Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110158 articles
Browse latest View live

DAWA NI KUACHA UHALIFU KUPUNGUZA MSONGAMANO MAGEREZANI-MWIGULU

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.Mwigulu Nchemba ametoa rai kuwa ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani ni vema jamii ikaacha kufanya matukio ya uhalifu nchini.

Dk.Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati anatoa ufafanuzi kuhusu madai ya uwepo wa msongamano wa wafungwa katika magereza mbalimbali yaliyopo nchini ambapo amelieleza Bunge si kweli kwamba magereza yote yana msongamano.

Amesema yapo baadhi ya magereza idadi ya wafungwa ni wengi na hiyo inatkana na wingi wa matukio ya uhalifu kwenye eneo husika na kule ambako hakuna uhalifu mwingi basi nako kwenye magereza hakuna msongamano mkubwa wa wafungwa.

Dk.Mwigulu amesema alifanya ziara katika gereza la Mkoa wa Lindi na baada ya kufuka huko ameshuhudia idadi ndogo ya wafungwa kuliko uwezo wa gereza lenyewe ambalo linao uwezo wa kuhifadhi wafungwa wengi na kufafanua udogo wa wafungwa unatokana na kutokuwepo na matukio mengi ya kihalifu ambayo husababisha mhusika kufungwa.

Ameongeza maeneo ambayo uhalifu ni mwingi unapoenda kwenye magereza nako utakuta idadi ya wafungwa ni kubwa, hivyo ili kuondoa hali hiyo ni jamii kuacha kufanya uhalifu tu.

"Nitoe rai kuwa ili kupunguza msongmano kwenye magereza yetu njia ni moja tu kuacha kufanya uhalifu.Hiyo itasaidia kuondoa malalamiko kwenye magereza yetu idadi ya wafungwa ni kubwa,"amesema Dk.Mwigulu.

Ameongeza Serikali haipendi kufunga watu ili wakajaze magaerezani bali msongamano huo unasababishwa na watu kufanya matukio ya uhalifu na matokeo yake kufungwa na kusababisha msongamano ambao unaelezwa kuwepo.

Wakati huo huo,Mbunge wa Tarime Mjini Estar Matiko(Chadema) ameelezea namna ambavyo wafungwa na mahabusu wanawake ambavyo wanateseka magaerezani na kuomba wale wenye kesi ndogo waachiwe kwani wapo ambao wamefungwa kwa makosa madogo madogo yakiwamo ya fedha ambapo , kiwango cha fedha anachotumia gerezani ni kikubwa kuliko makosa yake.

Amesema akiwa magereza ya Segerea ameshuhudia kuna mwanameke ambaye amefungwa na anatatizo la kuvuja damu, hivyo kila siku lazima apelekwe hospitalini ambako gharama inakuwa kubwa.Hata hivyo Wizara hiyo imejibu kinachofanyika sasa ni kwa mujibu wa sheria na hivyo kama inaonekana ni tatizo basi ni vema Matiko akapeleka hoja bungeni ili sheria ibadilishwe.

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUTANGAZA VIVUTIO VYA UWEKEZAJI VILIVYOPO NCHINI

Wanafunzi wa Watanzania waingia Tuzo za Kimataifa za DStv Eutelsat Star

$
0
0
Jumatatu Aprili 9, 2018; Tanzania imepata wawakilishi wawili watakaoshiriki katika msimu wa saba wa tuzo maarufu barani Afrika kwa wanafunzi wapenzi wa masomo ya Sayansi na Teknolojia ijulikanayo kama - DStv Eutelsat Star Awards. Wanafunzi hao Michael Ditrick wa shule ya Sekonday Ilboru – Arusha na Taher Rasheed wa Al-Madrasat Ussaifiyatul Burhaniyah ya jijini Dar es Salaam

Michael ameshika nafasi ya kwanza katika uandishi wa insha maalum na Taher kwa mchoro maalum kuhusiana na sayansi ya Setelait ambapo wanafunzi zaidi ya 150 kutoka shule mbalimbali nchini walishiriki katika mashindano hayo ya mwaka huu. Washindi hao walipatikana kutakana na utahini uliofanywa na jopo la majaji sita.

Kazi za washindi hao zimewasilishwa MultiChoice Africa ambapo zitapambanishwa na kazi kama hizo kutoka kwa washindi wa nchi nyingine kote barani Afrika na hatimaye kupatikana mshindi wa jumla katika kila kipengele yaani wale walioandika insha na wale walioandaa mchoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande, amesema tuzo za mwaka huu zimekuwa na ushindani mkubwa ambapo shule kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Dodoma, Pwani zimeshiriki. “Kuongezeka wa idadi ya wanafunzi wanaoshiriki katika tuzo hizi ni ishara njema na tunaamini kwa viwango walivyoonyesha, bila shaka mwaka huu tutapata ushindi mkubwa kuliko hata ule wa mwaka jana” alisema Maharage.

Amesema tuzo hizi zinalenga kuwajengea vijana wetu ari ya kushiriki katika masomo ya sayansi na pia kuhamasisha ubunifu na ugunduzi katika tasnia ya sayansi. Amewataka walimu kuwahimiza wanafunzi wao kushiriki katika tuzo kama hizi za kimataifa kwani ni kipimo kizuri kwa wanafunzi wetu na pia inajenga kujiamini kwa wanafunzi wetu.

Tuzo hizi ambazo zinahusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango vyenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait ni za wazi kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19.

Mwaka huu, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango kuhusu manufaa yaliyoletwa na uvumbuzi wa setelaiti katika maisha ya kila siku hapa ulimwenguni na ni jinsi gani setelait imekuwa kama kiungo muhimu kwa shughuli zote zinazofanyika kote duniani.

Kama kawaida tuzo hizi zina zawadi kabambe ambapo mshindi wa Insha atapata fursa ya kuzuru kituo cha Eutelsat nchini Ufaransa na pia kwenda Guiana kushuhudia mubashara urushwaji wa setelait angani.

Mshindi wa bango atajishindia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini na kutembelea kituo cha anga cha nchi hiyo na pia makao makuu ya MultiChoice Africa akiwa kama mgeni maalum. Shule zitakazotoa washindi hao zitapata zawadi ya kufungia huduma ya DStv bure.

Wanafunzi wengine waliofanya vizuri katika mchakato huo ni pamoja na Pio Mwita wa UWATA Sekondari ya Mbeya ambaye ameshika nafasi ya pili kwenye insha na Peter Kiama wa Feza Boys ya Dar es Salaam aliyeshika nafasi ya pili kwa upande wa bango.

Mwaka jana Tanzania iliibuka mshindi wa pili kwenye insha baada ya Davids Bwana wa FEZA Boys kunyakua nafasi hiyo nyuma ya mwanafunzi Leoul Mesfin kutoka Ethiopia.

MICHUZI TV: WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUTANGAZA VIVUTIO VYA UWEKEZAJI VILIVYOPO NCHINI

BALOZI SEIF AIPONGEZA KAMPUNI YA ZANRDEF

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliishukuru na kuipongeza Taasisi ya Kiraia ya Zanzibar Relief and Development Foundation { ZANRDEF} kwa uamuzi wake wa kusaidia huduma za msingi ya Kijamii za Maji safi katika azma yake ya kuona maisha ya Wananchi yanaendelea kustawika.

Alisema uamuzi huo wa ZANRDEF utasaidia kuwapunguzia machungu Wananchi walio wengi kupata huduma hizo sambamba na kuiunga Mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mipango yake ya kuwasogezea karibu mahitaji ya msingi Wananchi wake.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitoa shukrani hizo wakati akizungumza na Viongozi wa Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Mahonda mara baada ya kukikagua Kisima cha Maji safi na salama kinachochimbwa katika Skuli ya Mahonda kwa msaada wa Taasisi ya ZANRDEF.

Alisema zipo changamoto nyingi za upatikanaji wa huduma za Maji safi na salama kwa Wananchi walio wengi Visiwani Zanzibar licha ya juhudi kubwa inayoendelea kuchukuliwa na Serikali kwa kushirikiana na washirika wa Maendeleo kuitafutia ufumbuzi changamoto hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifika Skuli ya Mahonda kukagua uchimbaji Kisima cha Maji safi na salama kitakachowaondoshea usumbufu Wanafunzi na Walimu wa Skuli hiyo.
Balozi Seif pamoja na Uongozi wa Wilaya ya Kaskazini B na Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Mahonda wakishuhudia harakati za Uchimbwaji wa Kisima cha Maji safi na Salama katika Skuli ya Mahonda Msingi na Sekondari chini ya usimamizi wa Mhandisi wa Taasisi hiyo Bwana Doto Saleh wa kwanza Kulia aliyevaa Kofia ya Manjano.
Balozi Seif Kati Kati akipongeza na Kuishukuru Taasisi ya Kiraia kwa uamuzi wake wa kusaidia huduma za Maji Safi na Salama Ndani ya Skuli ya Msingi na Sekondari ya Mahonda. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Nd. Rajab Ali Rajab na Kulia yake ni Katibu wa ZANRDEF Bwana Ali Mohamed Haji.
Harakti za uchimbwaji wa Kisima cha Maji safi na Salama katika Skuli ya Mahonda zikiendelea licha ya mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha muda mrefu.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Rajab Ali Rajab akitoa shukrani kwa Uongozi wa Jimbo la Mahonda na Taasisi ya Kiraia ya ZANRDEF kwa jitihada za kusogeza huduma za Maji safi katika Skuli ya Mahonda Msingi na Sekondari. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAKAZI WA BONDE LA ZIWA RUKWA WAPATA SHILINGI MILIONI 16.5 KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA POLISI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amekabidhi shilingi milioni 5 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa alipotembelea ujenzi wa kituo hicho cha polisi tarehe 13.11.2017 na wananchi kumuomba kuchangia ambapo ukamilifu wa kituo hicho utasaidia kuhudumia kata 13 zilizopo katika bonde la ziwa Rukwa.



Sambamba na hilo Mh. Wangabo pia aliwasilisha ahadi ya Milioni 10 aliyoitoa Mkuu wa jeshi la Polosi nchini IGP Simmon Siro alipotemblea Mkoa wa Rukwa na kuongeza kuwa kuna shilingi milioni 1.5 ambayo pia ni ahadi ya mkazi wa bonde la ziwa Rukwa anayeishi nje ya Mkoa ambaye hakuhitaji kutajwa jina lake.

“Nimekuja kutekeleza ahadi yangu ambayo inaendana na mlichonisomea, mlisema ili kituo cha polisi kikamilike mlihitaji shilingi milioni 4, mkaniomba niwatafutie, mimi nimekuja na shilingi milioni 5, ila nilituma timu yangu ili kuangalia ile gharama kama ilikuwa sahihi, nikaambiwa na hiyo timu kuwa inahitajika shilingi Milioni 22, alipokuja Kamanda IGP niliteta nae na alipoona umuhimu wa kituo hiki aliahidi shilingi Milioni 10,” Mh. Wangabo alisema.

Wakati akikabidhi fedha hizo kwenye mkutano na wananchi niaba ya Mkuu wa Mkoa, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Albinus Mgonya alimtaka Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Hamis Mongela kukiri kupokea fedha hizo huku ahadi nyingine zikiendelea kufuatiliwa ili ujenzi wa kituo hicho ukamilike kwa wakati, nae Hamisi alikiri kupokea fedha hizo.

Diwani wa kata ya Mtowisa Mh. Edgar Malinyi alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho ni juhudi za wananchi wanaotaka usalama wa vitu na mali zao wakishirikiana na polisi huku mtendaji wa Kata ya Mtowisa Paulo Katepa akisesama kuwa wananchi hawatakata tamaa hadi kituo hicho kikamilike kwani ujezi wake ulianza tangu mwaka 2002.

BENKI YA UBA YAENDELEZA UJIRANI MWEMA KUPITIA MICHEZO

$
0
0
 Mchezo kati ya Timu ya Wafanyakazi wa Benki ya United Bank of Africa (UBA) Tanzania na taasisi mbalimbali kutoka nchini Uganda zilizopo nchini ukiendelea kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Ushindini Mikocheni jijini  Dar es salaam. Taasisi mbalimbali kutoka nchini Uganda ilishinda bao 2 kwa bila dhidi ya Wafanyakazi wa Benki UBA.

Kikosi cha Timu ya Wafanyakazi wa Benki ya United Bank of Africa (UBA) Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja. Wafanyakazi hao wamecheza mechi ya kirafiki na timu ya taasisi mbalimbali kutoka nchini Uganda zilizopo nchini. Uganda ilishinda kwa mabao 2 dhidi ya UBA (Tanzania) 0. Mechi hiyo ilichezwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ushindini Mikocheni jijini  Dar es salaam.

TIMU YA WATAALAM WA UJENZI KUTOKA NCHINI CHINA YAKAGUA ENEO LA UJENZI WA CHUO CHA VETA KAGERA ILI KUANZA UJENZI MARA MOJA

$
0
0
Serikali ya Watu wa China imetuma timu ya Wataalam wa Usanifu wa Majengo na ujenzi, kukagua na kujiridhisha na eneo lililotengwa na Serikali ya Mkoa wa Kagera kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Kisasa cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kinachotarajiwa kujengwa  kwa ufadhili wa Serikali ya Watu China, Mkoani Kagera katika Kijiji cha Burugo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

Timu hiyo ya Wataalamu kutoka katika Kampuni ya ujenzi ya “China Qiyuan Enginering Coorparation” ikiongozwa na Bw. Fang Ke Feng  walimueleza Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salim Kijuu juu ya ujuo wao huo, Ofisini kwake walipofika kumsalimia kuwa wamekuja kuona eneo la chuo cha VETA kitakapojengwa ili waweze kuchora michoro ya majengo inayoendana na eneo husika.

Baada ya kufika katika eneo la Burugo kitakapojengwa Chuo cha VETA, Wataalam hao waliridhishwa na eneo hilo na kusema kuwa ni eneo zuri linalofaa kwa ujenzi na michoro wanayotarajia kuichora itaendana na eneo hilo.
“Tumeona eneo ni zuri sana, Serikali ya Mkoa imefanya kazi yake ya kufikisha miundombinu ya umeme na barabara katika eneo la ujenzi, pia tumeridhika na juhudi zinazoendelea kufanyika ili kuhakikisha maji yanapatikana katika eneo hili na jambo lakufurahisha Ziwa Victoria lipo karibu sana kwa upatikanaji wa maji katika ujenzi,” Alieleza Bw. Fang Ke Feng.

Vilevile kiongozi wa Timu hiyo ya wataalamu kutoka Nchini China Bw. Fang Ke Feng alisema kuwa baada ya kuona eneo husika sasa itachukua muda wa miezi miwili kabla ya ujenzi kuanza kutoka sasa ambapo watasanifu  michoro ya majengo na kuiwasilisha Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ili iidhinishwe na ujenzi utaanza mara moja.
Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salim Kijuu (katikati) akiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Wataalam wa Usanifu wa Majengo na ujenzi kutoka Kampuni ya ujenzi ya “China Qiyuan Enginering Coorparation” ikiongozwa na Bw. Fang Ke Feng.

Kaimu Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Enock Kayani alisema kuwa ujenzi wa chuo hicho utagharimu jumla ya Shilingi bilioni 22.4 pia katika awamu ya kwanza  chuo kitadahili wanafunzi 400 na awamu ya pili wanafunzi 400 na kukamilisha jumla ya wanafunzi 800 mara baada ya chuo hicho kuwa kimekamilika.
Mkuu wa Mkoa Kagera, Meja Jenerali mstaafu, Salim Kijuu na ujumbe wake wakiangalia michoro ya namna ujenzi huo utakavyokuwa kuwa kupitia laptop.

TIC READY TO FACILITATE COMPANIES WISHING TO INVEST IN PRODUCTION OF MEDICINE AND MEDICAL EQUIPMENT

$
0
0
The Executive Director of Tanzania Investment Centre (TIC) Mr. Geofffey Mwambe was among the presenters during the meeting of pharmaceutical industry stakeholders from within and outside Tanzania who gathered to discuss strategies to accelerate investments in this sector. The meeting was held on 4 th April, 2018 at Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC).

During the meeting the Minister for Health, Community, Development, Gender, Elderly and Children Hon. Ummy Mwalimu (MP) said that, investors should strategically invest in pharmaceutical industry considering the fact that the Government spends huge sums of funds to import medicine and medical equipments. It was reported that about 94% of the medicine and medical equipments used in the country are imported hence depleting limited foreign exchange reserves.

It was noted during the meeting that long lead times are another issue where procured medicine and medical equipments get delivered after up to nine months. High storage cost poses a challenge as the order is placed in bulk to cater for massive demand. Hon. Mwalimu further said challenges in the economy said that investing in local pharmaceutical industry is crucial in order to address the said challenges in the economy.

The Minister for Industry, Trade and Investment, Hon. Charles Mwijage (MP) in his remarks said that the Government is focused on industrialization. Therefore, potential investors should consider such opportunities that are available in pharmaceutical industry. He said that the Government is working on regulatory reforms to remove unnecessary obstacles to investors. He further informed the audience that the Government is determined to ensure that at least 50% of essential medicine and medical equipments used in the country are produced locally by 2025.

In his presentation the Executive Director of Tanzania Investment Centre (TIC) Mr. Geoffrey Mwambe outlined support mechanism put in place by the Government to facilitate investors through TIC. He informed participants that investor wishing to invest in the country will be facilitated through TIC One Stop Facilitation Centre whereby investors are assisted to obtain various permits, licenses and approvals through one window. The services provided are company incorporation, tax payer identification number, industrial license, land derivative rights, work permits, residence permits, environment certificate and standard certificate.

Moreover, he said that projects registered under TIC enjoy fiscal as well as non fiscal incentives providing a soft landing for investors. He finally invited thirty eight (38) companies which expressed interest to invest in pharmaceutical industry to visit TIC for further guidance to enable them invest in the country.

ASSEMBLY TO SIT IN DODOMA

$
0
0
 
…the Sitting is a first for the regional Assembly in the designate capital

East African Legislative Assembly, Dodoma, 9th April, 2018: The East Africa Legislative Assembly (EALA) has commenced its sitting in Dodoma, United Republic of Tanzania. The Sitting which is the fourth meeting of the first Session of the fourth Assembly takes place from today (April 9th 2018) and runs through to 28th of April 2018. This is the first time the regional Assembly which embraces a rotational principle in holding its meetings in the Partner States, is sitting in Dodoma.
                                                                    
The Assembly is to be presided over by Speaker, Rt Hon Ngoga K. Martin. H.E. President Dr John Pombe Joseph Magufuli is expected to address the Assembly at a Special Sitting at a date to be communicated next week.

The Assembly shall also deliberate on a number of key issues over the three-week period. Bills and resolutions are expected to be brought before Plenary.  A number of Committee undertakings are also expected – particularly on scrutiny of Bills in preparation for the forthcoming public hearings. Currently, there are two key Bills that are pertinent to the Monetary Union Protocol. 

These are the EAC Monetary Institute Bill, 2017 and the EAC Statistics Bureau Bill, 2017, both of which were introduced by the Chair of the Council of Ministers, Rt Hon Dr Ali Kirunda Kivenjija at the 2ndMeeting of the 1st Session held in Kampala, Uganda, in January 2018 and sailed through the First Reading.

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA(TCAA)

$
0
0
Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi  ametembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).TCAA ni miongoni mwa taasisi na kampuni zinazoshiriki mkutano wa Saba (7) wa Umoja wa Kampuni za Ndege Barani Afrika(AFRAA) unaofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Kuanzia April 9-10, 2018. Mkutano huu unatoa fursa kwa watumiaji na watoa huduma za usafiri wa anga kuonyesha maendeleo katika sekta.
 Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa Pili Kulia o)  Akimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Vallery Chamulungu(wa Kwanza Kushoto) alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Katika mkutano wa Umoja wa Kampuni za Ndege Barani Afrika(AFRAA) Yanayofanyika Zanzibar Beach Resort kuanzia April 8-10, 2018.
  Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kushoto)  alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Katika mkutano wa Umoja wa Kampuni za Ndege Barani Afrika(AFRAA) yanayofanyika Zanzibar Beach Resort kuanzia April 8-10, 2018.Wengine kutoka Kushoto ni  Waziri wa Miundombinu, Uchukuzi na Mawasiliano Zanzibar, Dr. Sira Ubwa Mamboya na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Eng. Ladslaus Matindi.
Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa Kwanza kulia)  Akifurahia Jambo na Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Katika mkutano wa Umoja wa Kampuni za Ndege Barani Afrika(AFRAA) Yanayofanyika Zanzibar Beach Resort kuanzia April 8-10, 2018.

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU WATUMISHI WALIOONDOLEWA KWENYE MFUMO WA MALIPO

kesi inayowakabili vigogo wawili wa madini ya almasi yapigwa kalenda

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Aprili 9, 2018 imeelezwa kuwa, jalaa la kesi inayowakabili vigogo wawili wa uthaminishaji wa madini ya almasi wa serikali,  akiwemo  Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (TANSORT), Archard Kalugendo, bado liko kwa DPP.

Wakili wa Serikali, Salim Msemo amemeeleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbrad Mashauri, kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa, upelelezi bado haujakamilika. Kalugendo na mthamini almasi wa serikali, Edward Rweyemamu, walipanda kizimbani mahakamani hapo wakati shauri lilipopelekwa kwa kutajwa.

Msemo amedai jalada la kesi hiyo ambalo awali lilikuwa kwa DPP lilirudishwa kwa DCI ambaye ameshalifanyia kazi na limerudishwa tena kwa DPP na sasa  wanasubiri maelekezo ya DPP ili kesi iweze kuendelea.

Hata hivyo, upande wa utetezi ulidai Novemba 9, mwaka jana, upande wa jamhuri ulieleza upelelezi umekamilika na Februari 27, mwaka huu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage baada ya kuonekana ucheleweshwaji wa kesi bila ya sababu ilitoa siku 14 ya kuiambia mahakama ni lini wataendelea na kesi hiyo. Ulidai hoja hizo wanaona zinazidi kuchelewesha kesi, hivyo upande wa jamhuri useme kwa nini amri halali ya mahakama haitekelezeki.

Wakili Msemo amedai ili kesi ianze kusikilizwa lazima mambo yote husika katika shauri hilo yawe yamekamilika na kukamilika kwa upelelezi hakuondoi yale yanayojitokeza na kustahili kufanyiwa kazi katika shauri hilo. Kufuatia hayo, kesi imeahirishwa hadi Aprili 23, mwaka huu, kwa kutajwa na washitakiwa walirudishwa mahabusu.

Washitakiwa hao ambao wako mahabusu wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 2.4. Kalugendo na Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini wanakabiliwa na shitaka la kuisababishia serikali hasara ya sh. 2,486,397,982.54, ambalo waliposomewa mara ya kwanza hawakutakiwa kujibu kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Washitakiwa hao wanadaiwa walitenda kosa hilo, kati ya Agosti 25 na 31, mwaka jana, katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga. Inadaiwa washitakiwa hao kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa serikali na waajiriwa wa wizara hiyo waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43 (sawa na sh. 2,486,397,982).

KINANA AONGOZA VIONGOZI WA CCM MAOMBOLEZO YA WINNIE MADIKIZELA MANDELA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana akisaini kitabu cha maombolezo kwenyeOfisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Dkt Gaudensia Kabaka (MCC) akisaini kitabu cha maombolezo kwenyeOfisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akisaini kitabu cha maombolezo kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg.Shaka Hamdu Shaka akisaini kitabu cha maombolezo kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika Kusini kufuatia kifo cha Mwanaharakati na mke wa zamani wa Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini(Hayati Nelson Mandela), Bi.Winnie Madikizela Mandela Jijini Dar es Salaam leo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KATIBU MKUU NISHATI, AKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua ( kulia) akiongoza kikao kilichokutanisha wadau wa maendeleo na Wizara ya Nishati katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam tarehe 06 Aprili, 2017.
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani)


Wataalam wa Idara ya Nishati, wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (hayupo pichani)

MKUU WA MKOA GEITA AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KWENYE KAMPENI YA ELIMU KWA MLIPAKODI

$
0
0
Na Veronica Kazimoto-Geita

Wito umetolewa kwa wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Geita kujitokeza kwa wingi katika Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kwa ajili ya kuwasilisha malalamiko, changamoto, maoni pamoja na kupata elimu ya masuala ya kodi na ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Geita, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa, wafanyabishara na wananchi watumie fursa ya kampeni hii itakayomalizika tarehe 13 Aprili, 2018 kupata elimu sahihi ya masuala ya kodi na tozo mbalimbali.

“Nachukua fursa hii kutoa wito kwa wafanyabiashara na wananchi wote wa mkoa huu hususani wale wanaoishi katika maeneo ya Masumbwe, Ushirombo, Rulembela, Katoro, Lunzewe, Namonge, Nyanghw’ale, Bwanga na Muganza kujitokeza kwa wingi ili waweze kujifunza, kupata huduma na kutoa maoni yao kwa watalaam wetu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili waweze kuyatolea ufafanuzi na kuyafanyia kazi,” amesema Mhe. Luhumbi.

Nae Meneja wa TRA mkoani hapa, James Jilala amesema kuwa, lengo kuu la kufanya kampeni hii maalumu ni kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea mrejesho na maoni mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

“Kampeni hii ni mwendelezo wa Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi iliyofanyika nchi nzima kuanzia tarehe 5 hadi 9 Machi, 2018 katika ngazi ya mkoa. Kutokana na matokeo ya kampeni ile mkoani hapa, tumeona ni muhimu tuwe na kampeni nyingine maalumu ambayo inafanyika maeneo mbalimbali katika wilaya zetu tofauti na ile ya kwanza iliyofanyika Geita mjini tu,” amefafanua Jilala.Kwa upande wake kiongozi wa timu ya watalaam kutoka TRA Makao Makuu Maternus Mallya ameeleza kuwa, timu yake imejipanga vizuri na tayari kazi imeanza kufanyika katika vituo vyote vilivyotengwa kwa ajili ya kampeni hiyo.

“Hapa ninapozungumza, wenzangu wako kwenye maeneo husika wanaendelea kufanya kazi. Hivyo, kama alivyosema Mhe. Mkuu wa Mkoa, nami natoa rai kwa wananchi wote mkoani hapa, kujitokeza kwa wingi ili waweze kukutana na watalaam wetu kwa ajili ya kupata huduma na elimu ya mlipakodi,” amesema Mallya.

Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi mkoani Geita imeanza leo tarehe 9 hadi 13 Aprili, 2018 ambapo pamoja na mambo mengine, wafanyabiashara na wananchi watasajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) pamoja na kuelimishwa kuhusu ulipaji wa Kodi ya Majengo kwa njia ya kieletroniki.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani humo kuhusu Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi iliyoanza leo tarehe 9 hadi 13 Aprili, 2018 ikiwa na lengo la kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi wa mkoa huo.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita akizungumza wakati wa mkutano wa waandishi wa habari mkoani humo kuhusu Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi iliyoanza leo tarehe 9 hadi 13 Aprili, 2018 ikiwa na lengo la kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi wa mkoa huo.
Kiongozi wa timu ya watalaam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Maternus Mallya akizungumza wakati wa mkutano wa waandishi wa habari mkoani Geita kuhusu Kampeni Maalum ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi iliyoanza leo tarehe 9 hadi 13 Aprili, 2018 ikiwa na lengo la kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi wa mkoa huo.PICHA NA BENEDICT LIWENGA

MAADHIMISHO YA 70 YA SIKU YA AFYA DUNIANI 2018 MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KIJIJI MCHA KIJINI MATEMWE

$
0
0
  WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed akiangalia huduma mbalimbali zilizokua zikitolewa kituoni hapo.
 MWAKILISHI wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO Dkt Ghirmay Andemichael akizungumza katika maadhimisho hayo
 WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed akiwahutubia wananchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho hayo yaliofanyika katika Kijiji cha Kijini  Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Kutokana na mvua iliokua ikiendelea kunyesha Waandishi wa Habari hawakua nyuma kuchukua habari katika maadhimisho hayo.
 MKUU wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja Hassan Ali Kombo akitoa shukurani kwa  Wizara ya Afya Zanzibar  ilivyo ichagua Wilaya yake Kufanya maadhimisho ya mwaka huu.
WAZIRI wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed watatu kutoka kushoto akipiga picha ya pamoja na wageni mbalimbali.
(Picha na Abdalla Omar Maelezo – Zanzibar).​

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wasanii watakiwa kuwa makini wanapo saini Mikataba.

$
0
0
Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

Wasanii wa nyanja zote  wakumbushwa kuzingatia na kuwa makini kuzitambua aina 7 za sheria katika zoezi zima la kusaini mikataba mbalimbali katika kazi zao hapa Nchini.

Akizungumza na wasanii mbalimbali  leo katika ukumbi wa Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) Jijini Dar es Salaam Wakili wa kampuni ya Setla,  Noeli Chikwindo amesema kuwa ni vema kwa wasanii kufahamu sheria 7 za usaini wa mikataba ili kupata haki zao zinazostahiki.

" Ni vema kabla hujatia saini  ufahamu ni kitu gani unasaini pamoja na kuelewa vizuri  lugha iliyotumika katika mkataba huo ili kuepuka matatizo ya baade yatakayojitokeza"amesema wakili Chikwito.

Vile vile amewataka wasanii kuwa makini na kazi zao pindi wanapoingia mkataba na kampuni yoyote kuzingatia zile sheria 7 katika makubaliano hayo.

"Msanii ni muhimu kufahamu  masharti ya mkataba kabla ya makubaliano inasaidia kuepuka usumbufu wa kupata haki yako,na wakati mwinginine msanii hulalamika kumbe yeye ndo chanzo cha matatizo" amesema wakili Chikwindo.

Aidha msanii wa muziki wa dansi  Franswaa Makasi  amewataka wasanii wenzake wa nyanja mbalimbali wajitambue katika kuzingatia  mikataba wanayosaini kuwa na vipengele vyote  vya sheria ili kuondokana na usumbufu

"Wasanii wenzangu ifike mahari tujitambue  ili haki zetu zipate kutendeka sawa,kazi zipo mikataba ipo lakini hatujitambui na sisi tutende haki  upande wa pili maana wasanii wengine vile vile hawatendi haki" amesema makasi Junior.

MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO YATIMA YAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Na Salum Vuai, MAELEZO
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema jamii ina wajibu wa kuwalea na kuwatunza watoto yatima badala ya kuwakwepa, kuwanyanyasa na kuwadhulumu.

Katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Maudline Castico kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto yatima duniani huko Fumba, Samia amesema kuwapuuza yatima ni kubeba dhima kwa Mwenyezi Mungu.

Alifahamisha kuwa, ni lazima ndugu na wanafamilia wa wazazi wanaotangulia mbele ya haki, wakubali  kuwa walezi wa watoto wanaoachiwa kwa kila hali na kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwemo elimu na kuwafundisha maadili mazuri.

Makamu wa Rais, alieleza kuwa, haijuzu kwa mtu mzima kupuuza umuhimu wa kuwalea na kuwatunza watoto yatima, ikizingatiwa kwamba kila mmoja atakutana na kifo wakati wowote, hivyo naye pia kuacha watoto nyuma yake.

“Unapomnyanyasa yatima wa Mungu, ukamnyima matunzo, na mara nyengine ukamdhulumu mirathi na haki zake wakati nawe pia una watoto, na ni mgeni katika dunia hii, je, ukifariki utaridhika watoto wako wanyanyaswe?”, alihoji Makamu wa Rais. 

Alisisitiza kuwa, jukumu la kuwalea na kuwatunza  watoto waliopoteza wazazi wao ni la kila mtu na wanapaswa kuwapa upendo, matunzo pamoja na elimu ambayo ndio mkombozi wa maisha yao kwa sasa na hapo baadae.


 Mgeni rasmi Waziri wa  Kazi Uwezeshaji Wanawake Wazee na Watoto Maudline Cyrus  Castico akitoa Hotuba  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.   

 Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Swaleh Omar Kabi akitoa hotuba yamakaribisho kwa mgeni rasmi  katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.  
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kiislamu ya Muzdalifa Farouk Hamad  Khamis akizungumza machache kuhusu mtoto yatima katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Baadhi ya Watoto mayatima waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Watoto mayatima kutoka Skuli ya Alfarouk Aktas Muslim wakisoma Kasda maalum yenye maudhui ya kumlinda mtoto yatima katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto yatima yaliofanyika katika Viwanja vya Bakhresa Fumba Wilaya ya Magharibi B Unguja.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MKUTANO WA WADAU KATI YA SERIKALI, WAAJIRI, PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KUHUSU MASUALA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI UTAKAOFANYIKA DODOMA SIKU YA TAREHE 13 APRILI, 2018

$
0
0
Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Viwanda, Biashara na Kilimo Tanzania (TCCIA) pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), wanautaarifu Umma kuwa wameandaa Mkutano wa Wadau utakaojadili na kupokea maoni kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi. 

Mkutano huu utawakutanisha Waajiri  na Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) wa Mikoa ya Dodoma na Singida; na Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

Eneo:Jengo la LAPF,
Mtaa wa Uhindini, Barabara ya Makole,
DODOMA.
Tarehe: 13 Aprili, 2018
Muda: 7:30 Mchana

Imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu,
Jengo la LAPF,
Mtaa wa Uhindini,
Barabara ya Makole,
S.L.P. 2890,


DODOMA, TANZANIA.
Viewing all 110158 articles
Browse latest View live




Latest Images