Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

AJALI YA MAGARI KUGONGANA YAUA WATU 12, YAJERUHI 46

0
0
Ajali ya hii imetokea majira ya saa mbili usiku wa jana huko kijiji cha Makomero wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora ambapo Basi lenye namba za usajili T.983 DCE mali ya Kampuni ya CITY BOY likiendeshwa na EMANUEL ATUPENDA CHITEMO mkazi likiwa linatokea Ngara Mkoa wa Kagera kuelekea Mkoa wa Dar es salaam liligongana na gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T.486 ARB lilokuwa linaendeshwa na SALUMU ABDALAH KALAMBO na kusababisha vifo vya abiria 12 huku 46 wakijeruhiwa.

Akiongea na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi WILBROD MUTAFUNGWA ameeleza kwamba Abiria 12 walipoteza Maisha huku wengine 46 wakijeruhiwa na kati yao aliwataja abiria watatu ambao hali zao ni mbaya na wawili wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mkoa wa Mwanza na mmoja Nkinga Mission wilaya ya Igunga.

Kamanda Mtafungwa ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Gari aina ya Fuso kupasuka tairi ya mbele upande wa kulia na kusababissha kukatika kwa mfumo wa usukani likiwa katika mwendo mkali baada ya kuyaingia mashimo mawili yaliyo katikati ya barabara na kusababisha kupoteza mwelekeo na kisha kuligonga basi la abiria lililokuwa likipishana nalo.
Gari kampuni ya CITY BOY mara baada ya kupata ajali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora alipowatembelea na kuwajulia hali majeruhi katika Hospitali ya Igunga.

MUSTAFA HASSANAL AZINDUA MAVAZI YAKE MAPYA NCHINI NIJERIA,AZUNGUMZIA ANAVYOGUSWA NA MATATIZO YA WANAWAKE

0
0

 Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MBUNIFU nguli wa mavazi barani Afrika Mustafa Hassanali wiki hii amepata nafasi ya kuwa mmoja kati ya wabunifu 45 kutoka nchi za Afrika , ambao wameshiriki kuonesha mavazi yao ya kipekee katika jukwaa la kifahari la Arise Fashion Week lilofanyika jijini Lagos nchini Nigeria.

 Hassanali aligusa jukwaa la maonyesho hayo Aprili 1 mwaka huu kwa kuzindua mavazi yake aliyoyapa jina la Endometriosis, mavazi yaliyokuwa na nia ya kusambaza ufahamu kuhusu uwepo wa ugonjwa wa endometriosis na kutoa mchango kwa wanawake ambao wametambulika kuwa na ugonjwa huo.

Huku  wakiishi na mapambano ya kufanya matibabu tofauti tofauti iwe, upasuaji, vidonge, na dawa za vimiminika katika kutibu maumivu sugu wanayoishi nayo.

Akizungumza baada ya kupata nafasi hiyo amesemw “Nimekuwa na fahari ya kuingia katika sehemu ya maisha ya mwanamke, sio tu kwa kubuni nguo bali kutengeneza nguo yenye maana inayobeba ujumbe shawishi  kwa jamii.

"Mavazi yangu yenye jina la endometriosis yana nia madhubuti ya kumuunga mkono rafiki yangu Millen Magese ambaye safari yake ya kuishi na endometriosis imekuwa ya kusikitisha na yenye mhemuko wa huzuni, vilevile inaonyesha nguvu ya mwanamke kuwa hata ukipitia maumivu yote hayo, siku zote kuna mwanga na kuleta msukumo kwa wanawake wote dunia”

Amefafanua ni kama methali ya Kiswahili inavyosema, “ukiwa unataka kwenda haraka, nenda  peke yako, ukiwa unataka kwenda mbali nenda pamoja na wenzako”  na hivyo safari ya Mustafa katika ulimwengu wa mitindo ni mfano ulio hai unaoashiria umoja unaopigania matatizo mbalimbali ya wanawake kwenye jamii, iwe ujasiriamali au matatizo ya kiafya.


Amesema kwa miaka 18 iliyopita, Mustafa amekuwa akijitolea kuwa msaada kwa wanawake wanaokumbana na matatizo ya kiafya, huku akiwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na sekta hiyo.


Amekuwa mbele katika kutengeneza kampeni  zenye nia ya kusambaza ufahamu kuhusu  Festula, kansa ya matiti na endometriosis kupitia  majukwaa ya mitindo.

Imeelezwa hakika Mustafa ni mtu wa kipekee sana, na mawazo yake makubwa katika utengenezaji wa nguo zake uleta matokeo ya kuweka saini yake ya kuvutia katika ulimwengu wa mitindo.

Pia  kwa mara nyingine wadau wa mitindo nchini Nigeria wameshuhudia kuwa, kweli Mustafa ni mtu wa mitindo.

MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI

0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi kuwaweka ndani madereva wanaosababisha ajali kutokana na mwendo kasi na baadaye kupelekwa Mahakamani.

Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu muongozo wa Mbunge wa Ulanga Morogoro Mhe. Goodluck Mlinga, juu ya chanzo cha ajali ya basi la City Boy kutoka Karagwe Mkoani Bukoba kuelekea Dar es Salaam ambalo liligongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga usiku wa Aprili 04 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 12.

"Hatuwezi kuacha watu wanapotea kwa ajili ya uzembe wa mtu mmoja na kuleta hasara na vilio vikubwa kwa Watanzania," alisema Dkt. Mwigulu.

Amesema, ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasabishwa na mwendokasi na sio tatizo la miundombinu ambapo katika ajali zilizoripotiwa ajali 1500 zilisababishwa na mwendo kasi na ajali 89 zimetokana na miundombinu. 

Aidha Dkt. Mwigulu amesema, Tanzania ni moja ya nchi zenye barabara bora hivyo ajali nyingi zinazotokea husababishwa na uzembe wa madereva pamoja na mwendokasi.

Wakati huohuo bungeni hapo, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali imeweka utaratibu mashuleni wa kuwawezesha watoto wa kike kuripoti matukio ya udhalilishaji na pia imeanzisha klabu mbalimbali za kuwajenge uwezo na ujasiri wa kuweza kuripoti matukio ya udhalilishaji.

Hata hivyo Prof. Ndalichako amewataka watoto kutokuwa na uwoga wowote kwa sababu Serikali yao inawalinda, hivyo pale wanapofanyiwa vitendo kinyume na matakwa ya Serikali watoe taarifa ili Serikali ichukue hatua stahiki kwa wale wote wanao wadhalilisha na kusababisha watoto wasisome kwa amani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mjini Dodoma.

TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekutana wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa kwa ajili ya kupata miongozo ya kufanya kiwanda kiweze kujengwa na kuanza kuzalisha dawa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ,Adam Fimbo amesema kuwa kuwakutanisha wadau hao umetokana mkutano wa Mawaziri wa Viwanda , Biashara na uwekezaji pamoja Wizara ya Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto ambapo TFDA imeona ni muda mwafaka katika kuweza kuwapa muongozo wadau jinsi ya kuweza kuanzisha viwanda hivyo.

Fimbo amesema kuwa TFDA kazi yake kubwa ni kuangalia usalama wa dawa tangu inapozalishwa mpaka inaingia sokoni ikiwa lengo ni kumlinda mlaji na dawa hizo.Aidha amesema kuwa baada ili kiwanda cha dawa kiweze kusajiliwa na kuzalisha dawa hizo lazima vigezo vilivyokwa vizingatiwe.

Fimbo amesema baada ya kupata michoro na kuanza kuzalisha dawa usajili hauzidi siku 15 kutokana na hatua zote zilizofanyika TFDA inakuwa imepitia.
Hata hivyo amesema kuwa hakuna uarasimu wowote katika kusajili dawa au kiwanda nia kumlinda mlaji kwa dawa anazotumia.

“Bila kuwa na usalama wa dawa unaweza ukaua watu ndio maana TFDA tuka kwa ajili ya kazi hiyo ya kuangalia usalama wa dawa za ndani na zinazoingia”amesema Fimbo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Adam Fimbo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kukutana na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa kupata miongozo ya kufanya kuwekeza katika sekta hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkaguzi wa Viwanda vya Dawa wa TFDA, Proche Patrick akiwapitisha katika miongozo wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Msajili wa Dawa wa TFDA, Dk. Shani Maboko akizungumza na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa jinsi ya usajili wa dawa unavyofanyika katika mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa wakisikiliza mada zinazotolewa na TFDA . leo jijini Dar es Salaam

MAHAKAMA YA TANZANIA YAINGIA MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA POSTA KUSAMBAZA NAKALA ZA HUKUMU

0
0
Na Mary Gwera

MAHAKAMA ya Tanzania imeingia Mkataba na Shirika la Posta Tanzania kutoa huduma za usafirishaji wa nakala za hukumu, barua na nyaraka muhimu za Mahakama.


Mkataba huo ulisainiwa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta mapema Aprili 05 katika Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mahakama ya Rufani-Dar es Salaam.


Mkataba huu chini ya huduma mpya ya Posta mlangoni (The post at your doorstep) iliyoanzishwa na Shirika la Posta hivi karibuni, utalipa jukumu la kukusanya na kusafirisha/kusambaza nakala za hukumu na nyaraka mbalimbali za Mahakama na kuzifikisha kwa wahusika kulingana na anwani zao na mahali walipo (Anwani za makazi).


Akizungumza kabla ya utiani saini wa mkataba huo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Bw. Hussein Kattanga amesema kuwa hatua hii ni mwendelezo wa maboresho mbalimbali yanayoendelea kufanyika ili kuwafikia wananchi.Aidha; Mtendaji Mkuu amelitaka Shirika hilo kutekeleza makubaliano hayo kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kusambaza nakala za hukumu na nyaraka nbyingine kwa wahusika na kwa wakati.

“Sitarajii kuona wananchi wanapanga foleni Mahakamani kutafuta hukumu zao na nyaraka nyingine, nina imani kuwa Posta mtafanya kazi ya kukusanya na kusambaza nyaraka hizo kwa wananchi ipasavyo,” alisema Mtendaji Mkuu.Naye  Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati ameeleza kufurahishwa kwake na utiaji saini wa Mkataba huo kwani utasaidia kufikia ndoto ya Mahakama ya muda mrefu ya kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi.

“Naomba kusema kuwa, nimefurahishwa sana na hatua hii , kwani ni ndoto ya Mahakama ya muda mrefu, vilevile hatua hii itarahisisha utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Jaji Mkuu ya kutoa nakala za hukumu bure kwa zitawafikia wananchi popote watakapokuwa,” alisema Mhe. Revocati.Kwa upande wake Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Hassan Mwang’ombe alisema alimuhakikishia Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa watafanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa.

“Kusainiwa kwa Mkataba huu kutawezesha pia kuongeza kasi ya usambazaji wa barua za kawaida za Mahakama kuwafikia walengwa mapema zaidi kwani zitachukuliwa  Mahakamani na Maofisa wa Posta na kupelekwa moja kwa moja kwa wahusika/mhusika,” alisema Bw. Mwang’ombe.


Vilevile Mkuu huyo alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Maofisa wa Posta hususani kwa kuandika anwani za makazi pamoja na postikodi.

Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na baadhi ya Maafisa Waandamizi kutoka Mahakama ya Tanzania pamoja na Shirika la Posta Tanzania.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga (kulia), wakibadilishana mkataba huo, mara baada ya kusainiwa katika hafla hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba kati ya Posta na Mahakama ya Tanzania wa huduma ya Posta Mlangoni inayotolewa na shirika hilo. Hafla hiyo, imefanyika katika Ofisi za Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa TPC, Zuhura Pinde. Waliosimama nyuma yao, ni baadhi ya Maofisa waandamizi wa Posta na Mahakama.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi.
Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (kulia), akizungumza katika hafla hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Hassan Mwang’ombe na katikati ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Katanga. Wengine nyuma kutoka kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Fadya Zam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TPC, Elia Madulesi, Mtendaji wa Mahakama Kuu, Leonard Magacha, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani, Solanus Nyimbi. 

MATAYARISHO YA SAFARI IBADA YA HIJJA YANAENDELEA VIZURI

0
0
 Rais wa Biitha ya Hijja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheikh Abdulla Talib Abdalla (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi  habari (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya matayarisho ya safari ya Ibada ya Hijja kwa mwaka 2018 sawa na 1439 hijiria, kulia ni Mratibu wa Biitha Tanzania Bara Mussa Hemed Juma na kushoto ni Mtendaji Mkuu waShughuli za Biitha Ofisi ya Zanzibar Khalid Mohamed Mrisho.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao wakati Rais wa Biitha ya Hijja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheikh Abdulla Talib Abdalla (hayupo pichani) akitoa taarifa ya maendeleo ya matayarisho ya safari ya Ibada ya Hijja kwa mwaka 2018 sawa na 1439 hijiria.
Picha na Idara ya Habari    - MAELEZO.

VIDEO: MIAKA MIWILI YA USIKILIZAJI KERO ZA WANANCHI RC MBEYA ATANGAZA UFUATILIAJI KILA WILAYA

Article 2


BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI APRIL 05, 2018

FEDHA ZA UPANUZI VITUO VYA AFYA ZIFANYE KAZI ILIYOTARAJIWA- RC GALLAWA

0
0
Grace Gwamagobe-Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu fedha zilizotolewa na serikali Mkoani hapa kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya ili zifanye kazi zaidi ya ile iliyopangwa awali kutokana na kuongezeka kwa nguvu za wananchi.

Gallawa ameyasema hayo mapema jana wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbozi alipokagua maendeleo ya upanuzi wa vituo vya afya vya Isansa kilichopokea milioni 500 na kituo cha Afya cha Iyula Kilichopokea milioni 400, kwa ajili ya ujenzi wa maabara, nyumba ya daktari, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti.

“Fedha hizi lazima zifanye kazi iliyopangwa vizuri na pia tuongeze kazi nyingine ya ziada kutokana na kuwa tumepata nguvu ya wananchi lakini pia mafundi wetu hawa tunaowatumia ni wazawa na wenyeji wa maeneo ya kwetu kwahiyo gharama zao zitatupa unafuu ambao tunatakiwa kuutumia kuongeza kazi nyingine”, amesema Gallawa.

Ameongeza kuwa licha ya upanuzi wa vituo vya afya kuchelewa kuanza bado ana Imani kuwa wataweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa kutokana na uchapakazi wa mafundi wazawa wa maeneo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na mafundi wanaojenga katika kituo cha Afya Isansa Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na baadhi ya watendaji na wananchi wa kijiji cha Iyula waliojitokeza katika eneo la ujenzi katika kituo cha Afya cha Iyula Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.



SALMAN KHAN JELA MIAKA MITANO KWA UJANGILI

0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Jodhpur nchini India imemhukumu muigizaji wa filamu za kihindi  Salman Khan (52)  kwenda jela miaka mitano kwa   kukutwa na tuhuma za ujangili.

Khan anadaiwa kwamba mnamo mwaka 1998 Khan  akiwa katika maandalizi ya kutengeneza filamu yake ya Hum Saath Hain aliua swala wawili adimu kupatikana nchini humo maarufu kama Blackbucks huko Rajasthan India.

Akiongea nje ya mahakama wakili wa Khan Bw. Bhawan Sigh ameeleza kuwa mteja wake anaweza kukata rufaa na akikubaliwa anaweza kulipa faini au kuachiwa huru aidha hadi sasa Khan bado amewekwa gerezani kwa muda.

Bhawan ameeleza kuwa Khan alikamatwa akiwa na  waigizaji wengine maarufu  ambao ni  Saif Ali Khan, Sonali Bendre, Tabu na Neelam Kothari ambao waliachiwa huru baadaye.

Abdul Rashid Salim Salman khan maarufu kama Salman Khan alizaliwa Desemba 23 1967, ni muigizaji, muongozaji wa filamu na mwimbaji ambaye amepata tuzo mbalimbali kama National film awards na Filmfare Awards. Khan amecheza filamu zaidi ya 90 zikiwemo Kuch Kuch Hota Hai (1998) 
 Hum Aapke Hain  Koon (1994) na Ile ya kivita ya Karan Arjun (1995).

TBL YAJIKITA KUINUA KILIMO KWA NJIA YA UBUNIFU WA MIRADI YA KISASA

0
0
Na Humphrey Shao, GLobu ya Jamii

KAMPUNI ya Bia nchini (TBL) ambayo ni moja kati ya wanafamilia AB InBev imeandaa shindano linalowahusisha matumizi ya ubunifu na teknolojia kwa wakulima.

Shindano hilo lililozinduliwa jana, litafikia tamati Mei 10 mwaka huu, tukio litakalofanyikia ukumbi wa Mlimani City ambapo washindi watatu watapatikana.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa shindano hilo, linalofanyika kwa ushirikiano na Mradi wa masuala ya Teknolojia na Ubunifu Bits & Bytes, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin, alisema lengo ni kuwatambua na kuwaendeleza wakulima wanaolima kibunifu.

Alisema, kilimo cha kibunifu kinawanufaisha wakulima kwa kuwa wanapata faida ile ile iliyokusudiwa kwa kuwa kinaokoa mazao na mbegu kupotea wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.

“Tanzania Breweries tumeona nafasi ambayo kilimo inayo katika kuendeleza uchumi wa nchi na hilo linaweza kufanikiwa kwa kutumia teknolojia na ubunifu katika kilimo, hivyo shindano hili linalenga kuwafikia wakulima wengi zaidi”alisema Roberto Jarrin.

Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa Bits and Bytes Zuweina Farah, alisema katika kuhakikisha kilimo chenye kuhusisha ubunifu na teknolojia unafanikiwa mnamo April 9 watakua SUGECO, na tarehe 10 na 12 watashiriki kwenye kongamano la kilimo biashara mkoani Morogoro.

Aliongeza pia Arusha mnamo April 12 na 13 katika Chuo cha ufundi Arusha kutakuwa na mjadala kuhusiana na kilimo ikiwa pamoja na kutembelea miradi tofauti ya Twende. Huku April 14 hadi 15 itashirikiana na AIESEC kwa Dar na mipango mingine kufanyiwa kazi kufikisha ujumbe kwa wabia tofauti kwenye eneo hili..
Mkurugenzi wa Tasisi Bits and Bytes,Lilian Madeje akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mradi wa ubunifu wa kuinua kilimo nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia nchini(TBL),Roberto Jarrin, akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu udhamini wao wa kuwezesha bunifu za Kilimo
Waandishi wa Habari waliohudhuria Mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi wa TBL

WADAIWA SUGU WA MADENI YA “COMMODITY ORT SUPPORT (CIS) WATAKIWA KULIPA MADENI YAO NDANI YA SIKU 30

0
0
TANGAZO KWA WADAIWA SUGU WA MADENI YA “COMMODITY IMPORT SUPPORT (CIS)

Katika miaka ya 1980 hadi 2000 Wahisani walitoa fedha za kigeni kwa Serikali ya Tanzania kwa mpango maalum uliofahamika kama “Commodity Import Support (CIS)” kwa lengo la kuipa Serikali uwezo wa kuimarisha uchumi kwa kuzipatia Taasisi, Makampuni, Viwanda na wafanyabiashara uwezo wa kuagiza bidhaa na malighafi kutoka nje ya nchi, kwa kuwa wakati ule nchi ilikuwa na upungufu mkubwa wa fedha za kigeni.

Fedha za msaada za CIS zilitolewa kama mkopo wenye masharti nafuu kwa wanufaika, ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni bila kutozwa riba katika kipindi cha miezi 18. Kwa mujibu wa sheria ya CIS {The Commodity Import Support Regulation Act, CAP 261 R.E. 2002 (S. 8 (1) (b)}, mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asilimia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania inapoikopesha Serikali (discount rate) katika kipindi husika. 

Zaidi ya makampuni 980 yalikopeshwa chini ya utaratibu huu. Pamoja na juhudi kubwa iliyofanywa na Serikali ya kuwataka wakopaji wote kurejesha mkopo huo, ikiwa ni pamoja na tangazo la tarehe 30 Desemba, 2015, bado urejeshaji wa mikopo hiyo umekuwa sio wa kuridhisha.

Ili kuhakikisha wadaiwa wote wanalipa mikopo yao, Serikali imeunda Kikosi Kazi ambacho kinajukumu la kufuatilia na kukusanya madeni toka kwa wadaiwa wote ili fedha hizo ziweze kutumika kwa miradi ya maendeleo. Serikali inawataka wadaiwa wote kulipa madeni hayo ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili. 

Kwa wote ambao hawatarejesha mikopo hiyo katika kipindi cha siku 30, majina yao yatatangazwa katika vyombo vya habari na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Kikosi Kazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam, chumba Na. 352, Simu Na. +255 739 40 30 25.

WATUMISHI WA SEKTA YA UJENZI WATAKIWA KUJITATHIMINI

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amewataka wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi kujitathimini yale waliyoazimia kutekeleza kwa mwaka wa Fedha 2017/18 kama yamefikia lengo ili kuweza kusaidia kuboresha utendaji na kutafutia ufumbuzi masuala ambayo yanakwamisha ufanisi wa kazi na kuwezesha mazingira wezeshi kwa wafanyakazi.

Prof. Mbarawa amesema hayo mkoani Morogoro, wakati akifungua kikao cha baraza la wafanyakazi ambapo pamoja na mambo mengime amesisitiza umuhimu wa baraza hilo katika kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuleta matokeo chanya katika utendaji kazi wenye tija, staha na upendo.
Ni matarajio yangu kuwa kila mjumbe kwa nafasi aliyonayo katika baraza hili atatumia fursa hii kutoa michango ya mawazo ili iweze kuwa mwongozo mzuri wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi”, amesema Prof. Mbarawa. 

Aidha, ametoa wito kwa wajumbe hao kuhakikisha kuwa Wizara inashiriki kikamilifu katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuwajengea watanzania miundombinu bora na imara ili kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda na hivyo kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya kuifanya nchi yetu iwe na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi (hawapo pichani), wakati wa ufunguzi wa baraza hilo lililofanyika mkoani Morogoro.
Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), akizungumza na wajumbe wa baraza hilo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya sekta hiyo katika kikao cha baraza la wafanyakazi, mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bi. Elizabeth Tagora akiwasilisha rasimu ya bajeti na mpango wa utekelezaji wa sekta hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2018/19 kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi, mkoani Morogoro.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) wakifuatilia maelekezo ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika mkoani Morogoro.

WAKULIMA KUNUFAIKA NA KILIMO CHA PAMBA GEITA

0
0
Na Joel Maduka,Geita

Serikali imewahakikishia mazingira yaliyo salama wakulima wa zao la pamba ikiwa ni pamoja na kununuliwa kwa zao hilo bila ya kukopwa kwa msimu wa pamba ambao unatarajia kuanza tarehe 1 Mei mwaka huu .

Hayo yameelezwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru , Charles Kabeho wakati akifungua mradi wa zao la pamba katika kijiji cha Nyamalimbe Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo alisema serikali imejipanga kuhakikisha mkulima wa pamba mwaka huu ananufaika na zao hilo.

“ Zao la Pamba linamanufaa kwa mkulima na serikali kwani zao ambalo linatengeneza nguo kuliko kusubili kuletewa mitumba kutoka nje hivyo tulithamini zao hili kwani linasaidia pia kuondoa umaskini katika familia”Alisisitiza Kabeho.

Mussa Kabehe ambaye ni Mkulima wa zao hilo alisema kwa sasa kutokana na hali ya hewa na mvua kunyesha kwa wingi wamekuwa na matumaini machache ya kupata pamba Nyingi kwani asilimia kuwa zimeharibikia shambani na kwamba awana matarajio ya kuzalisha pamba Nyingi zaidi ingawa kwa mwaka huu wengi walijitokeza kulima pamba.

Kiongozi huyo wa mwenge pia amefungua miradi 12 katika Halmashauli ya Wilaya ya Geita iliyo gharimu kiasi cha shilingi bilioni tano na milioni miatatu ambapo pia kiongozi huyo aliwakumbusha wananchi wa kijiji hicho kutojihusisha na suara la rushwa kwa ni adui wa haki.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Charles Kabeho akizungumza na kuwasisitiza wakulima wa zao la Pamba kuwekaza nguvu zaidi kulima zao hilo wakati alipoweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa shamba la pamba kijiji cha Nyamalimbe Wilayani Geita. 
Baadhi ya pamba zikiwa shambani kabla ya kuvunwa. 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Charles Kabeho,akiweka jiwe la msingi kwenye shamba la pamba kwenye kijiji cha Nyamalimbe. 
Watoto ambao ni yatima wakipewa zawadi na Kiongozi wa mbio za mwenge Charles Kabeho kwenye Kijiji cha Bujura wilayani Geita. 

MAAFISA UGANI WAKABIDHIWA PIKI PIKI GEITA TC

0
0
Na Joel Maduka,Geita.

Halmashauri ya Mji wa Geita imetoa pikipiki nne(4) kwa Maafisa kilimo wa Kata ili waweze kutimiza wajibu wao wa kuwatembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na wakulima katika maeneo yao.

Akikabidhi pikipiki hizo,mapema jana katika Ofisi za Halmashauri ya Mji Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameipongeza Halmashauri hiyo kupitia viongozi wake kwa kuona umuhimu wa kununua pikipiki hizo ili ziweze kuwasaidia wataalam wa kilimo kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika kutoa huduma za ugani kwa wakulima.

Mkuu wa Mkoa wa Geita amewataka Maafisa ugani waliopatiwa pikipiki hizo wafanye kazi zao kwa weledi mkubwa katika kuwafikia wakulima wengi zaidi na kutoa huduma stahiki na tahmini ya kina ifanyike juu ya ufanisi wa Maafisa ugani wote wenye vyombo vua usafiri.

Mhandisi Robert Gabriel amefafanua kuwa Mkoa wa Geita umejipanga kuanzisha kilimo cha korosho ili kuongeza mazao ya biashara, hivyo ujio wa pikipiki hizo utasaidia sana kutembea na kubaini maeneo mbalimbali yanayofaa kwa kilimo cha zao la korosho.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ametumia fursa hiyo kuziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Geita kuiga mfano thabiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kufikisha lengo la asilimia 100 kwa kuwawezesha Maafisa Ugani wote nyenzo za usafiri ili wakasimamie shughuli za kilimo. Pia watenge asilimia 10 ya mapato yatokanayo na ushuru wa mauzo ya pamba ili fedha hizo zisaidie kutoa huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kununua pikipiki.

Kwa upande wao Maafisa Ugani wa Kata za Bung’wangoko na Mtakuja, Ndg. Allan Kisomeko na Jackline Otieno kwa niaba ya wenzao wameishukuru Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kuwapatia vyombo vya usafiri vitakavyowawezesha kufanya kazi kurahisi na kuwafikia wakulima wengi kwa muda mfupi, tofauti na awali walipokuwa wakitembea kwa miguu au kutumia usafiri wa baiskeli kuwafuata wakulia katika maeneo yao ndani ya Kata wanazozihudumia.

Halmashauri ya Mji wa Geita imetoa pikipiki nne aina ya Honda ambazo zimegharimu kiasi cha Shilingi bilioni kumi na mbili na laki nane(12,800,000/= )kufuatia agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Kassimu Majaliwa alipofanya kikao na Wakuu wa Mikoa kumi inayozalisha zao la pamba nchini mwezi Septemba 2017 mjini Dodoma, ambapo aliziagiza Halmashauri zote katika Mikoa hiyo kununua pikipiki kwa ajili ya Maafisa ugani wao ili waweze kuwafikia wakulima wengi kwa muda mfupi.
Halmashauri ya Mji Geita yatoa pikipiki 4 aina ya Honda zenye thamani ya Tsh. 12,800,000 kwa Maafisa ugani wa kata za Bung'wangoko, Kanyala,Nyanguku na Mtakuja. Pichani ni Bi. Jackline Otieno, Afisa Ugani wa kata ya Mtakuja akifurahi kukabidhiwa pikipiki na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel leo tarehe 5 aprili katika ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Geita. Halmashauri imefikia lengo la asilimia 100% kwa kuwawezesha Maafisa ugani wa kata zote 13 kupata pikipiki 

RAIS DKT. MAGUFULI AELEKEA MKOANI MANYARA Leo

0
0
Picha zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Marubani wa Ndege ya abiria ya ATCL wakati akielekea kupanda ndege hiyo kuelekea mkoani Kilimanjaro na badae mkoani Manyara kwa ajili ya shughuli mbalimbali za Kitaifa mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ndege hiyo ya abiria ya Shirika la Ndege la ATCL kuelekea mkoani Kilimanjaro na baadae mkoani Manyara.

PICHA NA IKULU

WAZIRI KIGWANGALLA AAGIZA KILA KIJIJI KUTENGA ENEO LA UHIFADHI WA MISITU

0
0

Na Hamza Temba, WMU, Kishapu, Shinyanga

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amewaagiza Wakuu wa Mikoa nchini kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinatenga maeneo katika kila kijiji kwa ajili ya uhifadhi wa misitu ikiwa ni pamoja na vijiji hivyo kuunda kanuni na taratibu zao wenyewe za kusimamia maeneo hayo. 

Ametoa agizo hilo jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wakati wa kuhitimisha kilele cha Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika mkoani humo kuanzia Aprili 03 mwaka huu.

Katika kufanikisha zoezi hilo ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuchagua mikoa 10 ya kuanza utekelezaji wa agizo hilo ikiwemo mikoa ya Shinyanga na Tabora ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa misitu.

Ameugiza pia we uongozi huo wa TFS kuweka mpango wa uhifadhi wa misitu ya asili katika maeneo hayo kwa kushirikiana na vijiji kupanga maeneo yanayostahili kuhifadhiwa sambamba na kuwapa elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa maeneo hayo.

Wakati huo huo Dk. Kigwangalla ametoa siku saba kwa uongozi huo wa Wakala wa Huduma za Misitu kuwasilisha kwake mpango wa tathmini ya uvunaji wa mazao ya misitu wa nchi nzima kwa kuzingatia kiasi cha rasilimali misitu kilichopo na kiwango halisi kitakachotakiwa kuvunwa ambacho hakitazidi robo ya rasilimali iliyopo.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakipanda mti wa kumbukumbu wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakipanda mti wa kumbukumbu wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia wananchi wakati wa kuhitimisha kilele cha Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yaliyofanyika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakielekea eneo la tukio la kupanda miti wakati wa kilele cha kuadhimisha siku ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika jana katika kijiji cha Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TAFITI ZINAONESHA NI MUHIMU KUWEKEZA KATIKA UFUNDI STADI KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA-DKT MMARI

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti ya REPOA Dk.Donald Mmari amesema kuna sababu ya kuwekeza zaidi katika kutoa elimu ya ufundi stadi nchini kwa lengo la kupika watalaamu wa fani mbalimbali ambao watashiriki kufanya kazi zenye tija na kuleta ushindani kimataifa.

Dk.Mmari ametoa kauli hiyo wakati akielezea changamoto ambazo wamezibaini kwenye warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na REPOA kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali katika kipindi hiki cha kuelekea Tanzania ya Viwanda.

Amesema wadau walioko kwenye warsha hiyo wamejadili kwa kina mambo mengi kwa maslahi mapana ya nchi yetu na katika mjadala huo wamebaini bado kunachangamoto ambazo ni vema zikafanyiwa kazi ili kufikia malengo ya ujenzi wa viwanda na kuwa na bidhaa zenye ushindani katika soko la kimataifa.

Ametaja moja ya changamoto ambao wameijadili ni uhaba wa wataalam katika nyanja mbalimbali na hiyo inatokana na kutowekeza zaidi kwenye elimu ya Ufundi stadi ambayo inaandaa vijana kujiajiri na kuwa watalaamu wazuri."Tumekubaliana na kutoa mapendekezo kuwa ili tuingie kwenye ushindani ipo haja ya kuhakikisha watanzania wanaalindaliwa katika elimu na ujuzi unaohusu masuala ya ufundi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tasisi ya Utafiti Nchini, REPOA, Dk. Donald Mmari akizungumza wakati wa kufunga Warsha ya siku mbili kwa watafiti iliyoandaliwa na tasisi yake juu ya kwanini ushindani ni muhimu kuelekea uchumi wa Viwanda.
Mlkuregenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Asspciation (TAHA) Jacqueline Mkindi akizungumza jambo wakati wa mkutano huo walipjadili nafasi ya kilimo katika uchumi wa Viwanda.
Mratibu na Mtafiti wa Warsha hiyo kutoka Repoa, Dk. Blandina Kilama akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo wakati alipokuwa akiongoza meza ya majadiliano.
Mtafiti Kutoka Repoa, Dk. Lucas Katera akizungumza jambo kaatika mjadala wa Nishati kuelekea Uchumi wa Viwanda wakati wa Warsha ya siku Mbili ya Watafiti iliyoandaliwa na Repoa.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya siku mbili kwa watafiti juu ya kwanini ushindani ni Muhimu kuelekea Uchumi wa Viwanda wakifatilia mada kwa makini.

Makazi ya Jebel Sifah nchini Oman ni fursa za kiuchumi kwa watu wote

0
0
Balozi Mdogo wa Oman Visiwani Zanzibar, Ahmad Mohamed Al Muzaini wa nne kutoka kulia akiwa amesimama baada ya kumaliza kuzungumza kwenye maonyesho ya makazi ya Oman Visiwani Zanzibar yakiandaliwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman. Maonyesho hayo yamefanyika katika Hoteli ya The Park Hyatt, Zanzibar. Wengine ni wadau wa ardhi na makazi waliohudhuria kwenye maonyesho hayo. Picha na Mpiga picha wetu.

HUKU maonyesho ya makazi ya Jebel Sifah yanayoonyeshwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman yakiendelea visiwani Zanzibar katika Hotel ya The Park Hyatt, baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, wafanyabiashara wa visiwani hapa wametakiwa kupanua wigo wao wa kibiashara kwa kununua makazi yao nchini Oman ili wajiwekee vitega uchumi kwa ajili ya maendeleo yao.

Ushauri huo umetolewa leo na Meneja Mauzo wa Muriya, Ghizlane El Gouchi, wakati wa kuelimisha wakazi na wananchi wa Zanzibar juu ya utendaji kazi wao katika sekta ya ardhi na makazi waliyojikita nchini Oman, huku wakijivunia maendeleo makubwa kwenye sekta hiyo muhimu dunian kote.
Wadau wa ardhi na makazi nchini Tanzania, Ali Al Maskary kulia na Aflah Al Maskary kushoto wakifuatilia jambo na mdau wa ardhi kutoka Oman, Faisal Said Rashid Alzakwani katika maonyesho ya makazi yanayoendeshwa na kampuni ya Muriya yenye maskani yake nchini Oman kwa ajili ya kununua makazi nchini humo. Tukio hilo linafanyika leo Aprili 6, katika Hoteli ya The Park Hyatt, Zanzibar kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni.
Faisal Said Rashid Alzakwani kushoto akipiga picha na aalozi mdogo wa Oman Visiwani Zanzibar, Ahmad Mohamed Al Muzaini.

Alisema kwamba ni vyema Watanzania wote wakiwamo wafanyabiashara wakaelewa umuhimu wa kujitanua kibiashara kwa kuangalia uanIshwaji wa biashara nje ya mipaka yao, huku Kampuni yao ikifungua milango kwa kuwauzia makazi kwa utaratibu mzuri na rahisi katika maeneo yenye solo kama vile pembeni mwa bahari ambako wanaweza kuyatumia kama fursa za kiuchumi bila kusahau hati ya kuishi nchini Oman.

Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images