Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110095 articles
Browse latest View live

DAWASCO YAWAOMBA WALIOUNGANISHIWA MAJI MRADI WA WACHINA KUJISAJILI BURE

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
MENEJA wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO)Ubungo Mhandisi Paschal Fumbuka amewaomba wakazi waliounganishiwa maji kupitia mradi wa Wachina kujisajili katika ofisi husika bure kabisa.

Akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es Salaam Fumbuka ameeleza zaidi ya wateja 250 hawajasajiliwa ila wanatumia maji kupitia idara hiyo, ameeleza mradi huo wa Wachina ulilenga kutoa huduma ya maji kwa wakazi wote katika mfululizo wa vipindi vinne kuanzia mwaka 2011 na wa sasa wanahitaji takwimu ya watumiaji wa maji hayo katika maeneo mbalimbali
.
Aidha Fumbuka ameeleza kama DAWASCO wameandaa dawati maalumu la usajili wa wateja hao na baada ya hapo watalipa bili za kawaida kama wateja wengine.

Kuhusu  maafisa wa DAWASCO kuhusika katika hujuma ya  kuuza maji kwa baadhi ya maeneo baada ya kukata maji Fumbuka amekanusha suala hilo na kueleza kuwa jiografia hupendelea maeneo yenye mabonde hivyo maji yakikatika  hukimbilia sehemu zenye mabonde na hudumu kwa siku 2 au 3 na baadhi ya maeneo hupata maji hivyo hakuna hujuma katika hili.

Pia ameeleza kuwa wana mpango mkubwa wa kufikisha huduma ya maji kwa wakazi wote na kwa asilimia 61 wamefanikiwa na kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za mradi wa maji katika maeneo ya Makabe, Msigani na Kwembe.
 Meneja wa  (DAWASCO) Ubungo, Mhandisi  Paschal Fumbuka, akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam juu ya wakazi wa Dar es salaam waliounganishiwa maji kupitia mradi wa Wachina kujisajili katika ofisi husika bure.
 Meneja wa  (DAWASCO) Ubungo, Mhandisi  Paschal Fumbuka akionesha vifaa mbalimbali.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Meneja wa  (DAWASCO) Ubungo, Mhandisi  Paschal Fumbuka (kulia) akiwa na Meneja Juma Kalemera wakionesha mabomba ya ukubwa tofauti ambayo yapo tayari kwa matumizi.

MICHUZI TV: VIGOGO CHADEMA WAACHIWA KWA DHAMANA...

MBOWE, VIGOGO WENZAKE CHADEMA WATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA

$
0
0

Na Bakari Majeshi, Globu ya jamii
HATIMAYE baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba na kusherehekea sikuu ya Pasaka wakiwa gerezani,Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe pamoja na vigogo wengine sita wa chama hicho leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana,baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka tisa yakiwemo ya Uchochezi wa Uasi na kufanya mkusanyiko isivyo halali kinyume cha sheria.

Mbali ya Mbowe washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu Bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na Katibu wa chama hicho Dk .Vicenti  Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ambaye ameunganishwa na wenzake hao leo.

Mdee  alikamatwa Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini.

Akisoma masharti ya dhamana, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amewataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja.

Pia wadhamini hao wametakiwa kuwa na barua za utambulisho zinazoamika na vitambulisho huku pia wakitakiwa kuripoti katika kituo kikuu cha polisi cha kati kwa mkuu wa polisi mara moja kwa wiki siku ya Ijumaa.

Mapema, kabla ya kusomewa masharti ya dhamana, washtakiwa walisomewa upya mashtaka yao baada wa Wakili wa Serikali Faraja Nchimbi kumuongeza Mdee katika kesi hiyo na kufanya idadi ya mashtaka kufikia tisa na washtakiwa saba.

Akisoma mashtaka hayo, Nchimbi amedai Februari 16, mwaka huu katika barabara ya Kawawa Mkwajuni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio halali kinyume na sheria wakiwa na nia ya kutekeleza lengo la pamoja  na kufanya watu waogope kwamba watakwenda kusababisha uvunjifu wa amani.

Aidha Nchimbi amedai Februari 16, mwaka huu katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni, washtakiwa wakiwa wamekusanyika wao na wenzao 12 ambao bado hawajafikishwa mahakamani, wakiwa kwenye maandamano hayo,licha ya kutolewa  tamko la kuwataka kutawanyika...waligoma kutii amri hiyo na kuendelea na maandamano na kusababisha kifo cha Aquilina Akwkilina kusababisha askari wawili kujeruhiwa kutokana na mkusanyiko  huo.

Katika shtaka la tatu imedaiwa Februari 16, mwaka huu katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, jijini mshtakiwa Mbowe peke yake wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo alihamasisha chuki isivyohalali kwa kutoa matamshi ya kuhamasisha chuki maneno yaliyosababisha chuki mioyoni mwa wana jamii.

Pia Mbowe anadaiwa kufanya uchochezi na kusababisha chuki miongoni mwa wanajamii ya watanzania kinyume na sheria.
Aidha Nchimbi amedai katika mashitaka ya uchochezi wa uasi yanayomkabili Mbowe, inadaiwa akiwa maeneo hayo katika mkutano wa hadhara, akiwa na nia ya kupandikiza chuki na dharau kwa watanzania dhidi ya uongozi wa kiserikali  uliopo madarakani kisheria,

Imedaiwa alitamka maneno yenye kupandikiza chuki na kuleta ushawishi wa uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani kisheria

Nchimbi aliendelea kudai, katika tarehe hiyo hiyo na maeneo hayo mkoani Dar es Salaam, Mbowe alitoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau dhidi ya mamlaka halali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Katika shitaka la saba, Mbowe anakabiliwa na tuhuma za kutenda kosa la kushawishi kutendeka kwa kosa la jinai, ambapo amedaiwa siku hiyo, akiwa pia amejumuika na wengine ambao hawako mahakamani, aliwashawishi wakazi hao wa Kinondoni, kutenda kosa la kufanya maandamano na mkusanyiko usio wa halali.

Mshtakia Msigwa anadaiwa kushawishi raia  kutenda kosa la jinai shtaka analodaiwa kutenda Februari 16, mwaka huu katika maeneo hayo hayo ya Viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Dar es Salaam,

Imedaiwa siku hiyo Msigwa aliwashawishi wananchi wa Kinondoni kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.

Katika shtaka linalomkabili Mdee, imedaiwa Februari 16 mwaka ,2018 katika viwanja vya Buibui vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam akiwa anahutubia wananchi na wakazi wa eneo hilo alitoa matamshi yafuatayo "Sitaki kusimulia madhila yanayomkumba kila mtu katika Serikali ya awamu ya tano, tunaomba tukamchinje Magufuli na vibaraka wake wote kama mbwai na iwe mbwai,"..
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 16 mwaka 2018 kwa ajili ya washtakiwa kuja kusomewa Maelezo ya awali (PH).

DIAMOND AKANG'ATA MENO MBELE YA HAMISA MOBETO

$
0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
MWANANA Hamisa Mobeto ameibua gumzo wakati wa utoaji wa tuzo za Sinema Zetu baada ya kuamua kumtaja msanii maarufu Nassib Abdul a.k.a Diamond Platnumz ndio amemvutia zaidi kwa wageni waliofika kwenye sherehe hizo za utoaji tuzo.

Jina la Mobeto si geni kwa Watanzania walio wengi na hasa wanaofuatilia maisha ya mastaa wa kibongo na umaarufu wake uliongzeka zaidi baada ya kubainika amezaa na Diamond.

Usiku wa jana Mobeto alikuwa moja ya wageni waalikwa katika utoaji wa tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Azam TV kupitia chaneli ya Sinema Zetu.Ndani ya ukumbi huo alikuwepo na Diamond.

Wakati mambo yakiendelea ukumbini hapo ndipo moja ya washehereshaji alipoamua kumfuata Hamisa Mobeto na kisha kumuuliza ni nani ambaye anaona amependeza ukumbini hapo kuliko mtu mwingine yeyote na anafurahia uwepo wake.

Jibu la Hamisa Mobeto bila kuchelewa akataja jina la Diamond.Wakati anaaza kuulizwa Diamond alikuwa anasikilizia kwa umakini mkubwa na baada ya kutajwa yeye akajikuta aking'ata meno kwa nguvu na kwa muda wa zaidi ya dakika tatu akiwa ameshika kichwa chake.

Hata hivyo ukumbini hapo wageni waalikwa walilipuka kwa shangwe kwa kupiga kelele.Wakati Hamisa akimtaja Diamond, Wema Sepetu aliyekuwepo eneo hilo yeye alionekana akiwa 'bize' na kuchati kwenye simu yake ingawa sura yake ilionekana kutofurahia.

Ilipofika muda wa kutoa zawadi kwa moja ya washindi wa tuzo hizo akaitwa tena Diamond na Hamisa Mobeto wapande jukwaani kutoa tunzo.Hali hiyo ikamfanya Diamond kukosa la kufanya.

Hivyo akatumia nafasi hiyo kupongeza Azam TV kwa kuandaa tuzo hizo kwani zimewakutanisha wasanii mbalimbali na hata yeye amepata nafasi ya kukutana na mzazi mwenzie(Hamisa) na kufafanua hata mtoto wao akiona atafurahia kuona wakiwa wawili jukwaani hapo.

WINNIE MANDELA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81.
Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake.
Msemaji wa familia Victor Dlamini amesema kupitia taarifa kuwa: “Amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, ambapo amekuwa akiingia na kutoka hospitalini mara kwa mara tangu mwnazo wa mwaka.
“Alifariki kwa amani mapema Jumatatu adhuhuri akiwa amezungukwa na familia na wapendwa wake.”
Askofu mstaafu na mshindi wa tuzo ya Nobel Desmond Tutu amemsifu kama “ishara kuu ya vita dhidi ya ubaguzi wa rangi,” kwa mujibu wa AFP.

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya (wa pili kulia) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na aliofuatana nao leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na baadhi Viongozi wa Ujumbe wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo chini ya kiongozi wake Mwenyekiti wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof Mark J.Mwandosya (katikati),[Picha na Ikulu.

Rais Magufuli amteua Dkt. Fidelice Mbaruku Simbagungile Mafumiko kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali

$
0
0
Rais Magufuli amemteua Dkt. Fidelice Mbaruku Simbagungile Mafumiko (pichani) kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA


ALICHOKISEMA RAIS MAGUFULI UZINDUZI MRADI UZALISHAJI UMEME WA GESI ASILIA KINYEREZI II

Watanzania waaswa kuchangamkia makazi nchini Oman

$
0
0


Meneja Mauzo Mwandamizi wa Kampuni ya Ujenzi wa Makazi ya Muriya, Ghizlane El Gouchi (wa pili kushoto) akiwaonyesha wageni waliohudhuria hafla ya kuitambulisha kampuni hiyo kuelekea maonyesho ya biashara yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam hadi Aprili 5 na Zanzibar Aprili 6. Kushoto ni Mshauri wa Mradi Mona Abel Malak, mshauri mwandamizi, Faisal Alzakwani,Mshauri Hamad Al Balushi na mshauri mwingine Omar Saleh.


Watanzania wameaswa kuchangamkia nyumba zinazouzwa na Kampuni ya Muriya yenye maskani yake Muscat nchini Oman, ili kujiweka katika kundi sahihi la kibiashara sanjari na kujipatia maendeleo makubwa kutoka kwa nchi ya Tanzania na Oman.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Masoko na Kampuni ya Muriya Ghizlane El Gouchi, wakati anazungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya nyumba zinazouzwa na kampuni yao huku maonyesho hayo yakifanyika jana katika Hotel ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wenye ndoto za uwekezaji wa majengo.
Maonyesho hayo yaoiendelea leo jijini Dar es Salaam leo latina Hoteli ya Hyatt.


Alisema kwamba Tanzania na Oman ni nchi mbili zenye uhusiano mkubwa wa kindugu na kibiasharaa, hivyo ni wakati wa Watanzania wenye ndoto za kuwa wafanyabiashara wakubwa, kujitokeza kwa wingi katika uwekezaji wa majengo yanayotolewa na kampuni yao pembeni mwa viwanja vya Golf na pembezoni mwa bahari.

Muriya ni kampuni kubwa iliyojikita katika utoaji wa huduma za makazi na utalii nchini Oman, ambao tumeingia katika soko la Tanzania baada ya kufanikiwa pia kwenye soko la ndani, tukiamini kuwa ni wakati mzuri wa kutoa fursa za makazi kwa Watanzania wote.

“Taratibu za malipo ni rahisi kwa sababu mtu atakayekuwa tayari kununua, anakuwa na fursa ya malipo kwa awamu nane ndani ya miaka miwili ambapo mteja atalipia asilimia 10 mara baada ya kujisajili na asilimia 10 ya mwisho ni atakapokabidhiwa, huku gharama zetu zikianzia Dola 98,000 tu,” Alisema El Gouchi.

Kwa mujibu wa El Gouchi, mradi wao wa Jebel Sifa ni mwendo wa dakika 40 tu kutoka Muscat, karibu na ufukweni ambayo yana ukubwa hadi wa square meter 365,000, ukiwa ni mradi mkubwa unaowahusu Watanzania wote na ni fursa nzuri za uwekezaji.

Maonyesho hayo ya kibiashara ya makazi yanayouzwa na Kampuni ya Muriya mbali na kufanyika jijini Dar es Salaam, Hyatt Regency Hoteli kuanzia tarehe Aprili 3 hadi 5, pia yanatarajiwa kufanyika Visiwani Zanzibar Aprili 6 Park Hyatt Hoteli kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni kwa ajili ya kuendeleza kutoa elimu juu ya fursa hizo za makazi inayotolewa na Muriya, kampuni iliyoanzishwa nchini Oman.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI YA STAR TIMES BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Makampuni ya Star Times Group, Bw. Pang Xin Xing kabla ya mazungumzo yao, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018. Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Makampuni ya Star Times Group, Pang Xin Xing (watatu kushoto) na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa aWaziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma Aprili 3, 2018.Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Star Media Tanzania Limited,Wang Xiao Bo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Makampuni ya Star Times Group,Zhang Ye na kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Star Media Tanzania Limited, Juma Suluhu Sharobaro.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

KUELEKEA MTIHANI WA TAIFA MEI 2018 WANAFUNZI 1003 KIDATO CHA SITA SIMIYU WAPIGA KAMBI YA KITAALUMA

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu

Takribani wanafunzi 1003 wa Kidato cha sita kutoka shule za Sekondri 11 zenye kidato cha tano na sita Mkoani Simiyu, wamepiga kambi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na Shule ya Sekondari Binza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa ambao unatarajia kufanyika mapema mwezi Mei mwaka huu.

Akifungua kambi hiyo Aprili 03 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema ili mkoa huo uweze kushindana na kufanya mageuzi katika Uchumi ni lazima kuwekeza katika elimu.

“Kama wanafunzi wetu wanakaa makambi ya michezo ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa kwa nini wanafunzi hao hao wasikae kambi kwa ajili ya maendeleo ya taaluma; tukitaka kufanya mageuzi ya Mkoa huu ni lazima tuweke nguvu kwenye elimu, maeneo yenye uchumi mzuri wamewekeza sana kwenye elimu” alisema Mtaka. Aidha, Mtaka awataka wanafunzi wote wa kidato cha sita kuwasikiliza walimu watakaokuwa wakiwafundisha na kuwaelekeza na akawataka kujiamini wakati wa mtihani wao wa mwisho.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Mwl. Julius Nestory amesema Mkoa huo una mpango wa kuondoa daraja la nne na sifuri katika matokeo ya Mitihani ya Taifa, hivyo wanayo matumaini makubwa kuwa, kupitia makambi hayo ya kitaaluma Mkoa utaweza kufikia lengo hilo kwa matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.

“ Tumeamua kuwaleta pamoja wanafunzi ili waweze kunyanyuka kama kundi moja la mama mmoja (Simiyu) na kuweza kupandisha ufaulu, tumewaleta hapa ili kuweza kunyanyua morali wa kazi kuwaleta pamoja anayeweza na asiyeweza ili tuweze kunyanyuka pamoja kama kundi” alisema Mwl.Nestory.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wanafunz wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Baadhi ya walimu mahiri 40 waliochaguliwa kufundisha na kuwaandaa wanafunzi wa kidato cha sita (kutoka shule 11 mkoani Simiyu) na Mtihani wa Taifa utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kambi ya  Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe.Dkt.Seif Shekalaghe akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa wa Simiyu wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani humo. 
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl.Julius Nestory akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa. 

BIL.39 KULIPWA FIDIA WANANCHI KATIKA MRADI MWINGINE MKUBWA WA UMEME-MGALU

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

SERIKALI imetenga kiasi cha sh.bilioni 39 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi ambao maeneo yao yatapitiwa na mradi wa umeme mkubwa unaotarajiwa kupitishwa kwenye maeneo yao.

Pamoja na hilo ,baadhi ya miradi ya awali ambayo fidia imechelewa kwa walengwa ,uhakiki tayari umekamilika na utaratibu ukikamilika malipo yatafanyika hivyo wananchi watoe shaka kwani serikali inataka ikabiliane na ubabaishaji.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu alipokuwa akizungumzia suala la fidia kwa baadhi ya wananchi watakaokuwa na haki ya kupatiwa.Alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na utagharimu fedha nyingi.

Subira alielezea mradi unaanzia Rufiji, Kinyerezi,Kibaha na Chalinze na baadaye Dodoma ambapo wananchi watalipwa wakati utakapoanza.“Suala la fidia ni kubwa na kwa ile miradi ya awali ambayo haijalipwa ni kweli kwani baadhi bado hawajalipwa lakini wananchi wasiwe na wasi wasi kwani watalipwa fidia zao mara uhakiki utakapokamilika,” alisema Subira.

Alielezea ,kwa bajeti ambayo inaendelea kwa sasa zimetengwa kiasi cha sh.bilioni 21 kwa ajili ya fidia kwa laini inayoanzia Kinyerezi, Kibaha, Chalinze na Arusha ya umeme wa KV 400.Kwa mujibu wa Subira,mradi huo ulifanyiwa tathmini 2014/2015 na fidia imechelewa hivyo serikali inaomba radhi kwa hilo.

"Serikali ina majukumu na vipaombele mengi, haikusudii kuchelewesha bali mwaka unaoendelea wa bajeti zitalipwa tu,” alisema Subira.

Aidha alisema ,wakati Rais Dk. John Magufuli anaingia madarakani kulibainika kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na wizi mkubwa kwenye suala la fidia kwani walikuwa wakilipwa watu wasiostahili ambapo fedha inayopangwa na serikali inabadilishwa na kuwekwa viwango vingine hasa inapofika ngazi ya wilaya.

“Walikuwa wanabadili watu wanaopaswa kulipwa wanabadilisha majina na kila kitu hadi picha hata akilipwa anayestahili analipwa kiwango kisichotakiwa hali iliyosababisha hazina kufanya uhakiki,” alifafanua.Subira alisema, uhakiki tayari umefanyika na utaratibu ukikamilika malipo yatafanyika hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi licha ya kucheleweshewa fidia zao bali serikali inataka iondokane na ubabaishaji

DKT SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA JUU WA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk. Ali Mohemed Shein, akizungumza na uongozi wa juu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulioongozwa na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Prof Mark Mwandosya  wakati uongozi wa chuo hicho ulipofika Ikulu ya Zanzibar kwa Mazungumzo .
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk. Ali Mohemed Shein, akiprana mikono na Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Prof Mark Mwandosya  mara baada ya kufika katika ikulu ya Zanzibar .
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk Ali Mohemed Shein,akiprana mikono na  Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Prof. Shadrack Mwakalila mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zanzibar kwa Mazungumzo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk. Ali Mohemed Shein, akiwa katika picha ya Pamoja na Uongozi wa juu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ulipofika kumtembelea Ikulu ya Zanzibar 

MAMA SAMIA MGENI RASMI WARSHA YA MWAKA YA REPOA

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa REPOA, Dr Donald Mmari akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Warsha ya siku mbili ya mwaka kwa Tasisi hiyo itakayofanyika katika  hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam yenye mada ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu anatarajia kuwa mgeni rasmi.
 Mtafiti kutoka REPOA, Dkt. Blandina Kilama , akizungumza na Waandishi wa Habari kufafanua jambo juu ya umuhimu wa mada hiyo Tanzania kuelekea Uvchumi wa Viwanda.
 Mtafiti Kutoka REPOA,Dk Jamal Msami, akieleza namna uchumi wa viwanda unavyoleta tija kutokana na tafiti zilizofanywa nchini.


--

KLABU YA ROTARY DAR NORTH KUTEKELEZA MRADI WA MAJI SAFI KISIJU WILAYANI MKURANGA

$
0
0

Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam North imeanza kutekeleza mradi wenye lengo la kupeleka maji safi katika kata ya Kisiju, wilaya ya Mkuranga- Mkoa wa Pwani.
Mradi huo unaoitwa Aquaplus unafadhiliwa na klabu ya Rotary Dar North ya Dar es Salaam Tanzania, klabu za Rotary za Milano nchini Italia, shirika lisilo la kiserikali la MLFM la nchini Italia na mfuko wa Rotary.

Kata ya Kisiju- Pwani iko katika fukwe ya wilaya ya Mkuranga na inajishughulisha na uvuvi na pia hakuna upatikanaji rahisi wa maji safi ya kunywa hivyo basi mradi wa Aquaplus una lengo la kutatua tatizo hilo la muda mrefu kusafirisha kwa mabomba maji safi kutoka katika kisima kilichopo kijiji jirani chenye maji yasiyo na chumvi kufikia Kisiju Pwani na vijiji jirani vya Maputo, Kwale na Koma.  

Akizungumzia mradi huo, Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa klabu ya Rotary Dar North Masato Wasira alisema kuwa, klabu hiyo pamoja na washirika wake wameshaanza kazi ya kutekeleza mradi huo utakaogharimu kiasi cha dola la marekani zaidi ya laki moja. Ikiwa kama mshirika aliyeko nchini, klabu hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha mradi huo unafanyika kuzingatia bajeti na malengo yaliyowekwa.

“Kila binadamu ana haki ya kupata maji safi ya kunywa na kwa kuzingatia hilo kunafanya klabu yetu kuwa na shauku kubwa ya kufikisha maji safi kwa wakazi wa Kisiju. Klabu yetu pamoja na washirika wetu tumekusanya zaidi ya shilingi milioni 200 ili kuweza kutekeleza mradi huu,” alisema Masato.

Mradi wa Aquaplus ambao unafanyika kwa ushirikiano kutokakwa wilaya ya Mkuranga na uongozi wa kata ya Kisiju pia utahakikisha watakaopokea kuendeleza mradi huo utakapomalizika wanapata mafunzo ya kuendesha na kutunza mfumo huo.

 “Shirika la shughuli za kijamii la Rotary linafanya kazi katika jamii ulimwnguni kote ili kuleta mabadiliko endelevu na sisi tunategemea kupitia mradi huu tutaleta mabadiliko ya kudumu kwa watakaofaidika na mradi huu. Vile vile kupitia mradi huu tunategemea kuwa magonywa yanayosababishwa na matumizi ya maji yasiyo salama yatakwisha na tuna furaha kubwa kuweza kusaidia wakina mama waliokuwa wnapata taabu kwenda umbali mrefu kutafuta maji safi sasa watayapata kaibu kabisa na makazi yao,” aliongeza Masato.

Mfuko wa ufadhili wa Rotary unaojulikana kama ‘Rotary Foundation’ umepata tuzo ya kuwa mfuko bora wa misaada duniani hivi karibuni na umetumia zaidi ya dola za kimarekani bilioni tatu duniani kote katika miradi mbali mbali ya kusadia jamii kupitia klabu za Rotary.

Rotary Foundation ilianzishwa mwaka 1917 “kufanya mema duniani” na inajulikana kwa juhudi iliyofanya katika mradi wake kubwa unaotekelezwa dunia nzima wa kutokomeza polio duniani.


Michuzi TV GOSSIP: SOO LA MASOGANGE, ALIKIBA APAISHWA WASAFI TV NA MENGINEYO

Promosheni ya Tigo yaongeza Matumizi ya Intaneti Nchini

$
0
0
 Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini ya Tigo Tanzania imezidi kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za intaneti nchini baada ya kuwazawadia wateja wake 676 simu janja aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.

Katika promosheni hii murwa ambapo Tigo inatoa jumla ya simu janja 12 kila siku, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter. 

‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo,’ Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo. 

Akizungumza katika hafla kama hiyo iliyofanyika mjini Morogoro leo, Mtalaam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G.
 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kushoto) na Mtalaam wa Bidhaa wa Tigo,  Jacqueline Nnunduma (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhi zawadi za simu janja aina ya Tecno R6 kwa washindi wa promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus. Tigo imetoa jumla ya simu 676 bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#. 
 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Gladness Mori (alieyeketi) zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo.
 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Diana Pumpuni (wa pili kushoto) zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (aliyesimama kulia) akimkabidhi Charles Shabani  zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi ya washindi wengine wa promosheni hiyo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018

$
0
0
TIMU ya soka ya Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF), imeichapa bila huruma timu ya soka ya ZSSF 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka.

Mchezo huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa kuzikutanisha timu mbili za mashirika ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na ZSSF ambapo lengo la michizo hiyo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya mashirika hayo mawili.

Mchezo huo uliianza kwa kasi kubwa iliwachukua dakika 4 NSSF kujipatia bao la kwanza baada ya mwamuzi wa mchezo huo Fikiri Yusuph kutoa Penalti baada ya beki wa ZSSF kuunawa mpira katika harakati za kuokoa, mshambuliaji wa NSSF Said Mwinyi aliipiga penalti hiyo na kuipatia timu yake bao la kwanza.

Kuingia kwa bao hilo la mapema kuliwafanya ZSSF kucharuka na katika dakika ya 10 nusura wajipatie bao la kusawazisha baada ya shuti kali lililopigwa na Juma Mbwana kugonga mwamba na kuokolewa na walinzi wa timu ya NSSF.

ZSSF waliendelea kulisakama lango la NSSF lakini walinzi wa timu ya NSSF wamkiongozwa na beki wa wa timu hiyo Hemed Kagobe waliweza kuondoa hatari hizo na kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa timu ya ZSSF.
 Nahodha wa timu ya netiboli ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Pili Mogella, akipokea kombe la Ubingwa wa michuano ya tamasha la Pasaka kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF, Dominick Mbwete (kushoto), baada ya kuifunga ZSSF magoli 23-19  katika mchezo ulifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya soka ya NSSF, Mzee Mfaume, baada ya kuwafunga ZSSF mabao 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Wachezaji wa timu ya soka ya NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akipokea zawadi ya mlango kutoka kwa Kaimu Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa ZSSF, Abdallah Mbwana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WATEJA VODACOM KUENDELEA KUPATA HUDUMA YA LUKU KUPITIA M-PESA

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc inapenda kuwataarifu wateja wake na Watanzania kwa ujumla kwamba, itaendelea kutoa huduma ya ununuzi wa umeme (LUKU) kupitia mfumo wa malipo wa serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG).

Kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa hivi karibuni na kampuni ya kuzalisha na kutoa huduma ya umeme nchini (TANESCO) kuhusu kuanza kutoa huduma ya kununua umeme kwa kupitia mfumo wa Serikali wa GePG, Vodacom Tanzania Plc inapenda kuwatoa hofu Wateja wake kwamba wataendela kupata huduma ya kununua umeme ya LUKU kupitia Vodacom M-Pesa kama ilivyokuwa mwanzo.

Mfumo mpya utaiwezesha Tanesco kuunganisha mauzo moja kwa moja kutoka makampuni mengine ya simu na mabenki kwenda GePG ikiwa ni matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.

Kutakuwa na ongezeko la asilimia moja nukta moja ya gharama halisi (1.1%) anayotozwa Mteja ili kununua umeme pindi atumiapo huduma ya M-Pesa. 

Vodacom inawahakikishia Wateja wake kwamba itaendelea kutoa huduma ya LUKU kupitia M-Pesa ambayo pia inapatikana katika App za Apple, na Android.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea www.vodacom.co.tz

Viewing all 110095 articles
Browse latest View live




Latest Images