa na asilimia 87.5 ya mkopo wote, na kwamba marejesho ya mkopo uliobaki wa Dola milioni 8.12 yatafikia ukomo wake mwezi Julai, 2019.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akijibu swali la Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Bungeni Mjini Dodoma, aliyetaka kujua sababu za Serikali kumdhamini mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Kagera, kukopa kiasi cha dola milioni 65 za Marekani ambacho amedai kimepelekwa kuwekezwa nchini Kongo wakati Tanzania ina uhaba wa sukari.

SAINT GABAIN YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA UJENZI NCHINI

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAKANDARASI, Wasambazaji na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi nchini wamepatiwa mafunzo yanayohusu ujenzi kwa lengo la kuifahamu vema sekta hiyo yenye ushindani mkubwa.

Mafunzo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na 
Kampuni ya Imports International Tanzania Ltd ambayo ni waagizaji na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi ambapo pia warsha imehusu mafunzo kuhusu  matumizi ya vifaa vya drywall gypsum partition and pro-plaster wall finish.

Lengo la mafunzo hayo ni kwa ajili ya kumalizia ukuta kutoka Saint Gobain ambao ndiyo watengenezaji wa vifaa hivyo.Akizungumza kuhusu warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa  Imports International Tanzania Ltd Trushal Jethwa amesema lengo la mafunzo lilikuwa ni kuwaleta pamoja  makandarasi, wasambazaji na wafanyabiashara.

"Lengo ni kuwajulisha  kuhusu maendeleo ya hivi karibuni katika sekta ya ujenzi ambayo ina ushindani mkubwa sana. "Katika ulimwengu ambao teknolojia inabadilika haraka sana katika sekta ya ujenzi daima ni muhimu kuwapa wadau baadhi ya maendeleo ya hivi karibuni ili kukua pamoja kama timu, haisaidii sisi kuendelea kuwa na ujuzi Hui bila wajulisha wadau wetu," amesema Jethwa.

Amefafanua mafunzo hayo yanayotolewa na kampuni yao ya Saint Gobain ambao ni wazalishaji wa gyproc ambao wanaamini kuwa aina hiyo ya mafunzo inasisitiza ahadi yao ya kujenga uhusiano mzuri na jamii iliyowazunguka kwa ujumla. 

"Hapa leo Saint-Gobain wanatueleza jinsi vifaa vyao vinavyochangia maisha ya kila siku, kwa kupitia bidhaa zake, wanaonesha utaalamu wa vifaa, utamaduni wa ubunifu, ufahamu wa mahitaji ya wateja na mbinu kwa njia ya uwazi na wajibu," amesema Trushal Jethwa. 

Ameongeza "Bidhaa za leo zinaonyesha thamani tunayowaletea wateja. Ninataka kila mtu ajue mambo muhimu ambayo Saint-Gobain inasimamia pamoja na nafasi za bidhaa zetu katika maisha ya kila siku.

" Saint Gobain kutokea Ufaransa inapatikana  katika nchi zaidi ya 67 duniani kote, mafunzo hayo pia yanatarajiwa kufanyika katika chuo cha Veta na Kariakoo kama sehemu ya uwajibikaji wao wa kijamii," amesisitiza.
Mtaalam wa Ujenzi , Member Mashabela akitoa maelezo ya vifaa vya ujenzi kwa wahandisi na wakandarasi waliofika katika ofisi Saint Gobain kuhusiana na ujenzi wa kisasa kwa vifaa vya kisasa leo jijini Dar es Salaam.
Mtaalam wa ufundi wa Saint Gobain Development East Africa, Stanley Katabarwa (Mwenye miwani
Baadhi ya vifaa vya ujenzi

Fursa za Usafirishaji Tanzania Zinaweza Kuendesha Nchi

0
0
Imeelezwa kuwa Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kwa fursa kubwa za maendeleo ya kiuchumi na biashara kuliko nchi nyingine zote za Afrika Mashariki, na kutolea tuu mfano wa sekta moja ya usafiri na usafirishaji, Tanzania imeelezwa kuwa ni nchi yenye bahati sana, kuzungukwa na nchi 8 ambazo hazina bahari, hivyo fursa tuu za usafirishaji kwa kutumia bandari, reli, maziwa na anga, zikitumiwa vizuri, zinaweza kuipaisha Tanzania kiuchumi na kujiendesha, bila kutegemea sekta nyingine zozote.

Bahati hiyo imeelezwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.

John Ulanga, amesema Tanzania imepakana na nchi nyingi ambazo hazina bahari kuliko nchi nyingine yoyote ya Afrika Mashariki, hivyo Tanzania ikichangamkia kutumia fursa hii kibiashara, itakuza uchumia sio tuu wa Tanzania pekee, bali hata wan chi za jirani zetu, na kule kote njia hizi zinakupita, maeneo hayo yana fursa za kustawi kiuchumi.

Ulanga amesema, Tanzania imekana na nchi nane ambazo hazina bahari, nchi hizo ni Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidekrasia ya Kongo, Zambia, Malawi na Msumbiji, na kusema kama tutazizatiti na kusafirisha mizigo yote ya nchi hizi, pato la usafirishaji pekee litakuwa kubwa kuweza kuendesha nchi, hata bila kutegemea sekta nyingine.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane, ameishukuru TradeMark kwa ufadhili huo na kueleza fedha hizo zitasaidia sana katika kutimiza majukumu ya CCTTFA ikiwemo uhamasishaji wa matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuelezea faida za Bandari ya Dar es Salaam ukilinganisha na bandari nyingine.

Naibu Mkurugenzi  wa Trademark East Africa, Bi. Monica Hangi amesema, kwa vile lengo la Trademark ni kusaidia kurahisisha biashara, hivyo ufadhili huo utasaidia sana kurahisisha biashara ya usafirishaji watu na mizigo kwa nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.

Mkurugenzi wa Miundombini wa TradeMark East Africa, tawi la Tanzania, Smark Kaombwe, amesema biashara ni ushindani, hivyo ili bandari ya Dar es Salaam iweze kuvutia zaidi nchi majirani waitumie, lazima iboreshe utendaji wake mizigo ichukue muda mfupi kutoka, na pia iwe na gharama nafuu kuliko bandari majirani zetu.

Meneja Mradi wa Uangalizi wa Usafirishaji wa Central Corridor, Eng. Melchior Balentandikye, amesema kabla ya msaada huo, Central Corridor imekuwa ikijihusisha na usafiri wa barabara pekee, lakini sasa msaada huo, utawasaidia kushughulikia usafiri wa barabara, reli na usafiri wa majini na usafiri wa anga.

Meneja wa Fedha na Utawala wa Central Corridor, Costaph Natay, amesema msaada huo utasaidia sana kuboresha ufanisi, hivyo Central Corridor itaboresha ufanisi wa shughuli zake, hivyo kuongeza ufanisi katika usafirisha abiria na mizigo katika ukanda wa kati.

Meneja Mawasiliano wa Central Corridor, Flory Okadju, amesema msaada huo utaisaidia Central Corridor kuboresha mawasiliano na utoaji wa elimu kwa umma katika nchi zote tano za Ukanda wa kati, hivyo kutoa uelewa mkubwa zaidi kuhusu ubora na unafuu wa bandari ya Dar es Salaam, hivyo kuvutia zaidi wafanyabiashara wan chi hizi, kupitishia mizigo yao bandari ya Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, akionyesha njia za Ukanda wa Kati, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, kushoto, na a Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane wakitia saini mkataba, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, kushoto, na a Katibu Mtendaji wa Central Corridor, Capt. Diodonne Dukundane wakibadilishana mkataba, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ufadhili wa Dola za Marekani Milioni 1.3, ambazo ni karibu na Shilingi Bilini 3 za Kitanzania, kwa Taasisi ya Central Corridor Transport Facilitation Agency, inayoshughulikia mizigo inayopitia Bandari ya Dar es Salaam, kuelekea nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, kwa kutumia njia ya Ukanda wa Kati.

TANZIA: CHAMA CHA MAPINDUZI CHAOMBOLEZA KIFO CHA MZEE MTOPA

0
0
Marehemu Mzee Ally Mtopa




JENGO MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO KIVUTIO CHA KIHISTORIA UTOAJI HUDUMA ZA UTALII JIJINI ARUSHA

0
0



Na Hamza Temba - WMU

........................................................
JENGO la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro jijini Arusha ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu litakuwa kivutio cha kihistoria cha utoaji wa huduma za utalii hapa nchini.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla muda mfupi baada ya kukagua jengo hilo ambalo linasemekana kuwa refu kuliko majengo yote jijini Arusha likiwa na jumla ya ghorofa 18.

Alisema jengo hilo ambalo linatizamana na Round About ya AICC katikati ya jiji hilo, limekusudiwa kuwa Kituo Kimoja (One Stop Centre) cha shughuli zote za utoaji wa huduma za utalii jijini humo kuanzia uwekezaji, utangazaji na menejimenti kwa ujumla.

Alisema jengo hilo litatoa fursa kwa wadau mbalimbali wanaotoa huduma za utalii kuweka ofisi zao ikiwemo mabenki, watoa huduma za usafiri, mashirika ya ndege, mawakala wa safari za utalii na huduma, maduka ya bidhaa za utalii na mahoteli.

"Tutapamba pia jengo hili na" live screen" (Mabango ya Video Mubashara) za vivutio, hivyo wanyama wakiwa wanapita huko porini watakuwa wanaonekana "LIVE" (Mubashara) kwenye jengo hili kupitia LED Screen ambazo zitakuwa zimezunguka jengo hili" alisema Dk. Kigwangalla.Alisema huduma nyingine zitakazotolewa katika Jengo hilo ni pamoja na zile za kuangalia jiji la Arusha kupitia darubini, huduma za burudani ikiwemo kumbi za starehe na migahawa.

Kwa upande wake Mkandarasi wa jengo hilo, Mhandisi Bismas Meela wa Kampuni ya Inter-Consult limited alisema ujenzi wa jengo hilo ambalo ulianza mwezi Novemba, 2013 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi juni mwaka huu.Alisema jengo hilo ambalo lina uwezo wa kupaki magari 67 kwa wakati mmoja katika ghorofa za chini linagharimu shilingi za Kitanzania bilioni 45.

Katika ziara hiyo ya siku moja ya ukaguzi wa jengo hilo, Dk. Kigwangalla aliongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Fredy Manongi na Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka hiyo, Asangye Bangu. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asangye Bangu kuhusu jengo la kitega uchumi la mamlaka hiyo lililopo katikati ya Jiji la Arusha ambalo limekusudiwa kuwa Kituo Kimoja cha shughuli zote za utoaji wa huduma za utalii jijini humo kuanzia uwekezaji, utangazaji na menejimenti kwa ujumla. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia mandhari ya Jiji la Arusha akiwa juu ya Jengo la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Kutoka kulia ni Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka hiyo, Asangye Bangu na  Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akishuka kwenye ngazi maalum zinazotumia nishati ya umeme ndani ya Jengo hilo. Kulia ni Naibu Mhifadhi wa Huduma za Uendeshaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Asangye Bangu na nyuma yake ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dk. Fredy Manongi. 
Muonekano wa jengo hilo kutokea barabara ya Makongoro Jijini Arusha.


TPA YAADHIMISHA MIAKA 13 TANGU KUAZISHWA KWAKE,WAELEZEA MAFANIO YAO

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imeadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa huku ikijivunia mafanikio ya kuongezeka kwa biashara kuanzia mwaka 2011.

Pia mapato yamekuwa yakiendelea kupanda na kuanzia Julai mwaka 2017 hadi mwaka 2018 shehena iliyokuwa ikiingia ilianza kupanda na meli zinazoingia kufikia takriban 3000 kwa mwezi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TPA wakati akielezea Wiki ya Mamlaka hiyo iliyoanza jana na kilele chake kufikiwa Jumapili.Ambapo watatumia maadhimiaho hayo kueleza walikotoka tangu April 2005, walipo na wanakotarajia kwenda kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma kwa biashara. 

Amesema TPA imekuwa ikiendelea kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza masoko huku wakikusanya Sh.bilioni 420 kwa kipindi cha miezi sita iliyopita."Mamlaka hiyo, inalenga kuboresha zaidi huduma zake, kwa kuandaa mazingira ya serikali kupata mapato yake kwa kuwa kati ya asilimia 45 hadi kufikia 55 ya kodi inayokusanywa na Mamlaka ya Mapato, hupatikana TPA," amesema.

Kakoko amesema wanatarajia kutekeleza mradi ya ujenzi wa bandari kavu katika baadhi ya mikoa ikiwemo Kigoma, Arusha, Mbeya na hata Mwanza wanalenga kuwapa unafuu wateja wao kutoka nje ya nchi wanaokuwa wakifuatilia bidhaa katika Mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Profesa Ignas Rubaratuka akizungumza kuhusiana na maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka usimamizi wa bandari yaliyoanza leo , jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mhandisi Deosdidit Kakoko akizungumza na waandishi kuhusiana na mafanikio ya kuanzishwa kwa mamlaka ya usimamizi wa bandari, leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Fransisca Muindi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma watazozitoa katika maadhimisho ya miaka 13 ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari, leo jijini Dar es Salaam.

MAMIA YA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA NA WAUME ZAO WAFURIKA KWA MAKONDA

0
0
*Majina ya wanaume waliotelekeza watoto kuanikwa hadharani

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

MKUU wa mkoa wa Dar es salam Paul Makonda leo April 9 amezungumza na akina mama waliotelekezwa na waume zao jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya wanawake hao wamejitokeza wakiwa na watoto zao.

Ambapo ameeleza  maumivu na masimango ya peke yao yamekoma sasa ni mguu kwa mguu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Makonda amesema kuwa mchakato huo utafanyika kwa siku tano na wasaidizi wake wa huduma za sheria watahudumia kwa haki.

Ameeleza hawapo kwa  ajili ya kumkomoa mtu ila ni kulinda haki za Mama na mtoto na kama baba wa watoto hao hawatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.Amesema Makonda  ameeleza wakiona sheria haitoshi watapambana hadi Bungeni kubadili sheria ili kila mwanamke wa kitanzania apewe haki zake pamoja na mtoto  na kuwe na usawa.

Amewataka akina  Mama waliozalishwa na wanaume wa kada zote kama walimu, wanasiasa, walio katika mabenki na kokote Tanzania watatafutwa popote ili kulinda haki za watoto na mama zao.Makonda ameeleza  Serikali Rais Magufuli imewapa kazi ya kuwasikiliza wananchi na hivyo hawapaswi kukaa na madukuduku yao, hivyo walete malalamiko yao kwani watoto wanategemewa kwa mustakabali wa taifa la kesho.

Akizungumza na Michuzi blog Lucy Peter wa Tegeta ameeleza kuwa alitelekezwa mara baada ya kupata ujauzito hadi sasa mtoto wake wa kiume ana miaka 5, na amefika kupata msaada kutoka kwa mkuu wa mkoa ili baba wa mtoto huyo aweze kutoa huduma mtoto huyo kwani hadi sasa mama huyo anaishi kwa wazazi wake.Aidha Nasra Mohammed ameeleza amefurahi kwa hatua ya Mkuu wa Mkoa ya kuwasaidia wamama waliotelekezwa, hivyo anaamini kuwa mtoto wake atapata huduma stahiki kutoka kwa baba yake aliyemwachia mtoto akiwa na mwezi mmoja.

Hata hivyo wamama hao wamefurahi na kumshukuru mkuu wa mkoa kwa kuamua kuwasaidia wao na watoto wao hivyo Mungu ambariki sana.Aidha mkuu wa mkoa ameeleza kuwa watahudumia watu 500 kwa siku na maeneo yote nchini hata kama si mkazi wa Dar es salaam kwani ni haki yao na hakuna kuogopau vitisho vya aina yoyote bali waangalie kupata zao za msingi.
Akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam waliojitokeza kupata huduma za kisheria wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kupata msaada wa kisheria.
  01.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Paul Makonda  akizungumza na  waliotelekezwa na waume zao juu   kulinda haki za Mama na Mtoto ambapo kama Baba wa watoto   hatajitokeza hadharani basi majina yao yatatajwa hadharani.(Pacha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)
 .Mkuu wa Mkoa akizungumza na maofisa mbalimbali wanaotoa huduma na kusisitiza wawasikilize  wakina mama wote hata wale wasio wakazi wa Dar es salaam. .(Pch na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
 Akina Mama wa MKoa wa Dar es salaam waliojitokeza kupata huduma za kisheria wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wakati wa kupata msaada wa kisheria.

Calling ALL professionals interested in maternal and child health: MASTERS DEGREE INFORMATION

0
0
Save the Mothers program offers a MASTERS DEGREE IN PUBLIC HEALTH LEADERSHIP at the Uganda Christian University (UCU) Mukono Campus.

The program is seeking working professionals in the fields of law, education, politics, social sciences, clergy, media, health care, and others. This self-sponsored program has two intakes: Ugandan students in October & non-Ugandans (international students) in September.

Intake for Ugandan students will start in October 2018 with three modules (each three weeks), three times a year for two years.

Intake for international students will start in September 2018 with four modules. Each module is 4 weeks, and two modules are completed each year. This allows students to study and continue working in their respective professions.

Applications are now being accepted until April 15, 2018. To apply, download and fill out a postgraduate application form at www.ucu.ac.ug/applynow. Also send your CV and a motivational essay to savethemothers@ucu.ac.ug     AND mimmutabazi@gmail.com

For more information contact:
Gladness S. Hemedi: +255 754 285 701
Rev. Meshack Kulwa Ezekiel +255 755 787 127
Liberatha Shija: +255784638010, +255715638010,
Jamila Hamudu: +2550713236165,
Saida Salim Mukhi: +255713253926/+255787253926)  
Or call Julie  +256-772 419 362
or Dr. Miriam + (256) 772 500649,
Topi +256-772311498

Uganda Christian University, a complete education for a complete person




tears flow as Ian Ferrao concludes term as Vodacom Tanzania Managing Director

0
0
Ian Ferrao speaks for last time with members of staff as he concludes his term as Vodacom Tanzania Managing Director at the company's headquarters in Dar es salaam
Members of staff listed to Ian Ferrao  as  the out-going  Vodacom Tanzania Managing Director bids them farewell  at the company's headquarters in Dar es salaam
Ian Ferrao throws in words of wisdom to members of staff as he concludes his term as Vodacom Tanzania Managing Director at the company's headquarters in Dar es salaam

Mbunge wa Mwankwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Khamis Aipongeza Muhimbili Kuponya Mwanae

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe, Zanzibar, Mhe. Ali Salim Khamis leo ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na watalaam wake wote kwa jinsi walivyompokea mtoto wake na kumpa huduma stahiki na kwa weledi wa hali ya juu. 
 “Leo natoa shukrani zangu za dhati kwa MNH na kukabidhi barua ya shurakni na cheti cha utambuzi wa huduma nzuri aliyopewa mwanangu Muniri Ali Salim tangu alivyopokelewa kupitia Idara ya Magonjwa ya Dharura na kisha kupelekwa Idara ya Upasuaji Kitengo cha Upasuaji wa watoto. Mtoto wetu alikuwa na uvimbe kichwani ambao ulisababisha afanyiwe upasuaji na kutolewa vizuri, sasa mtoto wetu anaendelea vizuri sana,” amesema Mh. Khamis. 
 Amepongeza kazi nzuri inayofanywa na MNH chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mtendaji, Prof. Lawrence Museru kwa kushirikiana na wauguzi, madaktari na watalaam wengine ambao wamekuwa wakijitoa kutoa huduma nzuri kwa mtoto wake pamoja na wahitaji wengine wanaofika MNH kupata huduma.
 “Nimeamua kutoa barua ya shukrani kwenu, cheti cha utambuzi kwa MNH, Idara ya Upasuaji kupitia Kitengo cha Upasuaji Watoto, Idara ya Magonjwa ya Dharura na kipekee kwa Dkt. Juma Mfinanga ambaye ni daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura pamoja na Dkt. Zaitun Bhokare ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji watoto kwa kazi nzuri ambayo imefanikisha matibabu kwa mtoto wetu,” amesema Mh. Khamis. 
 Akipokea cheti na barua kwa niaba ya MNH, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Makwaia Makani amemshukuru Mh. Khamis kwa utambuzi na kutoa mrejesho chanya kutokana na huduma ya matibabu aliyopatiwa mtoto wake. 
 “Sisi kama watoa huduma tunapokea maoni aina zote, lakni maoni ya kupongeza ni machache ukilinganisha na maoni mengine. Hivyo hii imetupa hamasa kubwa sana na watalaam wetu wamefurahi,” amesema Bw. Makani. 
 Daktari Bingwa wa Upasuaji Dkt. Zaituni Bokhari amesema walimpokea mtoto Munira Ali Salim mwezi mmoja uliopita na baada ya kumfanyia uchunguzi waligundua alikuwa na uvimbe kichwani (kichogoni) na hivyo kumpatia huduma ya upasuaji. 
 Dkt. amesema kuwa baada ya kujiridhisha kwamba ana uvimbe huo kwenye ubongo waliamua kumfanyia upasuaji na kutoa uvimbe huo. Dkt. Bhokari anasema mara baada ya upasuaji mtoto aliendelea vizuri na hatimaye kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Makwaia Makani akipokea cheti cha utambuzi wa huduma zinazotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe- Zanzibar, Mhe. Ali Salim Khamis ambaye mtoto wake alipatiwa huduma ya matibabu katika hospitali hiyo.
Daktari Bingwa wa Upasuaji Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Zaitun Bokhary akipokea cheti cha utambuzi wa huduma kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe- Zanzibar, Mhe. Ali Salim Khamis.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dkt. Kefa akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba ya Dkt. Juma Mfinanga ambaye ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo.
 Wa Pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Makwaia Makani akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge Ali Salim Khamis wa Jimbo la Mwanakwerekwe na madaktari wa hospitali hiyo.
 Cheti cha utambuzi wa huduma kilichotolewa kwa hospitali hiyo.
Cheti cha utambuzi alichokabidhiwa Dkt. Zaitun Bokhary.
Cheti cha utambuzi alichokabidhiwa Dkt. Juma Mfinanga.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

TRADEMARK EAST AFRICA AND CENTRAL CORRIDOR TRANSIT TRANSPORT FACILITATION AGENCY SIGN FINANCING AGREEMENT

0
0
TradeMark East Africa (TMEA) Tanzania Country Director, John Ulanga (L) hands over a Memorandum of Association (MoU) to the Executive Secretary of Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) Captain Dieudonne Dukundane (R) during the ceremony of signing a financing agreement to provide a total of USD 1.3m (Equivalent to approximately TZS 2.86 billion) over a 3-year period (2018 to 2021) held in Dar es Salaam last week. (Photos by Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG).
 TradeMark East Africa (TMEA)  Tanzania Country Director, John Ulanga explain to journalist how the TradeMark East Africa (TMEA) and the Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency whey are working. TradeMark East Africa (TMEA) is an aid-for-trade organization that was established with the aim of growing prosperity in East Africa through increased trade. TMEA operates on a not-for-profit basis and is funded by the development agencies of the following countries: Belgium, Canada, Denmark, Finland, the Netherlands, Norway, UK, and USA. TMEA works closely with East African Community (EAC) institutions, national governments, the private sector and civil society organizations.
Executive Secretary of Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) Captain Dieudonne Dukundane (C) explaining a few things to the journalist about their publications that help traders in offering them various education.
TradeMark East Africa (TMEA) and the Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA) have signed a financing agreement geared towards strengthening and enhancing the Central Corridor Transport Observatory (CCTO). The financing will specifically improve monitoring of the Central Corridor performance in-order to support evidence-based advocacy and decision making to remove trade barriers. To that effect, TMEA will provide a total of USD 1.3m (Equivalent to approximately TZS 2.86 billion) over a 3-year period (2018 to 2021). 

 “TradeMark East Africa is delighted to provide this support to CCTTFA because the organization is producing reliable and timely data on the performance of the Central Corridor Transport Network. This support therefore will further strengthen that work and enable the countries served by the corri dor to design interventions to further improve performance of the corridor” said John Ulanga, the Tanzania Country Director.

 “CCTTFA highly appreciates this funding support from TMEA for our Central Corridor Observatory work, the funding will go a long way to support our ongoing efforts and enable us to work with various stakeholders in central corridor partner states to further improve efficiency of the corridor and hence increase the volume of trade going through the corridor for the benefit of the countries”. said Captain Dieudonne Dukundane, Executive Secretary of CCTTFA.

 To accomplish the above, the CCTTFA will enhance the CCTO into a one stop center platform for availing and accessing relevant information and data related to movement of goods along the Corridor. Specifically, this support will enable CCTTFA maintain and improve the current online information portals, develop mobile data collection tools, roll out the central corridor dashboard to other member states, develop trade costs and transport predictive models and develop tools to monitor processes and effectiveness of initiatives along the Central Corridor.

MBUNGE CHUMI AITAKA SERIKALI KUSAMBAZA MBOLEA KWA WAKATI

0
0
Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ameitaka Serikali kuhakikisha inasambaza mbolea kwa bei nafuu na kwa wakati.

Chumi amesema hayo wakati akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu Bungeni.'Mhe Mwenyekiti, serikali imekiri kuwa usambazaji wa mbolea ulikuwa 64% mana yake ni kuwa 36% ya wakulima hawakupata mbolea'

'Sio hivyo tu, hata hiyo 64% hawakupata mbolea kwa wakati, sio haki kabisa, mkulima wa Itimbo, Kitelewasi, Isalavanu apelekewe mbolea ya kupandia mwezi February wakati uandalizi wa mashamba unaanza mapema Oktoba.'

Kuzuia kuuza ziada ya mazao ni kuwaonea wakulima Akizungumzia wakulima kuuza mazao yao,nje ya nchi, Chumi alisema kuna ziada ya tani 2.6milioni ya chakula, lakini Hifadhi ya Taifa ya Chakula imenunua tani 26,000(elfu ishirini na sita tu), afu mkulima anazuiwa kuuza mahindi yake, jambo ambalo sio sawa.

Tunawafanya wakulima wa nchi hii kama raia daraja la pili (second citizens),mbolea tuwacheleweshee, ziada ya mazao yao tuwafungie kuuza, hii sio sawa' alisisitiza Mbunge huyo na kuongeza kuwa ni vizuri serikali ikaangalia changamoto ilizokutana nazo katika usambazaji wa mbolea mwaka huu na kuboresha mazingira ili kumsaidia mkulima kupata mbolea kwa bei nafuu, kwa wakati na pia kuuza ziada ya mazao.

HERI YA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA BLOGGER CATHBERT KAJUNA

0
0
Leo Aprili 10 ni siku ya kuzaliwa kwa Journalist/Photojournalist na Blogger Cathbert Angelo Kajuna mmiliki wa Kajunason Blog (www.kajunason.com) na Mwandishi/Mpigapicha wa MMG. 
 
"Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunifikisha siku ya leo ya kuzaliwa kwangu, hakika yeye ni mwema maana amenivusha katika milima na mabonde na amekuwa akinifanyia mambo makubwa katika maisha yangu.
 
 Pili nipende kutoa shukrani kwa familia yangu, ndugu jamaa na marafiki wote ambao mmekuwa bega kwa bega pale ambapo nimekuwa nikikwama mmekuwa mkinishika mkono na kunivusha hakika sina cha kuwalipa bali mwenyezi Mungu awaongezee busara, upendo na amani. 
 
Tatu, kabisa nipende kutoa shukrani za pekee kwa Mke wangu, Mama yangu Mzazi, baadhi ya ndugu na marafiki ambao bila wao labda nisigekuwa hapa leo, nianze na Familia ya Kajuna Jr (Kennedy), Familia ya Michuzi Media Group ikiongozwa na Ankali Michuzi, Michuzi Jr na Othman hakika najivunia ukarimu na upendo wetu kwangu najivunia kuwa mmoja ya mwanafamilia, 
 
Familia ya Jackson Mmbando, rafiki zangu Seki David, Edwin David, Portnes, Mwesiga Kyaruzi, Shebby Mpondela, Franklin Alexander, Ally Jamal, Imani Ntila, James Jonathan na Dr. Heri Tungaraza. Wengine ni Raymond Maganga, Myoma Kapya - Chilala, Mike Mukunza, Muhidin Sufian, Bakari Kimwanga, John Bukuku, Abraham Mossi, Sylvia Mwehozi, Leah Mushi, Mary Masinda, Tiba Josephat Lukaza, Ruben (Baba Countinho) na wale wote ambao nimekuwa nikishirikiana nao kwa namna moja au nyingine katika kusaka ugali wetu wa kila siku. 
 
Mwisho, Shukrani za pekee ziwaendee wanachana wote Tanzania Bloggers Network (TBN) popote mlipo nawaomba tuendelee kushirikiana kwa pamoja, Umoja ni Nguvu.

Ni mimi Cathbert A. Kajuna.

10.04.2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards

0
0

Na Anitha Jonas – WHUSM
Utendaji uliyotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo.

“Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika,Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika,”alisema Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika sherehe hiyo ya kukabidhi bendera Mheshimiwa Mwakyembe aliwasisitiza wasanii wanchini kuendelea kuandaa kazi zinazoonyesha ubunifu wao kwani ukuaji wa tansia ya filamu Tanzania uko mikononi mwao na si vinginevyo.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa jana jijini Dar es Salaam anayetarajia kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akimkabidhi Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa tiketi ya ndege jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari yake ya kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,kutoka kulia wapili ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Bw.Godfrey Mngereza.


Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(wakwanza kushoto) akifafanua kwa waandishi wa habari na wadau wa sanaa (hawapo pichani) kuhusu tuzo za The Africa Prestigious Awards jana jijini Dar es Salaam zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni kwa kueleza heshima ya tuzo hizo na Tanzania imepata heshima ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli nae kuteuliwa kuwania tuzo ya kiongozi bora Afrika,wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.


Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa akiahidi kwa Waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kukabidhiwa bendera kuwa atarudi na tuzo hata kama yeye hatopata basi ataweza na kurudi na hata tuzo ya Msanii Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika au Tuzo ya Msanii King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika au Mpiga picha Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga picha Bora Afrika katika tuzo za The African Prestigious Awards zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni,wa kwanza kulia ni Mama Mzazi wa Msanii Monalisa Bibi Suzan Lewis maarufu kama Natasha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI KALEMANI AFUNGUA UMEME WA GRIDI NGARA

0
0
Na Veronica Simba - Ngara
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amefungua matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu hivyo kuwezesha Wilaya hiyo kuachana na matumizi ya umeme wa mafuta.
Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi huo, Waziri Kalemani alisema kuwa yeye pamoja na watendaji wote wa Wizara na Taasisi zake hususan TANESCO na REA, wamedhamiria kutekeleza kwa vitendo, azma ya Rais John Magufuli ya kuhakikisha kunakuwepo na umeme wa uhakika nchini kote ili kuchochea uchumi wa viwanda.
“Serikali imekusudia kujenga uchumi wa viwanda na kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati. Hayo yote yanahitaji nishati ya uhakika, na ndicho tunachotekeleza.”
Alisema kuwa, mpango wa serikali ni kuiunganisha nchi nzima katika umeme wa Gridi ya Taifa ili wananchi wote wanufaike kwa kupata umeme wa aina moja.
Akifafanua Zaidi, Waziri kalemani alisema kuwa uunganishaji umeme wa Gridi ya Taifa umeshafanyika kutoka Mbagala Dar es Salaam kupitia Mkuranga, Kibiti, Ikwiriri, Utete, SomangaFungu hadi Lindi.
“Kwa sasa tunaendelea kuunganisha Lindi mpaka Mtwara ambapo kufikia mwisho wa mwezi huu, watanzania watakuwa wanatumia umeme wa Gridi ya Taifa kutoka pembe ya Kusini mwa nchi Mtwara hadi pembe nyingine ya nchi iliyopo Magharibi ambayo ni Ngara Kagera,” alisema.
Aidha, aliongeza kuwa, kazi iliyobaki ni kuunganisha upande mwingine wa nchi ambao unaanzia Mbeya kupitia Sumbawanga, Kigoma, Mpanda, Nyakanazi hadi Geita na Bulyanhulu. Alisema kazi hiyo inatarajiwa kukamilika ifikapo 2020/21.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha Mtambo maalum unaoruhusu kuwaka kwa umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, baada ya kuzima ule uliokuwa ukiwasha umeme wa mafuta ya dizeli, Aprili 8 mwaka huu.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (waliokaa-katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, TANESCO na REA baada ya hafla ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka (wa pili-kushoto) akimweleza jambo Mbunge wa Ngara, Alex Gashaza (kulia), wakati wakimsubiri Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kuwasili kwa ajili ya ufunguzi wa matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Aprili 8 mwaka huu. Wengine pichani ni viongozi mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO na REA.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

CHANETA YAANZISHA PROGRAMU YA KUHAMASISHA MCHEZO WA NETBALI NCHI NZIMA

0
0
Na. Jumbe Ismailly 
CHAMA cha Netbal Tanzania (CHANETA)  kimeanzisha Program maalumu ya kuhamasisha mchezo wa Netball kuanzia ngazi ya wilaya, Mkoa hadi Taifa  ili kuhakikisha kiwango cha mchezo huo kinakua kwenye maeneo yote nchini badala ya sasa ambapo baadhi ya mikoa mchezo huo umeanza kutoweka kabisa.
Mjumbe wa Chaneta Taifa, Yasinta Silivester aliyasema hayo kwenye mafunzo ya walimu wa mchezo wa Netball yaliyohudhuriwa na walimu 19 wa shule za msingi na sekondari wa Mkoa wa Singida na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Mwenge mjini Singida.

“Mheshimiwa mgeni rasmi chama cha netball kimekuwa na Program sasa hivi ya kuhamasisha mchezo wa netball kuanzia ngazi ya wilaya,Mkoa hadi Taifa”alisisitiza Yasinta.

Kwa mujibu wa Yasinta mwezi wa nane,mwaka huu kutakuwa na semina ngazi ya taifa,hivyo walimu waliohudhuria mafunzo hayo yaliyofanyika shule ya sekondari Mwenge,angependa wasinyimwe ruhusa ya kuhudhuria mafunzo hayo yatakayofanyika Mkoani Manyara.
Hata hivyo kiongozi huyo wa kitaifa alisisitiza kwamba ni muhimu kwa walimu hao wakahudhuria kwenye mafunzo hayo ya kitaifa kutokana na Mkoa wa Singida kuwa bado upo nyuma sana katika mchezo wa netbali.

“Meshimiwa mgeni rasmi mimi kama mjumbe wa taifa wa chaneta nasimamia kanda za Kaskazini na kanda ya kati  yenye mikoa ya Manyara,Singida,Arusha,Kilimanjaro na Dodoma,kwa hiyo mwezi huu kulikuwa na semina ngazi ya basic ya Mkoa Kilimanjaro ,Manyara walifanya mwaka jana na mwaka huu Singida mwezi wa nane kutakuwa na semina ngazi ya taifa”aliweka bayana mjumbe huyo wa chaneta taifa.

Akizungumza na walimu wa michezo waliohudhuria mafunzo hayo ya siku tano,Afisa michezo wa Mkoa wa Singida,Martin Kapera pamoja na mambo mengine alitumia fursa kuvipongeza vituo  vya Televisheni vya Channel Ten Azamu kwa mchango wake wa kutangaza michezo katika Mkoa huo.
 Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo.Grace Irumba alisisitiza kwamba mchezo huo wa Netbali kidogo ulikuwa kama vile unataka kulala lala,lakini kwa uwezo wake Mungu uongozi wa Taifa na viongozi uliopo mikoani kila mmoja anataka kuuamsha mchezo huo katika Mkoa wake.

Katika risala ya wanasemina hao iliyosomwa na Luiza Mujah iliyataja malengo ya mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kupata ujuzi wa uamuzi wa mpira wa Netbali unaoendena na sheria mpya za mpira wa Netbali ili waweze kuutumia ujuzi huo kwenye maeneo yao                                                   
 Mjumbe wa kamati ya utendaji Taifa CHANETA,Yasinta Silivester akizungumza na walimu 19 waliohudhuria mafunzo ya siku tano ya mchezo wa Netiball yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Mwenye, mjini Singida.
 Afisa michezo wa Mkoa wa Singida,Henry Kapera akisaini vyeti vya kuhitimu mafunzo kwa walimu wa michezo wa Netibali Mkoani Singida.
 Mwalimu Luiza Mujah (mwenye fulana ya njano) akikabidhiwa na Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida, Henry Kapera cheti cha kuhitimu mafunzo ya mchezo wa Netibali.
Washiriki wa mafunzo ya mchezo wa Netibali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi,ambaye pia ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida, Henry Kapera(aliyevaa fulana nyekundu), viongozi wa Chaneta Mkoa na Taifa. (Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images