Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

ALICHOKISEMA DKT. ABBASI KWA WAANDISHI WA HABARI WA KAMPUNI YA GLOBALGROUP


DKT. KIKWETE ASEMA VIFO VYA WATOTO WACHANGA VINAWEZA KUZUILIKA, ASIFU JUHUDI ZA CSI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete amesema matatizo ambayo yanatokana na uzazi yapo ambayo yanaweza kuzuilika na kuhimiza wadau kushirikiana na Serikali kwa lengo la kuendelea kupunguza vifo vya mama mjazito na mtoto.

Pia ametoa pongezi kwa hatua zinazochukuliwa na Taasisi ya Childbirth Survival International(CSI) ya kuhakikisha wanatoa elimu ya afya salama ya uzazi na kushiriki kwa vitendo katika kufanikisha vifo kwa mama na mtoto vinapungua hapa nchini.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa hotuba yake kwenye Maadhimisho ya miaka mitano ya CSI na kutumia nafasi hiyo kuwapongeza waanzilishi wa taasisi hiyo Stella Mpanda na Profesa Tausi Kagasheki.

Rais mstaafu Kikwete amesema kumekuwepo na vifo ambavyo vinatokea kwa wajawazito na watoto ambao hawana hatia na kutumia nafasi hiyo kuhimiza wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kupunguza vifo hivyo.

Amesema ipo haja ya kuendelea kutolewa elimu ambayo itasaidia jamii kutambua umuhimu wa kuhudhuria kliniki kwa mama mjazito na kubwa zaidi kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwenye eneo la afya ya uzazi na vifo. Ameelezea hatua ambazo zinachukuliwa katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya ya taasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI) jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI) jijini Dar es Salaam
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda akitoa  historia ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo, mafanikio na changamoto wakati wa Maadhimisho ya miaka mitano jijini Dar es Salaam
 Mmoja ya waanzilishi wa Childbirth Survival International(CSI), Profesa Taus Kagasheki akitoa shukrani kwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kutokana na mchango wake katika kuhakikisha Tanzania tunapunguza vifo vya mama mjazito na mtoto.
 Mshehereshaji kwenye Maadhimisho ya miaka mitano ya tasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI), Babie Kabae akifafanua jambo wakati maadhimisho hayo ambayo yamefanyika jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya waalikwa wakifuatilia hotuba ya rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete wakati maadhimisho ya miaka mitano ya ya tasisi ya Childbirth Survival Internatinaol (CSI) jijini Dar es Salaam.


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI WA TAKWIMU ZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI NCHINI

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA WAZEE NA WATOTO



TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UFAFANUZI WA TAKWIMU ZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI NCHINI


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kutoa ufafanuzi wa takwimu za vifo vitokanavyo na uzazi nchini. Ufafanuzi huu unatokana na taarifa iliyorushwa na kituo cha Televisioni cha ITV katika moja ya taarifa zake za habari siku ya tarehe 29 Machi 2018 na baadaye kuanza kuzunguka katika mitandao ya kijamii inayosema “Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu-UNFPA limesema idadi ya vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi hapa nchini imeongezeka hadi kufikia vifo 556 kwa kila vizazi hai elfu moja (1000) kutokana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ikiwamo uhaba wa wauguzi na wakunga”.


Nikiwa Waziri mwenye dhamana ya Afya, napenda kuufahamisha umma kuwa taarifa hizo sio sahihi.  Na ukweli wake ni kuwa takwimu za tathimini iliyofanywa na Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mwaka 2015/2016 (Ikiwa ni miaka miwili na nusu iliyopita) ya Hali ya Afya za Watu Tanzania (TDHS - MIS) ni kuwa vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 (laki moja) na si vifo 556 kwa kila vizazi hai 1,000 (efu moja). Aidha nasisitiza kuwa Takwimu hizi ni za miaka miwili na nusu iliyopita.


Ni muhimu ikafahamika kuwa Serikali ya awamu ya Tano tangu imeingia madarakani Novemba 2015, imewekeza sana katika sekta ya afya hususani katika eneo la afya ya mama na mtoto. Tuna imani kuwa endapo itafanywa Tathmini kama hii iliyofanywa na kusimamiwa na Taasisi ya Taifa ya Takwimu  (NBS) hakuna shaka kuwa itatuonesha hatua kubwa tuliyopiga katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wetu wa maendeleo tumechukuwa hatua mbalimbali zenye lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Mikakati ambayo serikali ya Awamu ya Tano kwa kushirikiana na wadau wasekta ya Afya imewekeza na kuitekeleza  ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ni pamoja na:-

HOTUBA YA RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI UZINDUZI UKUTA WA MIRERANI.06 APRILI 2018

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

RAIA RWANDA WAADHIMISHA MIAKA 24 YA MAUAJI WA KIMBARI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia),  Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,  Eugene Kayihura (wa pili kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez (kulia) wakiwasha mishumaa wakati wa tendo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyoadhimishwa leo Aprili 7, 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii

LEO April 7 raia wa Rwanda waishio nchini Tanzania wameadhimisha miaka 24 ya mauaji ya kimbari yalipoteza zaidi ya watu milioni moja kwa siku 100 hasa kabila la Watutsi na kuacha yatima, wajane wengine wengi katika hali ngumu. Raia hao wameeleza kuwa kilichotokea  hawatakisahau na hakitatokea tena.

Mgeni rasmi katika kumbukizi hizo Waziri wa Habari, sanaa vijana Utamaduni na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe ameeleza kuwa tukio hilo ni la kusikitisha sana hata Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipofanya ziara nchini Rwanda mwaka 2016 alitembelea kituo cha mauaji hayo huko Kigali na kueleza kuwa haya yalianza kwa kupandikiza chuki katika jamii na kusisitiza kuwa mauaji haya hayatatokea tena Rwanda na kwingineko Afrika.

Aidha Mwakyembe ameeleza kuwa lazima tusaidiane na kushirikiana ili kuhakikisha haya hayatokei tena barani Afrika.

Naye Balozi wa Rwanda nchini ameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambalo liliathiri wananchi na taifa kwa ujumla lakini baada ya vita Rwanda iliungana tena na kuwa wamoja na kuleta maendeleo, ameeleza kuwa wanawakumbuka wenzao ambao walilengwa kuuawa na hawatasahaulika kamwe. Pia hadi sasa wananchi wameungana pamoja na wapo sambamba katika kuleta maendeleo nchini humo.

Naye Mwakilishi wa umoja wa mataifa (UN) Alvaro Rodriguez ameeleza kuwa waliouawa watakumbukwa Rwanda na kueleza kuwa kuokoa maisha ya watu  lazima kuwe na matendo na katika kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya haki za binadamu lazima kila nchi ijizatiti katika kutimiza malengo yake ya kulinda haki za binadamu.

Maadhimisho hayo yalianza kwa sala fupi na baadaye mishumaa kuwashwa kama ishara ya kuwakumbuka wenzao waliouwawa kwenye mauaji hayo.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,  Eugene Kayihura pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez wakiwasha mishumaa pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari za Kimasila na Chang'ombe wakati wa tendo la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyoadhimishwa leo Aprili 7, 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.
Balozi wa Rwanda nchini Tanzania,  Eugene Kayihura akitoa hotuba iliyolenga kuzungumza kuhusu mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda wakati wa maadhimisho ya miaka 24 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari yaliyoadhimishwa leo Aprili 7, 2018 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.


KUMBUKUMBU YA MIAKA 46 YA SHEIKH ABEID AMANI KARUME

NAIBU WAZIRI KWANDIKA AFUNGA BARAZA LA WAFANYAKAZI SEKTA YA UJENZI, MOROGORO

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa, akihutubia viongozi na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wakati akifunga kikao cha pili cha baraza hilo kilichofanyika mkoani  Morogoro.
????????????????????????????????????
Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kushoto), akizungumza na wajumbe wa baraza hilo kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, kufunga kikao cha siku ya pili cha baraza hilo, mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (kushoto), kabla ya kufunga baraza hilo lililokutana kwa siku mbili, mkoani Morogoro.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (hayupo pichani), wakati akifunga kikao cha siku ya pili ya baraza la wafanyakazi kilichofanyika mkoani Morogoro.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

DC KIGAMBONI ATOA AMRI KWA WASIMAMIZI WA MRADI WA LAKE OIL KUFANYIWA MAHOJIANO MAALUM NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA

$
0
0



Mkuu wa wilaya ya kigamboni kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama leo wametembelea kata ya Pemba mnazi eneo la Yaleyale panu kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Alhamisi ya wiki iliyopita walipokuwa wakikagua majengo yaliyopo pembezoni mwa fukwe za bahari.
DSCN1118
Akiongea na vyombo vya habari katika matembezi hayo Mh.Hashim Mgandilwa amesema kuwa takribani wiki mbili zilizopita walikuwa wanatembelea maeneo ya fukwe za bahari ili kufanya ukaguzi kutokana na wilaya hiyo ya kigamboni kuwa lango la biashara haramu na wahamiaji halamu.
DSCN1114
Pia amesema kuwa katika ukaguzi huo waliofanya eneo linalomilikiwa na mwekezaji wa Lake oil lilikutwa na tatizo kwa kuwa na gati linaloweza kutumiwa na chombo chochote cha maji katika kushusha na kupakia mzigo wowote na kuagiza gati hilo kubomolewa ndani ya siku tano lakini maagizo hayo yamekiukwa ambapo utejelezaji umeanza kutekelezwa leo kinyume na barua waliyoituma halimashauri ikionyesha utekelezaji huo kutendeka.
DSCN1001
Hata hivyo mkuu wa wilaya akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya usalama ameagiza kukamatwa kwa wahusika hao ili kufanyiwa mhojiano zaidi kwa sababu za kiusalama sambamba na kufika na vibali vinavyowaruhusu kufuga swala pamoja na hati miliki zinazoonyesha umiliki halali wa eneo hilo na kusisitiza kuwa kama hawatafanya hivyo watanyang’anywa eneo hilo na kukabidhiwa kwa mtu mwingine.
DSCN0930
Viongozi hao waliokamatwa ni kiongozi mkuu wa miradi kutoka lake oil Fahim Mohammed na Mkurugenzi msaidizi wa lake oil Halid Mohammed, hata hivyo viongozi hao wamekana kukaidi agizo la mkuu wa wilaya na kuomba kupewa angalau muda wa mwezi mmoja kwani shughuli ya ubomoaji waliyoagizwa kufanya ni ngumu na inahitaji vifaa maalumu.
DSCN0874
Kwa upande wake mwanasheria kutoka NEMC Manchale Heche amesema kuwa lake oil walipokea barua kutoka ofisi za NEMC ya kuwaruhusu kuendesha mradi pembezoni mwa bahari lakini hawakuruhusiwa kujenga nyumba za kudumu na walipewa masharti ambayo wameyakiuka.Hivyo Kufuatia ukiukwaji wa masharti hayo waliyopewa kutoka NEMC mwanasheria huyo amewafutia kibali cha kuendeleza mradi huo mpaka hapo watakapokutana na kufanya makubaliano ya kupata kibali kingine na kufuata masharti kama sheria inavyosema.

RAIS DKT MAGUFULI ATANGAZA AJIRA MPYA 1500 POLISI,ATAKA JKT WAPEWE KIPAUMBELE ,SI WATOTO WA VIGOGO

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ametangaza nafasi 1500 za ajira mpya kwa Jeshi la Polisi nchini huku akitoa maelekezo, anataka vijana wa JKT ndio wapewe nafasi hizo na si kutafuta ndugu,jamaa na marafiki wa makamanda wa wilaya na mikoa.

Amesema kuna tabia imejengeka  pale inapotokea nafasi za ajira kwa ajili ya jeshi la polisi,baadhi ya makamanda wanatafuta watu wao na hivyo hata wakienda kwenye mafunzo wanapewa mafunzo kwa kuangalia waliowapeleka.

Rais Magufuli ametoa tangazo hilo wakati anazungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha baada ya tukio la kuzindua nyumba npya za Polisi zilozojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wadau wa maendeleo wa mkoa huo.Ambapo ameagiza nyumba hizo wapewe askari wa vyeo vya chini.

Amesema kutokana na kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa salama hivyo ameamua kutoa ajira mpya 1500 na kufafanua anataka kuona wanaopata ajira hiyo ni watoto wa masikini na si vinginevyo.

"Nataka hizi nafasi ambazo nimezitangaza hapa leo hii zielekezwe kwa JKT ambazo waliamua kujitolea kupata mafunzo na kwa sehemu ni vijana ambazo hawana ndugu, kamanda wa Polisi,mkoa au kiongozi wa serikali." Bali ni vijana ambao wanatoka familia masikini.Hivyo niombe kipaumbele cha ajira hiyo kielekezwe kwa vijana waliopita JKT.Tabia  ya kusikia wanaopewa nafasi ni ndugu wa wakubwa hapana,"amesema Rais Kikwete.

Pia amezungumzia namna ambavyo Jeshi la Polisi linafanya kazi vizuri ya kulinda usalama wa raia na mali zao huku akielezea wakati ameingia madarakani kuliibuka mauaji katika wilaya ya Kibiti na Mkuranga mkoani Pwani.Amefafanua katika mauaji hayo watu 59 wamepoteza maisha na kati yao wamo askari 17 ambao wamepoteza maisha wakati wakilinda usalama wa wananchi wa maeneo hayo.

 Dk.Magufuli amesema askari waliopoteza maisha Kibiti walikuwa na nia ya kuhakikisha nchi inakuwa salama na kimsingi ni Polisi ambao ni watoto wa watanzania masikini.Hivyo amesema hata hivyo polisi wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha mauaji hayo yanakoma na leo kuko salama na hata kama waliokuwa wanatekeleza mauaji  hayo bado wapo Polisi wamejipanga na wanaendelea kuimairisha ulinzi.

MAJALIWA ASHIRIKI DUA YA KUMWOMBEA RAIS WA KWANZA WA ZANZIBAR ABEID AMAN KARUME

$
0
0
Makamu wa Rais, Samia Suluhu,  Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi   Seif Ali Iddi  (kushoto) na Balozi Ali Karume  (wapili kushoto) wakishiriki katika  dua ya kumwombea Rais wa  Kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume   kwenye  kaburi la Hayati Karume  lililopo Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mjini Zanzibar Aprili 7, 2018. Wanne kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,  Ali Hassan Mwinyi na watatu kushoto ni Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu,  Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi   Seif Ali Iddi  (kushoto) na Balozi Ali Karume  (wapili kushoto) wakishiriki katika  dua ya kumwombea Rais wa  Kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume  kwenye Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mini Zanzibar Aprili 7, 2018. 
 Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein  akishiriki katika dua ya kumwombea Rais wa kwanza wa Zanzibar, Aman Abeid Karume kwenye Ofisi Kuu ya CCM iliyopo Kisiwandui Zanzibar Aprili 7, 2018. Watatu kulia ni  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wanne kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,  Ali Hassan Mwinyi. Wapili kulia ni Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Kabi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Rais wa Zanzibar DKt. Ali Mohammed Shein  akishiriki katika dua ya kumkwombea Rais wa kwanza wa Zanzibar, Aman Abeid Karume kwenye Ofisi Kuu ya CCM iliyopo Kisiwandui Zanzibar Aprili 7, 2018. Watatu kulia ni  ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na wanne kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi.Wapili kulia ni Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Kabi .
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi  Augustine Mahiga wakati alipowasili kwenye Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kushiriki  katika dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume Aprili 7, 2018.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kushiriki  katika dua ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume Aprili 7, 2018. Katikati ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAMBURA AJIBU MAPIGO TFF BAADA KUTUPILIA MBALI RUFAA YAKE

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF), Michael Wambura ameamua kufunguka na kujibu hoja ambazo zimetolewa dhidi yake.

Wambura ameweka wazi kujibu hoja moja baada ya nyingine kuhusu rufaa iliyosomwa jana na Kamati Rufani ya Maadili ya TFF.

Rufaa ya Wambura ilitupiliwa mbali baada ya Kamati ya Rufaa kuona haina mashiko.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Wambura amesema yeye pamoja na jopo lake la Mawakili wanasubiri hukumu ya rufaa hiyo (Jumatatu) ili kuijadili kwa kina kuhakikisha rufaa inaendelea.

Amesema yaliyosomwa jana katika rufaa yake si yale yalioandikwa wakati wakupeleka rufaa hiyo.Amedai kuwa suala hilo lakisheria limetoka katika Mpira na badala yake linakwenda katika maisha yake binafsi.

Kuhusu Kesi ya Simba, Wambura amesema kuwa kesi hiyo ilifutwa tangu 13/4/2017, amesema haikuwa na mashiko mbele yake.Kwa upande wa Wakili wake, Emmanuel Muga amedai Kamati iliyotoa uamuzi ilibadirishwa kwa baadhi ya Wajumbe, amedai Kamati haikuwa halali.

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAGERA (KCU) CHAFAFANUA KUHUSU MALIPO YA AWALI YA KAHAWA YA WAKULIMA

$
0
0
Na Mathias Canal, WK-Dodoma

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila ametoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd kama ilivyojadiliwa kwenye Mkutano wao Mkuu tarehe 27/03/2018.


Amebainisha hayo wakati akizingumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mjini Dodoma na kusema kuwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera si Kampuni ya kununua kahawa bali ni ushirika wa wakulima wadogo wadogo wenye lengo la kuunganisha nguvu zao kwa  pamoja katika kuhudumia zao la  kahawa na kuliwasilisha sokoni kwa utaratibu wenye tija endelevu na kisha kugawana mapato  baada ya kufanya mauzo.


Alisema bei halisi ya mkulima kwa upande wa Ushirika inapatikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika ambapo  wakulima hulipwa malipo ya mwisho kwa kadri ya bei ya kuuzia iliyopatikana sokoni na hesabu ya mwisho kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu.


Hivyo kwa vile mchakato wa mauzo huchukua si chini ya kipindi cha mwezi mmoja tangu mkulima awasilishe kahawa yake kwenye ushirika hadi malipo ya mwisho kufanyika, basi ili kumuondolea mkulima adha ya kusubiri malipo yake yote baada ya mauzo wakati anahitaji kujikimu na kukidhi mahitaji yake muhimu, wakulima wenyewe kwa utashi wao kupitia  Mkutano Mkuu, wanajadili malipo ya awali atakayotanguliziwa mkulima wakati anasubiri malipo ya mwisho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Mwingine ni Kaimu meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg John kanjagaile. Picha Zote Na Mathias Canal, WK 

Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Kilimo (Kilimo 4).


KATIBU WA BUNGE AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KAMATI NDOGO TUME YA UTUMISHI WA BUNGE JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (kushoto) akizungumza na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo tarehe 7 MachI, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma. Kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi


Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (kushoto) pale ugeni huo ulipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa ajili kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi.


Wajumbe wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia kikao kati yao na Katibu wa Bunge, pamoja na Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge kikilenga kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi. Kutoka kushoto ni Mhe. Leontine Nzeyimana, Mhe. Aden Abdikadir (wa pili kushoto), Mhe. Dkt. Anne Leonardo (watatu kushoto) na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Ndg. Nenelwa Wankanga (kulia)
 

Wajumbe wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki walioongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Susan Nsambu (watatu kulia) wakiwa katika kikao cha pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge walioongozwa na Katibu wa Bunge, Mhe. Stephen kagaigai (wa pili kulia) kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi. 


Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioongozwa na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (watatu kulia) pale ugeni huo ulipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

KATIBU WA BUNGE AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA KAMATI NDOGO YA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0
 Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (kushoto) pale ugeni huo ulipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa ajili kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi.
 Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (kushoto) akizungumza na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kulia) pale ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipomtembelea leo tarehe 7 MachI, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma. Kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi
 Wajumbe wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia kikao kati yao na Katibu wa Bunge, pamoja na Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge kikilenga kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi. Kutoka kushoto ni Mhe. Leontine Nzeyimana, Mhe. Aden Abdikadir (wa pili kushoto), Mhe. Dkt. Anne Leonardo (watatu kushoto) na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, Ndg. Nenelwa Wankanga (kulia)
 Wajumbe wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki walioongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Susan Nsambu (watatu kulia) wakiwa katika kikao cha pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge walioongozwa na Katibu wa Bunge, Mhe. Stephen kagaigai (wa pili kulia) kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi.
Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki  ulioongozwa na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Tume ya Utumishi wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Susan Nsambu (watatu kulia) pale ugeni huo ulipomtembelea leo tarehe 7 Machi, 2018 ofisini kwake Mjini Dodoma, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kwenye mambo ya ajira ya wafanyakazi, nidhamu, maendeleleo na maslahi ya wafanyakazi. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAFUNGA MAFUNZO YA UZAMIAJI MAJINI KINA KIREFU

$
0
0
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage, akipokelewa na Maafisa wa Jeshi hilo pamoja na mwenyeji wake ambaye ni mmiliki wa Yatch Club Bw. Brian Fernandes, alipokwenda kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika katika kisiwa cha Bongoyo kilichopo ndani ya bahari ya hindi, Jijini Dar es Salaam.
Mzamiaji wa kikosi maalum cha Uokoaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajini Gift Longwe, akionesha mbinu mbalimbali za uzamiaji majini kwenye kina kirefu walizojifunza toka kwa wakufunzi kutoka nchini Ujerumani,  kwa mgeni rasmi Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, (CF) Billy Mwakatage (hayupo pichani). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam. 
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CF) Billy Mwakatage (katikati), akimkabidhi cheti mmoja ya wahitimu wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu, Sajini Gift Longwe (kushoto). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam. 
Wazamiaji wa kikosi maalum cha Uokoaji majini wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajini Gift Longwe (kushoto) na Koplo Siwizan Kazimoto (kulia), wakionesha umahili wao wa uzamiaji majini kwenye kina kirefu mbele ya mgeni Kamishna wa Operesheni wa Jeshi hilo, (CF) Billy Mwakatage (hayupo pichani). Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mapema leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)

SERIKALI YAPATA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 34 KUTOKA MFUKO WA MAENDELEO YA KIUCHUMI WA KUWAIT

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), na Serikali ya Tanzania zimetiliana saini rasimu ya mkataba wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 15.3, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34, kwa ajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, lenye ukubwa wa hekta 3,000.

Rasimu hiyo ya Mkataba imesainiwa na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait, Dkt. Abdulrida Bahman na kwa upande wa Tanzania ikisainiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, mjini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema hatua hiyo imfikiwa baada ya timu ya wataalamu kutoka Kuwait kutembelea eneo la mradi mkoani Kigoma na kuridhishwa na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.
“Mradi huo una umuhimu mkubwa kwa watanzania kwa kuwa wataweza kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga na Mbogamboga kwa mwaka mzima badala ya kilimo cha msimu cha kutegemea mvua, na katika siku zijazo Kigoma itakua miongoni mwa mikoa inayozalisha mchele kwa wingi”, alisema Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali ya Tanzania na Kuwait zitatia saini mkataba rasmi wa mkopo huo wenye masharti nafuu ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu ili mradi huo uanze kutekelezwa ili kuongeza kipato cha wananchi na kuwa na uhakika wa chakula.Amesema Nchi ya Kuwait imekuwa ikiisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ukarabati wa Hospitali ya Mnazi mmoja, Zanzibar kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, wakibadilishana rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma,

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akisaini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Ujumbe wa wataalamu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na Dkt. Abdulrida Bahman (kushoto), wakisikiliza maelezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani), kabla ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za  Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akiongoza mazungumzo kabla ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo  wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na mmoja wa wajumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, baada ya tukio la kusainiwa kwa rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34.4, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio lililofanyika mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano-Wizara ya Fedha na Mipango).



LAZIMA WAWEPO MADEREVA WAWILI KWA MABASI YAENDAYO MIKOANI-KAMANDA MWANGAMILO

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni kimesema mabasi yanayofanya safari za mikoani na nchi jirani lazima wawepo  madereva wawili na hilo haliepukiki.

Akizungumza na Michuzi Blog, leo Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam Solomon Mwangamilo amesema ukaguzi wa mabasi na madeva wawili ni endelevu katika kuhakikisha abiria wanasafiri salama.

Mwangamilo amesema wamiliki mabasi wahakikishe wanazingatia usalama wa mabasi na abiria.Pia wahakikishe kunakuwa na madereva wawili ambao watapokeza kuendesha wakiwa safarini.Amesema basi likitoka katika kituo cha Ubungo lazima madereva wawili wasaini na mpaka wanafika katika kituo chao mwisho wanahakikiwa, hivyo hakuna mtu anayeweza kufanya udanganyifu kutokana na mtando uliopo katika jeshi la Polisi.

Mwangamilo amesema wanaoingiza mabasi ambayo mabovu na kutegemea wataondoka na abiria kituo cha mabasi Ubungo wanajidanganya  na wataofanya hivyo watakwenda jela.“Kazi yetu ni kuhakikisha wananchi wanasafiri na mabasi yakiwa salama kutokana ukaguzi unaofanyika kila kukicha na hakuna basi litakaloachwa huku likiwa lina ubovu wa kuhatarisha watumiaji wa usafiri huo” amesema Mwangamilo.


Aidha amesema askari katika mkoa wa Kinondoni hasa kituo cha mabasi Ubungo kuwa kufanya kazi ya ukaguzi bila kikomo katika kuwalinda usalama wa abiria wanatumia mabasi ya mikoani na nchi jirani.
Mkaguzi Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi basi la Kampuni ya Tokyo Takara katika kituo hcho leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabani wa Kituo cha Mabasi Ubungo, Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi basi la Kampuni ya Tokyo Takara katika kituo hcho leo jijini Dar es Salaam.
Askari wa Usalama Barabarani Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo , Nuru Hussein akimpa maelekezo dereva wakati wakifanya ukaguzi mabasi kutuo hicho, leo jijini Dar es Salaam.
Abiria wakishuka katika Basi la Princess Line linalofanya safari zake Dar es Salaam ,Babati baada ya Basi hilo kuonekana na hitilafu takiribani ya masaa manne katika kituo cha Ubungo na kufanya kampuni kuwabadilishia basi lingine.
Askari wa Usalama Barabani katika kituo kikuu cha Ubungo, Koplo Rashid Abdallah akizungumza na abiria walio kaa zaidi ya masaa manne katika Basi la Princess Line, leo .jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mabasi yalikutwa na kamera yetu katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo

SERIKALI YAPATA MKOPO WA SHILINGI BILIONI 34 KUTOKA MFUKO WA MAENDELEO YA KIUCHUMI WA KUWAIT

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), na Serikali ya Tanzania zimetiliana saini  rasimu ya mkataba wa  kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 15.3, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 34, kwa ajili ya mradi wa  kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma,  lenye ukubwa wa  hekta 3,000.

Rasimu hiyo ya Mkataba imesainiwa na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait,  Dkt. Abdulrida Bahman na  kwa upande wa Tanzania ikisainiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, mjini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  amesema hatua hiyo imfikiwa baada ya timu ya wataalamu kutoka Kuwait kutembelea eneo la mradi mkoani Kigoma na kuridhishwa na umuhimu wake kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

 “Mradi huo una umuhimu mkubwa kwa watanzania kwa kuwa wataweza kuwa na kilimo cha umwagiliaji cha Mpunga na Mbogamboga kwa mwaka mzima badala ya kilimo cha msimu cha kutegemea mvua, na katika siku zijazo Kigoma itakua miongoni mwa mikoa inayozalisha mchele kwa wingi”, alisema Dkt. Mpango.
kutokana na ushirikiano mzuri, wa kihistoria, na wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, wakibadilishana rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akiagana na Kiongozi wa ujumbe wa wataalamu na Mshauri wa Masuala ya Kilimo wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), Dkt. Abdulrida Bahman, baada ya tukio la kusainiwa kwa  rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma, tukio lililofanyika mjini Dodoma.
Ujumbe wa wataalamu kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), ukiongozwa na  Dkt. Abdulrida Bahman (wa tano kutoka kulia), na ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kutoka kulia), wakiwa katika picha ya pamoja nje ya Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma, baada ya tukio la kusainiwa kwa  rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani, kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (SERA), Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akisaini rasimu ya mkataba wa mkopo wa dola milioni 15.3 za Marekani kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), kwa ajili wa kujenga mradi wa kilimo cha umwagiliaji maji katika Bonde la Luiche, mkoani Kigoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA NYUMBA ZA POLISI JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa kituo maalumu ya Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha ambacho kimejengwa na wadau wa utalii  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe akiwa na viongozi wengine pamoja na wadau waliosaidia  ujenzi wa kituo maalumu cha Jeshi la Polisi cha Utalii na Diplomasia  jijini Arusha  kwenye sherehe zilizofanyika leo Aprili 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro  wakifunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaidiwa  na viongozi wengine akikata utepe  kuashiria kufunguliwa rasmi kwa nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na baadhi ya familia za askari polisi baada ya kufungua  rasmi nyumba za makazi ya askari ya polisi za Naura zilizojengwa upya baada ya kuteketea kwa moto kwenye sherehe zilizofanyika jijini Arusha leo Aprili 7, 2018.
Picha na IKULU

Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images